Maua alibakia kumkodolea macho yule mzee, hakuamini masikio
yake, hakuamini kuwa mzee kama yule, ambaye kwake ni sawa na babu yake,
angeliweza kumtamkia maneno kama yale, ….hata hivyo hakuonyesha kukerwa, au
kutaharuki, alitulia, akasubiri, hadi yule mzee alipomaliza kuongea, …
Maua na mama yake mdogo walipofika, waliambiwa mzee
anawasubiri, na walipoingia walimkuta kakaa kwenye ukingo wa bwawa la
kuogelea,….kwani mle ndani kulikuwa na kila kitu, bwawa, na pembeni yake
kumepandwa miti, kuna ndege wanaruka ruka, utafikiri upo ukingoni mwa mto….
‘Karibuni,…naomba niongee na binti yako, ….kama hutajali,
wewe karibu kwenye chumba cha maongezi, au zunguka zunguka huko nje, nikimaliza
maongezi nitakuhijia na wewe….nakuomba sana tafadhali…’akasema huyo mzee,
akiinama kidogo kwa mama mdogo.
‘Hamna shida….ila nahitaji kifuta jasho, …siunajua kazi ya
kulea sio mchezo, na ….mimi kama mzazi huwezi kusema niachane na mtoto wangu
uongee naye hivi hivi tu…’akasema mama mdogo, na Maua akamwangalia kwa jicho
baya.
‘Haya..haya, naondoka, maana huyu naye,….’akasema huyo mama
akimwangalia binti yake kwa jicho baya.
‘Usijali….najua nini unakihitajia,…nakuhakikishia
utapata…’akasema huyo mzee na akawa kama anamsindikiza hadi mlangoni, akafungua
mlango, na alipotoka akaufunga ule mlango, na kwa mwendo wa haraka, akatembea
hadi aliposimama Maua, na kwa jinsi livyotembea utafikiria sio mzee…,
‘Samhani sana, huwa napenda nikiongea na wewe tuwe tumekaa
kwenye sofa, kwenye kiti change cha enzi….’akasema huku akiwa kaweka mkono
mmoja kwenye nyonga ya Maua. Maua, aliona ni utani wa babu na mjukuu wake,
akawa anatembea tete-a-tete na huyo
mzee hadi kwenye hiyo safa.
Akaanza kuongea, …..na huyo mzee akiongea, anaongea kweli,
…..
Maua akawa kama kapigwa na ganzi ya mshituko….hakusema kitu,
akatulia, na akawa anasikiliza, na wakati mwingine, …..na mwishowe yule mzee
akasema;
‘Najua utaona ajabu sana kwa hayo maneno yangu, sitanii,
ninazungumza kutoka moyoni….’ Akasema huku akishika kifuani, na Maua akawa kama
anatabasamu kwa zarau.
‘Huenda usijisikie kabisa kuwa karibu na mimi,….kwa vile
mimi ni mzee, utatembeaje ni mimi mitaani, lakini,mmh, sijui nikuambije, Maua,
kiukweli…wewe umekuwa ndio dawa yangu, …wewe umeniokoa maisha yangu,
isingelikuwa wewe muda kama huu, huenda nimeshajifia….’akasema na kujifunika
usoni kwa viganja vyote viwili.
‘Ninachokuomba, ujaribu…kuwa karibu na mimi, hata kama
itashindikana, ….lakini kwanini ishindikane, kwasababu ya uzee, ina maana uzee
ndio unifanye nisiwe na amani, nisiwe na raha,…hapana…nimevumilia sana…na
nakuhakikishia kuwa nitakupa raha zote za dunia, ilimradi tu, uwe mke mwema….’akatulia
huku akiwa kainama chini kama anawaza jambo, halafu akainua kichwa na kumwangalia
Maua.
‘Maua, wewe ndiwe kitulizo cha moyo wangu, na wewe ndiwe
dawa yangu, ukiwa nami sihitaji tena madawa yao ya hospitalini….hutaamini hilo,
hata docta hakuamini…na ameondoka akiwa na hamu sana ya kuona dawa
iliyonikoa,….dawa yangu ni wewe….’akashika kifuani na kuendelea kusema;
‘Maua wewe,….sema unachotaka nitakutimizia…ilimradi,…uwe na
mimi, na tutaingia makubaliano ambayo hayatakukwaza wewe….sitakuweka katika
hali ambayo hutakuwa na raha….nitahakikisha hivyo….nakupenda sana,…na
nitakujali sana…ilimradi tu, uwe
mke-mwema’akasema na kumwangalia Maua, hayo maneno ya mwisho aliyasema kwa
sauti ndogo.
Maua alijisikia vibaya, akahisi moyo ukimuenda mbio,
akatamani kutapika, lakini, akajizuia, …Mwanzoni alizania kuwa huenda huyo
mzee, ambaye alimuona kama babu yake, anatani, alijua ni ule utani wa babu na
mjukuu wake, lakini……mmmh
‘Mjomba,…mimi sikuelewi…maana mjomba wako, ambaye
ninamfahamu....kwangu namuona ni mkubwa,..sasa wewe je itakuwaje, ….ni kama
kuruka mkojo na kuja kukanyaga mavi….hapana kwa umri wako, nakuona kama babu
yangu, naona utani wako umezidi,…kwani mke wako yupo wapi?’ akauliza .
‘Maua mimi sitanii, hivi bado unaniona kama mtanii wako, ….ninalokuambia
linatoka moyoni mwangu,…..nina dhamira ya kweli ya kukuoa…., nakuhitaji wewe
uwe mke wangu, uwe karibu nami, hadi hapo tutakapotenganishwa na kifo,…najua
umri wangu ni mkubwa sana ….lakini nayajua mapenzi kuliko hawo vijana wenzako,
ambao watakudanganya na kukupotezea muda wako..’akasema na hapo Maua akainuka
pale pembeni yake, na kusimama.
‘Naomba nikuulize Maua, ina maana ulipokuja hapa hukuwa
umeshaongea na mtu….huyo aliyekuongoza hadi kuja hapa kwangu, huyo ni rafiki
yangu,….japokuwa kumbe ni msaliti wangu….lakini nakuhakikishia kuwa hiyo ni
dhamira yangu’ akauliza.
‘Dhamira gani…na ni nani huyo niliyeongea naye kuhusiana na
hili ambaye hana akili ya kufikiria, mimi msichana mdogo, nije kuolewa na mzee,
….ambaye ni sawa na babu yangu, ..hivi kweli, wazazi wangu, ndugu na jamii kwa
ujumla itanielewaje….wote watajua kuwa nimefuata pesa zako, hapana, kama ni umasikini
acheni tukae na umasikini wetu…’akasema Maua.
‘Usijali ya watu,..haya tunayoongea ni mimi na wewe…..,angali
jumba hili, kubwa la kifahari, lakini halina raha, wanaoishi humu ni sawa na
wafungwa,….mke wangu aliondoka, hatukuwa tunaelewana, ….tulipooana, nilijua
nimepata mke, kwani ni mrembo…..’akasema akingalia picha iliyokuwa ukutani.
Maua akaiangalia ile picha,..kweli alionekana mwanamke
mrembo, akiwa kakaa kwenye kiti, karibu na ua waridi…akawa anajiuliza kwanini
mke mrembo kama yule ashindwe kuishi na huyu tajiri, ni lazima kuna tatizo.
‘Uzuri wa sura…ulikuwa kazi bure,….. kumbe, mwenzangu
alikuja kwa lengo la kutumia, bila kujali,…..yeye akili yake ni kuwa pesa,
zipo, unachota kama unachota maji…., kila siku anataka pesa, na hata umpe
shilingi ngapi hatosheki,….nilishindwa’akasema.
‘Kwahiyo kumbe wewe ni bakhili….ndio maana mke wako
akakukimbia?’ akauliza Maua.
‘Huo sio ubahili,..hata uwe tajiri vipi, kuna mpangilio wa
matumzi, huwezi ukatumia tu, hata matumzi yasiyo na muhimu, kila siku sherehe,
…..kusafiri, gharama inakuwa kubwa kuliko hata kile kinachoingia,
hutaweza…..mimi nimejaliwa kuwa tajiri, lakini sikuupata kirahisi,…na kama
natakiwa kuendelea kuwa hivyo, tunahitajika kuzalisha na kuangalia gharama ,
matumizi na nini kinachoingia…’akasema na kusimama.
Maua alimwangalai yule mzee, pamoja na uzee wake, bado
alionekana mkakamavu, ….akawa anajiuliza maswali mengi, jinsi gani anaweza
kuishi na huyo mzee, eti kama mume wake….akajikuta akitabasamu, akageuka
pembeni…
‘Maua najua unavyojisikia, kuwa utaishije na mzee kama
mimi….ninakuahidi kuwa hutaweza kuiona hiyo tofauti,…vijana wa umri kama wako,
ni vijana jina, lakini hawana nguvu yoyote..miili yao umeshaharibika na
mavyakula wanayokula, madawa, sigara…hawana lolote zaidi ya sura ya ujana,
…ninakuambia ukweli, mimi nikisimama na wao, ….hawaniwezi, mimi nina
nguvu,…zote, kuliko hawo vijana, tatizo ni mashinikioz haya ya kimaisha..
‘Sasa hapo huoni, ni kuwa wewe sasa hivi unahitajika
kutulia, …huna haja ya kuwazia mke, …muda huo umekwisha, …’akasema Maua.
‘Kama ingelikuwa rahisi hivyo,…ningelifanya hivyo….lakini
hutaamini, …..vishawishi, mitihani, ninayokumbana nayo, ni mingi kuliko
maelezo, hasa waliposkia kuwa tumeachana na mke wangu, kila siku kuna hodi,
nikipita mitaani,..ooh, taabu kweli kweli, …kwa hali kama hiyo, …sioni kwanini
nisitafute mke…..’akatulia.
‘Na jingine kubwa zaidi ni hii hali ya kuishi hapa peke
yangu, ina maana ninaweza nikafa, bila kukosa mtu wa kunisaidia, angali
ilivyotokea, wewe ndiye uliyeweza kunisaodoa katika hali ngumu niliyokuwa
nayo,..kuna siri kubwa ya mwanamke…….ndio nyie mkibadilika mnaweza kuwa wabaya
kuliko hata nyoka mwenye sumu, lakini nyie hawo hawo ni wema kuliko ….chochote.
Hilo nimethibitisha, kwa uzoefu wangu…’akatulia na kumsogelea Maua.
Maua kwanza alitaka kurudi nyuma, au kumsukuma, lakini mwili
haukuweza kufanya hivyo, akatulia, na kusubiri aone huyo mzee anataak kufanya
nini…na mara mlango ukagongwa…
**********
Maua alishikwa na
mshangao mkubwa, akajikuta akatahayari na akajiskia aibu, maana wakati ule
mlango unafunguliwa, ndio wakai huo, huyo mzee alikuwa keshamkaribia, na mikono
yake ilikuwa hewani ikitaka kumshika sehemu za nyongani, …
‘Aaah, nani huyu tena….’akasema huyo mzee akaigeuza kichwa
kuangalia mlangoni, lakini mikono yake ilikuwa bado hewani, karibu kabisa na
kumshika Maua kwenye sehemu za nyongani.
‘Oh, …ni Mama….mama ..ooh, mama..’Maua akajikuta akisema…kwanza
akiwa katulia, na baadaye akashindwa kuvumilia, kwa haraka akamkimbilia mama yake na
kumkumbatia. Mama yake alikuwa kashikwa na butwaa, alikuwa kama yupo kwenye
njozi, hakuamini kile alichokiona, …
‘Ina maana ,….ni kweli, binti yangu anataka kuolewa na mzee….na
kumbe mzee mwenyewe ni huyu, mbona makubwa…sikubali..’akawa anajisemea moyoni.
‘Ina maana huyu ndiye mzee nilyesikia kuwa ndiye anayetaka
kukuoa?’ akauliza kwa sauti ndogo
‘Hapana mama sio huyu, …..’Maua naye akasema kwa sauti
ndogo.
‘Lakini…..mbona nimekuona kama….’akatulia kumazia.
‘Huyu ni mzee wake,….na hawa babu, na wajomba wamezidisha
utani,….ni utani tu mama, na wala sivyo hivyo unavyofikiria wewe….’akasema Maua
na kumfanya mama yake, atulie kidogo, lakini kwa jinsi alivyoona, ule ulikuwa
sio mzaha, ….mzaha unajulikana.
‘Sivyo ninavyofikiria, nimekuambia nafikiria nini…wakati
nimeona kwa macho yangu mwenyewe…’akasema mama yake.
‘Mama dunia hii imebadilika, watu tunakwenda na wakati,
kukumbatiana, ni jambo la kawaida, hata mkwe anaweza kumkumbatia mkewe…haina
shida…’akasema Maua.
‘Haya mwanangu, lakini angalia sana ….usije ukaangukia
kwenye masahibu yaliyonikuta, maana mimi nilijua muda kama huu upo Dar,unafanya
kazi , sasa nimefika hapa nasikia upo huku Arusha, …unasubiri kuolewa, na mtu
anayeitwa Tajiri, hivi ni nani huyo,…..’akatulia alipokumbuka kuwa wapo ndani
ya chumba cha mtu, lakini wakati wote huo walikuwa wakiongea kama wananong’ona.
‘Mama hayo tutaongea baadaye, lakini nakuhakikishia kuwa
..nilijitahidi kufuta yale yote uliyonifundisha, lakini ilishindikana….mama
mdogo, …mama nakuambia ukweli mama mdogo sio mama….hana uchungu kabisa na watoto
wa wenzake…’akasema Maua huku machozi yakianza kumtoka.
‘Nilijua tu….na najuta , ….na kwa hilo nitajilaumu sana
mwenyewe kwa kukuruhusu kuondoka na huyo mwanamke…ni ndugu yangu, lakini…..ooh,
sasa sijui tufanyeje mwanagu..’akajikuta naye akitamani kulia, lakini moyo wake
ulishakuwa sugu , na machozi yalioka moyoni, sio machoni.
‘Mama maji yameshamwagika, ….hatuna budu kuyaoga,
imeshatokea, ..wewe huna la kufanya, hayo sasa niachie mwenyewe, na wala
usijiingiize kabisa kwenye haya yaliyonikuta, huu ni mpira wangu, niachie
niucheze mwenyewe, …nakuomba mama usiumize moyo wako, mimi nimeshakuwa mkubwa,
najua nini cha kufanya ….nitapambana na haya yaliyonikuta, hadi nihakikishe
haki yangu imepatikana’akasema Maua.
Mama yake akamwangalia binti yake, huku moyo ukisononeka, na
kila alipokuwa akimchunguza mwanae, alihisi kuna mabadiliko,mwanzoni alifikiria
na mambo ya mjini, kujiremba na kujikwatua, lakini…
Aakukunja uso na kumwangalia Maua machoni, wasiwasi ukamzidi,
akamsogelea binti yake na akainua mkono kutaka kumshika tumbo, Maua akasogea
nyuma, na mara wakasikia yule mzee akikohoa,..wakashituka, wakakumbuka kuwa
wapo ndani ya chumba cha watu, wakageuza kichwa kumwangalia yule mzee.
‘Samahanini…..sikutaka kuwaingilia, lakini…nilikuwa na
mazungumzo nyeti na huyu binti,….oh, kumbe ni binti yako, ..kwani wewe ni nani
mama yangu…?’ akauliza akiigiza lafudhi ya wazungu. Na mama Maua akawa anasita
kuongea, na yule mzee akasema.
‘Mimi kwa ujumla nimefurahia sana kukuona, kumbe wewe ndiye
mama yake mzazi…kwa kweli mnafanana…mimi walipokuja na yule mama yake mwingine,
nijua kabisa kuwa ndiye mama yake mzazi, japokuwa tabia haziendani….’akasema
huyo mzee akimwangalia yule mama, na akawa anajaribu kukumbuka ni wapi waliwahi
kumuona huyu mama.
‘Shikamoo baba….’akasema yule mama, na yule mzee hakusema
kitu, akawa anatikisa kichwa kama kukubali jambo, na baadaye akatembea hadi
mbele kidogo, ambapo kuna meza kubwa ya kiyoo na akabonyeza kitufe, ikawa
inazunguka, …juu ya ile meza kulikuwa gilasi, matunda ya kila aina yalipangwa
kama ua, katikati ya hiyo meza.
‘Jamani karibuni hapa….hiki chumba changu, kina kila kitu, lakini
sio chumba cha wageni, ni chumba changu maalumu cha kujinafasi, nikiwa humu,
najisikia nipo Ulaya,au sijui wapi, nisije nikakufuru …mara nyingi sipendi
kuwakaribisha wageni humu ndani, ila kwa wageni maalumu,..hasa kama
nyie….’akasema akisogeza viti viwili nyuma ili wageni wake wakae.
‘Tunashukuru sana…..mzee usihangaike maana mimi sio mkaaji…’akasema
mama Maua, kwanza alisita kukaa, kwani alikuwa na haraka ya kuondoka, lakini
moyo ukawa na dukuduku, la kutaka kumjua zaidi huyo mzee, akakaa kwenye kiti.
‘Kwasasa nahisi kila kitu kinakwenda kama nilivyotaka iwe,
maana ningelifunga safari ya kuja huko kwako, kwani wewe mama….unaishi wapi
hapa Arusha,?’ akauliza.
‘Mimi sio mkazi wa hapa Arusha, kwetu ni huko Singida,…nimekuja mara moja tu kikazi,
…..ninafanya vibishara vyangu na mume wangu, …nilipofika hapa nilikutana na
rafiki yangu mmoja, akaniambia kuwa kamuona binti yangu, …huyu hapa, …..’akasema
huyo mama huku akimuonyeshea Maua kwa mkono wake
‘Singida..singida…huko ndipo wazazi wangu, walipotokea, mimi
nilihama kabisa huko, ni muda mrefu kidogo, ..nikiwa mdogo, …kwangu ni hapa,
mimi siwezi kusema Singida ni kwangu, huko ni kwa wazazi wangu,…maana huko
nilipaasi nikiwa mdogo, na sipendi kabisa kurudi tena huko’akasema.
‘Jamani kuna mtu anayekataa kwao, kweli wewe ni mtu wa ajabu
sana….hata uhame, na kuishi wapi, kwenu ni kwenu tu…’akasema mama Maua.
‘Kuna sababu nyingi zilitokea,….lakini kwa sasa ni
historia,….na maisha ni popote,…..sio kwamba kwa vile umezaliwa sehemu hiyo,
basi ndio ung’ang’anie kuishi hapo,eti kwa vile ni kwenu , hapana …dunia hii
tumepewa na mungu, tumeambia tutawanyike, tutafute riziki, na riziki ni
popote…mimi kwangi ni hapa na hata watoto wangu siwezi kuwang’ang’aniza kuwa
wakae hapa, popote wanaweza kuishi…’akasema.
‘Wao kama walivyotaka, wanapenda kuishi Ulaya, na wanasema
kwao ni Ulaya….haya waende waishi huko,…siwakatazi, kwani duniani kote ni kwa
kila mtu…rangi, utaifa sio hoja,…..hoja ni je unamiliki kitu, una nyumba,
una…vile vitu ndio vyako, lakini dunia, wapi unahitaji kuishi, mimi sioni
kwanini watu wawekewe mipaka,…hilo naona kama tunaingilia mamlaka ya Mungu….anyway, hayo hayanihusu kwa sasa…’akasema.
‘Ina maana una watoto wakubwa eehe, na nahisi hata wajukuu na
vituku, au sio?’ akauliza mama Maua.
‘Kwa umri kama huo hilo swali sio la kuuliza, ninao…..lakini
sijabahatika kuwa na wajukuu….watoto wangu wanaishi kiUlaya….hawana haraka ya
kuoa, au kuolewa….’akatulia na akawa kama anawaza jambo, halafu akasema;
‘Maisha yangu, ….sikupata mud asana wa kukaa na watoto
wangu, walipozaliwa tu, …mama yao akapendekeza tuwapeleke, Ulaya, ..nilikuwa na
jamaa yngu mzungu, ulikuwa tukifanya naye biashara, akawachukua….
‘Kwahiyo watu wengi wanajua kuwa mimi sina watoto, nahata
wengine walifikia kuniona sizai, sio kweli, watoto ninao, na bahati nzuri, wamekulia
huko na wamesomea huko Ulaya, na wanataka makazi yao yawe huko huko….’akakunja
uso kuonyesha huzuni, na alikuwa kama anajizuia kuongea jambo fulani, na
baaadaye akasema;
‘Na bahati mbaya,….mmh,…. mama yako hatukuelewana….tangia
awali…yaani tulikuwa tunaishi u, kwa vile tulifunga ndoa, lakini hakuna raha,
hakuna maelewano, mpo ndani kama chui na paka….ni ndoa ambayo ilinitesa sana…..’akatulia
kidogo na mama Maua akaona aongee kidogo kama kumliwaza, akasema;
‘Yote ni maisha, …..kila mtu kapitia kwenye maisha yake, na
ana matatizo yake,…..lakini umshukuru sana mungu,….kama umeshajaliwa kuwa na
watoto wakubwa na wanajitegemea,….unataka nini tena. Kwa umri kama huo wako,
unachohitajia kwa sasa ni wajukuu, kwa umri kama huo tena, ni wa kujipumzisha tu
, na kula mali yako, na huhitajii watoto tena,..labda kama unahitajia wajukuu
wa kucheza nao,…’akasema mama Maua.
‘Na hilo ndilo nataka kuongea na wewe…sio kweli kwamba umri
kama huu sistaili kuishi na
mke,…nahitajiak sana,…maana mke ni nini…ni
….u-ba-vu- wa-ko….’akasema na kuyatamka hayo maneno kama anatajisha herufi.
‘Mke ni mwenzako wa shida na raha, hadi mmoja atakapoondoka
duniani…..kuna siri kubwa sana hapo..mfano naumwa, ni nani atanisaidia, kama
sio mke, ….sitakiwi tena eti mwanangu..eti ndugu, eti jirani…ndiye aje
kuniogesha pale ninapozidiwa…..’akatulia
‘Ni kweli hayo unayoyasema, wewe ulistahili uwe na mwenzako,
na hasa mwenye umri sawa , au karibu kidogo na wa kwako, wanaojua kulea, na
wenye uzoefu…..lakini kwa mfano kuna wazee siku hizi wanakimbilia mabinti
wadogo, wadogo kabisa….huoni hawo ni sawa na watoto wao?’ akauliza mama Maua .
‘Ni kweli wazee wanakimbilia mabinti wadogo, sikatai….hii ni
kuonyesha kuwa kila mtu anapenda kizuri,….sizani kuna mtu anapenda apate mzee
kama mimi,…mmh, sisemi ubaya,…ila ikibidi, sio mbaya, maana inaliwaza, na ni
dawa…..’akasema na kutabasamu.
‘Kiujumla kila mtu anapenda jinsi nafsi inavyomvuta…lakini
nikuambie, kuna tofauti ya mke na mtoto…mke ni pale mnapofunga ndoa, haijalishi
umri, ilimradi kama mumefunga ndoa basi….huyo ni mkeo, sio mtoto wako tena,…huwezi
ukasema kwa vile ni mdogo, hastahili….hapana pale mumeshaidhinishiwa kisheria…na
wapo wanaweza, wanajua kulea, hata zaidi ya hawo wakubwa, wakubwa wengine ni
shida….’akatulia.
‘Hapana, mimi na umri wangu huu, siwezi kuolewe na
kijana,..sawa na mtoto wangu,…mimi kwangu ni aibu,siwezi kumkalia uchi,…mtoto
kama huyo…siwezi….lakini nyie wanaume hamna haya…..hamjali…na hapo ndipo dunia
inapoharibika….mnatupeleka pabaya’akalalamika mama Maua.
‘Usiseme hivyo mama, kwani hata mimi ninaweza
kuwalaumu…maana kwa mfano mimi sasa hivi nilitakiwa niwe na mke wangu,…ambaye
ni umri sawa, au karibu na mimi,…haya yupo wapi, …kaamua kuondoka, kisa hataki
kuchungwa, kisa..hataki kupangiwa, anachotaka ni kutumia,….anadai aliolewa kuja
kutumia, sio kutumikishwa…yaani, mengine mnaulaumu waume bure tu, lakini hata
nyie ni wakaorofi….sasa kwa hali kama hiyo nifanyeje?’ akauliza.
‘Yaani hilo tu, ndio mkaachana?’ akauliza Maua.
‘Hilo tu….sio dogo, hilo naliongelea kwa uchache wake,
lakini kuna mengi yaliyopita humo, mabaya siwezi hata kuyaelezea, hiyo ni siri
yangu, na mungu wangu,….ilikuwa ni vigumu sana, hadi kufikia uamuzi kama ule,
hasa nikizingatia kuwa nimezaa naye watoto, …..ilinipa shida sana hadi
kukubalina na uamuzi huo, na sio mimi niliyetaka iwe hivyo….yeye mwenyewe
alimua….kashinikiza kwa kashfa juu,….nikasema hewala, kwaheri….’akatulia.
‘Kwahiyo sasa unataka kuoa mke mwingine?’ akauliza mama
Maua.
‘Sasa nyie mnataka nife peke yangu …..na hili jumba, na mali
yangu, ni nani atakula, ina maana mimi nikae humu peke yangu , huku wenzangu
wanakula jasho langu….hapana nahitaji mwenzangu , ambaye ataweza kuniliwaza,
ataweza kuishi na mimi na kunifanya nisahau machungu,…ambaye atakuwa dawa…..na nimehisi,
….’akatulia na kumwangalia Maua, halafu akageuka kumwangalia mama yake.
‘Mama nakuomba sana mama, na unielewe na kunisaidia, najua
huenda ikawa ni vigumu kwako….samahani sana nitapenda kukuita hivyo, mama….nakuita
mama, japokuwa mimi ni mkubwa kwako, nakuita hivyo kiheshima, kwasababu nataka
uwe mkwe wangu…’akasema huyo mzee.
Mama Maua akainuka kwenye kiti na kusimama, akageuka huku
kapanua mdogo, kama vile anataka kupiga yowe, akamwangalia binti yake, na zile
kumbukumbu za wakati anaingia pale mlangoni zikamrejea, akamuona binti yake
wakiwa….au wapo, ….wakitaka kukumbatiana…
‘Haiwezekani….
‘Mama….tulia kwanza , ….’akasema Maua.
‘Nimesema haiwezekani, inuka twende zetu, kama mimi ni mama
yako, niliyekuzaa, nikateseka kwa ajili yako, na mwenye uchungu na ….basi inuka
twende zetu..’akasema mama akimshika mwanae mkono.
‘Mama tulia kwanza…..’akasema Maua, na kumfanya mama yake
ashikwe na mshangao, akamwangalia binti yake huku macho yamemtoka kwa mshangao.
‘Ina maana ni kweli,…una mahusiano na huyu mzee…ina maana
umeshakubaliana kuolewa na huyu mzee….?’ Akawa anauliza huku macho yamemtokwa
kwa hasira.
‘Kwa kipi unachokitaka, utajiri….ufahari,..mwanangu hayo
peke yake hayatakusaidia kamwe, utaishi maisha kama mfungwa, utajuta,…..na hata
huyu mzee akifa, usitegemee kuwa utarithi hii mali,…’akasema akionyeshea kwa
kidole kuzunguka mle ndani…
‘Ukumbuke kuwa, wapo watoto wake,…mwenyewe kasema kuwa ana
watoto wake wakubwa,….ana mke, japokuwa anasema wameachana, lakini huyo mke akisikia
tu huyu aliyekuwa mume wake kafariki, atakuja hapa kama sio yeye kudai,…ana
haki zake, ujue kuwa mzee kama huyu, ninavyomuona, ni lazima atakuwa na watoto
wa pembeni…..mwanangu inuka tuondoke….’akasema mama yake.
‘Mama…nisikilize kwanza….mimi nina maana yangu ya kuwepo
hapa…kuna tatizo kubwa, nahitaji kulimaliza na huyu mzee,….nina ujazito wa…wa..’akasema
Maua akishindwa kumalizia, kwani mama yake alimkatiza.
‘Ujauzito?’ akauliza mama yake huku akipepesuka kutaka
kuanguka kwa mshituko, akashika ukuta, akafumba macho, kama anahisi maumivu
makali…..
`Unasema una jauzito, wa nani?’ akauliza huyo mzee akiwa
kashika mdomo, hakuonyesha kushituka kama ilivyotokea kwa mama Maua…..
NB.Ningeliendelea lakini muda, tatizo la umeme, ooh…lakini hata hivyo nashukuru mtandao umekubali!
WAZO LA LEO: Kila
mtu anapenda kizuri, kila mtu anapenda raha, kila mtu anapenda starehe, lakini
yote hayo ni gharama, na gharama inahitajia kufanyiwa kazi, haiji kwa kuota,
kwa kuwaza,….tufanye kazi kwanza, ili vyote hivyo uvipate kwa wasaa.
Ni mimi:
emu-three
13 comments :
Kazi nzuri sana wala usikate tamaa..Wazo la leo ni bonge la wazo nimelikubali sana tena mno. Ijumaa njema
It's an remarkable article designed for all the web viewers; they will take advantage from it I am sure.
my web site: one month loan
My website - one month loan
It's amazing to go to see this website and reading the views of all friends on the topic of this paragraph, while I am also keen of getting knowledge.
Also visit my web page; visit the next web site
If you want to increase your know-how only keep visiting this website and be updated with the most up-to-date gossip posted here.
Also visit my homepage: casinobonusfree.org
My family all the time say that I am wasting
my time here at net, except I know I am getting familiarity all the time by reading thes nice
content.
My blog post just click the following document
my web site :: onlinecasinogamescasino.com
Υоur current artiсle pгоvides
proven hеlpful to mе. Ιt’s really informаtive and
you're obviously very educated in this field. You have got opened my own face to varying opinion of this kind of topic along with interesting and sound written content.
Also visit my page :: soma
Your oωn post has сonfirmed helpful tο mе.
It’ѕ quite еducatiоnal and you're simply obviously very knowledgeable in this region. You possess opened up my own eye for you to numerous views on this specific topic along with intriguing and sound written content.
My webpage http://www.hermeticuniversityonline.com
Thanks a bunch for sharing this with all of us you actually recognise what
you're speaking about! Bookmarked. Kindly also seek advice from my
web site =). We may have a hyperlink exchange
contract between us
my homepage frisbee plastic flying
With havin so much content and articles do you ever run into
any issues of plagorism or copyright infringement? My site has a lot of unique content I've either authored myself or outsourced but it appears a lot of it
is popping it up all over the web without my agreement. Do you know any ways to help stop content from being
ripped off? I'd truly appreciate it.
Feel free to visit my web-site; quest protein bars
Admiring the hard work you put into your website and in depth information you
provide. It's nice to come across a blog every once in a while
that isn't the same outdated rehashed material. Wonderful read!
I've saved your site and I'm including your RSS feeds to my Google
account.
my blog post ... online surveys for money
My brother recommended I might like this website.
He was entirely right. This post actually made my day.
You can not imagine simply how much time I had spent for this
info! Thanks!
My website ... minecraft.net
You ought to be a part of a contest for one of the highest quality
sites on the internet. I am going to recommend this web site!
My website; minecraft games
I pay a visit everyday a few blogs and websites to read content, except this blog gives quality based content.
Here is my web-site - free music downloads, http://twitter.com/Music0Downloads/status/596035206915559424,
Post a Comment