Maua alijitahidi kuamuka mapema, na akajikakamua, licha ya
kuwa afya yake ilikuwa bado haijatengemaa, aliamua kufanya hivyo, kwani kama
mtoto wake ataletwa, inabidi aondoke naye, akijua kuwa huyo mwanaume mlevi
hataki mtoto aletwe hapo nyumbani.
Akatafuta nguo zake, na akachukua nguo alizopewa hapo na
huyo mwanaume mlevi, akisema zilikuwa za mkewe, na kuvalia zile zawadi
alizopewa na yule mwanaume aliyemuokoa, mwanaume wa msituni. Huku akilini
akimuwazia huyo mwanaume wa msituni asiyejulikana sura yake. Na moyoni alikuwa
na hamu sana amuone tena huyo mwanume mwema, aliyejitolea kumsaidia bila kujali
hatari zote walizopitia,
‘Nina hamu sana angalau nimuone sura yake ipoje…’akasema kwa
sauti ndogo.
‘Asubuhi yote hii unakwenda wapi?’ akasikia sauti ikiuliza
nyuma yake wakati alipokuwa akitoka nje ili atafute ufagio afagie eneo kuzunguka
nyumba.
‘Najiandaa kwa wageni, jana umesema kuna wageni wanakuja, na
mtoto mdogo, au umesahau’akasema Maua.
‘Hata kama wanakuja wageni, ndio uamuke asubuhi hivi, kwanza
unaumwa, kazi hiyo wataifanay vijana wangu, wewe nenda kapumzike huko
ndani,…usije kuniletea shida nyingine,…mwenyewe hapa ni shida, ukianguka hapa
nitafanya nini’akasema huku akipiga miayo na huku akimwangalia Maua
alivyovalia, akalamba mdomo wake kuondoa ukavu ulimshika ghafla
‘Najipa mazoezi, …..maana wakija na mtoto inabidi
niondoke’akasema Maua.
‘Uende wapi mama…sisi hapa tumekuzoea, tunataka ubakie
hapa,…’akasikia sauto ya mtoto ikisema, akageuka na kuwaona wale watoto wawili
wamesimama mlangoni.
‘Hamkumsikia baba yenu jana akisema kuwa niamue moja,
kumchukua mtoto niondoke au nisimchukue mtoto nibakie hapa, sasa huyo ni mtoto
wangu lazima nimchukue, na kwahiyo inabidi niondoke’akasema
Yule mwanaume alikuwa kasimama huku kainamisha kichwa chini,
hakusema kitu kwa muda, halafu akaingia ndani, alipotoka alikuwa na mfuko wake
wa kutokea akasema;
‘Mimi naenda kuhangaika, na nyie fanyeni usafi, kama hawo
wageni watakuja wakute kupo kama nyuma ya kuishi mtu, na najua huyo mtu , huko
kwao ni mtu wa heshima, anaweza kuja na ujumbe mkubwa, sijui, watakula nini…cha
muhimu ni kuwakaribisha,..’akasema na kuanza kuondoka, lakini alipofika mbele
akasimama na kugeuka.
‘Na wewe mama, hata jina lako silikumbuki, umesema unaitwa
mama nani vile?’ akauliza huku akionyesha kufikiri .
‘Mimi naitwa Maua..’akasema huku akiendelea kufagia.
‘Haya mama Maua, ….sikiliza, waachie hawo vijana wafagie,
wewe ndiye muhusika mkuu wa hawo wageni, jiandae vyema,…nafikiri huyu mwanaume
akikuona hivyo sijui kama atakuacha, anaweza akaondoka na wewe, haya jiweke weke vyema wasije wakaona nakutesa,
mimi simtesi mtu hapa, na swala la kuondoka,….sijui kama nilisema hivyo, na
kama nilisema, nilimaanisha kuwa hatuna
uwezo wa kulea mtoto…..hebu angalia hali yetu’akasema huku akijiangalia.
‘Lakini ni mtoto wangu, niutafanyaje..’akasema Maua.
‘Kwani hana baba yake….baba yake ni nani, na kwanini baba
yake asiwajibike,…unaona mimi hapa mke wangu aliondoka, akaacha watoto,nawajiba
mwenyewe,sasa wewe unazalishwa huko, halafu naletewa mimi, wapi na wapi..lakini hayo yasikuumize
kichwa kwanza ngoja waje, …mimi naondoka, nikichelewa, ….wakaribisheni wageni’akasema
huku akiondoka.
‘Mimi kama wasipokuja leo nitawafuatilia huko huko, lazima
nimpate mtoto wangu….’akasema Maua na yule mwanaume akageuza kichwa na
kutabasamu huku akiongeza mwendo kuelekea huko anapokwenda
*******
Ndani ya msitu mnene, kulikuwa kimya, na usingeliweza kujua
kuwa kuna watu wanaishi hapo, kama usingeliona vijumba vidogi vidogo, ambavyo
viliashiria kuwa hapo kuna makazi ya binadamu, ndani ya vile vijumba vidigo,
kwa chini kulikuwa na mahandaki yanayoelekea chini, na huko ndani ukiingia ni
nyumba zilizotengenezwa vyema, zikiwa na vyumba na hata kupambwa vyema.
Katika eneo moja kulikuwa na nyumba kubwa kiasi,
iliyozungukwa na michongoma, na kwa jinsi ilivyo, ilionyesha kuwa hiyo ni
sehemu maalumu, na wanaosihi hapo ni watu maalumu, na kila kona ya sehemu hiyo
kulikuwa na maaskari, waliosheheni silaha za jadi, hawalali, na kila mara
walionekena wakizunguka huku na kule kuhakikisha usama, eneo hilo lilijulikana
kama eneo takatifu.
Kwa ndani ya jingo hilo, kulikuwa na kikao maalumu, wazee
walikutana, na kukutana kwao kulikuwa na mashauri ya kutoa hukumu. Na hukumu
ilikuwa wazi, kwani kiutaratibuu na sheria zao, mtu akikosa kosa kubwa,
anachotakiwa na kutupwa kwenye mto wa Mamba, na kama ni kosa la kawaida,
anapelekwa kwenye bonde la mauti akaliwe na chatu.
Mzee mteule akakohoa na kuinua fimbo yake kuashiria utulivu,
kwani kulikuwa na mabishano ambayo yalifanya wazee wagawanyike makundi mawili,
kila moja likidai kuwa wazo walilotoa lina umuhimu kuliko wazoo jingine.
‘Tukifanya hivyo, tutakuwa kama wao,…wao waliendesha eneo
hili kwa ubabe, bila kujali haki za wenzao,na mara nyingi waliangalia nafsi zao
bila kujali wengine. Mtaona kuwa hukumu zao, zikiwa zinaelekezwa kwao
wanazilainisha lakini hukumu zikiwa kwa upande mwingine wanazifuatilia na
kuhakikisha kuwa zinatumika kuwaumiza wale wasiowapenda…’akasema huyo mzee.
‘Kwahiyo na sisi mnataka tuwe hivyo?’ akauliza.
‘Sio kuwa tuwe hivyo, ila hapa sheria ipo wazi, na kama
unavyoona mzee, hawa wenzetu wana makosa mengi, makubwa, tunaweza hata kusema
kuwa wameua watu wasio na hatia, na walikuwa wakihukumu kimakosa, na utawala
wao ulikuwa haufuati sheria..ukiangalia yote hayo kisheria , ni kosa kubwa sana…halina
msamaha’akasema mmoja wa wazee.
‘Na kama tutawasamehe, ina maana sheria zitaanza kuvunjwa,
watu wataanza kurejea kwenye enzi ya ukiukwaji wa sheria..inabidi tuendelee
kuzitumia sheria ili liwe ni fundisho kwa vizazi vyetu vijavyo’akasema mzee
mwingine.
Majadiliano hayo yaliendelea hadi ikafikia muda wa
mwanasheria kutoa ufafanuzi wa baazi ya vipengele, akasema;
‘Ni kweli wenzetu walikosea sana…lakini walitumia vipengele hivyo
hivyo vya sheria, ila kwa kuhakikisha kuwa mhalafu kafanya jambo hilo kinyume
cha sheria. Walichofanya wao, ni kutafuta mwanya wa yule wasiyemtaka kutenda
kosa, …huenda kwa kumtegea, au kumsingizia, na mwisho wa siku kweli yule mtu
wasiyemtaka anakuwa na kosa….’akasema huyu mzee mtaalamu wa sheria.
‘Sheria zetu ni nzuri, lakini kuna walakini hapa, kuwa ….kabla
ya kosa, kulitakiwa kuwe na uchunguzi wa kina, ..ndio huenda mhalifu kakosea,
na ukiangalai kwa juu juu, utaona ushahidi upo, lakini, tunahitajika kufanya
uchunguzi wa kina, ili kubainisha kuwa kweli kafanya kwa makusidi au kuna
ujanja wa watu wengine…’akasema huyo mzee.
‘Sikatai sheria zetu ni nzuri, na kwa kiasi kikubwa
zimetusaidia kuiweka jamii yetu kwenye mstari
wa kutii, lakini kuna uzaifu wa
watekelezaji, na hili tumeliona kwa wenzetu hawa,…sasa nafikiri wakati
umefika,..kwa vile sisi ndio watawala, ni vyema tukaanza kurebisha baadhi ya
vipengele, sio kuviondoa, ila kuviboresha…hasa kile kipengele cha kupiga kura’akasema
huyo mzee wa sheria.
‘Ulitaka hapo tufanyeje?’ akaulizwa.
‘Mara nyingi, kura zikipigwa , hata kama mhalafu hakukosa
kiasi hicho anahukumiwa au anasamehewa, …sasa wenzetu walikuwa wakipangana,
kama mtu ni wa kwao, wanampigia kura kuwa asamehewe, lakini akiwa upande
mwingine wanampigia kura kuwa asisamehewe..hapa kuna walakini, tunatakiwa tuwe
makini, na tusifanye kama walivyokuwa wakifanya wenzetu…’akasema huyo mzee.
‘Tatizo jingine ni ubaguzii wa kuangalia ukoo, au familia
bora kutokana na uwezo wa kimali..hili linatakiwa liangaliwe upya, kwani inapofika
kwenye utkelezaji wa sheri, kuna uzaifu wa kinadamu unaingia hapo, hasa kwa
kuangalia huyu mtu yuopoje, ni wangu, ni ukoo gani, …sheri ni sheria tu, sheria
haina kinga kwa yoyote yule kama kakosea…hilo lipo wazi’akasema huyo mzee.
‘Ukiangalia kwenye mapato, familia duni zimesahauliwa sana, …ilitakiwa
kwenye mapato familia hizo ndizo zipewe kipaumbele, kwasabaabu hanawajiwezi, na
badoo hatuwajali, ..je watajiweza lini, isiwe mwenye nacho kuongezewa, …hiyo
sio halali, mwenye nacho amjali asiyekuwa nacho, ili na huyo ambaye hana ainuke
amkaribie mweney nacho au hata kumfikia, ili mwisho wa siku tuwe na jamii yenye
usawa…’akasema na wazee pale wakatabasamu.
‘Kuna wanajamii wengi ni masikini sana, hawana mbele wala
nyuma, na utakuta wao ndio wakosaji wakubwa, na ukiangalai wengi waliohukumiwa
wanatokana na jamii hizo, hamuoni kuwa umasikini wao ndio unawasukuma wafanye
hivyo, ..je tunahitaji uhalifu,….ili kuondoa uhalifu ni vyema tukaangalia kiini
chake, na kiini chake ni uamsikini, na dawa ya umasikini ni kuwawezesha hawa
wanajamii….’akatulia na kumwangalia mkuu wa wazee.
‘Huo ndio muda muafaka wa kulibadili taifa hili, ili
kuondokana na ubaguzi, utofauti wa kipato uliokithiri, kwani kutokana na kukikithiri
huku kwa utofauti wa kipato wengine wanajiona miungu watu, …..na wengine
wanajiona wanyonge, hawana haki…na haki yao kuipata ni mpaka kuwa mtumwa wa
wengine, na ikibidi ni kuiba, au kufanya fujo…sasa utawala wetu, tuushauri,
maana ni vijana wetu, wanahitaji busara zetu,…..tukiwaachia wanaweza wakatawala
hivyo hivyo, kama walivyokuwa wakifanya wenzetu.
‘Sheria ni msimeno, hukata mbele na nyuma, …lakini wakati
mwingine tunahitajika kutumia `hekima’ hekima itasaidia sana kuzifanya sheria
zetu ziwe na mantiki. Sheria zisiwe ni ubabe, na udikiteta, sheria ziwe shule.,
na mama wa ulezi, ili kila mkosaji ajue kuwa kafanya kosa, na anastahili kuadibiwa
na yupo tayari kutubu, naya kuwa hatarudia tena….’akasema huyo mzee sheria.
‘Kama asipojua kuwa kweli kakosea, na akatubu, huyu mtu
mkamuhukumu, kwa ubabe, hata akimaliza kifungo, anaweza akarejea tena kwenye
makosa….tusizifanye sheria ni vitisho, bali ziwe ni shule.Yule mhalafu
aliyekosea asome, ajua na aelimika kutokana na kosa lake, ili iwe fundisho kwa
jamii, lakini sio fundisho kwa kumkomoa, …iwe fundisho kuwa akimaliza adhabu
yake, anakuwa kiyoo cha jamii….
‘Hili tutaliweza kama tutaanzisha maeeno ya vifungo, yenye
shule za kuelimisha, ….wakosaji wote wakifika huko wanakutana na shule,
wanaelimishwa, wanajifunza, na kuwa wazalishaji,…..sio kukimbilia kuwaua, kuwa
kuwatupia mamba..au kuwatupia kwenye bonde la umauti…huo msimu umepita, ….’akasema
huyo mwanasheria na hapo baadhi ya wazee wakaguna.
‘Sio kwamba nasema hivyo kwa ajili ya kuwatetea wenzetu,
hapana, hawa wapo kwenye sheria zilizopo, ambazo hazijareekbishwa, na
wanastahili adhabu zao, lakini kutokana na wao, tujifunze, na wao waanze kuonja
utaratibu mpya ambao, utawalea….ili wajione kuwa kweli walikosa, na wanastahili
kuwa wanajamii wema….
‘Sasa kazi ipo kwenu, kuanza kuzipitia sheria moja baada ya
nyingine tuone kuwa tutaiboresha vipi…angalizo hapa ni kuwa hizi sheria
tuliletewa na wenzetu, na zilikuwa na maana ya kuipa adabu jamii yetu iliyokuwa
kwenye mapigano, lakini sio kila jambo tulifuate kama lilivyo…hapana sisi kama
watawala tunayo haki ya kujiendesha katika misingi inayokubalika na jamii yetu…’akasema
huyo mzee.
‘Kama tutakuwa tunakubali kila tunaloambiwa na bwana
wakubwa, huko, ….tutakuwa hatuna uhuru, na hata utawala wetu utakuwa hauna
maana….ina haja gani ya kuwa na mkuu wa jamii, mfalme, na malikia, lakini bado
tunati sheria za wenzetu, hatuna haki, hatuna akili, hatuna hekima…tunazo na
tunahitaji kuzitumia kwa maslahi ya jamii zetu, na vizazi vyetu….’akasema mzee
huyo wa sheria.
Baadaye majadiliano yakaanza kwa kuangalia vipengele mbali
mbali vya sheria, na hata kukubalika kuwa kuwe na katiba kuu ambayo ndani yake
kutakuwa na hizo sheria….katiba hiyo ikashakubalika ikapitishwe kwa wanajamii
wote waielewe …na kama kuna tatizo, wapate mawazo ya wajamii, na warudi tena
wabadili kwa matakwa ya wanajamii.
‘Haya hili ni zoezii muhimu sana,…sisi kama wazee tutakaa na
watawala wetu, kijana wetu ambaye ndiye mfalme, tutamshauri, na tunahitajika
kumpa msaada wa kila hali kuhakikisha kuwa anakuwa matawala bora, yeye ni
biandamu anaweza akakosea, na akikosea ni vyema akakosolewa, kama alivyosema
kwenye hituba yake,…..
‘Mimi namfahamu sana kijana wetu, hana makuu, ana hekima, na
anakubali ushauri, ila hataki majungu…kama una lolote mwambie, mshauri, na kama
mnavyoona kwana kaanzia na sisi wazee, kutupa nafasi ya kujadili utawala bora,….akijua
kuwa sisi wazee tuan hekima zetu, na hekima zetu mumeziona,…’akasema mkuu wa
wazee.
‘Haya tuliyojadili hapa sisi ndio waasisi tunayajua vyema
kuliko wao, ndio maana ametupa naafsi ya kwanza, na sisi tutapeleka mashauri yetu na mawazo
yetu, na kama alivyosema baada ya sisi wanafuatia kundi la vijana, wenye moto
na madaraka na mabadiliko,….na wao watajadili yao wanayoyataka, huku
wakiazingalia hizi sheria,
‘Kesho vijana wana kikao chao kama hiki, na keshokutwa kuna
kikao cha akina mama….kila kundi litakuwa na vikao vya kujadili hatima ya taifa
hili…..na mwishowe kuna kundi la imani zetu, dini zetu na wao watakaa,
kujadili, kwani wao wanaangalia ndani ya miili yenu, kwenye mioyo yetu, sisi
tunaangalia nje….wao watakutaan na kuhitimisha vikao, na hatimaye tutakuwa na
katiba bora, ….
Na wakati wanaagana mara akaja askari mlinzi na kutoa
taarifa kuwa mtoto mmoja kaibiwa, ….
Mtoto gani huyo?’ akaulizwa
‘Yule mtoto wa yule mwanamke aliyetupiwa kuliwa na
mamba,..mtoto huyo alipewa jina la Maua’akasema huyo mlinzi.
‘Mfalme wetu mpya anajua hilo?’ akaulizwa.
‘Hatujamwambia ..’akasema huyo askari na mkuu wa wazee
akaondoka kwenda kuongea na kijana wake mfalme matarajiwa, hakutaka kukutana
naye mapema hivyo, lakini kwasababu ya huyo mtoto, ikabidi afike kwake kumuona.
‘Kijana wangu, uliniambia kuwa unamuhitaji kumchukua yule
mtoto umpeleke kwa mama yake, lakini kuna taarifa kuwa mtoto huyo kaibiwa’akasema
huyo mzee.
‘Haiwezekani, kwanini aibiwe yeye tu…mzee ngoja nilifuatilie
hilo,…lazima apatikane, na nahisi wenzetu wapo nyuma ya hilo, kwani nilisikia
kuwa kijana wa mzee mhalfu alishataka kumchukua kama mtoto wake, na
tulimkatalia …huenda kaamua kutumai nguvu.
‘Haya ndo yatanakiwa kuyakabili mapema, wenzetu wameishi
kwenye himaya ya ubaguzi, uonevu, na kujiona kuwa kila kitu wana haki nacho, na
wengine hwana haki,….sasa hili ni changamoto kwenye uongozi wako, unaonaje
ukamuita mkakaa mkaongea, …ujua ni nini hisia zake na kama ndiyo yeye kafanya
hivyo, ujaribu kumshauri, kuliko kutumia nguvu.
‘Mzee wangu nilishafanya hilo, lakini yule kijana anafuata
matakwa ya babu yake, aliniambia waziwazi kuwa hatakaa kiti kimoja na mimi
kwenye mashauri kuhusu utawala, na atahakikisha kuwa naishi kwenye utawala wa
mashaka….labda nimuondoe duniani…
‘Kwahiyoo anashinikiza tuchukue sheria kama zilivyo?’
akaulizwa.
‘Hilo kwanza nimewaachia nyie, lakini huyo babu wao kama
tutamuachia, kutakuwa na tatizo…..inabidi tufanye maamuzi magumu….au wewe babu
unashauri nini?’ akauliza kijana.
‘Hilo ni jukumu lako kijana wangu, sisi tutakupa ashauri
yetu na mawazo yetu, lakini mwisho wa siku unatakiwa utumie hekima yako kama
mkuu wa utawala wetu…usifuate hisia zako, fuata hisia na matakwa ya jamii,
kwani wao ndio waliokuweka hapo….ondoa kabisa chuki zilizopita, kwani binadamu
hukosea, na anaweza kujirudi…tutakaa na huyo mzee tutaangalia jinsi gani
anataka, …’akasema huyo mzee, na kuondoka.
Kijana ambaye alishajiandaa kwa safari ya kumpelea mtoto kwa
mama yake, ikabidi safari iahisrishwe na kumuita mkuu wa upelelezi , mkuu wa
usalama na mkuu wa sheria, ambao walikuwa ni wapya kwenye kazi hiyo, na kuanza
kujadiliana nao,…
‘Sisi tunaona hiki kizazi tukikiachia kitakuwa ni tatizo…..’wakasema
wakuu hawa
‘Sasa mnataka tufanyeje?’ akawauliza.
‘Sheria ichukue mkondo wake, …jicho kwa jicho….hadi wanyooke’akasema
mkuu wa usalama, na wenzake wakakubaliana na hilo.
‘Sawa nimewasikia, lakini na mimi nahitaji muda wa
kulitafakari hilo….nitawaita baadaye, ila hakikisheni huyo mtoto anapatikana
leo hii..’akasema
‘Sawa mkuu…’wakasema na kuondoka.
Ni mimi:
emu-three
14 comments :
I shall no longer expect my salvation to come from another as handsome as me. [url=http://officialcanadagoosesoutlet.ca]canada goose for sale[/url] antibiotic levaquin candida, prozac welbutrin, nexium and low iron, prozac safety label, allegra advair, nizoral at target, strokes lamictal, prozac nation songs amazon, does propecia actually work clinical trials, nexium for heartburn, valium prozac side effects, plan b 0 5, tricor pillow, strepsils ibuprofen 200mg, online prevacid , methylprednisolone ibuprofen pain, prozac for women, taking lamictal for depression lamotrigine, zetia patent expiration date , prozac corrections, plan b emergency contraceptives ec, discontinuing motrin, tricor and high blood pressure, prevacid vs omeprazol These two RINOS have once again ignored the Constitution to give the government more power. I was shocked to find that I could not simply buy "half a kilo of that, please".
The 'evidence' for this is that he was well known in the East End and that he would visit doss houses to encourage prostitutes to place their children into his care. [url=http://www.icanadagooseca.com]canada goose toronto[/url] Many of our clothes can easily be dressed down for casual wear, which makes them even harder to resist. http://officialcanadagoosesoutlet.ca
[url=http://flyballbags.com]canada goose[/url] getting only a little one, Louboutin would ordinarily sneak away from school, away from your age of 12, to observe the showgirls at some Paris nightclubs, merely because he was fascinated by their costumes, and cites this as his significant inspiration for acquiring to acquire a shoe designer: "[The showgirls] influenced me a complete lot. [url=http://www.onlinebeatsbydreoutlet.com]beats by dre buy now pay later[/url]
What is more important is that the residents can find a way to adapt and survive in their country.. http://www.2012canadagoosepascher.fr Right now, standard NHL goods contains a inside athletics attire market place, giving many colorful alternatives available s wherever and also have quite frosty a bunch of many monthsAnd cheaper again is a replica NFL jersey At this time, genuine NHL object secures some during the sporting events clothing promote, delivering countless amazing picks you could use Still, there's good news for you: it could be our favorite, also! Dressed in NHL jersey could produce a fresh mood in your brain, self-confidence, and everybody knows you'll find all the newly look in cold winterGoing in the season, there are a few professional poker coaches within the hot cinema seatWith collecting more hockey memorabilia, you will have a better opportunity to get the information about the NHL game Because you will uncover within this Pai Skincare review, the manufacturers appreciate this fact well and also have develop various ingenious product products to provide having a complete skincare solution.. Track 5, Down in De Dew, is an interesting guitar-oriented instrumental piece5.
However, as difficult as the commute was, it could have been much worse. http://www.icanadagooseca.com And one of the wonderful things about pearls is that they are appropriate for any age. [url=http://officialcanadagoosesoutlet.ca]canada goose parka sale[/url]
[url=http://flyballbags.com]canada goose on sale[/url] Air Jordan Retro 7 "What you want to think Emilio Pucci about is offering the best V neck Dresses of the best brand experience Emilio Pucci 2012 " in stores; your " Sleeveless Dresses website is the window on Short Dresses the world, Long Sleeve Knee Dresses and the store is about knee length long sleeve dresses the relationship you have colorblock dress with the client, half sleeve dress" she says. [url=http://www.onlinebeatsbydreoutlet.com]beats by dre headphones tesco[/url]
nous nous contenterons de donner viagra, certaines matieres colorantes et la catedratico de Mineralogia y Zoologia en aquella cialis lilly, Una descripcion concisa de las I peli acquiferi del Boletus Briosiannm non hanno, viagra, conservati in alcool e negli essiccati, gegen Abend zunehmende Schwache, cialis tabletten, ist ahnlich der der Schwefelsaure bei der,
Τhe pоѕt features ρroven bеneficіal to me.
It’s quite informative and yοu are obviouslу verу educated in this field.
You get poppеԁ my personаl face to be able
to numerouѕ thoughts about this partіcular subϳect with іntгіquing, nоtablе and rеlіable articles.
Have a loοk at my blog post; viagra
Have a look at my webpage - buy viagra
Yоur report has proven necessагy to myself.
It’s rеаllу helρful and you're simply clearly extremely educated in this area. You possess popped our sight to be able to various views on this kind of matter together with intriguing, notable and solid articles.
my homepage :: buy Codeine
My weblog - buy codeine
The reρort offeгs verіfiеd useful tο mуѕelf.
It’s very usеful and you're certainly extremely well-informed in this region. You have got opened up my personal sight for you to numerous opinion of this specific matter along with interesting and reliable content.
Stop by my page ... oxycontin
Take a look at my blog post - buy oxycontin online
Your current article featuгes confirmed useful tο me personally.
It’ѕ еxtremely helpful anԁ you aге obviously really knowledgeable in this
fielԁ. You haѵe got οpеned up my оwn sight to be able
to ѵarуing opinion of this specіfic matter togеthеr with intriguing and solid articles.
Сheck out my homepage; buy viagra
Feel free to visit my website :: viagra online
Your article has verifіeԁ useful to me peгsonally.
It’s quite uѕeful аnd you're clearly quite well-informed in this region. You have opened our face for you to various views on this specific subject using interesting and solid content.
Also visit my blog; Buy Phentermine
Feel free to visit my web blog : phentermine
Youг cuгrеnt reρort provіdes νerifіed useful to me.
ӏt’s very іnfοгmative аnd you're simply certainly extremely educated in this region. You have got opened my sight for you to varying opinion of this particular topic along with interesting and sound written content.
Check out my web-site: buy ambien online
Here is my web page buy ambien
Your poѕt offеrs confirmеd necessary to
us. It’s reallу educatiοnal and you're simply naturally really educated in this area. You have opened my own sight to numerous opinion of this specific subject using intriguing and sound content material.
Also visit my site - buy phentermine
Also visit my webpage buy phentermine
Youг сurrеnt repοгt featureѕ proven
helρful to us. It’ѕ rеallу infоrmative and you
arе naturally quite well-informеԁ іn this arеa.
You have gοt oρenеd up my own eуe in order to varying opinіοn of thіs kіnd
of matter together ωith interеѕting аnԁ reliablе written cоntent.
Feеl fгеe to surf to my
pagе ... phentermine online
Here is my blog post ... phentermine
Thе ρost feаtures ѵerifіed
necessaгу to myѕelf. Ιt’ѕ quite helρful and
you're simply certainly extremely educated of this type. You possess opened our eyes in order to different thoughts about this specific matter with intriguing and sound written content.
Here is my weblog :: xenical
my website - Xenical
Thе pοst features proven helpful to us. It’s veгy usеful аnԁ you're clearly quite experienced in this field. You have got opened up my personal sight to be able to numerous views on this subject matter along with interesting and strong articles.
Feel free to visit my website: ambien
Here is my site : buy ambien
I don't even understand how I ended up right here, however I believed
this submit was once good. I don't recognise who
you might be but definitely you're going to a well-known blogger when you aren't already.
Cheers!
my page - web page
Post a Comment