Mama akaendea kuongea;
Nilipohakikisha kuwa
yule mwanaume, keshaondoka, kwa haraka nikarudi ndani, na nilipofika, nilimkuta
babu yako, ndio anamsogolea yule mwanamke, na panga likiwa limeinuliwa juu, na
yule mwanamke , rafiki yangu alikuwa kapiga magoti, huku kainua mikono juu,
akiomba msamaha..…
‘Baba unataka kufanya nini…..’nikasema huku nikimkimbilia na
kujaribu kuudaka ule mkono wenye panga, na nilikuwa kama nimechelewa , maana
lile panga, lilishashuka,na lilikuwa likitua kichwani mwa yule mwanamke,
nikaweka nguvu zangu zote, kwanza kwa kumsukuma huyo mzee, na pili kuudaka mkono
wa huyo mzee ulioshikilia panga.
Babu yako ana nguvu, japokuwa alikuwa kazeeka, lakini nguvu
zake zilikuwa pale pale, maana hata kumbipa kikumbo cha kumsukuma kwa nguvu
zote, lakini hakutikisika, ilikuwa kama mtu anapiga kikumbo mti ,mnene,
…..lakini hata hivyo, kwa kuwahi kuudaka ule mkono, niliweza kupunguza ile
nguvu kushuka lile panga, na likawa limemgonga yule mwanamke kichwani.
Kutokana na ile hali ya kutumia, nguvu nikajikuta
nimemdondokea yule mwanamke, na sote wawili yaani mimi na yule mwanamke, tukaanguka
chini na kulaliana, na baba alikuwa bado na lile panga mkononi, akitaka
kulitumia tena, lakini akashindwa kufanya hivyo kwani mimi nilikuwa juu ya yule
mwanamke nimemlalia na hiyo ndio ilikuwa salama yake.
Akiwa anatetemeka kwa hasira babu yako akalitupa lile panga
chini na kugeuka, akatembea kwa mwendo wa tambo,….hadi dirishani na kuangalai
nje, huku mwili mzima ukiendelea kumtetemeka kwa hasira,…sijui alikuwa akiwaza
nini, kwani baadaye akageuka, na kipindi hicho nilikuwa nikimsaidia yule mwanamke
kukaaa vyema.
Yule mwanamke rafiki yangu alipomuona babu yako kageuka, akajua
atamreejea tena….na kwa muda alikuwa akielekea pale lilipokuwa panga,….yule
mwanamke kuona hivyo, akajua salama yake haipo tena,akanisukuma,….haraka
akasimama, na bila kujali, alivyokuwa, maana kule kuanguka chini, nguo zake
hazikuwa zimemfunika vyema, yeye akainuka, na mbio akaelekea mlangoni,
akafungua mlango hakugeuka nyuma, akakimbia, na mimi nikamshukuru mungu
Babu yako akalifikia lile panga lake, akaliokota na kulishikilia
mkononi, huku mkono ukiwa umetuna na kuonyesha nguvu, kuashiria kuwa alikuwa
kalishikilia kwa nguvu, alilishikilia lile kwa muda huku akiwa kaliangalia, na
baadaye bila kugeuka kuniangalia , akasema;
‘Bahati yake, lakini bado hajaniponyoka….hawa watu
hawastahili kuishi, maana ni sumu ya maisha ya watu, kazi yao kubwa ni fitina,
na mfitinashaji ni zaidi ya mchawi…..watu wanakimbilia kuwaua wachawi, na
ingelikuwa basi wanawau kweli wachawi, lakini wao wanawaua watu wanaowafikiria
kwa dhana zao kuwa ni wachawi, na kuwaacha hawa watu wabaya …..hawa watu ni wabaya
zaidi kuliko mnavyowafikiria, wana sumu kali zaidi ya nyoka mwenye sumu ya
kuua, na mimi mzee jemedari wa vita, nimeamua kupambana nao, usiku na mchana…..’akasema
na kuliinua panga lake juu, halafu akaondoka.
‘Sasa baba unakwenda wapi…?’ nikamuuliza huku nikijizoa zoa
kumfuata.
‘Hiyo sio kazi yako, mimi sasa ,….nipo vitani, …..’akasema
na kutoka nje kwa hatua za askari wakiwa vitani.
Nilijaribu kutoka na mimi ili nimuwahi, ili ikiwezekana,
nimzuie,….hata kwa kumsihi…lakini haikusaidia kitu, alikuwa keshafika mbali.
Maana babu yako ana mwendo wa haraka sana, na uzee wake huo, lakini aliweza
kutembea kwa mwendo kasi , kuliko vijana wenye nguvu zao.
‘Oh, …Sijui nifanyeje,….’nikawa nahaha, nashika hiki
hakishikiki, na huku naongea peke yangu kama mtu aliyechanagnyikiwa;
‘Na huyu mume wangu naona kachelewa kurudi,….siku hizi
kaamua kulewa tuu, pombe na yeye , ..’nikawa naendelea kuongea peke yangu, na ghafla
nikasikia kilio, kilio kilichoashiria
hatari, nikajau kuna janga tena limetokea……
********
Nikawa nakumbuka babu
alivyokuwa akielezea sehemu hiyo, na muda huo alikuwa kaegemea kiti chake cah
enzi, kikinesanesa, alisema;
‘Nikiwa na panga langu mkononi, nikaelekea sehemu jengo
langu, kwani mama yako aliamua kunijengea nyumba ya kisasa, sio ile ya miti na
majani,….na ujenzi ulikuwa bado ukiendelea, sikupenda kubakia pale nyumbani kwa
mama yako, kwani akili yangu ilikuwa imesimama kufikiria zaidi,…kilichokuwepo
ndani ya akili yangu ilikuwa hasira, kisasi….
Nilijua kabisa , ndivyo nilivyokuwa nikiwaza kuwa kama
nitakuwa karibu na mama yako nitashindwa kutimiza malengo yangu,…..nipo vitani,
na ukiwa vitani, rafiki yako ni yule atakayekusaidia kumshinda adui yako…hekima
za utu uzima kwa muda huo zilikuwa zipo mapumziko,…na mimi nilijiona nadaiwa
kwa kutokuweza kumlinda mke wangu hadi akafanyiwa hicho alichofanyiwa,…..hata
kama nitafanya nini, sitaweza kulipa, lakini….hilo linalowezekana kwa ajili ya
wengine, lifanyike….
Nikawa natembea haraka haraka kijasiri, uzee, ulisahaulika….,
na nilipofika kwenye njia ya makutano, inayoeleka kwangu, na ile inayoelekea
kwa yule mwanamke mfitinashaji nikasimama, nakuangalia kushoto, kulia, halafu
kuelekea njia ya huyo mbaya wangu,….kwanza inabidi uwe na malengo, huwezi
kwenda kumvamia adui yako bila malengo….
Oh, sio mbali na pale niliposimama, nikawaona watu wawili
wakigombana, na pembeni yake, alikuwepo yule mwanamke mfitinashaji, …..alikuwa
kashika kichwa, na akipiga ukulele wa kuomba msaada, nakumbuka kuusikia huo ukelele,
lakini sikuwa nimeujali sana, nilijua labda ni wale vijana wanaendelea
kuteketea……nigeuka na kumwangalia yule mwanamke, nay eye akaniona
Yule mwanamke aliponiona, kwanza alipanua mdomo kuendelea
kupiga ukelele, lakini, akatulia, hakutoa sauti, macho yake yakamtoka pima kwa
woga, akaniangalia,…hakukimbia, akabakia kasimama kama kapigilia
misumari,akijua kuwa sasa yupo hatarini, lakini haweza kukimbia…...
Mimi sikujali, nikamueleka na sikuwa ninawajali hawo watu wawili
waliokuwa wakipigina, na kwakweli, walihitajia msaada, mtu wa kuwaamulia,…walionekana
kuwa wameumizana sana, na sijui ilikuwaje, maana jicho langu lilimuona mmoja
kati ya wale wapiganaji, na hisia za udugu, zikapenya ndani ya akili yangu, na
kulegeza hisia za hasira,… nikamuona…alikuwa kachoka, na kama nisingelimuwahi,
angelimalizwa na adui yake…
‘Baba nipo chini ya miguu yako, mume wangu atamuua,
…..mwenzake, nakuomba nipo chini ya miguu yako, nakuomba uwagombolezee….’akasema
huyo mwanamke mfitinashaji, huku sasa akipiga piga miguu chini, hakujua
afanyaje, maana mimi ni adui yake, mumewe, anataka kuua, na yeye hawezi tena
kugombolezea, kwani kwa muda huo, alishaumizwa, uso ulionekana kuvimba…..
Na kwa vile nilishamuona baba yako, akiwa taabani….kuwa ndiye
anayepigwa na karibu kuuwawa,na huyo ni mume wa binti yangu wa kufikia , yaani
mama, yako, hasira kwa huyo mama mfitinashaji zikawa zimeisha, na nguvu
zikaelekezwa kwa huyo anayempiga baba yako. Nikainua panga, kwa nguvu, nikiwa
nataka kufanya jambo ambalo kama lingelifanikiwa tungelikuwa tunazungumza
mengine.
Lakini lile panga likiwa hewani, nikaligeuza, kwenye makili
kukawa juu, na kwa haraka likatua kwenye mkono wa huyo jamaa anayekuwa akimsindilia
baba yako, bila huruma, damu zikiwa zimejaa kwenye mkono na kwenye nguo zake,
alikuwa na dhamira moja, ya kummaliza baba yako.
Lile panga lilitua kwa wakati muafaka, na sijui wazo la
kuligeuza juu chini lilikujaje, labda ni huruma, labda…sijui ila liliokoa
mengi, la sivyo, huyo jamaa asingelikuwa na mkono,…., kwani kuligeuza kule
likiwa hewani, lilipunuza hata ile kasi ya kupiga, lakini lilifanya kazi yake iliyokusudiwa,
likajeruhi, na kuvunja nguvu ya huyo jamaaa…likauumiza ule mkono ambao ulikuwa
ukipiga, ukipiga, na kupiga, kwa lengo la kuua,…na kila pigo, lilikuwa
likiashiria kummaliza huyo anayemuona ni adui yake..
‘Ooooh….’mguno wa maumivu ukasikika kwa huyo jamaa, na
haraka akashikilia mkono wake na kugeuka kuniangalia. Na baba yako ambaye
alikuwa akigugumia kwa kila kipigo, akiwa hana nguvu tena ya kujitetea, akalala
chini….kuashiria kuwa yupo katika hali mbaya, alihitajia msaada wa haraka.
Nikamsukuma huyo adui yake ambaye aliserereka hadi chini, alidondoka kama
gunia, huku nikisema kwa sauti ya ukali.
‘Wewe unataka kuua…hivi wewe unapigana na mtu ambaye hana
lolote, mtu huyo ni mgonjwa, kama una nguvu kweli pigana na mimi…uone ni nini
nitakufanya…’nikamwambia huyo jamaa huku niligeuza lile panga tayari kwa pigo
jingine….nikawa namwendea pale alipodondoka, alikuwa kakaa huku akshikilia
mkono wake, akiniangalia kwa uwoga, …ujasiri, hasira vyote, vilinywea, huenda
ni kutokana na maumivi aliyokuwa akiyapata kwenye mkono wake….
‘Baba tafadhali,….’nikasikia
sauti….na moyoni nikasema; `huyo tena
kaja hadi huku…’
Ilikuwa ni sauti ya
mama yako, alikuwa akija mbio mbio…sikugeuka kumwangalia, kwani huyu jamaa
ninayeambana naye, sio mchezo na lengo langu ni kuhakikisha ninamaliza nguvu,
lakini yule jamaa alikuwa kakaa, na sasa alikuwa akijitahidi kusimama, akigugumia
maumivu, ilionekana wazi kuwa pigo lile la langa huenda limevunja mfupa wa
mkono wa huyo jamaa.
‘Oooh…’akawa anagugumia, lakini mimi sikumjali, nikamsogelea
kwa ujasiri, na yule jamaa aliponiona namsogelea, na panga mkononi, kwanza
alitoa macho ya uwoga, na akapanua mdomo kutaka kupiga ukulele, na baadaye
nikashangaa kumuona akiyumba upande kama vile ananikwepa,…, na ghafla
akadondoka chini na kulala, akatulia kimiya, nikajua ni janja yake, lakini
haikuwa hivyo, alikuwa kapoteza fahamu, na ndio ikawa ahueni yake.
‘Baba…..mwache, utaleta makubwa zaidi….’akaita mama yako, na
nilipogeuka nilimuona akiwa kamshikilia mume wake, baba yako alikuwa kajaa damu
mdomoni na puani, na alionekana katika hali mbaya sana, ..nikageuza kichwa huku
na kule, na mara uso wangu ukakutana na yule mwanamke mfitinashaji,…hasira
zikanipanda, na yule mwanamke akafahamu hilo, akatimua mbio…
Watu wakawa wamefika kwa wingi, na wale walioshuhudia huo
ugomvi, wakawa wanahadithia, mimi sikuwa na cha kuongea, nikawa nahangaika na
baba yako,…na hatimaye, tukafanikiwa kumpeleka hospitalini, akiwa taabani.
‘Sijui kama atapona…’nikasikia watu wakiongea, na hapo
hasira zikazidi kunipanda, nikijua kuwa hawo ni watoto wangu japokuwa sikuwazaa
mimi, na kama nimeshindwa kuwalinda ni nani atawalinda. Unajua unaopokuwa mtu
mzima, haijalishi kuwa una uwezo, au nguvu kiasi gani, mtoto bado unamuona kama
ni mtoto, na unajiona wewe una nguvu zaidi yake, japokuwa sio kweli….
Kwa hasira nikawageukiwa watu waliokusanyika hapo, nikasema
kwa sauti ya ujasiri;
‘Nawaambieni nyie watu mumetangaza vita dhidi yangu….na sasa
ni vita kwa yule yoyote anayehusika na hili ajue kuwa yupo vitani na mimi….ambaye
yupo uapnde wangu ni yule atakyenisaidia kuhakikisha hawa wanahusika na hili, na
pia hawo wanahusika na mauji ya mke wangu, wanasambaratika na kusahaulika
kwenye hiki kijiji….’nikasema kwa sauti, nikiwa nina uhakika kuwa watu watakwenda
kumwambia huyo jamaa na jamaa zake.
‘Yeye anajifanya ana nguvu hapa kijijini, kuwa anaweza
kupiga wenzake kama watoto wadogo, sasa atakuja kupambana na mimi,…’nikasema
nikiangalia ule upande aliolala yule jamaa, alikuwa bado kpoteza fahamu.
‘Na ole wake, huyu mtu apoteze maisha, ….ajue ni mimi
nitalipiza kisasi kwake, labda ahame huu mji, na akihama nitamfuta huko huko….mjue
sasa ni jicho kwa jicho….’nikasema kwa hasira na watu wanaonifahamu wakaguna,
na wengine wakaana kuondoka wakiogopa, hasa pale niliposimama. Mjukuu wangu usnione hivi na huu uzee,
lakini ninapobadilika, natisha….walikimbia…’ Babu akasema ajiangalia
maungoni mwake.
Japokuwa nilikuwa mzee, lakini historia ya ushujaa wangu
ilikuwa inatambulikana, kwani enzi nzetu, tulikuwa na mapigano ya hapa na pale,
kugombea maeneo, mifugo, na mimi nilikuwa mmoja wa majemedari walioaminika
kwenye ukoo wetu, na hakuna aliyeweza kupambana na mimi, hadi nikawapewa
uongozi wa ukoo wetu.
Kwahiyo kwa wanaonijua, hasa wazee wa rika langu na
waliokuja baadaye , karibu karibu na marika yetu, walijua nimemaanisha nini, na
haraka haraka wakakutana , na sikujua walikutana saa ngapi, maana wazee toka
vijiji vya jirani, waliokuwa wamehama, waliitwa, wkajipanga kuja kulisuluhisha
hiloo jambo kabla mambo hayajafika kubaya.
Kesho yake asubuhi na mapema, wazee wa huo ukoo wa huyo
jamaa wakafika kwangu, wakiwa na ngombe, na mazao kwa kufuata mila za kwetu,
kunapotokea jambo kama hilo, suluhu kwa mkosaji, ni kuja na ngombe dume, kuja
kumuomba yule aliyekosowa na wanakuja wazee wenye busara, sio wazee tu, kwani
enzi nzetu, kulikuwa na wazee walioheshimika,….wakiongea jambo, linasikilizwa,
linaheshimika, na hawaongea maombo ovyo ovyo tu kama siku hizi…
Sikutaka hata kuongea nao, nikawaambia;
‘Suluhu hapa ni huyo jamaa apone, …akifa hakikisheni na huyo
aliyempiga…huyo mgonjwa, maana mnamuona wenyewe ni mgonjwa, hajiwezi…yeye anakwenda
kutunisha misuli kwake, anakwenda kummalizia, haoni aibu….sasa kama akifa
hakikisheni na yeye mnamuua wenyewe,….’nikasema huku panga likiwa mkononi.
‘Hebu niambieni, huyo mgonjwa ana nguvu gani ya kupigana,
mtu mwenyewe mnamuona keshajifia,….anaumwa,….kabakia mifupa…keshaisha, bado
mtoto wenu anatunisha kifua, anapiga kama mtu anayeua mnyama….mngaliona jinsi
gani alivyokuwa akimsindilia mwenzake migumi, msingelifika hapa,…..kwakweli
suluhu hapa hakuna, nendeni kwa huyo jamaa yenu, shujaa wenu, mwambie
akijtundike kamba, kabla sijakutana naye…………..’nikasema na nilikuwa naongea kwa
hasira kweli kweli.
‘Mzee mwenzetu, hawa ni watoto, na sisi tunatakiwa
tuwaonyeshe kuwa sisi ni wazee wao, tuwafunde,…maana kama unavyoona, dunia ya
sasa sio kama ile ya kwetu….watoto wa siku hizi hawana adabu, hawasikilizi
wazee wao, sasa sisi ni wazazi tunahitajika tujitahidi hivyo hivyo…kwa ujumla
kakosa sana, katuabisha sana, ndio maana sisi wazee tuliobakia ambao
tunaheshimu mila na desturi tumeamua kuja kukuona.
‘Mzee mwenzetu… kimila mtu jasiri, mwenye hekima, huruhusiwi
kupigana na mgonjwa, au kupigana na akina mama, au kupigana na wazee
wasiojioweza, lakini mwenzetu huyo hasira zimemtawala…hana adabu,…hatusikii….wazee
tumemchoka, tunakiri hilo, lakini yeye asiwe kisingizio cha kuvunja udugu,
mshikamano…na kuvuruga amani za eneo letu hili….’akawa anaongea kiongozi wa
wazee wao.
‘Sasa kama hasira zimemtawala, tunataka tuzione kwenye uwanja
wa mapambano….si ndio anavyotaka,, kuonyesha kuwa yeye ni mwanaume….sasa
mwambieni kuwa leo nataka kuonana na yeye kwenye uwanja wetu wa mapambano,…mimi
na yeye, nimemaliza….’nikasema na kugeuka na kuwaashiria kwa mkono waondoke.
‘Mzee mwenzetu, tunakuomba tena sana,….maana hata hivyo
jamaa mwenyewe mkono umevunjika, imebidi na yeye apelekwe hospitalini,
amefungwa muhogo, …sasa kawa kama kachanganyikiwa kila anayemsogelea
anamuogopa,…sasa hivi anamuogopa kila mtu, ….utafikiri anaona vitu gani. Hata
mkewe hivyo hivyo amekuwa kama kachanganyikiwa, wote sasa ni wagonjwa,
wamelazwa wodi ya vichaa, hawajiwezi, wapo taabani….’ Akasema huyo mzee,
akionyesha masikitiko .
‘Wakati mke wangu anaungua, wakati haya yanatokea kwenye
familia yangu, hamkusikitika, mnasikitika kwa ajili ya familia yenu, hamuhisi
wenzenu wnavyoumia, ….kama kweli mlikuwa mkijali, mngelihisi maumivu ya
wenzenu, kama nyie, hamuwapendi majirani zenu, mkajipenda wenyewe, mnafikiri
salama itakuwapo…..’nikawaambia.
‘Mzee mwenzetu, tunajua tumekosa, na ndio maana tupo hapa,
tunakuomba sana,familia kwa hivi sasa ipo kwenye hali ngumu,….tunakuomba tuikoe
hiyo familia kabla mambo hayajawafika pabaya….tunaelewa ni nini kitafuata baada
ya hapo…sisi wazee tunalifaham hilo, …kizazi hicho kitakwisha, kitasahaulika,
na huenda chuki hizo zikasambaa, na….kuvuruga mshikamno wetu, ….tunakuomba
ulione hilo kwa hekima zako jemedari….tunakuomba, ten asana…’akasema huyo mzee.
‘Na bado….nawaambia na bado, yeye na wale wote wale
walioshirikiana, kutaka kuiangamiza familia yangu,yatawapaat makubwa, mlikuwa
kimiya wakati watu wanatanagza fitina, wanaitanagzia familia yangu mambo ya
kichawi, mlikuwa hamuoni, nafahamu kabisa wengi wenu wenye maono ya mbali
mlijua kabisa kuwa sio kweli…mke wangu yupo mbali kabisa na hayo
waliyoyasingiziwa ….’nikawaambi nikawaangali wazee wale, ambao walikuwa
wametulia kimiya.
‘Au ninaongopa, ni nani mwenye uhakika na huo uzushi
animabie, ,…..aaah, sitaki kuwalazimsiha, kama kuna ambaye ana ushahidi wa kuwa
mke wangu alikuwa mchawi animabie, ili na mimi niwe na amani….nani ana huo
ushahidi, au twendeni tukale amini, kuwa kweli hayo yaliyozungumzwa ni kweli,
kama ni kweli mimi niangamie, na kama sio kweli nyote mnahusika muangamie,
twendeni tukale amini….’nikasema nikaanza kuondoka.
‘Mzee mwenzetu, sio kweli, tunajua kabisa kuwa huo ulikuwa
ni uzushi….lakini watu wengi walikuwa wakimuamini sana huyo mtaalamu, na sisi
hatukuwa na la kusema….hilo linahitajia kukaa kijiji kizima na kutubu, maana
matokea yake ndio hayo yanaanza kutokea, mabya yatatuandama, na tujuavyo, mabaya
yakiendelea yatatuasiri sote, …..’akasema huyo msemaji wao.
‘Sasa mnaanza kuogopa, kipindi kile mlikuwa mumejifungua
ndani….au mnajidai kuwa hamukuwa an nguvu ya kumwambia huyo mtaalamu kuwa
anachofanya sio kweli….kumsingizia mke wangu kuwa ni mchawi, hilo sijui
mtalimaliza vipi….wote ni lazima waishie kubaya,…nawaambia ukweli, kilio changu,
kilio cha mke wangu, alicholia wakati anaungua na moto, hakitaisha hivi hivi
mpaka, wote waliohusika na wao wayapate kama hayo yaliyompata mke wangu
……’nikasema.
Mara ghafla, wale wazee wakapiga magoti mbele yangu….kwa
wazee kama hawo kupiga magoti, ni jambo kubwa sana, na haijalishi una nguvu au
hasira za namna gani, kama wazee wenzako watafikia hatua ya kukupigia magoti,
inabidi usalimu amri, na hapo nikaduwaa, nikajikuta nimesimama mwii mzima
ukinitetemeka kwa hasira, ….hadi nikawa sina nguvu tena, na sijui kilinikuta
kitu gani,
`Mjukuu wangu, naona lwa leo tuusihie hapa maana hasira
chuki…bado vipo moyoni,…nakumbuka hali niliyoiskia pale sikuweza kuvumilia, nikadondoak
chini, na giza likatanda usoni mwangu, na sikujua ni nini kiliendelea hapo tena….’akasema
babu huku machozi yakimlenga lenga
*****
NB: Tusemeje, tukatishe kisa, maana huenda nawaboa…sawa,
tuombe mungu, akitujalia tunaweza tukaendelea
WAZO LA LEO:
Inapotokea hali ya mtafarauku, watu wakakosa kuelewana, jambo jema ni suluhu, sio
mababu,na suluhu haiji mpaka watu, wenye hekima wakutane, waongee na waone
jinsi gani wataliondoa hilo tatizo.
Jamani Propoganda potofu, uchochezi, fitina, ni adui mkubwa,
mkubwa zaidi ya bomu la nyukilia,..tuvikwepeni hivi vitu…tusione ni rahisi tu
kuandika, kuongea,…madhara yake ni mbaya. Tukaeni, tuongeeni, na tuangalia wapi
tumeteleza. Haya ni kwa maslahi ya vizazi vyetu, na taifa letu kwa ujumla,
ubinafsi, hautatusaidia kamwe, tusipopendana, na kumpenda jirani yako,…haki
ikatawala hakutakuwa na amani kamwe.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
I blog often and I genuinely thank you for your content. This great article has truly peaked my interest.
I will book mark your site and keep checking for new details about once per week.
I opted in for your Feed as well.
Also visit my homepage: http://hotgirlsexcam.com
Excellent post but I was wondering if you could
write a litte more on this subject? I'd be very thankful if you could elaborate a little bit further. Thank you!
Here is my homepage - party sex
Post a Comment