Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, February 27, 2015

NANI KAMA MAMA-38


Katika kupata ukweli wa tukio zima, askari hawa waliotumwa waligawana katika makundi matatu, nia hasa ni kutafuta ukweli na chanzo, cha watu kuuwawa ovyo, hasa wazee na akina mama kupigwa hadi kuumizwa, na kwanini kunakuwa na ajali za moto za mara kwa mara.
 Tulishaliona kundi la kwanza , ambalo liliingia kumchunguza mmoja wa wahanga wa moto ambaye ni mama wa mkono wa karama, au wengine kama wanavymuita, mama kutoka mbinguni, na wale wasiompenda wakamuita, mama kutoka kuzimu…na kundi la tatu lilikuwa na kazi ya kuchunguza chanzo cha moto.

Katika kundi hili la pili, ambalo kazi yake ilikuwa kuwahoji watu ili kujua kinachoendelea hapo kijijini, …na kuhusiani na hilo tukio la moto uliotokea karibuni hadi kueleta maafa.

Askari hawa wakiwa wanaendelea kumhoji, baba mwenye nyumba maswali mbambali na kwa muda huo walikuwa wakitaka kufahamu huyo mama mhanga wa moto ni nani…..

Akiendelea na maswali, askari kanzu akamuuliza baba mwenye nyumba swali ambalo kwao lilikuwa na umuhimu wake, japokuwa alitarajia kupata maelezo kutoka kwa kundi la kwanza lakini kutokana na utata uliopo, akaona amuulize baba mwenye nyumba ambaye aliweza kuishi na huyo mama kwenye nyumba moja kwa muda sasa…akamuuliza swali;


‘Je wewe uliwahi kuiona sura ya huyo mama…maana nasikia muda wote kajifunika usoni?’ akaulizwa baba mwenye nyumba,  na baba mwenye nyumba kwanza akatulia akijua hilo swali sasa linamuingiza kwenye mtihani, na pia inawezekana ni mtego kwake, akasema;

‘Mwenyewe umesema kuwa mama huyu muda wote huwa anajiunika,sasa kama muda wote anakuwa amejifunika, mimi nitawezaje kumuona sura yake..’akajibu akiwa kakereka na maswali ya mwanzoni ambayo hakuyaenda.

‘Hivi ni kweli mtu mumeishi naye nyumba moja karibu miaka mingapi,…akawa anakulelea mtoto wako…mkazoeaan akawa kama mmoja wa familia yako, ina maana haikutokea hata siku moja kuiona sura yake au ni kwa vile hutaki kutoa siri zake, labda kwa kujali utashi wake…?’ akaulizwa.

‘Nikuambie ukweli, akina mama kama hao wanakuwa makini sana…inaweza ikatokea bahati mbaya kama unavyosema,..kwa bahati mbaya,na kwa vile ni kwa bahati mbaya huwezi kuwa makini kumuangalia …’akasema.

‘Tunataka hiyo bahati mbaya,…maana wewe kama baba wa nyumba,una jukumu la ulinzi na usimamizi wa nyumba na familia yako , huwezi kumpoeka mtu tu, humjui, hujui sura yake, hujui jina lake..haya limetokea kama hili janga, tunahitajia ukweli na unatakiwa kusema ukweli wote li tuweze kuhakikisha kuwa haki inatendekea, na pia tuweze kumaliza hili tatizo linaloendelea haapa kijijini kwenu..’akasema

‘Lakini hamuwezi kulimaliza kwa kupitia kwangu tu au…?’ akauliza baba mwenye nyumba.

‘Chanzo kimoja kinaweza kuwa sababu ya vyanzo vyote, hapa tumeona ndipo pa kuanzia, na kwa jinsi ilivyo, hawa watu waliofanya hivi hapa ndio hao hao wamekuwa wakifanya kila siku sehemu mbali mbali za hapa kijijini,…sasa ukituficha inawezekaan tukahisi kuwa unashirikiana na hao watu….’akasema askari.

‘Ndio tatizo lenu hilo..mtu akijitolea kusema ukweli anaweza akapata taabu hata kuliko muhusika mwenyewe au muhalifu mwenyewe mnayemtafuta…sawa mimi sikatai kushirikiana nanyi kuupata ukweli, maana hata mimi kama raia mwema wa hiki kijiji napenda tuishi kwa amani..lakini sio kwamba kila kitu nitakifahamu mimi..’akajitetea

‘Ndio maana tunakuuliza maswali ambayo tunahisi wewe unayafahamu na sio kwamba tunahisi lakini kiukweli haya maswali tunayokuuliza, tunaamini wewe unayafahamu..hasa kuhusu huyu mama…’wakasema

‘Haya mnataka mimi niseme nini?’ akauliza

‘Utujibu swali letu tulilokuuliza awali , au niulize tena, je, wewe uliwahi kumuona huyo mama sura yake,…usoni,… hata kwa bahati mbaya tu…?’ akaulizwa

 ‘Mhh..,hata kwa bahati mbaya tu, mmh….?’ Akauliza huku akisita kusema kitu na kumbukumbu la tukio la nyuma likamjia akilini na kujaraibu kuwazia sura ya huyo mama, akawa hakumbuki vyema  ….maana mara zote ilikuwa kwa bahati mbaya na kwa haraka.

Wakati baba mwenye nyumba anatafakari akilini akahisi kuonywa, kuwa asiseme, akisema atakufa au kupatwa majanga kama yalivyowapata wengine…lakini kwa upande mwingine akawa anajipa matumaini, akisema; mmh huenda ndio yeye, kama ndio yeye kwanini niogope kusema ukweli, lakini hata hivyo, mwenyewe hakutaka sura yake ionekane kwanini mimi niwe mtoaji wa siri zake,…

Tuendelee na kisa chetu

****************

Baba mwenye nyumba akakumbuka tukio wakati alipoingia kuhakikisha kama kweli huyo mama kateketea na moto uliounguza chumba hicho alichokuwa akilala huyo mama…na kwa kumbukumbu zake tukio hilo ndilo lililomuwezesha kumuona huyo mama, japo, sio kwa uhakika sana,.. ni kwa muda mchache sana, na kilichotokea pale alipoivua ile nguo iliyokuwa imefunika kichwa, alijikuta akipata msituko na akili yake kuwa kama imeganda.

Akili ilikuwa kama imeganda kwa kutokuamini kwa yale aliyoyaona ambayo mengine hataki hata kuyakumbuka, sembuse kuyasema..macho na akili ikawa kama haiamini kile alichokiona…na mengi yalipita kichwani na hata hakuweza kukariri vyema kile alichokiona..

Ilivyotokea ni kama vile umepita njiani ghafla ukaona kitu cha aajabu au kisichochofaa, ukakwepesha macho yako kwa haraka usikiingalie, na kwa tabia ya macho hutuma taarifa kwenye ubongo, na ubongo hutaka uhakika, kwahiyo utageuza kichwa kuangalia kile kitu tena….ndivyo inavyokuwa kwenye akili ya kibinadamu na ndivyo ilivyotokea kwa huyu mjamaa….

  Akajaribu kukumbuka…na kuvuta akili, kuanzia pale alivyomfunua….na nguo ya kichwani ilipotoka, uso ukaonekana, ..kwa kumbukumbu za uhakika, kilichotanda usoni kilikuwa ni damu na majeraha yakuonyesha kuwa mama huyo alikatwa na mapanga, na damu bado zilikuwa zinavuja….

‘Hawa watu jamani ni wanyama..’akajikuta akisema kimoyo moyo

Lakini pia aliona kitu kingine cha ajabu ambacho kilimfanya ashindwe kuamini, kilimkumbusha jambo, jambo ambalo hakutka alikumbuke tena,..na kwa mchanganyiko wa yote hayo, akili ikashindwa kuhimili, kilichofuatia hapo ni yeye kudondoka chini…macho….macho

‘Macho, macho yana nini?’ akawa anajiuliza bila kupata jibu

Akakumbuka kuwa aliposimama ili kuangalia tena, kama akili ilivyomtuma, akakuta ile nguo iliyomfunika huyo mama usoni, ilikuwa imerudi kama ilivyokuwa, uso umefunikwa,…hiyo iliashiria kuwa kumbe mama huyo kwa muda huo alikuwa bado yupo hai,…. akataka kujaribu tena kumfunua, huyo mama akazuia…na baadaye kukaja dalili za kuonyesha kuwa huyo mama anakata roho…

Sasa hapo atawaaambia nini hao askari kuwa huyo mama yupoje…?

‘Afande,… huyu mama alijitahidi sana kujifunika, alijitahidi sana kuhakikisha hata mimi, hata mke wangu, hata mfanyakazi wa ndani ambaye wamezoeana sana, hakuna anayefanikiwa kumuona sura yake…’akasema

‘Unajua unaongea na nani?…sisi sio watoto wadogo….ni lazima kuna siku ulimuona huyo mama,…sisi tunachotaka ni uhakika tu, je huyo mama yupoje, na kwanini watu wanafikia kumuona sio mtu wa kawaida,…’akasema askari.

‘Mhh,sijasema huyo mama sio mtu wa kawaida, maana anakula anafanya kila kitu tunachokifanya, najua wengi wamehadaika na huo uvumi kuwa huyo mama ni mama wa mbinguni,..mimi sijui, maana kwangu mimi nilimuona kama mwanadamu tu….ila..tofauti yake ni hiyo kuwa matendo yake yalikuwa na utofauti kidogo na watu wengine, kwa jinsi walivyozoea..’akasema baba mwenye nyumba

‘Tunakuuliza tena hili swali kwa kumbukumbu zetu, maana kama itatokea kuwa ulimuona..na unatuficha, sheria itachukua mkondo wake, sikufichi ndugu, hapa tunaongea kirafiki, lakini ukifika kwenye anga zetu…hutaaamini…utajuta kuzaliwa..’akasema

‘Ina maana mnanitisha?’ akauliza.

‘Sio kwamba tunakutisha…, ila tunakuambia ukweli, sisi tuna njia nyingi za kupata ukweli..kuna njia hii ya kirafiki tu, kwa raia wema wanashirikiana nasi tunapata tunachokitaka basi mambo yanaishia kwa usalama kabisa lakini kwa wale wanaojifanya vichwa ngumu,..hatuna jinsi….tunakwenda kama wanavyotaka wao..hujawasikia watu kaam hao, hujawaona…..?’ akauliza

‘Afande, huko unapokwenda sio sahihi, tangu mwanzo nimejaribu kuwajibu maswali yenu, na nikawajibu kwa jinsi ninavojua, nikasema ukweli wote, ili kusaidia kama raia mwema…, kwanini sasa msiniamini kwa hili, na surayake itasaidia nini kwenu..mimi hapo sielewi ina maana na nnyie mnaamini kuwa huyo mama hakuw amtu wa kawaida….ni..ni …?’ akauliza huku akishindwa kumalizia hicho alichotaka kusema.

‘Sisi tunajua kwanini tunakuuliza hivyo na wajibu wako kutujibu,…je kama huyo mama alikuwa mhalifu sehemu fulani, na sasa kaamua kuja kujificha hapa ili asionekane…’akasema huyo askari

‘Lakini huyo mama yupo hapa,…na kwa urahis kabisa mnaweza kumuona, kwasababu keshakufa, hawezi kuzuia kumuona, au…. kama mnataka kuthibitisha kwanini msiende kumuona wenyewe,…mnaogopa nini..’akasema kwa sauti kubwa kidogo.

‘Unajua sisi tunakuuliza maswali mengine kukupima ulivyo, je wewe ni mkweli, …unaona eeh…tunaweza hata kukuuliza swali wewe ukaliona ni la kitoto, lakini sisi tuna malengo yetu..nia ni kukupima ukweli wako, ….’akasema

‘Najua….mnataka kunibambikia kesi ..nyie ndio kawaida yenu mkishindwa kupata ukweli, mnalazimishia mambo…acheni hizo bwana…’akasema

‘Ndugu, sisi tunajua ni nini tunachokifanya..naona tukuambie ukweli…ili ujue hilo,sio kwamba tunaogopa kwenda kumfunua na kumuona huyo mama, …marehemu..kwanza kwanini, tuogope, na wenzetu wapo wanaifanya hiyo kazi, tulichotaka kutoka kwako ni kujua ukweli kutoka kwako,..ukweli wao tutakwenda  kuulinganisha na ukweli halisi kutoka kwa wenzetu..sasa kama umeamua kuficha basi….’akasema

‘Mama huyo kwa shida sana, na sio kwa usahihi,  nilimuona nilipokwenda kuona kama kateketea kwa moto…’akasema.

‘Sasa kwanini ulikuwa unatuficha..ehe tuambie alivyokuwa..yupoje.?’ wakamuuliza kila mmoja akiwa na hamasa ya kusikia atakachosema huyu jamaa.

‘Nyie mliuliza niliwahi kumuona kipindi nipo naye….sio kwenye tukio la moto, ndio maana nikashindwa kuwajibu, ila…hapo alipokuwa hajitambui mimi nilimfunua nikitafuta upenyo wa kuweka vidole ili kupima mapigo ya moyo kwenye mshipa wa shingoni…kuhakikisha kuwa yupo hai, na ili aweze kupata hewa, maana alivyokuwa kajifunika asingeliweza kupumua vyema..’akasema

‘Eheee, unaona eeeh,ile hamu ya kutaka kumuona, kama ilivyo kwa wengine ikakujia, ukaona kuwa wakati ndio huo..au ulikuwa na sababu nyingine..hebu tuambie ndugu…?’ akaulizwa.

‘Sababu gani nyingine mbona siwaelewi?’ akauliza huku akiwa kakunja uso.

‘Hebu tuambie ukweli, ….wewe na huyu mama hamjawahi kujuana kabla…?’ akaulizwa swali na akajikuta kama mtu kapigwa na kitu usoni, akahisi kichwa kikilia nziiiiiiii, akakunja uso kama kukasirika , akatikisa kichwa kama kuondoa hayo mawingu, halafu akajikuta akisema;

‘Kujuana na huyu mama !?, wapi , mbinguni…au…mbona siwaelewi…?’ akauliza na kabla hajaendelea mara mkuu wa hao askari aliyekuwa kundi la kumchunguza huyo mama akaingia.

‘Samahani kuwakatiza, lakini hili ni muhimu sana..’akasema.

‘Afande hakuna shida, tulikuwa tunamuhoji ndugu yetu na tunaendelea vyema sana, na sasa tulitaka kupata ukweli wake maana yeye ndiye aliyekuwa akiishi na huyo mama, kwa kipindi cha muda,..akawa analea mtoto wake,…walipata bahati hiyo maana wenzake wanakuja kuipata ile baraka ya mkono wake, lakini wao baraka ilikuwa ndani…’akasema

‘Sawa sawa, nimekuelewa, lakini kuna jambo muhimu sana..’akasema mkuu wao huyo.

‘Ndio afande,..’akasema huyo askari aliyekuwa akimuhoji huyo baba mwenye nyumba, akimuangalia mkuu wake wa kazi.

‘Sisi tunamuhitaji huyu mtu huko …kuna kitu tumeona ni muhimu yeye awepo,..’aaksema akimuangalia baba mwenye nyumba.

‘Eti….si wewe uliyemuona huyo mama, yaani wewe ulikuwa mtu wa kwanza kumuona huyo mama baaada ya moto?’ akaulizwa baba mwenye nyumba na akili ilikuwa haijatulia vyema akasema;

‘Unasema…kwenye moto..ndio mimi ndiye niliyemuona…’akasema

‘Mbona unakuwa kama hujiamini, unaulizwa swali na mkuu…je wewe ndiye mtu wa kwanza kumuona huyo mama baada ya moto kuisha, ?’ akauliza yule aliyekuwa akimuhoji kabla

‘Nimesema ndio…kwani nimesema vipi, sijakataa..’akasema baba mwenye nyumba kwa hasira.

‘Usijali, tunachohitajia ni ukweli wako…maana wewe ndiye uliyemuona kwanza, na pia wanasema wewe ndiye uliyethibitisha kuwa huyo mama amekufa, kweli sio kweli?’ akaulizwa na kubakia kimia, akawa anajiuliza akilini ina maana yeye alipotoa kauli ile kuwa huyo mtu keshakufa, hakuna aliyetaka kuthibitisha zaidi…,

Lakini ana uhakika yeye alimuona huyo mama akikakata roho, na dalili zote za kukata roho zilikuwepo, hakumbuki kumchunguza zaidi..lakini hata hivyo..hana shaka yule mama alishafariki, kama ingelikuwa bado muda wote huu angekuwa ameshazindukana, sasa wanataka nini zaidi, ..akawa anawaza.

‘Ni kweli afande, mimi nilipofika nilimpima kwa vidole, mkononi na shingoni,…kwanza alionekana yupo hai, alikuwa hajakata roho, ..lakini baadaye akapiga zile tatu, tatata… za kukata roho, kujivuta mguu, mara tatu, akawa kimia..kimia kabisa..

‘Kwahiyo afande…mmh, na …kwa hali aliyokuwa nayo, mimi niliwaambia mtu huyo mtu keshakufa….mimi niaondoka nikawaachia wao wakiendelea, walitakiwa na wao kuthibitisha hilo…sasa mimi sijui..’akasema.

‘Je hukuhakikisha tena kwa vidole..maana mwenzetu wewe ni mtaalamu, ukajua kuwa kweli keshakata roho..?’ akaulizwa.

‘Lakini kwanini mnaniuliza maswali hayo, huyo mtu yupo mikononi mwenu, mnaye,au si yupo mikononi mwenu…bado tu mnanisakama kwa maswali ni kama vile mnanishuku kwa jambo fulani…je mumeona nini kwake?’ akauliza.

‘Swali uliloulizwa na mkuu, je uliweza kuhakikisha tena kuona kuwa amekata roho, au hizo dalili za kutikisha miguu kama mtu anakata roho, kwako zilitosheleza kuonyesha kuwa ameshafariki?’ akauliza yule askari aliyekuwa akimhoji awali, na yeye akasema;

‘Hivi…mbona siwaelewi, …ina maana huyo mtu kazindukana, kafufuka..kiukweli, hata ingelikuwa na nyie mngajua hilo…sikuwa na haja ya kumchunguza tena kwa vidole, nilijua tu ameshakufa, kwa hali aliyokuwa nayo,…na zile dalili…hata hivyo mimi niliondoka nikawaachie wengine wenye mamlaka,…je wao hawakuthibitisha…walitakiwa kuanya hivyo…’akasema.

‘Wewe uliwahi kuwa docta?’ akaulizwa

‘Nilianza kusomea…, lakini nikaishia kati nikaamua kujiunga na fani nyingine..kwasababu zangu binafsi…’akasema

‘Kwanini ulibadili fani,…hatuhitajiki kuzitambua hizo sababu?’ akaulizwa

‘Niliona hakuna muelekeo,…hasa nilipoona madocta awali walivyokuwa wanalipwa, ..maisha yao ni kama wanavyofanyiwa walimu, nikaona huko hakunifai, nikageuza kibao na kusomea mambo mengine..’akasema

‘Kwahiyo una ujuzi wa kidakitari japokuwa sio kamilifu au sio?’ akaulizwa

‘Ndio nilikuwa nimeanza kusomea,..siwezi kujinadi kuwa nilikuwa na fani hiyo, maana sikuingilia undani wake, ilikuwa ni mwanzoni tu mnafundishwa…aaah nikaona huko hapana sitakuweza, basi nikaamua kubadili mchepuo na kuijiingiza kwenye mchepuo wa masoko na manunuzi(sales and marketing) ‘akafafanua kwa kiingereza.

‘Kwahiyo kwa ujuzi huo mdogo, ukajua kuwa huyo mama amekata roho au sio..ndio mkuu anakuuliza hivyo…’akasema huyo askari.

‘Sio swala la ujuzi,..hata uzoefu tu kwa mtu mzima, ambaye umewahi kukutana na watu wakikata roho utajua huyo mama alikuwa anakata roho….maana alifikia sehemu akazima …watu wakaanza kuja,..muda huo nilishachanganikiwa, nimechoka,nikaona niondoke niwaachie wenzangu waendelee…pale kulikuwa na joto, hewa ngumu, sikuweza kukaa zaidi…ndio hivyo’akasema.

‘Unasema wewe una uzoefu wa kuona watu wakikata roho, ulishawahi kuona watu wangapi wa namna hiyo, yaani wakikata roho?’ akaulizwa.

‘Unajua maswali yenu yananipa mawazo, hiivi mnanishuku nini mimi, siwaelewi…hebu niambieni ukweli kama wanaume, je mimi mnanishuku nini mimi?’ akauliza kwa jaziba.

‘Aaaah, hebu njoo huku…’yule mkuu wao akamshika mwenye nyumba mkono, na kutoka naye hapo kwenye chumba na wale askari wawili wakasema;

‘Ei kama wanaume kweli…hahaha,….sawa mkuu,  sisi tunaendelea na mtu mwingine naona tuongee na mama mwenye nyumba, tuitieni huyo mama…sijui nay eye itakuwa mume kama mke…’wakawa wanaongea wale askari wawili, huku mkuu akiondoka na yule baba mwenye nyumba.

Baba mwenye nyumba aliposikia hivyo, akahisi kama janga sasa linaikumba familia yake, anavyomjua mkewe ataongea kila kitu, na hata kile alichokuwa akikificha yeye…lakini hakuwa na la kufanya, na hakuwa anajua nini mkewe anafahamu zaidi,..na sijui hata mfanyaakazi wao watamuhoji pia,mmh, mungu aepushie mbali ….

‘Lakin nina wasiwasi gani…’akawa anajiuliza, halafu akasema

‘Mimi sina kosa, ..kosa langu ni kulinda utashi wa mtu, kama mwenyewe hakupenda kuonekana akiwa anajitambua, kwanini nitoe siri yake akiwa hajitambui, akiwa keshakufa,..mimi naona nimefanya sahihi, ..sina kosa..’akajipa moyo hivyo

‘Lakini kwanini huyu askari ananishuku..naona kama hawa watu wananishuku, ni kama vile wanajua jambo, ambalo linanihusu na mimi,..je ni jambo gani, kwanini asema; wewe na huyu mama hamjawahi kujuana kabla

Kauli ile ilijirudia rudia kichwani mpaka akahisi kichwa kinamuuma, kichwa, ikawa kichwa akajitahidi kujizuia,lakini ikawa ni shida…na huku akizidi kusikia sauti nyingine na nyingine,..akajaribu kutiliza kichwa na sasa ikaja sauti nyingine ikisema;

Tulikuambia usiseme lolote ..kama ulimuona huyo mama, hutakiwi kusema yupoje, sasa umeanza kusema,..ole wako..utakufa..utakufa…’sauti ile ikawa inasema na ile ya awali ya afande ikawa inafifia,..kwa jinsi ilivyo, akili haipo inawaza mengine, huku kashikwa mkono na fande, anakuwa kama  anakokotwa tu hajitambui.

‘Sasa sikiliza, wewe ndiye uliyemfunua kule….kwenye tukio au sio, ukahakikisha kuwa amefariki au sio...na wewe kwa bahati nzuri una utaalamu wa dakitari au sio..’akatulia akimungalia huyo jamaa, na jamaa alikuwa katulia akiwa kwenye mawazo yake.

‘Sasa,…sisi yupo mtaalamu, ndio..lakini kapatwa na dharura….hajitambui..unemuona yule kalala pale..’akasema na mwenye nyumba akageuka kumuangalia huyo anayeonyeshwa,, akamuona ni yule askari aliyekuwa akaimfunua huyo mama, hapoa akshituka, akili ikaanza kufanya akzi tena, akauliza;

‘Kwani imekuwaje..?’ akauliza sasa akijaribu kupambana na maumivu ya kichwa

‘Aaah, nahisi hajisiki vyema, toka tulipotoka naye huko ofisini alikuwa akidai kichwa kinamuuma, sasa na tukio hili linaonekana limemuathiri sana, unajua huyu mama, haeleweki…kuna mambo tunataka msaada kutoka kwako, wewe ulikuwa unaishi naye na unamfahamu vyema, kwahiyo kwako haitakuwa ni taabu sana..’akasema

‘Kwa-kwa-kwahiyo mnataka mimi nifanye nini?’ akauliza huku akianza kuhisi jambo, akawa anaanza kujihami.

‘Usijali, au kuogopa,..unajau maiti anatakiwa sana sana kukaguliwa na wanandugu kuhakikisha kuwa ni ndugu yao, au sio..lakini pia sisi kama askarii eeeh, tunahitajia kumpiga picha ili kama ikibidi tukatangaze , ili ikiwezekana ndugu zake waje kumuona au kumchukua, au sio..?’ akauliza yule afande.
‘Sasa tatizo ni nini, kwanini hamfanyi hivyo..haina haja ya kuniomba mimi kibali..kwanza hata hivyo mimi sio ndugu yake….sio mtu wake wa karibu..ni watu tulioamua kukaa naye tu…kwani kuna tatizo hapa?’ akauliza.

‘Unamuona yule….yule yupo kitengo cha udakitari ..nilikuwa naye hapa…sasa hajiwezi, kichwa kinamshumba ndio nikaaona nikuchhukue wewe unisaidia,..si umesema wewe umesomea udakitari, unajua jua..nakumbuka uliniambia wakati naingi, si ndio…?’ akauliza

‘Hapana…nitaka..na sikuweza kuusomea..hata hivyo afande, kwani ni tatizo sana kumfunua na kumpiga picha..?’ akauliza

‘Unajua kuna tetesi kuwa huyu mama hakutaka sura yake ionekane na mtu baki..sana sana ni ndugu zake na jamaa zake, hasa nyie mliokuwa mkiishi naye karibu,..nimesikia wenzangu wakisema walikuwa wakikuhoji kama uliwahi kumuona sura ya huyo mama, na ukawa unawaelezea alivyo, au..sio, kwahiyo kwako wewe ni rahisi..au sio’akasema

‘Rahisi kufanya nini,..afande, naona nyie mnakwepa majukumu yenu, mimi, siwezi kufanya mnalotaka …naona kama…hahaha afande, nimeshawashitukia, kama huyo mwenzenu kajaribu kumfunua yaka mkuta yaliyomkuta, mnataka na mimi yanikute hayohayo..mumenoa…siwezi…’akasema huku akirudi kinyume nyume

‘Aaah, wewe si ulikuwa unaishi naye bhanaa..eeh?’ akasema huyo afande kwa sauti ya chini kwa chini.

‘Afande, kwanza kiukweli hata mimi  kichwa kinaniuma sana…naomba nikatafute dawa, …unajua nikuambie kitu kama huyu mama angekuwa hai angekitibu hiki kichwa, hua inatokea hivi, nikisemakichwa kinauma, akikishika tu kinapona…, ‘akasema

‘Oh, kumbe,…kwako haitakuwa ni shida….wewe fanya hivi, mpiga picha yupo wapi tena, tusaidia, jambo, nenda kamfunua halafu mpiga picha atafanya kazi yake na tumemaliza kazi, unasemaje?’ akawa akama anauliza

‘Afande kichwa kinaniuma..sitanii, mara nyingi kichwa changu kikiuma hivi, akinishika kichwa huyo mama kinapona, sasa ndio huyo..’akasema na kugeka kumuangalia huyo mama pale alipolazwa…ile kugeuza kichwa kuangalia,..akashituka, ule mshituka wa kama kuruka,

Na afande aliyekuwa karibu yake, akaruka hatua mbili nyuma kama kukwepa kitu, huku akauliza

‘Kuna nini tena, umeona nini….’

NB: Kidole kinauma, tuonane kesho

WAZO LA LEO:Kuna watu hupenda kukwepa majukumu yao, hasa pale wanapoona kuwa jambo hilo au kazi hiyo ina matatizo, au ni ngumu kwao,…hawataki kusema moja moja kuwa imewashida, au ina jambo ambalo wanaliogopa,… lakini hapo hapo, wanahitajia masilahi yake au faida yake au sifa kutokana na jambo hilo  au kazi hiyo. Wanachofanya watu hao ni kusakiziana, au kuwategea wengine waifanye, huku wakisubiri matunda yake wayafaidi pamoja.


Huu kiukweli sio uungwana, kama kuna jukumu au tatizo liangaliwe kihekima, au litafutiwe njia yenye muafaka kwa kusaidiana…, na sio kukwepa wajibu na kuusogeza jukumu hilo kwa mwingine kwasababu mbambali. Wajibu ni dhima, na kila anayestahiki ana takiwa kuwajibika nao, ndio kujitoa muhanga huko, kwa nia njema na kwa malengo ya kulitaua hilo tatizo, ukikwepa wajibu wako, utaulizwa,..
Ni mimi: emu-three

Wednesday, February 25, 2015

NANI KAMA MAMA-37



''Nataka kuongea na baba mwenye nyumba…..’akasema na kugeuka kushoto na kulia kuwaangalia watu waliokuwepo, na alipoona kupo kimia akaongeza kwa kusema;

‘Yupo wapi?’ akauliza askari wa kundi la kuwahoji watu, na wakati huo baba mwenye nyumba ndio alikuwa katoka kumfuatilia mjumbe, aliporudi tu akakutana na huyo askari kanzu.

‘Askari anataka kuongea nawe..’akanong’onezwa na mmoja wa watu waliokuwepo hapo.Mwenyenyumba akamsogelea yule askari na askari mwingine akawa anawaambia watu walikuwepo hapo watoke wakakakae nje, ili wapate nafasi ya kuongea na watu wanaohitajika.

‘Mimi ni askari, na ule mwenzangu,  na kazi yetu ni kutafuta ukweli kuhusiana na huo moto..kwanza nikupe pole kwa maafa hayo..najua ni hasara na ikizingatia kuwa huku kijijini hatuna huduma za bima, kwahiyo ni hasara isiyo na marejesho, au sio…?’akasema huyo askari akimuangalia mwenzake aliyefika kutoka kuwaondoa watu. Na askari mwenzake akatiskisa kichwa kukubali , japokuwa hakuwa na uhakika mwenzake kaongea nini

‘Tumeshapoa…afande..’akasema baba mwenye nyumba.

‘Kwanza tunataka ukweli…je ilikuwaje siku hiyo..kwa hivi sasa usijali hasara ukaongea kwa jaziba ukihisi hasara na kutaka kulipiza kisasi, maana …utalipiza kisasi kwa nani…’akasema

‘Muhimu ni kujua ukweli..hata kama kuna hasara lakini je hasara hii ni ya ajali kweli au ni ya watu wameamua kufanya hujuma..’akasema askari mwingine akiwa sasa nay eye katulia akiwa kashikilai kidaftari kidogo kuandika kinachoongewa.

‘Na ukweli huo hatuwezi kuupata kama hatutapata ushiriakino kutoka kwenu..na ni vyema ukatuelezea kila kitu, ili tuweze kuchanganua wenyewe, maana kuna kusikia, kuna kuona, na kuna kudhani..yote sisi tunahitaji..’akasema na mwenzake.

‘Ila mara nyingi ukifika mahakamani wao sana sana wanahitajia ulivyoona wewe…unaona…’akawa anaongea akiwa anaangaliana na mwenzake kama wanajadili jambo kabla hawajakabiliana na muulizwaji.

‘Lakini  sisi tunataka yote…si unaona hapo…, kama uliona, itakuwa ni bora zaidi..lakini kama hukuona umesikia yule aansema, huyu anaongea hivi,..tunahitaji hilo pia,eeeh,’akasema na kugeuka kumuangalai muhojiwa.

‘Hata hilo litatusaidia katika kufuatulia, au pia jinsi wewe unavyodhania..maana una maadui, kuna watu hawakupendi..kitu kama hicho…sasa hivyo unavyofikiria wewe hata lenyewe tunalihatajia ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu…’akasema askari mpelelezi.

Baba mwenye nyumba akawa katulia akiwaaangalia wanavyoongea kwa kupkezana, japokuwa alikuwa akiwaangalia na kusikia wanachoogea, lakini akili yake kwa isai kikubwa haikuwepo hapo…na akili ilivurugika pale alipoambiwa na mtu aliyekutana naye mlangoni, akimtahadharisha kwa kusema;

‘Uwe makini sana na hao askari, ni wajanja kupita kiasi, utafikiri wanaigiza lakini… ..mmh,…. sasa jifanye unajua kuongea sana, ..hao hao ukifika maeneo yao, utafikiri sio yeye..uso umebadilika, anakuonyesha kumbukumbu zake ulivyosema….sikutishi ila uwe makini..’akasema.

Kwahiyo mwenye nyumba lipofika mbele ya askari hao akawa anajaribu kuwazia, lipi la kuongea,..japokuwa watu hao wamesema aongee kila kitu….alichoona, ni kweli aliona moto, ….ni kweli alimuona huyo mama, tena akikata roho mbele yake, ni kweli huyo mama kakatwa na mapanga,..ni kweli…..’akatulia.

Ya kusikia ndio usiseme…kuwa kweli moto huo sio ajali, kuna vijana wameonekana, na kuna….oooh, kasikia mengi sana, lakini je ana uhakika nayo..hapana hapo napo natakiwa kuwa makini

Mara akili ikaanza kumuwaza huyu mama,…ambaye sasa anajulikana ni marehemu pamoja na mengi, yeye kama binadamu, hakustahili kuwawa kihivyo,yeye kwanza mwanamke….mama…hapana huo ni unyama, na yeye kama binadamu mwenye utu, anatakiwa kumtetea, hata kama kafa, lakini….mmh, nikijifanya kuongea sana nitawezeza kuishia jela au kusmbuliwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

‘Mhh, hapa naogopa, kujiingiza kwenye mambo yasiyonihusu, ..nina mke , nina mtoto, nina maisha yangu…sasa nifanyeje….’akajikuta akiongea taratibu, bila kutoa sauti

‘Sasa kwa kuanza, hebu tuambia ilivyotokea….?’ Akasikia swali likiulizwa
‘Mhh…..kabla yakuuliza hili tuanzie mbali zaidi, huyu mama…eeh huyu marehemu, wewe unamualewaje, ni nani kwako..?’ swali likaulizwa na huyo askari mwingine?

‘Sasa nijibu swali gani,…?’ akauliza

*************
‘Huyu mama ni nani kwako?’ akaulizwa

‘Huyu mama alifika hapa kwangu tu, sina udugu naye…kama raia mwema nikajitolea kumuhifadhi…’akasema.

‘Ina maana alifika kwako akakuomba hifadhi?’ akaulizwa.

‘Hapana,…sio kwamba alifika kwangu na kuniomba hifadhi..haikutokea kihivyo.., mama huyo alikuwa na kawaida ya kuja kwangu usiku na kulala upenuni mwa nyumba yangu…’ akasema

‘Kila mara alikuwa akija kulala upenuni mwa nyumba yako tu…?’ akaulizwa

‘Hapana sio kila mara, ila ni mara nyingi sana,…alikuwa akija kwangu…na usiku kunakuwa na baridi sana, ukitoka nje muda huo unamuona jinsi alivyojikunyata,..mmh kama binadamu, nikaona hapana ngoja alale banda la uwani…’akasema.

‘Wewe ndiye ulisema hivyo, au ni mke wako, au…ilikuwaje?’ akaulizwa

‘Mke wangu ndiye alitoa pendekezo hilo, na mke wangu alilipata pendekezo hilo…’akatulia kidogo, na askari hakutaka kuliuliziai zaidi akauliza swali jingine

‘Kwani huyu mama katokea wapi?’ akaulizwa

‘Sijui…’akajibu kwa mkato na askari wakawa wametuli wakijua atatoa ufafanuzi lakini haikuwa hivyo na mmojawapo akauliza;

‘Mimi naona ajabu mtu humjui kaja kwako, unamkaribisha, huoni hiyo ni hatari,wewe una kawaida ya kukaribisha watu kihivyo, au ilitokea bahati tu kwa huyo mama…?’ akaulizwa.

‘Kijijini ni sehemu yenye ubinadamu, sisi pamoja na hali zetu ngumu, lakini pale unapoona mtu anahitajia kusaidiwa unafanya hivyo,..na kwa huyo mama , sisi tuliona tunawajibika kufanya hivyo…’akasema.

‘Sisi swali letu ni hili, ni kwanini uliamua kumkaribisha mtu ambaye huna udugu naye, humjui alipotokea, na hali kwa hivi sasa sio ya kueleweka, wema unaweza ukawa ni hatari kwako, hebu tuambie ukweli, ulifanya hivyo kwa ubianadamu tu, au kuna sababu nyingine….?’ Akaulizwa na swali hili akaliona kama mtego, akajibu;

‘Kikweli afande, hatua ya kuamua aje kulala kwenye banda la uwani, haikuja kirahidi hivyo…kuna mambo yalitokea, najua umeshayasikia kwa watu wengi…kwanza huyu mama ana mambo ya ajabu, anaonekana kama hana akili sawa..’akasema.

‘Anaonekana kama hana akili sawasawa....au ndivyo alivyo…kuwa ana matatizo ya akili?’ akaulizwa
‘Kwa mimi ambaye nimewahi kuishi naye kwa karibu, siwezi kusema ana mtindio wa akili kihivyo wanavyosema watu..ndio ukimuangalia juu juu, ni kweli hana tabia za kawaida…lakini siwezi kumuita hivyo..hapana..’akasema

‘Kumuita hivyo kwa vipi, hebu faanua hapo vyema..?’ akaulizwa.

‘Mimi, nahisi kuna jambo…huenda…nasema huenda, maana sina uhakika…maana ukimuuliza mambo ya nyuma,… hakumbuki…, au huenda hataki kusema…sasa nahisi huenda ana matatizo ambayo yamefanya awe kama kachanganyikiwa,..lakini …mmh..nasema huenda..mnielewe hivyo…’akatulia alipogundua kuwa kaongea yale ambayo alitakiwa awe na tahadhari nayo…hisia zake nay a kuambiwa.

‘Unajua tunaona unaongea na kujipinga mwenyewe, unasema huyo mama alivyo, anaonekana kama kachanganyikiwa, kuchanganyikiwa maana yake ni nini..na unaposema hana mtindio wa akili, una maanisha nini,..?’ akalizwa

‘Mtu unaweza kuwa na mawazo sana ukafikia kuchanganyikiwa japokuwa huna mtindio wa akili…unapagawa tu, na ukienda kupimwa ..hutaonekana kama mgonjwa wa mtindio wa akili, kweli si kweli..?’ akawa kama anauliza na hakusubiria jibu akaendelea kuongea;

‘Na ndivyo ilivyo kwa huyu mama…mimi nahisi kuna tatizo lililomfanya awe hivyo, sizani kama ana mtindio wa akili, nahisi, naomba hapo mnielewe vyema, nahisi ana matatizo aliyokumbana nayo hadi akafikia kuwa hivyo…’akasema.

‘Hebu hili tumuachie mtaalamu wa mambo hayo, anaweza kulifuatilia hilo wakati ukifika kama ikibidi…’mwenzake akasema .

‘Sawa….tutafanya hivyo, sasa umesema hadi kumkaribisha kwako, ilichukua muda kutoa maamuzi hayo, huenda mlikuwa mnajadiliana na mkeo, huenda…mliogopa kuwa huyo mama ‘huenda’…ana matatizo ya akili, au..hebu tuambie ilikuwaje mpaka mkafikia maamuzi hayo….achilia mbali hilo la hali ya hewa, ubaridi..’akaulizwa.

‘Huyu mama ni mpenzi sana wa watoto…tangu afike hapa, utaona muda wote yupo na watoto, anatembea mitaani akiimba na watoto….akiona mtoto analia, atamuhurumia sana, na kumuendea mwenye mtoto kuomba ambembeleze…sasa hapo ndipo watu wakaanza kumuona ni mtu wa aajabu…’akasema

‘Mtu wa ajabu kwa kupenda watoto…!?’ akauliza askari kwa mshangao.

‘Mtu wa ajabu kwa vile kama kamuona mtoto analia, akamchukua yeye mtoto huyo hutulia, huacha kabisa kulia, hutaamini lakini ndio hivyo…’akasema.

‘Ni kwamba anajua vyema, kubembeleza sana watoto kwa vile anawapenda..au inakuwaje?’ akaulizwa

‘Hapana,..sio hivyo…yeye kwanza anamchukua mtoto ……eeh, hambembelezi sana,…’akaonyesha kama kambeba mtoto na kuigiza wanavyombembeleza mtoto.

‘Yeye anachofanya ni kumshika huyo mtoto kichwani na kusema;  ‘mtoto mnzuri nyamaza eeeh…’’yaani hivyo tu, mtoto anatulia na kunyamaza, na hata kucheka…ni ajabu kabisa….’akasema

‘Mhh, hilo unalionaje mwenzangu…’wakaulizana wakiangaliana huku wakionyesha kutabasamu kama vile ni kitu kisichoaminika.

‘Mhh, labda uone kwa macho yako,….yaani yeye anaweka mkono wake kichwani kwa mtoto aliyekuwa akilia sana…na kwa hali hiyo wewe kama mzazi, mlezi ...hujui kwanini mtoto analia si ndio…labda mtoto kanyamaza..nasema, `huenda mtoto huyo alikuwa na  sehemu inamuuma, au alikuwa akihitajia nyonyo ya mama yake..sasa anakuja huyu mama,  yeye bila kujali hayo anamshika mtoto kichwani, mtoto ananyamaza, na kuanza kucheka…ndio hivyo….?’ Akaulizwa

‘Afande hata mimi nilipoambiwa hivyo nilikataa..sikukubali haraka kihivyo…, hadi niliposhuhudia kwa macho yangu mwenyewe..’akasema

‘Ulishudiaje…hebu tuelezee..’akasema huyo askari.

‘Kuna siku mtoto alikuwa akilia mimi mwenyewe nilikuwepo hiyo siku,…nikaona nimchukue mwenyewe, nijaribu kumbembeleza, nikahakikisha mtoto hana kitu cha kumpa joto, kila kiuongo kipo safi… nikambembeleza weeeh, nikachemsha nikampa mama yake, akafanya hivyo, na kujaribu kumnyonyesha, lakini wapi…akachmesha..’akasema

‘Haat nyono ya mma yake alikataa..?’ akaulizwa, hapo mwenye nyumba akajibu kama alivyoulizwa, hakusem zaidi kuhusu nyonyo anayotumia mtoto kwa njia ya kuficha jambo akasema

‘Hata nyonyo aliyompa mama yake pia alikataa., ..tulihangaika wee, na mara tukamuona mfanyakazi wa ndani akakimbia nje..haikuchukua muda yule mfanakazi akarudi akiwa na huyo mama, yule mama akamchukua huyo mtoto, akamshika kichwa, na kusema maneno kama hayo, ..haya mtoto nyamaza eeh, nyamazaeee..’mtoto akanyamaza..’akasema

‘Labda alishachoka kulia..labda sehemu iliyokuwa ikimuuma ilishatulia…labda…hilo mimi siwezi kulithibitisha kuwa kweli inaonekana huyo mama ana kipaji hicho..hebu niambie wewe licha ya kuliona hilo kuna nani na nani alifanyiwa hivyo mpaka ukakubali kuwa mama huyo ana kipaji..ana..nini tuseme…uwezo wa kumtuliza mtoto anyamaze…?’ akaulizwa

‘Mimi nina mtoto mdogo..mtoto wangu alikuwa na tabia ya kulia lia kipindi fulani…huyu mama akaliondoa hilo tatizo,…watu , majirani, waliokuwa na watoto wao wanaolia lia, au wana matatizo kama dege dege…kushitika shutuka na kupiga kelele,..’akatulia kama anawaza.

‘Na..na vitu kama hivyo…wengine  hata watu wazima wana matatizo ya kichwa kuuma tu ukija kwake akakushika kichwa, akasema haya kicha pona, kama sio kichwa cha maradhi pona…kichwa kinatulia….lakini kwa watu wa kubwa sio sana,…yeye hasa ni kwa watoto kulia..kuna kule kulia kusipo kwa kawaida,..mtoto analia hadi kukakamaa, si kuna mataizo kama hayo…’akawa kama anauliza na kuendelea kusema;

‘Basi, mama huyu anauwezo wa kuyaondoa hayo matatizo hayo kwa watoto..hasa kwa watoto kwa mkono wake tu…’akasema

‘Mhh..hilo nalo linahitaji utaalamu wake eti mwenzangu, unalionaje hilo, mimi nahisi lina hitajia utaalamu…kulithibitisha…sasa kutokana na hilo ndio ukaamua aje akae kwako, kwa kulipa fadhila au?’ akaulizwa

‘Kama nilivyosema, mama huyo kwa kiasi kikubwa alipenda kuja kukaa eneo la nyumba yangu..hasa wakati wa usiku…, na usiku akawa analala upenuni mwa nyumba yangu…mhh, kibinadamu,….hapana hatukuweza kuvumilia, hatungeliweza kumfukuza…’akasema na kukaza macho kuangalai mbele, huku skiendelea kuongea;

‘Na mtoto wetu akawa anampenda sana huyo mama,….akiwemo huyo mama, mtoto wetu anakuwa na raha muda wote, utafikiri yeye ndiye mama yake aliyemzaa,..ikafikia muda…, tukaona kwanini tusiwe na ubinadamu…basi siku moja mimi na mwenzangu tukaamua huyo mama awe analala chumba cha uwani…’akasema.
‘Wengine pia wana watoto au sio, na hufanya hivyo kwa wengine kama anavyofanya kwako, au sio..lakini nyie ubinadamu ukawazidi..nahisi kuna jambo zaidi..huenda kuna kitu mlitegemea kutoka kwake, ….hebu tuambie ukweli…’akasema askari.
‘Kitu gani kutoka kwa mama kama huyo..hakuna ..ni ubinadamu tu….’akasema

‘Nyie mna mfanyakazi wa ndani?’ akaulizwa

‘Yupo, tunaye, alikuwepo hata kabla ya huyo mama hajafika kukaa na sisi..’akasema

‘Kwahiyo huyo mfanyakazi yupo anamlea mtoto na kazi nyingine za ndani, na akaja huyo mama, na wote wakawa wanaishi pamoja,..na huyo mfanyakazi akiwa na mtoto akianza kulia hata yeye ambaye tunaweza kusema mtoto kamzoea zaidi kwa vile anashinda naye mtoto…mtoto akianza kulia hanyaamzi hadi huyo mama awepo?’ akaulizwa

‘Kuna kipindi mtoto analia kupitiliza..nazungumiza kipindi hicho, kuna kule kulia kwa kawaida,..huko ..aah,…sasa mtoto akianza kulia kwa hali hiyo..ile hali ya kulia kusipo kwa kawaida..hataki mfanyakazi mama wala baba…, ni mpaka huyo mama afike..ndio ananyamaza..’akasema.

‘Hebu niambie tatizo hilo la kulia watoto mnalichukuliaje,..lilikuwepo kabla au baadaya huyo mama kufika ndio likazidi, kwa mtizamo wako, umelionaje hilo?’ akaulizwa

‘Watoto wanalia ..ni kawaida lakini kuna kilio kingine sio cha kawaida..ilikuwepo…mimi nakumbuka hata wazazi wangu walishaniambia hivyo..inatokea, hukuna sababu, …ni hali ya makuzi…’akasema na kutulia.

‘Hebu nikuulize hivi, sitaki ujibu kama alivosema mama yako au nani..nauliza katika ujuvi wako, hapa kijijini, …hii hali ilikuwepo, watoto kulia, au hata ilikuwepo, lakini unavo wewe imezidi zaidi baada ya kuonekana kwa huyu mama?’ akaulizwa

‘Nataka unielwe na mimi hivyo,..maana tusikuze mambo, huku kijijini watu wanapenda kukuza, utasikia ooh, bundi kalia usiku msiba, oooh, nyoka wa vichwa viwili..ni hisia kwa vile ilitokea ikatokea..mimi japokuwa naishi huku lakini sipendi sana hizo hisia…na imani hizo, nashkuru hata mke wangu anaelekea huko..’akasema

‘Sawa..lakini ulivyoona,..sema ukweli wako,…’akaambiwa.

‘Kiukweli..kuna hali ya kuzidi…siji ni kwanini, lakini siwezi nikasema limetokana na huyo mama,..hapana, ..labda ni hali ya hewa..na sio kwamba halikuwepo kabla..hapana…kwa watu wenye watoto wanalifahamu sana, kuna kipindi mtoto analia tu….unajua mtoto hawezi kuongea, kuongea kwake ni kulia..sasa siwezi kusema hilo tatizo halikuwepo,…lilikuwepo, na limekuja kipindi huyu mama yupo, sasa yeye anabebeshwa lawama…’akatulia.

‘Kwahiyo hiyo dhana ya watu kuwa watoto wameanza kulia sana alipofika huyo mama wewe kwako sio kweli?’ akaulizwa

‘Mhh..mimi hapo sijui..mimi kama baba muda mwingi nakuwa kazini..sasa kama kuna kuongezeka kwa kulia kwa watoto baada ya huyu mama kuja,mimi sijui…labda kwa hao wenye watoto siku ningi, ..ila mimi siwezi kukubali huo usemi..’akatulia kama anawaza jambo.

‘Wewe unamtetea huyo mama, kwa vile ni marehemu au kwa vile umeishi naye na umafahamu au kuna nini mpaka usiwe na msimamo sawa na wenzako?’ akaulizwa

‘Hahaha..afande, mimi nimtetee huyo mama kwa lipi….mtu simjui…nasema ukweli tu….lakini…wenzangu huenda wana mtizamo wao, siwezi kuwapinga, ila mimi nasimamia kama mimi..’akasema

‘Na huoni ajabu, watoto wengi kuletwa kwa huyo mama, kama ingelikuwa ni kawaida wasingelisumbuka ..wewe walionaje hilo?’

‘Mimi, nahisi kwa vile imetokea hivyo kuwa huyo mama akifanya hivyo mtoto hutulia, basi hata mtoto akilia kidogo tu, kikawaida..kihivyo…basi wazazi wanachukulia …kihivyo.. kitu ambacho kilikuwepo…ni imani  tu..mimi naona ilikuwepo, sema watu walikuwa hawalichukulii maanani..’akasema.

‘Kwahiyo kutokana na hali ya ..hewa, kutokana na kipaji cha huyo mama, kutokana na upendo wake kwa watoto, nyie mkaona mchukue nafasi hiyo,..mumuwahi huyo mama mapema ili aje kukaa kwenu,..kuna fadida ndani yake vizawadi eeh.. si ndio hivyo..au kuna sababu nyingine, maana huyo mama ni mgeni hamjui wapi alipotokea, pia wengine wanahisi kuwa ana matatizo ya akili…?’ akaulizwa

‘Kama nilivyosema, maamuzi hayo ya kumchukua, sio maamuzi ya siku moja..ilichukua muda, …nikuambie ukweli afande, hebu fikiria na ubaridi ulivyo huyo mama kajikunyata, anahangaika kujifunika na kiganja cha mkono, anatetemeka baridi unatoka unamuona alivyolala kwa shida..hapana… utu ulijaa…’akasema na kuweka mkono kifuani

‘Utu…’afande mmoja naye akaweka mkono kiuani kumfuatishia.

‘Ndio utu…hata kama ingelikuwa ni wewe, …utu utakuingia tu, hata kama una kutu ndani ya moyo, kutu italainika na kubakia utu, huruma ya kibandamu itakutawala…pamoja na mengineyo, lakini kwangu mimi hilo lilinigusa sana, hata mke wangu alipotoa pendekezo hilo, mimi nilimkubalia tu…’akasema.

‘Uliwahi kuongea na huyo mama kwa karibu?’ akaulizwa

‘Mara chache sana..’akasema

‘Hizo mara chache mliongea nini?’ akaulizwa

‘Niliwahi kumuuliza yeye ni nani, katokea ,….jina lake ni nani..’akasema

‘Ulipata majibu yake..?’ kaulizwa

‘Majibu yake…hahahha..’hapo akacheka, na wale maaskari wakaangaliana na kuuuliza;

‘Mbona wakacheka…kuna cha kuchekesha hapo..?’ akaulizwa

‘Labda kwa hayo majibu ndio unaweza kusema huyo mama huenda …lakini mimi siwezi kusema ana mtindio wa akili..sijui wa ubongo,…majibu yake yanakuwa hayana uhalisia..’akasema

‘Alikujibuje..ndio swali letu…sizani hilo jibi linachekesha au…’akaambiwa

‘Jina laki nani…anajibu `mama mtoto….’ Nimekuuliza jina lako nani, atasema; ‘Nani kama mama…ukiuliza tena jina lako nani….’namtaka mtoto wangu…jina lako nani…anatoa majibu yasiyoendana na  swali…yaani majibu ni mengi tu…’akasema

‘Haya ulipomuuliza katokea wapi alisema nini?’ akaulizwa

‘Katokea mbinguni…’akasema na askari wakaangaliana

‘Anaseme hivyo, kuwa katokea mbinguni au watu ndivyo wanavyosema…au wewe wasema hivyo?’ akaulizwa

‘Mimi nilimuuliza swali umetokea wapi, akajibu nimetokea mbinguni, wasikia sana…nikamuuliza mbinguni wapi, akaangalia juu kuniashiria hivyo…’akasema

‘Unasema ulimuuliza swali, yeye ni nani, na baadaye ukamuuliza jina lake ni nani…?’ kwanini ukauliza maswali yenye mtizamo mmoja, ..ulitarajia majibu gani na kwanini ukauliza maswali kama hayo….sijui umenielewa hapo,..hebu fikiria unamuuliza mtu wewe ni nani, na baadaye unamuuliza jina lako ni nani…?’ akaulizwa

‘Ni kweli nilimuuliza hivyo nikiwa na maana yangu, nilimuuliza yeye ni nani..maana hafahamiki,..haeleweki, ni mwanadamu au ni mtu gani, maana ….hahaha’akacheka kidogo na askari wakaangaliana tena na mmoja akatabasamu na mwingine akacheka kabisa…

‘Maana nini…?’ mwenzake akauliza akiwa anatabasamu, ..kiukweli hawa askari wanavyoongea hapo, waliondoa kabisa ile hali ya uaskari, ya kukunja uso, ukakamavu, kulazimisha jambo, waliongea kama raia, …hii imewawezesha kupata taarifa kwa watu bila kuogopwa, lakini wanaowafahamu, ukifika ofisini kwao, hutaamini, kuwa ni hao hao waliokuwa wakiongea kwa tabasamu mitaani.

‘Watu walishavumisha kuwa huyo mama sio wa kawaida…ni mama kutoka mbinguni, ..na mimi nilijiwa hivyo hivyo baadaye..kabla nilisikia hivyo…, au sio…’akasema akma anauliza

‘Wengine wenye imani zao,….tunatofautiana walidiriki kwenda mbali n akumuita eti ni malaika..ajabu kabisa na wale wenye nia mbaya wakamuita shetani…wengine wakamuita…’akashika kichwa kama kutafakari jina, halafu hakumalizia akasema

‘Ndio maana nacheka, kwani hata mimi nilishindwa nimuoneje huyo mama…ni mtu kawaida, au kachanganyikiwa,…., je ni binadamu, na je ni hivyo wanavyotafsiri watu..basi mimi nikajikuta namuuliza hilo swalo, wewe ni nani…nikajiona na mimi kama nimetekwa ndio maana najicheka…’akasema

‘Yeye alikujibuje, ulipouliza swali kama hilo….?’ akaulizwa

‘Mama mtoto…’akasema

‘Mama mtoto!…hilo jibu,…walionaje,  ni kama vile wewe ulizaa naye, kwahiyo anakutanabahisha kuwa yeye ni mama wa mtoto wako, au….’akasema na mwenye nyumba akawa kama kakereheka, akageuka upande wa pili, halafu akasema;

‘Hilo ndilo jibu alilonipa…na mimi simjui, mimi nina mke na mtoto, angekuwa mke wangu amesema hivyo ningekubaliana na kauli yako..lakini huyu ni mtu nisiyemjua, katokea wapi sijui,….anasema hivyo..nilichukulia hivyo kuwa hajui analoliongea..na jibi sio hilo tu..ukimuuliza swali hilo hilo atajibu vinngine..’akasema

‘Hakuwahi kusema mimi ni mpenzi wako, mimi ni mke wako, mimi..vitu kama hivyo..?’ akauliza askari akiwa haonyeshi tabasamu mdomoni.

‘Hapana sikuwahi kusikia jibu kama hilo..’baba mwenye nyumba akasema baada ya kumuangalia huyo askari kwa muda bila kumjibu.

‘Kwa majibu hayo…wewe huoni kuwa mama huyo hayupo sawa,…hukubali kuwa ana matatizo ya akili..au..?’ akaulizwa

‘Sijsema hivyo….’akasema

‘Kama hana matatizo ya akili…ina maana yote aliyokuwa akiyajibu yana usahihi, anajua ni nini anachokisema, yana mantiki….au….na unakiri kuwa yupo sawa, kama ana akili sawa, kwanini atoe hilo jibu kuwa ni `mama mtoto’….?’ Akaulizwa nay eye akakaa kimia, na huyoa skari akasema;

‘Sio kwamba tunakutuhumu, sisi tunajaribu kutafsiri haya maneno yake huenda yana ujumbe tusioujua na tukujua tunaweza kugundua jambo…..’akasema

‘Afande…mimi smjui huyu mama..na kusema hivyo, unaweza kutafsiri upendavyo maana inaweza ikawa ni mama wa mtoto fulani..akini sio maana ya kumaanisha kuwa ni mama wa mtoto wangu..kuwa labda mimi nimezaa naye la khasha….’akajitetea hivyo.

‘Swali muhimu…uliwahi kuiona sura yake…maana nasikia muda wote kajifunika usoni?’ akaulizwa

‘Mwenyewe umesema ..na kujipa jibu mwenyewe..mama huyo muda wote kajifunika kichwani, ningemuonaje..’akajibu akionyesha kuwa kidogo alishakirihika na swali lililopita, na watu hao walishagundua hilo na kwao ni muhimu sana.

‘Mtu mumeishi naye nyumba moja..hata siku moja usipate muda wa kuiona sura ake haijatokea akajifunua, au ikatokea ukaingia kwake ukamkuta hajajifunika..au mke wako hakuwahi kumuona…?’ akaulizwa.

‘Nikuambie ukweli, akina mama kama hao wanakuwa makini sana…inaweza ikatokea bahati mbaya kama unavyosema, lakini akigundua atajifunika haraka sana..na kama hukuwa makini huwezi kugundua ..kukumbuka alivyokuwa, na kwa vile najua kuwa muda wote anajifunika, siwezi kuwa makini na hilo…’akasema.

‘Tunataka hiyo bahati mbaya, ilitokea…swali je uliwahi kumuona sura yake iwe bahati mbaya, au …vinginevyo, kukusudia kutaka kumuona, …unaweza kama mdadisi kutaka kuona anafananaje, huyu ni nani maana ni mtu kaja kwako, kama mchungi wa familia, kama mlinzi wa familia, unatakiwa kuwa makini na watu wasiojulikana, je wewe hukufanya hilo, kwa nia njema tu ya uchunguzi…, ya kiusalama..?’ akaulizwa.

‘Mhh..,kama ilitokea, ilikuwa bahati mbaya,..lakini ….’akasita na kumbukumbu za tukio hilo zikamjia akilini…

‘Sawa…ilikua bahati mbaya….hatuna nia ya kumzalilisha, maana ana sababu yake kujifunika hivyo na wewe unalinda utashi wake, au sio….yeye yupoje, anafananaje…ni binadamu kama wengine au….maana watu wamesema mengi, wengine huyo ni shetani , wengine..yaani kila mtu kasema lake, ..je wewe ulipomuona ulimuonaje….?’ Akauliza askari na jamaa akajikuta kaduwaaa..akili ikawa sasa haipo hapo,na kuna kitu kikawa kinamkanya, sauti ikawa inasema akilini

‘Usiseme..ole wako useme..unakumbuka eeh,.., waliosema ukisema unakufa…hebu kumbuka wenzako, hivi hawajitambui, usiseme utakufa…..utakufa..utakufa..’neno utakufa likawa linajirudia rudia akilini….

NB: Haya mambo ndio hayo


WAZO LA LEO: Siri ya mtu uitunze, moja ya dalili za mnafiki ni mtu kupewa siri akaahidi kuitunza, na badala yake akaitoa, pi a ni mtu akongea huongopa…. Kuna marafiki wanakutana na mmoja anamuelezea mwenzake siri yake anamuambia usije kusema kwa yoyote yule,,,,na huyo rafiki anakutana na mpenzi wake, au yupo yeye na mke wake ambaye waliahidiana kutokifichana siri , na huyo mkewe akauliza jambo lile lile aliloambiwa na rafiki yake asimwambie yoyote,au mkewe akataka kujua walikuwa wakiongea nini na rafiki yake…swali hapo, wewe kama wewe utafanyaje?
Ni mimi: emu-three

Tuesday, February 24, 2015

NANI KAMA MAMA-36


‘Kuna nini tena huko ndani, mliambiwa hamuhusiki sasa mnakimbia nini..?’ akauliza baba mwenye nyumba naye akijaribu kutafuta upenyo wa kuona ni nini kinachotkea huko ndani, walipo polisi na huyo mama wanayemchunguza

Mara mmoja wapo aliyekuwa pale mlangoni, ndani akatokeza na kumwambia baba mwenyenyumba;

‘Huko ndani naona hakukaliki, ...mimi naona nijiondokee zangu..’akasema

‘Kwani wewe umeona nini?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Hata sikuona vyema, maana nilipopata upenyo wakuangalia...nikamuona askari mmoja yupo chini, na mwenzake anataka kukimbia…’akasema na mwingine akadakia.
‘Asari anakimbia....! hapana, sio kweli, labda hukuona vyema, mimi nasikia askari hawaogopi uchawi..’akasema mtu mwingine.

‘Kwani ilikuwaje?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Ohh, kweli yule mama hatakiwi kufungulia, hata akiwa mfu …hutaamini yule askari aliyekuwa akimfunua kala mwereka,..kadondoka chini na mwenzake ....mimi nimeona kwa macho yangu mwenyewe...’akatokea mwingine akiongea huku akionyesha hamasa.

‘Yule askari aliyekuwa akitoa amri, kuona mwenzake kala mwereka...akageuka kukimbia..’akasema huyo aliyetokea ndani.

Baada ya huyo mtu kusema hivyo, kila mtu akakimbilia pale mlangoni kutizama ndani, na wale waliokuwepo ndani ambao walikaidi amri ya askari kuwa wasiingie ndani lakini baadaye wakaingia kwa uchu wa kujua kinachoendelea, wakawa sasa wanataka kutoka nje, wakionyesha wasiwasi, na kwa hali hiyo ikawa sasa ni mgongano pale mlangoni, wanaotaa kutoka, na wanatotaka kuingia kuona kilichotokea.

‘Tupisheni tupite…hili sasa ni balaa..’wakawa wanasema waliokuwepo huko ndani

‘Kwani kumetokea nini?’ wakauliza waliokuwepo nje, na baba mwenye nyumba ambaye pale aliposimama hakuweza kuone vyema, akawa anahangaika kuchungulia lakini hakuona kinachotokea zaidi ya askari mmoja kuwa yupo sakafuni, na mwenzake akiwa kasimama huku akiwa anaangalia pale alipolazwa huyo mama.

Haikupita muda akatokea mjumbe mlangoni, mjumbe alikuwa ndani na sasa anataka kutoka nje, na wale waliokuwepo nje walipomuona mjumbe wakaona ndiyo nafasi yao ya kujua kilichotokea huko ndani, wakambana kwa maswali;

‘Ehee mjumbe wewe umetokea ndani, kwanza tuambie kwanini unatoka mbio mbo kama unakimbia...?’ akauliza mtu mmoja

‘Mjumbe tuambie kumetoeka nini huko ndani mbona watu wanakimbia kutoka nje..?’ akauliza mtu mwingine

‘Ohooo, sina muda wa kujibu maswali yenu, kwanza niacheni nipite,..mimi niliwaambia hawakutaka kunisikia...yule mama sio wa kawaida, wakaona mimi ni naamini ushirikina...sasa unaona....wenyewe wamathibitisha..’akasema

‘Eheee..ona eeeh, sasa mjumbe tupe picha kamili....imetokea nini....maana haya mambo uyaone mwenyewe..’akasema mtu wmingine.

‘Hawakutaka kuamini yamekuwa kama yale yale .....ya hao walioambiwa hakutaak kusikia,..., nasikia hata hao washukiwawa humo moto japokuwa jawajakamatwa… hali zao ni mbaya…wanaweweseka ovyo…’akasema mjumbe na aligeuka upande wa pili akamuona baba mwenye nyumba akashituka na kugeuka upande mwingine akitafuta sehemu ya kupita, huku jamaa mmpja akiendelea kumhoji mjumbe

‘Ina maana unawafahamu hao watu mjumbe..hao washukiwa wa moto, kumbe kweli kuna watu walifanya hujuma, mjumbe unawafahamu ni akina nani?’ akaulizwa

‘Hapana nimesikia watu wakisema tu..oh, jamani niacheni maana nina haja….nataka kwenda haja…nipisheni jamani, waliyoyataka wameyapata…nipisheni nitawakojolea..’akasema mjumbe huku akiharakisha kutoka nje, na alipopata upenyo, mbio akatokomea upande wa pili ambapo haonekani.

Tuendeele na kisa chetu


‘Ina maana ni kweli kuwa kuna hujuma zilifanyika, na mjumbe anafahamu hili,…wamechoma nyumba yangu kwa …aaah, …hapana ?’ alikuwa baba mwenye nyumba ambaye aliweza kumsikia mjumbe pale aliposema;

‘’….nasikia hata hao washukiwawa huo moto japokuwa hawajakamatwa… baadhi yao hali zao ni mbaya sana…wanaweweseka ovyo…’’

Na jinsi alivyoshituka alipomuona baba mwenye nyumba inaonyesha dhahiri alitaka kuongea mengi, ila alikatisha tu alipomuona baba mwenye nyumba,..

Baba mweny nyumba akageuka kuangalia upande ule alipoelekea huyo mjumbe hakumuona, …alishatokomea upande wa pili wa nyumba, ambapo hakuna choo, sasa sijui alikuwa anakwenda haja ipi, yaonyesha kabisa mjumbe alikuwa na nia ya kuondoka hapo.

Baba mwenye nyumba akaamua kumfuata , akijia huenda atamkuta hapo nje, au au kama kaamua kuondoka atamkuta akiwa hajafika mbali, ..akatafuta upenyo na kutoka nje, akaangalia huku na kule hakuona dalili za mjumbe, akajaribu kuwauliza watu walikuwa wanakuja hapo kama walimuona mjumbe, na watu hao wakasema hawajamuona.

‘Atakuwa kaenda wapi..?’ akajiuliza na alipohakikisha kuwa kweli mjumbe keshakimbia, hayupo sehemu ya kuonekana akaamua kurudi ndani tu.

Akilini mwake, hata yeye alishahisi huenda moto huo si wa ajali, lakini hakutaka kuweka tetesi za uvumi kichwani mwake, akajipa moyo kuwa akikutana na mjumbe atamdadisi ili ajue vyema, akakumbuka jinsi mke wake alivyoongea walipokutana baada ya kutoka kule kwenye jengo lililoungua….
‘Mume wangu una hatari kweli, sasa ni nini kilikupeleka huko, na hali moto bado ulikuwa haujazimika vyema..angalia ulivyounguza hiyo shati…na mbona una damu..?’ mkewe akamuuliza na alipogundua hilo, akakimilia ndani na kubadili shati, akatoka na kukutanana mkewe.

‘Mke wangu sasa tutafanyaje,…maana sasa huu ni msiba na upo haa[a nyumbani, inabidi utoe akiba yao, kuwahudumia watu…’akasema mume mtu.

‘Kwani wanasemaje,..ulihahakikisha wewe mwenyewe kuwa amekufa..?’ akauliza mkewe.

‘Ina maana hmjaamini kuwa kafariki…nimemshuhudia mwenyewe akikata roho..muhimu kwa sasa ni kuona tutajipangaje…tukijua huu msiba ni wa hapa, labda watokee ndugu zake…’akasema mume mtu.

‘Haya sisi tunawasikiliza nyie.. ujue pamoja na yote huenda huyu mtu ana ndugu zake, hatuwezi kutangaza msiba huo kama wetu, wakati ndugu zake wapo..inabidi kuangazwe kama kuna mtu anamfahamu, au ana tetesi zozote wapo anapotokea..’akasema mke wake.

‘Tumekaa naye hapa, hakuwahi kusema ana ndugu, hajui ..na sina uhakika kama anaficha…mimi nahisi hataki au hakuwa anaelewana na ndugu zake…sina uhakika..’akasema mume wake.

‘Yote hayo hayatasaidia kitu…mimi naona tujipange tu, kuwa msiba ni wetu…’akasema mama mwenye nyumba.

‘Basi ngoja niongee na mjumbe nitarudi baadaye, tatizo mjumbe yupo na askari, wanamuhoji,..’akasema

‘Lakini mumewangu kuna kitu nataka kukuambia…’akasema na kumshika mume wake, wakasogea mbali kabsa na watu, akasema;

‘Mume wangu unasikia watu wanavyosema..eti moto huu umewashwa na watu wakikusudia kumuua huyo mama, wanadai huyo mama ni mchawi, kwahiyo watu wakaamua wamchome moto…’akasema mke wake.

‘Maneno hayo umeyasikia kutoka kwanani, usiwasikilize watu, najua yatasemwa mengi ..sisi kwa hivi sasa tuchukulie ni ajali tu…maana tukitaka kudadisi sana, tutazidi kuumia, na hasara tumeshapata hata aikijulikana kuwa kuna watu wamefanya hivyo, unafiri tutajengewa, hiyo imekula kwetu....’akasema mume wake.

‘Mimi nakuambia nilivyosikia kwa watu,..hata mimi sikutaka kuamini mambo yao, lakini kuna wanawake watatu wanasema waliona kwa macho yao wakiwa wametokea mjini …’akasema

‘Wanawake gani hao, na wameonaje?’ akauliza mume mtu akiwa na hamasa, mke mtu akageuka huku na kule kuhakikisha hakuna mtu anayewaona au kuwasikiliza wanachoongea, alipoona kuna uhakika wa kutokusikiwa akasema;

‘Mume wangu…hao akina mama ni wenyeji wa hapa,..ni mabinti wanaofanya akzi mjini, mimi naona wewe huna haja ya kuwajua,maana wanawake wenyewe hawajatulia, ukikutana nao, nikujuavyo..mmh,...’akasema

‘Mke wangu ina maana huniamini, hilo limetokea wapi tena,..yaani bado tu..aah, kama mambo yenyewe ni hayo haina haja ya kuniambia, wewe rudi kwa akina mama muendelee na mipangilio….’akasema mume mtu.

‘S.ilaio kwambasikuamini….ila sizipendi tabia zao , nilishawahi kuongea nao…sasa wao wakati wanatokea mjini, wakati wanapita, wakaona kundi la vijana,…kama watano hivi au zaidi, ilikuwa ni usikuwa giza..hakuna mbalamwezi,…walimuona mmojawapo akiwa na galoni , hizi za mafuta ya taa..’akasema.

‘Hao wanawake usiku wote huo walikuwa wanatokea wapi?’ akauliza mume mtu.

‘Hao wanawake wanafanya kazi mjini, inavyoonekana walikuwa wamekuja likizo, wao walisema, gari lao liliharibika walipofika maeneo ya huku kwetu ni mbali …, walisubiria sana gari hilo litengenezwe, lakini halikutengemaa, ikabidi waanza kutafuta njia za kufika huku, kwa mgu ni mbali sana,…wakahangaika mpaka kukatokea gari moja ndipo wakaweza kuletwa hadi hapo njia panda, na wakawa wanatembea kwenda majumbani mwao..

‘Sasa walipofika eneo karibu na nyumbani kwetu, kwanza wakahisi harufu ya petrol, wakawa wanaulizana, harufu hiyo imetokea wapi…mara wakawaona watu wakitembea kuzunguka eneo la nyumba yetu..wakasikia mmoja akisema;.

‘Lazima yupo humo ndani…hakuan sehemu nyingine ya kutokea..’mmojawao akasema, na ara wakaonekana hao mabinti, na hakukuwa na njia nyingine ya kujificha

‘Wanadai kuwa wale vijana walipowaona hao mabinti wakaanza kuwakimbiza hao wasichana,hao wasichana wakatimua mbio, kila mmoja kivyake…walikimbizwa hadi wakafika mbali na baadaye hao vijana wakarudi, inaonekana hawakutaka kuendelea kuwafukuza hao wasicahana. Baadaye wale wasichana wakakutana na kwenda kulala sehemu moja kwa mmoja wao.

Wale vijana wakarudi wakijua wana kazi ya kufanya..’akasema

‘Kwahiyo hawakuthibitisha kwa kuona huo moto ukiwashwa na hao vijana …?’ akauliza mume mtu.


‘Hilo hawakuthibitisha, ila waliona hao vijana wakiwa na galoni,..na harufu ilisikika wazi kuwa ni ya petrol , kwahiyo hiyo harufu ilikuwa na maana gani, ina maana walishamwaga hiyo petrol..’akasema.

‘Walimwaga wapi, nani aliwaona wakimwaga..polisi watakuhoji sana ukitoe taarifa za tetesi…je waliona dalili kuwa petrol hiyo ilimwagwa wapi?’ akauliza mume mtu.

‘Ina maana hunielewi,..hao wasichana hawakuona maana wao walipofika hapo, na kuonekana tu, walikimbizwa..na walisikia hiyo harufu wakati wanapita wakawa wanaulizana kuhusu hiyo harufu ndipo wakawaona hao vijana mmoja akiwa na galoni..sasa wangejuaje hiyo petrol ilimwagwa wapi..’akasema mama mwenye nyumba

‘Kwahiyo kwa kifupi ni kuwa hawakuona wapi wapomwaga hiyo petrol, na hawakuona moto ukiwashwa...ila walihisi harufu tu…na kuwaona hao vijana…hawa ushahidi kuwa ndio wao waliwasha huo moto…’akasema.

‘Ndio hivyo….’akasema mke mtu

‘Huo ushahidi hautoshi mahakamani....maana hao vijana wakikamatwa watadai kuwa kweli walikuwa na galoni ya petrol, na huenda hiyo petrol ilimwagika kwa bahati mbaya wakati wanakwenda kwenye shughulizi zao..je hao wasichana hawawezi kuongea na polisi?’ akaulizwa.

‘Hao wasichana hawapo, ..’akasema mke mtu

‘Hawapo! si umesema walitokea mjini, wamekuja likizo au kuwatembelea ndugu zao au sio..sasa iweje waondoke haraka kihivyo? Akauliza baba mwenye nyumba

‘Ndivyo ilivyokuwa,…kuwa wamekuja likizo, au mapumziko ya siku kadhaa,… lakini wanadai walipata taarifa usiku huo huko, taarifa za vitisho kuwa wakionekana hapa kijijini watauwawa, kwahiyo asubuhi na mapema, wakaondoka kwa haraka na hawajulikani kama wamerudi mjini au wameelekea wapi, wanawake wenyewe hawajatulia…’akasema.

‘Sasa wewe nani kakupa hizo taarifa..ni isiwe na wao wanahusika ndio maana wamekimbia?’ akaulizwa.

‘Unajua masikio hayana pazia, wakati nipo kwenye mihangaiko ya kuangalia watu wakae vipi, nikawafuma akina hao akina mama wawili wakiongea..mama mmoja ni mama wa kati ya hao mabinti…’akasema

‘Ehee ukamuuliza?’ akauliza baba mwenye nyumba

‘Mama huyo hakukubali kuniambia ukweli….’akasema

‘Sasa yote hayo uliyapataje…?’ akaulizwa

‘Niliwasikia wakiongea na shiga yake , hawakujua kuwa mimi nipo nyuma yao ….’akasema

‘Kwahiyo wewe uliwasikia wakiongea nini haswa kitakachosaidia…?’ akaulizwa

‘Kama hivyo nilivyokuambia kuwa hao wasichana walitokea mjini, wakafika eneo hilo, wakasikia harufu, wakakimizwa…..huyo mama mmoja ndio alikuwa akimsimulia mwenzake, na waliponiona wakanyamaza,na yule aliyekuwa akimuhadithia mwenzake akawa anaondoka, nikaona nimfuate kumuulizia, nikamfuatilia hadi nje, …, nikamuuliza, akakataa kata kata kuniambia ukweli, akasema yeye hajui lolote…’akasema.

‘Haya mambo sitaki kuyakuza sana maana kama ni hasara tumeshapata , muhimu ni kutoa ushirikiano na polisi ikibidi…nasema ikibidi, …lakini tusiongee lolote kuhusu fununu au kusikia, hayo wao wenyewe watajua jinsi gani ya kufanya, ukijianya unajua sana, siji umesikia, utaingia matatani...’akasema mume mtu.

‘Mume wangu, mimi nawaogopa sana polisi maana wakianza kukuhoji unaweza kujikuta umetegewa, ukaongea hata yale uliyokuw a hukukusudia kuwaambia,… na hao vijana wamesikiwa wakisema atakayewataja watahakikisha wanamuua…wapo tayari kufa, kwani kufa kwao ni kitu cha kawaida tu…’akasema.

‘Sikiliza mke wangu, hata mimi siwezi kusema lolote kwa hivi sasa, maana hapa nilipo kichwa changu hakipo sawa…nahitajia muda wa kuliwazia hilo, najua polisi watatuita kutuhoji, ninachokuomba ni kutokuongea hayo ya kusikia, waachie polisi wenyewe wagundue hilo…najua watafikia huko na watagundua ukweli…’akasema.

‘Hata mimi nilikuwa na wazo hilo hilo...na jingine nimeonana na mke wa mjumbe na yeye akawa ananimbia yake…’akasema.

‘Mhh, mjumbe, mkewe…ehe,…na yeye kasemaje, yeye uliongea naye, ..hukumsikia.. niambie maana huyu mjumbe mimi simuamini sana, anaongea kupitiliza..’akasema mume mtu.

‘Mkewe anasema , mume wake wakati anatoka usiku kufuatilia…’akasema

‘Kufuatilia nini usiku?’ akadaikia muem wake.

‘Si baada ya kusikia ukelele wa huo moto, …sasa wakati mume wake anaamuka kutoka nje, akasema huenda hao wapinzani wake wameamua kumfanyizia…’akasema.

‘Kwa vipi?’ akaulizwa

‘Anadai wamekuwa wakitafuta upenyo wa kuonyesha kuwa kijiji hiki hakina amani, hakina mjumbe anayefaa, na yakuwa mjumbe hajui wajibu wake, anawakaribisha watu wasiofaa akiwemo huyo mama …’akasema mkewe.

‘Mhh, najua yatasemwa mengi, …na hasa kama limegusishwa na kisiasa, basi sisi tusubiri ..tutasikia mengi…lakini bado sijaelewa, unasema mke wa mjumbe  alimsikia mume wake akisema… anawakaribisha watu wasiofaa akiwemo huyo mama sasa,..walijuaje kuwa moto huo umetokea kwa huyo mama…?’akasema mume mtu na kuuliza.

‘Aaah, mimi sijui…hebu na wewe nikuulize ulipofika huko alipokuwepo huyo mama, ulimkutaje..watu wanadai hawezi kufa maana ni mama kutoka mbinguni…na hata huo moto hauwezi kumuunguza…ati ni kweli hajaungua kabisa?’ akaulizwa

‘Hajaungua sana na moto, ni majeraha machache, sana sana..miguuni na mikononi lakini sio saana…kwenye mwili hajaungua maana angelikuwa kaungua nguo alizovaa zingekuwa zimengua, nimekuta na nguo zake kama kawaida…’akasema na kuongezea;

‘Kiukweli kama ni kufa, labda kafa kwa kukosa hewa, ..na pia jinsi alivyojifunga,..moshi hakuweza kumuathiri sana, labda huko kukosa hewa…sasa sijui ..sina uhakika ,..ila ana mjeraha ya mapanga,..sasa hapo ndio nahisi kuwa huenda kafa kwa kupoteza damu nyingi…’akasema

‘Uliona damu hapo alipokuwepo?’ akaulizwa.

‘Ndio hapo nashindwa kuelewa, hakukuwa na damu pale ardhini,  ..sikuona damu zaidi ya matone kidogo tu…, niliangalia kote sikuona sehemu kuna damu nyingi ardhini, maana hayo majeraha ni makubwa,.damu itakuwa imetoka kwa wingi...’akasema.

‘Ina maana gani sasa mume wangu..?’ akauliza.

‘Nahisi atakuwa katendewa hivyo, kakatwa na mapanga nje ya chumba, na huenda alikimbilia hapo ndani, na..kuingia mvunguni kujificha…wakawa wanamfuatilia, walipofika hapo nyumbani hawakumkuta, na kwa vile wana uhakika kuwa aliingia hapo ndani,ndio wakaona wachome nyumba moto…’akasema mume mtu.

‘Duuh,  unaona eeh,…kwa vile ni mama kutoka mbinguni, hana damu…na nikuambie kitu mume wangu..huyo mama yawezekana hajafa..mwenyewe utaona…hapo anatafuta upenyo, watu wakizubaa tu..huyoo, anapaa anaondoka zake…’akasema mkewe

‘Mke wangu hebu acha hizo imani haba….mtu yupo kalala pale mfu…unasema hajafa, ina maana sisi ni wajinga..’akasema mume wake.

‘Haya, sasa mwili wake si unatakiwa upelekwe hospitali, maana kama ni majeraha namna hiyo akiendelea kukaa hapo, mwili utaoza haraka, …?’ akauliza mke mtu.

‘Ndio polisi wanamchunguza huko ndani…ngoja niingie nisikie kinachoendelea nitakuja kukuambia la kufanya, jipangeni tu , …’akasema mume mtu na kuondoka upande huo walipokuwepo akina mama.

*************

Kwa upande mwingine kulikuwepo na kikosi kingine ambacho kilipewa kazi ya kuchunguza sehemu ya moto na pia kati yao kulipokuwepo na askari wawili waliokuwa wakikusanya maelzo ya watu.

Kikosi kile cha kuangalai moto ulivyowaka, kama ni wa kawaida au ni hujuma, kiliweza kwenda mbali zaidi, na kugundua baadhi ya vitu vinavyoweza kusadikiwa kuwa ni vifaa vilivyotumika kuwashia huo moto, lakini havikiwa na nguvu sana, kilipatikana kibiriti, na njiti zake na kitambaa kilichoungua nusu, chenye harufu ya petrol

‘Bado hatujapata kitu cha uhakika..lakini harufu iliyoenea huku, hasa hapa kwenye majani aonekana ni ya petrol…’akasema mwenzake.

‘Na huu moto ulianzia pale….’.akasogea hadi hapo anapohis moto ulianzia,..

‘Huu moto waonekana ulianzia hapa…ukazunguka,…mmh, unaona…kuna galani hapa mkuu, hebu njoo uione…’akasema mwingine na mwenzake akasogea hadi hapo ilipo hiyo galoni

‘Mkuu..unaona huu moto umeanzishwa na watu kwa makusudi..unaona hata hii galani haijateketea kabisa..haijaungua sana..’akasema na akiwa kavalia kinga akasogea kutaka kuichukua.

‘Subiri…ngoja nikamuite mkuu, aje aone mwenyewe..nilijua tu..huu moto umeanzishwa na watu..’akasema na kuelekea huko kwa mkuu wake, na baadaye akarudi.

‘Nimekuja na huyu mpiga picha, ngoja achukue matukio,..na mkuu kasema tuendelee, sasa cha muhimu kabla hatujaingia ndani kabisa, kwenye mabaki mabaki naona tuzunguke kote kwa nyuma…’akasema

Kabla ya hapo, kundi hili lilikuwa na watu zaidi, ila waliamua kugawana majukumu, wawili wakabakia kutafuta chanzo cha moto,na kukusanya ushahidi, na wengine wakaenda kuwahoji watu walioshuhudia huo moto…na kundi la kuangalia chanzo cha moto likiwa linaendelea kwa upande mwingine kulikuwa na kundi la kuwahoji watu…

*************

‘Nataka kuongea na baba mwenye nyumba yupo wapi?’ akauliza askari wa kundi la kuwahoji watu, na wakati huo baba mwenye nyumba ndio alikuwa katoka kumfuatilia mjumbe, aliporudi tu akakutana na huyo askari kanzu.

‘Mimi ni askari na kazi yangu ni kutafuta ukweli kuhusiana na huo moto..kwanza nikupe pole kwa maafa hayo..najua ni hasara na ikizngatia kuwa huku kijijini hatuna huduma za bima, kwahiyo ni hasara isiyo na marejesho, au sio…’akasema

‘Tumeshapoa…’akasema baba mwenye nyumba.

‘Muhimu ni kujua ukweli..hata kama kuna hasara lakini je haara hii ni ajali a kawaida au ni ya watu wameamua kufanya hujuma..’akasema askari mwingine

‘Na ukweli huo hatuwezi kuupata kama hatutpata ushiriakino kutoka kwenu..na ni vyema mkatuelezea kila kitu, ili tuweze kuchanganua wenyewe, maana kuna kusikia, kuna kuona, na kuna kudhani..yote sisi tunahitaji..’akasema na mwenzake akaongezea kwa kusema.

‘Ila mara nyingi ukifika mahakamani wao sana sana wanahitajia ulivyoona wewe…unaona, lakini  sisi tunataka yote, kama uliona, itakuwa ni bora zaidi..lakini hukuona umesikia,..tunahitaji hilo pia, litatusaidia kufuatulia, au unavyodhani, unavyofikiria wewe hata hilo tunalihatajia ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu…’akasema askari mpelelezi.

Baba mwenye nyumba akawa katulia akiwaza ni nini akiseme na ni nini asikiseme maana ya kusikia ni mengi na hayo ya kusikia yanaweza kumtia mtu hatiani , ….alpwaza hivyo moyini akasema ‘hapa natakiwa kuwa makini.

Akilini akawa anamuwaza huyo mama,…ambaye sasa anajulikana ni marehemu pamoja na mengi, pamoja na kumbukumu zake, lakini moyoni aliona hakustahili kufa kifo cha namna hiyo…walivyomkata kata na mapanga, ni unyama….hata hivyo hakupenda kujiingiza zaidi, akaona akijiingiza zaidi anaweza kujitia matatani.

NB: Haya kwa leo inatosha


WAZO LA LEO: Usiwe mwepesi kukubali taarifa za kusikia, kwani nyingine zinaweza kuwa uchonganishi tu, na unaposikia taarifa kama hizo kama zina umuhimi kwako zifanyie uchunguzi kwanza kabla ya kuziamini au kuzitangaza kwa watu wengine.
Ni mimi: emu-three