Malikia mtarajiwa akawa anaendelea na safari yake na sasa
walikuwa wametoka kabisa kwenye eneo linalokaliwa na jeshi lao, na ili wafike
huko wanapokwenda inabidi wakatishe eneo ambalo kikosi cha hasimu kimeweka
kambi yao, hapo wale waongozaji wanaojua njia, wakasimama;
‘Mtukufu malikia, sehemu hii tunayohitajika kuvuka ndipo
sehemu yenye kikosi cha hasimu, na mwenzangu kafanya utafiti, kgundua kuwa
sehemu zote za njia za kutokea nchi za walipototea wamezizingira….’akasema.
Malikia akatulia kwa muda bila kusema kitu, na wazo likamjia
kuwa atume ujumbe wa Hasimu amwambai kuwa anapita , lakini anahitaji
kuwasalimia maana yeye ni mama wa wote, na sio vyema kubagua watoto wako hata kama
wamekuasi.
Akawaambia washauri wake, washauri wake, waliogopa sana
kukutana na watu, hasa askari wa hasimu, kwani pamoja na yote wanaweza hata
kuwazalilisha, wakamwambia hilo, na malikia aliposikia kuwa askari hawo wana
tabia hiyo, akamwambia muongozaji wa msafara.
‘Ina maana hayo yalishawahi kutokea na hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa mbona kuna sheria kali zinasema askari atayemzalilisha mwanamke
adhabu yake ni kutupiwa mamba?’ akauliza.
‘Hizo sheria zipo kwa watu wengine, lakini inapofikia kwa
watu wa mzee hasimu, na askari wake, sheria hizo zinakuwa hazina meno, na ni
nani atathubutu kwenda kushitaki,…maana ili ufike huko kwenye mhakama inabidi
upitie kwa hawo hawo askari, akasema mshauri mmoja wa malikia akikimbuka kisa
kilichotokea kwa mama yake.
‘Mimi hilo lilitokea kwa dada yangu, ambaye sasa ni
marehemu, na kuuwawa kwake ni kwasababu ya hayp hayo madhila. Dada yangu
alikuwa mrembo sana, na wengi tulijua kuwa huenda akaolewa na mmoja wa watu
mashuhuri wa ukoo wa mzee hasimu.
Kumbe kuna wengi walimtaka na mmojawapo walikuwa mkuu wa
kikosi cha maaskari, na huyo akawa kila mara anamshawishi dada yangu aolewe na
huyo jamaa, lakini dada ayngu alikuwa hampendi, na wengu hawampendi huyo
askari.
‘Kwanini watu hawampendi, mbona namuona ni mwanaume mwenye mvuto,
jasiri…?’ akauliza, kwani malikia anmfahamu.
‘Tabia yake sio nzuri, hatulii na mwanamke , anapenda kila
mwanamke, na akilewa, anaweza akapiga hadi kuua, …ana hasira sana, ..na
wanaamini kuwa ukoo wao ni kichawi’akasema huyo mshauri.
‘Mbona niliskia kiongozi wa jeshi, au kiongozi yoyote
anachagulia kwa uadilifu wake, na sababu kubwa inayoweza kumzuia kiongozi
asipate hiyo nafasi ni kama ana ukoo wake ni kichawi, au kama ana tabia mbaya
za kulewa sana…..’akauliza malikia akizidi kushangaa
‘Mtukufu malikia, jeshi la mzee hasimu, limejaa watu wa
ajabu ajabu na wamewekwa hapo kwasababu maalumu, ili wamtii, kwa vile wanajijua
kuwa wanamakosa, au kisheria hawatakubaliwa, basi mzee, akawachukuati kwa masharti kuwa wamtii kwa kila jambo, na
wasipofanya hivyo, sheria zao zitawaandama kwa tabia zao na makosa yao.
‘Kwa kuogopa hilo, na kupata nafasi ya kupewa uongozi au
kuingia jeshini, ndio maana wengi wao wanamtii sana mzee huyo wakijua kuwa
anawalinda kutokana na tabia zao. Na huyo jemedari anasifika kwa huo uchawi
wake, kuwa anaweza kupambana na adui, na akamshinda kiajabu ajabu…anaweza
akapambana na hata askari kumi peke yake, kwasababu ya mazingara yake…’akasema
huyo mshauri.
‘Kwahiyo ilitokeaje kwa dada yako?’ akauliza.
‘Dada yangu na familia nzima haikukubaliana na maombi hayo,
ndipo huyo askari akaamua kufanya uchawi wake, na dada yangu aliondoka siku
moja akamfuata mwenyewe huyo askari hadi kwenye nyumba yake….’akasema huyo
mshauri kwa huzuni.
‘Alipofika hapo, akasema yupo tayari kuolewa na huyo askari,
hapo alikuwa sio yeye, alikuwa katekwa na hizo dawa zake, …basi akaolewa na
huyo askari, …watu wakabakia mdomo wazi, na hata familia haikuamini hilo ikajua
kuna madawa yametumika, na ikabidi familia ianza kufanya njia za kumuondoa
binti yako kwenye makucha ya huyo askari.
‘Huyo askari kama anavyojulikana hatosheki na mwanamke
mmoja, japokuwa limuoa dada yangu, lakini bado alikuwa akiwatafuta wanawake
wengine, na wakati mwingine kwa nguvu, na dada aliyaona hayo kwa macho yake, na
hata alipochoka, na zile dawa zilipoisha, akaamua kumkimbia..
‘Alipofika nyumbani, akawa kama kachangayikia,…anaongea
maneno ya ajabu ajabu,…na wakati mwingine anasema huyo mume wake, alikuwa akimkamatisha
askari wengine na kumzalilisha mbeel yake…’
‘Eti nini, si umesema alishaolewa na huyo askari?’ akauliza
malikia kwa hamaki.
‘Ndio, eti alikuwa akianya hivyo, kama kutoa adhabu,kwani
huenda alifanya kosa, au hakutii amri ya jambo Fulani, basi adhabu yake ilikuwa
kama hivyo….’akasema huyo mshauri.
‘Hayo ni madogo, jeshi la huyo mzee lina vituko vingi,
wengine wanasema kuna wakati wanachukua watoto wachanga na kuwaua, kwa ajili ya
kufanikisha madawa yao’akasema huyo mshauri…
‘Hayo sasa umezidisha, hilo siwezi kuliamini…maana pale
kwenye kundi lao kuna wanasheria, kuna wazee mashuhuri wanaoaminika,…ina maana
wao hawajui hilo?’ akauliza malikia.
‘Wanajua lakini wanaogopa, kama nilivyokuambia wengi wao
wamewekwa hapo kwa masharti, na kwa vile wanajijua , basi inabidi wamtii
tu,..vinginevyo, wanaweza kujikuta wakitupiwa mamba, ni kwa mshari kuwa nitii,
au nitoboe siri zako, ambazo mwisho wake ni kuishia ziwani kwa mamba, au hata
ukipona huwezei kupata tena hicho cheo…
‘Na wengine wanaogopa siri za uchawi, kwani mzee huyo ana
wataalamu wake, ambao humsaidia katika kufanikisha mambo yake..’akasema huyo
mshauri, huku akiangalia huku na kule.
‘Sasa kwanini unaongea kwa mashaka mashaka?’ akauliza.
‘Kuna imani kuwa ukiongolea kuhusu machafu ya huyo mzee
hutamaliza siku, …sasa mimi naanza kuogopa’akasema huyo mwanadada ambaye ni
mmoja wa washauri wa malikia. Malikia anampenda sana huyo mwanadada , kwani
pamoja na kuwa na akili sana , ni jasiri , anaweza kupambana kama mwanaume, na
pia humtumia katika kuchunguza mambo ambayo anahitaji kuyajua.
‘Kwanini uogope, mbona sisi hatuogopi…..na huwa tunayazungumza
machafu yake,…ujue mambo kama hayo ukiogopa ndio yanakupata, lakini ukiwa
jasiri, ukasema mimi siyaogopi, na hayawezi kunipata, na kweli hutaweza
kuzudhurika na uchawi…ukiwa na mimi
usiogope kabisa mambo ya uchawi…’akasema malikia.
‘Nashukuru sana, na kweli tangu niwe na wewe nimejikuta
nikiwa na moyo wa ujasiri, na hata yale yaliyokuwa yakinitokea, ..hayanitokei
tena…’akasema huyo mwanadada.
‘Kama yapi yaliyokuwa yakikutokea?’ akauliza malikai akizidi
kuingiwa na hamasa ya kumjua huyo mwanadada, ambaye kwa kweli alikuwa mmoja wa
warembo.
‘Mara kwa mara nilikuwa nahisi nafuatwa na uchawi wa huyo
askari aliyemchawia dada yangu, kama nilivyokuambia hutamani kila mwanamke, na
dada yangu alipofariki, akata na mimi nishike nafasi yake, nilimkatalia kata
kata, nikamwambia albda achukue maiti yangu…
‘Haya dada yako alifariki je,…na kweli mna uhakika kuwa
aliuwawa na huyo kiongozi wao wa askari, maana mimi mwenyewe nitahakikisha watu
kama hawo wanapambana na mkono wa
sheria, lakini ili iwezekane hilo, nahitajika kupata ushahidi, na ina maana
nyie mliowahi kuzalilishwa, inabidi mjitokeze, mseme ukweli wa hayo
mliyotendewa..
‘Malikia hapana, usifanye hivyo, kwani mwanamke
aliyezalilishwa hataweza kujitokeza tena na kusema uchafu aliofanyiwa, hatapata
mume, na kila mtu atamnyoshea kidole , akisema huyo alibakwa, huyo, alifanyiwa
uchafu, siwezi kumuoa…tunaomba malikia hayo yaliyopita yaache kama
yalivyo….’akalalamika huyo mshauri.
‘Inaonyesha kuwa hata wewe uliwahi kufanyiwa hivyo….sema
ukweli kwangu, na msiwe na wasiwasi kwa hilo, kwangu nyie ni watoto wangu,
nitahakikisha mnaolewa na waume bora, na kwa ajili ya kuwa wakweli, na
waaminifu….unanisikia, ukweli, uaminifu, …’akatulia akiwa anawaangalia wengine
ambao walikuwa wakisogea wakitaka kuja kusikia nini malikia anaongea.
‘Nyie mliopo karibu na mimi , na wanawake wengine wote,
watakajenga tabia ya uaminifu, wakawa wakweli, …wakawa wanatenda mume,
ninawahakikishia kuwa maisha yenu yatakuwa mema, kwani nyie mumedhihirisha kuwa
ni wanawake bora, ambao hawakupenda hayo machafu yawafike,lakini ukificha madhambi,
uliyotendewa, unamficina mkosaji, ina maana mumeshirikiana naye kuyatenda hayo
madhambi, najua kabisa hakuna alipenda yatokee hayo, kumbuka mifcha uchi hazai…
‘Mtukufu malikia, mimi yalinikuta lakini sio kwa huyo mkuu
aliyemfanyia hivyo dada yangu, ….ilikuwa ni mdogo wake huyo mkuu, ambaye pia ni mkuu wa kikosi kidogo, …wote
tabia zao ni moja,…..na kila mara nahisi vibaya ninapomuwaza, natamani
nipate silaha niitumie kulipiza kisasi, na
malikia siku nikumuona tena, naomba unipe nafasi hiyo, nilipize kisasi….’yule
binti akaanza kulia.
‘Nilishakuambia ili uwe jasiri, ili uweze kuyashinda madhila
yaliyokupata, unahitajika kutokuwa mnyonge, hayo yalishatokea, ni kama maji
yaliyomwagika, huwezi tena kuyazoa,…kisasi hakitasaidia kwani hutakuwa
umeliweka hilo kwani mizani ya sheria, na huyo mtu akajulikana kuwa kweli ni
mkosaji…’akatulia kidogo.
‘Wewe kweli ulitendewa hivyo, lakini kosa lako ni kuwa
ulinyamaza, hukulifuatilia kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake….ni kweli
kulikuwa hakuna nafasi ya kulisema hilo kwa vile utawala haukuwapa nafasi hiyo,
lakini usingeishia hapo, ungeenda hata kumwambia babu wa mume wangu, wao
wangejua jinsi gani ya kuwatetea, …..’ akilini alijua hilo kwa jinsi ilivyo
lisingeliwezekana.
‘Hata hivyo, bado ipo namna,…..’akatikisa kichwa kama
kukubalina na hilo wazo lake, akasema kwa sauti ya chini, kama kuwaambia jambo
la siri;
‘Mimi na mume tunajua madhila hayo na mengine
mengi,..nawahakikishia kuwa sasa tutahakikisha kuwa sheria inafuatwa, lakini
yote hayo hayatawezekana bila ushirikiano wenu,….kuna mengi yanaweza
yakaendelea kufanyika huko majumbani, hatutaweza kuyajua, kama nyie msipotoa
sauti, pigeni kelele tusikia,..kwenye vikao ongeeni bila kificho,….mkifanya
hivyo, watendaji wote kama viongozi, wataogopa kufanya makosa,
watawajibika…’akatulia hapo, na kuwaangalia kwa macho ya huruma.
‘Kwahiyo nawaomba tushirikiane….kosa lilishatokea, kwasasa
usikubali kosa hilo lijirudie tena. …’akatulia huku akimwangalia huyo
mwanadada, kama mama anavyomwangalia bintI yake
‘Sawa hivi nyie ni majasiri, mna nguvu sawa na hawo wanaume,
na hata kuwashinda baadhi yao,mnaweza kupambana na yoyote yule …msijiweke wanyonge,
…mnanisikia….’akasema akiwageukia wengine ambao walishasogea karibu, na wote
wakasema;
‘Tumekusikia malikia,…’wakasema kwa sauti ya ukakamavu.
Malikia akawaangalia mmoja mmoja, na moyoni akawa anatamani
kusikia madhila waliyofanyia HAWO wengine, na ikibidi atafanya hilo zoezi,
kusikia nini alifanyiwa nani kwa kila mmoja wao, akasema kimoyo moyo,
‘nitahakikisha waliyofanyiwa hayarudii tena, akamgeukia yule mwadada aliyekuwa
akiongea naye, akasema;
‘Hebu niambie dada yako aliuwawa vipi?’ akauliza
‘Dada yangu, alikutwa kajiua….na kujiua kwake ni kwasababu
ya kuzalilishwa huko, kwani taarifa zilishavuja kuwa alikuwa akizalilishwa na
maaskari wa mzee baada ya kujipeleka kwa huyo mwanaume ili aolewe kwa kutaka
utajiri…kwa kule kunyanyapaliwa na watu, hakuweza kuvumilia, na kweli tukamkuta
kajinyonga na kamba…’akasema huyo mwanadada huku akizuia machozi.
‘Kama tuhuma hizo zilizisikika kwanini mzee Hasimu, kama
kiongozi ambaye alionekana mbele ya watu kama kiongozi jasiri, kwanini hakuchukua
hatua yoyote kwa hawo maaskari, na kwanini aliendelea kumlea huyo mkuu wake,
ambaye ana nafasi kubwa kwenye jeshi lake…?’
‘Hizo tuhuma zilipofika kwake, kesi ilifanyika, lakini
hakukuwa na ushahidi, na wazazi wangu walioshitaki wakaonekana kuwa wao ndio
wenye hatia eti kwa kumpakazia mkuu wa kikosi cha mzee, uchafu kama huo, na
karibu wazazi wangu hawo watupwe kwenye bonde la mauti, lakini akapona kwa
kuombewa masamaha na huyo kiongozi wa askari, akasema yeye kawasamehe na ndio
ikawa salama yao…
Malikia alimwangalia yule binti kwa muda huku mwili
ukimtetema kwa hasira za ndani kwa ndani, baadaye akasema;
‘Siku nitakapokutana na huyo kiongozi, nitahakikisha anatubu
hayo makosa yake…..na kama nitapata ushirikiano wenu, adhabu kali itawaandama
watu kama hawo…’akasema malikia akiwa na huzuni, akageuka kwa yule muongozaji
wa msafara na kusema bila kuogopa;
‘Chagua njia unayohisi inaweza kutuvusha kwa usalama zaidi,
na kama tukikutana na hawo maaskari nitajua nni cha kufanya, ….’akasema na
msafara ukaendelea mbele na kabla hawajakatisha na kupita hilo eneo
wakasimamishwa.
Mara kundi la maaskari wa ahsimu likatokea, lilipomuona kuwa
ni malikia wote wakainamisha vichwa chini, na kama ilivyo ada, malikia ikabidi
ashuke na kuwashika wote kichwani kwao, na baadaye akawauliza;
‘Nyie najua ni askari wa mzee hasimu, je mimi mnaniamini mimi
kama malikia wenu?’ akawauliza.
‘Tunakuamini malikia mtukufu, na tunaomba baraka zako..’wakasema.
‘Basi mimi nina safari za kuwatembelea watoto wangu na
nimefurahia kuwakuta nyie mpo salama na poleni sana kwa kazi hii ngumu ya
kumtumikia mzee hasimu, lakini nawaombeni kwa vile nina haraka, nahitajika kuondoka,
ili nimalize ziara yangu ya kuwatembelea wote waliopo huku msituni…’akasema
malikia.
‘Mtukufu malikia, sisi tunakuamini na tunakuheshimu, lakini
tumapewa taarifa kuwa tusikuruhusu kuondoka, hadi mkuu wa kikosi hiki afike
…’akasema kiongozi wa hicho kikosi.
‘Hapana, sitaweza kumsubiri…mwambieni kuwa nina majukumu
mengi, kusubiri kwangu hapa tunawanyima wengine haki yao ya kukutana na mimi….’na
kabla hajamaliza mara kikaja kikundi kingine, cha maaskari na walipokaribia
pale alipokuwa malikia na watu wake, wakainama kwa heshima;
Na mara kiongozi wa kile kikosi akajitokeza akiwa kavalia
mavazi ya kiaskari, na kichwani kafunikwa na kaofia ya chuma, alipomkaribia
malikia akainamisha kichwa chake na malikia akamshika kichwa, na wote
alioongozana naye wakafanya hivyo, na alipomaliza hilo zoezi, yule kiongozi
akavua kofia lile lilokuwa limefunika sehemu kubwa ka kichwa chake, ili apate
baraka , kwani ilistahili ashike kichwa kikiwa wazi
Kipindi akalivua hilo kofia alikuwa kageukia upande mwingine
ambapo malikia hakuweza kumuona sura yake, na baadaye akageuka kumwangalia
malikia;
Yule mwadada mshauri wa malikia alipomuona huyo
jamaa,akamsogelea malikia na kuonyesha wasiwasi , ni kama vile mtoto kuona kitu
cha kutisha, na akawa anamsogelea mama yake, kupata ulinzi, na malikia
akamuuliza kwa sauti ya ndogo, ya chini kwa chini kuwa anaogopa nini;
‘Ndiyo yeye malikia, ni mdogo wa yule mkuu wao wa askari,
ndiye aliyenizalilisha mimi…naomba idhini yako nilipilize kisasi cha hayo
aliyonifanyia….’akasema huku akionyesha uso wa hasira, na kweli alichomoa
silaha yake akawa tayari kufanya lolote.
Malikia akainua uso wake, na wakawa wanaangaliana na huyo
askari, ambaye kwa muda huo, hakuwa ametamtambua yule binti, alikwa muda mwingi
akimwangalia yule malikia, na macho yake yalionyesha hisia zake, hakuweza
kuzificha, akabenua mdomo, na kusema ..
‘Mimi ni mmoja wa wakuu wa vikosi vya mzee hasimu….salamu
kwako malikia, tunaomba baraka zako katika uwajibikaji wako…je tuambie
mnakwenda wapi, na kipindi kama hiki ambacho mume wako yupo mbele ya kesi kubwa
ya kukiuka sheria, ya kujitangazia kuwa yeye ni mfalme mtarajiwa, wakati sio
kweli..?’ akauliza huyo kiongozi.
Malkia alihisi kama kutaka kutapika,…akamwangalia yule
askari,….na alishindwa hata kusema neno, moja, kwa wakati huo, akatikisa kichwa
chake, na moyoni akawa anataka kusema neno baya lakini akajizuia , na hapo hapo
akainua mkono wake hewani, akasema;
‘Tubu dhambi zako, kabla mabaya hayajakufika…’
Yule askari akabenua mdogo wa dharau, akamsogelea malikia,
akainua mkono wake, kutaka kumshika malikia,…na kabla mkono wake haujamfikia,
akatoa jicho …na kuanza kutetemeka,…..mara akadondoka chini, na askari zake
kuona hivyo, wakamsogelea, ….domo zikawa zimatoka mdomoni, akaanza
kukoroma,….haichukua muda, akatulia …uhai ukatoweka.
NB: Je kulitokea nini kwa huyo askari, je hawo maaskari
wengine watachukua hatua gani, tuzidi kuwepo, na kama ninakwenda ndivyo sivyo,
tuambiane.
WAZO LA LEO:
Imani ya kweli ya kumwamini mungu ni pale utakapowapenda najirani zako, na
ukawa tayari kutoa kile unachokipenda wewe kwa wenzako, kwa kuona kuwa ni vyema
, kwanza akipate mwenzako kabla yako…je upendo wa namna hiyo upo katika dunia
hii. Kama ungelikuwepo, dunia ingekuwa kisiwa cha upendo na amani.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Ahsante kwa kuandika. Ulitutosa kwa muda ila nashukuru umerudi. Unakwenda vizuri keep it up
Post a Comment