Kais, aliona ajabu sana, kwake ilikuwa kama vile anaangalia sinema
ya ukweli, jinsi gani yule mwanaume alivyojitosa kuokoa maisha ya mtu mwingine,
bila kujali kuwa yeye mwenyewe anajiingiza kwenye hatari, kwani kwa muda huo
mamba wengine walishajitokeza, na kila mmoja akijaribu kuruka ili awahi kumnyakua
yule mwanamke, wakiwa wamepanua midomo yao na kuonyesha meno yao makali.
Yule mwanaume alijirusha kama wanavyoruka magolikipa kudaka
mpira, na mruko ule alitua juu yam domo wa yule mamba, akaukanyaga kwa juu, na
huku mikono yake ikiwa inamuwahi yule mwanamke kumsukuma mbali na ule mdomo wa
mamba, uliokwisha panuliwa,na kwa haraka ya ajabu akajipinda, ili kuweza
kumuinua yule mwanamke.Yote hayo yalifanyika karibu na ule mdomo wa mamba.
Nafikiri yule mamba alishikwa na butwaa maana alishajiandaa
kuweka kitoweo mdomoni,lakini ghafla kimeondolewa kwa haraka, na huyo mwanamke
akarushwa kwa mbele, na kwa vile isingeluwa rahisi kufanya mtendo hayo kwa
haraka, na kwa wakati mmoja, mamba akabahatika kumdaka yule mwanaume mguu wake.
Ilikuwa sasa ni vuta ni kuvute, Kais alipoona hivyo, akajua
na yeye hapo anahitajika kutoa msaada, licha ya kuwa nay eye huenda anajiingiza
kwenye hatari, lakini akaona ajaribu bahati yake. Maisha ya kuishi porini peke
yake yalishamjengea ujasiri, na moyoni alimshukuru bibi yake aliyemlea kwenye
mazingira ya kuweza kusihi katika halii yoyote ile.
Alichofanya pale ni kuangali huku na kule, na kwa bahati
nzuri, karibu yake kulikuwa na tawi la mti, wenye mwiba, lililovunjika,
akalichukua na kukimbilia pale ufukweni, na kwa haraka akalichomeka, kweney ule
mdomo wa mamba uliokuwa umefunuka kidogo, ukiwa umeshikilia mguu wa yule
mwanaume. Aliweza kuupenyesh ule mti wenye mwiba, mdomoni mwa yule mamba huku
akiaangalia wale mamba wengine wasije wakamrukia.
Naona ni kwa mipango
ya umngu, maana kutokana na ile mimba ule mtu aliouchomeka mdomoni wa yule
mamba, yule mamba akihisi maumivu, akapanua domi lake zaidi na ndipo yule
mwanaume akaweza kuvuta mguu wake.
Yule mwanaume, akajikokota hadi kwa yule mwanamke, na
kumuinua akaanza kutembea naye kwenda mbali na ule mto, bila kujali kuwa
kajeruhiwa, bila kumjali yule aliyemsaidia kumuokoa, alichokuwa akihangaika
nacho ni yule mwanamke ambaye kwa muda huo alikuwa kaduwaa tu akishangaa kuona
yale yanayotokea.
Kais, akawafuatilia kwa nyuma, huku akiangaza huku na kule,
kuona kama kweli kuna usalama, na kuhakikisha kuwa hakuna watu wengine, asije
akaingia mikononi mwa maadui, na alipohakikisha hilo, akawafuata hawo watu wawili
hadi sehemu ambayo ilikuwa mbali na ule mto, na ilionekana ndio kutakuwa makao
yao ya muda.
‘Umaumia sana, ni bora kwanza tukatibu hayo majeraha ya meno
ya mamba, yanaweza kukuleta madhara..mguu unaweza ukaoza’akasema Kais. Yule
mwanaume kwanza alitupa jicho kwa Kais, lakini kwa vile lile kofia lilificha
kilakitu usoni mwake, Kais hakuweza kumtambua vyema.
Yule mwanaume akaangalia mguu wake, na ndipo akagundua kuwa
kweli kaumia, na anahitaji matibabu, akainuka kwa shida na kuanza kuangali huku
na kule, kutafuta dawa za majani.Ilionekana kuwa ni mtaalamu, kwani aligundua
aina ya majani, na kuna dawa alikuwa nazo, akayatafuna yale majani na
kuchanganya na ile dawa, akaanza kujiganga mwenyewe.
Kais aliona jinsi gani, yule mwanaume anavyopata taabu
kuyaweka yale majani kwenye yale majeraha yake, akamsogelea na kuyachukua yale
majani na kuanza kumsaidia kuyaweka kwenye yale majeraha yaliyosabaishwa na meno
ya mamba. Na wakati anafanya hivyo, akawa mara kwa mara anajiiba kumwangalia
yule mwanaume, hakuweza kuiona sura ya yule mwanaume vyema zaidi ya macho
yaliyopo kwenye matundu ya lile likofia alilovyaa, lile likofia lilikuwa na
sehem ndogoo ya matundu ya macho mdomo, na puani, na huenda huyu jamaa alifanya
hivyo kwa sababu maalumu.
Kila alipotupa jicho, alikutana na macho ya yule jamaa
akimwangalia, na alihisi tabasamu au hali fulani ambayo hakuweza kuigundua.
Alipohakikisha kuwa keshamweka majani na ile dawa kwenye yale majeraha, na kuyafunga vyema kwa
kamba ya mti, akajiinua na kutaka kusogea pembeni, na katika kutaka kusogea
kule akawa kajikwaa na kutaka kudondoka.
Yule mwanaume, ambaye kwa muda ule alikuwa akigugumia kwa
amuimvu, maana ile dawa huvuta sumu iliyoingia mwilini, na ilitakiwa iwe hivyo,
ili sumu yote iliyotokana na yale meno machafu ya mamba itoke mwilini,vinginevyo mguu huo ungeliweza
kuoza.Na dawa hiyo ikifanya kazi, kuna maumivu makali sana unayapa, na
inatakiwa ujasiri wa hali ya juu kuvumilia, na mara nyingie mtu akifungwa hizo
dawa,anatakiwa awe amefungwa mikono na miguu, ili asiweza kuiondoa ile dawa.
Kais alipojikwaa, akawa anaserereka kuanguka, yule mwanaume
bila kujali yale maumivu anayopambana nayo akainuka, na kwa haraka akafika na
kumdaka Kais, na Kais akawa kalalia mguu wa yule mwanaume,na akawa kama
anaangalia juu, macho yake yakawa yamatizama moja kwa moja yule mwanaume..aliona
macho kupitia kwenye matundu ya ile kofia.
Yule mwanaume akawa anahangaika kumweka sawa, huku
akitaabika na maumivu. Kwa Kais muda huo alishasahau kuwa mwenzake yupo kwenye
matseo ya mauimvu, na mguu mmoja hauna nguvu, kwahiyo alitakiwa ajitahidi
ainuke kwa haraka, ili kumuokoa mwenzake kutokana na yale maumivu, lakini
alijikuta akijilegeza ili tu apate mwanya wa kuyaangalia yale macho, na
kutamani kama ingeliwezekana angelifikia lile kofia na kuliondoa, ili aione
sura ya huyo mtu….
Kais, alihisi aina ya mvuto fulani, nafsini mwake, ni kama
vile anamjua huyo mwanaume,ni kama vile amempenda kwa muda huo mfupi, hata kama
hamjui, lakini itakuwaje kupenda mtu usiyemjua, na utampendaje ilihali uso
hauonekani, akajiuliza bila kupata jibu….hisia na nafsi ikawa inatamani kama
ingeliwezekana awe karibu yake hivyo hivyo.
‘Aaah,samahani ,nimesahau kuwa wewe ni mgonjwa…’akasema
Kais, na kujikakamua kujinua kwenye miguu ya yule jamaa, ambaye alishazidiwa na
kujaribu kumweka Kais chini ili aweze kujituliza, na katika harakati hizo,
akawa kazidiwa na kujilaza chini huku akikunja uso kwa maumivu makali. Na muda
huo Kais alikuwa kalala kwenye paja la yule mwanaume, na ndipo Kais akagundua
kosa lake na kusema hivyo.
‘Unisamehe, maana haya maumivu, …aaah, ni makali kweli sijui kama nitaweza kuyavumilia,….’akawa
analalamika yule mwanaume na kwa muda huo akawa anaipeleka mikono yake kutaka
kuindoa ile dawa. Kais alipoona hivyo, akajua hapo asipofanya juhudi ya ziada,
huyo mwanaume mguu utaoza na utaishiwa kukatwa. Akaona ajitolee kwa kile
kinachowezekana, na akitumia ujasiri, wa hadithii za bibi, akajitolea bila
kujali hali yake aliyokuwa nayo.
‘Utanisamehe, inabidi nifanya hivi ili kukusaidia….’akasema
huku akamsogelea yule mwanaume na kumshika mikono yake yote miwili kwa mbele,
na kwa kufanya hivyo, wakawa wamelaliana, Kais akiwajuu ya kifua cha huyo
mwanaume ili kuweza kuzuia ile mikono isifike miguuni, huku kaishikilia mikono
ya yule mwanaume mbali kabisa na kichwa, ilibidi atumie nguvu zake zote ili
aweze kumzidi yule mwanaume , na hiyo ilisadia , kwani yule mwanaume kila
alipojaribu kuinua mikono yake, alishindwa, na hata alipofanikiwa kumzidi
nguvu
Kais, alijikuta mikono yake ikimshika mwili wa Kais, na akimshika,
anatahayari, na kurudisha mikono yake.
Hali ile iliendelea, hadi muda ukapita sana, na dawa ikawa
imefanya kazi yake,na maumivu yakaanza kuisha kidogokidogo na taratibu, hadi maumivu
yakaisha kabisa. Na wawili hawa wakawa wametulia, huku Kais akiwa bado kifuani
mwa huyu mwanaume, kalowana mijasho, na sasa kilichokuwa kikifanya kazi ni
hisia za miili yao ambayo imekuwa imeshikana na kunataka kwa muda mrefu.
Mungu alipoumba mume na mke, aliwajenga kama sumaku, kama
mmoja akiwa karibu na mwenzake kwa muda mrefu kuna hali ya mvutano inaweza
kuwashika, na hasa ikiwa watu hawo hawana udugu wa karibu, na zaidi watu hawa
wawe na hisia za namna ya kupendana, au kutaka kupendana.
Kwa ujumla hali hii ilimuathiri zaidi Kais,na ikizingatiwa
kuwa yeye amekuwa porini kwa muda mrefu peke yake, akajikuta mwili wake wote
ukilegea, na akajikuta akivutika na hisia za mwili wake na kufanya kile
asichokitegemea, licha ya kuwa mwenzake alijaribu kujizuia, lakini mwishowe nay
eye akajikuta akivutika kufanya kile mwenzake alichokiwa akikitaka.
Kilichokuja kuwashitua ni kikohozi,…na wote wakageuza vichwa
vyao kutizama ni nani huyoo aliyewavurugia maisha ya dunia nyingine, maisha
ambayo mungu mwenyewe anajua kwanini aliyaweka hivyo, kwani binadamu akiingia kwenye
hisia za dunia hiyo ya hisia, anakuwa hajijui tena, na akirudi kwenye maisha ya kawaida, huanza
kujijutia, na wengine hata kulaani kuwa kwanini wamerudi kwenye dunia hiyo ya
kawaida.
‘Oooh,…’akasema yule mwanaume na kuinuka sehemu ya kichwani
na kukaa kwa haraka, hakuweza kusimama, kwani Kais alikwa nusu kamlalia,na
alipogundua nini alichofanya akawa katahayari, akajifuta mchanga kwa haraka
huku akiangalia kule kikohozi kilipotokea, akagundua wajibu wake, na
alichofanya na kumuinua Kais ambaye alishazama kwenye kausingizi na kumlaza
chini na wakati anafanya hivyo, akawa anamuangalia usoni, na baadaye akasema;.
‘Unanikumbusha mbali kweli wewe binti….’aliyatamka hayo
maneno kwa taratibu,pengine akijua kuwa Kais kalala hatayasikia hayo maneno, na
hata kabla Kais hajafungua macho yake kumtizama huyo aliyetamka hayo maneno,
yule mwanaume akawa keshageuka na kuondoka kuelekea kule kwa yule mwanamke
mwingine ambaye ndiye aliyekohoa na kuwazindua toka kwenye dunia ile ya hisia.
Na huku nyuma, Kais, alikuwa
kama yupo kwenye njozi, kwani sauti ile ilipenya kwenye ubibgo wake, na
kumkumbusha mbali. Alikumbuka, kuna mtu alikuwa na sauti kama hiyo hiyo, na
alikuwa mtu wa karibu, lakini hakuweza kumchanganua na kumtambua alikuwa nani.
Akafungua macho yake na kuanza kuwaza yupo wapi.
Akili ilipokaa sawa,
akabakia kuwaza, hii sauti aliwahi kuisikia wapi, licha ya kuwa haisikiki
vyema kwa jinsi alivyoiskia. Lakini myoni, aliingiwa na shauku kubwa ,
kumgundua huyu mwanaume ni nani, lakini angelimgundua vipi, wakati kava hiyo
kofia ya ngozi, iliyofunika, uso wote, na kuacha vitundu kwenye macho,
masikio,na pua yake. Kukaa kwake porini mwenyewe kwa miezi mingi, alishaanza
kujijenge hisia za kiporini, na kuanza kuondoa kumbukumbuu za maisha ya kawaida,
lakini hiyo sauti alihisi aliwahi kuisikia kabla, na sauti hiyo ilizindua hisia
zake nyingine, na badala ya kujutia lile tendo alilolifanya kwa muda mchache
uliopita, akawa anatamani lijirudie tena.
‘Kwani wewe ni nani, na kwanini huvui hilo kofia lako?’
akauliza Kais akiwa amekaa pale alipokuwa amelele, huku akimwangalia yule
mwanaume.
‘Siwezi kulivua kwasababu za kiuslama,na ni bora usinijue
kabisa kuwa mimi ni nani,….’yule mwanaume akasema, na kwa vile lile kofia
limembana sana mdomoni , sauti yake ilikuwa haitoki vyema.
‘Kwanini hutaki nikujue wakati inaonyesha sisi ni marafiki,
wewe ni mtu mwema, …’akasema Kais.
‘Mimi nionavyo rafiki yako wa kiukweli, ni huyo
aliyekubebesha huo uja uzito ulio nao….najua anakupenda sana,na wewe unampenda
sana…’akasema huyo mwanaume, na kauli ile iliashiria hali ya wivu, lakini Kais
hakuwa na uhakika na hilo akatulia huku akimwangalia huyo mwanaume.
‘Wewe hujui ni nini imetokea juu yangu, kama….’akakatisha
maneno yake na kumwangalia huyo mwanaume, ambaye aligeuka na kuangalia upande
mwingine, inaonyesha alikuwa akiwaza jambo, akasema kwa sauto ile ile
isiyosikika vyema;
‘Nahisi hilo ulilofanyiwa ni dhuluma tu za dunia, nahisi
ndio maana umetengana na huyo mwanaume aliyekupa huo uja uzito, labda
nikuulize, ni nani mwenye huo ujauzito ulio nao, na kwanini upo huku kwenye
kisiwa hiki cha umauti?’ huyo mwanaume akauliza.
‘Unavyoongea inaonyesha kama vile unajua ni nini kimetokea
juu yangu ….niembie ukweli wewe ni nani, maana kama unajua ni nini kilitokea,
ni heri ni kukimbie, maana mimi siruhusiwi kukutana na watu wangu tena,
nimeshatengwa na jamii, mimi nastahili kuwa mfu, kuwa chakula cha chatu na
mijoka…ndio maana nimetupwa huku kwenye kisiwa cha umauiti’akasema Kais.
‘Usilazimishe kile kisichowezekana, niamini mimi kuwa hili
ninalolifanya ni kwa manufaa yenu,…ila kwa uwoni wangu , ingawaje sijui nini
kilitokea juu yako, lakini nahisi sio sahihi kupewa hiyo adhabu,nafikiri,
waliokufanyia hivyo, wamefanya hayo kwa dhuluma tu, sizani msichana mrembo kama wewe
ulistahili kufanyiwa hayo uliyofanyiwa, sijui umefanya kosa gani kustahili
mateso kama hayo, na nashukuru mungu kuwa bado upo hai, na naahidi nitawalinda
hadi nihakikishe mpo kwenye mikono salama..’akasema huyo mwanaume kwa sauti ya
kukatika katika kutokana na lile likofia alilovaa.
Kais akainuka, na lengo lake lilikuwa kufanya juhudi hadi
huyo mwanaume aliondoe lile kofia kichwani, lakini alipowaza sana, akaona haina
haja,….akasema;
‘Toka lini haki, na upendo, vikatwala hii dunia,mimi tangu
nizaliwe, naiona hii dunia kama ni sehemu ya wale wenye uwezo, ambao wana haki
ya kuwatendea wapendavyoo wale wasio na uwezo. Wao wamejiona ni haki yao
kufanya hivyo, na wana haki ya kuishi kwa raha,…..hata hawana huruma na wenzao
ambao wanaishi maisha ya dhiki, taabu na mashaka…’akasema Kais.
‘Hilo usemalo sio kweli, kuwa dunia hii ni ya kudhulumiana,
kiukweli dunia hii ni sehemu ya raha, kupendana na kusadiana, ndivyo muumba
alivyotupangia tuwe hivyo, tatizo niubinafsi na uchoyo wa nafsi zetu. Kama kila
mtu angejenga upendo kwa mwenzake, akamhurumia binadamu mwenzake, mbona dunia
hii haina shida. Utajiri na mali asili zilizopo hapa duniani zinamtosha kila
mtu aishi kwa raha, lakini wachache wenye uwezo wameamua kujilimbikizia wao
wenyewe…’akasema yule mwanaume.
Kais, alitamani yule mwanaume aendelee kuongea hivyo hivyo,
utamu wa yale maneno, ulimuingia akilini na kumsisimua, na hapo alipo alitamani
kuwa karibu na huyu mwanaume na kama inawezekana awe hivyoo hivyo maisha yake
yote, lakini akajua kuwa huyo mtu huenda ni miongoni mwa watu wanaomjua, na
akiondoka hapo huenda akaenda kutoa taarifa kwa yule mzee anye mchukia kila
wazee wote duniani,na kijua kuwa bado yupo hai, atahakikisha kuwa anatupiwa
kwenye mamba wamtafune baada ya yeye kujifungua.
‘Mimi najua wengine hatuna haki kwenye hii dunia, juhudi
zote nilizozifanya zilinifikisha hapa nilipo, na hata wale niliowasaidia
sijawaona wakija kuniokoa, wao wameshafanikiwa najua wapo kwenye raha zao.Na
hawa walionifanyia hivi wameshajua kuwa mimi nipo tumboni mwa mijoka, nashukuru
kuwa bado nipo hai, lakini….’akatulia Kais na kumwangalia yule mwanamke ambaye
kwa muda huo alikuwa bado amelala.
Alikuwa hajajiwa na hilo wazo kabla, na hilo wazo lilipomjia
akilini akashituka na kuanza kuoana aibua, akatahayari, na kuhuzunika, akajikuta
akijuta, alijutia lile tendo alilolifanya muda mchache uliopita, na alijua ni
kosa lake, kama asingelimlazimisha yule mwanaume kwa kutumia hali aliyokuwa
nayo ya kupambana na yale maumivu, huenda huyo mwanaume asingeliweza kufanya
hayo waliyoyafanya na kufuta matakwa ya nafsi zao,….akahisi kutenda dhambi
kubwa sana, akamgeukia yule mwanaume, halafu akamwangalia yule mwanamke, ambaye
bado alikuwa kalala na kwa huzuni akauliza.
‘Huyo ni mwanamke ni
mke wako,kwanini mumekuja maeneo haya mabaya, maeneo ya gizani, huku wanaishi
watu wasiojua ubinadamu, maisha yao yapo gizani, yametawaliwa na mambo ya kale,
na zaidi mumekuja huku kwenye kisiwa cha umauti kwanini mumefanya hivyo,
usiniambie kuwa na nyie mumehukumiwa kama mimi…?’akasema Kais, huku akimwangalia
yule mwanaume,licha ya kuwa nguo alizovyaa ni kama wanazovaa wanaume wa huko anapotoka
yeye, lakini alimuona kama mtu tofauti na tabia yake ni tofauti na wanaume wa
huko kwao.
‘Huyo sio mke wangu…ila nimejitolea kumsaidia, huenda
nisingelifanya hivyo, ningelijutia maisha yangu yote, lakini naomba
tusiliongelee hili kwasababu za msingi..kwanza tuangalieni jinsi gani
tutaondoka hapa’akasema huyo mwanaume.
‘Kwenda wapi, mimi sirudi huko nilipotolewa,mimi nilishahukumiwa
kufa, sasa unataka nirudi tena huko,hilo haliwezekani, kama ni kuondoka
ondokeni nyie wawili, maana hawo watu wanguwakiniona najua nitakuwa chakula cha
mamba’akasema Kais.
‘Kama ni hivyo,…. mimi nitawatafutia sehemu tofauti na hiyo,
na ndio lengo langu kwa huyo mwanamke unyemuona hapo, kwani na yeye kanusirika
kufa huenda kwa mambo kama hayo yako, na ninachotaka kukifanya nikumpeleka
mbali kabisa na hiii jamii, ili mimi nirudi hukoo nilipotoka’akasema huyo
mwanaume.
‘Kwani huyo mwanamke umemtoa wapi, nakwanini umeamua
kumsaidia na wewe kwenu ni wapi?’ akauliza Kais.
‘Nimekuambia kuwa sitaweza kukujibu hayo maswali yako, na siwezi
kabisa kukusimulia hayo, kwasababu ya usalama wake, na pengine wa kwako pia, ni bora hata wewe usihangaika kuyatafuta hayo
yaliyotakiwa kumkukuta huyo mwanamke, yachukulie tu kama ni dhuluma za wanadamu
wengine wanaojali nafsi na tamaa zao..’akasema huyo mwanaume.
‘Kwa tabia hiyo lini dunia hii itakuwa na amani,maana kama
kafanyiwa hivyo, kuna jamaa zake wanaompenda, na huenda atakuwa na mtoto, huyo
mtoto akisimulia alivyofanyiwa mama yake, atajenga kisasi, chuki na hawo
waliomfanyai hivyo. Na hata kama huyo
mtoto au jamii yako haitaweza kuwaona waliofanya hivyo, lakini kihisia watu waliotendewa
hivyo huwa na kinyongo, na wakibahatika kuwaona watu wenye tabia kama za hawo
waliowafanyia hivyo hasira za visasi hutawala nafsi zao…’akasema Kais.
‘Ni kweli, hayo yapo, na tunahitajika kubadili huo
mtizamo,na wa kuibadili hiyo tabia ni mimi na wewe, kila mmoja kwa nafasi yake.
Kwanza cha muhimu ni kujenga upendo,bila kujali huyu ni nani. Kusaidiana kwa
hali na mali, na unaweza kumsaidia mwenzako bila kujali huyo unayemsaidia
atakupa nini…nikiwa na maana umpende jirani yako, kama unavyoipenda nafsi yako,
tukiwa hivyo, basi mbona dunia hii haina shida…’akasema huyo mwanaume.
‘Mbona unapenda kutamka hilo neno,….`haina shida..’
unanikumbusha zamani nilikuwa na rafiki yangu mmoja, lakini keshaoa,…nilimpenda
sana, lakini tofauti za kibinadamu, tofauti na sheria za ajabu ajabu, zikanifanya
nishindwe kuwa naye, na nilimuona kama mbadili wa mwanaume mwingine niliyempnda
kabla yake na kwa vile ni wa ukoo wetu niliwza juwa huenda naweza kuolewa
naye…lakini haikufanikiwa’akasema Kais.
Yule mwanaume akatulia kwa muda kama anawaza jambo halafu
akasema kwa taratibu kama vile anawaza
hilo analoliuza asiliulize kwa namna ambayo inaweza kuharibu jambo,
akasema;
‘Kwahiyo ulikuwa na wanaume wawili, wote unawapenda, sasa
nikuulize swali, samhani kwa kuuliza hilo swali,….’akatulia.
‘Wewe uliza tu, usiogope, ….’akasema huyo Kais.
‘Kati ya hawo wawili ni nanii uliyempenda zaidi,huyo wa uko
wenu auu huyo mwanume mwingine ambaye umemuelezea?’ akaulizwa.
‘Kupenda ni kitu cha ajabu sana, nilipogundua kuwa huyo
mwanaume wa ukoo wetu sitaweza kumpata, nafsi yangu ikafa ganzi, utapendaje
kusipopendeka?. Kwa bahati nzuri ndipo nikakutana na huyo mwanaume mwingine,
niligundua kuwa na yeye nimempenda, naye akaonyesha kunipenda pia na anaweza
akawa mume wangu…lakini haikuwa rahisi, kwa mnyonge hakuna kitu rahisi, kwa
fukara siku zote ni taabu tu, hata pendo kwake ni shida, ….kwa kifupi wote
niliwapenda wote, lakini kila mmoja kwa nafasi yake…’akasema Kais.
‘Kwa mfano wangetokea wote wawili ukaambiwa umchague
yupokati ya hawo wawili ungemchagua nani?’akaulizwa.
‘Hilo swali ni gumu kujibu,….kwani sisi wanawake tuna mengi
tunayoangalia kwa mwanaume, na jinsi tulivyoumbwa tunaweza kubadilika kama kinyonga…wote
nawapenda, ila nitampenda yule ambaye atakuwa karibu nami, na akawa ananipenda
kwa vyovyote vile. …ila kama nitakuwa nimeshaolewa na mmojawapo, na tukawa
hatuna kipingamizi tena, mwingine hatakuwa na nafasi kwangu…’akasema Kais.
‘Je uliwahi kuolewa na mmojwapo kati ya hawo wawili?’
akaulizwa.
‘Niliwai kuolewa,na bahati nzuri ni kuwa tuliwahi kutimiza
nguzomuhimu ya ndoa, ambayo zawaidi yake kubwa ni huu uja uzito,….lakini ndoa
hiyo haikudumu, ikavunjwa kwa nguvu za wazee wenye itkadi zao, na kwahiyo hivi
sisi sipo kwenye ndoa tena…’akasema huku akizua machozi kutoka.
‘Inaonekana ulimpenda sana huyo mwanaume…inavyoonyesha
ulimpenda sana kuliko huyo mwanaume mwingine?’akauliza huyo mwanaume.
‘Unaweza kusema hivyo,kwasababu ndiye niliyeweza kumruhusu mwili
wangu kwa mara ya kwanza, na hilo ndilo nililoahidi kuwa kati ya hawo wawili,
atakayewahi nikamruhusu kuupata mwili wangu, ndiye atakyekuwa mume wangu wa
kudumu…sasa ni nini nimefanya,…ndio maana inaniuma sana, na sasa nimekuwa
kama…kama ….malaya…maana hata ‘akaanza kulia.
‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza huyo mwanaume.
‘Kwasababu nimeshindwa kuzizuia nafsi zangu, na kuvunja
kiapo changu, na nimeshindwa kuvumilia na kukulazimsiah kitu ambacho sikuwa
nacho awali…najuta na naomba unisamehe sana…nakuomba sana tena sana, unisamehe
kwa lile lililotokea …’akaanza kulia.
‘Sikiliza Kais….’akasema yule mwanaume,na Kais akashituka,
huyu mwanaume kajuaje jina lake, akamwangalai yule mwanaume kwa makini, lakini
yule mwanaume, akawa kama anainama chini, na hapo Kais, akaanza kuhisi jambo, akaanza kurudi kinyume
nyume,….woga ukaanza kumjia, akajua huyo anaweza kuwa mmoja wa maaskari wa mzee
wao,na anavyowajua hawo maaskari wa mzee, ni watiiifu sana, hawaweze kumsaliti
hata siku moja yule mzee, aliyesababisha yeye kufikishwa mahali hapo.
‘Wewe ni nani….’akasema Kais, na alipoona yule mwanaume
katulia, akageuka kwa haraka na kuanza kukimbia….
NB: Natamani kuendelea lakini muda huo umekwisha. Lakini naona kuna matatizo kwenye Google Chrome, sijui ni mimi mwenye au vipi, na hii imechangai sana nisiweze kuwa nanyi siku mbili zilizopita. Tukijaliwa
tukutane sehemu ijayo
WAZO LA LEO: Tabia ni kitu cha ajabu sana, kila mtu ana
tabia yake, ambayo huenda nii udhaifu alio nao, lakini wengi wetu hatupendi
kuukubali kuwa tuna udhaifu huo na tunatakiwa kuondokana nao.
Kuna watu wana udhaifu wa matendo ambayo kijamiii ni mabaya,
lakini ukiambiwa kuwa ana tabia hiyo ambayo ni mbaya na haipendezii kwa jamii,
mtakosana, na huenda watu kama hawo wafikia hata kupinga kwa nguvu zote kuwa
hawana tabia hiyo, au hata akikubali kuwa ana uzaifu huo, bado ataona kuwa
kwake yeye ni haki yake kuwa nayo, na watatafuta mwanya, hata wa maandishi ya
imani zao na kuyapotosha ilimradi, kuhalalisha matendo yao mabaya.
Tusijidanganye kwa hilo…kama metendo yako yanawakera
wengine, kama matendo yako yamejengwa na ubinafsi, kama matendo yako yamejengwa
na tabia za kiulevi, kiuchoyo, usengenyi, uchochezi,wizi, uzinzi, propaganda potofu, nk, huo ni udhaifu,
unahitajika kuondokana nao.Na kama umepata bahati ,mwenzako akaja kukushauri, akakupa
neno la kuondokana na tabia hiyo, msikilize,na mshukuru sana kwa kuuona ugonjwa
huo, kwani atakuwa ni dakitari wako mwema, na atakuwa kakuokoa kwenye ugonjwa
mbaya wa nafsi.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Hapa inaonyesha ulitulia wakati unaandika sehemu hii, HONGERA SANA MKUU
Post a Comment