Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, January 4, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-70 hitimisho-14




Nilikuwa nimetembea kwa muda mrefu, katika jua kali, mpaka nikachoka, nakutamani maji, lakini sikuyaona hayo maji, na baadaye sana nikafika kwenye mbuga iliyojaa miti mirefu na hapo nikasema afadahli nimefika kivulini, na miti kama hiyo ni ishara ya kuwa kuna maji mahali, ….nikavuta hatua,…huku nikiomba mafanikio, nimpate mke wangu, kwani nina uhakika atakuiwa maeneo hayo hayo…kama nilivyoeleekzwa na mtabiri mmoja niliyekutana naye kabla, mtabiri huyo aliniona nikihangaika, aakniuliza shida yangu, nilipomuelezea akasema, nenda kupitia mlima ule, uvuke lile bonde ukatishe mbuga na nyika, hadi kwenye msitu wa matumaini, hapo utampata mke wako, …

Nikatembe kama nilivyoagizwa, nikavuka bonde na kukatisha mbuga, hadi kuufikia huo msitu wa matumaini, nilipofika hapo nikasema kimoyomoyo, sasa, nimefanikiwa,, nikaingia ndani ya huo msitu kwa matumaini huku nikimuwaza mke wangu ambaye aliniacha kwenye sherehe nakuniambia anakwenda kuchota maji, alipotoka hapo hakurudi tena, tukamsubiri kwa muda mrefu, baadaye nikaamua kutoka hapo kwenye sherehe kumtafuta, kwani watu wengi walidai kuwa wanawake wengi huwa wanapotea wakienda kuteka maji, na usipofanya juhudi ya kumtafuta mke wako, unamkosa moja kwa moja.

Nilipoingia ndani yam situ, nilijikuta nipo kati kati ya miti mirefu ajabu, na baada ya kuzunguka kwa muda mrefu nikafikia sehemu yenye upepo mkali, upepo ambao ulitanda kila mahala, na sauti kama ya kuvuma ilisikika na kufanya masikio yangu yaingiwe na ukungu. Ukungu huo ukanifanya niwe kama kiziwi, …hata pale nilipojaribu kuyapikicha masikio yangu, sikuweza kusikia vyema, hutaamini, hata huko kupikicha hayo masikio, nilikuwa nafanya kama hisia,,…maana mkono ulikuwa mzito ajabu….

Licha ya yote hayo, sikuchoka kutafuta kile nilichokuwa nikikitafuta, nikasogea mbele zaidi na kuangali huko na kule, lakini sikuona chochote, ilionekana kana kwamba nipo kwenye dunia yangu mwenyewe.

Mara kwa mbali nikaona taswira za watu, sikuweza kuwajua ni nani kwa umbali ule, nikaona nisogee mbele zaidi na kila nilipowasogelea niliona kama na wao wananisogelea, mpaka tukakaribiana, lakini cha ajabu nilichoweza kuona ni kama watu wale walionekana kufunikwa na kitu kama ukungu, kiasi kwamba sikuweza kuwaona sura zao vyema!.

Nilichofanya ni kupikicha macho yangu, ili labda kama ni sababu ya macho yangu kuwa na hali ya kutoona vyema, niweze kuona…, lakini haikusaidia kitu, nilichogundua ni kuwa pale mbele yangu kulikuwa na watu wanne, na wote wamesimama sio kwa karibu karibu sana, wameachiana nafasi. Na kingine nilichogundua ni kuwa watu hawo ni wanawake, lakini sikuweza kabisa kugundua ni wa rika gani, kwani ule ukungu ulikuwa umewaficha kiasi cha kutokugundua hilo.

‘Nyie ni nani na mnataka nini kwangu..?’ nikaweza kuwauliza, kwa sauti isiyoweza kutoa sauti, lakini cha ajabu walinielewa na sauti ikajibu, sauti hiyo ilikuwa sio ya kwako, ilikuwa suti tofauti isiyoelezeka kuwa ni ya kiume au ya kike, lakini ni sauti yenye kueleweka kabisa, ikasema;

‘Kwani wewe unafanya nini hapa..?’ akauliza.

‘Mimi namtafuta mke wangu..’ nikasema.

‘Unamtafuta mke wako, ….halafu unauliza nyie nani, huoni kuwa unayemtafuta ni miongoni mwa hao waliosimama mbele yako…ile sauti ikasema kwa mzaha. Nami nikapepesa macho kuzingalia zile taswira, nikasema;

‘Mbona siwaoni vyema, wamefunikwa na ukungu mwingi, nitawezaje kuwagundua kwa hali kama hiyo…’nikasema.

‘Hahaha ndivyo ilivyo, sio rahisi kumgundua mwenzako , ndivyo ilivyo hata katika maisha ya ndoa, kila mmoja hamjui mwenzake, na wengi hawajitahidi kuliondoa hilo tatizo, siri inabakia ndani ya kila mmoja wao, na hatimaye mnafikia hata kukosana, kwanini mnafanya hivyo, basin a wewe ni mtihani wako huo, ukifaulu basi utamuona mke wako…’ile sauti ikasema.

‘Mitahani gani huo, maana sijaelewa, naomba ufafanunuzi…’nikasema kwa mashaka na huku nikijaribu kuziangalia ziel tawira ambazo wakati mwingine niliona kama zinaongea na hata kusogea huku na kule lakini hazikuondoak mbele yangu.

Mtihani wako ni huu, unachotakiwa ni kuchagua kati ya hawo wanawake wanne, maana hapo mmojawapo ni mke wako,… ukampatia vyema umeshinda, lakini ukikosea na kuchague asiye kuwa yeye, basi mkeo hutampata tena,…’ ile sauti ikanyamaza.

‘Sijakuelewa …’nikasema.

‘Umenielewa ila akili yako haitaki kukubali ukweli, wewe chagua kati ya hao wanne, ukipatia umempata mkeo ukikosea basi hutaweza kumpata mkeo tena, …’ile sauti ikasema na ukimiya ukatanda.

‘Sasa nikimkosa itakuwaje, huoni kuwa nitakuwa nimetendewa isivyo haki..’nikasema kwa kujitetea.

‘Kwanini unajihami hivyo, hujiamini, …kama kweli unamtafuta mke wako kwa dhati, lazima ujiamini, …’ile sauti ikasema na kutulia kidogo, na kabla sijasema kitu ikaendelea kusema;

`Hata hivyo haki ipi unayoizungumzia, na haki ipi unayoitaka,…kama unamjua vyema mkeo, utamchagua bila wasiwasi, hakuna aliyekuzuia kumpata,…’ile sauti ikatulia tena, na kama vile ilijua nini kilichopo moyoni mwangu, ikasema kwa msisitizo;

‘Lakini hata hivyo wewe unadai haki, unajueje kuwa ni haki yako, huenda hiyo unayoiona ni haki yako, siyo haki yako, na huwezi kujua kwanini ikawa hivyo, huenda ni kwa manufaa yako,…na kama hivyo unavyotaka iwe hivyo, hakuna shida, wewe chagua tu, hakuna atakayekudhulumu, wewe unachotakiwa na kuichukua hiyo haki yako…chagua kati yao hawo wanawake, mmojawapo ndiye mkeo,..nina uhakika matokea yake ni kwa manufaa yako ya baadaye…na tusipoteze wakati, maana wenzako wanakusubiri..’ile sauti ikasema.

Nilichofanya ni kujaribu kufumba macho na kuomba, niliomba mungu anijalie ni mpate mke wangu, maana nimehangaika nyika na mbuga kumtafuta bila mafanikio na sasa nimepata nafasi ya kumpata bado najikuta na vikwazo, nikasogea na kunyosha mkono mbele nikiwa na maana huyo nitatake mgusa ndiye mke wangu, sikuwa na jinsi nyingine, sikuweza kabisa kugundua yupi ni yupi na wao walikuwa ahwatulii, mara huyu ksogea huku na yule kasogea kule, na mara mkono wangu ukamgusa mmojawapo….

‘Hebu mwangalie kama ndio yeye mkeo…’akasema yule mtu, nami nikamwangalia na sura niliyoiona ilikuwa tofauti nay a mke wangu.

‘Je huyo ndiye mkeo…?’ ile sauti ikaniuliza .

‘Hapana sio yeye..’nikasema kwa wasiwasi.

‘Kwahiyo umekosea…bahati mbaya sana, oooh, bahati mbaya ndugu yangu, kama nilivyokuambia awali ukikosea basi mke hutampata tena,…pole sana..’ile sauti ikasema na kuonyesha kuwa inafifia kama kuondoka, name nikauliza kwa haraka haraka.

‘Sasa nitafanyaje, ina maana mke sina tena, kwanini nifanyiwe hivyo…hapana, mke wangu nimefunga ndoa naye kihalali, kwanini nifanyiwe hivyo…’nikasema kwa huzuni.

‘Kumbuka kila jambo hufanyika kwasababu maalumu,… lakini kwa vile ulimpenda sana mkeo hatutakutupa , …utapata kile kilichokuwa sawa sawa na mkeo, usijali….’ile sauti ikasema na kutulia kimiya

‘Sijaelewa, kwanini..mnanifanyia hivyo…hapana, mke wangu Maua….’nikasema na mara kitu kama mtu anazibuliwa masikio kikasikika masikioni mwangu na mara nikahisi macho yakiingiwa na wmanga mkali, kiasi kwamba nilishindwa kuangalia na kufumba macho na baadaye nikayafumbua taratibu,…na cha ajabu kabisa, nikaona watu wamesimama mbele yangu, walikuwa wawili wamesimama kwa kuniangalia usoni na wawili wamesimama kushoto na kulia kwangu kuzunguka kitanda….

Niliona ajabu kubwa sana kwani waliosimama mbele yangu walikuwa wakifanana kwa kila kitu, kuanzia magauni , sura na kila kitu, lakini waliosimama kushoto na kulia kwangu walikuwa watu wazima, wakiwa ni wanawake. Na wote niliwaona wakipepesa midomo yao, na kila mmoja alijaribu kusema kwa hamasa fulani, lakini sikuweza kusikia nini wanachoongea, ule ukungu niliousikia kwenye ule msitu, ulikuwa umeniathiri kwa kiasi kikubwa sana.

Mara wale wanaofanana walinisogelea karibu na kinama kwa pamoja, ilikuwa kama mtu na picha yake, au mtu anajiangalai kwenye kiyoo, jinsi wale wanawake walivyofanana, na ilionyesha kuwa kila mmoja anachofanay na mwenzake anafanya hivyo hivyo, walinisemesha kitu, lakini sikuweza kusikia wanasema nini…

Nikajaribu kuwaambia wanipe maji ili nisafishe koo, maana nilikuwa na kiu, koo lilikauka kabisa, sijui ni kwasababu ya kule kuzunguka kwenye ule msitu kwa muda mrefu nikimtafuta mke wangu ambaye tena niliambiwa sitampaat tena, …kwanini nisimpate wakati ni mke wangu, hapana ile …ooh, najua sasa, ile ilikuwa ni ndoto tu, sasa nipo katika hali halisi, sasa nipo duniani, njozi inaweza ikawa kweli au si kweli…ingawaje katika kumbukumbu zangu, mara nyingi nikiota jambo la ajabu ajabu kama hilo huwa inatokea kweli….ooh, safari hii sio kweli …nikajipa moyo.

Wakati nahangaika kuonyesha ishara kuwa nataka maji, mara akaja mtu mwingine, huyu alionekana tofauti, mavazi yake yalikuwa meupe, kiasi kwamba yaliweza hata kuathiri macho yangu, nikayafumba kwa haraka halafu nikayafumbua ili niweze kumuiona vyema, na yeye akawa anafunua mdomo kama anaongea lakini sikusikia anachokiongea. Hali ili ilitia wasiwasi sana, na kuhisi huenda nimekuwa kiziwi.

Baadaye nikamwangalia huyo mtu mwenye mavazi meupe, kuona atafanya nini, nikiomba ajue shida yangu ya kuwa nina kiu, na sisikii…lakini cha ajabu alichofanya ni kuangalia ile kamba iliyoning’inia kamba hiyo ilionekana kutoka kwenye mwili wangu, sikujua imetokea sehemu gani, na mara akatoa sindani , na kuidunga kwenye kitu nisichokiona vyema, kwani wale wanawake wawili walikuwa wamesimama nyuma yake na kunikinga nisione alichokuwa akifanya huyo mto, kilichofuatia hapo , ni giza….

NB: Ndio nimerejea toka kuhesabiwa kama wengine wanavyoita, nikaona nifanye haraka kuhitimisha, lakini naona bado kidogo tumalizie kisa hiki. Nilipofika sehemu ya kujishikiza nikapata taarifa kuwa wiki hii nifungashe, kwasababu nilishajua hilo, sikukata tamaa, basi nimekuwa nikihangaika huku na kule, siunajua tena, watoto wanahitaji kwenda choo...riziki mtoaji ni mungu! Tupo pamoja

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel Siwa said...

Baraka iwe nawe daima ndugu wa mimi,kheri ya Mwaka mpya,Pamoja sana tuu ndugu yangu!!!!

emu-three said...

Na iwe nawe pia Swahili na Waswahili, Heri ya mwaka mpya. Tupo pamoja ndugu yangu.