Malaika wa Mererani kama anavyojulikana alikuwa kakaa kwenye,
kwenye chumba cha hoteli, huku kashika
shavu, alikaa vile kwa muda akiwa kajiinamia, akili ikiwa imetulia bila kuwaza
chochote, na baadaye, akageuka pembeni ambapo kulikuwa na simu yake , akaichukua
na kupiga namba, lakini ikawa haipatikani, ….
Alipojaribu tena mara mbili, bila kupata majibu, akasonya na
kuitupa ile simu kwenye kitanda, akasimama na kutembea hatua mbili mbele,
halafu akatulia, na kugeuka kuiangalia ile simu aliyotupia kitandani, akaifuata
tena,….akaichukua kwa haraka, na kutafuta namba nyingine.
‘Halloh, hebu niambie huyu Malaya ambaye ulimuona akiwa na
Adam, anaishi wapi, au ni hawa wanawake wa kuja toka huko kijijini?’ akauliza.
‘Huyo ni mgeni kabisa, hatujawahi kumuona mwanamke kama huyo
hapa Mererani, na inaonyesha ni wale wanawake wa kijijini haswa, tena sio
kijijini ni wa kutoka maporini,….kwani hata nguo, na mitindo ya kusuka, ni ya
wale watu wanaotoka huko ndani ndani, maporini’akaambiwa.
‘Kwahiyo ina maana huyo mwanamke alikutana naye huko
kijijini, akampa mimba, sasa ndio amakuja kuleta hiyo mimba kwa Adam, na ndio
maana kakimbilia kuja huku, …unasema keshajifungua, kwa gharama za Adam,…hiyo
ni pesa yangu inateketea tu…’akatulia kidogo, halafu akasema;
‘Hebu niambie ilikuwaje, mbona hamielezi kitu cha uhakika,
kwasaabbu sizani kama Adam ana mke, hajawahi kuniambia hivyo,….aliwahi kuniambia
kuwa alikuwa na rafiki wa kike, lakini familia ya hawo wanawake, wakawa
hawamtaki, na kama ingelikuwa ni yeye,…ningelijua, na huyo hawezi akawa hawo
watu wa maporini….sasa, ilikuwaje?’ akauliza.
‘Kwa undani sana sijui, kama unavyojua kuwa nay eye alikuwa
kajificha kwa ajili ya kuwakimbia askari, sasa gafla ndio nikasikia kaonekana
akiwa na mwanamke mwenye mtoto mchanga,..nikawauliza mrafiki zake,ndio
wakaniambia kuwa Adam, alijitolea tu kumsaidia huyo mwanamke’akasikia simu
ikisema.
‘Unaweza kuamini kitu kama hicho kweli, kuwa Adam, kageuka
msamaria mwema wa kusaidia wanawake asio wajua, kwa pesa gani aliyo nayo, ….Adam,
kapata wapi moyo wa kusaidia, mtu, ..hilo siamini, lazima kuna kitu hapo, …mimi
hili sijali hata akiwa na Malaya kibao, lakini kinachoniuma ni pesa
zangu..’akatulia kwa muda.
‘Sasa bosi tufanyeje?’ akaulizwa.
‘Cha kufanya kwa sasa….ni kumtafuta na kujua wapi alipo,
lakini muwe makini, maana polisi wanamtafuta, wakimkamata, alivyo, anaweza
kutuingiza hatiani,…’akasema na kusonya.
'Je mna uhakika yeye ndiye aliyemlipia huyo mwanamke gharama
zote?’ akauliza
‘Hilo hatuna uhakika maana hatujaonana naye tangu
alipoonekana na huyo mwanamke’akaambiwa.
‘Sasa mtafuteni, na mjue wapi walipo, au huyo mwanamke
anaishi wapi, nataka nikaonane na huyo
mwanamke uso kwa uso, ili anijue kuwa
mimi ni nani’akasema na huku akiwa kakunja ngumi.
‘Sawa bosi, tutamtafuta hawezi kujificha ndani ya mji huu,
bosi…’akaambiwa.
‘Na nyie msipompata, kazi hakuna….’akasema na kuitupa ile
simu kitandani tena akatulia na kurudi kukaa pale kwenye kiti chake, huku akiwa
kaangalia juu, safari hii alikuwa kashika kidevu, akayarudia yale maneno ya
mwisho ya yule mtu aliyempigia simu.
‘Bosi…bosi….bosi ...’ akasonya na kutulia, na mawazo yake
yakahama kutoka kwa Adam, na kuanza kuwaza tatizo alilo nalo ambalo limemfanya
hadi ajifungie mwenyewe kwenya kifungo cha hiari, akawaza jinsi gani atafanya
ili aweze kutoka humo,….
*******
Malikia amekuwa kajifungia kwenye hicho chumba kwa siku
nzima, hakutaka kutoka nje kabisa, kwani polisi walikuwa waklimtafuta, baada ya
kugundulikana kuwa yeye ndiye aliyewaajiri vijana kwa biashara hiyo na madawa
ya kuelevya. Hiyo sio mara ya kwanza kutokea jambo kama hilo, na kitu
alichokizoea. Kinachomsaidia ni kuwa kama kuna mpango maalumu wa kusakwa wauza
madawa ya kulevya, huwa ana watu wake wanaompa taarifa.
Siku hiyo alipopata taarifa, ndio siku alipopokea mzigio
mkubwa, na baada ya kuusambaza kwa mawakala, wake, ndio akapokea simu kutoka
kwa rafiki yake mmoja ndani ya polisi, ambaye alimpa taarifa kwamba kuna
operesheni maalumu ya kukakamata wauza madawa ya kulevya na akaambiwa nini cha
kufanya. Akakumbuka jinsi alivyoambiwa;
‘Nakupa taariha hii muhimu, kuwa kuna opereshemi maalumu ya
kamata kamata, wauza madawa ya kulevya, na safari hii wameagiza vijana wageni
kabisa, ambao sio rahisi kuwafahamu….’akaambiwa.
‘Sasa nifanyeje, maana kila siku nawapatia mshiko wenu,
kwanini safari hii iwe hivyo, au hamjamkatia jamaa yetu fungu lake?’ akauliza.
‘Hilo ni jambo la kawaida ni moja ya operesheni zetu, cha
muhimu ni wewe kuhakikisha huonekani kabisa,..’akaambiwa.
‘Yaani nijifunge mwenyewe, haiwezekani,…unajua kuna mzigo
mkubwa, nispousimamia hawa watu wangu wanaweza wakanizika….’akalalamika.
‘Inabidi iwe hivyo, mpendwa, hali sio shwari,…kama
inawezekana nenda kijijini kakae kwa muda, kukipoa ndio urajee’akaambiwa.
‘Niende kijijini, na huo mzigo, itakuwaje,…ndio nimeusamabza
hata senti moja sijashika….hilo haliwezekani’akasema huku akikunja uso kwa
hasira.
‘Basi tafuta chumba, jifiche, sehemu ambayo hakuna mtu
anayepajua, na usitoke kabisa, sisi huku tutajua jinsi gani ya kutuliza hili
jambo, kinamna..unasikia usitoke kabisa..’akaambiwa.
‘Nikifanya hivyo nitakusanya je pesa zangu, hamjui mshahara
wenu unatoka wapi, ..’akasema kwa hasira.
‘Sikiliza mpendwa, anayeongoza hicho kikosi ni afande
Komando..’akasema na Malikia akashituka kama vile kashituliwa na umeme, akasema
kwa sauti ya wasiwasi.
‘Unasema huyo mwanaume mwenye sura mbaya karudishwa tena
hapa…mungu wangu, …’akasema huku akiangalia huku na kule, kama vile anaogopa
kuwa huyo Komando atatokea muda wowote hapo alipo.Kwa muda hup alikuwa kavalia kikazi, makoti na nguo ambazo huwezi kumzania kabisa anafanya shughuli kama hiyo.
‘Kama ni huyo mtu, nitatafuta chumba ambacho hakijulikani
kabisa…mungu wangu, siwezi kwenda jela tena’akasema huku akiangalia huku na
kule.
‘Kama utafuta ninavyokuagiza, hawezi kukuona, hawezi akazunguka
kile hoteli, …na ikibidi tafuta hoteli za vichochoroni, au nyumba ambayo mtu
hawezi kuhisi kuwa unaishi…kama unavyomjua huyu jamaa ananusa kama mbwa, sasa
ni vizuri ukawa makini…..ukiona ishara yangu ujua yupo nyuma yako, …’akaambiwa.
‘Sawa, nitapambana naye, namuogoap kwa vile alishawahi
kuniweka ndani, lakini safari hii tutakua naye sahani moja, na ikibidi
…..anaweza akatangulia’akasema na kukumbuka jinsi gani alivyoweza kukamatwa na
huyo askari.
Siku zote anapokamatwa huwa ana mbinu nyingi za kupambana na
askari wa hapo na wote anawafahamu vyema, anaweza akatumia pesa au akatumia urembo wake, lakini kwa huyu askari,
ilishindikana, na akajikuta akiswekwa ndani, na kama isingelikuwa ukaribu wake
na wakubwa wengine, angelifungwa muda mrefu, lakini huyo jamaa alipohamishwa
hapo, akafanya mipango akatolewa.
‘Huyu mtu nina kisasi nay eye…’akasema kimoyo moyo. Lakini
ni nani atanisaidia kwa kazi hii, maana kama huyu jamaa yupo, lazima nilipize
kisasai, hawezi kunizalilisha kiasi hiki, mimi malikia wa Mererani, nisweke
ndani, na nizalilishwe na wafungwa…hapana, lazima nimuonyeshe kuwa mimi sio
moto wa karibu.
`Nitahakikisha safai hii, anatangulia kuzimu…….’akasema huku
akiwa nani anaweza kumtumia kwa kazi hiyo, anajua vijana wake wote wanamuogopa
sana huyo askari, na hapo akakumbuka, kuwa Adam hamjui huyo askari, anaweza
kumtumua kuifanya hiyo kazi. Lakini Adam hajawa jasiri wa kuweza kuifanya hiyo
kazi, na hata hivyo, badi mi mzembe, ….
‘Hata hivyo ninaweza kumkamatisha tu, lakini sasa ndio yupo
na huyo Malaya wake, sijui nitampata wapi?’ akajiuliza
Akakuna kichwa, akijilaumu, kwanini alimuamini huyu Adam,
tangu amuingize kwenye shughuli zake, amekuwa ni tatizo, na badala ya kumletea
faida imekuwa ni hasara, imebidi atumie pesa nyingi kumuokoa na hata kumshikia
dhamana….
‘Huyu mwanaume ana bahati sana, yaani namlea kama….nini
sijui, hata siwezi kujua jinsi gani ninavyomthamini, kama vile mume wangu,
ajabiu kabisa, sijawahi kufanya hivi katika maisha yangu, lakini ndio huyo
anataka kunitosa.
‘Kwanza hivi anajiona ana nini cha maana, …huyu mtu ana bahati
sana, hajui kuwa mimi sina mapenzi na mtu mzigo, mtu asiyena faida, kama
isingelikuwa huyo mjomba wake, kwa vile nilitaka nimtumie ili nimuingie mjomba
wake, nisingelimuingiza kwenye anag zangu...Lakini sasa nanona muda umefika,
nitamtumia yeye,….siku zake zimefika, …’akasema huku akikuna kichwa.
‘Huyu mjomba bado sijamweka mikononi, na ili nimuweke
mikononi nilitakiwa nimtumie huyo mwanaume, lakini mtu mwenyewe haelekei, sasa
nifanyeje, ..’akawa aongea peke yake kama vile kachanganyikiwa.
‘Sasa tena hii habari ya kuwa na mwanamke mwenye kichanga,
mbona huu sasa ni mzigo, maana hataweza kutulia kwenye kazi, …mimi siwezi,
..siwezi kabisa kulea mwanamke na mtoto mchanga…kwanza lazima nijua huyu
mwanamke ni nani? Nikimpata nitahakikisha namtolea hasira zangu zote’akasema
huku akijaribu kufumba macho.
`Kwa mtaji huu, lazima nitoke humu, …’ akasema na kuanza
kutafuta nguo na nywele za bandia za kujibadili, …Lakini akili yake ilikuwa
ikimuwaza huyo Komandoo, anamjau vyema, hata ujibadili vipi, kama akikamia kukukamata
atakupata tu, ….ananusa kama mbwa…..
Akajiweka sawa kutaka kutoka, na kabla hajainua mguu
kusogelea mlango, akasikia mlango ukigongwa, moyo ukaanza kwenda mbio,..mwili
ukamsisimuka…akaangalia huku na kule,……..mlango uliopo ni mmoja tu, dirishani
huwezi kutokea,…..akaangalia mvunguni, kama anaweza kuiingia, na hapo
akakumbuka mzigo aliouficha mvunguni…
Mlango ukagongwa tena….
NB Nipo internet cafe, ...
WAZO LA LEO :Maisha ni kupambana ili upate mkate wako wa kila siku, ukikosa leo, usikate tamaa.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Mbona kimiya mkuu
Post a Comment