‘Mhh....kama mtoto
wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wa huyo rafiki yako atakuwa anafanana na mume wako au
sio?’ akaniuliza, ni swali lililonifanya niwaze sana japokuwa sikuwa
nimelipenda kwani lilikuwa likilenga fitina.
Kama kuna kitu nisichokipenda katika maisha yangu ni uzushi
wenye lengo la ufitinashaji, hasa kwa watu wanaopendana na kuaminiana, mimi namwamini
sana rafiki yangu, mimi namwamini sana mume wangu. Na rafiki yangu huyo tunapendana
sana, nawatu wengu hawafahamu kuwa urafiki wetu huo hakuanza leo, ni kutoka
shuleni, na zaidi ya hayo, nilimchukua rafiki yangu huyo akawa mikononi mwangu
nikamjenga, akawa jasiri, na yeye aliniona
mimi zaidi ya rafiki, aliniona kama dada yake,japokuwa kiumri tulikuwa sawa.
`Sasa iweje anifanyie
hayo wanayohisi watu...’
Nilipoona kauli za huyo dakitari zinaelekea kwenye hiyo fitina,
nikapanga kuzikataa na kama akiendelea kuongela hilo, nilipanga kumzimba mdomo,
na ananifahamu nilivyo, ndio maana pale aliposema;
‘Mhh....kama mtoto
wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wake anafanana na mume wako au
sio?
Nilifahamu ana nia gani kwngu, ndio maana nikamjibu kuwa, watoto wangu wanafanana pia na baba yao
mdogo, kwahiyo huenda, shemeji yangu huyo akawa na mahusiano ya rafiki yangu,
lakini kwa vile rafiki yangu hakupenda kuzalilika kwa kutembea na kijana mdogo,
akaona anifiche,..
Hilo linawezekana pia, lakini pia kufanana kwa sura sio
lazima kuwa mume wangu au mdogo wangu ndio baba wa mtoto wa rafiki yangu, ...inaweza
ikatokea, ...mbona hayo hawayaoni....au kwa vile wana chuki na ndoa yangu ndio
maana wanataka kuniharibia, ama kwa hilo hawanipati ng’ooooo
Nilijiona naandamwa na
mawazo, wakati najiandaa kuondoka, na hata tulipokuwa ndani ya gari, akili
yangu ilikuwa kichanganua mambo, ...na nilijipa tumaini pale niipokumbuka kauli
yake ya kushindwa pale aliposema;
‘Yawezekana,.kuwa huenda mdogo wa mume wangu
anaweza kuhusika na mtoto wa rafiki yangu.’ Na hili nililiwekea asimilia
nyingi kwa vile kwanza mtoto huyo anafanana kabisa na sura zao, na mdogo wa
mume wangu anafanana sana na kaka yake. Pili tangu rafiki yangu huyo ajifungue,
mdogo wa mume wangu amkuwa kama ananikwepa...
Lakini kwanini alitoa hi kauli , ina maana kuna ukweli
anaoufahamu, na kauli hiyo ilinifanya intake kumuuliza maswali mengi,
nikaikumbuka ile kauli yake alivyosema;
‘Lakini mwisho wa siku
ukweli utajulikana....’
Je ni ukweli gani huo, ikawa ni fumbo jingine,
ambalo liliachwa kichwani mwangu bila kupata majibu, na kwa hali hiyo
nikajikuta nikikunja uso kwa hasira, sikupenda tabia ya namna hiyo, ya
kunichezea, akili yangu, na kila tukiangalia na huyu jamaa nijakuta nimekunja
uso kwa hasira, ndio maana akawa ananisihi mara kwa mara, na hata tulipokuwa
kwenye gari aliniambia tena;
`Mpendwa,nakuomba tafadhali,...ukifika kwa mume wako, hakikisha
unaonyesha tabasamu,....usije ukamuonyesha mume wako sura ya chuki, na mkiongea
naye , kama atakuwa akikuuliza maswali yenye mlengo wa kuongelea mambo
yatakayomuumiza moyo wake, hasa kwa tukio hilo lililopelekea kupatwa na haiyo jail,wewe
uwe makini wa jinsi gani ya kumjibu , majibu yako yasimfanye ahisi vibaya, na
kuona kuwa hujamsamehe,....’akasema
Kwa muda huo tulikuwa tumeshafika mapokezi na tulikuwa
tunasubiria muda wa kuingia, kwani walisema madakitari wapo kwenye shughuli
zao, tuwape muda....
‘Hivi kusamehe huko ni kwa kuigiza, maana hadi sasa, hata
sijui namsamehe kwa kosa gani...’ nikasema.
‘Kiukweli kwahivi sasa inabidi ufanye hivyo, kumbuka kupona
kwa mume wako,pamoja na tiba anayopata, lakini kwa kiasi kikubwa, atahitajia
sana faraja, hasa kutoka kwako, ....sijui kosa alilofanya, lakini inaonekana
kwake ni kubwa sana, ...kwahiyo uamuzi ni wako, kama unataka mume wako apone
kwa haraka fanya hivyo, igiza kuwa umemsamahe, kama hujafikia uamauzi wa
kumsamehe....’akasema
‘Kwangu kumsamehe sio tatizo , tatizo ni kuwa, mimi natakiwa kumsamehe kwa kosa gani...mbona
hutaki anieleze kosa alilolifanya, kwani siku ile yeye mwenyewe alionekana
kutaka kunielezea, wewe ukamzuia kiujanja...sijui kwa maslahi gani’nikasema.
‘Kosa hilo mimi na wewe hatulifahamu, kwahivi sasa
halijafahamika, ni kukisia tu, hata sisi hatutaki kumshinikiza aeleze
ilivyokuwa, hata askari waliokuja kuchukua maelezo yao tuliwaambia wasimuulize
chochote kuhusu ilivyotokea,..bado muda wa kumuuliza hayo,....ipo siku yeye
mwenyewe atakuambia, na mimi siku ile nilifanya hivyo kwa masilahi yenu, hasa
ya afya yake...ila kimtazamo wangu, nahisi yeye anafahamu kuwa wewe unafahamu
hicho alichokitenda, au kosa alilolifanya, ...’akatulia.
‘Mimi nitafahamuje hayo mambo ya kufikirika, maana hayo yote
ni dhana, tena dhana potofu, na kama ungelimfahamu vyema mume wangu, na hata
huyo rafiki yangu usingelikimbilia kujenga dhana kama hizo,....ndio hapo
siawaelewi,..eti nafahamu, nitafahamu vipi, halafu nihangaike kutafuta ukweli’nikasema.
‘Ok, kama hufahamu lolote ni bora iwe hivyo, na mwanzoni
nilikushauri tuutafute ukweli, lakini kutokana na hali ilivyo, mimi
ningelikushauri usahau hayo yaliyotokea, na uangalia mambo ya mbeleni, ...kwanza
cha muhimu,tuone kuwa mwenzetu huyu, anaondoka kwenye hiyo hali aliyo nayo...’akasema.
‘Hilo ndilo la muhimu, ...ila nataak kujua , na sitaacha
kutaka kujua, ni kitu gani kilitokea, hadi ikafikia hapo, na je hizo dhana zenu
potofu zina ukweli gani,...nataka kuyajua hayo ili nafsi yangu itulie, hamjui
jinsi gani ninavyopata taabu kuwaza jambo lisilojulikana, na jambo lenyewe
linaonekana sio jema kawa jinsi ninavyowaona, kwa jinsi mnavyoigiza, na sijui
mnataka nini...’nikasema.
‘Kitu kimoja ufahamu ,kama mtu anafikia kukuomba msamaha,
ina maana jambo hilo lina uzito fulani, kwake kinafsi na kwako pia,....japokuwa
ukimtendea mwenzako jambo lisilopendeza, hata kama ni dogo kiasi gani ni vyema
kiuungwana ukamuomba mwenzako msamaha,...’akasema.
‘Mimi ninachotaka kujua ni jambo gani lilitokea hadi mume
wangu akataharuki kisai hicho, na je linahusiana vipi na rafiki yangu,... maana
kila tukiongea na wewe unapenda kumchomekea rafiki yangu, kama vile kuna kitu
kimefanyika kati yao wawili, kitu ambacho nakiona hakipo,na kama rafiki yangu
huyo angelikuwepo, lingekuwa ni rahisi kwake kuligundua , namfahamu kikazi, na
sijui kitu gani kimemkumba, hadi kubadilika kwa muda mfupi, sijui, na hilo tena
linakuwa tatizo jingine, nahitajika kulijua, maana yule nilikabidhiwa mimi na
wazazi wake, sipendi aje kupata matatizo...’nikasema.
‘Inaonekana unamwamini sana rafiki yako, hujui kuwa rafiki
yako anaweza kuwa adui yako mbaya kuliko unavyodhania,...maana yeye anakufahamu
udhaifu wako, kwahiyo akitaka kukufanyia ubaya anaweza na ushindwe
kufahamu...maana unamwamini, ubnakuwa kiziwi na kipofu mbele yake, ...ukipenda
hata chongo utaliita ni kengeza..’akasema.
‘Acha fitina...huniwezi kwa mtaji huo..hilo niachie
mwenyewe...nafahamu kabisa hakuna tatizo kubwa kwa watu hawo, huenda ni tatizo
la ...mambo ya kibiashara, au...mh, siwezi kusema maana jambo gani linaloweza
kuwaunganisha hawa wawili....na kwanini niwashuku wapendwa wangu hawa ubaya,
hapana,...hizo ni fitina tu’nikasema
‘Kama una uhakika na hilo, hakuna shida, ila sisi kama
madakitari, tunajaribu kukwepesha jambo lolote la kumkwaza mgonjwa, ....wakati
kama huu sio wa kukaa na kulumbana naye kwa hayo yaliyotokea, upo muda utafika
yeye mwenyewe ataamua kukuambia, hilo ni moja, na la pili, kama kuna tatizo
ambalo linahitajia maamuzi, uchunguzi, jaribu kutumia hekima, maana kila
mwanadamu hukosea, huenda kosa hilo, ni dogo sana ukilinganisha na makosa
uliyowahi kuyatenda....’akasema.
‘Ina maana wewe hujui kosa alilolifanya rafiki yako, kama
kweli lipo kosa, sijui ni kosa gani maana kama ananiomba mashamaha, naona lipo
kosa, ...hebu sema ukweli wako, maana kama utanificha na siku nikaja kugundua,
basi wewe nitakuweka kwenye kundi la watu wasio na umanifu kwangu, nitakuchukulia
wewe kama adui yangu, anayenivizia kwa nyuma, ..na nakuambia ukweli, kama kuna
jambo nzito,.. sizani kama nitakuja kukusamehe, unanifahamu nilivyo...’nikamweleza.na
yeye akatabasamu, na bila wasiwasi akasema;
‘Kama ningelikuwa nafahamu ni kitu gani, ningelishakuambia, unaifahamu
ninavyokujali,...lakini pia natawakiwa kuwa makini, kwani wote nyie ni mar na
kwanini nisimame upande wa mume wako, kuliko kwako, ...mimi nakupenda sana wewe,
na yote haya nayafanya kwa vile najali, nakujali na nitendelfiki zangu,...na
inavyoonekana wewe unawaamini sana wenzako kupita kiasi,....na wameshakusoma
udhaifu wako....'akasema mimi nikitabasamu kwa dharau.
'Mimi najaribu kukuweka sawa ili uzindukane, maana mimi nakujali
sana wewe,na nakuahidi kuwa sitakubali upate shida wakati mimi naona, wakati
mimi nipo hai....unakumbuka niliwahi kukuambia hilo kabla na hata baada ya wewe
kunikataa...’akasema akinisogelea, na mimi nikarudi nyuma kumkwepa.
‘Unataka kufanya nini..’nikasema nikigeuka huku na kule
kuangalia kama kuna watu wanaotutizama, lakini niliona kila mtu na hamsini
zake, huwa sipendi jinsi gani huyu jamaa anavyofanya tukiwa karibu naye, ....
‘Sikiliza nilihskaukanya hii tabia yako ya kujiweka karibu
karibu na mimi, kunishika shika, sitaki, ..sipendi maana watu wanaweza kujenga
dhana mbaya ambayo haipo...sipendi, acha kabisa, kwani kuna siku nitakuadhiri
vibaya sana...’nikasema kwa ukali.
‘Nimekuelewa mpenzi, ...mpendwa, samahani....nafaya haya
bila kujijua,...’akasema.
‘Na mimi sio mpenzi wako..kumbuka hilo,...haya endelea na
fitina zako, ulikuwa unasemaje..?’ nikamuuliza nikisawazisha uso wangu, maana
nilishabadilika kwa hasira.
‘Unakumbuka nilivyokuwambia siku ile, tukiagana,siku ambayo
sitaweza kuisahau maishani, unakumbuka nilivyokuambia siku ile, ...kuwa nipo
tayari kufanya lolote kuhakikisha kuwa hakuna atakayekuumiza, ...japokuwa
ulinikataa,na kusema nisikufuate fuate kwenye maisha yako, lakini bado moyo
wangu upo kwako...ndio maana bado natunza ahadi yangu’akasema na mimi
nikajikuta nacheka kwa kebehi, nikasema;
‘Acha zako hizo, wewe sasa ni mtu mzima, una mke na watoto
hutakiwi uwe na mawazo kama hayo, ina maana mpaka leo hujakubali ukweli, kuwa
mimi nina mume ninayempenda zaidi yako, hata kama nilikupena kablsa, hata kama
sasa nakupenda, nilikupenda,na nakupenda kama rafiki , ila ujuekuwa kupendana
kuna kuzidiana, mume wangu nampenda zaidi yako wewe, ..tuache hayo yaliyopita
maana hayawezi kusaidia lolote, hizo ni zilipendwa, hebu nikuulize ina maana
mkeo humpendi?’ nikamuuliza.
‘Mkewe wangu nampenda, nilishakuambia hilo, nampenda tenasana,
nampenda kama mke wangu, lakini wewe ndiye niliyekupenda kabla, na pendo la
mwanzo, halilinganishwi na pendo la mbadala, maana ilibidi nimuoe yeye kwa vile
wewe ulishanikataa, sikuwa na jinsi,na sikuwahi kukukataa hata siku moja, ....kiukweli
wewe hujaondoka kwenye nafsi yangu..nilijaribu sana kukubembeleza, nilijaribu
sana kukuondoa kwenye nfasi yangu, lakini mmh, mungu mwenyewe ndiye anayefahamu
, na ni kweli ....ilifikia wakati
natakiwa nikakubali ukweli, lakini ilinitesa sana.’akasema na nikajikuta
nacheka.
‘Hivi hayo maneno unaweza kuyaongea mbele ya mke wako, au
mbele ya mume wangu?’ nikamuuliza nikimkazia macho na yeye akatabasamu na
kuangalia pembeni, akasema kwa unyenyekevu.
‘Mke wangu nilishamwambia hayo, anayafahamu sana, na
nashukuru mungu kuwa yeye ni mwelevu, na kama kuna mtu ambaye aliweza
kunisaidia kuiponya nafsi yangu, iliyokuwa imeathirika, basi ni mke wangu, yeye alichukua nafasi ya udakitari wa kulitibu
jereha ulilolisababisha wewe..., aliweza kunisaidia na kuijenga nafsi yangu
ikubali hali halisi kuwa wewe sio wangu tena, wewe ulishakuwa mke wa mtu
mwingine na mke wa afiki yangu, ...namshukuru sana kwa juhudi zake hizo,...na
kiukweli hata kama angelikuwepo hapa angelithibitisha hilo...namshukuru sana
mke wangu.’akasema kwa sauti ya huruma.
‘Mhhh, pole sana...’nikasema huku nikiguna kwa kebehi na
nilipotaka kusema neno yeye akasema kwa haraka haraka;
‘Hata ,mume wako mara kwa mara tukiongea huwa namwambia
hivyo japokuwa tunaongea kwa utani, ....niliwahi kumwambia kabla kuwa kama
itatokea akakuumiza, kama atafanya makosa, basi ajue mke wake nitamchukua
mimi....ni utani wenye ukweli ndani yake’akasema.
‘Usinichekeshe, ina maana mke wako mnaishije, kama moyo na
nafsi yako ipo kwangu, kuna upendo gani kati yako na mke wako, kama muda wote
unanifikiria mimi..na haya tusema mume wangu kaniumiza, au tukaachana utaweza
kunioa mimi na kumuacha mkeo, au ndio nitakuwa nyumba ndogo?’ nikamuuliza.
‘Sijafikia huko zaidi, sijawazia kufanya hivyo,....kukupenda
kwangu sio lazima nimuache mke wangu, kukupenda kwangu kupo moyoni, ..nafikiri
unafahamu hivyo, na siombei uachike,japokuwa ikitokea hivyo na nikakuoa mimi
ningelifurahia sana, lakini sijasema
nimuache mke wangu au wewe kukufanya nyumba ndogo,....’akasema.
‘Sikuelewi....una maana gani., na sihitaji kukuelewa, maana
hilo halipo, na halitakuwepo...’nikasema.
‘Sio kwamba muda wote nakufikiria wewe..hapana hilo ni jambo
lipo, kuwa nakupenda, lakini sio kwamba ni jambo la kunifanya nisimpende mke
wangu, nampenda sana mke wangu, kwani pamoja na yote hayo, alikubali ukweli,
akanisaidia, na anaendelea kunisaidia kuponyesha jeraha uliloisababisha
wewe....’akasema.
‘Mhh, usinitwike, mzigo nisiostahili, mimi sijasababisha
jereha lolote kwako, kama ni jeraha umejisababishia mwenyewe, maana hatukuwa
tumeoana, tulikuwa marafiki tu, na unakumbuka wakati ulipotaka kunichumbia
nilikuwambia nini, kuwa mimi bado sijafikia umauzi wa kuwa mchumba au mke wako,
nahitajia muda wa kufikiria, sikuwa na malengo ya muda mrefu na wewe,...na baadaye
nikaja kukuambia kuwa nimempata ninayempenda zaidi yako, je ulitaka tuishi kwa
kudanganyana...?’ nikamuuliza.
‘Hilo siamini,..eti ulikuwa hunipendi, , huwezi kunidanganya
mimi, ninafahamu fika ulikubali kuolewa na mume wako, kwa nia ya kulipa
fadhila, moyo na nafsi yako ilikuwa kwangu, hilo nina uhakika nalo, ila kwa
vile wewe una tabia yako, kuwa ukitaka jambo liwe, huwa hugeuki nyuma, hata
kama litakuleta madhara, wewe unataka ulifanye tu, au ulipate,hata kama
litakuumiza, sio vizuri hivyo huoni sasa mnavyoishi, hamna raha, tusidanganyane
ndoa yenu haina raha, na kosa ni maamuzi yako ya haraka, ya kujifanya mwema,
eti unalipa fadhila.....’akasema na mimi nikatabasamu na kusema.
‘Hayo yamepita tugange yaliyopo na yajayo, ambayo ndiyo
ukweli wenyewe, wewe una mke wako, na mimi nina mume wangu, tusiingiliane, na
tusiharibiane ndoa zetu, heshimu ndoa yako, na mimi niache niheshimu ndoa
yangu..hayo ya kusema hatuishi kwa raha, ni hisia zako potofu, na kila ndoa ina
matatizo yake, sio kwamba ndoa yangu ni ya kimiujiza, sisi ni wanadamu ....’nikasema.
‘Hilo nalifahamu, lakini sitakubali mtu akuumize, hilo ni
ahadi yangu, hata kama hutaniamini hivyo, hata kama hutakubaliana na hilo, hilo
ni nadhiri kwenye nfasi yangu, hadi naingia kaburini,hata kama hutakuwa mke
wangu, lakini mapenzo kwako yapo pale pale ...’akasema na mimi nikajikuta
nikimwangalia kwa mashaka.
‘Hivi wewe mwanaume una akili kweli....sikiliza, wewe ni
msomi, dakitari, nilitarajia wewe kunionyesha njia na masimamo wa mambo kama
haya, ambayo tunahitajika kukubali ukweli, umesahahu kazi yako eehe..unajiona
wewe ni bora, sio wale, au yale unayoyashauri kwa wenzako, ukumbuke kuwa na
wewe ni mwanandoa na una ndoa yako, unavyowashauri wengine, na wewe ujishauri
pia.’nikasema.
‘Sijasahau mpendwa, hata nikiwa dakitari, ubinadamu na
utashi wa kupenda upo pale pale...nashukuru kuwa na wewe unalikubali hilo, kuwa
ukiwashauri wenzako na wewe ujishauri hivyo hivyo,....ukumbuke ulismhauri nini
rafiki yako....’akasema na kuniangalia machoni.
‘Kwani nilimshauri kitu gani kibaya..?’ nikauliza kwa
mshangao.
‘Kama sio kibaya kwanini unapata shida...kwanini unataka
kujua baba wa mtoto wake ni nani, kwanini haya yanatokea, ...nalitumai
ungelikaa kimiya na kumpa mwenzako hongea kwa kufuata ushauri wako...’akasema.
‘Kwani mimi nimefanya nini kibaya, kwani nimemshutumu kwa
hayo aliyoyafanya, ...wewe hujui tu, mimi nilikuwa nye bega kwa bega, kumpa
hongera, na mengine ya kutaka kujua baba yake, nafanya hivyo kwa vile mimi
ninakaa naye, ni kama mzazi wake, nataka kumjua ili nijue jinsi gani ya
kumlinda, hakuna tatizo hapo...’nikasema.
‘Ok, tuyaacha hayo,, ila nakuomba unisikilize kwa makini,
fanya kama nilivyokuambia,kama kweli unampenda mume wao, kama kweli unampenda
mume wako apone haraka, fanya kama nilivyokuambia, ni bora uigize kuwa huna
chuki, huna kinyongo naye huyajui yoyote yanayomzunguka na hayo aliyoyafanya, yapotezee,
kuliko kuonyesha hiyo hali ya kukasirika, ...wakati kama huu anakuhitajia sana...’akasema.
‘Nimeshakuelewa, tunaweza kwenda...maana inachukua muda, ina
maana hawo madakitri hawajamaliza kuwapitia waginjwa?’ nikamuuliza.
‘Tunaweza kwenda, ila hilo ni muhimu, kuliko kwenda kumuona
na ukawa ndio chanzo cha kumfanya asipone, kwa hivi sasa yupo kama kapagawa, ukimuuliza
jambo anakuangali tu machoni, haongei kitu, na docta wake kasema tumpe muda,
ila akashauri wewe uje, ili tuone kama itasaidia, kila mtu anajiuliza je kuna
kitu gani aliongea na huyo rafiki yako, mimi ninaona wewe ndiye unayeweza
kuibadili hiyo hali, kama kweli unampenda mume wako....’akasema.
‘Kama nisingelikuwa nampenda, nisingelikubali kuolewa na
yeye, na kuzaa naye watoto wawili, nampenda sana mume wangu na nitaendelea
kumpenda, hata kama nyie mafitina mtaendelea kuchochea chuki na fitina
zenu...’nikasema huku nikitembea kuelekea huko hospitalini na huyo docta
alikuwa bado kasimama,kama vile haniamini.
‘Sawa nimekusikia, ila nazidi kukusisitizia, kuwa....kama
hutaki mume wako apone haraka endelea kujenga sura ya chuki,sahau kabisa
kujenga hiyo sura ya kuonyesha hasira na chuki, kwani kosa dogo, mbele ya mume
wako, linaweza kuleta madhara makubwa sana, kwa sasa hivi akili na ubongo wake,
hauhitaji mzigo wowote wa mshituko,au shinikizo la kumsononesha, usipofuata ushauri
wangu.....utakuja kujilaumu mwenyewe, usije ukasema sikukukanya ...ni muhimu
sana..’
Maneno hayo yalinifanya niwe kwenye mtego, na ulikuwa mwiba
nisioweza kuutoa, nikawa nagugumia kimoyo moyo, japokuwa nilitaka kufanya
jambo, japokuwa nilikuwa nataka kujua ukweli,kuna nini na kwanini ananiomba
masamaha,....je ina maana nife na tai shingoni, hapana, kuna namna, ama kutoka
kwake, au kutoka kwa mtu mwingine, ni lazima nifahamu ukweli,..nikakumbuka.
‘Ni lazima nimuona mdogo wake...huyu anaweza kujua jambo
nikasema, na wakati huo tulikuwa tunaingia chumba alicholazwa mgonjwa...
NB:Je nitaweza kuvumilia....
WAZO LA LEO:
Tunapopenda, tusiwe tumependa kupitiliza, na hata kusahau udhaifu wetu wa
kibinadamu , mwenzako anaweza kukosea, mkosoe kwa hekima, usiogope kuwa ukimkosa
mtakosana na wewe ukaamua kukaa kimiya, huko sio kupenda, ni kupondana kwani
mwisho wa siki likahar elezaneni ukweli, japokuwa ukweli unauma, ...ila kwaibika
jahaz mtazama wote. Kama mume au mke wako yupo kwenya hali mbaya ya ugonjwa, au
yupo kwenye matatizo, basi uwe na hekima, usikimbilie kuhamaki, kulaumu,
kuhusiana na hilo kosa, cha muhimu ni kuvuta subiri , hadi kuwe na wakati
muafaka.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Huyu mdada anatia huruma kaingia shimo alilochimba mwenyewe..
[url=http://effexorgeneric.eu/]effexor generic[/url] [url=http://cleocin.in.net/]cleocin topical[/url] [url=http://colchicine.mom/]colchicine[/url] [url=http://buytadalafil.accountant/]tadalafil[/url] [url=http://buy-zithromax.cricket/]zithromax pack[/url] [url=http://buy-nexium.in.net/]nexium 20[/url] [url=http://cleocin-gel.mom/]cleocin gel for acne[/url]
Post a Comment