‘Baba Tv haiwaki…..’sauti
ya mtoto wangu ikaniamusha
asubuhi na mapema mwanzoni nilijua na hizo kelele za nje za usiku za
kusherehekea mwaka mpya, lakini nikakumbuka kuwa tulishaambiwa kuwa dunia
imebadilika inaelekea kwenye mfumo mwingine, mfumo ambao, maisha yake
hayatakuwa na cha bure tena.
‘Baba
hajanunua king’amuzi….’akasema mtoto mwingine. Niliposikia hivyo hapo roho
ikaniuma, nikainuka kitandani, na kupikicha macho, sio kawaida yangu kuchelewa
kuamuka, lakini mawazo ya usiku kucha yalinifanya nishindwe kulala.
Nikamtuma
mtoto akanunue mkate,…kwa bajeti yangu, sikupenda kufanya hivyo, lakini nilijua
kuwa huenda kumuonyesha mtoto kwa mfani itasaidia. Mkate ulipoletwa
nikawakalisha watoto, na kuushika mkate juu.
‘Huu ndio
mshahara wangu,…huu ndio mfano wa mshahara wangu,….ada aenu za shule, ni zaidi
ya huu mshahara wangu..ina hutuwezi kulipia ada zenu zote kwa huu mshahara
wangu, kwa muhuma mmoja tu, ndio maana nataka kwenda kuongea na walimu wenu
angalau tuweze kulipia kwa miezi miwili miwili, kidogo kidogo…
‘Kama
watakubali, basi katika huu msharaha, robo tatu yake, itakuwa ya kuwalipai ada
zenu za shule, ..mkate utabakia kiasi gani?’ nikawauliza.
‘Robo…’wakasema
pamoja.
Nikaondoa
robo tatu ya mkate tukabakiwa na robo, nikainua ile robo ya mkate, nikasema;
‘Hii robo
iliyobakia ndio bajeti ya mwezi, hapa tunahitajika tule, tuvae, tulipie
kodi,…hebu niambie nitaukatakata vipi huu nkate ili vitoshe hivyo vitu
vingine..haiwezekani au sio?’ nikawauliza kwani walishasema haiwezekani.
‘Ndio maana
yake, haiwezekani ….ndio maana seehmu ya kununulia king’amuzi kwa hivi sasa
haipo,…tuombe mungu, huenda mwaka 2013 ukaleta neema, ili tupate pesa ya
kuongezea mkate wetu, bila hivyo…hatutaweza,..’nikasema na watoto wakainamisha
vichwa chini, kwa huzuni….
Kabla sijaweza
kuwafafanulia vyema watoto wangu, nikasikia nje watu wakiongea, na mazunguzmo
yao yalinifanya nivutike kuwasikiliza,
‘Umeshalipia
pesa za maeneo, maana nasikia watu wameshaanza kupimiwa maeneo yao?’ sauti
ikasema.
‘Sijalipia,
pesa nitapatia wapi, wakati mtoto wangu kafaulu, nahitajika kumwaandalia sare
za shule, kuna ada….’sauti nyingine ikasema
‘Hongera,
hata wa kwangu kafaulu pia, lakini sitampeleka huko kwenye shule za kata, maana
kutoka hapa mpaka huko shuleni ni kumtesa mtoto. Usafiri wa kufika shuleni ni
mgumu, na hata ukipiga hesabu ya hiyo nauli kila siku na pesa ya matumizi, na
muda wa kuchelewa , kupigana na makondakta, gharama yake ni kubwa zaidi ya ada
ya shule za kulipia….’sauti nyingine ikasema.
‘Kwahiyo ina
maana unampelekea mtoto wako shule za kulipia, ..heri yenu nyie wenye pesa ,
sisi hatuna jinsi,….huko huko, kwenye shule za kata,….maana pesa yenyewe ya
kula ni matatizo, tunakula mlo mmoja kwa siku,asubuhi ukijaliwa ni chai ya
rangi kwa andazi moja…sitaweza kulipia hiyo ada ya shule za kulipia…mimi na
asenti Kikwete tu.’sauti nyingine ikasema.
‘Lakini
mpendwa, hebu niambie nauli ya kila siku ya mtoto kwenda shule na kurudi ni
shilingi ngapi,….na sizani kama mtoto atakwenda shule bila hata senti ya
matumizi, na angalia umbali wa kutoka hapa hadi huko shuleni, ni zaidi ya nauli
yako ya mtu mzima ya kwenda na kurudi kazini,…..’sauti ikasema.
‘Wewe unasema
tu,…hiyo nauli naipata kwa kuuza vitumbua, lakini sitaweza kudunduliza hadi
kupata hiyo ada kwa mkupua…., maana ili apate hiyo nauli, inabidi nijinyime,
..hapo hakuna jinsi, hutaweza kudunduliza,..ili upate ada kubwa, wakati huna
pesa ya kula, kuna ugonjwa, kuna vitu vingi vinahitajia pesa…
‘Nikuambie
ukweli, ukimpa mtoto nauli, unakuwa umefunga mikanda matumboni,….mnajinyima
kula ili mtoto aende shuleni, au utabana bana au kukopa ili siku iende, hata
kwa kushindia maji….sio rahisi kukuelimisha kitu kama hicho, kama haupo katika
maisha yangu…’sauti ikasema.
‘Halafu
nasikia jana wameshazima mitandao yao ya kuangalia runinga,…?’ sauti ile ikasema
baada ya ukimiya. Hapo na mimi akanitonesha kidonda, nikikumbuka kuwa na mimi
nahitajika kutafuta pesa ya kununulia hicho kidude..ili kuwe na amni ndani ya
nyumba…
‘Kwani
ulikuwa hujanunua hicho king’amuzi?’ sauti ikauliza kwa mshangao.
‘Unanichekesha
kweli, runinga yenyewe, niliipata kwenye mitumba, ….na nilihangaika hadi
kumalizia hilo deni, na huyo jamaa niliyenunua kwake, ilibidi anisamehe tu,
maana alifuatilia wee, hadi akachoka,….ningemlipa nini.
‘Niliamua
niichukue kwa mkopo, kwa vile watoto
walikuwa hawakai nyumbani,….kama wameamua kuwa ili uone mambo yao ni mpaka nilipie
kila mwezi,kwa hali yangu …sitaweza kabisa, ni heri nikaize tu, kama nitampata mtu wa kumuuzia hiyo runinga
nitafurahi, …’sauti ikasema.
‘Tatizo lenu
hamtaki maendelea mpo dunia ya kale, na ujue kabisa maendeleo ni gharama, sio
rahisi kama unavyofikiria,…kila hatua ya maendelea inabebwa na gharama zake, na
ili uweze kupata faida, inabidi uongeze juhudi, vinginevyo, utabakia
kulalamika’sauti nyingine ikasema.
‘Najua wenye
nazo mtasema hivyo, lakini …..’akatulia kidogo.
‘Lakini nini
, mbona umesita kuongea?’ akaulizwa.
‘Nimemuona
baba mwenye nyumba yangu, najua anakuja kudai pesa yake ya pango, na
keshapandisha kodi ya nyumba, anadai gharama za uendeshaji zimepanda, sijui
gharama gani wakati nyumba yenyewe hajawahi hata kuikarabati…..’sauti ikasema
na akainama chini kwa huzuni.
‘Na baba
yangu kaja toka huko kijijini , anaumwa, akisikia vurugu za huyu jamaa kudai kodi yake, atazidi
kuumia,siunajue tena uchungu wa mwana kwa mzazi hauishi…sijui nifanyeje kumzuia asifike nyumbani….’sauti ikasema kwa huzuni.
‘Ndio hayo hayo
ninayokuambia kuwa maendeleo yana gharama yake, …pesa ya kwetu thamani yake
haipandi,….shilingi ya leo, kesho haina thamani, hebu niambie hivi leo unaweza
kuipata shilingi ishirini, au kumi, ….hata ukiiona njiani huwezi kuikota. Na
hata hamsini sasa ni pesa ya pipi…je unafikiria huyo mwenye nyumba atawezake
kununua saruji, …’sauti ikasema.
‘Na huyo
mwenye mshahara thamani ya pesa yake inashuka au inapanda…?’akauliza mwingine
Mazungumzo
hayo yaliendelea lakini mimi sikuweza kuyasikia tena maana nilishazama kwenye
kuwazia mshahara wa mwezi ambao upo pale pale,thamni yake kila siku inashuka,…japokuwa
mambo yanapanda, gharama za kimaisha zinapanda, ….lakini kipato cha Mtanzania
kipo pale pale…Mwaka mpya unaanza na mambo mapya.
Mwaka
unapoanza, mambo mengi sana yanamkabili mzazi, kuna ada za shule, ambazo shule
nyingi, wameweka kiwango kikubwa cha kuanzia mwaka,…tofauti na katikati ya
mwaka, kuna kulipia kodi za nyumba, kuna malipo mengi ya kuanzia mwaka, na
ukumbuke kuwa mwishoni mwa mwaka kulikuwa na sikukuu nyingi…sasa tena tunapata
pigo jingine,…heri pigo hilo lingesogezwa hadi mwezi wa tatu,….
‘Najua nyie
mtasema ni gharama ndogo tu, vijisenti tu,….kwa vile mnazo, lakini kama
mngelikuwa katika hali kama yangu, msingeliweza kusema hivyo, maana siri ya
mtungi aijueye ni kata…’nikasikia hiyo sauti ikilalamika na mimi nikasema ni
kweli, kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake.
‘Ndivyo
ilivyo, maisha ya sasa hakuna cha bure tena, tutalipia kila kitu, hewa, maji,..itafikia
hata kuongea utatakiwa ulipie…maisha ya dunia yanabadilika siku hadi siku ,
ujima ujamaa, undugu, ..upendo hautakuwa na nafasi tena,,,,,maana hata ndugu
yako akikutembelea hutaweza hata kumkirimu, …tutafukuzana ndugu ili tuweze kumudu
maishi,hapo kutakuwa na upendo tena….hayo ndiyo maendeleo, ukiwa nacho utaweza
kuishi, kama huna….
‘Ina maana
kama sina…. sina uhai tena….?’akauliza
‘Jibu unalo
mwenyewe, nikuuliza, kama huna king’amuzi utaweza kuangalai tena runinga?’
sauti ikauliza.
‘Utaona
chenga chenga tu, huwezi kuona kitu.’sauti ikasema.
‘Sasa kumbe
unajua..hayo ndiyo maisha, mwenye nacho, ataongezewa, kama huna kitu,..ulie tu…utaishia
kuona chenga-chenga tu,, hata hicho kidogo ulicho nacho, watakuja
kukunyang;anya , maana kuna kodi za watu, kuna kulipia majengo, dukani hakukamatiki,
unafikiri hapo una maisha tena…wewe ni mfu tu.
Ni hayo kwa leo kutoka kwenye diary ya tarehe 1-1-2013Ni mimi:
emu-three
2 comments :
bear grylls messer
Review my weblog ... bear grylls messer
Ujumbe huu kweli umetulia,Ndudu wa mimi wewe ni mwisho!!!!!!!Pamoja saaana....Mmhhh kweli kitanda usichokilalia hujui Kunguni Wake!!!!!!
Post a Comment