Malikia akiwa njiani na watu wake alikumbuka tukio la yule
kiongozi wa askari akikauka mbele yake, na mwanzoni alijua labda kwa vile huy
askari alitaka kumzuru, na kukatkea nguvu nyingine zilizomuadhibu huyo askari
kiongozi, lakini kutkana na maelezo ya huyo tabibu wao, ilionekana kabisa kuwa
kilichotokea hapo ni mamb yao wenyewe.
Wakiwa kwenye mwendo wa polepole walikaribia kambi nyingine,
kambi hii aliwakuta akina mama, na wale akina mama walipomuona tu, wakakimbia
mbele yake na kupiga magoti, huku wameinua mikono juu, wakisema kwa sauti;
‘Mtukufu mama malikia tuokoe,…tukoe, tuokoe mama yetu,…’
Mama malikia akashangaa, na haraka akashuka kwenye yule
punda, na kuwasogelea, akawabariki kwa mkono wake, kama ilivyo ada,. ..huku
akilini akiwaza haya matukio ya ajabu, maana kila hatua anayopita, anajikuta akikutana
na matukio yanayomshangaza, .. na hata yeye mwenyewe alikuwa haamini kuwa ana
uwezo wa namna hiyo.
Na wakati anaendelea kuwashika vichwani mmoja baada ya
mwingine, akisubiri muda wa kuwaulizia shida zao, akilini akawa anakumbuka
tukio lililpita, tukio ambalo, lilimtia hofu kidogo, hakutarajia kuwa kuna mtu
anaweza akamfia na huenda watu wakamnyoshea yeye kidole….
Kifo cha yule kiongozi askari, lilikuwa gumzo, na huenda
lilishafika mbali, na hata alipoona hawo akina mama wakipiga magoti mbele yake
huku wakiomba kuwa eti yeye awaokoe, na sijui waokolewe kutokana na janga gani,
na kwa akili ya haraka akahisi huenda ni kutokana na tukio la huyo askari
aliyekauka mbele yake.
Akiwa anawapitia wale akina mama, tuki lililopita lillikwa
likimpitia kichwani, kwani yeye kama mama, mama wa jamii, alitakiwa kuwaona wanajamii wote kama
watoto wake, ndio maana yule askari lipodondoka mbele yake na kuanza kutoa damu
alichofanya ni kumuinua kama vile mama anavyofanya kwa mtoto wake.
Malikia akakaa chini na kuinua kichwa cha yule askari na kukiweka
mapajani mwake, na wakati huo yule askari alikuwa katoa jicho la uwoga, akinyesha
kuwa aliona kitu cha kutisha, na wakati huo hakuweza kusema lolote zaidi ya
kuweweseka mdono, na baadaye akalegea kuonyesha kuwa mwili hauna uhai tena.
Malikia alipona vile,akaamrisha aletwe tibabu haraka, na
tibabu alipoletwa haikusaiida kitu, kwani baada ua kumchunguza huyo kiongozi wa
kikundi hicho cha maaskari, alisema huyo jamaa keshafariki, na inavyoonekana
huyo kiongozi kafa kwa kunyonywa damu.
‘Kunyonywa damu na nani, mbona hakuna aliyefanya tendo
hilo?’ akauliza malikia.
‘Mtukufu malkia haya ni mambo ya kimazingara, huenda huyu
mtu ana mapepo ambayo yametumwa kwake, kumuangamiza, au kuna yeye alikuwa na mapepo, ambayo kayakosea na
matokea yake ndio haya…’akasema huy tibabu.
‘Kwahiyo keshakufa…..?’ akauliza malikia.
‘Ndio keshakufa….na ni vyema ndugu zake wakafuatilia hili
tatizo maana sio kitu cha kawaida kama ndivy nionavyo, tatizo hili litatafuna
familia hii yote, hata hivyo, …huwezi jua, tatiz hili linaweza kuwaathiri hata
wasiohusika…’akasema huyo mtaalamu.
Malikia alitulia kwa muda, kama mama ilibidi awe na busara,
akawaambia viongozi wengine wa hichi kikundi, kama kuna uwezekano wa kupatikana
ndugu wa huy marehemu.
‘Ndugu yake ndio mkuu wa vikosi vyetu vya mzee hasimu,
kwasasa hivi hataweza kupatikana kwani wapo kwenye kikao kikubwa sana….ila
tumeshamtuma mtu kuelekea huk’akasema.
‘Sawa naomba mlifuatilie hili tatizo , mjue mimi ni mama
yenu, nahitajika kujua afya za watoto wangu. Kwahiyo naombeni ushirikiano wenu,
na tofauti zetu za kisiasa zistufanye tuwe maadui wa kila kitu. Mimi nipo
pamoja na nyie,….’akawaambia na baadaye ikabidi andoke.
**********
‘Kwanini mnaniambia niwaokoe, kuna tatiz gani?’ malikia
akawauliza wale wanawake, na huku wakiangali a huku na kule, kwa wasiwasi kuwa
huenda walinzi wakasikia. Na mmojawapo akasema kwa sauti ya kinyonge.
‘Mtukufu malkia, mzee hasimu akija hapa sisi ni kitowe cha
mamba, kwahiy tunaomba utumie busara zako kumshawishi asituadhibu maana hata
sisi hatuji nini kilitokea, walinzi waliokuwepo wameshakimbia,…’akasema huyo
mama.
‘Niambieni kumtokea nini?’ akauliza.
‘Ni kuhusu kupotea kwa mtoto…..katoweka kiajabu, na mama
mkuu wetu naye katoweka,..hatujui ni kitu gani kinachotuandama, sisi tunahisi
na kwa vile tumekwenda kinyume na siku ile iliyotabiriwa…’akasema huyo mama.
‘Mama gani ambaye katoweka?’ akauliza.
‘Mama mkunga, ambaye kama angelikuwepo, ndiye angetusaidia, …yeye
anaweza kuongea na mzee hsimu bila kuogopa,…..’akasema huyo mama.
‘Huyo mtoto ndiye huyo aliyeibiwa ….?’ Akauliza.
‘Sijui hatukuwa tunajua kuwa mtoto huyo aliibiwa, tulikuja
kujua baadaye, wakati tumeshafika huku….na tumekuwa tukiishi huku kwa mashaka ,
kwani tunajua wazi kuwa hili lililofanyika ni makosa, na sasa hivi tumeongea
hivi, tumeshatia kwenye hatari…’akasema huyo mama.
‘Mimi ni mama yenu, tupo pamoja, na ninachowaomba, kwasasa,
tungozane kwenye hii safari yangu, ili tuwe pamoja, ili turudi pamoja huko
nyumbani, lakini hili linategemea uamuzi wenu,…’akasema.
‘Mtukufu malikia …tupo tayari kuondoka na wewe maana
tukibakia hapa, keshi haitafika….’akasema yule muongeaji mkuu, huku akinaamisha
kichwa chini, na akatabasamu, na baadaye wakajiandaa wakaongozana na mtukufu
malikia na msafara ukawa mkubwa.
*********
‘Huyu mlevi mbona hataki kutupisha…?’ akauliza mlinzi wa
malikia.
‘Wewe mlevi ondoka njiani, malikia anataka kupita’akasema
yule mlinzi, akimsogelea yule mlevi, na yule mlevi alipomuona, akashtuka na
kusimama huku akionyesha wasiwasi, na baadaye akageuka na kuanza kukimbia,
lakini yule mlinzi mwingine akawahi kumshika.
‘Sasa unakimbia nini, huoni ulivyolewa kukimbia hivyo
unaweza ukatumbukia kwenye mashimo ukavunjika mguu. ..’akaambiwa, na yule mlevi
akawa katoa jicho la uwoga, na baadaye akasema.
‘Jamani sio mimi,….’akapiga magoti, na kuendelea kusema
maneno hayo kuwa sio yeye
‘Sio wewe ni nani….?’ Akauliza malikia akitaka kujua kwanini
huyo mlevi anasema hivyo kuwa sio yeye
‘Mimi nilimuona akitaka kumuua, …..mama, yule mama ,
mwanamke ninayekaa naye, nikaona nimuwahi, kabla hajafanya mabaya, lakini sikuwa
na lengo baya la kumu…u….’akasema huku akiwa kanysha mikono juu.
‘Ni nani huyo mwanamke ?’ akaulizwa.
‘Mimi simjui, alikuwa kava kama nyie…mimi simjui
kabisa,..’akasema huku akiangalia huku na huku.
‘Kwahiyo ukaua, ukimtetea mke wako, ?’ akaulizwa
‘Sio mke wangu ni mwanamke ninayeishi naye, yaani kuja
kwake, kumeniletea matatizo kila siku shida, sasa kaniletea mtoto,….eti ni
mtoto wake,…yaani …’akasema huku akinyosha mikono juu kama mwizi
anayejisalimisha kwa polisi.
‘Hebu tuambie, huyo mwanamke unayesema anataka kukuleta
mtoto, anataka kukuletea mtoto gani?’ akauliza.
‘Mimi sijui, yeye anadai alikuwa akiishi porini, na
alipojifungua wakamchukua mtoto wake, na yeye wakataka kumuua, lakini
akaokolewa …’akasema huku akiendelea kunyosha mikono juu. Malikia aliposikia
hivyo, akaamrisha huyo mlevi asimamishwe .
‘Huenda huyo mwanamke ndiye Maua tunayemtafuta..’akasema
malikia.
Yule mlevi akasimama huku akiwa na wasiwasi, bado alikuwa
hajawa na uhakika wa maisha yake, kwani anawajua sana watu wa msituni, huwa mmoja
wao akiuliwa, ni lazima walipize kisasi.
‘Huyo mwanamke unayeishi naye anaiitwa nani?’ akaulizwa.
‘Ana…ana..itwa Maua….’akasema.
Malikia akamsogelea yule mlevi na kumshika kichwani, yule
mlevi akashangaa, na kuinama ili ule mkono utulie vyema kichwani mwake, na
baadaye akainua uso kwa mashaka kumwangalia huyo malikia, halafu ule mkono
ulipoondolewa, akabakia kainama vile vile, hakujua ina maana gani.
‘Tupeleke kwa huyo mwanamke, sisi ni wageni wake’akaambiwa,
na aliposikia hivyo, akaanza kuogopa zaidi, kwani inawezekana wanataka
kumchukua Maua wakamue, kwani kama alivyoelezewa na Maua, kuwa alishahukumiwa
kuuliwa, …
‘Hapana….msameheni, hana hatia ..’akasema.
‘Sisi hatuna ubaya na yeye, sisi lengo letu ni jema kabisa,
tunahitaji kumuona yeye, ili tumuelezee kuhusu mtoto wake’akaambiwa.
‘Mtoto wake ?’ akauliza yule mlevi,kwa kushangaa.
‘Wewe tuambie yupo wapi ili tukaongee na yeye, hatukuja kwa
shari..’wakasema.
‘Oohoo, sasa hilo balaa, kwani nyie ni akina nani?’
akauliza.
‘Mim ni malikia,…na mume wangu ndiye aliyemuoka huyo
mwanamke, kama ndiyo yeye unayemuongolea, na ili tuwe na uhakika huo tunaomba
tukutane naye yupo wapi.
‘Ohoo….hilo sasa balaa….’akasema na akageuka kushoto ,
halafu kulia, tahamaki, alihomoka akaanza kukimbia….’malikia alipoona hivyo,
akaamurisha askari wamkimbize….
‘Hakikisha mnamkamata, kwani yeye ndiye atakayetufikisha
hukoo tunapokwenda, …..’akasema malikia, kwani muda mchache uliopita walikuwa
wameshatuma wajumbe nyumbani ambapo, walitarajia kufikia. Sehemu ambayo
inajulikana kuwa Maua ndipo anaishi na mwanaume muuza pombe za kienyeji, lakini
walipofika hapo, walikuta nyumba haina watu, wenyeji wake wamehama. Na
hawajulikani wapi walipohamia.
NB: Kisa chetu kinaelekea ukingoni, ambapo, sasa tunataweza
kukutana na Maua, msimuliaji wa kisa hiki.
WAZO LA LEO:
Yakikufika machungu usikate tamaa, ukipatwa na taabu, usivunjike nguvu, kwani
yote ni mapito,na wewe sio wa kwanza kukutana na hiyo mitihani. Omba mungu,
jitahidi kupambana nayo, ipo siku utashinda, kwani muomba mungu hachoki,
akichoka keshapata.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment