Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, January 12, 2012
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-73 hitimisho 17
‘Hebu niambie ilikuwaje maana muda wote ulioniacha pale na akina mama, sikuwa na amani kabisa...’akauliza Rose baada ya kimiya cha muda mrefu, wakifuata maagizo ya madakitari kuwa wakiwemo humo ndani wasiongee kwa sauti. Muda mrefu ulishapita tangu shangazi na mama yao walitoka na kwa vile walikubaliana wakae kizamu zamu, haikuwa shida kwao, na walipendelea kama ingeliwezekana wabakie wao hapo hadi mgonjwa wao watakapozindukana.
‘Unauliza kuhusu ule mpango wetu, au unauliza kuhusu nini...?’ akauliza Maua huku akipiga miayo ya kuchoka, na Rose naye akafuatilia kupiga hiyo miayo,halafu Rose akasema;
‘Unajua Maua, kwanza sikuamini kuwa mama na shangazi hawajui kuwa nilyekuwa nimebakia pale ni mimi, sio wewe,... nilijitahidi kujifanya mtu asiyejua kitu kabisa, lakini kuna muda shangazi alikuwa kama anahisihisi , lakini kwangu asingeliweza kuona ndani, naweza nikaigiza sehemu yoyote , nikajikausha hata usinifahamu,...’akasema Rose kwa kujiamini.
‘Kwa jinsi tunavyofanana, sio rahisi mtu kujua yupi ni yupi, mara nyingi kutujua sisi inatagemean na tabia na vitendo tofauti tulivyovizoea kuvifanya, ambavyo vimezoeleka,...sizani kama shangazi angeligundua kwa haraka, hata kama ndiye aliyenilea...’akasema Maua.
‘Mh,, kuna muda nina uhakika, shangazi alihisi kitu... siunajua tena watu mlioishi pamoja, lazima kuna kitu alihsisi, na akaingiwa na wasiwasi, hebu niambie ilikuwaje...?’ akauliza Rose kwa sauti ya kunong’ona, na Rose akatulia kimiya...
Maua alipoona mwenzake akatulia bila kusema kitu, akamgeukia na kumuoa amelala, ni kweli atakuwa kachoka sana, kwani muda mwingi yeye ndiye alikuwa macho akihakikisha mgonjwa yupo salama, kuna kipindi Maua alipitiwa na usingizi, na alipozindukana alimkuta Rose akiwa macho akimwangalia mgonjwa. Sasa akajua ni zamu yake kubakia macho.
Na kabla hajamwambia Rose aendelee kulala, yeye atabakia macho, mlangoni kukaingia docta na alipofika pale walipokaa, Maua akajifanya na yeye kalala, huku anafunua macho kwa kujiiba kumwangalia nini docta anafanya, kwa mwanzono hakuwa na wasiwasi, alijua kuwa ni dakitari tu, na hata hakutaka kumgutusha Rose, aliyeonekana kulala.
Kuna kipindi Maua aliingiwa na wasiwasi, akataka kuinuka pale alipokaa aangalie nini yule docta anafanya,...au hata kumgusa ndugu yake ambaye ni docta ainuka angalia nini mwenzake anafanya, lakini baadaye akaghairi, na kutulia huku akimwangalia yule dakitari kila hatua, na tendo analofanya,baadaye yule dakitari akaondoka na kuwaacha Maua na Rose wakiwa wametulia...,
Na baadaye kidogo wakaja mama na shangazi na kusema sasa ni zamu yao, inawabidi Maua na Rose watoke wakapate chakula nje.
********
Wakati Rose na Maua wakiwa nje, akili ya Maua haikukubali kutulia,kulikuwa na wasiwasi akilini, na hata kufikia kujuta kuwa kwanini hakumgusa ndugu yake ambaye i dakitari akaangalia nini yule dakitari anafanya, na tangu muda ule hakupenda kumwambia ndugu yake, alihisi kuwa hata yeye atakuwa alimuona, na kwa vile ni dakitari atakuwa hakumtilia mashaka.
Na muda ule wakati wameingia wazazi wao, ndipo alikuwa kaamua kumuulizia ndugu yake kuhusu huyo dakitari aliyeingia na kutoka, lakini kabla hajafnaya hivyo ndio wakaamurishwa kutoka nje, ...
Walipofika nje, wakatulia kwamuda bila kusema kitu, na hapo ikampa muda Maua kuwaza kuhusuu huyo docta aliyeingia, alishindwa kujua kwanini anamhisi vibaya yule docta. Akatulia kwa muda bila kumsemesha ndugu yake akichekecha hayo mawazo kichwani, baadaye kwa kujipa moyo akazania ni kwasababu ya ule mtindo wake wa kutowapenda wanaume, ....
Na baadaye akasema kimoyomoyo, kuwa hakuna tatizo akageuza mawazo yake na kugeuka kumwangalia ndugu yake , ambaye naye alionekana mwingi wa mawazao, hakujua kitu gani mwenzake alikuwa akiwaza kwa muda huo,labda na yeye alikuwa akimuwaza yule dakitari, au sijui anawaza nini..na mata akagutushwa na mwenzake,;
‘Haya sasa niambie maana hapa tunaweza kuongea kwa sauti,ingawaje moyo wangu unanituma nirudi ndani nikaangalie vyema ni nini kinachoendelea , kwasababu akili yangu haimuamini mtu yoyote tena...’akasema Rose.
‘Huwaamini wazazi wetu, sasa na wewe umezidi, au ni kwasababu wewe ni dakitari ndio maana huamini mtu, lakini hata hivyo kwanini usiwaamini madakitari wenzako, inabidi uwaamini maana wao ndio wamemfanyia upasuaji, na wao ndio wanaowajibika kwa lolote lile..., vinginevyo utajifanya kujua sana na hata kuingilia kazi zao na matokea yake wanaweza hata wasituhusu kuingia tena mle wodini.....’akasema Maua.
‘Ni kweli nimeliona hilo, lakini ...ok, tuyaache hayo hebu niambie ilitokeaje pale ulipotuacha na wazazi, unajua baadaye nilijuta sana, kwanini nikakutuma wewe, ...kama baya lingelitokea ningejilaumu maisha yangu yote...lakini naona mungu ametusaidia ...’akasema Rose akitabasamu na kumkazia ndugu yake macho, akilini akifurahia kumpata ndugu yake huyo na kumlaumu mama yake kwa kuwatenganisha kwa muda wote huo, ilitakiwa wakue pamoja toka utotoni....
‘Ni kweli mungu ametusaidia...na waakti mwingine nilijuta kwa nini nilikubali harakaharaka bila kufikiria zaidi,...hata hivyo, nilikuwa tayari kufa kwa ajili ya ndugu yangu, niliogopa kama ungelikwenda wewe ungezuruka,...., hata hivyo, moyo wangu haukuwa na amani kabisa, ilifikia hatua nikataka kurudi maana hata pale hospitalini kwenyewe kulianza kunitia mashaka, sikujua kabisa niingilie wapi au nitokee wapi..nilifuata hisia zangu tu...’akasema Maua.
‘Pole sana ndugu yangu, najuta kwanini nikuingize kwenye maswala yasiyokuhusu, ...lakini ilikuwaje, mbona unaniweka roho juu...elezea kwa haraka basi?....’akauliza Rose.
‘Nilipofika pale mapokezi, nikawa naelekea sehemu ile wanapokaa watu wa kutoa huduma kwa wageni, , nikawa natembea kwa mwendo wa mashaka, nilikuwa nikifuata ulivyonielekeza,...’akasema Maua huku akitabasamu, na kabla ndugu yake ahajasema kitu akaseme;
‘Wakati natembea kwa mashaka,nikasogelea ile sehemu ya mapokezi, mara akatokea mtu na kunigusa begani na kusema `twende huku...’ hapo moyo ukalipuka, nikajua sasa napelekwa kusipojulikana, na sijui wakigundua itakuwaje...’akasema Maua.
‘Lakini nilikuambia kuwa ukimuona huyo mtu ubonyeze simu kwenye alama ile ya kupigia na ile namba ingeita huko polisi , ulifnaya hivyo..?’akauliza Rose.
‘Nilifanya hivyo, lakini sikuwa na uhakika kuwa nilibonyeza sehemu sahihi, maana mkono ulikuwa ukitetemeka...na ukumbuke sikujua kuwa huyo jamaa atanitokea kwa haraka kiasi hicho...’akasema Maua.
‘Tatizo lako umekulia huko kijijini, na hukutaka kujiweka kikakamavu, mimi mafunzo ya ujasiri niliyopitia yamenijenga kuwa imara, siogopiogopi ovyo, ....lazima tukirudi nyumbani nitahakikishia unapitia hicho chuo,unajua mawazo yangu kuanzia sasa ni kuwa ni lazima tukaishi pamoja, ....nitamshawishi mume wako akubali hilo, kwanza...hebu endelea ilikuwaje baada ya hapo....’akasema Rose akiwa na hamu ya kuongea mengi na kusikia mengi pia.
‘Wewe unanichekesha kweli,...eti kijijini, kwani nani kakwambia tunaishi kijijini, ...halafu unadai, tukaishi pamoja hukuo nchini kwenu, yaani niache nchi yangu ya amani nije kuishi nchi yenu hiyo yenye mapigano kila kukicha, hata hivyo wewe kiujumla unatakiwa urudi kwenu,kinachotakiwa ni kubadili utaifa wa katratasi, maana wazazi wako wote utaifa wao ni huko kwetu...’akasema Maua.
‘Unasema nini wewe....hahahaaah, mimi siondokii nchini nilikozaliwa, kwani utaifa unaangalia nini ulipozaliwa au ulipokulia? Akauliza Rose kama vile akimuuliza Maua, lakini alikuwa akijiuliza mwenyewe.
‘Mimi sijui hayo zaidi, wewe msomi ndiye nikuulize hilo swali....?’akasema Maua huku akiangalia saa,na moyo wake ulitaka kumwambia mwenzake warudi ndani wakaangalie nini kinachoendelea.
Muhimu ni cheti cha kuzaliwa na nyaraka za nchi husika za kukuthibitisha uraia wako, lakini nashangaa kuwa siku moja nilizifuma hizo nyaraka zangu nikakuta nimeandikishwa kuwa mimi niii....’akasita kumalizia na Maua aksema;
` Mtanzania...’ akmalizia Maua
‘Ndio... , nikawa na hamu ya kumuuliza mama, lakini ndio kipindi ambacho mambo yalikuwa magumu nay a kutisha na sikuwa na jinsi , ila kuhama hapo nyumbani...’ akasema Rose akionyesha uso wa huzuni, huku akiwa kama mtu anawaza kitu.
‘Mambo gani hayo, ya kivita au ya hawa watu wanaokufuatilia...:? akauliza Maua.
‘Hayo nitakuja kukusimulia baadaye kwanza tuendelee na kisa chetu, ilikuwaje...? akauliza Rose.
‘Yule mtu aliyeniambia twende huku, akaniona kama ninasita sita, akanishika mkono, ....oh, mkono ulikuwa kama chuma, au kitu gani sijui, sijawahi kushikwa na mkono wa namna hiyo, ulikuwa huwezi hata kuutikisa mkono au kujikwamua, ikabidi nimfuate kama goigoi Fulani, kuongea siwezi kukataa siwezi...’akasema Maua.
‘Mungu wangu mbona unanitisha, maana hapa nilipo, utafikiri naona jinsi ulivyokuwa ukichukuliwa na huyo mtu,,,ooh, sasa akakupeleka wapi...?’akauliza Rose.
‘Alinipeleka hadi kwenye mlango wa kutokea nje, hapo akasimama kidogo na kuangalai nyuma, na baadaye akanivuta kwa pembeni na kuniuliza swali...’akasema Maua na kutulia.
‘Swali gani hilo?’ akauliza Rose.
‘Wewe unataka mgonjwa wako awe hai au unataka awe maiti...’ akaniuliza hilo swali huku kaangali mbele, alikuwa haniangalii usoni...’akasema Maua.
‘Ulikaa kimiya au ulimjibu kitu...’akauliza Rose kwa hamasa, na Maua hakujali hilo swali akaendelea kuelezea;
‘Huyo mtu akasema;, unakumbuka nilikuambia kuwa uhai wa mgonjwa wako upo mikononi mwangu...au unafikiri natania...?,’ akasema Maua na kumfanya Rose ashituke na ghafla Rose akasimama juu na kumfanya Maua ashituke na kuuliza kwa mshangao;
‘Vipi mbona hivyo...?’ akasema Maua alipomuona Rose akisimama kwa haraka na uso ulionyesha dhahiri wasiwasi, na hata sura kubadilika....!
Rose alitulia kimiya kwa muda, baadae akageuka kumwangalia Maua machoni kwa muda bila kuema kitu,...na baadaye akachukua simu yake akapiga namba...mara simu ikaitikiwa,
‘Mimi ni Docta Rose, docta nina wasiwasi na usalama wa mgonjwa wetu, naomba muweke ulinzi wakutosha, nina wasiwasi mkubwa na wale watu....’Rose kabla hajamaliza akasikia docta akisema.
‘Rose hapa kwetu kuna ulinzi wa kutosha na isitoshe mimi sasa hivi naeeleka huko kumwangalia huyo mgonjwa, kwani ni muda sasa, hajaonana na doctari yoyote....’ akaambiwa kwenye simu.
‘Ina maana hakuna docta aliyewahi kuingia kumuona mgonjwa tangu ulipotoka wewe?’ akauliza Rose.
‘Hakuna, maana mimi ndiye ninayemshughulikia na ndiye nipo zamu, nikimaliza kumwangalia kwa hivi sasa nitamkabidhi mwenzangu, ...kwani una wasiwasi gani, ...usijali nitakwua naye kwa muda,...’akasema huyo dakitari.
‘Mnanipa wasiwasi, sijui ilikuwa ni ndoto au ni kweli, nahisi kama aliingia docta wakati nimepitiwa na usingizi, sina uhakika na hilo, ...’akasema na kumgeukia Maua ili kupata uhakika, kama yeye alikuwa macho, lakini Maua alikuwa kazama kwenye mawazo, na alikuwa kaangalia upande mwingine, hakuona kuwa Rose alimuhitaji kumhakikishia hilo....
‘Sizani kama amewahi kuingia docta huko wodi maalumu, na kama ilitokea hivyo, atakuwa ni dakitari msaidizi au mtoa huduma, na mtu kama huyo asingeliweza kugusa chochote kwa mgonjwa bila kibali changu... , hata hivyo usiwe na wasiwasi,...nimeshafika wodi maalumu, ....’ akatulia kwa muda na baadaye akasema
`Una wasiwasi na hawo watu uliosema wanamfuatilia huyo mgonjwa, usijali polisi wanawafuatilia kwa karibu sana, wameniahidi hilo ...baadaye basi, ..’akasema huyo aliyepigiwa simu na kumfanya Rose akae kimiya bila kusema kitu na baadaye akajipa moyo kuwa hakuna tatizo, akamgeukia Maua na kusema;
‘Unajua moyo wangu wote umejaa wasiwasi, tangu nikutume kwenye hilo tukio la hatari, nahisi kama kuna kitu kibaya kitatokea, lakini usijali, hizo ni hisia zangu tu mumeo yupo kwenye mikono ya usalama, niambie haraka ilikuwaje , maana nahisi maelezo yako yatanisaidia zaidi....’akasemaRose.
Maua akamwangalia Rose machoni, na baadaye akasema; ‘Unafikiri kuna jambo baya litatokea kwa mgonjwa wetu, mbona hapa ni hospitalini, na unakumuka wakati tupo pale, wewe naona ulipitiwa na usingizi, lakini aliingia docta akamtizama mgonjwa wetu na kuonyesha ishara kuwa hakuna tatizo lolote...’akasema Maua.
‘Aliingia dakitari, una uhakika na hilo.....?’ akauliza Rose kwa wasiwasi mkubwa na kusimama juu,alitaka kukimbilia kule wodini, lakini akatulia na kuhakikisha shinikizo la damu halipandi. Alirudi pale alipokuwa amekaa mwanzoni na kutulia kwa muda, huku akimsikiliza ndugu yake.
‘Ndio...aliingia dakitari muda ule lipopitiwa na kausingizi, ina maana wewe hukumuona, au ulishapitiwa na usingizi...mimi nilijua usingizi wako ni wa kidakitari, utakuwa umemuona, lakini nina uhakika alikuwa dakitari,kwani kuna masha yoyote....?’ akasema Maua kwa mshangao.
‘Ndio kwa muda ule nilipitiwa na usingizi, ila nikawa kama naota, kuwa kaja dakitari akawa anafunguafungua ile mipira aliyofungwa magonjwa, na nilipojaribu kumuuliza akawa hajibu kitu, na hata nilipojaribu kupiga ukulele , sauti ikawa haitoki.....sasa unanitaia wasiwasi, una uhakika na ulilosema kuwa aliingia dakitari, mungu wangu eee...’akasema Rose na kuinuka, akajaribu kumpigia simu yule docta, lakini simu ikawa inaiita tu bila kujibiwa.
‘Huyo docta uliyemuona, namtilia mashaka....alifanyaje alipoingia....?’ akauliza Rose kwa wasiwasi.
Maua akatulia kama kukumbuka, halafu akasema `Huyo Docta alipoingia, alitutupia jicho lakificho, na bahati jicho lake likakutana na jicho langu, ...kwani mwanzoni nilijifanya kama nimelala, lakini muda ule alipotutupia jicho, akanifuma nikiwa nimefumba macho, na macho yetu yakakutana, hakuonyesha dalili ya kushituka, ...'akasema Maua akatulia kidogo na baadaye akaendela kusema;
'Nikiwa namwangalia, hakujali, sana, lakini nakumbuka , nilihisi mwili ukinisisimuka kama vile niliwahi kuiona hiyo sura mahali,...na wakati mwingine nilihisi hatari nikataka kukugusa, lakini baadaye nikajua ni dakitari anafanya mambo yake tu...’akasema Maua.
‘Oooh, usingizi huu jamani,kwanini nilipitiwa na huo usingizi, ungenigusa kidogo tu, ningeliamuka mara moja....lakini hakuna cha kufanya kwa sasa, ...unakumbuka alifanya nini...? akauliza Rose kwa mashaka.
‘Nilimuona akikagua ile mipira na alitumia muda mwingi kwenye hiyo mipira inyotoka mwilini kwa mgonjwa kwenda kwenye ile mashine, ya kuingizia hewa, na maji na damu...mnajua wenyewe ni mipira ya nini, na baadae akahamia kwenye mashine nilihisia kama anafanya kitu Fulani kwenye hiyo mashine, lakini kama alifanya kitu, najua yeye ni dakitari tu,.....’akasema Maua huku akimwangalia Rose ambaye alikuwa hatulii, mara akae mara asimame na baadaye akakaa nakutulia.
‘Sasa kama unahisi kuna tatizo kwanii usiwafahamishe madakitari haraka, ....’akasema Maua na kusimama , safari hii moyo wake ulikuwa ukimwenda mbio kwa wasiwasi....
‘Nimeshamfahamisha huyo dakitari anayemshughulikia na sasa hivi atakuwa na mgonjwa wetu, tuombe mungu awe amefika wakati muafaka, vinginevyo.....mmmh, sina uhakika zaidi, tuombe mungu tu, kwasasa hatuna la kufanya, ...wewe nieleze ilikuwaje baadaye. Kwenye kisa chetu...’akasema Rose, ili kujiondoa kwenye yale mawazo, kwani hakuwa na la kufanya kwa muda ule.
‘Kisa kipi sasa, cha huyu dakitari au kile chetu cha mwanzoni, ulichinituma kuwa jasusi....’akasema Maua na kutabasamu...
‘Haswa hicho cha ujasusi, hicho cha dakitari, kipo juu ya uwezo wetu kwa sasa, ....ilikuwaje ulipoulizwa lile swali, ulimjibu nini...?’akauliza Rose.
‘Nilikaa kimiya, sikumjibu kitu, na alipoona nimekaa kimiya akageuka kuniangalia usoni, na baadaye akanivuta kwa nje, tulitoka pale mapokezi hadi kwenye sehemu ya kusubiri lifti, akasimama na kunigeukia, akasema;
‘Rose, jua haya yote yanafanyika kwasababu ya mapenzi, vinginevyo, tungelifanya jambo baya ambalo hutalisahau maishani, lakini wewe una bahati kubwa, na yote ni kwa ajili ya misha yako ya baadaye, unafikiri kuna nini ulicho nacho cha ajbu ambacho wanawake wengine hawana, lakini tunakuhangaikia wewe tu...sasa sikiliza, hapa tutaondoka, na kesho tunapanda ndege kurudi nyumbani, tukifika huko ndoa inafungwa kwa haraka....’akasema huyo mtu
‘Ulisema chochote....kumbuka nilikuambia usiseme neno hata moja....’akauliza Rose kwa mashaka.
‘Hapo nilishindwa kujizuaia nikamuuliza, `ndoa hiyo nitafunga na nani...?’ akasema Maua na kumfanya Rose amgeukie kwa wasiwasi.
‘Wewe umeharibu,...nilikuambia hata aseme nini, wewe unachotakiwa ni kukaa kimiya tu, ...haya niambie alisemaje ulipomuuliza hilo swali..?’akasema Rose huku akimwangalia Maua kwa mashaka.
‘Unajifaya hujui na nani....alisema hivyo na mara lifti ikafunguka, akanishika mkono kunivutia kwenye hiyo kifti, na kabla hatujaingia ndani ya ile lifti, simu yake ikaita...tukasogea pembeni na akuiacha lifti ikijifunga, wakati wote huo alikuwa kanishika mkono,hakutaka kabisa kuniachilia, akawa anasikiliza ile simu huku kanishikilia....’akasema Maua.
‘Waliongea nini,...?’ akauliza Rose.
‘Alichokuwa akiongea huyo mpigaji sikuweza kukisikia, ila nilisikua huyu jamaa akimjibu kwa makato mkato, kuna muda alisema, `haiwezekani, ina maana wameshafika wapo hapo nje, ...hata kama wamefika lazima niondoke naye.....’akasema Maua.
‘Endela, maana natakiwa kujua kila kitu, ila baadaye wazazi wakiniuliza nijue nini cha kuwaambia, niwe kama mimi nilikuwepo huko, usiache hata kitu kimpoja....’akasema Rose.
‘Baadaye sijui aliambiwa nini, akasema haiwezekani ndio yeye....akanigeukia ni kuniangalai kwa makini sana, halafu akaniuliza swali ambalo sikujua ana maana gani...’akasema Maua.
‘Aliuliza swali gani?’
‘Sijui swali gani, maneno nisiyoyajua , sijui ni ya kidakitari, lakini baadaye aliponiona kimiya akaniluza swali jingine, .....’akasema Maua.
‘Swali jingine aliulizaje, ongea kwa haraka usikatishe katishe ....’akasema Rose.
‘Aliniulizia swali kwa kusema `Rose fani gani uliyokwenda kusomea huko nje...?’ sikumjibu nikakaa kimiya, na alipona nipo kimiya akanisogelea na kuniangalia machoni, akanikagua kwa makini, halafu akasikiliza simu na kusema `Nyinyi mna uhakika mbona kila kitu ni sawasawa kabisa, mimi namjua sana maana nimefanya kazi naye kwa muda mrefu, akaniangalia kwa makini, halafu akasema ....ngoja kidogo, ....akaguza na kuniangalia machoni kwa muda, halafu akaniuliza tena lile swali huku akinitikisha kwa hasira....’akasema Maua.
‘Ulisemaje,au ulifanya nini....?’akauliza Rose.
‘Kabla sijasema kitu, mara wakatokea madakitari wawili wakawa wanakuja ule uswa tuliosimama, na lango langu likawa kupiga ukulele pale wakitufikia....’ akasema Maua.
‘Ungeliharibu kila kitu, kumbe wewe hujui kazi ya ujasusi, ehe, ikawaje...?’ akauliza Rose.
‘Yule mtu, akasema, kama mna uhakika, inabidi tumtafute huyo mwingine, na sasa inabidi niyeyuke, ...’akasema huku wale madakitari wakitusogelea, na huyo jamaa alipoona hivyo, akaniachilia mkono na kuingia kwenye lifti ambayo ilishafunguka tena, na kuondoka bila ya mimi. Na wale madakitari waliponijia , wakaniuliza kuwa kuna lolote baya...nikawaambia hakuna, ...nikaondoka pale haraka haraka na kurudi mapokezi nikawasubiri hadi mlipokuja...’akasema Maua.
Wote walitulia kimiya kwa muda, na kabla maongezi hayajaanza tena, mara wakasikia kilio, na wote wakageukia kule kilio kilipotokea....
Kule mlangoni kwenye wodi maalumu, wakawaona shangazi na mama wakitoka, ....Rose na Maua wakasimama kuwaangalia,...
Shangazi alikuwa kaweka mikono kichwani, mama alikuwa kamshikilia begani shangazi kuonyesha kumzuia,na aliposhindwa akshikwa kichwa na yeye kuanza kulia.......hapo hapo Rose na Maua wakajua mambo yameharibika, bila kusema kitu kimetokea kwa haraka wakakurupuka mbio kuelekea huko wodini.....
NB Sikujua kabisa hitimisho hili litachukua muda mrefu, maana kila nikitaka kukatisha na kumalizia naona mambo bado yamebakia, je mna maoni gani na hitimisho hili, je linawachosha?...tumalizie au tuweke kila kitu hadharani, majibu yenu ndiyo yatanipa changamoto la kuendelea zaidi au kumaliza hiki kisa ? Mungu ni muweza na yeye ndiye tegemeo letu sote.
Ni mimi: emu-three
5 comments :
Hitimisho ni zuri tu m-3, ni kweli ni refu lakini ni zuri halichoshi na linavutia sana kusoma. So please endelea this way taratibu hadi hapo tutakapofika mwisho inshallah. halaf nadhani hii ni sehem ya 17 na sio 18 maana iliyopita ni 16. Ahsante kwa kuandika na Mungu atakujaalia
we hadharani pls! whats happen to mhuja
Aisee watu wana vipaji...nakuamini kwa kweli..yaani kila nilipokuwa nikisoma uhondo ulizidi kuongezeka mpaka raha...mimi ushauri wangu usikatishe kwani utakuwa umekatisha uhondo ila kama unaweza kukatisha kwa namna ya kunogesha labda..na pia wala hitimisho hili binafsi halijanichosha...ni kweli Mungu ni muweza ...kila la kheri
naungana na Yasinta!
ni nzuri sana tuna subiri kitabu
Post a Comment