Marejeo: Tukumbuke hiki kisa alikuwa akisimulia yule binti
niliyekutana naye akiwa kajiinamia kashika shavu, ….akiwa kasimuliwa na mama
yake. Huyu binti kwa hali aliyokuwa nayo, alifikia hadi kukusudia hata kujiua.
Binti aliona kabisa , kuwa maisha kwake hayana thamani tena.
Na binadamu anapofikia hapo, ujue kweli kuna jambo…nani asiyependa kuishi, hata
yule anayekusudia kujiua, muda roho ikitaka kutoka, huwa anajitahidi kuiondoa
ile kamba shingoni, lakini anakuwa keshachelewa, siku yake imeshafika, inabidi
aonje umauti…na jamani kutoka kwa roho sio kitu cha mchezo.
Katika kisa hiki utagundua kuwa kuna mwanamama hapo ambaye
ana jina hilo hilo, …jina ambalo nilisikia akiitwa huyu binti na mama yake
mdogo, wakati namuulizia kuhusu maisha yake, kwanini imetokea hivyo, sasa
tuendelee na kisa chetu, ………….
*********
‘Mimi sikujua kabisa huyo baba mlevi ninayeishi naye sio
baba yangu wa kunizaa, kumbe alikuwa ni baba wa kufikia, hayo niliyajua
baadaye, wakati najiandaa na safari ya kuja kuishi huku Dar, mji ambao kila
mmoja kule kijijini alitamani kuja kuishi.
Mama yangu aliniambia huyo baba ndiye aliyekuja kumuokoa
pale alipoachwa pale porini…..ili wenzake wafike huko wanapohitajika kwa wakati
muafaka, na baadaye watarejea kumchukua, au kumtafutia sehemu ya kumuhifadhi.
Wakati kaachwa pale, akiwa kachoka, kwani mwili ulikuwa
hauna nguvu, baada ya safari ndefu, baada ya mapigano, na yeye kujitolea
kumsaidia huyo jamaa aaliyeficha sura yake kwa kofia ya ngozi ….na haat
kujeruhiwa tena…akawa anatamani kulala tu.
‘Wewe pumzika hapa, na utakula nyama hii…mimi nahitaji huko
kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji
haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu walikuja kuniua, lakini tumeweza
kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka, halafu nitarudi kuhakikisha kuwa
upo mikono salama….’akasema.
‘Sawa wewe nenda tu, na nakutakia mafanikio mema, mungu yupo
pamoja na wewe, ila ninachokuomba ni kuhusu mtoto wangu…..naomba siku ukija,
uje na mtoto wangu, usije bila ya kuwa na mtoto wangu….’akasema huyo mwanamama.
‘Naahidi nitafanya hivyo…na wewe hakikisha unakuwa salama,
usiondoke, hapa, …hapa ni salama zaidi’akasema na akambusu kichwani na
kuondoka. Huyu mwanamama alikaa pale kwa muda, halafu akaona akatafute maji ya
kuoga, maji yaliyokuwepo pale yalikuwa ni machache, …
Alitoka pale akaanza kutembea huku na kule akitafuta maji,
akafika sehemu, na ghafla aaksikia kitu kama mchakato, mwili ukaanza
kusisimuka, akahisi kuna balaa…akageuka nyuma,….mungu wangu, akaduwaa,
akashikwa na ganzi, …simba, ambaye alikuwa kafunua domo lake akitoa sauti,
alikuwa kajeruhiwa, sauti iliyotoka hapo, ilimziba masikio, ……hakusubiri, ….hajawahi
kumuona huyu mnyama kwa karibu kiasi hicho, akageuka, ….kosa alilolifanya ni
hilo.
Alipogeuka, akaanza kukimbia, kumbe ni kosa, aheri
angelisimama, maana huyu mnyama alikuwa kajeruhiwa huko alipotoka,…na, alipona
hivyo, akaanza kumkimbilia, kwa vile alikuwa kajeruhiwa hata ukimbiaji wake,
ulikuwa ni wa kuchechemea,
Huyu mwanamke hakugeuka nyuma, kumbe hata hivyo huyo simba
alishamkaribia, akawa anajiandaa kumrukia, lakini akatulizwa na mshale mkubwa …..mshale ambao ulilenga shabaha yake
vyema na kuzama shingoni mwa huyo mnyama, mshale huo ulitupwa na kijana shupavu,
akitafuta ujasiri, wa mila zao, na yule simba akadondoka,
Yule mama alipogeuka kuangalia nyuma, akamkuta yule simba
kalala chini,..na mara akasikia watu wakishangilia, na mara kundi la watu wa
porini likatokea,..yule mama akaona kaokoka na simba sasa ataingia mikononi wa
wale watu waliotaka kumuua, akakimbia zaidi, alikimbia , akakimbia na kujikuta
ametoka nje kabisa ya ule msitu, akawa sehemu tambarare, na pale alipo alikuwa
kihema sana.
Kichwa kikawa kinamuuma, akawa hawezi hata kuhema,
akadondoka chini,…hakuweza kuinuka tena, akapoteza fahamu na alipozindukana
akajikuta yupo kwenye kibanda cha majani, kalala kwenye mkeka, na pembeni yake
yupo baba mmoja akiwa kakaa na watoto wake, wawili, ….na kitu kingine alicho
kihisi ni harufu kali ya pombe...
*******
Maisha yangu yalikuwa hivyo, kuokoka, au kuokolewa kiajabu
ajabu, ….akasema mama yangu.
‘Lakini mama hujanimaliza jinsi ilivyotokea huko porini, na
huko Mererani, umekimbilia mwishoni, ilikuwaje siku ile wakati watu
wanasubiria, …watu wanamsubiri mfalme kutokea?’ akauliza huyu binti, akimuuliza
mama yake.
Maua, kabla hatujafikia huko, tukarudi siku ile malikia
mtarajiwa alipojiwa na wageni, na wageni hawo walikuwa yule kijana wa mzee
mhasimu akiwa kaandamana na mkunga, mkunga ambaye ndiye aliyemzalisha yule mama
aliyetupwa ziwani ili aliwe na mamba. Mkunga huyu ndiye anayeaminika sana na
ukoo wa mzee mhasimu.
Malikia aliposikia hivyo kuwa wageni waliofika hapo ni
mkunga aliyemzalisha yule mama na kaja na yule mtoto mchanga, kumbukumbu zake
zilirejea nyuma, akakumbuka kauli ya mama wa huyo mtoto, kuwa ajitahidi sana
amlele mtoto wake. Kauli ile ilikuwa ikimuandama sana akilini mwake huyo
malikia, lakini kwa utaratibu ulivyo, yule mtoto hakutakiwa kulelewa na mtu
mwingine yoyote zaidi ya kulelewa na watu maalumu kwenye eneo wanalolitambua
kama sehemu takatifu.
Watu hawo ni waumini wa imani za hapo, wanalea hawo watoto,
waje kushika nafasi zao baadaye, wawe walimu, na wahudumu wa sehemu hiyo. Kwani
sehemu hiyo, licha ya kuwa ni sehemu ya utawala , lakini pia kuna mahakama,
kuna shule ya imani zao, na kuna sehemu maalumu ya kulea watoto wasio na wazazi
wao.
Ndio maana kila msimu, ni lazima kila mwanamchi apelike sadaka
huko....
Sadaka hizo za mavuno ziliweza kuwahudumia hawo watoto, walimu na wazee,
viongozi na shughuli ambazo zilihitaji vyakula. Kulikuwa na utaratibu ambao,
uliwawezesha watoto hawo, wasipate taabu, lakini mtoto bila mzazi wake, ni
kumnyima haki ya msingi, hasa ikizingatia kuwa mzazi yupo, au kazulimiwa ….
Malikia alisimama haraka na kuelekea chumba cha wageni, na
huko akamkuta kijana wa mzee hasimu, akiwa kasimama pembeni huku kambeba yule
mtoto, akamchekesha chekesha. Malikia akamwangalia na huku akiwaza mbali,
akiwazis siku ambayo nay eye atakuwa na mtoto kama huyo na baba yake awe
amempakata kama vile, anamchezea, akatabasamu.
Tabasamu lile lilitafsiriwa vinginevyo na wale waliokutwa
mle ndani, yaani yule mkunga na huyo kijana, wakijua mpango wao umefanikiwa, na
iliyobakia ni kusubiria siku hiyo ya kuapishwa mfalme, na kijana huyo atakuwa
mume halali wa huyo malikia.
‘Nashukuru kuwa umefika, pole sana na majukumu, na
mihangaiko ya hapa na pale, najua jinsi gani unavyotaabika, na nashangaa
kwanini wazee wa hapa hawataki kusema ukweli, ….’akasema huyo kijana wa mzee
hasimu.
‘Ukweli gani huo unaoutaka wewe, ambao hawajausema, hebu fikiria
kama wewe ungelikuwa katika nafasi yao ungelisema nini…je ungalikubali uvumi,
bila ushahidi,…ina maana wewe kama ungelikuwa mzazi ungelikubali tu, kuwa
mwanao kafa bila ya kuthibitisha,….hii ni kuonyesha jinsi gani, usivyokuwa na
hisia kwa watu wengine…’akasema malikia.
‘Sio kweli kuwa sina hisia na watu wengine, ningelikuwa
hivyo, nisingelikuja hapa tena, kuwa nawe karibu, kuja kukuambia ukweli, ili
usiszidi kuteseka, ..hawo wazee wa upande huu , ndio wasio kuwa na hisia za
watu wengine, kwanini waendelee kukutesa, wakati wanaujua ukweli’akasema huyoo
kijana.
‘Bado hujaniambia huo ukweli, ni upi, na una ushahidi gani?’
akauliza malikia huku akimwangali yule mtoto, ambaye alikuwa anafanana sawa
kabisa na mama yake.
‘Ukweli ni kuwa mume wako hayupo tena duniani, na
wanachotaka kufanya hawo wazee ni kupoteza muda, kwa ajili ya maslahi yao
binafsi. Kwa hli hiyo, wewe huoni kuwa wanachojali hapo ni maslahi yao kuliko
kujali hisia zako, hisia za jamii, ….je hawo wanakupenda kweli, je hawo wanafaa
kuwa watawala bora?’ akauliza huyo kijana.
‘Wewe una ushaidi gani kuwa mume wangu hayupo tena duniani?’
akauliza malikia.
‘Kwanza hawo walioandamana na yeye walisemaje,….walisema
kuwa mume wako kwa kujitia ujasiri, alizamia kwenye ziwa, akitaka kuokoa huo
mzigo uliozama, hebu fikiria , mtu hajali maisha yake, hajali kuwa nyuma kaacha
mke, kaacha majukumu, anazamia mzigo…mzigo unathamani gani mbele ya maisha
yake, mbele ya nyie aliowaacha huku nyuma…’akasema huyo kijana.
‘Je kuzamia huko ndio ushahidi wa kuwa alikufa, kuna wangapi
waliwahi kuzamia kwenye mazingira hayo, na bado wakawa hai….?’ Akauliza malikia.
‘Hivi wewe ulishawahi kukutana na mamba, akiwa na njaa,
ukumbuke kipindi kile, ni kipindi ambacho mamba ni wengi na wana njaa sana,
hakuna mifugo, na wengi wanategemea wanyama wanakuja kunywa maji mtoni, na
wanyama kipindi kama hicho ni adimu kweli….sasa mtu azamie akutane na hawo
mamba atoke mzima, haiwekani…’akasema huyo kijana.
‘Kuna ushahidi mwingine zaidi ya huo…?’a kauliza malikia.
‘Huo ni ushahidi mzito sana,….na kama angelikuwa hai, ….angelionekana
baadaye, wenzake walisubiria kipindi kirefu, na hawakumuona akiibukia sehemu
nyingine, na baadaye waliona moja ya vitu vyake alivyokuwa kavaa mwilini
vikielea ….hapo unataka kusema nini tena, na kama kweli yupo hai, kwanini
asionekane muda wote huo, ina maana hana mapenzi na wewe?’ akauliza huyo kijana
wa mzee hasimu.
‘Tatizo lenu, mnakimbilia hitimisho,….na hilo io jambo jema,
mikimbilia hitimsihao kwa vile mnaona litawasaidia nyie, …tafuteni ushahidi wa
kutosha, unahalalisha hilo hitimisho lenu,..ni waulize kwanin kabla ya yote
haya, kwanini msiombe uchunguzi wa pamoja, ili kuthibitisha hilo, kwanin
mnakimbilia kutaka madaraka….kutaka kunitoa mimi hapa?’ akauliza malikia.
‘Jamii yetu ina utaratibu, utaratibu huo uliasisiwa, na ndio
uliotufanya hadi tukafika hapa, ukumbuke jamii hizi zilipofika hapa kwa mara ya
kwanza, zilikuwa haziaminiani, zikawa na uhasama, kukawa na vita vya wenyewe
kwa wenyewe, na wenzetu wakaja wakasuluhisha, na kukaweka sheria za kulinda, …sheria
hizo zimesaidia kuiweka jamii hii katika mariziano…’akatulia huyo kijana,
halafu akamwangalia yule mtoto.
‘Tunataka sheria hizo ziweze kuwepo na kuwezesha vizazi hadi
vizazi kuishi kwa amani, na moja ya sheria hizo ni kuhakikisha utawala
unakuwepo..na kama kumetokea tatizo, kama la msiba, mmoja wa mtawala, au
mtarajiwa, kafariki, kuna kipengele cha jinsi gani, ya kufanya…
‘Unajua kunapotokea tatizo kama hili, watu wanataharuki, …na
kama hakuna utaratibu wa haraka wa kuweka mambo sawa, kunaweza kukatokea fujo,
kwahiyo wenzetu waliliona hilo, kuwa kama mtawala au mtarajiwa kafariki ni nini
kafanyike kwa haraka, na isizidi siku saba…kuwe na mtu anakaimu ile nafasi, ili
mambo yaendelee kama kawaida.
‘Na malikia hatakiwi awe anasononeka kwa muda mrefu, ujua
huku malikia ni mama wa jamii, kila mmoja anamtegemea yeye, sasa tukimuachia
akawa anasononeka kwa ajili ya mtu mmoja, je hawa wengine watahudumiwa na nani,
ukizingatia kuwa huduma hizo zinahitajika kila muda…ndio maana sisi tunaojua
sheria, tukalichukulia hilo kwa uzito wake’akasema huyo kijana.
Yule kijana akamchukua yule mtoto na kumuinua juu, na akawa
kama anamchekesha, akasema;
‘Mtoto huyu ni mzuri sana,…., na wapo wengine kule makaoni
kwao, hawajapata huduma , …hawajapata baraka zako, ukiuliza unaambiwa malikia
yupo kwenye mjonzi, …sasa huduma za watu kama hawa zinapatikana wapi, ndio
maana wenzetu waliliona hili, wakaona kuwa pindi ikitokea jambo kama hili
haraka, utaratibu unafuatiliwa na mambo yanakwenda kama kawaida’akasema huku
akimtizama huyo mtoto.
Malikia hapo akatulia, na kumwangalia yule mtoto kwa mbali,
na ilimsikitisha sana, aliposikia kuwa kuna watoto wengine, wanasubiri huduma
zake, na yeye amekuwa kikwazo,….akamsogelea yule mtoto, pale aliposimama huyo
kijana, na alimpokaribia akatulia, amgeukia yule mkunga, na kusema;
‘Nakuomba umchukua huyo mtoto’akasema na yule mkunga akasita
na kumwangalia yule kijana, ambaye alikuwa bado anamchezea yule mtoto kwa
kumshika vidole vyake vidogo, akasema
‘Sasa hivi ndio unaliona hilo…au kwa vile huyu mtoto ni mtoto
wa aliyekuwa rafiki yenu,….?’ Akauliza huku akiwa bado kamshikilia yule mtoto.
‘Ndio maana tumekuja naye, ili huruma ikujae, , kwani huenda
tungelikuja na mtoto mwingine usinglijali hilo’’akasema huyo kijana, na
malikia, akaenda na kumchukua yule mtoto mkononi mwa yule kijana na kwenda
kukaa naye karibu na yule mkunga.
‘Zaidi ya kupaat baraka, ana matatizo gani mengine, ….na
kuna watoto wangapi wanahitaji huduma zangu?’ akauliza
‘Matatizo yake makubwa, ni kulia….analia sana, lakini cha
ajabu tulipomfikisha hapa ametulia kabisa, utafikiri sio yeye, hii ni kuonyesha
kuwa alikuwa kihitaji huduma zako, na pili, anakuhitaji wewe kama mama, na
huenda anakuhitaji wewe zaidi, uwe naye karibu’akasema yule kijana, badala ya
kuonge ayule mkunga, yule mkunga akatikisa kichwa kukubaliana na hayo maelezo.
‘Kutokana na hayo, mimi nikawaona wazee, kuomba kibali chao,
kuwa huyu mtoto, anahitaji watu wa karibu, na mmoja wa watu ambao wanakubalika
ni mimi, nikaomba kuwa mimi niwe baba yake, …..wakakubali, lakini bado akawa
analia, …mimi nimeshakuwa baba yake, na anahitajika mama yake, na huyu mtoto
anakulilia wewe….baba yupo , mama yupo wapi’ akawa kama anauliza.
Malikia mtarajiwa akainua uso na kumwangalia yule kijana,
safari hii, akawa anaiona sura ya mume wake, hakujau ni kwanini…akatukisa
kichwa kuondoa ile taswira, na kugeuka haraka kumwangalia yule mtoto, akauliza;
‘Kwahiyo hata jina bado hajapatiwa?’ akauliza malikia.
Kijana yule akacheka na kusema; ‘unaona ulivyo…unasahau hata
majukumu yako, huyo angelipatiwa wapi jina wakati wewe upo na mambo yako….hamjali
jamii, mnajali ubinafsi,….huyo na watoto wengine bado hawajapata huduma yako,
ahwajapata majina..kwa sababu yenu,..je hili mtalisahihisha vipi, hasa kwa
wazee wenu, hawaoni kuwa wamekiuka sheria na katiba yetu, na mtu akikiuka
sheria na katiba yetu ni ni adhabu yake?’ akauliza huyo kijana.
‘Sheria na katiba haijavunjwa…tulikuwa katika kutafuta
ukweli, na kwa hili , nasikitika sana, kama nimekuwa kikwazo, na leo
nitajitahidi kuhakikisha kuwa natimiza wajibu wangu…’akasema malikia huku
akimshika yule mtoto kichwa.
‘Je na hilo na kuwa mimi ni baba yake, na kwasasa
anamuhitaji mama yake, unalionaje,….maana kwa vyovyote iwavyo, kesho ndio siku
ya mwisho siku ambayo, unahitaji kufika sehemu yako ya utawala, na huwezi
kufika hapo hadi uwe na mume…na …na kwa mapenzi yako kwa huyu mtoto, unatakiwa
unikubalie mimi kuwa mume wako’akasema kijana.
Malikia akaacha ile kazi aliyokuwa akitaka kuifanya na kusimama,
akamwangalia yule kijana, na mara ile sura ya mume wake ikawa anamzonga machoni
mwake, akatikisa kichwa na kujiuliza kwanini hali kama hiyo inamzinga machoni
mwake, akageuka na kuangalia kule alipokuwa yule mtoto, akasema;
‘Nakuomba tafadhali….utoke, ili niweze kutimiza wajibu wangu…’akasema
kwa sauti ya huzuni.
‘Vyovyote iwavyo….wewe kesho ni mke wangu, na inatakuwa kwa
furaha ya mtoto huyu, je unamtafutia jina gani, maana ..mtoto huyo ni mrembo, ….namfananisha
na ua …kama ura waridi,….au tumuiite ua waridi?’ akauliza yule kijana.
‘Ataitwa Maua….’akasema akikumbuka jina la mama wa huyo
mtoto.
NB: Niliona niiandike sehemu hii kabla ya kuendelea mbele
ili tuwekane sawa,
WAZO LA LEO: Tuweni
makini kwa dhamana za watu, kuna baadhi ya watu walikabidhiwa dhamana za watu
wengine, wakaahidi, na kwa bahati mbaya, huenda hawo watu ni marehemu kwa sasa,
na kwa tamaa zao, wamezitumia au hawakufuata jinsi walivyokubaliana na hawo
marehemu. Hilo kosa kubwa,…..dhamana ni deni, na kama usipotimiza ahadi yako
kwa huyo uliyemuahidi, deni hilo halifutiki hata kama mwenzako keshafariki, hadi
utimize ahadi yako mliokubaliana naye,.. kufa kwake, sio tija, timiza wajibu
wako, au fikisha ahadi hiyo kwa walengwa..tukumbuke kuwa ahadi ni deni.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
Hongera mkuu
Mmmhh ndugu wa mimi kazi nzuriiiii!!!!
Asante pia kwa Wazo la Leo;Pamoja DAIMA!!!!
Everything is very open with a precise explanation of the challenges.
It was definitely informative. Your site is very helpful.
Thank you for sharing!
Also visit my site :: Liver Active
Woω that wаѕ unusual. I juѕt wrоtе
an гeallу long commеnt but afteг Ӏ clickeԁ submit mу comment ԁidn't appear. Grrrr... well I'm not writing all that oveг agaіn.
Rеgаrdlеѕs, ϳust ωаntеd to say supеrb blοg!
Also visit my blog ; Capsiplex Reviews
Pretty component of content. I simply stumbled upon your weblog and
in accession capital to claim that I get actually loved account your blog posts.
Anyway I will be subscribing in your augment and even I success you get entry to persistently rapidly.
Also visit my weblog - wycieczka szkolna do krakowa
Post a Comment