Inspecta
Moto alifika nyumbani kwake, na kushika kitasa, kuzungusha ili afungue mlango,
mara mlinzi akaja nyuma yake na kusema;
‘Mkuu
ngoja nkfungulie ufungua ninao mimi…’akasema na Inspecta akasogea pembeni na
huyo mlinzi akafungua mlango wake, na yeye akaingia nyumbani kwake.
Upweke
huzuni, vikaanza kumtawala,, japokuwa mwanzoni, alijitahidi kutokuliwazia hilo,
lakini akili ya kibinadamu ikamjia, akaanza kuhisi upungufu fulani akilini na
mwili ukaanza kuisha nguvu…
Akajitutumua,
na kuingia ndani akaangaza huku na huku kwa haraka, halafu akaingia chumbani,
hali ikaanza kubadilika zaidi, akaanza kuhisi upweke, huzuni, na kwa hali hiyo hakuweza
kukaa hapo chumbani kwake, akatoka nje, na kukaa sebuleni, lakini baadaye
akasimama alikumbuka jambo,akarudi chumbani;
Akaangaza
macho huku na kule, lakini aliona chumba kipo kisafi, hakuna kitu cha kuweza
kumsaidia, hakukata tamaa, akarudi tena sebuleni, akili ilikuwa haijawa safi,
kuna kitu kinamsumbua,…
‘Ngoja….’akasema.
Japokuwa
alijua kuwa polisi wameshafanya uchunguzi wao, na hataweza kupata chochote cha
kumsaidia, lakini aliona ajaribu tena, safari hii akatoka nje kabisa, akazunguka
zunguka nje, alifanya hivyo mara nyingi, baadaye akarudi ndani na safari hii,
akawa anatembea kwa taratibu, akikagua kila sehemu hatua kwa hatua, na kwa muda
huo haukujua anatafuta nini.
Alipofika
chumbani,akakukumbuka jambo,… leso…
Akakumbuka
siku ile, aliona leso ngeni karibu na kitanda, alipokumbuka hivyo, akaona kuna
kitu anatakiwa kukifanya kwanza,
Akasogea
kwenye kabati lake na kuchukua mfuko wa plastiki , ni mifuko maalumu ya kuweka
vidhibiti vya polisi kwa ajili ya uchunguzi, alijua ataweza kuona kitu, na ni
vyema kuvihifadhi kwenye chombo maalumu, akachukua na soksi za mikono, kwa
tahadhari…
Akachuchumaa
na kuangalia eneo la kitanda, kwa chini, akasema;
‘Nakumbuka
hapa kulikuwa na leso hapa chini….’akasema na kuinama kuangalia, na kweli ile
leso ilikuwa imesogezwa na kuzama chini ya mguu wa kitanda, kwa uangalifu akaitoa
na kuweka kwenye huo mfuko maalumu wa plastiki.
Akaendelea
hivyo hivyo, na kila alichokiona kipya kwenye chumba chake akakiweka kwenye huo
mfuko, halafu akaelekea chooni na bafuni, huko kulikuwa kumesafishwa, na harufu
ya madawa ilitapaa kila mahali, ilionekana walihakikisha hakuna kitu
kinachobakia,…akafika kwenye beseni la kuogea,…
Alipofika
hapo akashindwa kuvumilia, maana akili yake ilikumbuka lile tukio lililopita,
hapo akachuchumaa na kuanza kulia, alilia kwa muda mrefu, na alishitushwa na
mtu akimgusa begani.
‘N-nani
wewe…?’ akauliza na kusimama kwa hasira
‘Rafiki
yangu, usisononeke sana, najua hii hali inachukua muda kuondoka kichwani,
lakini yote yakubali kama ni mapenzii ya mungu….’sauti ikasema, na hapo akasimama
na alitaka kumvamia huyo jamaa na kumfanya kitu kibaya, lakini akakumbuka
masharti, akageuka na kuangalia lile beseni la kuogea
‘Unajua
rafiki yangu, hata mimi kuna muda hali hiyo inanijia na huwa nalia sana,…nalia
sana maana shemeji nilimzoea sana, alikuwa kama dada yangu , mshauri wangu
mkubwa, kuna muda nakorofishana na mke wangu, lakini nikikutana na mkeo,
natapata maneno ya hekima, ..na kuyasahau yote….namrudia mke wangu kama hakuna
lililotokea….’akasema
‘Naomba
uondoke…’akasema Moto.
‘Nitaondoka
tu, nimekuja mara moja, kwanza kuhakikisha usalama wako, hali yako, na kama
kuna lolote naweza kukusaidia…’akasema Maneno.
‘Hakuna
cha kunisaidia, nahitahi muda wa kukaa peke yangu…..’akasema
‘Najua,
nafahamu sana,…lakini mimi ni rafiki yako, ujue haya yote ya kuhakikisha
unatoka jela, na hatima ya kesi hii, ni mimi nimejitolea, kwa ajili ya urafiki
wetu….’akasema
‘Nashukuru,
kama sio kwa masilahi fulani…hata hivyo, sizani kama hili litapia hivi
hivi…’akasema.
‘Kwahiyo
unataka kufanya nini, kumbuke niliyokuambia, usije ukajifanya kichwa ngumu,
nakuhakikishia utakuja kujuta, na …sijui, labda kama hujui hatari ya hao
watu…’akasema
‘Ndio
maana nataka uondoke, …sitaki kuwa na mtu hapa kwa hivi sasa…’akasema
‘Sawa,…upendavyo……‘akasema
Maneno
‘Leo
sitaki kukutana na mtu, nimemwambia hata mlinzi hapo nje, sijui kwanini
umeingia?’ akauliza.
‘Samahani nimeingia
kwa nguvu, nimemwambia nataka kuhakikisha kuwa upo salama, na kuhakikisha pia mambo
mengine yanakwenda kama tulivyokubaliana…’akasema.
‘Leo
sitaki kuongea na mtu naombeni mnielewe…samahani sana, sio nakufukuza lakini
inabidi … nakuomba uondoke, leo ni siku ambayo nakumbuka mengi, na sitaki
kuongea lolote, moyoni nina hasira…ninaweza kufanya jambo bay asana, nakuomba
uondoke…..’akasema huku akikunja ngumi kwa hasira.
‘Ni
sawa lakini lililonifanya nije hapa ni kukupa habari njema….’akasema Maneno.
‘Habari
gani?’ akauliza Moto , sasa akikunjua ngumi aliyokuwa ameanza kuikunja.
‘Uchunguzi
umekamilika, na mambo yamekwenda vizuri, ushahidi uliopatikana umethibitisha
kuwa kweli mke wako alijiua, na hata hakimu kakubaliana na huo ushahidi, hata
ndugu wa mkeo,…mama mzazi wa mkeo wako, amekubaliana na huo uchunguzi…’akasema.
‘Hata
mama mzazi kakubaliana na huo ushahidi wenu, haiwezekani mumeonana naye lini ?’
akauliza.
‘Sasa
hivi nimetoka kwake, na mara nyingi nakutana naye, nikimpa maendeleo ya
uchunguzi wetu, na sasa kaamini, na ndio maana anataka kuja hapa kukuomba
msamaha, kwa dhana yake dhidi yako…..’akasema.
‘Ipo
siku ukweli utagundulikana tu….’akasema.
‘Ni
mpaka, kama kuna ukweli mwingine ambao mimi siujui, ila ukweli halisi ndio huo….’akasema
na Moto akawa akimiya kwa muda na mwenzake alipoona kuna huo ukimiya akasema;
‘Ni
hilo tu nililokuja kukuambia na mimi nakushauri, ni vyema kuanzaia sasa ukaanza
kujipanga upya, uwe kama mimi sahau yote yaliyopita,ujue katika haya maisha,
hakuna anayepoteza muda kuangalia jinsi ya maendeleo ya mwenzake, kila mmoja
yupo katika maisha yake, maendeleo yake binafsi, hata ndugu…sembuse mtu baki,
jaribu kujiangalia wewe mwenyewe kwanza….utafanikia..’akasema.
‘Wewe
unasema tu, hujafiwa, hasa na mtu ambaye ndiye ubavu wako…we sikia tu kwa
wengine, hilo kwangu halitaisha hivi hivi, mpaka nijirizishe, bado nahisi kuna
jambo, sizani, kama mke wangu alijiua mwenyewe….’akasema.
‘Sasa
utafanyeje, ni hali halisi ndio hiyo, na kiukweli imeshatokea hivyo, huna la
kufanya, au sasa unataka kufanya nini, ujiue na wewe, kama unaona hiyo ndio
njia rahisi basi jiue, unafikiri ukifanya hivyo utaipunguzia nini dunia, kila
siku watu wanazaliwa, wanakufa, wanazaliwa…au una mipango gani?’ akauliza.
‘Moyo
wangu unglitulia, kama ningeligundua ukweli wa hili jambo, na kama kuna wau
wapo nyuma ya hili, waweze kufikishwa mbele ya sheria…’akasema.
‘Basi
nikaushauri hivi, nenda kwa hakimu ukasema wewe ndiye uliyemuua, ili mambo
yaishe, au ?’ akawa kama anauliza.
‘Mimi
sijamuua mke wangu, hilo lilipangwa, na kama lilipangwa, nataka kujua kwanini,
na kama kuna mtu kamuua mke wangu nataka ajulikane ni nani, na sababu, mimi nina
imani kuwa kweli mke wangu hakujiua, na kwa vile nimesingiziwa mimi kwa mipango
maalumu, ni muhimu kumpata muuaji wa kweli ni nani, na kwanni wanisingizie
mimi, huoni hapo kuna jambo limejificha, huoni ni sababu ya mimi kukubaliana na
hayo matakwa yao…’akasema Moto.
‘Hilo
unasema wewe kujikosha, lakini hakuna haja ya kuhangaika tena, hayo mambo
yamekwisha, wewe sio muuaji tena kama ilivyozaniwa, muhimu ni kujipanga kwa
jinsi inavyotakiwa, ila hapo nakukunya, na mhimu uwe makini , maana kila hatua
, kila unachofanya kinachunguzwa, ukionekana unakwenda kinyume cha makubaliano
huwezi kuamini yatakayofuata baadaye…’akasema.
‘Kutoka
kwa nani?’ akauliza.
‘Kwa
hao waliokusaidia…’akasema
‘Akina
nani?’ akauliza
‘Hivi
hapo kuna umuhimu kweli wa kutaka kuwajua hao waliokusaidia….?’ Akawa kama
anauliza, na kabla hajapata jibu akasema
‘Cha
muhimu kwa sasa ni kushukuru kuwa wewe sasa upo huru, huna kosa, unahitajia
nini tena?’ akauliza, na aliposema hivyo, Inspecta akakumbuka jinsi
alivyoletewa hiyo taarifa akiwa mahabusu, kuwa dhamana yake imekubaliwa.
***********
Inspecta
akiwa kaduwaa, kajichokea, akakaa chini na kujiegemeza ukutani, na ghafla akahisi
usingizi ukimjia;
Sauti
anayoitambua vyema ikamuambia;
‘Mume
wangu usisononeke sana, haya yote yana mwisho..’sauti ikamuambia, na akajaribu
kuinua uso, kuona ni nani anayemuelezea hayo maneno, na taswira akiwa mahali, wapo mahali, na mkewe mara yupo mbele yake, wakati mwingine wamekaa, lakni haonyeshi ni wapi.
‘Mke
wangu, wewe hujui ni nini kinachoendelea, dunia hii ni ngumu na ina mambo
magumu, yasiyoelezeka…’akasema
‘Najua,…na
sasa najua hata usiyoyajua, lakini vyovyote ufanyavyo, ujue kuwa kuna leo na
kesho, hata uhangaike vipi, ujue kuna siku mimi na wewe hatutakuwa
pamoja…’akasema mkewe.
‘Kwanini
unasema hivyo…?’ akaumuuliza na kujaribu kumuangalia mkewe, lakini uso wa mkewe
ukawa hauonekani, alikuwa kainama na baadaye akainua uso na kuangalia mbele,
hakuangalia muelekeo wa mumewe, kama vile hataki mume wake amuangalie usoni.
‘Ni
kuthibitisha kuwa vyovyote tufanyavyo, hatujui hatima ya kesho, kwahiyo kila
linapotokea jambo mshukuru mungu wako,…yeye ndiye mwenye neema, yeye ndiye
anajua hatima ya kesho…je wewe unajua kesho kutatokea nini…hujui,lakini mola
wako anajua…..’akasema
‘Ni
kweli..lakini ina maana tusihangaike kutafuta ukweli jambo likitokea?’ akauliza
na mkewe akaonekana kama anatabasamu; na kusema
‘Kama
ukweli upo utajulikana tu…cha muhimu ni kutokuushinikiza , kwani ukitumia nguvu
sana utaumia mwenyewe, na kwa namna hiyo unaweza hata kushindwa kuupata huo ukweli wenyewe, wapo watu wanatafuta
mwanya wa kila hali, wanaangala kasoro zako, makosa yako kwao ni sababu ya
kukuharibu, muhimu sana, wewe tuliza kichwa, tumia hekima, na mwisho wa kila
jambo utafika, kwaheri…’akasema mkewe
‘Kwaheri
kwani unakwenda wapi?’ akauliza akitaka kumshika mkewe asiondoke karibu yake
lakini hakuweza kuinua mkono wake, ilikuwa kama viungo hivyo havipo
‘Nakwenda
kuupumzika…’akasema, na alipojaribu kujikakamua ainuke amshke mkewe asiondoke,
sauti ikasikika kigonga mahali,…oooh
Inspecta
akashtuka, kumbe alikuwa akiota, akapangusa uso, na kuangalia huku na huko kama
anamtafuta mkewe, na wakati huo moyo wake ulikuwa ukimuenda mbio, akasimama, na
mara akasikia sauti ikisema;
‘Moto,
unaitwa kwa mkuu….’akaambiwa
Akageuka
sauti ilipotokea, akamuona askari akiwa kashika kirungu, kumbe yeye ndiye
aliyegonga ule mlango wa geti, akamuangalia yule askari, bado akiwaza kuhusu
ile ndoto.
‘Twende….’akasema
yule askari, huku akifungua geti la chumba chake, na Inspecta hakuwa na
kipingamizi, akatoka na kumfuata huyo
askari mlinzi kwa nyuma, na alipofika kwa huyo mkuu, hakuambiwa mengi
aliyoambiwa, zadi ya kuambiwa kuwa dhamana yake imekubaliwa, na akapewa mashart
ya dhamana kwa mujibu wa sheria…’akaambiwa
‘Kwahiyo,
unataka kusema nini?’ akauliza kwa sauti ya kutoamini hayo anayoambiwa
‘Upo
huru kuondoka…kama unahitaji kujiandaa, rudi sehemu yako kajiandae, ama kama
upo tayari, unaweza kuondoka sasa hivi….’akaambiwa.
Inspecta
hakutaka hata kurudi mahabusu, akatoka na kuelekea nje na alipotoka tu nje mara
akaja mtu mmoja na kumwambia kuna gari linamsubiri kumpeleka nyumbani kwake,
hakutaka hata kuuliza gari hilo kaleta nani, akaingia kwenye hilo gari na
kufikishwa nyumbani kwake…
************
‘Kwangu
mimi cha muhimu ni kujua ukweli…nahitaji kuujua ukweli, ni nani alimuua mke
wangu,…’akasema akiendelea kuongea na Inspecta mwenzake.
‘Kwahiyo
wewe huamini kuwa mkeo kajiua mwenyewe?’ akaulizwa
‘Siamini,
hata wewe huamini hilo, …yoyote hawezi kuamini hilo, ndio maana nikakamatwa
mimi, kwa hisia za kuwa nimemuua mke wangu, haya ya kujiua mwenyewe yamekuja
baadaye, je nitaamini kivipi….’akasema
‘Sasa
mimi nakuambia kama rafiki yako, kiukweli mke wako alijiua mwenyewe, kukamatwa
kwako ilikuwa ni moja ya kukuweka sawa,…japokuwa dhamira ya ililenga utumiwe
mwanya huo, kama hutakubaliana, basi uwajibike kama muuaji,…na kama
tusingelikusaidia, ungehukukumiwa kama muuaji, lakini sasa ukweli wenyewe wa
jinsi ilivyokuwa umefichuluwa, na kuwekwa wazi, kiukweli mke wako alijiua
mwenyewe….’akasema
‘Umayajuaje
hayo, kama sio mipango yenu mipya?’ akauliza
‘Sikiliza
Moto, kila kitu kilichokuwa kikifanyika hapa kwako kilikuwa kinajulikana, hilo
nakupa kama siri, lakini pale ulipokubaliana kuwa upo tayari kukubali na
kushirikiana, basi hali hiyo ya kumulikwa kila mahali ikaondolewa,…sasa tukio zima
la mke wako kufika hapa hadi kujiua lipo,…ila wewe hutaonyeshwa, kwa usalama
wako….maana inatisha…’akasema
‘Kwa
vipi?’ akaulizwa
‘Sababu
za kuchukia, kuogopa kudhalilika hadi kufikia kujiua,….mmh ni vyema usione
kabisa, itakuumiza sana, mimi mwenyewe nimeumia sana moyoni, lakini
nitafanyaje,…wewe ni rafiki yangu, niamini haya ninayokuambia, na ukubali
hivyo, kwanii ndivyo ilivyo….’akatulia kidogo kama anawaza jambo halafu
akasema;
‘Kwahiyo
hata wenzangu tulioshirikiana kuupata huo ushahidi wameonelea hivyo kuwa wewe
ufahamu hivyo tu, kuwa mke wako alijiua mwenyewe,inatosha, ukitaka kupekenyua
kuwa ilikuwaje, hutafanikiwa na hata kama ungefanikiwa, utasononeka maisha yako
yote, nakushauri ni bora iwe hivyo, na amini hivyo….’akasema
‘Inaonekana
kuna mengi ambayo siyajui, na huenda hata wewe unahusika kwa namna moja au
nyingine, na hutaki nifahamu au sio….’akasema
‘Ngoja
nikuache, maana umechoka, unahitaji kupumzika, na kupumisha kichwa chako, kwaheri,
tutaonana ukiwa tayari…’akasema Inspecta Moto, na usoni alionekana kujawa na
huzuni, akawa anatembea huku kaangalia chini, na alipofika mlangoni akasema
‘Jiandae
mama mkwe wako anaweza kufika hapa kwako leo, na kama hutaki muonane naye leo
useme, mimi nitawasiliana naye aje kesho….’akasema
‘Nitaonana
naye hata leo…ila mimi sijarizika na hayo uliyoniambia, ukumbuke wewe ni rafiki
yangu tumetoka mbali, lakini kama nitakuja kugundua kuwa unahusika na haya
yote, hasa kwa kifo cha mke wangu, sitajali kabisa kuwa tulikuwa marafiki…’akamuangalia
mwenzake na wakawa wanaangalia, na akiwa kakunja uso wa hasira akaendelea
kuongea
‘Kama
unahusika, nitahakikisha ni jino kwa jino…unanielewa, nitalipa kisasi ambacho
hutaweza kuamini…hujui ni kiasi ninavyoumia moyoni, nasema tena, ole wako, kama
unahusika, ole wa hilo kundi…’akasema Moto, na Inspecta akabenua mdomo wa zarau
na kusema;
‘Kumbuka
ahadi na masharti kuzingatiwa, usije kujijutia baadaye, mimi nimetimiza wajibu
wangu, nimekusaidia kama rafiki yangu, ili usije kuhukumiwa kwa kesi ya mauaji,
sasa upo huru, lakini bado unachunguzwa, nikushauri kama rafiki yangu,
unachotakiwa kwa sasa ni kujipanga, angalia maisha yako mbele, hayo mengine
hayana umuhimu kwa sasa, utajipotezea muda wako bure….’akasema Maneno
‘Natumai
kauli yangu umesikia, na unafahamu vyema nilivyo…’akasema Moto
‘Na
mimi nakutahadharisha kuwa ukihini huo mkataba, yatakayotokea mimi sitakuwepo….’akasema Inspecta Maneno, na
Moto akawa kimiya, na baadaye Inspecta Maneno akasema;
‘Hata
hivyo, karibu ndani ya ulimwengu wa kisasa, uione dunia ilivyo, hiyo ndio dunia
ya kisasa, ya sayansi na tekinolojia, …’akatabasamu, na kuangalia chini, halafu
akaendelea kusema;
‘Unajua
kila mtu ana ndoto zake za kufanikisha maisha yake, na ingeliwezekana kwa jnsi
akli za watu zilivyo, ni kama vile kila mtu ana dunia yake mwenyewe,..ni
nadharia ya kufikirika, ila kwa hili nakuomba tushirkiane,kwani mmi
nmekudhamni,… au sio, kwahiyo ninachoweza kukisema kwa sasa ni kukaribisha
ndani ya dunia yangu…’ akasema na
kuondoka.
Inspecta
akiwa katingwa na mawazo,hakujali alichokuwa akiongea mwenzake, lakini neno la
mwisho llilotamkwa na Inspecta Maneno lilidumu kichwani mwake, na kujirudia
rudia kichwani mwake,….dunia yangu, dunia
yangu…mwishowe akasema;
‘Eti
nini, Dunia yangu…!’
WAZO LA LEO: Ugumu wa jambo,
raha na shida za jambo lolote alijuaye ni muhusika mwenyewe, ndio maana watu
wengine hukimbilia kusema yule analalamika sana, yule hawezi kuvumilia. Lakini
mpaka mtu anafikia kulalamika, kulia au kusema...., ujue keshafikwa, siri ya mtungu aijue kata.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment