Baba mwenye nyumba alipogundua kuwa kaota
ndoto inayomkumbusha maisha yake ya nyuma, na alipozindukana akajikuta karibu
yake yupo yule mama aliyekuwa kwake ambaye wengi walijua kuwa kaungua na moto,
lakini kwa bahati nzuri hakuungua na moto, lakini…
‘Watu wakiwa wanajua kuwa huyo mama
keshafariki, lakini bado waliogopa kumsogelea au kumfunua, na waliojaribu
kufanya hivyo, wakajikuta wakipatwa na mambo ya jabu hata kupoteza fahamu,
mmojawapo alikuwa askari, …
Mwishowe
mwili wa mama huyo ukafikishwa hospitalini, pamoja na baba mwenye nyumba ambaye
alipoteza fahamu pia.
Sintofahamu hii ya huyu mama, ikawagusa
wengi, na hata alipofikishwa hospitalini, kukawa na ucheleweshaji wa kumpokea
huyo mama, kwania anyehusika na kupokea maii alikuwa hayupo, katoka, na
dakitari wa zamu alikuwa akihudumia mgonjwa wa dharura.
‘Kama mna uhakika amefariki, hamna shida,
..nyie muwekeni hapo..na huyo mwingine naona hana tatizo kubwa…kazindukana, na ….mengine
docta atamuangalia..’akasema mpokeaji, ambaye ni dakitari pia lakini alikuwa
hana mamlaka, na alikuwa kamaliza zamu yake anajiandaa kuondoka.
‘Alipoteza fahamu tu,lakini hana matatizo….’akasema
askari aliyekuja na hao watu ambaye alikuwa kiongozi wa msafara, akawa anamtikisa tikisa baba mwenye nyumba.
Na baba mwenye nyumba akawa anajinyosha nyosha.
‘We muache tu…kama ana tatizo jingine
docta atakuja kumuangalia..’akasema docta huku akichukua vifaa vyake,lakini
akasema;
‘Oh ..unajua mashine yangu hii ina
matatizo, ngoja tumsubirie docta atakuja sasa hivi, naona huyu mtu wenu hana
matatizo….’akasema baada ya kumshika mkono nakuangalia mapigo ya moyo, akafunua
kope za macho…
‘Sasa kuhusu huo mwili wa huyo mama,
msubirini docta kwani ndiye mwenye dhamana, atampokea na mtaandikishiana,na kwa
vile mpo watu wa usalama mumethibitisha hilo, sioni kama kuna tatizo…..mimi
natoka maana muda wangu wa kazi umekwisha..’akasema docta huyo na kuondoka.
‘Sasa unasemaje baba mwenye nyumba upo
tayari kuitambua hiyo maiti na kufanya yale tuliyoahidiana maana kwangu ni
muhimu sana…ili nimalize uchunguzi wangu?’ akasema huyo askari, na baba mwenye
nyumba akainua uso na kumuangalia aaskari huyo, akatabsamu na kusema;
‘Nipo tayari kuitambua ….kuufunua huo
mwili…lakini kwa masharti..’akasema
Na
yule askari akatabasamu na kusimama, alionyesha kufurahia kauli hiyo akasema;
‘Safi kabisa sema lolote..tupo tayari..,
ilimradi umtambe na umpige picha, tunahitajia sura ya huyo mama, ni masharti
gani hayo…..?’akauliza.
‘Sharti langu ni hili..nataka nikitambua,
nikimfunua huyo mama,…huyo…eeh, hiyo maiti..nataka niwe peke yangu, sitaki mtu
mwingine humu ndani..ili kukidhi stahiki zake, kwani kama hakutaka watu wamuone
kwanini sasa tuvunje miiko yake…, pili siwezi kumpiga picha….’akasema
‘Lakini tunahitajai hiyo picha ni muhimu
kwetu…’akasema huyo askari.
‘Kwani picha yake itasaidia nini,..sawa
kwanza niachieni nimtambue, ..sitampiga
picha kwasasa mpaka nijirizishe kama kweli ndio yeye..’akasema
‘Ujirizishe….?! Ok, lakini sisi
tunachohitajia ni picha yake….ni muhimu sana…kabla madakitari hawajamchukua,
maana bado sijamtambua sura yake, na ikiid tunahitajika kumtangaza kama ana
ndugu zake waje kumtambua..unaona ilivyo muhimu ….’akasema afande
‘Mhh, ina maana dakitari hajamchunguza..?’
akauliza na kala hajajibiwa akasema;
‘Kwanini wanasubiria nini,…au na wao wana,muogopa..? akauliza na kabla
hajajibiwa akaongezea tena kwa kusema;
‘Masharti yangu ndio hayo,…lakini ni
muhimu madakitari wangemuona kwanza, …hata hivyo kama ni yeye..ooh sijui,…ni
bora tu ….iwe hivyo…sitaki na simtaki…ila kama ni muhimu mpaka mimi nihakikishe, basi naomba mtoke nje,
..’akasema na yule askari akamuangalia kwa uso wa kujiuliza akasema;
‘Kama kweli ndio yeye!?…una maana gani,
sisi tuna uhakika ndio yeye, tuna uhakika..naona kuzimia kwako kumekuchanganya
sana…wewe fanya ufanyalo lakini sisi tunataka picha yake kabla madakitari
hawajamchukua kumkagua…naona docta aliyeingia sasa kajiukuta na kazi
nyingi..alifika mwanzoni tukamzuia kwanza,…maana kuna hilo zoezi hatujalikamilisha,
…’akasema
‘Mkamzuia ,kwanini..maana yeye ndiye
angelithibistisha kuwa huyo mama kafariki au …’akasema
‘Kafariki, afariki mara ngapi…we acha
kuota, au kupoteza fahamu huko kumekupoteza akili..sasa sikiliza, fanya haraka…we
mkague , mpiga picha…kamera hii hapa si unajua kuitumia…’akaambiwa.
‘Nafahamu…’akasema akipokea ile kamare, na
wale askari na watu wengine waliokuwepo wakatoka nje.
Baba mwenye nyumba akiwa kabakia peke yake
akasimama na kujinyosha, akasimama akiwa hajaangalia pale alipolazwa huyo mama,
baadaye akageuka…
Akageuka kuangalia pale alipolazwa huyo
mama…akatulia kwa muda akiangalia, akijitahidi kutokuogopa, alikaa vile kwa muda, hadi aliposkia mlango
ukifungwa nyuma yake, ..akajua sasa yupo peke yake….
Tuendelee na kisa chetu…
************
Baba mwenye nyumba kichwani alikuwa katawaliwa na ile ndoto, akawa
anajiuliza kwanini hiyo ndoto imsumbue,…
‘Tausi…sizani kama nikikutana naye nitamsamehe, alichonifania sio
ubinadamu..japokuwa…anaonekanahana kosa, ..hasa kutokana na ndoto alivyoota ma kwani
wazazi wao walikuwa hawana nguvu ya kufanya lolote, lakini kilichomuuma ni kuwa
kwanini Tausi asiweze kutoroka kama walivyoahidi, ina maana aliona mali ni bora
kuliko yeye masikini.
Badala ya kufanya kile alichotakiwa kufanya, akajikuta anawaza jingina
akawa kasimama pale pale…, hasira zikamshika akawa akshikilia kitanda
alichokuwa kalazwa, mkono ukitetemeka kwa hasira…mara akasikia sauti…
Akabakia vile vile akitega sikio, ..hiyo ni sauti kama ya mguno,
kama mtu anathema..imetoka wapi, maana humo ndani wapo yeye na hiyo maiti…taratibu
akageuza shingo kutizama pale alipolazwa huyo mama.
Akabakia kaduwaa…hakuamini macho yake, akajikuta akitamani
kukimbia, lakini mwili hakuweza, akataka kupiga yowe lakini mdomo haukufungua,…akabakia
katoa macho huku haamini anachokiona,..ilipita dakika mbili, baadaye kukawa
kimiya.
‘Ina maana huyu mtu hajafa…’akasema sasa akawa anaogopa hata
kumsogelea huyo mama, akilini akawa anajiwa mawazo mengi, ya vibwengo..ya
..shetani yaani ya vitu vya kutisha, na baadaye akukumbua ile sauti inayomjia
mara kwa mara ikimuonya, ikasema;
‘Unaona..nilikuambia, sije kujaribu kuanya wanayotaka hao watu…huyo
mama sio wa kawaida….ni mzimu huo…ukicheza utakunyonya damu, na utabakia mkavu…toka
humu ndani haraka..’sauti ikamwambia.
‘Hapana siwezi kutoka humu mpaka nihakikishe huyu mama ni nani…’akasema
na kujipa moyo, akatembea kwa haraka hadi pale alipo huyo mama, akamkuta
katulia, na taratibu akainua mkono wake unaotetemeka na kuushika mkono wa huyo
mama…joto, joto la uhai, akalihisi, akauachia haraka, na kugeuka nnyuma nia ni
kama docta aje kuhakikisha.
‘Yupo hai, yupo hai….’akawa anema akirudia rudia maneno yake,
lakini kuna kitu kikawa kinamvuta , akawa na hamasa ya kutaka kuhakiki kile
kinachomsumbua akili yake, akageuka na kumtizama huyo mama.
‘Wewe ni nani?’ akauliza, akisahau kuwa swali kama hilo alishawahi
kuliuliza mara nnyingi na hakuwahi kupata jibu la kumsaidia…kukawa kimia,
akatulia, na kwa haraka akainu amkono na kushika ile nguo iliyomfunika huyo
mama kichwani akaivuta kwa hasira..ikavuka, na kichwa kikabakia wazi..
Unajua mshituko, unajua kushangaa..jamaa alibakia mdomo wazi,
..akajikuta hawezzi kusema kitu, akawa anacheza mdomo,…na mwisho wake akasema;
‘Mamamama..kwanini…wamekukata hivyo…ooh,..ina maana ni
wewe,,haiwezekani..haiwezekani,….oh,…’akajikuta akisema na huku akiwa aktoa
macho, na sauti ikasema;
‘Umerizika,..nifunike kichwa changu..’ilikuwa sauti..japokuwa
inakwaruza, lakini ni sauti ile ile, sauti ambayo aliipenda kuiskia, sauti
iliyokuwa ikimliwaza hata akia na shidd zake akisikia sauti hiyo
huliwazika..lakini…
Kwa haraka bila kubisha akachukua ile nguo na kumfunika huyo mama,
halafu akasema;
‘Siamini …umeonaeeh,…, hiyo ndio adhabu ya msaliti….wameiharibu
sura ako na mapanga..uziri wote sasa haupo, ….imebakia macho…hahaha…unakumbuak
eeh,…’akasema.
‘Nataka mtoto wangu…’sauti ile ile ya yule mama ikasema, na
akainua uso kumuangalia huyo mama, sasa alikuwa keshajifunika.
‘Unataka mtoto wako, unataak mtoto, unajianya umechenganyikiwa, au
sio..au mume wako alikufania nini, mbona niliskia umeshafariki..au ndio
umefufuke, au wewe ni mzimu wake tu..hahaha, …haya huyo mtoto uneyemtaka yupo
wapi?’ akauliza
‘Namtaka mtoto wangu….’akasema
‘Tausi ndio wewe,…kweli dunia ina mambo, siamini,….hii kweli ni
miujiza ya mungu….Tausi ndio wewe…siamini..’akasema
‘Tausi!….mimi so Tausi…na…namtaka mtoto wangu haraka..’sauti
ikasema sasa ikitokea kwenye nguo iliyofunika mdomo wake,na kabla baba mwenye
nyumaba hajasema zaidi, mlango
ukafunguliwa,akageuka kutizama ni nani aliyefungua mlango, akamuona dakitari.
‘Vipi …mbona..’docta akawa kasimama na yeye kuonyesha kushangaa,
na mwenye nyumba, hakusema kitu akaanza mdogo mdogo, …..taratibu akatembea
kutoka nje, huku akilini akiwa na yake….akiwa kachanganikiwa, akiwa haamini,….hakusema
neno hadi akafika nje.
‘Tayari umeshampiga picha?’ akaulizwa na askari
‘Picha!? picha ya nini, ..sizani kama picha ina umuhimu huo..’akasema
akitembea kuelekea pale aliposimama huyo askari.
‘Kwanini..umeshindwa, ..sasa umefanya nini, docta atampiga
masindano yao, na hatutaweza kupata picha tunayoihitajia..’akasema huyo askari.
‘Ili iweje?’ akauliza huku akiwa kainua mkono juu kumkabidhi huyo
askari kamera yake.
‘Tukamtangaze kwenye nyombo vya habari, ili wenyew e wakisikia…wafika,
unajua vyombo vya habari vinasaida sana… wanaweza kupatikana ndugu zake, na hata
wakisikia wataelekezwa kuwa maiti yao ipo hapa..’akasema huyo askari.
‘Hakuna maiti humo ndani….’akasema akiinua mkono kumkabidhi huyo
askari kamera yake, na huyo askari akawa katulia akionyesha kushangaa, akasema;
‘Una maana gani kusema hivyo, kaenda wapi huyo maiti?’ akauliza
huyu askari akiwa na wasiwasi.
‘Docta atawaambia mimi nawahi usafiri narudi nyumbani kwangu na
sitaki ..mnasikia sitaki tena huyo mama kukanyaga nyumbani kwangu..sitaki..mumesikia,
sitaki sitaki..nimuone nyumbani kwangu…’akasema huku anatembea kuelekea
barabarani….
Na kule kwenye mlango
alipokuwa huyo mama, docta aakjitokeza,
akiongea na simu,…na mara kukaja kigari cha kubebea wagonjwa…kikaingizwa
ndani haikupita muda, kile kigari kikatolewa huku kimebeba mtu, na mtu huyo sio
mwingine ni yule mama.
‘Haiwezekani….’akasema huyo askari
‘Mpelekeni chumba cha uchunguzi nakuja..’akasema docta akielekea
upande mwingine na askari akawa sasa anawafuatia nyuma wale watu waliombeba
huyo mama, akitaka kupata maelezo.
‘Ina maana huyo mama hajafa?’ akauliza wale wahudumu wakageuka
kumuangalia na wakasema;
‘Kwani alikuwa amekufa?’ wakauliza hao manesi, kwani wao walikuwa hawajui
lolote.
‘Oh ni miujiza, sisi tulileta maiti…sasa tunaona ajabu..’akasema
huyo askari
‘Labda maiti ipo…. imebakia huko ndani lakini hakuna maiti kule
ndani, kwanini hamkumpima kabla ya kusema amekua..huyu mtu yupo hai, ila ana hali
mbaya…anahitajia matibabu na uchunguzi wa hali ya juu..’akasema mmoja wa nesi
‘Mhh, sijawahi kukutana na tukio kama hili..na anhitaji
kulifuatilia kwa karibu,…nataka nionane na huyo docta..’akasema
‘Kuna mgonjwa mwingine kaletwa yupo kwenye hali mbaya..sasa sijui
atajigawaje..leo ipo kazi..’akalalamika nesi mmojawapo.
‘Hivi nesi mkuu anainga saa ngapi?’ akauliza,
‘Yule anakuja…’mwenzake akasema.
Askari akageuka kumuangalia
huyo nesi mkuu ambaye alionekana akija kwa mwendo wa haraka kuonyesha kuwa
kachelewa…, akahisi kama anamkumbua akasubiria hadi huyo nesi akawakariba, na huyo
nesi akawasalimia, huku akimuangalai huyo askari kwa amshaka, na kuulizia;
‘Docta yupo wapi?’ akauliza
‘Ana mgonjwa wa dharura..’akaambiwa
‘Mhh, jamani hospitali hii…yaani hakuna kulala, kila dakika
mgonjwa anayeletwa hapa ni mahututi,..ni wa dharura…na wengie wana majeraha..na
huyu vipi..?’ akauliza na kugeuka kuangalia, pale kwenye kigari cha wagonjwa,
na kumuona huyo mama, kwanza akashituka, halafu akageuka kumuangalia
askari..akaona wenzake wamebakia kimiya, nay eye akabakia kaduwaa…lakini
akajiweka sawa, na kusema;
‘Katokea wapi huyu..naona mkono umeungua?’ akauliza
‘Katokea kijijini..’akaambiwa
‘Kijini ..kijiji cha wapi…. ?’ akauliza
‘Unamfahamu huyu mama?’ yule askari ambaye kwa muda mwingi alikuwa kimia alipofika huyo nesi akijiuliza ni wapi aliwahi kumuona huyu nesi, akauliza, baada ya kuhisi huenda alimuona hapo hapo hospitalini.
‘Sina uhakika kama ndio yeye…’akasema huyo nesi akimsogelea huyo
mama...kumkagua akamuinamia na kusema;
‘Nataka mtoto wangu….’akasema na mara yule mama aliyekuwa kama
kalala akashituka na yeye akasema;
‘Nataka mtoto wangu…’wote wakabakia wameduwaa, hasa askari, ambaye
alikuwa akiangalia hilo tukio kwa aina yake, akasema;
‘Nesi unafahamu huyo mama?’ akauliza na mara docta akafika, na
doct akaongea kidogo na huyo askari walipomaliza kuongea huyo askari akawa
anaondoka,..na alipowapita hao manesi akamgeukia huyo nesi mkuu na kusema;
‘Nesi nikija kesho nataka kuongea na wewe..’akasema na nesi akabakia
kaduwaa tu, hakusema neno, na yule askari akaondoka zake.
************
Kwa hali aliyokuwa nayo huyo mama ailibidi apelekwe chumba maalumu
cha uchunguzi, kwani hali yake ilikuwa mbaya, kwa majeraha ya moto na majeraha
ya mapanga. Kwa muda huo alikuwa keshazindukana vyema, ila alikuwa akigugumia
kwa maumivu na damu ilikuwa inamvuja kidogo kidogo.
‘Huyu mama anahali mbaya sana, kwani wamemkatakata na mapanga
usoni, miguuni, lakini hawakugusa sehemu
za mwili, ..tumboni hawakugusa kabisa…ndilo
limesaidia…halafu kaungua sehemu kubwa ya mwili…mkononi na miguuni ….uzuri ni
kuwa damu haikupungua sana, kwahiyo haina haja ya kumuongezea damu, ila
anahitaji matibabu ya haraka..vdonda vimekaa muda bila kutibiwa…’ akasema
dakitari.
‘Halafu huyu mama hasemi na wala hakumbuki kitu gani kimemtokea,
ina maana ana matatizo mengine, ambayo yanahitaji utaalamu zaidi, ama ya akili
au ana tatizo la kusahau…’ akasema dakitari, baada ya uachunguzi wa awali..
‘Hata jina halijulikani..’akasema nesi
‘Mhh, wewe andika mama mgonjwa wa moto…’akasema docta na wote
wakacheka.
‘Na majeraha ya mapanga,..nafasi haitoshi..’akasema huyo nesi.
‘Lakini huyu mama kama sikosei nilishamuona huko kijijini kwetu,
kuna kipndi nilikwenda huko, kabla sijakwenda kozi…nilimuona huyu mama akipita
pita mitaaani na kuimba kuwa anamtaka mtoto wake, sijui ndio yeye, maana hata
sura siijui, na hata sasa hataki kufunuliwa funuliwa, anamuamini docta wake tu…’akasema
nesi.
‘Oh, nyie niachieni mama yangu kanitunuku, msione wivu ..lakini,
mbona hajafika na ndugu yake yoyote?’ akauliza docta
‘Ina maana hana ndugu, kama ni huyo mama, …, nijuavyo mimi,
alikuwa akipita pita mitaani akiimba imba tu,..na hulala popote..hata kule
kijijini hawaju katokea wapi…’akasema
‘Aliletwa hapa na askari na jamaa mmoja ambaye tulijua ni ndugu
yake, lakini kumbe sio ndugu yake, na huyo jamaa kaondoka hata bila kuaga,….huyo
jamaa alikuja hapa akiwa naye kapoteza fahamu..’akasema docta
‘Kwasababu hii hii ya moto?’ akauliza nesi
‘Sina uhakika..labda tusubiri akija askari, maana huyu mama bado
yupo mikononi mwa askari, wanasema hawajamaliza uchunguzi naye..’akasema
‘Oh,…jamani, sijui ni akina nani walimfanyia hivi huyu mama, wamekata
kata na mapanga, hadi kuiharibu sura yake....halafu wakamuunguza na moto…naona
pale hakutaka watu wamuengalie, mimi nikajiiba na kumuangalia, ....’akasema
nesi.
‘Ndio hivyo dunia imeharibika kabisa..’akasema docta.
‘Kwanza umenikumbusha ngoja niwapigia ndugu zangu huko kijijini
nijue kinachoendelea, …nina hamu ya kujua mtoto anaendeleaje…na siku yaani
tangu niende kozi ..tunawasiliana kwa shida, kule mawasiliano mabovu..aaaah,
nikaona kwanini njipe shida, nikaachana na simu..mpaka narudi sijui
kinachoendelea huko kijijini kwetu..yaani nina hamu sana na ndugu zangu...’akasema
nesi
‘Kwani wewe una mtoto..?’ akamuuliza docta
‘Hahaha..ninaye mtoto ndio…’akasema
‘Mbona hufanani kuwa na mtoto..’akasema
‘Mmmh, hapana ni mtoto wa dada yangu….nampenda sana huyo mtoto ana
historia ya aina yake…’akasema
‘Ipoje hiyo historia?’ akauliza huyo docta.
‘Siwezi kukuambia, wewe jua hivyo tu….ngoja niongee na ndugu
zangu, akasema huku simu ikiita bila kupokelewa.
‘Hawa watu vipi toka juzi simu inaiita hawapokei..sijui kuna nini,….oh,
wananipa mashaka kweli…’akasema akijaribu tena na tena lakini simu ikawa haipokelewi.
NB: Sasa tupo mjini,…
WAZO LA LEO: Utu sasa haivi haupo, watu wanachojali
zaidi ni masilahi,…watu wapo tayari kuua, kwasababu ya mali, ndugu kwa ndugu
wanakosana kwasababu ya mali , marafiki wanakosana kwasababu ya mali,…hata mke
na mume wanakosana kwasababu ya mali.Mali imekuwa ni mtihani, ..jamanii hebu
turejeshe utu wetu, ..tupendane, tusaidiane..kwani utu una thamani kubwa zaidi
ya hiyo mali tunayoithamini.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
I Ьlߋg often and I serioսsly thɑnk you for yоur information. The
article has truly peakeɗ my interest. I am going to book marƙ your website аnd keep checking fоr new
details about once per week. I opted in for your Feed as
well.
my page: halloween costumes for girls
Hi there i am kavin, its my first occasion to commenting anyplace, when i
read this post i thought i could also make comment due
to this good paragraph.
Take a look at my web-site - Used Stationary bikes
Post a Comment