Unapopanda mche au mbegu kwenye ardhi, unatarajia mavuno
ambayo yatakuwa mbegu kwa mavuno mengine. Lakini mavuno hayo yanatategemeana na
jinsi gani ulivyoiboresha hiyo ardhi, na mazingira mazima ya eno hilo.
Kwa utaalamu wa kilimo, mimea mbali mbali, ina stahili yake
ya udongo, ndio maana kahawa ya kagera haistawi vyema Kilimanjaro, japokuwa zote
ni kahawa. Mahindi na mharage yanahitaji aina fukani ya udongo ili yazae vyema,
japokuwa sasa hivi kuna utaalamu wa kuboresha ardhi, lakini kama huo uboreshaji
utakosekana, basi ina maana mazao hayo yaliyopandwa kwenye udongo usiostahili
hayatastawi vyema.
Wakati nikiwaza hili nikajikuta nikiwazia watoto wetu,….nikaangalia
haya matukio yanatokea katika dunia yetu hii, nikakumbuka usia wa babu yangu.
‘Wajukuu zangu, watoto
wa leo, yaani nyie, ndio mtakaokuwa chachu ya amani kesho na kesho kutwa, mjue
msipojiweka sawa, kimaadili, mkakazania elimu yenu, mtarajie mavuno mabaya
baadaye . Ni sawa na kama vile tunapanda mbegu ya mahindi mahali ambapo, hapana
mbolea
…..Na hata kama pana mbolea, lakini bado tumepanda kwenye udongo
usiostahili….leo mlitakiwa msome kwenye shule zilizo na vifaa vya kisasa ili
mjue sayansi muwe madakitari, lakini wapi…hata chaki ya kuandikia hakuna….tutafika
kweli’
‘Lakini wajukuu zangu
msikate tamaa….kama mnajitambua wenyewe, na mnajua nini kipo mbele yenu,
msikate tamaa, sisi hatukata tamaa, ndio maana mumezaliwa nyie….cha muhimu sana
tambueni vipaji vyenu vya kitaaluma vitawasaidia sana….’
Ni kweli kila mtu amejaliwa kipaji chake, huenda hilo watu
wengi hawafahamu, inawezekana vipaji vikalandana, hiyo sio tija, lakini cha
muhimu kwanza ni kukitambua kipaji ulichobarikiwa nacho ambacho ukikitambua
vyema, utaweza kufanya jambo fulani kwa uwezo mkubwa, kuliko mwingine ambaye
hana kipaji hicho. Kuna vipaji vya kujifunza, hilo hatukatai, lakini vipaji vya
kujifunza, mtu hawi na wito nacho, kwake yeye ni sehemu ya kukidhi matakwa
fulani tu.
Wakati watu wanahangaika kutafuta ni kwanini watoto wetu
wanafeli mitihani,…elimu inazidi kudorora, na kujikuta tukilaumiana kuwa
kwanini watoto wetu hawafanikiwi kwa kiasi kikubwa, nafikiri pia
tungeliliangalia hilo la vipaji kwa watoto wetu, kama sehemu mojawapo
yakuwezesha kuboresha elimu za watoto wetu kwa kiasi kinachotakiwa.
Ili kulitambua hili kwa mapana, chukua watoto kadhaa
wafundishe hesabu kwa mtizamo sawa, jitahidi sana somo hilo lieleweke kwa kila
mmojawapo, utagundua kuwa kati yao kuna watakaoelewa zaidi yaw engine na
wengine wanaweza wasielewe kabisa. Sasa je utasema hawa wasioweza kuelewa
kabisa au wameelewa kidogo, hawana akili, hapana, kila mtu anakili,…, lakini ni
kuwa taaluma hiyo wanaojifunza sio kipaji chao.
Ni kweli ni muhimu, kila mwanafunzi akajifunza karibu kila
kitu, (kila somo), maana maisha yetu ni kila kitu, huwezi ukasema nisisome
kabisa somo fulani, mfano hesabu kwasababu sio kipaji changu, lakini maisha yetu
yanakuhitaji kujua hesabu, ili uweze kwenda na maisha ya kawaida, kuna mambo
yatakuhitajia kujua hesabu,kiinhereza, sayansi jiografia nk …., ndio maana kila
mmoja anatakiwa angalau ajue kila somo kwa manufaa yake ya baadaye. Lakini kwa
muda gani?
Tatizo hapa, ni jinsi gani ya kutambua vipaji vya watoto wetu
toka utotoni, na je vipaji hivyo vitawekwa kwa madaraja gani, kwani
tukizungumzia vipaji, tunazungumzia kwa lugha pana, yaani kwa ujumla wa maisha
yetu….kuna vipaji vya michezo, vipaji vya kitaaluma na vipaji vya kiutendaji,
vyote hivi vinatofautiana kati ya mtu na mtu…
Shule za awali zingelikuwa sehemu muhimu ya kutafuta vipaji
hivi,…na kumbukumbu za mtoto huyu zianze kuhifadhiwa hapa, ili akifika shule ya
msingi, walimu wanakuwa wakimfahamu mtoto huyu mapema, na itakuwa kwake rahisi
kumfuatilia kwa karibu, kwa vile atakuwa keshajulishwa umakini wake toka huko
awali na yeye ajue vipi atamkazania huyu mtoto zaidi , ili aweza kuendana na
mitaala.
Hebu tuulizane vyema, kuna kumbukumbu gani mtoto wa
chekechea anakwenda nazo na kukabidhiwa mwalimi wa shule ya msingi, kuwa huyu
alikuwa vipi kwenye masomo yake ya awali. Hili halipo,….na halikadhalika kuna
kumbukumbu gani za mtoto wa shule ya msingi anakwenda nazo sekondari , ili
mwalimu wake ajue ni vipi mtoto huyu alikuwa….sina uhakika kuwa haya yapo. Sisi
tunachofanya ni ule usemi wa kiingereza…`try and error’….au kubahatisha.
Zama hizi ni za kitekinolojia zaidi, kumbukumbu za watoto
zinaweza kuhifadhiwa kwenye mitandao, siku hizi mitandao ipo wazi, ni swala la
kutilia maananitu. Tukaondoa ubinafsi na kuwekeza kwenye elimu, tukatumia
rasilimali za madini, kwa ajili ya elimu ya watoto badala ya kununua magari ya
kifahari. Hili linawezekana,….
Kama tutaamua kuwa elimi ni muhimu kwa watoto wetu na vizazi
vyetu, sio tu kwa familai zetu, bali kwa taiaf zima, na tukawa na mipangilia thabiti
ya kuhifadhi haya, kwa ajili ya baadaye tunaweza kabisa. Na hili pia
litatusaidia kupata viongozi waadilifu, maana kumbukumbu hazijifichi, ilimradi
ziwe zinahifadhiwa kwa umakini na kwa usiri unaostahili kama kumbukumbu binafsi
zinavyohifadhiwa, hadi hapo zitakapohitajika.
Hili nalo tutahitaji wafadhili. Au kwa vile , huenda, hata ukiweka
amira halitaweza kuhumuka tukapaat cha juu,…haya tusubiri hadi wenzetu
watakapolala, huenda na sisi tutaamuka, na sijui labda ndio itakwua miwsho wa
dunia. Twajidanganya tukizania mtoto ni mtoto wangu wa mwingine atajua mzazi
wake.
Tunashinda kujua kuwa matatizo yanayoikumba dunia sasa hivi
ni kwasababu ya kukwepa majukumu, kuwa kila mzazi ni mzazi wa kila mtoto,
ubinafsi umetutawala, na kujiangalia sisi,…na
wenyewe ndio sisi….au sio. Moto ukiwaka , wa majanga, matatizo, tujue chanzo
ni sisi wenyewe…
WAZO LA LEO:
Usikate tamaa katika maisha, kila mtu anacho kipaji chake ambacho akikitumia
vyema kinaweza kuwa mtaji wa maisha yake. Tusibweteke kwa kuiga yale yawenzetu
kwa vile wao wamefanikiwa zaidi, tukazania huenda na sisi tukifanya hivyo tutafanikiwa
kama wao. Inawezekana mkawa sawa na yeye kwenye vipaji,….hilo hatukati, ni sawa
kabisa, kama ni hivyo basi,jitahidi uwe kama yeye, au zaidi. Tatizo hap ni je
umeshajichunguza na kugundua kipaji chako kipo kwenye Nyanja ipi, anza leo
kukitafuta kipaji chako, ukikigundua, utafanikiwa kwa kiasi kikubwa, usikate
tamaa.
Hebu msikilize LUCK DUBE HAPA
Ni mimi:
emu-three
4 comments :
Howdy just wanted to give you a quick heads up and let you know a few of the
images aren't loading properly. I'm not sure why but I
think its a linking issue. I've tried it in two different browsers and both show the same outcome.
Here is my web-site: friendmend.Com
Kila mtu sna kipaji chake kweli.
Nimependa simulizi hii. Hata ujirani mwema ni kipaji. Ahsante jirani mwema.
I used to be recommended this website by my cousin.
I am no longer certain whether or not this put up is written through him as nobody else recognize
such specific approximately my difficulty. You are incredible!
Thanks!
Feel free to visit my page - mammoth sea creature
naturally like your web-site however you need to check the spelling on quite a few of your
posts. A number of them are rife with spelling issues and I in finding it very bothersome
to tell the reality then again I will surely come back again.
My website; Www.Goolloo.com
Post a Comment