Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, March 9, 2012

akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-87 Mwisho




Kilikuwa ni kikao cha wanafamilia wa pande mbili,kwa mume ambaye sasa ni marehemu na kwa uapnde wa kikeni, kama ilivyo ada, inapotokea mmoja kati ya wandoa kutangulia mbele ya haki.Pamoja na hayo pia kilikuwa ni kikao maalumu ambacho wao walikiita kikao cha kuagana, maana wakitoka hapo kila mtu anatawanyika kuelekea sehemu yake. Hata hivyo ndani ya kikao hicho walikuwepo waalikwa, ambao nia yao ni kuhakikisha kuwa kuna usalama na maridhiano.

‘Ninayo furaha sana kuwepo kwenye kikao hiki, najua mimi ni kama mualikwa tu, kwani sio sehemu ya familia hii, lakini sasa najiona kama mwanafamilia....pamoja na kuwa mwanafamilia mualikwa, lakini mimi nimefika hapa kama wajibu wangu kuhakikisha kuwa usalama unakuwepo, lakini pia kuhakikisha lengo letu la maridhiano linakuwepo....hasa katika zile pande ambazo tulizona zina msigishano wa hali ya juu...’akasema mpelelezi.

‘Karibu sana, jisikie kama mwanafamilia, ....’akasema mzee mmoja huku akigeuka upande ule waliokaa akina mama.

‘Unajua mimi babu yangu anatokea Tanzania, na alipofika hapa aliona ndani ya familia iliyokaribu sana na familia yenu wazee wangu,najua mnaifahamu sana familia yangu, babu yangu . Kwahiyo ukilinganisha hivyo najikuta kama nahusika sana kwa familia zote mbili, na nashukuru sana, licha ya kuitwa kama mualikwa, lakini naona mumenipa jukumu kubwa sana la kuwa mwenyekiti, wakatii wazee wangu mpo,....’akasema mpelelezi.

‘Wewe unafaa sana, maana sisi wazee tunaachia maadaraka,....na wewe nakuona ni sehemu kabisa ya familia, na labda babu yako anaweza akawa ni damu miongoni mwa familia hii, huwezi jua, lakini vyovyote iwavyo, sisi sote ni ndugu, sisi sote ni watoto wa Adamu,au sio ...’akasema yule mzee huku akiwageukia wenzake ambao nao walitingisha kichwa kukubali.

‘Unajua mambo mengi yanayotokea hadi watu wanatofautiona chanzo kikubwa ni ubinafsi tu na roho mbaya, kila mtu anapenda kuangalia tumbo lake na utashi wake, hili ndilo linaloharibu dunia, umimi, unazidi na unatawala dunia.....’akasema Mzee mwingine.

Maneno ya mzee huyo yalimfanya mama amuangalie yule mzee mara mbili, akitaka kumuuliza hivi hamjioni kuwa mnayoyafanya nyie ndio hayo hayo anayoyasema yeye, akaguna ....na moyoni akasema; kweli nyani haoni kundule ni ajabu sana watu kusema yale wasiyoyatenda...

Na mara simu ya mpelelezi ikalia na hapo Mpelelezi akainuka na kuchukua fimbo yake ambayo anaitumia, kutokana na kuumia kwenye lile tukio la bomu,...ilibidi afungwe POP mguu mmoja, aliwaomba tafadhali wenzake akatoka nje kusikiliza hiyo simu.

‘Ndio mkuu habari za huko bongo, ...?’ akauliza mpelelezi huku akicheka, halafu akasikiliza nini mwenzake anaongea na huku akigonga gonga ile fimbo kwenye mguu wake uliofungwa muhogo akacheka na kusema;

‘Nashukuru sana...nimepoa na hali inaendelea vyema ,... na tunakushukuru sana kwa msaada wako na mawazo yako yenye tija, kwani kweli tumegundua kuwa vita na miguvu sio tija, kwani tungeendelea kuuana na kulipizana visasi mpaka mwisho wa dunia, kwakeli hata mimi nimeligundua kuwa jambo jema ni muafaka,....’akasemahuku akiangalia juu.

‘Ndio na demokrasia ya ukweli...sio ya kudanganyana danganya....ndio ...kabisa mkuu, cha muhimu ni kuangalia nini kinakosekana hasa katika swala la uongozi na siasa....’akasema na kutulia kuskiliza na baadaye akasema;

‘Ndio kabisa mkuu , haya yametokea kwasababu ya uongozi mbovu, usiojali maslahi ya watu....na taizo kubwa ni kuwa mbali na watu waliokuajiri, tunasahau kuwa sisi tumeajiriwa na wananchi....ni kweli kwa mtizamo huu, sasa naona dalili njema inakuja...’akasema na kuchungulia ndani .

‘Ndio namshukuru mungu maana sasa hivi tungeongelea mengine,....’akasema na kutulia kidogo akisikiliza, na baadaye akasema;

‘Ni kwel, ina maana bomu lile lilikusudiwa kutuangamiza sote, nafikiri mlengwa alikuwa mimi, ...lakini liliwahi kulipuka kabla hatujaingia kwenye hilo gari, na kuna mtu ambaye alikuwa kawekwa kuhakikisha kuwa sote tunakufa, ....’akasema na kutulia kidogo akisikiliza , halafu akasema;

‘Huyu jamaa alikuwa juu ya jengo jingine, yeye nafikri aliwekwa kuhakikisha mimi siponi, na aliyetuokoa na kijana wetu mmoja ambaye alikuwa hayupo hapo, alifika muda mfupi baada ya hilo bomu kulipuka, ndiye aliyemuwahi huyo jamaa na wakaanza kujibishana kwa risasi na jamaa alipoona nazidiwa akakimbia...’akasema mpelelezi akijiangalia kwenye mguu wake ulio na POP.

‘Hutaamini ...huyo rafiki wa Mkuu wetu, au tumuite mshirika menza, ingawaje mwishoni wamekuwa wahasimu, alitoweka kiajabu-ajabu, ...siamini kuwa yule mtu ana ubinadamu gani maana kuna muda nilipata fahamu, nilipofunua macho nilimuona kwa macho yangu, akiinuka pale alipokuwa kadondoka, na kujikokota, maana ilionekana kabisa amevunjika mguu, lakini bado alikuwa na ujasiri, akajikokota hadi pale alipokuwepo mkuu,....yaani unashindwa hata kusimulia kilichotokea,,....’akasema mpelelezi.

‘Kumbe alikuwa na kisu mfukoni, akamfuata mkuu pale alipokuwa kalala, ...mkuu kwa muda huo alikuwa katika hali mbaya, akihitaji msaada, maana kila mmoja pale aliyekuwa hai alikuwa akihitaji msaada, ....hakujali hali aliyokuwa nayo mkuu, akatoa kile kisu na kumchinja kama kuku....halafu akachukua chupa na kukinga damu, na kuhakikisha kabisa kichwa kimetengana na kiwiliwili , akakibeba kile kichwa na kukimbia nacho...’akasema mpelelezi akiwa na uchungu...

‘Hayo ni mambo yao ya kishirikina,...na ukatili wa hali ya juu, kwani huyo jamaa hatujamuelewa vyema kuwa ni nani, lakini anaonekana ni mtu aliyesoma kwa mtizamo wa haraka haraka, lakini bado anaamini mambo hayo,...kama kweli alifnaya hivyo kwa ajili ya shiriki, kwahiyo sio swala la kusoma au kutokusoma, ni swala la imani. zao...lakini hayo yote yana mwisho, nina imani hiyo, kuwa siku zinavyozidi kwenda mambo kama hayo yatakuwa ni historia tu...’akasema mpelelezi huku akichungulia tena ndani .

‘Mama wa hawo mabinti hajambo, aliwahiwa kabla hawo w atu hawajafanya mambo yao,na wanasema ni mara ya kwanza kutokea hali kama hiyo, kwani mtu anapofikishwa hatua hiyo, wao wanaiita ya hukumu yao, huwa hakuna kizuizi,na huyo mtu hawezi kukimbia au kufanya lolote maana nguvu zao za mizimu zinakuwa zimemzingira huyo mlengwa, ....’akasema mpelelezi akionyesha hisia Fulani usoni.

‘Kwa mtizamo huo tunaweza kusema hivyo kuwa labda hiyo mizimu yao kama wanavyoiamini, ilikuwa haijakubaliana na hilo,... lakini wao nasikia wamedai lazima huyo mama atachukuliwa tena, kuhakikisha kuwa hukumu hiyo imetekelezwa, vinginevyo inabidi kutolewa kafara la mtu mwingine, anayehusiana naye...., serikali imejaribu kuingili kati, ...lakini imeachia sana mambo hayo ya kimilia, najua kabisa kama wamekusudia hivyo watafuatilia....ndio maana naona kama inawezekana huyu mama na familia yake waondoke hapa....’akasema mpelelezi.

Sijaongea naye kuhusu hilo, lakini leo tuna kikao na wanafamilia wa pande zote mbili,na wazee upande wa mume wapo hapa ,ni wazee wawakilishi wa hiyo familia, na nawajua sana hawa wazee ni watu wenye msimamo sana na mambo yao, huwa hawaambiliki, lakini tutaangalia lile litakalowezekana, ikishindikina mimi naona haina haja ya kulazimishana, haina haja ya kushindana na watu hawa ambao hawajali uhai wa mtu, na wala hawajali sheria,inapofikia katika mambo yao ya kimila...nawaju sana maana nimeishi nao...’akasema Mpelelezi.

‘Nitawashauri, ngoja nikaongee nao halafu nitakuhusisha kama ikibidi...ahsante....’akakata simu na kuingia ndani.
***********
Mama akiwa kalala kwenye sofa huku wakimsubiri mpelelezi arudi ,aliwaangalia wale wazee huku hisia za uwoga na hasira zikiwa bado zimemtanda akilini,...kila mara alipowaza nini kilitokea huko alipokwenda, alikuwa bado hajaamini kuwa yupo salama, hali aliyoiona kule haijawahi kutokea katika maisha yake, mengi alishawahi kusimuliwa na masimulizi, ....aliyachukulia kama hadithi za zamani tu, lakini sasa ameamini kuwa kweli kuna watu muumiani,..
‘Najua ndugu zanguni mtatushangaa sana na imani zetu, ...najua hata huko kwenu zipo, labda mnaficha fiche tu, hata hivyo sisi wengine kuna mambo yanafanyika hata wenyewe tunayashangaa ....ni imani za ajabu kamahupo ndani ya familia husika, ...na kamaniiamni yako na umekulandani ya imani hizo hana budi kuziafuata, ukikiuka masharti yake, hutakatisha siku mbili, ...’akasema mzee mmojawapo.

‘Mimi mwenyewe nilikuwa mkaidi baada ya kusoma kidogo nikaona mambo hayo yote ni kishetani, nikwa napuuzia , yaliyokuja kunipata sitaweza kusahau, na kama wasingelikuwa wazee wangu kufanya juhudi za ziada huenda muda kama huu ningeshasahaulika kwenye uso wa dunia....’akasema mzee mwingine.

‘Nyie hamtaweza kuamini hata tuwaambie nini, lakini mama yenu alionja kidogo yale yanayotokea kwa mtu anayekaidi, pale ni kionjo tu, kama angeanzishiwa hayo machungu, hata msingetamani kumuona, maana huwa sura hiyo inabadilika na kuwa kikongwe, sura inakunjamana, macho yanatolewa, au unaweza ukaozeshwa sehemu za siri, ..na mateso mengine ambayo mwisho wa siku utasalimu amri...’akasema mzee.

‘Sasa ndugu zanguni, sisi tumetumwa kama wawakilishi, licha ya kuwa tuekubali kuridhiana, na cha muhimu ni kuwa kila ulilolikuta mama huruhusiwi kuligusa, ikiwemo hii nyumba, na miradi mingineyo, lakini kama kuna sehemu ya mkono wako, unaruhusiwa kuchukua, uwe na uhakika kama kweli kuna mkono wako, maana vinginevyo, sisi hatutalaumiwa kwa lolote lile...’akasema mzee mmojawapo.

‘Ni hivi, inapofikia mume kaondoka, kawaida ya milazetu, mke anarithiwa na ndugu wa huyo mume,na mali yote inakuwa mikononi mwa huyo mwanaumemrithi,lakini kama mwanamke hatakubali, basi haruhusiwi kuchukua chochote,...kwa kesi yako, ni zaidi ya hayo, kwasababu inavyoonekana mlikuwa mkiishi kinyume cha matakwa ya familia, lakini hata hivyo kama utaridhia hayo matakwa na ukakubali kurithiwa na ndugu wa mume wako ....wazee wataangalia jinsi gani ya kuwapooza hawo mizimu..’akasema mzee mwingine.

‘Lakini kama hutakubaliana na matakwa yao, kwa uoni wetu na ushauri wetu, huo ni ushauri wetu, tunakuomba uondoke humu nchini, maana kiuzoefu hutakuwa na amani, na nina imani kabla ya siku arubaini utasikia vumbi lake,mara nyingi haziishi siku arubaini, ...’akasema mzee mwingine na mara mplelelezi akaingia.

*******

Rozi alimwangalia Maua pale alipokaa, na huku akili yake ikiyasikiliza yale mazungumzo ya hawo wazee, kila hatua iliyokwenda , alitamani awaambie waondoke, aliwaoana ni watu wa ajabu sana, na hasa aliposikia nini kilitaka kumpata mama yake, aliwaangalia wale wazee kwa jicho la hasira, na alitamani kuwaambia kuwa wao hawatakii chochote kama ni mali ndiyo inayosababisha yote hayo, na hawataki kabisa mambo yao, lakini hakutaka kuingilia mambo ya wazazi mapema hivyo, akawa msikilizaji kama walivyo wengine.

Na baada ya muda aligeuka kumwangalia Mgonjwa, jina hilo lilishazoeleka, licha ya kuwa mgonjwa keshapona, lakini kila mtu keshazoea kumita hivyo, na mhusika naye keshalizoea kiasi kwamba akiulizwa jina lake anasema anaitwa Mgonjwa, akiwa namuangalia fikira na kumbukumbu zamazungumzo yao yaliyopita zilimjia akilini na kujikuta akicheka.


********

‘Unajua kama nitaishi mbali na wewe sijui kama nitakuwa na raha, ikizingatia kuwa Maua sio wangu tena, na nimekubali matokea...’alisema mgonjwa.

‘Kwanini unasema hivyo, kwani mipango yako ni kuwa hatutakuwa karibu tena, hebu niambie una maana gani kwa hilo...’akauliza Rose huku moyo ukimdunda kwa hamasa, alijua huo ndio mudamuafaka wakuyaweka mambo yote hadharani, kwani kulikuwa hakuna kipingamizi tena, kama kweli ndugu yake ana mume wake,na hakuna jinsi ya kumuacha tena,.....

‘Sikiliza Rose, tuseme ukweli, wewe hapo ni mja mzito, na hujawahi kuniambia ni ujauzito wa nani, nahisi ipo kama ilivyo ya Maua,sizani kwamba uliupata kwa kubakwa na huna mpango na aliyekupa huo uja uzito..’akasema mgonjwa huku akiangalia tumbo la Rose ambaye alikuwa kasimama mbele yake.

Rose alikaa karibu na alipo Mgonjwa, akamshika bega, haikutosha,akaegemea kwenye bega lake, haikutosha, akautoa mkono begani na kuiviringa mkongoni akatulia kusikiliza mapigo ya moyo, na kwa hali ile alijihisi yupo karibu na mtu anayemjali , mtu ambaye kwa sasa anaona ndiye pekee katika maisha yake.

‘Huenda nilibakwa kweli na mbakaji hajui kuwa nina mimba yake, na leo hii imefikia hatua hii utamwambiaje ...ni kazi kubwa na wakati mwingine inabidi uchukuea maaumuzi magumu kama aliyoyachukua dada yangu.....’akasema Rose huku akiwa kajiegemeza kwenye bega la mgonjwa.

‘Hata kama kamaimefikia hatu ya kuzaa,ni bora kumwabia mhusika ukweli na kama alikubaka kwa nguvu yeye alitarajia nini....mimi nakushauri umwambie ukweli, ili mwisho wa siku hata mtoto akizaliwa ajue ni nani baba yake, na kwa hali hiyo hiyo ndio maana nahisi kuwa mpweke kuliko watu wote duniani...’akasema mgonjwa.

‘Kwanini ujihisi mpweke,wakati mimi nipo, hata kama Maua hatakuwepo karibu yako, lakini mimi nipo, sioni kwanini uwe mpweke...’akasema Rose huku akipitisha pitisha mkono wake nyuma ya mgongo wa Mgonjwa.

‘Upo, lakini utakuwa na mwenyewe, baba wa mtoto huyo atakayezaliwa, unafikiri atakubali...mmmh, kweli nahiusi kuwakosa watu niliowapenda kwa moyo wangu wote...’akasema na mgeukia Rose , wakaangaliana machoni. Rose akatabasamu na halafu akainuka pale alipokuwa amekaa na kusimama,akageukia upande mwingine huku akiwaza .

Rose alikuwa kafikia uamuzi baada ya kutathimini hali ilivyo, na alishakuwa na uhakika na hilo alilotaka kuliongea, lakini kila mra aliona ugumu fulani, na kila alivyowaza, aliona lazimaiwe hivyo, ...hata hivyo yeye kama mwanamke aliona siyo vyema....,Kwanza aliona labda njia bora ni kusubiri mpakaajifungue, lakini ....

Rose aligeuka kumwangalia Mhuja na kumtizama huku anatafuta ukucha kwenye kidole chake, alimwangalia kwa makini aliyekuwa Mgonjwa wake ambaye kwa muda huo alikuwa kainama chini huku kashika kichwa, akamuonea huruma, na kusema;

‘Mhuja, kama alivyokupenda dada yangu ndivyo ninavyokupenda mimi....hilo kwanza uliweke akilini, huenda mimi nikawa nakupenda hata zaidi yake..lakini.’akasema Rose.

‘Hiyo,....lakini, sawa hata mimi nakubali hivyo,.... ndio maana nilikuambia toka awali kuwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda Maua haina tofauti na ninavyokupenda wewe, maana sioni tofauti yake, nashindwa kuwatofautisha....lakini kama ulivyosema, nahisi una mtu wako...’akasema Mgonjwa.

‘Nina mtu wangu, nina mtu wangu, mmmh, ndio ninaye, nisikudanganye, ila tofauti kati yangu na Maua ipo, kwasabaabu Maua sasa ni mke wa mtu na ulishakubali iwe hivyo kwasababu za kimsingi,sio kwamba kweli Maua hakupendi, anakupenda sana, lakini hakukuwa na jinsi, ...tofauti na mimi ni kuwa mimi sina mume, mimi bado ...’akasemahalafu akatulia na kutabasamu huku akiona aibu.

‘Utakuwa naye karibuni au sio, niambie kwanza ni nanii alikubaka,maana kama inawezekana naweza kuchukua sheria mikononi mwangu...eeh’akasema Mgonjwa.

‘Una uhakika unataka kumjua aliyeni baka, ....nawezakusema sio kubakwa kama ilivyotokea kwa huyo ....mmmh...’akatulia na kuwaza kwa makini, halafu akasema;

‘Kutokana na tarehe, na mahesabu yangu, mwenye uja uzito huu, hakunibaka ...yeye ilikuwa tofauti, ingawaje ilikuwa sio nia yangu, kilichotokea pale nashindwa hata kukielezea. Mwanzoni nilichanganyikiwa nilipogundua kuwa nina ujauzito huu, ilibidi nichanganyikiwe nikiwa sijui nifanyaje, kwanii ni kitu kimetokea bila matarajio, licha ya kuwa mimi ni dakitari, lakini pia mimi ni binadamu kaam wengine, hata hivyo....’akatulia kidogo halafu akasema;

‘Hisia za mwanzo zilikuwa hivyo ....kuwa huu ujazito ni wa huyo mbakaji,...ndio maana nilitaka kabla ya kusema lolote nisubiri kwanza nijifungue ili niwe na uhakikana hilo, ....lakini nilipotuliza kichwa, nakufanya tathimini, kiuatalaamu, sasa nimeona kua kweli sio yeye ...kama dakitari nimeligundua hilo, kuwa huyo aliyenibaka- kiubakaji sio mwenye hii mimba, nina uhakika huo...’akasema na kugeukia dirishani.

‘Hapo sikuelewi ina maana una mwanaume mwingine tena ...’akasita kumalizia.

‘Nina...nini, mwanaume mwingine...ooh, ndiyo yupo, lakini sio kama unavyowaza wewe, ....?’ akamtizama mgonjwa kwa makini halafu akatabasamu na kusema;

‘Sivyo kabisa kama unavyozainia hivyo kuwa labda nina wanaume zaidi ya mmoja, kuwa, Hapana sina tabia hiyo na sina maana hiyo ,....’akageuka pembeni na kusema kwa sauti ya uchungu;

‘Kiujumla katika maisha yangu, mwanaume wa kwanza ni yule aliyenitelekeza wakati tukiwa tunajiandaa kufunga ndoa, na ndiye aliyenifanya niwachukie wanaumewote duniani, na mwanaume wa pili ni huyo aliyetumia nguvu katika mwili wangu, bila hata ridhaa yangu....sitamsamehe kwa hilo, namchukua kuiko maelezo, na mume wa tatu ndiye yule aliyenibadili,....’akatulia kwa halafu akasema;

‘Aambaye ndiye mwenye uja uzito huu,nampenda kuliko wanaume wote duniani...’akasema Rose halafau akageuka na kumwangalia Mhuja.

‘Mhh,huyo mwanaume ana bahati duniani,....kama ingelikuwa mimi ningetamani dunia isimamehata kwa sekunde moja,...kama ule wimbo wa mlimani park, unaimbwaje vile, rafiki yangu mmoja anaupenda sana, unasema...` Uliponikubalia tuwe mke na mume. Nilitamani Dunia isimame hata kwa sekunde moja. Ili niione nuru ya mapenzi yako. Na roho yangu iwe…’akajikuta akiuimba huo wimbo halafu alipoona Rose anamwangalia huku akitabasamu akanyamaza na kusema;

‘Maana nikuambie nini Rose, wewe umejaliwa kila kitu ambacho mume anatakiwa akipate,.....sio siri, kama isingelikuwa huyo mume unayemependa kuliko wote duniani ningelikuambia kitu, mimi nisingelijali huo ujauzito, nipo tayarii.....’akasema Mgonjwa.

‘Hahaha..hivi hujanielewa hadi hapo, ninachotaka kusema nikuwa ujauzito huu ni wa kwako....’akasema Rose na kilichofuatia hapo na Mhuja kusimama , wakajikuta wanakumbatiana....

*********

Baada ya kuingia mpelelezi ambaye alionekana kama ndiye mwenyekiti wa kikao, mazungumzo yaliendelea na waongeaji wengi walikuwa wanaume, na aliyejaribi kuhoji hoji likuwa shangazi na wakati mwingine wale wazee wakawa kama hawamsikilizai. Mama alipoona hapewi nafasi ya kuongea akaingilia katu na kusema nay eye ana yake ya kuongea, na mwenyekiti akamruhusu,...

Mama alipopewa nafasi hiyo ya kuongea kwanza alitulia kwa muda bila kusema kitu , na alipofunua mdomo machozi yalianza kutiririka machoni kama mirefeji ya maji, wifi yake akamsogelea na kumshika begani akampa moyo;

‘Sema wifi hapa semakilakitu unachotaka kusema, sisi tupo kwa jili yako, mimi hapa nasimama kama mume wako, licha ya kuwa ni mke....’akasema wifi yake.

‘Ni uchungu uliojaa moyoni, sikuamini hayo niliyoyaona, na sikuamini kabisa kuwa kumbe mume wangu alikuwa na mke mwingine na watoto, ....lakini sio mbaya, hilo sio kosa lake maana milana desturi zake zilimtaka awe hivyo, kinachoniuma sasa ni kuwa hatutaonana naye tena, na baya zaidi ni tafsiri za watu ...’akasemana kufuta machozi.

‘Ya watu ni yao, wanasema kwasababu wana midomo yao,na misemo yao sio njia kuwa itakuzuia ...hayo yakubali kama uzaifu wa kila binadamu na lililobakia na kuwasamehe, na kumuombea mema aliyetangulia ...’akasema wifi yake.

‘Namuombea sana mema,ila tafsiri za watu kuwa niliolewa naye kwasababu ya mali sio sahihi,hawajui jinsi gani nilivyompenda huyo mume, kwasababu alikuwa na tabia ile niliyoipenda, ...hawajui watu jinsi gani tulivyoishi, tulivyohangaika pamoja, hawajui, wanachojua wao ni kuangalia mali,....hawaangaliii utu, ...sawa kama nilimbambikia mtoto...haiwahusu , hawajui makubaliano yetu wawili ,..'akatulia kidogo halafu akasema;

'Hata hivyo ilikuwa iwe hivyo, hakukuwa na njia nyingine...kwahiyo nataka kusema hivi....’akatulia kimiya alipoona mzee mmoja akitaka kuongea kitu na wote wakamwangalia huyo mzee kwa makini lakini hata hivyo hakusema kitu akatulia akimwangalia mwenyekiti wa kikao.

‘Mimi nimeamua kuwa nyie wanafamilia ya mume wangu, muamue lile mnalolitaka, kama mnaona hiki kinanistahili nipeni,kama mnaona hakinistahili, chukueni,sitaki tena kulumbana na kuingia katika hatari zisizo na msingi, kwasababu yote yanayogombewa hapa ni mali, ....niwaulize je mume wangu alijua kuwa atakufa na mali alizozihangaikia miaka mingi ataziacha,.....?’ akauliza na kwaangalai wale wazee.

‘Hakuna anayejua kitu kama hicho....’akasema mzeemmoja.

‘Na hivyo hivyo hakuna anayejua lini litatokea lipi katika uhai wa wanadamu,...lakini nyie mumeshajua kuwa haitapita siku arubaini litatokea baya kwangu,mumeshajua kuwa huyu anastahili afe kwa kafara. Mumeshajua hata yale yaliyo mamlaka na mungu, au sio, nyie sio wenzetu...’akasema mama akiwa kawakazia macho wale wazee, ambao nao walimkazia macho huyo mama wakiwa kama wanashangaa.

‘Kama tulivyokuambia toka awali ni kuwa hayo mengine ni imani,...wewe kama mwanamke kuyapinga, na hta hivyo hukustahili kuongea wewe...walitakiwa wawakilishi wako ...wazee wako,...lakini huenda nyie huko hamna uaratibu huo, ...huku kuna msharti na ukijitia kiburi utajuta, ....huwezi kuamini kama hujakumbana nayo, sisi tumekulia huko tumeyaona na tumeshuhudia, kwahiyo.....’akasema mzee mmoja na mama akamkatiza.

‘Ngojeni niongee,....maana mumeshanipa nafasi yangu ya kuongea, ni vyema mkanisikiliza, au kwa sababu ya mila zenu, na imani zenu mke hastahili kuongea, kujitetea, ....sasa kwanini mkanipa nafasi hii niongee, na nimeanza kuongea mnanikatili, kama ni hivyo basi haina haja....ya mimi kuongea, ...lakini kwasababu mlishaniruhusu nasema hivi...’akatulia na kuwaangali watoto wake.

‘Sisi kesho kutwa tunaondoka..., tunarudi kwetu, na kesho naomba kila mlichoamua upande wenu, mje mniambie, na mnikabidhi yale mnayoyaona kuwa ni haki yangu, ....mengine tulishakabidhiana na mume wangu wakati akiwa hai, hayo hayastahili nyie kuyajua, lakini kama kuna ambayo mnayaona kuwa nimeyachukua isivyo halali yenu na hamkubaliani nayo, naomba muyaseme wazi, mimi nitawakabidhi, sina zaidi....’akasema mama na kutulia kimia.


***********



Ilikuwa siku ya shangwe na watu wengi walifika hata wale wasioalikwa mpaka ikabidi vyakula kuongezwa kinyume za bajeti iliyowekwa, na ndivyo ilivyo katika shughuli nyingi za Kiafrika, kuwa kama umesikia mwenzako ana shughuli hata kama hakukupa kadi au mualiko, ilimradi wewe ni jirani yake, kiujirani mwema, unatakiwa kuhudhuria, na ndivyo ilivyotokea siku hii maalumu.

‘Chereko chereko, baba kapata mama na mama kapata baba...’akashangilia shangazi huku akicheza huku na kule na kuwa burudani ya aina yake.

‘Ama kweli hakuna shughuli ndogo,mimi sikutarajia kuwa siku moja mngeliweza kuandaa yote haya, nawapa heko sana...’akasema Mzee mmoja akikaribishwa kwenye kiti chake alichoandaliwa na kabla hajamaliza kukaa vyema, mara vigelegeel vilitanda hewani, maana gari maalumu lililombeba bwana harusi liliwasili.

Kila mmoja alikuwa na shauku ya kumuona huyo bwana harusi, kwahiyo watu wakasimama na kuangalia huko liliposimama gari na haikupita muda akatokea mpambe wa bwana harusi halafu kwenye gari la mbele yake akatokea Mpelelezi akiwa kama muwakilishi wa mzazi wa bwana harusi akamsubiri bwana harusi atoke na akamshika mkono wakaongozana kuingia ndani kwenye sehemu maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kufungia ndoa.

‘Ndoa hii ni ya kipeke sana, maana kiutaratibu ilitakiwa bibi harusi ajifungue kwanza ndio ndoa ifungwe, lakini kwasababu za uharaka maana bibi harusi anatarajia kusafiri kwenda kusoma nje, inabidi tuifunge hi indoa kama iafuatavyo, na kama kuna mengine yatafuata baadaye....’akasema msemaji mkuu.

‘Yote sawa, bwana kapata bibi na bibi kapata bwana...chereko chereko.....’akasema mama mmoja

‘Lakini mimba ni ya kwake....?’akauliza mama mmoja na kuwafanya watu waangue kicheko.

‘Bila shaka, mimba ni ya kwake, ilipatikana katika majaribio....’akasema msemaji na watu wakaangua kicheko , na kilichofuatia hapo ni kufungishwa ndoa, kutokana na taratibu za imani zao, na baadaye zilifuata shughuli za kutoa zawadi na kuwasalimia wanandoa hao, na mara Rose akahisi kitu na kugeuka upande ule waliposimama watu, na mara macho yake yakatua kwa jamaa mmoja ambaye alikuwa kavaa miwani ya jua, na kwa muda ule alikuwa kaivua...
Rose alihisi mwili ukimwenda mbio, akabakia kaangalia kule kwa muda mpaka Mhuja akashituka na kumgusa mkono, ....

‘Nimemuona Adam, yule pale...’akasema Rose akimnong’oneza Mhuja.

‘Adam!?,....Adamu yupi huyo...!?’akauliza kwa kushituka.
Mhuja akageuza shingo taratibu upande ulealiokuwa akiangalia Rose, na watu karibu wote waligeuka upande ule waliokuwa wakiangalia, na mara mtu mmoja aliyekuwa kasimama upande ule akageuka na kuondoka....

‘Achana naye hayakuhusu hayo kwasasa au kuna jambo hujaniambia mpenzi...?’ akauliza Mhuja huku akizidi kuangalia kule alipookuwa huyo jamaa, lakini hakuwepo tena.

‘Rose akatabasamu na kumshika mikono huku akiwa kasimama Jambo ambalo sijakuambia ni kuwa....’akasema Rose na kumsogelea Mhuja, akasogeza uso wake na kuwa kuangaliana machoni, halafu akasema;

‘Nakupenda sana mume wangu,nakupenda kuliko wanaume wote wewe nakukabidhi mwili wangu na naahidi kuwa nitakupenda kwa moyo wangu wote katika misha yetu aliyotukadria muumba....’akambusu na vigelegele vikatanda hewani, na wengine wakasema ‘tena....hatujaona ....’

‘Hata mimi nakupenda kuliko maelezo,, ...nitakuwa mume mwema katika maisha yetu yote aliyotukadria muumba,.....’akasema Mhuja na wote wakakumbatiana na vigelegele vikatanda kila kona.

Mwisho.

NB: Nawashukuruni sana kwa kuwa name na hata kunivumilia kwa muda huo wote, sio nia yangu kukichelewesha sana hiki kisa, ila ni yale yaliyokuwa juu ya uwezo wangu.Nasubiri ushauri, maoni, ...

WAZO LA LEO: Hakuna refu lislo na ncha, na hakuna masika yasiyokuwa na mbu na kila zuri halikosi kasoro, ....kama mumekipenda hiki kisa nashukuru sana na mungu awajaze heri.


Ni mimi: emu-three

19 comments :

Anonymous said...

Kama picha vile, mmh na ndio hivyo imekwisha, kwanza nakupa pongezi, pili nakubuku nakala moja ya kitabu

Yasinta Ngonyani said...

Hakika kazi umeifanya tena kubwa na wengi wamejifunza na pia kuelimika. HONGERA HONGERA HONGERA SANA. Pamoja daima ndugu wangu:-)

emuthree said...

Nawashukuru sana kwa kuwa nami,dada Yasinta tupo pamoja

Anonymous said...

HATIMAYE IMEFIKIA TAMATI NNA IMANI MWISHO WA KISA HIKI NI MWANZO WA KISA KINGINE KIZURI NA CHA KUSISIMUA ZAIDI YA HIKI.AHSANTE NA HONGERA SANA JAPO ULIKUA UNAKIANDIKA KISA HIKI KTK MAZINGIRA MAGUMU MIMI BADO NIPO PAMOJA NA WW.

AMMY K said...

hadithi nzuri sana sana iwe kwenye kitabu jamani m3. tunashukuru sana kwa hadithi yako isiyochosha kila siku tulitamani iendelee. mungu akubariki uje utoe kitabu

Precious said...

Jamani jamani jamani huu ubusy wa hii dunia acha tu maana nina miezi kama 5 hv sijaingia huku unakuta natamani kuingia lakini nafasi nakosa nashukuru Mungu nimepata chance na nimeweza kumalizia hiyo series...M3 hongera sana sana na ss tuko pmj kwa mkasa upya unaofuata. M3 ur so talented i wish watu wa movie za bongo wangekufahamu am sure ungeleta mapinduzi makubwa katika tasnia yetu ya filamu Tanzania maana kwa mikasa yako tayari ni filamu nzuri na ya kusisimua isiyotabirika mwisho wake maana zilizopa ukianza kuangalia tu dk 5 za mwanzo unajua mwisho wa sinema utakuwaje. GOD BLESS U M3

emuthree said...

AMMY kitabu nakitamani sana kukiandaa,lakini kila hatu ninayofikia amakuuliza nakutana na vikwazo vingi,lakini sijakata tamaa, kwani kwanza nahitajika niwe na jembe,maana kwenye cafe huwezi kukipitia kitabu kizima,pili wapi pa kuanzia.

Mpendwa Precious, nilikumiss sana, maana ulikuwa ukinipa moyo kila hatua,nashukuru umerejea tena. Ama kwa hawa wenzangu waigizaji wa movie,mara nyingi wansema wanatunga wenyewe...lakini ipo siku!

Na Anon. wa March 12, 2012 2:16 PM, karibu sana kisa kingine ndio hicho kinaanza kuchanja mbuga.

Tupo pamoja daima

AMMY K said...

KILA LA KHERI M3 JAMANI. MUNGU ATAKUWEZESHA TU SIKU MOJA UTAFIKIA MALENGO YAKO INSHAALLAH. HAYO NI MAPITO TU. KUNGEKUWA NA AWARD YOYOTE YA UTUNGAJI HADITHI HAKIKA NINGEPIGA KURA KILA SIKU.

emuthree said...

AMMY Nashukuru sana kwa dua zako amina Rabillalamina.

Anonymous said...

A beautiful and beneficial piece of home furnishings to use to warmth and
keep your newborn nearby is actually a bassinet. com pay a
pretty penny for these products, unless you manage to find
discount Samsonite luggage. All small babies also seem more at home
in a confined space then in a large, airy crib.
Here is my webpage - baby Bassinets

Anonymous said...

Hi therе! Someοnе in my Facebook grоuρ shared this website with
us so Ӏ came to lοok it оver.
I'm definitely loving the information. I'm booκmarking and will be tweеting this to my followers!
Εхcellent blog and wοnderful deѕign and
style.

Fеel free to surf to my wеb-sitе .
.. Www.Youtube.Com

Anonymous said...

Way cool! Some extremely valid points! I appreciate you penning this post and the rest of the website is also really good.
Feel free to visit my web blog - jamón serrano

Anonymous said...

I sіmply could not go аwаy уour
ѕite before suggеѕtіng that Ι
actually еnjoyеd the usual info an indiѵіdual pгovide
on your ѵisіtors? Is gοnnа
be again ceaseleѕsly to check up on nеw posts

Also visit my blog credit counseling lafayette indiana

Anonymous said...

Whats uρ are uѕіng Wοrԁpress
for your blοg ρlatfoгm?
I'm new to the blog world but I'm tryіng to get started anԁ set uρ my oωn.
Do you need any html coԁing knowlеdge tо mаkе youг
own blog? Any hеlp ωoulԁ bе reаlly appгеciated!


Alѕo viѕіt my wеbsite Credit Counseling Services

Anonymous said...

I hardly leave a гeѕρоnse, hοwеver i did ѕome searching anԁ
wоund up here "akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-87 Mwisho".
And I do hаve 2 questionѕ fοг уou іf іt's allright. Could it be only me or does it look like some of these responses appear like they are coming from brain dead people? :-P And, if you are writing on additional sites, I'd like to keep up with еνerything new you havе to poѕt.

Would you make a liѕt of аll of
уour publіc pages like your linkеԁin profіle,
Facebook page or twitter feed?

Here is my blog; information

Anonymous said...

Αwesomе site yοu have hеге but
I wаs ωanting to κnow if you knew of any forumѕ thаt сover thе
same topicѕ talked about in this article?

I'd really like to be a part of online community where I can get suggestions from other experienced people that share the same interest. If you have any suggestions, please let me know. Appreciate it!

Here is my web page: info *cityzine.net*

Anonymous said...

Numerous individuals will definitely benefit from quality article like this one.
Do place me on your news letter subscription in order that I can be up
to date with your most up-to-date posts. Thank you upfront.


Feel free to surf to my web blog ...coconut oil uses for dogs

Anonymous said...

I am really impressed with your writing skills as well as with the layout on your blog.
Is this a paid theme or did you customize it yourself?
Either way keep up the nice quality writing, it is rare to see a great blog like this one these days.


Have a look at my web site - top information [onbrd.info]

Anonymous said...

Way cool! Some extremely valid points! I appreciate you penning this post and the rest of the website is very good.



my web-site - interesting info ()