Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, January 31, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-77 hitimisho-21




‘Doctor Rose…mmh, tunafurahi sana kukutana na wewe kwani nyie madaktari ni watu muhimu sana, na ni watu tunaowahitaji sana kule kwetu, mimi ni muwakilishi wa nchi yangu hapa India, na kukutana na wewe ni kama nimekutana na ndugu yangu,…’akanyosha mkono kumsalimia Rose na Rose akaupokea mkono wa shangazi na akatambulishwa kwa wengine na kusalimiana nao.

Yule jamaa aliyeonekana kama msemaje mkuu akaendelea kuongea na kusema `Kwani tukiwa huku nchi za nje tukikutana watu wa nchi moja ni sawa na kukutana wanandugu mliozaliwa na baba na mama mmoja au sio…’yule jamaa alianzia mbali, na hakujua kuwa kwa kufanya hivyo, alikuwa akimkera Rose, Kwa Rose alijua ni maongezi madogo tu, lakini alivyoona lile jopo la watu akajua hapo kuna muda mrefu utatumika nay eye hakuhitaji muda mwingi alikuwa na hamu ya kukaa na mgonjwa, amuone kwa macho yake akifunua macho amtizame, …..

Alipowaza hilo, akakumbuka jinzi alipoonana na huyo mgonjwa kwa mara ya kwanza, ilikuwa hivyo hivyo akiwa kazimia, alipofunua macho wakaangaliana , kuna hisia zilijijenga tangu siku hiyo, hisia ambazo kwakwe yeye aliziona kama chanzo cha mabadiliko katika maisha yake. Lakini alipoundua kuwa huyo alikuwa ni mume wa ndugu yake, aliona kama ndoto yake imepotea kabisa, ….hata hivyo mazungumzo aliyosikia kwa huyo mgonjwa yamemchanganya kichwa. Na hilo alilitaka kulijua haraka iwezekanavyo, sasa anaitwa tena huku na hawa watu, wangelijua kuwa hawana umuhimu kwake…..

‘Sasa Rose, Dakita Rose, kuna jambo muhimu sana tumekuitia hapa, sisi ni watu wa usalama, kazi yetu kubwa ni jukumu mlilotupa….’ Yule mtu akaawa anaongea lakini kwa Maua mawazo yalikuwa mbali, hata hivyo alijitahidi kumsikiliza.

‘Na tunafanya hili tukijali kodi zenu ambazo zinatoka kwenye mishahara yenu, lakini hata hivyo, hili jukumu ni letu sote,mimi na wewe, siwezi kufanya hii kazi kama sitapata msaada wako wewe na raia wema wengine, …bila msaada toka kwa raia wema, katu hatutaweza kufanikiwa katika kazi zetu…’akatulai kidogo na kumwangalia Rose kwa makini. Rose akajitahidi kumwangalia machoni, lakini baadaye akaangalia chini.

‘Docta Rose, hili nataka ulielewe kwa makini…’akasema na kuwageukiwa wenzake ambao walitingisha kichwa kumkubalia.

‘Unaona….’akasema na kumeukia yule dakitari mwingine aliyekuja na Rose na kumeukia Rose tena. Sisi watu wa serikalini, tunajivunia hasa tukifika nchi za wenzetu tukawakuta watu kama nyie,….tuna bahati sana, ndani ya nchi ya India tuna madakitari wetu mabingwa, wanafanya kazi kubwa sana….’akatabasamu na kuwaangalia wenzake huku akiendeela kuongea kwa kusema;

'Kwanini hawa watu wetu wasingelifanyai kazi hizo ndani ya nchi zetu, kwanini wewe Rose, usingelisomea ndani ya nchi yako , kweli hatuna vyuo vinavyotoa hayo masomo….?’ Akawa kama anamuuliza Rose, lakini hakuwa anamwangalia yeye akasema;

`Inafikia hatua watu wetu wanakimbilia nchi za nje…wanatafuta nini, elimiu, maslahi bora au kuna jambo jingine….ndio huenda ni maslahi duni, lakini sizani kuwa ni hilo tu peke yake…’akaeuka na kuwaangalia wenzake.

‘Kuna jambo kubwa sana ambalo tunatakiwa mimi na wewe na raia yoyote wa nchi yetu tusaidieani, na hili hatutasaidiwa na watu wengine hatutasaidiwa na India au Marekani au Ulaya, kwanza tunatakiwa kujisaidia wenyewe. ….’akatulia kidogo na kukohoa kama vile anarizika na kile anachokionea kuwa kaongea jambo ambalo ni muhimu sana.

‘Sikatai kusaidiwa n hilo hata Marekani au Ulaya wanasaidiwa, lakini tutaweza kusaidiwa endapo na sisi wenyewe tumejisaidia, na hili ni muhimu sana kwako wewe, na vizazi vijavyo…na hili ndilo tulilokuitia hapa, kuwa bila wewe, bila raia wema ndani ya nchi yetu hatuweza kufanikiwa kwa lolote lile, tutaishia kukimbilia kwa wenzetu na mwisho wa siku tutasutwa, tutachekwa , na hata kusimangwa na wenzetu,…’akaonyesha uso wa huzuni na kuwageukiwa wenzake huku akisema;

‘Hamjasikia watu wanapigwa vita na raia wa nchi wanapoishi, vijana wao hawana ajira wanaona raia wageni wanakwenda kufanya kazi katika nchi zao…..kwanini …’akamgeukia Rose na kumkazia macho. Rose akaangalia saa na kubetua mdomo, na alipoona huyo mtu anamwangalia yeye akamkazia macho na yeye kujifanya anamsikiliza kwa makini.

‘Najua wewe kama mtaalamu utaona nakupotezea muda, wewe kwako sasa hivi unafikiria wagonjwa, hapo ulipo unamfikiria mgonjwa wako, lakini na hili ninalotaka kukuambia hapa ni muhimu sana, lakini huenda hutaweza kulielewa kwa hivi sasa na kama nisipokupa mifano hai hutaweza kulielewa kabisa, na ndio maana nakuanzia mbali kwa mifani hai…’akawageukiwa wenzake na kusema;

‘Unajua siasa ni muhimu, ili kuzijenga nyoyo za hawa vijana, hawaelewi hilo , wao wamekongwa na tekinolojia, na nyenzo za kuwarahishia maisha, matokea yake wanapupika, kunakosekana hekima,…siasa ni hekima, hekima ya kumjenga mtu awe na subira , hekima za kujenga uzalendo, bila uazalendo hamtaweza kuzijenga nchi zenu….’akasema yule mtu. Wenzake wakatikisha vichwa kumkubalia na kama isingelikuwa ni hospitalini wangelimpigia makofi.

‘Sasa Rose, jambo kubwa ambalo wengi wanashindwa kulielewa na ambalo sasa ni donda ndugu katika nchi zetu za Afrika. Na watu wetu wanashindwa kuelewa kuwa hata hawo wenzetu wanapenda hiyo hali iwepo, wakiuma na kupuliza, ili wauze silaha, ili wapate ajira, ili wataalamu kama nyie mkimbilie kwao,…donda ndugu hili tunalisababisha wenyewe, ….kwasababu hatutaki kuelewa, hatuna muda wa kusubiri wakati wa shida, hatuna hekima, mioyo yetu imegubikwa na chuki za kibinafsi…tunachotaka ni tiba, badala ya kinga…, na bora ya kinga kuliko tiba, au sio docta…’akasema na kumgeukia Rose huku akwia akmkazia macho.

‘Saamhani, lakini…’Rose akaanza kulalamika.

‘Najau , najua Rose, unaona nakupotezea muda wako, lakini haya ninayokuambia hapa sio yako tu, hayataishai hapa kwako wewe tu, ni kwa ajili yako na wengine, ipo siku ujumbe huu ninaoutoa hivi leo utawafikia wenzako kuwa nilikuwambia hili, …unajua donda ndugu hilo ni gonjwa gani…?’ akamgeukia Rose na kumwangalia kwa makini.

‘Mmmm, wewe ni docta, huenda unafikiria nini nakizungumzia, gonjwa hili halihitaji mavyombo yenu, lakini cha muhimu ni kujua gonjwa hili ni gonjwa gani, ni kinyume cha amani. Ugonjwa wa kutokuwa na amani katika nchi unachangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha mendeleo yetu nyuma, badala kufikiri kutengeneza miuno mbinu, mnafikiria kununua silaha, kujenga maghala, kukodisha maaskari, na mambo mengi ambayo kama amani ingelikwepo, …tusingeliwaza hayo…’akasema na kuwageukiwa wenzake.

‘Amani haipotei tu kwa kupigana, amani pia hupotea kama nafsi hazijatulia….maisha magumu, maadui ujinga na maradhi, umasikini uliokithiri….vyote hivyo ni chanzo cha kuvurugika kwa amani…’akatulia na kuwaangalia wenzake kwa makini, halafu aaksema;

‘Kuna tatizo la uongozi, hasa atika nchi zetu, tatizo hili ni la kubeza nguvu kazi, serikali nguvu kazi yake ni raia wake, kama raia wana njaa, raia ni wagonjwa, raia hawapati huduma muhimu, unafanya nini kwenye hayo madaraka, achia ngazi, umeshindwa…kwasababu mtu ni kama gari, gari kama halina mafuta haliwezi kwenda, mtu bil achakula ataweza kufanay akzi kweli, hawezi, ndivyo ilivyo katika serkali, katika mashirika yetu, makampuni,kama hawatawajali wafanyakaz wao, wakawa na afya wasitarajie miujiza…’akawageukia wenzake kulia na kushoto.

‘Usione watu wanaingai misituni, wao sio wajinga, ….hilo inabidi viongozi wakae watafakari, kwanini, tuskimbiulie kusema wanaofanya hivyo wana uchu wa madaraka, hapana, tuangalie chanzo ni nini, utagundua hilo, kuwa hakuna amani katika mioyo ya watu,…ukiangalia kwa makini utagundua kuwa ni njaa, maradhi na haki isiyo sawa,…hakuna kingine….chunguzeni hilo, nawaambia….’akasema na kutulia tena halafu akamgeukia Rose na kusema;

‘Nazungumza hili kwasababu nyie watendaji ndio mihimili muhimu , ni watendaji lakini mtakuwa na madaraka maofisini mwenu, uwe dakitari, lakini kutakuwa na dakitari kiongozi, ..walimu, lakini kutakuwa na walimu viongozi, nakadhalika, kama kiongozi unatakiwa ueelwe hilo, kuwa unaowaongoza, sio watumwa, ni watu , na watu kama wewe, ….kama unatembeela gari na wao wanahitaji pia, kama unakual vizuri na wao wanahitaji kula vizuri, ….na kama watoto wako wanasoma shule za kimataifa,kwanini usiwasaidie na wafanyakazi wako, watoto wao wakasoma angalau shule za kati na kati na kati….ubinafasi unaanzia hapo, umimi, na kujenga matabaka…’akaonyeshea kwa mikono .

‘Kwahiyo viongoz wanatakiwa walielewe hilo, na wewe raia mwema , mtaalamu uwajibike katika sehemu yako ili hayo yasiwepo, kwa kufanya hivyo utakuwa umeijenga amani…na ili kufanikiwa hilo, tunatakiwa tuwe kitu kimoja, tuwe raia wema, tuwe wazalendo, ili hapa kukiharibika, tuwe pamoja kupajenga , kwani nalawa yetu ni moja, …kukiwa na matundu tutazama sote…hilo ni muhimu kulijua, sio kwa vile wewe ni kiongozi au raia wa kawaida hutohusika,…hapana.’akasema na kwa msisitizo huku akimwangalia yule docta mwingine, ambaye alikuwa akipitia majalada mbali mbali na kuyatengeansiha katika mafungu mawili.

Yule jamaa alipomuona yule docta mwingine hamuangalii akamgeukia Rose na kusema;

‘Sasa Rose, amani hujengwa na mimi na wewe, bila wewe kazi yangu haitaweza kukamilika, nakuomba tushirikiane kwa hili, hapa namkabidhi mwenzangu mtaalamu wa mambo hayo aendelee,… samahani kwa kukupooteze muda wako, muda wenu, ila mimi ni mtu wa usalama, lakini katika kitengo cha siasa na utawala bora, ndio maana nikawa muongeaji sana, lakini ni kwa manufaa yako, …ngoja mwenzangu akuhoji halafu kama una swali, utaniuliza, hasa kwanini nikakuambia haya yote…’akawa aanongea kwa haraka kama vile anataka kuondoka kuwahi jambo fulani, lakini badala ya kuondoka akamgeukia mwenzake na kuinama kidogo kama kumkaribisha.

Rose akachoka, maana alijua huyo atamaliza kila kitu, kumbe ndio kazi imeanza, akatulia na kumwangalia kwa makini huyo mtu mwingine aliyekaribishwa, hata ukimwangali huyo mtu mwingine alivyojengeka, utakua tu kuwa huyo ni askari….akatulia na kusubiri nini ataulizwa, au ni siasa kama za huyo aliyepita, akasubiri…

‘Shukurani mkuu wangu, hayo ni mambo ya kisiasa, sasa hapa kwangu ni utendaji mtupu, nakuomba Rose uwe huru, na ujisikie kuwa upo na ndugu zako, na lengo letu ni moja, kuleta amani ndani ya nchi yetu, najua wengi mnataka hata kuikimbia nchi yenu kwasababu ya uzaifu huo, sisi tupo bega kwa bega na nyie tumeapa kuilinda nchi yetu, hatutakuwa wasaliti wa nchi yetu , sisi ni wapiganaji kama ulivyo wewe…’akasema huku anafungua jarida lililopo mbele yake.

‘Unajua wewe Rose ni mpiganaji mwenzetu, nafikiri unalijua hilo,….’akatulia kidoo bila kumwangalai Rose, akiwa anaangalai ukurasa ndani ya lile jarida, na kabala Rose hajasema kitu akasema;

‘Rose sasa nitakuuliza maswali machache naomba uyajibu kwa ukweli wa dhati na ukiwa huru na ukijua haya ni kwa ajili ya kulimaliza hilo tatizo ambalo mkuu wetu kaliita donda ndugu, ni tatizo kubwa , lakini ni dogo kama tukishirikiana, …mimi nikiwa an dhima ya dhamana niliyopewa ya kuilinda na kuitetea nci yetu, ….dhima hiyo kakabidhiwa kila mtu, au sio…..? ’akasema huyo mtu mwingine sasa akimwangalai Rose usoni.

Rose alipona kaangaliwa sana usoni, akajua hapo anatakiwa kujibu kitu, akasema kwa sauti ya kuchoka;

‘Sawa Mkuu, nitajibu kama ninavyojua, na kwa kadri ya ufahamu wangu,….’akasema Rose na kugeuka kumwangali yule dakitari ambaye naye alishajichokea kwani hawakuzoe hali ya kukaa na kuongea tu, wamezoea kukimbizana huku na huko kuwahudumia wagonjwa….

‘Rose unamfahamu Docta Adamu..?’ swali lilikuja haraka bila kutegemea kuwa muulizaji angeuliza swali kama hilo mapema hivyo, na liliulizwa kama mahakamani, na kichwani kwa Rose, akawa anawaza mengi, kuhusiana na hilo swali, je huyo docta Adam kakamatwa au amekufa, na vyovyote iwavyo kwanini wamuulize yeye hilo swali….akatulia kidogo halafu akaona haina haja ya kupoteza muda kwa kuuliza swali kwenye swali.

‘Ndio namfahamu….’akasema Rose akijua swali gani litafuta baadaye.

‘Hebu tusaidie ufafanuzi, unamfahamu kivipi,….?’akauliza huyo mtu wa usalama, na kwa vile Rose alishajua kuwa hilo swali litafuata, akaona ajibu kwa sasa kwa ufafanuzi ili kuondoa mlolongo wa maswali mengine baadaye.

‘Namfahamu kwasababu alikuwa bosi wangu katika hospitali niliyokuwa nikifanyia, na kwa nje tulikuwa marafiki wa kawaida, sio urafiki wa kipenzi, hapana, ni marafiki waliozoeana kwasababau ya kuwa pamoja katika shughuli za utendaji na kwahiyo ilifiki ahatua tukawa tunasaidiana katika hili na lile…ndivyo ninavyoweza kusema hivyo…’akasema Rose.

‘Sawa kabisa umejibu vyema, je katika mazoea yenu, ulimuonaje docta huyo , hakuwa na mambo mengine ya ziada nje ya kazi yake, nakuuliza hili kwa haraka ili tusikupotezee muda, na wewe tujibu kwa ufafanuzi kwa kadri unavyojua, ili tusaidieni kwa hili, ni muhimu sana kwetu, na kwa taifa lako na vizazi vya nchi yetu, sizani kuna mzazi au raia yoyote anayeifurahia hiyo hali, kwanini tusiishi kwa amani, eti Rose….’kabla hajasema zaidi simu ikaita, na jamaa akaipokea na kusema;

‘Saamhani kidogo Rose, huyu mtu ni muhimu sana, ….anahusiaa na hili, ..’akaipokea ile simu na kusikiliza kwa muda, halafu akamgeukia Rose, na kusema;

‘Natumai unamfahamu Inspekta yule wa nchi jirani, anataka kuongea na wewe kidogo….’akamkabidhi Rose ile simu, na Rose kwanza akasita kuipokea, na baadaye aaknyosha mkono na kuipokea kwa mashaka kidogo , halafu akaiweka sikioni kama vile hataki kuisikia hiyo sauti, na kuanza kuisikiliza hakusema halooh, akatuia kusikiliza kwani muongeaji alikuwa keshaanza kuongea jambo….

‘Rose, mimi ni Inspekta, nimekupigia hii simu kupitia hawo jamaa zenu wa usalama, hawo nilikuwa nikifanya kazi nao kwa karibu sana, ni watu wa kuaminika,…natumia neno wa kuaminika, kwani kama unavyoelewa ilifikia hatua hatujui nani umwamini na nani usimwamini, lakini kwa hali ilivyo sasa, mambo yanakwenda vyema, nakuomba sana, wape ushirikiano wako,…’akatulia muongeaji kwenye simu kidogo.

‘Sawa inspekta, lakini, mimi sijui lolote zaidi ya …..’akaanza kujitetea Rose.

‘Hicho hicho kidogo unachokijua, unavyohisi, na ulivyomuona, …. waambie wao ni wataalamu wa ammbo hayo, nakuambia hivyo kwasababu tumegundua kuwa Docta Adam, yupo nyuma ya mambo mengi yaliyotokea hasa kuhusiana na mgonjwa na pia anakuandama sana wewe kwa namana ambayo mwanzoni tulifikiria ni mapenzi …lakini tunahisi ni zaidi ya mapenzi, kwahiyo kwa usalama wa mgonjwa wenu, na usalama wako, na usalaam wa taifa lenu, toa ushirikiana kwa kila watakachokuuliza….sawa Rose…?’ akauliza huyo Inspekta.

‘Sawa, nitatoa …lakini kama nilivyokuambia, sina zaidi ya jinsi watu wanavyofikiria, mipaka yangu ilikuwa kwenye kazi tu….’akasema Rose na kutulia huku akiwajaribu kuwaangalia wale watu waliopo mle ndani, na alipogeuza macho yake pembeni akagundua kuwa kumbe kulikuwa na mashine ya kunasia sauti, ina maana kila wanachokiongea kinanakiliwa kwenye hiyo mashine.

‘Rose nikuambie jambo moja, katika uzoefu wangu, vita uhasama na chuki, kulipiziana visasi havijengi kamwe, nimewashauri wenzangu hawo, kuwa hata wakiwashika hawo watu, wawe na baraza la mariziano, ni vyema hata ujumbe ukamfikia huyoo Docta Adamu, kuwa suluhu, ipo, ajitokeze watu wariziane, kama anataka kujiuna kweney vyama vya siasa, kama ana dukuduku,basi watu wake yaishe, amani ni muhimu sana katika mataifa yetu haya….’akasema muongeaji kweney simu.

‘Nimekuelewa sana Inspekta…..’ akajibu Rose, huku akijiskia vibaya, kwani midume yote iliyokuwemo humo ndani ilishaanza kumchefua…akamkabidhi huyo mtu wa usalama ile simu ambaye aliendela kuongea kidogo na huyo mpigaji simu, halafu akairudisha ile simu kwenye mfuko wake na kumgeukia Rose.

‘Huyu jamaa ametusaidia sana, na hivi tunavyoongea yupo nchini kwetu, anamalizia baadhi ya kazi, na ndio maana akaamua kukupigia, naomba tuendelee na mahojiano yetu, ni maswali machache tu , tukimaliza hapa tutajua nini la kufanya….wewe ongea kile unachokifahamu, hatukulazimishi kwa jambo ambalo unaoana litakukwaza, lakini angalia faida na hasaar yake, …..’akasema yule mkuu na Rose akainamisha kichwa kuashiria kuwa hajisikii vyema, na mwenzake ambaye ni dakitari akaligundua hilo akamsogelea na kumgusa Rose begani…

‘Upo safi, kama hujisikii vyema sema, nakuona kama … sema, tuahirishe kidogo, usiwe na wasiwasi kuhusu mgonjwa, sasa hivi nimepata habari kuwa kazindukana nimemtuma msaidizi wangu akahakikishe mambo yanakwenda vyema, maana siwezi kuondoka hapa bila kuhaikisha kuwa hawa watu hawakusumbui….mgonjwa anaonega na familia yenu, usihofu kwa hilo…’maneno yale yalimuongezea nguvu Rose, akaanza kujisikia vyema, na kumpandisha hamasa Rose na hapo akaanza kuongea kila kitu anachokijua kuhusu dakitari Adam.

*********

‘Hivi mbona Rose amekawia kurudi….?’ Akauliza Maua.

‘Kwani amekwenda wapi…au ndio kaamua kuingilia kazi, maana hawa watu wanaopenda kazi zao, wanaweza wakajitolea popote pale, huenda kweli yupo kwenye kazi ya kuangalia wagonjwa…?’ akauliza shangazi kwa utani.

‘Aaangalie wagonjwa kwani hapa hospitali kwake, yote aliyofanya hapa haikuruhusiwa alitoa kama msaada tu…’akasema Maua.

‘Sasa kama isingelikuwa yeye huoni wenzake walishakata tamaa…’akasema shangazi.

‘Tatizo hapa wana wagonjwa wengi, kwahiyo docta anahitajika kumhudumia huyu na akiona kazi yake kamaliza anataka amfuate mwingine, na hivi vipimo wakati mwingine wasivitegemee sana, mimi inanitia wasiwasi , kama ndio hivyo, watamuua mgonjwa kabla sio siku zake, maana watatoa kila kitu, kumbe bado alihitaji muda….’akasema Maua

‘Hiyo kama ni kutokea ni mara moja kwa bahati…na kama mtu kandikiwa kufa atakufa tu, kama sio siku zake, itatokea kama ilivyotokea hapa….’akasema shangazi.

Mara mama akarudi, alionyesha uso wa wasiwasi kidogo, na alipofika pale waliposimama wenzake, akawa kama anawakwepa wasimuuliza maswali, na kukimbilia kumtizaam monjwa pale alipolala, akainama karibuna uso wa mgonjwa kama kazindukana, alipoinama kumtizama machoni, akainua kichwa haraka na kumgusa wifi yake kwenye bega;

‘Wifi hivi Rose hajarudi anafanya nini wakati wote huko, mimi nahisi kama magonjwa keshazindukana , ukimtizama machoni ingawaje kayafumba, lakini yanaonekana kucheza cheza, hebu tumuuiteni ajae amtizame,….’akasema mama.

‘Si aliitwa kwa hao watu wa usalama, isije ikawa yamegeuka ya usalama na kuwa mengine..naona hata yule dakitari alikuwa akimwangalia Rose kwa jicho la kimahaba, naingiwa na wasiwasi sasa….’akasema shangazi kwa utani.

Mama ambaye ndio alikiuwa karudi huko alikokuwa katoka kusikiliza simu yake baada ya kupigiwa na kuamua kwenda kuipokelea nje ya hiyo wodi maalumu, kwani haparuhusiwi kupokea simu humo ndani akakunja uso kuonyesha hakupendezewa na hayo maneno aliyozungumza wifi yake akasema;

‘Huyo docta kama alimwangalia kwa macho ya mahaba kachelewa, kama ni macho ya mahaba akawatizame manesi wake, mbona nimeona wasichana wengi warembo humu ndani tu, ….nafikiri kuna jambo huko, inabidi tutafiti kuna nini….’akasema mama.

‘Tutatafiti kwa vipi unajua wapi hiyo ofisi ilipo, basi fuatilia….’akasema Maua huku akimwangalia Mgonjwa .

‘Kwanza tuambie hiyo simu uliyokuwa ukiisikiliza ina heri maana ulivyokuja ulionyesha kuwa na wasiwasi sana…?’ akauliza Shangazi.

’Sijui kama kuna heri au la…, ila nahisi kuna jambo, ….mmh, ndio mume wangu alikuwa akinifahamisha kuwa keshafika, na ameniagiza nimalizie baadhi ya kazi alizokuwa kaziacha, ili zikikamila nirudi na mzigo, maana yeye hatapata muda wa kurudi huku kwa sasa , …na atanipa maelekezo mengine baadaye, kwahiyo nihitajika kuondoka …nasubiri huyu mgonjwa azindukane tu, nikawajaibike, …..yeye hakusema zaidi kuhusu kuwa kuna tatizo huko, ila sauti yake iliashiria kuwa kuna tatizo…’akasema mama.

‘Kwanini usimuulize kuwa kuna tatizo….?’ Akauliza Maua ambaye alionekana kuvutiwa na hayo mazungumzo ya mama yake.

‘Wewe unanioje mimi, unaniona kuwa na akili za kitoto,…’akacheka kwa kebehi halafu akasema;

‘Nilimuuliza ndio, na aunajua nini alichokisema; ‘hakuna tatizo lolote, wewe fanya niliyokuagiza haya ya huku hayakuhusu…’akasema mama na kugeuka pembeni kama vile anaona aibu kuzungumzia mambo ya mume wake.

‘Mama samahani nikuulize swali moja, hivi kweli mna mahusiano mazuri wewe na huyo baba, maana unavyoongea hapo inaashiria kutokuelewana kwa namna fulani, au nimekosea..?’ akauliza Maua
Mama akacheka tena kwa kebehi , halafu akamgeukia Maua na kumtizama machoni, hakupenda kulijibu hilo swali, na pia hakupenda kumvunja binti yake ambaye hakuwahi kulelewa na yeye, na asingeliepnda amuelewe vibaya, akasema;

‘Mambo ya baba na mama ndivyo yalivyo, leo utaona watu wanaongea vyema na utaishia kusema hawa watu wanpendansa sana, kesho inakuwa vinginevyo, lakini mwisho wa siku itaishia kukubali ukweli kuwa hayo ndio maisha ya ndoa…’akatulia kidogo, akijau hapo hajajibu swali la binti yake, akauka kumwangalai wifi yake, kama vile anaomba msaada, lakini kabla hajatulia vyema akasema;

‘Siwezi kusema hakuna maelewano kati yangu na mume wangu, usiwe na wasiwasi na hilo binti yangu, kuna kushuka na kupnda hayo ni ya kawaida. Binti yangu, wewe ndio umeingia kwenye ndoa…najua ulishaisi na mume wa awali, na sasa ndio umempata mwingine, kama nilivyosikia juu juu, utakutana na maisha kama hayo, na kukitokea migongano, usikate tamaa ukiona unajibiwa vibaya, au unaweza hata uisjibiwe ukiuliza swali, usitaharuki, ndivyo maisha ya ndoa yalivyo….’akasema mama na akakatiza waliposikia sauti ya kuhema ya mgonjwa.

Maua haraka haraharaka akamgeukia mgonjwa na kuinama kumtizama usoni, alipotua macho yake usoni mwa mgonjwa akashituka na kupepesa macho yake, kwani alijikuta macho yake yakiangaliana moja kwa moja na macho ya mgonjwa, ….aakhema kwa nguvu, na hakugeuka au kupepesa macho yake, akaendelea kumwangalia mgonjwa, na kwa muda wakawa watizamana,….

Na hali ile ikamkumbusha siku walipokutana kwa mara ya kwanza, siku walipotupiana jicho katika basi la daladala, akatabasamu na mgonjwa naye akajitahidi kutabasamu….na wakati huo huo mama ambaye naye alishaiona ile hali, akakimbilia nje kumuita docta, …..

NB. Kwa leo inatosha, kama nimeacha sehemu tuambizane, maana ndio tunamaliza maliza. Neno la siku ya leo;Amani ya kweli hujengwa toka nyoyoni, kama ulivyo upendo wa kweli . Hata kama hakuna vita vya silaha, lakini kukiwa na vita vya nafsi, amani itakuwa kama kitendawili….Ni hayo tu wenzangu tupo pamoja.

Ni mimi: emu-three

Thursday, January 26, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-76 hitimisho-20




‘Hivi kweli huyo docta Adam mumeshindwa kumkamata, anaweza kutupotea kirahisi hivi, na mbona hospitali yake inafanya kazi, inaendeshwa na nani, maana naona ipo inafanya kazi kama kawaida, lazima kuna mtu yupo pale ambaye anawasiliana naye, hatujafanya uchunguzi wa kutosha…’akasema mkuu wa polisi.

‘Mkuu uchunguzi wa kutosha umfanyika, na kumbukumbu zinaonyesha kuwa , Docta Adam, alishaondolewa kwenye uongozi wa juu wa hiyo hosptali, na alishawekwa mtu mwingine, kwahiyo kutoweka kwake kumetokea baadaye, na wao wanahisi hakupenda kuondolewa, ndio maana baadaye aliandika barua ya kuacha kazi, lakini wadhamini wa hospitali hiyo wakakata….’akaongea askari wa kitengo cha upelelezi

‘Walipokataa ndipo akaondoka, au ilikuwaje mpaka akatoweka kwenye hiyo hosptali…?’ akauliza mkuu wa kituo.

‘Kutoweka imetokea akiwa likizo, yeye alichofanya ni kuomba likizo yake ya mwaka, alipoidhinishiwa haikujulikana alisafiri kwenda wapi, kwani kwa jinsi inavyoonekena hayupo hapa nchini… na sisi tuliposikia kuwa huko India kuna watu wetu tukafikiria huenda ndiyo yeye, lakini kwa maelezo tuliyoyapata sio yeye kabisa, lakini kwa uhakika tukataka tuwakamate wote wale ambao wapo India kwasababu kwa taarifa tulizopewa, wamekuwa wakijihusisha na ugaidi…’ akasema huyo mpelelezi.

‘Na ugaidi….?’ Akashituka huyo mkuu.

‘Ndivyo walivyotuambia, unajua neno ili ugaidi limekuwa likitumiwa kila mtu anapofanya mambo makubwa nje ya ncho yake , hasa yakihusiana na uvunjaji amani, kuhatarisha maisha ya watu….sasa hawa watu wamesadikiwa kuwa walikuwa nyuma ya mambo hayo, lakini walifuatiliwa kwa karibu sana na wao walipogundua kuwa wanfuatiliwa wakaacha hicho walichokuwa wamepanga..’akasema huyu mpelelezi.

‘Sasa ikawaje, hawo watu wapo wapi maana nimeambiwa hamkumpata hata mtu mmoja hapo uwanja wa ndege imekuwaje?’ akauliza mkuu wao.

‘Ni ajabu kabisa maana picha na kila kitu cha hawo watu tunazo, lakini abiria wote waliotoka kwenye hiyo hakuna hata mtuu mmoja anayefanana na hizo picha, tulishindwa kabisa tumkamate nani, lakini watu wetu wanawashuku baadhi ya abiria waliokuwemo humo na wanafuatiliwa kwa karibu, lazima tutagundua jambo, tunahisi kama watakuwa waliteremka njiani , hawakufika huku moja kwa moja, sijui watakuwa waliteremkia nchi gani, tunajaribu kutafuta mawasiliano sehemu zote ambazo ndege hii ilisimama…’akasema mpelelezi huyo.

‘Vituo vyote hivyo havikuweza kuleta maelezo yoyote ya maana, kwasababu kwa maelezo yako unayotoa hapa umefanya ndege kama gari, na nijuavyo ndege kutoka India haina vituo vingi...au..?'akasema mkuu huyo akiwa anakagua zile taaarifa.

‘Ni kweli hakuna vituo vini na kote huko wametuambia kuwa hakuna mtu kama huyo aliyeteremka kwenye kiwanja chochote, na isitoshe mbona watu kama hawo hawakuonekana kuondoka na ndee hiyo iliyotoka India,…maelezo haya yalituchanganya kidogo, ikabidi tuwasiliane na wenzetu huko India , wao wakasema wana uhakika na hilo, labda kama kuna njia nyingine walitumia, lakini wao wana uhakika abiria hao walipanda hiyo ndege…’akasema mpelelezi huyo.

‘Hapa naona kuna kuchanganyana, nahisi kuna jambo limefanyika, kwasababu haiwezekani watu hawo waonekane upanda hiyo ndege na ghafla wayeyuke…fanyeni uchunguzi wa kina hakikisheni abiria wote waliopanda hamo mumewafauatilia kwa karibu, hilo mumelifanya?’ akauliza mkuu.

‘Hilo tumelifanya na ndio maana watu wetu wametawanyika kila sehemu kufuatilia nyendo za abiria ambao walitoka India, ni kazi ngumu kidogo, maana wapo wengi, lakini shabaha yetu imewalenga wanaume na wale ambao wanasifa zinazokaribiana na hawo watu tunaowatafuta…’akasema huyo mpelelezi.

‘Safi, sasa hata hivyo hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kutusaidia kwa hili, yaani mtu ambaye alikuwa karibu sana na huyo dakitari…?’ akauliza mkuu huyo.

‘Kuna watu wawili, kwanza mkuu, tulikuomba umuombe Inspekta yule wa ncho jirani aje kutoa msada, kwani swala hili ndiye tangia awali alikuwa nalo, anaweza akatupa msaada mkubwa, ….’akasema huyo mpelelezi,

‘Hilo tumeshalifanya, lakini ukumbuke kuwa yule sio raia wan nchi hii, kwahiyo kibali chake mpaka kikubaliwe ni maswala makuba ya kiserikali, hata hivyo kwa vile serikali imelipa hili jambo kipa umbele, wakiwa na lengo la kuondoa haya matatizo haraka, basi huenda kwenye wiki hi atakuja…najua ana masaaa mkubwa sana, lakini bado sisi wenyewe hatujashindwa, kwani nimeulizwa, ina maana sisi kazi hiyo imetushindwa….hatujashindwa, ila tunahitaji baaadhi ya maelezo ambayo hayajajitosheleza, au sio, na kuachia huyo hakuna mtu mwingine….’akauliza mkuu wakituo.

‘Kuna binti mmoja ambaye alikuwa akifanya akzi na huyo docta, ingawaje walikosana naye na kuacha kazi inasadikiwa kuwa huyo docta licha kuwa walikuwa wakifanya kazi naye na huyo binti alikuwa msaidizi wake, lakini pia alikuwa mpenzi wake…tunasadiki kuwa huyo binti anaweza akatupa msaada wa kutosha, lakini hapo hapo ndio maana tunamuhitaji huyo Inspekta kutoka ncho ya jirani, kwani unakumuka karibuni alitupigia simu kuwa alikuwa akiwasilina nao…..’akasema huyo mpelelezi.

‘Hapo nimekuelewa, na kweli lazima huyu Insepkta tumuombe aje, na pili lazima huyo binti tuwasiliane naye, ikibidi aitwe, kwasababu ni raia wetu na anaweza kuleta mchango mkubwa, na mna uhakika hana mahusiano na hilo kundi kisirisiri….?’ Akauliza mkuu huyo.

‘Hapana, hayo yote mwanzoni tuliamini hivyo, lakini baada ya uchunguzi wa kina tulithibitisha kuwa hahusiki, na ndio maana kwa ushaurii wa Inspecta, tuliamua tumtumie yeye kama chambo ili tuweze kuwakamata hawo wahusika, kwani walionekana kumfuata fuata sana huyo binti, na unakumbuka jamaa wale wa msituni walioamua kurudi serikalini walivyosema, kuwa huyo binti anawindwa na maadui, sasa hatukujua ni maadui gani, ndio maana tukamtumia yeye kama chambo….na hilo ndilo lililotusaidia kumgundua Docta Adamu, kuwa ana mafungamano na kundi hili la ajabu…kundi ambalo liliamua kuendeleza mapigano ndani ya mji….’akasema huyo mpelelezi.’

‘Kwanini walikuwa wakimtafuta sana huyo binti, hamkuligundua hilo….niliwaagiza mtafute sababu ilikuwaje hamkufanikiwa …?’akauliza mkuu

‘Sababu kubwa iliyoonekana mwanzoni , na natumai waliitumia kama kiini macho , ili ionekane kama ni sababu ya kimapenzi, maana ilivyobainika awali ni kuwa Docta Adamu, alikuwa akimpenda huyo binti, na huyo binti akawa hana mapenzi nay eye, alionekana kumpenda au alikuwa karibu sana na huyo mgonjwa aliyepelekwa India….’ Akasema yule mpelelezi na kutulia kidogo, kumpa nafasi mkuu wake kuoanisha hayo maelezo yake na taarifa iliyopo mezani kwake.

‘Baadaye huyo mgonjwa, ambaye watu walikuja kuamini kuwa ni mume wa huyo binti, kumbe sio mume wake, tulichobaini ni kuwa Docta Adam, alishampenda huyo binti na alipoona huyo binti yupo karibu sana na huyo mgonjwa akajenga wivu, na ndio chanzo cha kutaka kumuondoa huyo mgonjwa duniani, kama unakumbuka ile taarifa yangu ya mwanzo…’akasema huyo mpelelezi.

‘Sizani kama ni mapenzi tu, hilo tuliliwekea ulizo, na niliwaambia mjaribu kufanya uchunguzi kama tunaweza kupata sababu nyingine,….je hilo mlifikia wapi, maana sioni lolote kwenye hii taarifa…?’ akauliza huyo mkuu na kabla hajajibiwa hilo swali akaendelea kuongea kwa kuuliza swali jingine ;

‘Na huyo mgonjwa anaendeleaje, kuna taarifa yoyote toka huko India, …kwani nilipata taarifa nyingine zenye utata kuhusiana na uraia wa huyu mtu, je uchunguzi haujabaini kuwa ni raia wetu au ni raia wa nchi gani?’akauliza mkuu.

‘Mpaka sasa anaonekana ni raia wetu, lakini familia yake haijabainika ni ipi, kitu cha kushanagaza ni kuwa watu wa karibu waliokuja na kwenda kumsaidia huyo mgonjwa ni raia wa nchi jirani, na hii inaweza ikatufungua macho kuhusiana na uraia wa huyu mtu, na hili pia bado linamuhitaji jamaa yetu, tunahitaji msaada wa huyo Inspekta, nahisi atakuwa kagundua jambo ambalo hakuliweka wazi…’akasema mpelelezi.

‘Haya cha muhimu kwa sasa ni kuwasilina na huyo binti, unasema anaitwa jina gani, mmh, Rose au sio.., fanya kila iwezekanavyo tupate maelezo yake, ukumbuke hii ni kazi yako muhimu ukifanikiwa kwa hili utaoana matunda yake, mimi nitawasilina na huyo Inspekta kwa simu, na ninafanya mpango wa kumuomba aje huku kumalizia kazi yake…ingawaje hatujashindwa kwa hili, lakini yeye ni mtu muhimu sana kwetu…sawa tutawasilina baadaye, hakikisha sasa hivi unawasilina na huyo binti nani vile vile…

‘Ndio mkuu, nitawasilina na huyo binti anayeitwa Docta Rose.

*********

Rose hakuamini kuwa mtu aliyempenda ndio siku zake zimefika, akamsogelea na kumshika shingoni, akaondoa mkono haraka, ilikuwa kama mtu aliyeshika kaa la moto, akageuka kumwangalia Maua ambeya likuwa kamshikilia mkono huku akiwa kafumba macho, ikiashiria kuwa bado yeye alikuwa kwenye kuomba, na utafikiri hajasikia docta alichosema;

‘Sasa mumeamini, mashine yote inaonyesha kuwa uhai haupo,m safari nashukuru kuwa mpo na siono umuhimu wa kusubiri tena, lakini kama huamini docta Rose, nakuachia muda wa kufanya miujiza yako tena, kwani umesema ilishatokea mara nyingi ukiwa naye, mimi inabidi nitoke kidogo, kwani nina mgonjwa mwingine….’akasema na kuanza kuondoka.

Rose akatizama mashine na kila kitu kitu kilionyesha kuwa mambo yamekwisha, lakini hakukata tamaa, alipomshika shingo na kuona ujoto wa uhai upo, akaingiwa na ujasiri , akijua hiyo siyo mara ya kwanza kupambana na huyo mgonjwa,….akamsogelea na kuweka shavu karaibu kabisa na mdomo, ….akainua kichwa na haraka, na kwamangalia Maua.

‘Maua mbona siamini….mashine ianyoneyesha vingine, lakini mgonjwa huku anaonekana kabisa….’hakumalizia, akainuka na kushike ile mipira inayotoka mwilini mwa mgonjwa, akashikwa na mshangao, maana ile mipira ilikuwa imeachia kabisa ina maana hakuna mahusiano kati ya mashine na mwili wa mgonjwa….

‘Ohh, mbona hivi, …..’akashangaa, akaivuta ile mipia yote miwili akagindua imeacahia kabisa, akamsogela mgonjwa na safari hii karibu adondoke kwa mshituko, kwani alichoona kilimfanya atoe macho ya kutokuamini….

Maua alikuwa kakodo amacho kumwangalia mgonjwa, naye alikuwa kshikwa mshangao ule ule aliokuwa nao ndugu yake, hakuamini alichokuwa kakiona, na wote wkageuka kuangaliana, na kabla hajawasema kitu wakgeuka kwa pamoja kumwangalia monjwa, wakakuta kinyume na walivyoona mwanzoni.

‘Alikuwa kafumbua macho…nina uhakika huo..;akasema Maua

‘Ndio alikuwa kafumbua macho, sasa nahisi karudi kwenye usingizi, kuna kitu kinanipa wasiwasi, kwanini hii mipira haijaunganishwa na mwili wa mgonjwa, nina uhakika docta aliondoka ikiwa haipo hivyo..’akasema Rose

Rose kabla hajapata jibu akatoka mbio kumwahi docta kwani kulikuwa na dawa zilihitajika na pia hakutaka kabisa docta atoe taarifa yoyote kwa wazazi wao, na alipofika mlangoni akamuona docta anawakaribia wazazi wake, hakutaka kutoa sauti, akamkimbilia na alipomkaribia akamshika mkono , na docta akashituka kuona mtu anamshika mkono na wakati huo alishajiandaa kuongea na ale wazazi ambao walikuwa wameshikwa na butwaa..

‘Docta twende ndani haraka, nataka ukanipe dawa, mgonjwa anahitaji dawa…’akasema Rose.

‘Mgonjwa gani huyo….’akasema Docta kwa mshangao.

‘Wewe twende ndani haraka, hakuna muda wa kuulizana maswali,….wewe unauliza jibu, kwani tulikuwa na wagonjwa wangapi…’akasema Rose huku akimvuta Docta mkono kuelekea ndani. Na yule docta akamfuata huku haamini alichosikia. Akawa anajiuliza ina maana yule mgonjwa kazindukana tena, kweli huyo mgonjwa ana roho saba, ….

Mama na shangazi safari hii hawakukubali wakaamua kuwafuatilia nyuma Rose na Doctor, na bahati nzuri mlinzi alikuwa akijishughulika na mambo mengine kwa vile alikuwa anajua kuwa docta anaonea na hiyo familia, na alipoona wote wanamfuata Docta nyuma, akajua labda wote wameitwa kuingia huko ndani, wakapita mlangoni bila kuzuia na hata alipofika ndani ya ile wodii maalumu wakajikuta wakiwa wameduwaa, na macho yao yote yalikuwa kitandani.

Docta yeye alikuwa mbio mbio akikimbilia kule kitandani alipokuwa kalala mgonjwa, alipofika pale kitandani akamtupia jicho yule mgonjwa halafu akaangalia kitandani, akaangalia ile mipira ambayo ilikuwa imewekwa pembeni ya kitandu kwa mpangilio usio wake, hakujali kwa hilo kwa muda huo, alichokuwa anajali ni hali ya huyo mgonjwa, na alipomuona mgonjwa kakaa na kujiegemeza kwenye bega la Maua akajikuta akisema kwa sauti;

‘Hii ndio miujuza ya mungu, na kweli kama huamini, ukikutana na miujiza kama hii ndipo utagundua kuwa kila mtu hufa kwa siku yake…sasa kwanini umejiondoa hii mipira kwa namna ambayo sivyo inatakiwa iwe hivyo, ni nani kafanya kazi hii?’ akauliza Docta.

Pale kitandani alikuwa kakaa Maua na pembenii yake alijiegemeza yule mtu ambaye wote walijua hayupo dunia, na mkononi Maua alishika gilasi ya maji ambayo ilionyesha ilishatumika, je ni muda gani haya yote yalifanyika, kumuondoa yule mgonjwa ile mipira na Maua kuchuku maji na kumnyishwa mgonjwa, ikawa ni swali la kila mmojawapo, na kabla mshangao wao haujaisha mara wakasikia sauti ya mgonjwa ikisema;

‘Hivi wewe docta mna malengo gani na mimi mlitaka kuniua na hii mipira yenu, au nini…?’ akalalamika mgonjwa.

Docta akamwangalia kwa makini, huku akitabasamu, akageuka kuwaangalia wanafamilia ambao wote walikuwa na sura za furaha isiyomithilika, na bila ya kumgeukia mgonjwa akasema;

‘Tulitaka kukuua au tulikuwa tunakusaidia , hujui kwa muda mrefu ulikuwa ukiishi kwa kutumia msaada wa hii mipira na hewa inayotoka kwenye huo mtungi, …au una maana gani kusema tulitka kukuua..? akauliza docta.

‘Hii mipira yenu ,mliyokuwa mumenitumbukiza mdomoni na puani ilikuwa inaniumiza sana na koo lilikauka na kiu ya maji ilikua haielezeki, kuna muda nilizindukana na kuiondolea mbali hiyo mipira yenu….’akasema huyo mgonjwa.

‘Pole sana, …’ndicho alichoweza kusema docta huku akijaribu kumpima huku na kule kuhakikisha kuwa mambo yapo safi.

‘Sasa unaendeleaje..?’ akauliza docta

‘Sijambo kabisa , najiona kama nimezalwa leo, hakuna maumivu kabisa, mnaweza hata kuniruhusu nirudi nyumbani….,’akasema na kuwafanya wanafamilia wote kucheka kwa furaha.
Mgonjwa akabakia kushangaa, akawatizama wote huku akijiuliza kwanini wanamcheka, na alipoona wote wametulia wakimwangalia, akasema;

‘Hivi hamjaamini kuwa nimepona, mnaniona bado mahututi, au mlishaniandika kwenye kitabu cha marehemu watarajiwa, …sote ni marehemu watarajiwa, au sio. Au ni kweli kama nilivyoota kwenye hizo ndoto nyingi, hata nyingine sizikumbuki vyema, hivi kwanza niwaulize, maana nimemuuliza mhusika mwenyewe hataki kunijibu, sijawa na uhakika kuwa ilikuwa ni ndoto au hayo mambo yametokea kweli, kwanza kabisa nataka kujua kuwa kweli mke wangu kaolewa na …….’ Hapo akageuka kumwangalia Maua halafu akamwangalia Rose.

‘Mbona mambo yanaonekana kama ilikuwa sio ndoto, yupi ni mke wanu kati yenu wawili…?’ akauliza Mgonjwa.

‘Tukuulize wewe, maana unaona halafu usimjue mke wako, bahatisha , ukikosa umemkosa, au tunakutoza faini…?’ akasema Docta akiwa na yeye hana uhakika ni nani kati ya hawo wawili ni mke wa huyo mgonjwa.

‘Sasa inakuwa kama nilivyoota kwenye hiyo ndoto, na inanitiaa wasiwasi, maana kama kweli mke wangu kaolewa, basi haina haja ya mimi kupona,, nitunduke hayo mapira, nataka kurudi huko nilipokuwa, maana mke wangu nampenda, na sioni sababu ya yeye kuolewa na mtu mwingine, kwani imepita muda gani tangu haya mauza uza yatokee, na mimi nina tatizo gani, hadi….’akapitisha mkono nakushika yale mabandeji aliyofungwa kichwani.

‘Usiyaondoe bado kabisa kuondolewa hayo mabandeji, na naona upumzik kidogo, usijilazimishe kuongea na kukumbuka saana…’akasema Docta.

‘Kukumbuka kupi tena docta, mimi hapa nakumbuka kila kitu, ispokuwa hayo yaliyotokea baada ya hiyo ajali ya meli, nakumbuka wakati naruka toka ndani ya meli hadi kwenye maji, tulipoona meli inazama, niligonga kichwa kwenye machuma ya hiyo meli, na kichwa kiliniuma sana, na tangia hapo, hakikuacha hadi aple nilipopoteza fahamu, na tangu hapo mengine yote yaliyotokea …siyajui vyema, ndio nayaona kama ndoto…’akaeuka kuwaangalia tena Rose na Maua.

‘Kwenye ndoto nakumbuka, kulikuwa na docta, mmmh,…’akawaangalia kwa makini Maua na Rose, halafu akauliza ; `Kitu cha ajabu kwenye hiyo ndoto, nilishangaa kumuona mke wangu akiwa dakitari, wakati sikumbuki yeye kusoema huo udakitari, na sasa …nimegundua kitu , ina maana mke wangu ulikuwa na pacha mwenzako, ….ndio …nimegundua, huyo pacha mwenzako ni dakitari, au sio…anaitwa nani vile….’akageuka kitandani kama anajinyosha,

‘Ndio anaitwa docta Rose,..mmh, nakushukuru sana, kama hiyo sio ndoto , ni kweli, basi wewe ndiye uliyebeba dhamana na masiha yangu nikiwa katika kipindi hicho kigumu, sijui nitakulipa nini, munu mwenyewe ndiye anayejua, kama sio ndoto, basi mungu ndiye ajuaye nini ninachowaza moyoni…kama sio ndoto, hebu niambieni ni nani kati yenu anaitwa Rose..?’ akageuka kuwaangalia kwa makini, lakini wote walibakia kimiya.

‘Kama mnataka nibahatishe kama nilivyobahatisha kweney hiyo ndoto, sitafanya hivyo tena, maana nilikosea, na matokea yake huyo mtabiri aliniambia jambo ambalo sitalisahau maishani,….kama ni kweli, sijui, nitaishije, kama ni kweli, sijui…nitaishije….’akawa aanyarudia yale maneno mpaka wote wakashituka, lakini docta alijua ni kwasababu gani, na akamsogeela mgonjwa na kumshika kichwani na akasema;

‘Sasa anahitaji upumzika, akizindukana tena, muwe na majibu sahihi ya kumjibu, haina haja ya kumtesa kufikiri sana, kwani sasa akili yake ipo safi, ila mengi yaliyotokea kipindi akiwa hana kumbukumbu ndiyo yatakuwa yakimsumbua kidogo, ….kwahiyo msitie shaka, cha muhimu ni kutomshinikiza katika kufikiri sana.Na ni vyema mkampa muda , msimjalie wote kwa pamoja….’akasema docta na kumsogelea Rose.

‘Nashukuru sana Docta Rose , kweli wewe ulibeba dhamana ya huyu mgonjwa, na nina mengi ya kukuuliza, na huenda mojawapo litakuwa hilo alilokuuliza mgonjwa, ni wewe mke wake au ni huyo mwenzake, ..lakini tutaongea baadaye…’akasema Docta na kugeuka kuondoka. Lakini aipofika mebela akaeuka na kusema;

‘Kuna watu wa usalama wanataka kuongea na wewe Docta Rose, kama upo tayari nakuomba ofisini kwangu, ...'akasema yule Docta huku kaweka mikono mfukoni, na kutoa tabasamu, huku akiiniwa nfsi yake ikiwa imezama kweney hisia za kumpenda huyu binti, na akilini aliomba kama ni kumpata mke ampate mke kama huyu.

Rose akaeuka kuangalia kitandani, baada ya kumuona huyo Docta akimwangalia kwa muda bila kuendelea kusema neno, na kabla hajasema kitu yule docta akageuka kuwaangalia wale wazazi, akiona aibu kuwa huenda wamehisi kitu, akamgeukia tena Rose na kusema;

'Watu wa usalama wapo wanakusubiri...kama hutajali tuongozane ukaonane nao, hakuna jipya, ila ni mambo ya usalama, labda pia wana yo ya kukuuliza....'akasema halafu akawageukia wale akina mama bila kumwangalia Maua ambaye aikuwa bado kamwiinamia mgonjwa, huenda alikuwa kazama kwenye maombi....docta akasema kwa sauti ya utawala, huku akiwa kaangalia upande ambao una viti vya kupumzikia madakitari ;

'Na ndugu zangu wengine tafadhali mkasubiri pale, msimzunguke sana huyo mgonjwa, ningeliwatoa nje, lakini najua jinsi gani mlivyo na hamu ya kumuona mgonjwa wenu, hana matatizo kwa sasa, akizindukana mtaongea naye mpendavyo…’akasema na kuanza kuondoka.

‘Rose watu wa usalama wanakutakai nini…?’ akauliza mama mtu.

‘Sijui, na wala sitaki kujua zaidi, nitajua nikikutana na wao, sina wasiwasi, wasiwasi wangu ulikuwa usalama wa huyu mgonjwa, na ndicho kinachonifanya nisikae mbali nayeye…lakini ngoja nikawaone hawo wanaojiita watu wa usalama, …..nawaomba msiondoke mkamuacha huyu mgonjwa peke yake, nikirudi tuna mengi ya kuongea, hasa...mengi kuhusu monjwa na ndugu yangu….’akasema na kugeuka kumfuata docta.

‘Kweli yapo mengi yakuongea….’akasema shangazi na kumeukia mama mtu, ambaye muda mwingi alikwua kainama, na kabla hajasema kitu simu yake ikaita, akaangalia mpigaji, na kuwageukia wengine , akitaka kuipokea pale , lakini alikumbuka kuwa hawaruhusiwi kupokea simu humo ndani, akaitizama tena ikiendelea kuita, akataka kuikata, hakutaka kuondoka mle ndani, ….akaitizama ile simu ikiendelea kuita…


NB: Sikupenda niishie hapa katika sehemu hii, kwani mambo yapo mengi yakuandika, lakini wakati ukuta. Ama kwa wazo la leo, ni kuwa: Baada ya dhiki tarajia faraja, kwani mchumia juani hulia kivulini, …hangaika na kutafuta maisha, kwani tumeambiwa, fanya kazi, jibidishe na kutafuta maisha kama vile utaishi milele, lakini usisahau kumkumbuka mola wako, na unapomuelekea yeye muombe sana, kama vile ndio saa yako ya mwisho ya kuishi…Tupo pamoja

Ni mimi: emu-three

Wednesday, January 25, 2012

Uso wa binadamu umeumbwa na haya




Siku hiyo nilikuwa nyumbani, nikawa nawapa kuku wangu wa kienyeji dawa na chakula, kati ya hao kuku mmoja alikuwa katotoa vifaranga karibuni, nikawa nawaangalia wale vfaranga , ambao kwa muda ule walikuwa wakimzunguka mama yao huku na kule. Mama yao alikuwa kalala na aliponiona akalia ule mlio wa tahadhari, mlio wa kuwaashiria watoto wake kuwa wawe makini, na mara kweli wale vifaranga wakakimbilia ndani ya mabawa ya mama yao kujificha na kutokeza vichwa tu.

Wkati nahangaika kuwapa chakula, baadhi ya wale vifaranga wakawa wanatoka ndani ya mabawa ya mama yao na kukimbilia kile chakula, licha ya mama yao kulia mlio ule wa tahadhari, lakini wengine hawakuajli, ikabidi mama yao ainuke na kuanza kutanua mabawa kwa kunitishia mimi nisiwakaribie watoto wake, hakuniamini hata mimi ambaye nawajali nakuwalisha, alikuwa akitimiza wajibu wake wa mama mzazi.

Nikiwa namalizia kazi ya kuwapa chakula na dawa na wakati huo mama wa wale vifaranga akikwakura chakula nilichowawekea, ambacho kilikuwa safi, tu lakini kama wajibu wa mama wa vifaranga lazima ahakikishe anawatengenezea watoto wake kile ambacho anaona kinafaa, na pia kuonyesha kuwa anawajali, na kweli watoto walikuwa wakimzunguka na kudonoadonoa kile chakula mama yao alichoshikilia mdomoni, nikasema kweli nani kama mama.


Wakati huo mara akazuka jogoo toka nyumba ya jirani, jogoo yule alikuwa hajaniona, akafika pale aliposimama yule mama wa vifaranga na kuanza kumbugudhi yule kuku mama wa vifaranga, yule mama kuku akawa anatanua mabawa kujihami, lakini jogoo yule hakujali akawa anataka kumparamia mama kuku yuke, na mama kuku hakukubali, akaanza kukimbia na hapo watoto wake wakawa wanakimbia huku na kule kujihami, na ghafla akashuka kunguru na kumchukua kifaranga mmojawapo.

Mama kuku yule huku akihangaika kukimbizana na yule jogoo, huku akitafuta mwanya wa kuwalinda watoto wake, na yule jogoo naye akawa kashituka na kuanza kulia mlio wa tahadhari kuwa kuna adui. Baadhi ya vifaranga wakakimbilia kujificha, ila mmoja ambaye alikwua bado mdogo akashindwa kujificha haraka, na kunguru akashuka kumwahi. Mana kuku hakubalai akaruka juu naye kumwahi yule kunguru na mimi kwa vile nilikuwa karibu nikarusha jiwe, yule kunguru kwa woga akamuachia yule kifaranga, kikadondoka chini na kilikuwa hoi.

Baadaye nikamfukuza yule jogoo na mama kuku akaingia kwenye banda na kulala na watoto wake, na mara vifaranga wawili wakamrukia mama yao juu na kusimama juu ya mgongo wa mama yao, hawa ni majogoo, ndivyo inavyoaminika kuwa ukiwaona vifaranga wanamrukia mama yao na kukaa juu ya mgongo wake watakuwa ni majogoo.

Nilijaribu kufanya uchunguzi huo kwa kuangalia alama za wale vifaranga. Na kweli hapa karibuni wale kuku wameshakuwa wakubwa, sasa hawaishi na mama yao, mama yao ana vifaranga wengine wakubwa tu, wale niliowaona siku ile wengine wanatetea na majogoo yanaanza kuparamia mitetea, na cha ajabu sasa wanaparamia hata ndugu zao, na cha ajabu zaidi wanamfukuza hata mama yao,…hiyo ndiyo hulka ya wanyama, wakishafikia umri fulani hawatambuani tena, mama hajuani na watoto wake tena, watoto nao hawajuani na wazazi wao, mtoto atampanda mama yake!


Wakati nawaza hili nikakutana na baba mmoja akiwa kamshika mtoto wa kike mkono, mtoto huyu wa kike alikuwa kavaa sare za shule, na mfuko wa vitabu upo mgongoni, binti yule alikuwa akilia, na wote tuliokuwa karibu tukageuka kumwangalia baba yule kulikoni.

Wengi wetu mawazo yalitupeleka mbali maana dunia hii imeharibiwa na watu wabaya, na mwisho wake unakuja na mambo ya ajabu ajabu, ukiona jibaba limemshika mtoto na ukalitilia mashaka chukua hatua haraka, kuna visa vingi vya kubakwa watoto wadogo wa kike an wa kiume kwani watu hawa waliolaniwa wanafanya unyama wao kwa mtoto yoyote kwahiyo ukiona jibaba limemshika mtoto wa kiume usizarau, maana wengine tunatilia mashaka tu kwa watoto wa kike, liwe limemshika mtoto wa kike au wa kiume, ukamtilia mashaka, chukua hatua za haraka, uokoe hawa watoto wasio kuwa na hatia.

Sisi tulipoona vile tukaamua kumfuatilia yule baba nyuma, kusikiliza nini wanachoongea, na mara tukasikia yule baba akisema;

‘Wewe binti yanu, jana uliniambia kuwa umekwenda shule, nimeuliza walimu wako wamesema hukufika shule, ulikuwa wapi, leo tunaenda mguu kwa mguu hadi shuleni kwako, kama kweli unanidanya nitakupiga mikwaju mbele ya walimu wako…’akasema yule baba.

‘Baba mimi nilifika shuleni, kwasababu nilikuwa naumwa, muda mwini nilikuwa darasani, ndio maana mwalimu uliyemuuliza anasema hakuniona….’akajitetea yule binti huku akilia,

‘Nitayajulia huko huko kwa walimu wako kwani hakuna kitabu cha mahudhurio, na sasa hivi nitakuwa nikifanya hivi hivi, kuhakikisha unasoma, unafikiri mimi hili litanisaidia nini, haya ni kwa ajili ya maisha yako ya baadaye , na sana sana ni kwa ajili yako na mume wako na watoto wako…nahangaika kutafuta ada, nihanaike kukufuatilia kusoma, hivi mnataka mimi nianguke kwa shinikizo la damu, nife, au…'

‘Hapana baba, siku hizi nimebadilika, nasoma baba, …’akawa analia yule mtoto huku baba wa mtoto kamshikilia mkono na mwendo wake kwasababu yeye ni mtu mzima ulikuwa ukimzidi yule binti kwahiyo muda mwingi alikuwa kama anamvuta ili wawe sambamba,…tulipoyasikiliza yale mazungumzo weni tukaridhika kuwa huyo ni baba yake na hana nia mbaya na yule mtoto. Na kwa muda ule dada mmoja akaanza kulia na kasema;

‘Baba huyo ananikumbusha mbali anafanya kama nilivyofanyiwa na marehemu baba yangu,..nilipomuona nikakumbuka maisha yangu, yalikuwa hivyo hivyo, sasa baba ni marehemu, mungu amlaze mahali pema peponi, asingelikuwa yeye, sijui sasa hivi ningelikuwa wapi, kama sio kuwa changudoa, na kuzalilika mitaani, maana hawa machangudoa wanatembea na mibaba sawa na baba zao, ni kama binti kutemeba na baba yake.

Aliposema hivyo `sawa na baba yake’ ndipo nikawakumbuka wale kuku zangu, ambao sasa wanatemeba na mama yao, hawakumbuki tena kuwa huyo alikuwa mama yao aliyewalea kwa shida na taabu sasa wao ni vijogoo, wanamfukuza hata mama yao. Lakini hayo ni maisha ya wanyama, sio sisi binadamu, binadamu tuna haya zetu, huwezi kumkuta baba akitemba na binti yake au mama akitembea na mvulana au kijana . Labda hawo wanaoitwa machanudoa, na wanaume sijui wanaitwaje….


Kama unabisha hili, muda wa jioni na kwenda mbele nenda mitaa ya Ohio hapa Dar, na huko Moshi kama sikosei kuna mtaa wa Mafuta, na kila mji sasa una mitaa fulani ambapo wapo wakina dada, nasiki hata wanaume wanajiuza, …wanajizalilisha kwa kufanya biashara hiyo haramu, na mwisho wa siku wanakuja kutembea na mibaba sawa na baba zao waliowazaa, mabinti hawa au wanaume hawa uso wao umevuka haya ya kibinadamu,…tumegeka kuwa wanyama au kuwa kama kuku….

Jamani tunakwenda wapi? Na hii hali iliyozuka sasa hivi ya watu kuwazalilisha watoto, na kila kukicha hukosi kusikia visa kma hivi, jamani tutauliwa wazazi, tutaulizwa katika swala hili la ulezi, kwani kila mmoja ni mchungaji, kila mmoja ni mlezi, watoto wote ni wetu sote, tuhakikishe jukumu hilo tunalitekeleza sote.

Ngoja niishie hapa maana, muda ni mali...naishia hapa huku nikitafakari kisa cha huyu mwanadada aliyeangusha kilio baada ya kumuona huyo binti akikokotwa kwenda shuleni na baba yake, kama nitapata nafasi hiyo nitakiweka hewani. Tukumbuke blog hii ni `diary' niliwajibika kila mara kuweka vitu kama hivi,lakini ipo siku ndoto ya blog hii itakamilika. TUPO PAMOJA

NB: Kisa chetu cha `akufaaye kwa dhiki ...' akinaendelea na kinafikia ukingoni, lakini sijapata mahala muafaka pa kuweza kukimalizia vyema.



Ni mimi: emu-three

Saturday, January 21, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-75 hitimisho-19



‘Una uhakika na unachokisema, sasa ilikuwaje taarifa zikamfikia kuwa anahitajika huko haraka?’ akauliza Baba Rose.

‘Kwahiyo ndege haijatua na ikitua wapo watu wanamsubiri, kumkamata, na nyie mumechukua hatua gani za kumsaidia..?’ akauliza kwa hasira. Na aliposikia maelezo ambayo hayakuweza kusaidia akasema kwa hasira;

‘Sasa sikilizeni, kama atakamatwa, haraka mfahamisheni wakili wetu, na mimi nipo njiani, na jaribuni kukwepa majibishano ya silaha, sitavumilia kama kutatokea mauaji yoyote, hakikisheni mnamlinda huyo jamaa iwezekanavyo na jaribuni kuhakikisha hakamatwi, na kama hakuna jinsi na akakamatwa , harakisheni kumtafauta huyo wakili amtoe haraka iwezekanavyo,...'akatulia halafu kabla mwenzak hajasema kitu akasema;

`Nitajitahidi niwezavyo kutoa msaada…kama ikibidi nitafika, lakini sijui kama nitawahi..’akasema huku akiwa uwanja wa ndege, na hakutaka kusema yupo uwanja wa ndege anakuja huko.

Baba Rose au Tajiri Mzungu, alifika uwanja wa ndege akiwa hajatulia vyema, kichwani alikuwa akimuwaza ndugu yake ambaye alimpenda sana kuliko maelezo, na katika maisha yao wamekuwa wakisaidiana kwa kila hali. Alikuwa akibahatisha, lakini kwa taarifa alizozipata toka kwa jamaa anaowafahamu ni kuwa ndugu yake akitua uwanja wa ndege tu anakutana na pingu, na kesi anayokabiliana nayo ni kubwa sana, ikiwemo ugaidi na mauaji. Na kubwa zaidi na maelekezo ya Mzee anayemtokea, sfari hii alikuja hadi huko alipo.

Wakati amekaa akisubiri usafiri akakumbuka maonezi yake ya mwisho na ndugu yake , ambaye wengi hawamjui, Alikumbuka alipopokea simu toka kwa ndugu yake huyo kuwa anahitajika nyumbani haraka sana kufuatilia maswala muhimu, na alipoulizwa maswala gani, ndugu yake huyo hakutaka kuyasema akasema tu ni mambo yao ambayo asipokuwepo mambo yataharibika, ikiwemo miradi yake.

‘Una uhakika kuwa huo sio mtego?’ akauliza kaka yake.

‘Sizani kuwa ni mtego, kwani aliyenipa hizi taarifa ni mtu wetu, na nikathibitisha kwa msaidizi wangu na zaidi nikapata uhakika katika vyanzo vyetu vya habari, usitie shaka na mimi....’ akasemandugu yake huyo kwa kujiamini.

‘Ni hilo tu au kuna jingine na vipi kuhusu yule binti na mpinzani wako,,..?’akauliza kaka mtu.

‘Huyo mpinzani wangu, huenda sasa hivi yupo chumba cha kuhifadhia maiti, kama ana roho saba kama paka, safari hii nimemalizia ile ya saba, nilihakikisha kuwa nimeziba ile mirija waliyomuwekea ambayo ukichelewesha muda mchache tu, mawasiliano yanakatika, …sijui kama watakuwa wamemuwahi….’akasema kwa kujiamini.

‘Wewe sio mungu bwana, mbona mke wangu kasema hali yake inaendelea vyema, wameshamwuahi mapema, kabla hajafikia hali mbaya…’akasema kaka mtu.

‘Ilivyo ni kuwa hata kama watamuwahi wajaribu kumshtua ili mapigo yaanza kufanya kazi, haitachukua muda, maana nilishakatisha mawasiliano muhimu, hayo ni mambo ya kitaalamu tunajua sisi kaka…..’akasema ndugu mtu.

‘Basi huyo ana roho nane, kwani hapa tunapoongea huenda keshazindukana anaongea na mpenzi wake, wewe umekosa mwana na maji ya moto….’akasema kaka mtu.

‘Kwasasa sina jinsi kwani nilichoitiwa huko ni muhimu sana kaka, nimejaribu kuwapanga watu fulani wanisaidie hiyo kazi, …najua watammaliza huyo jamaa, kazi itakuwa jinsi ya kumshawishi huyo binti…hilo naliweka kiporwa, kwasababu tusipofanya hivyo, mali itakwenda kusipositahili, wewe kwa pupa zako umemwandikisha huyo binti ukijua na binto yako, sasa….’akakatiza.

‘Usinikumbushe,….we acha tu, na wewe ulishanipa uhakika kuwa utamchukua, ….sasa sijui, …haloh, upo hewani….’akajiona kama anaongea peke yake.

'Nipo hewani, nilikuwa nafikiria kidgo, unajua kaka, kama atakubali nimuoe, huoni itakuwa maajabu, mtu na kaka yake wanaoa familia moja hiyo ipo kweli, ….?’ Akauliza.

‘Hili lisikutie hofu, maana nimegundua mengi, hasa baada ya kusikia kuwa ana pacha mwenzake, sasa huyo pacha mwenzake alikuwa wapi, kazaliwa na nani, huoni hawa watu wanatufanya sisi wajinga?....’akasema na kukohoa kidogo.

‘Bado hawajafanikiwa kutufanya wajinga, tutawashitukizia, ngoja nifike nyumbani nijipange upya, utaona mambo yangu…;akasema ndugu mtu

‘Unataka kusema unatka kufanya nini, wakati wahusika weneywe umewaacha nyuma, …’akasema kaka mtu

‘Kwanza ujua hawa watu walishampanga huyo binti kama chambo cha kuninasa mimi, na ilibakia kidogo tu waneninasa pale hospitalini,…..na kitu walichofanya ni kunichanganya , wakijua kuwa hawa mabinti wapo mapacha, wakanitumia huyo ndugu yake asiyehusika…… maana wanfanana kama mtu akijiangalai kwenye kiyoo...na baya zaidi wameshaniwekea mitego ambayo nisipoondoka hapa haraka wataninasa, na wakininasa huku nimekwisha, ....kwahiyo ni bora niwahi nyumbani haraka iwezekanavyo....’akasema ndugu mtu.

‘Sawa, ..kwa mtaji huo huna jinsi, na sasa ina maana tumepoteza ule mpangilio mzima, ....lakini sio mbaya, tutaangalia la kufanya, ila hawa watu lazima tuwaonyeshe kuwa tunajua zaidi, huyu mke wangu kanihadaa toka awali, kuwa huyo mtoto ni wangu,….lakini kwangu sio mbaya sana…atakuja kuumbuka mwenyewe..isingelikuwa hawa wazee na mambo ao ya mizimu, nisingelijali sana….unajua kwasababu yao nashindwa hata kurudi nyumbani, maana nikirudi , yule mzee wa ajabu atanitokea na safari hii akinitokea sijui atahitaji nini, huenda ataitaka roho yangu tu…..’akasema.

‘Hayo mambo ya mizimu sijui ya nini, sipendi kuyasikia, ....mimi nawahi tutawsiliana nikifika huko, , ila nakuomba kitu kimoja hakikisha unanipa habari kamili za Rose, nahisi ana ujauzito, sijakuwa na uhkaika kuwa hiyo mimba ni ya nani, na kwa mtaji huo, tunazidi kuwekewa kizingiti, sijakuwa na uhakika na hilo, maana kama nilivyokuambia wapo mapacha , sasa sizani kuwa wote ni waja wazito….?’ akasema kwa haraka haraka.

‘Unafikiri hiyo mimba ni ya kwako, kwani uliwahi kukutana naye, au ulikuwa ukishika pembe, hahaha, mdogo wangu kweli umezidi upole, yaani ulishindwa kabisa kumpata huyo bint mpaka wengine wanakuja kubebesha mamba, hapo sasa umeshindwa wewe, una uhakika ni mja mzito, na je mamba hiyo ni ya nani, au ni ya kwako....?’ akaulizwa.

‘Kaka sijui zaidi, ..kwaheri muda umefika wa kuingia kwenye ndege, tutawasilina baadaye....’akasemana mawsiliano yakakatika.

**********

Wakati anaongea na ndugu yake huku akipata kinywaji baridi, akataka kuinuka kuondoka, mara, ikasjisikia kizunguzungu, kichwa kikawa kinamuuma isivyo maelezo, mara…kukawa kama kitu kimempitia machoni, akatulia kwa muda hadi ile hali ikapita, akainuka na kutoka nje, alipofika kwenye kona ambapo ni karibu na aliposimamisha gari lake, akaona mwanga mkali ukipita mbele yake. Alitizama huku na kule, lakini hakuona kitu kilichomulika, akatulia kwanza na kuwatizama watu ambao walikuwa wakiwa na sughuli zao na hakuna mtu aliyekuwa akishangaa kama yeye.

Akaanza kuinua mguu kulifuata gari lake, mara ule mwanga ukatokea tena, na safari hii ulikuwa mkali kiasi kwamba ulifanya macho yake yashindwe kuoan vyema, na hata wale watu waliokuwa wanapita au kusimama karibu naye akawa hawaoni tena, anachoona ni ule mwana tu. Na cha ajabu ule mwanga ulikuwa ukionekana njiani ambapo watu wanapita, lakini watu hawo hakuweza kuwaona zaidi ya ule mwanga.

Na wakati anahangaika kusafisha macho yake kutokana na ule mwanga mkali ili ajaribu kuona vyema, mara kukatokea kitu kama kivuli, kwanza kilinza kwa kuonekana kitu kimoja kimoja kama vile mtu anachora picha, na chaki kwenye ubao, lakini ubao huo ni mweupe, na chak ni nyeusi, kukaanza sehemu ya kichwa, sehemu ya kiwiliwili, ikashuka hadi kwenye mguu, na kuelekea upande wa pili wa mwili, mguuni, ikapanda hadi kiwiwili, hadi kichwani na kuja kuunganika na sehemu ile ya upande wa kwanza na baadaye kikakamilika kiwiliwili kizima….

Kabla hajamliza kushangaa, ile sura ya mtu, ikafunuka mdomo, na kuanza kuongea hapo hapo….

‘Unafikiri kuja kujificha huku nchi za watu ndio umenikimbia, mimi nitakufuata popote pale, isipokuwa kwenye kaburi lako, ambalo sasa linakaribia kuchimbwa….’ Ile picha ikawa ianongea, na sauti ilikuwa ikisikika waziwazi, kiasi kwamba jamaa yetu alijua kila mtu anasikia hayo maneno, kumbe yalikuwa yakisikiwa na yeye pake yake.

‘Umeshahu nilichokuagizia au unataka tuanze vurugu zetu, umesahau yale mateso uliyokuwa ukiyapata kabla hatujakusaidia, au kwa vile umepata mwanamke mrembo, unahisi kila kitu kimekunyookea, au kwa vile unaona biashara yako huku nje inakuwa ndio unazania hutafirisikia. Kwanza nikuambie ukweli, wewe unadanganyika na huyo mwanamke humjui vyema huyo mwanamke, yeye anachokupendea ni huo utajiri, na ukiisha, na wewe hakutaki tena, je untaka tujaribu hilo ili uone ukweli…?’ ile sauti ikatulia kwa muda. Na kabla hajasema kitu, ile sauti ikaendela kusema;

‘Tunaweza tukakufanya hohe hahe, ili uthibitishe huo ukweli, kuwa huyo mwanamke yupo kwa ajili ya mali yako, na ukifilisika anakukimbia, na kama unataka tufanye hivyo, hatari yake ni kuwa ukifirisika utaishia kuchanganyikiwa na katu hutakuwa tajiri tena, kitakachofuata ni kaburi lako, nasi tutakukaribisha huku kuzimuni, ….unasemaje….?’ ikasema ile sauti na kutulia tena kwa muda…na jamaa yetu hakujibu kitu.

Baada ya muda mfupi ile sauti ikitokea tena, ile picha kama mtu ikawa kama inafifia na kubakia meno, au sehemu ya mdomo tu, huenda ni kutokana na ule mwanga ulivyo mkali.

`Kwani wewe ni nani na unataka nini kwangu?’ akauliza baada ya kuvumilia kwa muda mrefu akimsikiliza, moyoni alishahisi kuwa ni nani huyo, lakini alitaka kujena ujasiri, kwani alishachoka kuwa mtumwa wa mambo hayo, hakuona tena raha ya huo utajiri, lakini je angeliweza kuachana na hayo mambo kirahisi hivyo!.

‘Umeshanisahau sio, au kwa vile siku hizi unaishi nchi za ugenini..?’ ile sauti ikacheka kwa kebehi, halafu ikasema;

`Au kwa sababu ya huu mwanga mkali, ndio maana hunioni vyema, hebu pikicha macho yako halafu halafu uniangalie tena….’kile kitu kama picha kikasema. Na jamaa akapangusa macho yake kama alivyoambiwa na alipoondoa mkono wake machoni akajikuta anatizamana na mzee mmoja , mzee ambaye kila alipokutana naye alikuwa kama kakutana jinamizi la kutisha, na aheri ingelikuwa ni jinamizi , kwasababu ni ndoto, sasa hiyo haikuwa ni ndoto, unakutana na hilo jinamizi moja kwa moja.

Ile sura ya yule mzee ilipotokea, kwenye ule mwanga, na ule mwanga mkali kufifia, Jamaa yetu alianza kuishiwa nuvu, miguu ilikuwa kama imevunjwa vunjwa, alijitahidi kusimama imara, kuogopa kuanguka pale mbele za watu. Tukio kama hili lilipokuwa likimtokea awali, alikuwa akiogopa na hata kuzimia, lakini huyu mzee alipokuja kumtokea na kumpa ujasiri, akawa anajitahidi kuvumilia n kukabiliana nalo. Akimtizama yule mzee huku kumbukumbu za mateso ya nyuma zikimrejea akilini.

Wakati akiwa mtoto, Tajiri Mzungu, jina alilokuja kuitwa baadaye baada ya kuibuka na kuwa tajiri, na kuanza kuishi kizungu, licha ya masharti makali aliyokuwa kawekewa, kuishi huko ilikuwa tu kwa nje, lakini kiundani alikuwa hana raha.

Maisha ya utoto wake yaliubikwa na ndoto za kuogofya karibu kila siku, na mara nyingi aliombea usiku usije, ili asije akakutana na hayo mauza uza ya usiku. Wazazi wake walimuhangaikia huku na kule na hospitalini yote walimaliza na mwishowe waliishia kusema hana tatizo na hali itakuja kwisha tu akiwa mkubwa. Na kwa vile akiwa mtoto, alikuwa akilala chumba kimoja na mdogo wake, matatizo yaliyokuwa yakimtokea yalimuathiri sana ndugu yake huyo aliyekuwa akilala naye kitandu kimoja, maana kaka yake akikurupuka usingizinii anaweza hata kukimbia nje, kwahiyo mdogo mtu ndiye aliyekuwa akijitahidi kuhakikisha kuwa milango imefungwa kabisa….

‘Baba mimi nitakuwa ninamfunga kamba kaka usiku maana akiota anakuwa mtu wa ajabu sana, anakuwa kama sio yeye, kwani anajibamiza chini na wakati mwingine anakimbia kwenda nje, naona jambo jema ni kumfunga kamba, ili akianza fujo zake asiweze kuumia….’akasema mdogo mtu ambaye zoezi hilo alishalianza kulifanya bila hata kuwaambia wazazi wake, ambao mara nyingi wakifika wanakuta mtoto keshatulia, kwahiyo hawakujua zaidi ya hayo wanayohadithiwa, hadi pale walipoamua kukaa naye karibu na walichokiona , kiliwafanya wahangaike zaidi.

‘Haya mambo ya kimila yapo, na kote tulipoenda tumeambiwa kuwa hayo yanatokana na mizimu ya mababu, huyo anayemsumbua ni babu yangu…babu huyu alinipenda sana, na kabla ya kufa alisema sikuu moja atakuja kunitokea kwa kupitia mtoto wangu, sasa naona ndiyo huyo kamjia mwanangu, na hili kuliondoa inabidi kafara kubwa sana….’akasema baba wa huyo mtoto.

‘Hapana mambo hayo yanakwenda kinyume na dini, mimi sitayakubali….’akasema mama wa mtoto kwa mara ya kwanza, na yeye akaamua kwenda kwa watu wa dini, ambao walihangaika kiasi cha uwezo wao, lakini walikutana na vizingiti vya baba mtu, na hata kutishiwa uhai wao, na walipooona hivyo, ikabidi wasalimu amri na kuwaachia wanafamilia wao wenyewe. Mama alijitahidi sana, lakini mwishowe naye akatishiwa kuuwawa, na hata kuachika, na kuambiwa hilo halimuhusu, amuachie baba mwenyewe, anajua nini cha kufanya. Hayo mambo yalipozidi sana, mama ikabidi ashirikiane na mumewe na ndipo siku moja wakampata mzee wa kale akawaongoza na kuwapelaka kwa mtu aitwaye ‘mtaalamu’ .

Kwa jinsi alivyokuwa akipata taabu na ndugu yake huyu, akawa kajenga ukaribu sana na hawakuweza kukaa mbali na hata kaka yake alipochaguliwa kwenda sekondari, mdogo mtu alipinga kwa nguvu moja, akijua kuwa ndugu yake hatakuwa na mtu wa kumlinda pale akianza kukurupuka na ndoto za usiku. Mtaalmu wao alikuja na kumpa dawa za kumsaidia na akasema huko anapokwenda hatapata shida sana, na ikitokea shida wamuite, atayamaliza hayo matatizo.

Kaka mtu akaenda sekondari ya bweni, na mwaka wa kwanza hali ilikuwa nzuri, na mambo yaliazna alipofika kidato cha pili na mbaya zidi kidato cha nne. Siku moja akiwa amelala, aliamuka usiku wa manane na kuanza kupiga makele, hadi bweni zima likaamuka, na wenzake walipomkaribia akaanza kuwapiga, na hata kuanza kujibamiza ukutani. Hali hiyo ilikuwa mbaya hadi asubuhi, ambapo ndipo alipata usingizi na alipozindukana wenzake walipomuuliza alibakia kushangaa tu, hakujua kulitokea nini.

Hali hii haikuishia hapo jamaa huyu akawa anaona vitu vya ajabu ajabu, na wakati mwingine anaona watu ambao wengine hawawaoni, na hali hii ilifikia hatua hata wanafunzi wenzake wakaanza kumuogopa. Wengine wakamuita mwanga, wengine, mganga wa kienyeji, maana wakati mwingine, aliweza kutafuta dawa zilizoweza kuwatibia wenzake , pale wanapoumwa magonjwa kama ya kichwa au matumbo, …na wakati mwingine aliweza kutoka nje ya bweni na kuanza kukimbia ovyo akidao anakimbizana na watu wasioonekana, akadai alikuwa akiwakimbiza wachawi….

‘Hivi wewe una matatizo gani, …?’ akaulizwa na mwalimu wao baada ya kesi yake kupelekwa kwake.

‘Mwalimu hata mimi sijui, maana sijitambui, inakuwa kama ndoto, au sijui nisemeje, haielezeki, ila mara nyingi inaanza kwa kusikia maumivu makali kwenye kichwa, najisikia vibaya vibaya…au wakati mwingine inaaanza kama ndoto, najikuta kama nakabwa halafu kunatokea majitu ya kutisha, yakiwa na meno makubwa na sura mbaya, yote yanataka kunivamia mimi, ndipo hapo naanza kupiga ukulele, na wakati mwingine yakitokea napotelewa nafahamu na wala sijijui kabisa kinachoendela, nasikia watuw akisema nakijibamiza, nakujiga- piga, mimi hayo siyajui, nasikia kwao tu….’akasema huyo kijana.

‘Na wakati mwingine anajibamiza sakafuni au ukutani, usipomshika anaweza kuumiza watu, na huwa anabadilika hata sauti anaongea kama mzee, sauti ya kizee nay a kutisha, ….cha ajabu anadai kuwa anamuhitaji yeye….yaani anataja jina la huyu kijana kuwa anamuhitaji arudi kwao, akapewe majukumu….’akasema mwalimu wa malezi.

‘Majukumu gani hayo anatakiwa kupewa mtoto kama huyu badala ya kusoma kwanza...mbona mimi siyaelewi hayo mambo…hebu nifahamisheni kwa mapana….’akasema mwalimu mkuu.

‘Kuyaelewa kwake mpaka umuone akiwa katika hiyo hali, kwakweli anateseka sana, mimi ningelishauri arudishwe kwao kwanza wakamuangalie kienyeji, maana akipelekwa hospitalini hakuna kinachogundulika, hana malaria wala hana tatizo jingine lolote….’akaongezea mwalimu wa malezi.

‘Hivi sisi tutaelewekaje na hawo wazazi wa mtoto, wakituona tunamrudisha mtoto wao nyumbani eti anaumwa bila ushahidi wa dakitari, …..mimi bado sijarizika na hilo, tunahitaji ushahidi wa kimaandishi, na ushahidi huo utoke kwa dakitari, maana huo ni ugonjwa, au sio uonjwa jamani, ….?’ Akauliza huku akiwageukia wenzake ili kupata ushauri, na walipokuwa kimiya akaendelea kusema;

‘Na ni bora likitokea tena hilo tatizo awepo huyo dakitari alishuhudie mwenyewe, nami nitafurahi nikiliona hilo tukio, ili njirizishe mwenyewe. Akiwepo dakitari, basi ataweza kuandika lolote kuhusiana na tatizo lenyewe, na huo utakuwa ushahidi wetu kwa wazazi, na yeye ataweza kuanisha kitaalamu zaidi, ili hawo wazazi kama wataamua kuendelea na matibabu zaidi wajue ni wapi pa kuanzia….’akasema huyo mkuu wa shule na kuwangalia wenzake kuwa wana la zaidi na alipohakikisha kuwa hakuna la nyongeza, akauliza;

‘Je mnakubaliana na hilo, au kuna jingine la nyongeza..?’ akauliza na wote wakakubalika na hilo wazo na kweli siku moja likatokea tukio la aina yake, maana bweni zima walitoka nje kumkimbia, jamaa alikuwa akinuruma kama samba, na aliyemsoelea alipata kipigo cha aina yake, akaja mkuu wa shule na dakitari ambaye alipoona hivyo, alisaliu amrii na kusema;

‘Haya mambo siyo ya kihospitali, mimi ni dakitari na kazi yanu haishughuliki na mambo kama haya, mimi nawashauri kuwa, huyu mtoto mrudisheni kwao, wao kama familia watajua nini la kufanya, vinginevyo apelekwe wodi ya vichaa, hilo ndilo lipo ndani ya uwezo wanu, lakini swali ni kwa ugonjwa upi, maana ukimpima na ukimchunguza vyema, hana tatizo, na akiwa hana hiyo hali huwezi kujua lolote….’akasema huyo dakitari ambaye siyo mara ya kwanza kuletewa huyo kijana mweney hayo matatizo.

‘Basi tunaomba utuandikie huo ushauri wako, ili tupate ushahidi wa kuwapelekea wazazi wake….’akasema mwalimu mkuu na dakitari huyo akakubali, akafanya kama alivyoombwa, ni ikawa ndio mwisho wa mtoto huyu kusoma kwenye shule hiyo, kwani aliporejea nyumbani na kukutaa na mtaalamu aliyekuwa akimtibia alitoboa siri kubwa ni kwanini hayo yalikuwa yakimtokea huyo mtoto.

Waliambiwa ndani ya familia yao kuna mizimu ambayo inamuhitaji huyo mtoto ashirikishwe katika mambo yao ili kuendeleza desturi za mila za mababu zao, ambao wamekasirika kwa kutengwa…., la isipofanyika hivyo, hayo matatizo kwa huyo mtoto hayatakwisha…na yanaweza kuwa ambaya zaidi…, na hata hivyo huyo mtoto ana nyota ya utajiri ambayo imeshikiliwa na hawo mizimu, kwa masharti ambayo atakuwa akielekezwa mwenyewe…’akasema huyo mtaalamuu na kuwaacha hawa wazazi hawana la kufanya.

‘Sasa tufanyeje maana haya ni mateso kwa mtoto wetu..’ akauliza mama akiwa an huruma ya mwane ambaye kwa wakati huo alikuwa kalala chini hoi baaada ya kujibamiza chini na ingwaje walijaribu kumshika lakini walishindwa kabisa, hadi alipokuaj huyo mtaalamu na kumpa dawa zilimyamazisha . Dunia hii kuna mambo…

‘Cha kufanya kwa sisi hakuna, ila nitajaribu kuliondoa hilo tatizo kinamna , hilo jambo lisiwe linamtokea mwilini mwake, litakuwa linamtokea moja kwa moja, yaani hiyo mizimu atakuwa akiiona moja kwa moja na kuongea naye huyo mtu au mzimu wake unaomsumbua, lakini inatakiwa ujasiri, na yeye mwenyewe ataambiwa nini la kufanya, …mimi sitaweza kuingilia huko zaidi…’akasema huyo mtaalamu.

Na kweli baada ya jitahada za huyo mtaalamu, akafanya alichofanya na ile hali ikaondoka na jamaa yetu akawa anatokewa na huyo babu moja kwa moja. Wanasema ni babu yake aliyekufa zamani….
Kwa mara ya kwanza jamaa huyo aliogopa sana, kwani sura ya huyo mzee mwanzoni ilikuwa ikija kwa sura ya kustisha kidogo, na baadaye alipoona hivyo, huyo mzee akajiweka aktika sura ya kawaida isiyo ya kutisha.

Na siku zilivyokwenda akawa anazoeana na huyo mzee, na akimtokea anajua kuna jambo anataka kuambiwa. Huyu mzee akawa anampa mashrti ambayo yalianza kumjenga huyo jamaa katika hali ambayo hakuwa nayo, akaanza kupewa utajiri , lakini utajiri huo ulikuwa na masharti kadhaa, na kwa vile aliutaka huo utajiri, akawa anayatimiza hayo masharti, hadi pale alipoanza kuyavunja baadhi ya hayo masharti moja baada ya jingine, na mambo yakaharibika, na alichoona ni kukimbilia nje,akijua kuwa hatakutana na huyo mzee!.

*********

`Oh, ni wewe mzee tena, unataka nini tena huku, tulishaahidiana kuwa hutaniingilia mambo yangu yangu ya biashara nikiwa huku nje, sasa mbona umevunja ahadi yetu…oh, tafadhali hapa ni sehemu za watu….nakuomba usiniumbue, tafadhali….’akasema huku akitetemeka.

‘Nani aliyevunja ahadi yake, mimi au wewe, unakumbuka nilivyokuwa nikikuambia, ..unakumbuka mashrti uliyokuwa umepewa , na sasa umayakaidi hayo masharti moja baada ya jingine. Umeniahidi mengi, ambayo hujatimiza, wewe hujui nimekuwa nikiteseka kwa ajili yako, mimi nimekuwa mdhamini wako, na nikawaahidi wenzangu kuwa utatimiza yote,…wao walishanimbia kuwa wewe hufai, wanataka damu yako …lakini nikawaomba na kuahdii kuwa nitakudhibiti…. je lipi ulilowahi kulitimiza, au unataka niwaachie wenyewe wafanye kazi yao…?’ akauliza yule mzee.

‘Wenyewe akina nani, mimi nilishasema sitaki tena mambo hayo… sitaki tena, na kama ni utajiri wenu chukueni, ni heri niishi masikini kuliko kujiingiza kwenye mambo kama haya, siwezi tena kujiingiza kwenye kuua watu ili eti nipate utajiri….utajiri gani usio na raha, kila mara damu ya mtu, damu ya nini sijui, kwani lazima iwe damu ya mtu, hakuna kitu kingine kwanini isiwe damu ya kuku, ng’ombe au mnyama yoyote, lakini kwanini iwe damu ya watu, wasio na hatia….hapana, naombeni mniache huru, sitaki tena…’akasema jamaa yetu huyu.

‘Hahaha, sasa hutaki utajiri tena, sasa umechoka na utajiri, au kwa vile unaishi kwa raha huku nje, sawa hatukatai, umeshajena jina la kibiashara…., ila nakuonya jambo moja,..hilo linahitaji uharaka wako, usijali cha mkeo au nani…na hapa unavyozidi kupoteza muda ndio unazidi kuweka mambo hayo katika hatari zaidi. Unavyozidi kuchelewa huku, ndivyo unavyozidi kuhatarisha maisha ya damu yenu, …na tulishakuambia kuwa kama sio damu ya mkeo, basi damu ya mwanao, au damu ya ndugu yako, na naona damu ya ndugu yako ni bora zaidi….’ila taswira ikaanza kupotea.

‘Hebu tafadhali subiri kwanza, una maana gani kusema damu ya ndugu yangu ni bora zaidi , ndugu yangu yupi huyo….?’ akauliza kwa mashaka.

‘Eti unasema `Ndugu yangu gani huyo…!’…’ila sauti ikatulia halafu ikasema kwa haraka;
‘Hivi wewe unafikiri hatujui hilo, ndugu yako huyo anayejibadilisha kama kinyonga, na yeye kavunja masharti na ahadi yetu tuliyompa, unafikiri kujibadili kule anafanya kwa utaalamu wake mwenyewe, hahaha..yote hayo ni kutokana na miujiza yetu,…’akatulia na kuwa kama anapotea potea, halafu aaksema tena;

‘Yeye ndiye aliyeanza mapema, kuvunja masharti, akijiona kawa mtaalamu, eti docta…sawa ni docta, lakini mengine hayaendani na ujuzi wake, ni yetu sisi tuliompa…anajua lakini sasa anatuzarau….alianza kubadilia mapema, lakini hatukuwa na kazi naye sana, maana mengine alikuwa akiyafanya hata bila ya sisi kumwambia….na sasa tulipokutana naye anajidai kuwa hataki tena kumwaga damu, ….huyo ndugu yako tunamjua na ananijua mimi kwa sura nyingine,…ananiita mwalimu, wewe ukikutana naye muulize habari za mwalimu wake, atakuambia….hahaha…..’akasema huyo mzee kwa dharau.

‘Sasa mbona mumeniambia mimi hayo na wakai nilikuwa siyajui….?’ Akauliza huyo jamaa kwa mshangao.

‘Kwasababu mambo yameharibika …hilo ndilo ninaloweza kukuambia kuwa mambo yameharibika na mlioharibu ni nyie wenyewe……Ndugu yako anakwenda huko alipoitiwa, na huko ndipo mambo yanaenda kumaliziwa,hakuna jinsi …yeye sasa hivi anakuja kwenye mikono yetu kilaini, ….damu yake tutaipata bila ya kukutegemea wewe…umesikia `anajileta mwenyewe…’ na wewe zamu yako itafuata….ndivyo mambo haya yalivyo, hasa ukikiuka masharti…’akasema yule mzee na kuanza kupotea.

‘Subiri tafadhali, subiri kwanzaaah, nakuomba tafadhali, nitatimiza mnayotaka,ila kwa sharti kubwa msimfanyie lolote ndugu yangu, naombeni msimdhuru ndugu yangu, kwani mnataka nini zaidi…kama ni damu ya mwanagu nitawapa, na hata mkitaka ya mke wangu ni-na-na-weza kuwapa-pa-tiaah…., lakini nawaomba msimzuru ndugu yangu…..’akasema huku akianza kuogopa.

‘Hahaha, hata ya damu ya mke wako unaweza kutupatia kweli…mbona unasema kwa kigugumizi, najua damu ya mtoto wako ukitaka utaipata tu, kwasababu huna huruma naye kwasababu sio damu yako, au sio, lakini mke wako je, ….’ Ile sauti ikanyamaza kidogo, na baadaye ikaendelea kuongea kwa kusema;

‘Haya tunaisubiri hiyo damu ya mkeo….hahaha….unajidanganya, mambo yamefikia tamati, kinachotakiwa ni kumuwahi ndugu yako kama unampenda kweli, ….kwani kwasasa hatuna la kufanya, unachotakiwa ni kumwahi ndugu yako, kabla hajaingia kwenye makucha ya watu wanaomsaka, huenda ukafanikiwa kwa hilo kwa muda, ukichelewa unajua nini kitakachofuata….’yule mzee akapotea na ule mwanga ukapotea pia, na hali ikarudi kama kawaida, na jamaa akazindukana kutoka kwenye ile hali.

Ile hali ilipokwisha, na akili ikamrudia vyema, akatizama huku na kule na kugundua kuwa baadhi ya watu walikuwa wamemzunguka wakimshangaa,…hakutaka hata kuongea nao, kwani wengine walishaanza kumuhiji na kumbe wengine walishaita watu wa usalama, …alipogundua hilo, akaona sasa ataumbuka, akakimbilia gari lake na kuondoka harakaharaka. Na aliofika sehemu ambayo alikuwa kaiweka kama ofisi ya muda akampigia mkewe simu kumwambia kuwa anatakiwa kurudi nyumbani haraka….

NB Naona hii ni zawadi ya wiki end. Na wazo la leo ni kuwa; Matendo mema ni msingi mwema wa maisha, usijali wasemayo, wewe tenda wema hata kama kwa kufanya hivyo ni kuwauzi wengine, kwani Wema katu hauzi.
Ni mimi: emu-three

Friday, January 20, 2012

Siku ya kuf nyani, miti yote huteleza




Unajua siku nyingi nimekuwa nikiwaza kwanini wakwe wanaogopana. Yaani wewe ukioa, basi kukutana na mkweo inakuwa taabu, nikajiuliza hivi mama mkwe au baba mkwe si sawa na mama au baba yako tu? Lakini inakuwa kinyume chake, wanageuka kuwa watu wa kuogopwa kama mtu mwenye ugonjwa wa kuambukiza. Nimesikia kuwa kuna hata wengine wanazidi kiasi, hasa wenzetu wa huko Kusini, nasikia kuna masharti kadhhaa ya kukutana na wakwe, mbona , na wakati nawaza hili nikakutana na tukio moja mbalo linahitaji kutafakari kwa wale wenyewe kuelewa.

Tuwasikilize watoto wetu, tuwe karibu nao, kwani huwezi juanini kinaweza kutokea leo au saa fulani, kwani , siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.

Kidsa hiki kimenifundisha mengi, hebu kisome kwa makini,hasa kwawale wanaopenda kuvaa vibukta,na wale wasiopenda kuwasikilza watoto wao.

Yupo jamaa mmoja alikuwa ndani kwake akiwa busy na laptop yake,mara akasikia hodi ikipigwa, kwanza akakunja uso,kwani hakutaka usumbufu, na akaendelea kufanya alichokuwa kifanya, wakati huo pembeni yake alikuwepo mtoto wake...

Mtoto yule mara kwa mara alikuwa akimwangalia baba yake kwa jicho la kujiiba, na mara nyingi akawa kama anamuonyeshea baba yake kwa ishara fulani , ambayo baba yake hakuielewa. Na baba yake akazania ni utundu wa mtoto wake ,kwahiyo akawa hamjali, baadaye akaona ni kero akamfokea na kusema;

'Nimeshakuambia sitaki usumbufu,....huoni nina kazi hapa..nenda kacheze nje…'yule baba akaendelea kuwa busy na laptop yake, siunajua tena siku hizi mambo ni vilaptop, laptop ni kama simu ya mkononi...kama huna kama mimi ulie tu...

Mara huyo mgeni kaingia na yule, mtoto alipogundua kuwa huyo ni mgeni gani, haraka akakimbilia palealipokaa baba yake na kutaka kumnong'oneza kitu sikioni, baba yake akang’aka na akarusha kibao, na kusema `hebu kule mtoto mtukutu wewe, hutaki hata kunielewa...'

Kibao kile kikampata mtoto shavuni, naye kwa hasira akaondoka zake akilia.
Mara yule mgani aliyeingia, akakutana na yule motto akikimbilia nje huku analia, alijaribu kumsemesha, lakini yule motto hakutaka kumsikiliza, akakimbilia nje…Kumbe mgeni yule aliyeingia ni mama mkwe. Mama kwasababu alikuwa na mazungumzo muhimu na baba yule, akaingia na kukaa kwenye kochi, ambalo lilikuwa wazi,mengine yalikuwa na vikorokoro vya yule mtoto, alivyokuwa akichezea, basi, mama yule kwa aibu ikabidi akae mkabala na mkwewe,akijua mazunguzmo yake ni mafupi tu ataondoka zake.

Mama alikaa baada ya kusalimia na jamaa yule, na jamaa yule akarudia kukaa mkao ule ule aliokaa mwanzoni,hakuwa na habari nyingine, , lakini ghafla ,mara akaona mama mkwe akiinuka na kuondoka, akashikwa na mshangao kidogo, hakujali, akazania huenda ni mambo ya ukweni tena, kwasababu mkewe hayupo ndio maana hakutaka kukaa kwa muda mrefu akaendelea kudonoa laptop yake.

Bahati nzuri mkewe akaja, na alipoona mama yake yupo nje kasimama, akasema kwa utani, `mama kwanini unamuogopa mkweo, hamjazoeaan tu, huku mjini mama, kaa ndani uongee naye...siulisema una shida naye mbona umesimamahuku nje…?’ akauliza binti wa huyo mama.

Baadaye mke mtu akampita mama yake na kuingia ndani, lakini wakati anataka kumpita mama yake, mama akamsogeela akitaka kusema jambo,, lakini yule binti alifikiria kwua huenda mama yake aliataka kumpokea, ule mzigo, akaona sio vyema, ngoja auingize ndani kiheshima,…..

'Mama wewe usijali karibu ndani,
'Sikiliza kwanza, ...'akasema mama akitaka kumwambia kitu binti yake, lakini yule mke-mtu akaingia ndani kwa haraka, na kuuweka ule mzigo kwanza, ili baadaye atoke nje ikibidi , na alifikisha ule mzigo, akasogea chumba caha maongezi kuhakikisha kuwa mumewe yupo, au kalala ndani, na abahati akamkuta yupo busy na kilaptop chake.
‘Mbona hukamribishi mama ndani….?’ Akauliza mke mtu.
‘Mbona nimekaribisha….’akasemahuku akiangalia jambo kwenye laptop yake.
Mkewe akatupa jicho, oooh, mungu wangu, ile bukta ….akakumbuka…aakjiuliza ina maana mama alishaingia ndani au bado…aakgeuza macho kuhaikisha kile alichokiona ni kweli au macho yake…akajikuta akiishiwa nguvu, lakini akajipa moyo kuwa huenda mama, alikuwa hajaingia ndani. Jamani hizi bukta sio za kuvaa wakati wote..zingine zinafumuka hata bila kujua..kumbe...

'Mume wangu…hebu inuk hapo haraka…na ukivaa hiyo bukta tena nitakuchapa viboko , sinilishakumbia kuwa bukta hiyo imefumuka....hebu toka kabadili hiyo nguo haraka, …huona mama mkwe yupo nje anataka kuingia...'akasema mkewe
Jamaa alipoinama kujiangalia karibu azimie, aliona aibu ya mwaka,...akaitupa ile laptop pembani na kukimbilia chumbani, huku akisema ;

'Duuh, kumbe ningemsikiliza mtoto wangu nisingeumbuka kiasi hiki, kumbe mtoto wangu alikua akitaka kuniambia jambo...ooh…nimeumbuka mzee mzima, kweli nyani akitaka kufa , miti yote huteleza…siku ikaharibika.

Wenzangu, hata tukiwa ndani kwako...usijiachie sana , wakati mwingine tuangalie na nguo za kuvaa, na pia tupende kuwa karibu sana na watoto wetu, ….

Hebu soma hii toka kwa Da Mija..mdau jirani …inafanana na hiki kisa:

Ni mimi: emu-three

Thursday, January 19, 2012

Kisa kinaendelea lakini.....



Kama nilivyokwisha sema tangu awali kuwa mtiririko wa kisa chetu utakuwa ukichelewachelewa kwasababu zilizopo nje ya uwezo wangu. Lakini hata hivyo, kuna jambo ambalo lilinifanya nikawie kidogo kuiweka sehemu inayofuata kwani ilihitaji utafiti fulani, kwani mambo yaliyotokea hapo yalikuwa hayaniingi akilini, na wengine natumai itakuwa hivyo hivyo, lakini yapo, na yanatokea..

Nilipofika sehemu hii hata mimi mwenyewe nilijiuliza hivi kweli haya mambo yapo,...na siku kadhaa nikayakuta yakitokea kwa mtu....nikajiuliza haya mambo kama yapo kwanini hayajawahi kuwekwa kitaalamu na dawa zake zikawekwa wazi, maana asikuambe mtu haya mambo yapo pia hadi huko uzunguni, lakini kwa silimia ndogo, ...pengine wenzetu hawayajali sana, na wakati mwingine, ikitokea mtu kapatwa na hayo mambo, wao wanaishia kumpeleka mtu huyo kwenye hospitali za wenye mtindio wa ubongo.

Nikajiuliza pia kwanini hayo mambo hayapo kwa kiasi kikubwa huko uzununi, yapo ndio, lakini ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na huku kwetu, ... Na ni ukweli usipingika kuwa wenzetu nikimaanisha wazungu, hawafuatilii sana dini, ili tuseme wao hawayajali hayo mambo kwa vile ni watu wa dini…, lakini huku kwetu, watu wanajitahidi kwa dini, na bado yapo, kwanini, ina maana hayo mapepo, mashetani yanahitaji watu masikini...nikajiuliza, na kujiuliza, je nyinyi wenzangu mnasemaje kwa hili?

Swali langu kwenu linakuja hivi, je kuna mizimu au mashetani?, Na kwa wale waliowahi kukutana nayo au kuwaona ndugu zao waliowahi kutokewa na mambo hayo, ilikuwaje na je walitumia njia gani kupambana nayo. Najua kwa ujumla njia pekee na ya uhakika ni kwa kutumia uwezo wa mungu(dini), lakini uwezo huu unahitaji imani kamilifu kwa muathirika, bila imani utaweza kweli kuyashinda haya matatizo sijui, nakuachia wewe useme uonavyo wewe au ukweli unaoujua wewe….

Wapo watu wanataabika kwa matatizo haya yanayojulikana kama kukumbwa na mapepo au mashetani na wapo watu wanayatumia kujipatia utajiri, na wengine wanakuwa ni mawakala wa mashetani , kwani wanayatumia mambo haya kuwachawia wengine,…na wengine wanayatumia mambo haya kujipatia riziki zao kwa kutibia mambo hayo, ….swali langu ni watu hawa wanaotumia mambo haya kihasi, kuawadhuru wengine, …. sijui nini kikubwa wanachofaidi hapo, na je kwanini wasingeliweza kuyatumia mambo haya katika njia chanya, wakafaidii na kuwasaidia wasio na uwezo.

Kisa chetu cha Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli, kimepiga hodi katika sehemu hiyo, kwani sehemu inayokuja itaingilia mambo hayo, nimeona niliweke wazi mapema, msije mkafikiri mimi napendeela hayo mambo au kuyaamini, hapana,…lakini kwa vile visa vyetu vimetokea kwa watu , nikaona ni vyema, pamoja na kupata maelzo ya kina, lakini ni muhimu na mimi mwenyewe nifanye utafiti kwanza, nisikie zaidi kuhusiana na mambo hayo ya mizimu, mashetani na nguvu za giza, kabla sijaiweka sehemu hiyo ambayo itakuwa ikitisha kidogo, lakini ndivyo ilivyotokea kwa jamaa yetu huyo , na waliomshuhudia wamesema ndivyo ilivyokuwa, sio kwamba kajitungia hadithi ….

Mkumbuke yote haya yalitokea baada ya ile ajali ya MV Bukoba, na hayo mengine yalifuatia badaye….

Swali kwako wewe mpendwa wa blog hii, tunaomba mchango wako kuhusiana na mambo haya ya mashetani na kwanini hapa Dar sasa hivi watu wengi, hasa wanawake wanakumbwa na matatizo haya, na utashangaa hata mashuleni kwa watoto, yanatokea haya mambo, kuna lini kulikoni?

Hebu soma sehemu hii toka wikipedia

Ni mimi: emu-three

Sunday, January 15, 2012

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-74 hitimisho 18



‘Docta nakuomba tafadhali usiviondoe kwanza hivyo vifaa...subiri subiri tafadhali..’akasema Rose huku akimsogela yule docta aliyekuwa akihangaika, kuondoa vile vifaa na kuanza kuviweka sawa, kitendo kile kimlishanagza yule Docta msaidizi na kubakia kumwangalia kwa muda kabla hajasema kitu.

Yule Docta in a bosi hakujua afanyeje kwa tukio lile la haraka, kwani alishapewa amri na bosi wake kuondoa vifaa hivyo mwilini mwa mgonjwa kwani uahi wa huyo mgonjwa ulikuwa haupo tena, akageuka haraka kumwangalia bosi wake ambaye naye alikuwa kashikwa na butwaa, ....

‘Nimeshapewa amri niondoe hivi vifaa na bosi wangu, sasa kwanini unaniingilia nisiviondoe, wewe huoni kuwa hakuna uhai tena hapa ...docta keshaona hilo na kuizinisha, na kila kitu kimeonyesha wazi, wewe unataka kufanya nini zaidi,....!’akasema yule dakitari msaidizi.

Wakati huo docta muhusika alikuwa kama kachanganyikiwa , maana hakutarajia kabisa ile hali kama hiyo itatokea hivyo, kila kitu kilienda sawa, na dalili zote za kupona mgonjwa zilionekana...hakujua tatizo hilo limetokeaje, ...alijuta kwanini alichukua muda kidogo kuja kuona nini kinaendele, hata hivyo hakutarajia tatizo lolote..., alishindwa kabisa kuamini kuwa kazi yake aliyoifanya kwa ufundi mkubwa haikuzaa matunda!

Wakati anawaza haya, alikuwa akitembea mwendo wa taratibu kutoka nje, na huku akisema kimoyomoyo, siku za mgonjwa zilishafika, hakuna jinsi ngoja nikawape taarifa wanandugu...akawa anaondoka huku akisita sita na wakati anafika mlangoni, ndipo akakutana na hawo mabinti wakija mbio mbio, wakampita bila hata kusema neno, na kukimbilia pale alipolazwa huyo mgonjwa, ambaye kwa sasa docta alishamuita maiti....

Alisimama ghafla na baadaye akageuka kuwaangali kwa masikitiko,... na pale aliposikia sauti ya Rose ikisema kuwa wasiondoe yale mashine, akashikwa na butwaam kwanza, akijiuliza kwanini huyu binti anasema hivyo, ndio ni docta, lakini hastahili kuingilia mambo yasiyomuhusu akasubiri aone nini anachotaka kufanya, kwani yeye alishajitoshekeza kabisa kuwa mgonjwa hana uhai tena, kila kitu kilishaonyesha dhahiri kuwa yule mgonjwa alishakata roho, kumwekea mashine ile ni kupoteza muda tu.

‘Sikilizeni, mimi nina uzoefu mkubwa na huyo mgonjwa, sio mara ya kwanza kutokea hivi,nawombeni msubiri kidogo,..hata hivyo nina wasiwasi na jambo moja...’akasema Rose na kusogelea ile mashine ya kusaidia kupumulia na akawa anaichunguza kwa makini, na wakati anafanya hivyo, Maua akamsogela yule mgonjwa na kumshika mkono wake huku akiomba kwa dhati... akisema kimoyomoyo.;

‘Oh, Mhuja, wewe ndiye uliyekuwa mume wangu wa dhati, niliyekupenda kwa dhati, licha ya yote yaliyotokea, lakini moyo wangu hautakusahau kamwe, nakuomba ewe mola, mjalie apone, mjalie ayashinde haya mauti, ili aje nimsimulie kwanini niliamua kuchukua uamuzi ule mgumu wa kufunga ndoa na rafiki yake...oh, mola wangu, nakuomba kwa dhati yako umsaidie huyu mgonjwa apone, kwani nina hisia kuwa bado umri wake wa kuishi upo....oh..ewe mola..’akaendelea kuomba na ni wakati ule docta alipoondoa kile kitu kama kichuma na ndio wakati huo machozi ya Maua yalikuwa yametua kwenye mkono wa mgonjwa, mara...


********

Wakati Maua anaendelea kuomba huku kamshikilia mkono mgonjwa wao, Rose alikuwa na kazi kubwa ya kuchunguza ile mipira iliyokwenda mwilini kwa mgonjwa na mara alipofika sehemu akashituka, aliona kitu kama kichuma kidogo sana, mara nyingi kinatumika kubania karatasi, ilikuwa sio rahisi kukiona kwani kilibandikwa kwa chini na sehemu iliyojificha, ni karibu kabisa na pale mpira huo ulipoanzia,...

Rose akasogeza mkono, lakini akasita, hakujua ni kwanini kichuma kile kiwepo hapo, na kabla hajakivuta akageuka kumwangalia Docta.

‘Unataka kufanya nini...’akasema yule docta huku akimsogelea Rose, kwani alishaona kuna haja ya kuingilia kati, kwani mtu akifikiwa na hali kama hiyo, hata kama ni docta anaweza akapagawa, asiamini ukweli ulivyo.

‘Vipi umeona nini, huyu kama mashine inavyoonyesha hana uhai, hebu angalia mwenyewe kule kwenye mtiririko wa mapigo ya moyo...hakuna uhai kabisa..kila juhudi tumefanya hata kumzindua kwa kumsukuma kwenye mapafu, kifuani, haikusaidia kitu...’akasema yule Docta, huku akimwangalia Rose na macho yake yakafuatilia kule anapoangalia Rose!

Docta macho yake yakatua pale..., naye akakiona kile kichuma, ambacho hakuwahi kukiona kabla, akasogea karibu kuhakiki macho yake, na hapo hapo akasogeza mkono na kukitoa....kilikuwa kimeweka kitaalamu, na rangi yake ilikuwa sawa sawa na mpira, kiasi kwamba usingeliweza kukigundua kwa haraka, kilikuwa kimakata kabisa mawasiliano.

‘Hiki kichuma kakiweka nani hapa, ...unajua hii,....,haiwezekani, ...kuna mtu kakibandika hapa ,....hebu niambieni mlipokuwa humu ndani aliingia docta yoyote, ulisema umeota, au ni kweli aliingia mtu...?’ akauliza yule docta huku akihangaika kuurekebisha ule mpira, hakuwa na haraka ya kuchunguza zaidi kwani ilijua haitasaidia kitu, maji yameshamwagika hayazoeleki..

‘Kwanza hakikisha kile kitu kipo sawa, tutayazungumza hayo baadaye.....’akasema Rose huku akiangalia ule mpira.

‘Haitasaidia kitu, kama ni makosa hayo yameshafanyika, iliyobakia ni kufanya uchunguzi, lakini sioni itamsaidiaje mgonjwa....huyu sasa ni marehemu, wewe ni docta bwana, ...’akasema yule Docta.

‘Nakuomba uhakikishe kila kitu kipo sawa, niamini nisemavyo,....’akasema Rose huku akikagua kila kitu kama kipo sawa, na Docta yule hakukaidi tena, akafanya lile lilowezekana, ili kumrizisha huyo binti, na mra hali ya hewa ikabadilika, hewa iliyokuwa imezuiwa kuingia mwilini ikaonekana kupita na mara mashine ikaanza kutoa mlio, kila mmoja akageuka kuangalia sehemu ile inayoonyesha mapigo ya moyo, ile misitari iliyokuwa imenyooka , taratibu ikaanza kujipinda...

‘Haiwezekani...’akasema yule docta na huku akihangaika kuweka kila kitu sawasawa, hakuamini...namara wakasikia sauti ya Maua kwa mara ya kwanza, kwani yeye alishazama kwenye kumombea mgonjwa...

‘Rose angalia huku, anatingisha mkono....oh, Rose, ndio nini hii, ina maana kazindukana, oh, ahsante munguee...Rose, angalia huku...’ilikuwa sautI ya Maua akiangalia vidole vya mgonjwa vikicheza cheza,....Rose alitaabsamu kidogo, hakusema kitu, aliendeela kuwajibika na mambo yale anayoyaona yanastahili kwa mgonjwa katika hali kama ile, hakujali kuwa pale yeye ni mgeni tu, alifanya yale anayojua ya kumuokoa mgonjwa anapokuwa katika hali kama hiyo, ...

‘Nakushukuru sana Docta Rose, sitakusahau katika maisha yangu, umefanya kazi nzuri sana...’ alisema yule docta huku akimkumbatia Rose,...na wakati anafanya hivyi, zile hisia zake tangu alipomuona kwa mara ya kwanza zilimjia, ...alitamani sana awe karibu na huyu binti, alitamani amtamkie kuwa anampenda na kumhitaji zaidi ya akzi...lakini cha ajabu hata pale alimpojaribu kumkumbatia Rose , rose yeye hakuinua mikono yake, alikuwa katulia kimiya...

Na alipoona kuwa Rose hakuvutika na lile tendo, akamwamchia haraka na kusema samahani, ...hata hivyo Rose mawazo yake hayakuwepo hapo, yeye akilini alikuwa akimuombea huyo mgonjwa, akiombea miujiza zaidi itokee, mgonjwa azindukane haraka...kwa uzoefu wake, hayo yalitokea, na hutokea hata mara tatu, na akizundukana, anazindukana kiukweli...hakukata tamaa. Na yule docta alimuachia Rose na kumsogelea mgonjwa, huku akionyesha uso wa furaha na kusema;

`Huu ni mujiza mmoja mkubwa sana katika kazi yangu hii ya udakitari, haijawahi kutokea hivi, mgonjwa kufikia hatua hii na ....ooh, hili swala lazima lifanyiwe kazi haraka, lazima huyo docta au sijui ni muumiani gani ashikwe haraka iwezakanavyo...’akasema yule docta huku akimalizia yale mambo muhimu yanayohitajika, na baadaye kila kitu kikawa sawa,na aliporidhika na hilo akachukua kile kichuma na kukiweka kwenye karatasi ya nyepesi ya nailoni, kama ushahidi ...akatoka akiwa na nia ya kukipeleka kwa wana usalama na kuwapa wale akina mama taarifa.

Na aliporudi akakagua ile mashine , na akawa kama ana mashaka Fulani, baadaye ile mashine ikawa inaonyesha kuzima tena, ile mistari ikawa inashuka kuonyesha kuwa mapigo ya moyo yanakwisha, Rose akaanza kuichunguza kwa makini ile mikanda kwa uhakika, moja baada ya mwingine, kuanzia mwilini hadi kwenye mashine, hadi kwenye mtungi wa gesi....sasa akawa hajali kuwa hiyo sio kazi yake kwa sasa, alijiona kama ndio yeye docta mhusika mkuu, na huyo ni mgonjwa wake, akawajibika ipasavyo, na mwenzake hakumsemesha naye akawa anahangaika kuangalia huku na kule, lakini hali iliendelea kuwa mbaya, tena mbaya zaidi....

Na ile mistari ikanyooka, kuashiria sasa hakuna matumaini tena.....


********


Wakati haya yakiendelea huku nje shangazi na mama walikuwa wakihaha huku na kule, walitamani kuingia kuona nini kinaendelea huko ndani lakini walishindwa, kwani walipojaribu mara ya kwanza walizuiwa na kuambiwa kwasasa hawaruhusiwi kuingia mapaka hapo watakaporuhusiwa, na wakati wanahangaika hivyo, walibahatika kuwaona watoto wao wakiwa ndani na shangazi alishikwa na butwaa kidogo, akasema;

‘Wewe umeona kule ndani, toka lini Maua akajua kazi ya udakitari, nimeona pale akisaidiana na docta kumshughulikia mgonjwa na cha ajabu Rose ndiye kaka pembeni akiwa kamshikilia mgonjwa mkono...’ akasema shanagzi.

‘Una uhakika na hilo, mimi hapa nawachanganya nashindwa hata kuwatofautisha, umejuaje kuwa ni Rose ndiye kaka na Maua ndiye anamshughulikia mgonjwa...?’ akauliza mama.

‘Wewe huoni walivyokuwa mwanzoni, kitambaa cha Rose kimefunika kichwa chote na Maua kajiachia na nywele zinaonekana...hajavaa kama Wahindi wenyewe...’akasema shangazi.

‘Mhh, mimi nahisi hawa watoto walituchezea,ina maana basi huyo tuliyekuwa naye muda wote toka nyumbani alikuwa ni Rose, ...kuna kitu kimefanyika hapa, nah ii ni hatari, inabidi tuwakanye, la sivyo tutkuja kujuta...’akasema mama.

‘Ndio maana tangu mwanzo nilikuwa na shaka, maana Maua namfahamu sana, lakini alipoondoka Rose, sijui ndio Maua, nilipokuwa nikiongea naye baada ya mwenzake kuondoka, niligundua utofauti katika majibu yake...nikahisi kitu, lakini nilidharau nakusema Maua hawezi kujiingiza kwenye hayo mambo , kwanza yeye ni mgeni kabisa katika miji mikubwa kama hii...’akasema shangazi.

‘Tuyaache hayo, sijui huko ndani mambo yanaendeleaje, maana kipndi kimepita, huenda alikuwa hajafa , sisi tulichukulia pupa...’akasema shangazi tena.

‘Hajafa, ile mashine haiongopi, ile mistari kwenye mashine inayoonyesha kwenye runinga, ikiwa ina miinuko miinuko inaonyesha mapigo ya moyo, lakini ikitulia na kunyooka moja kwa moja kama mstari, basi hakuna kitu...mgonjwa keshapoteza mapigo ya moyo na maana yake hana uhai, na unakumbuka yule docta alimwambia mwenzake aandike saa ya mwisho ya uhai wa mgonjwa...unakumbuka, halafu wakatuambia token haraka...’akasema mama.

‘Lakini hawakutuambia moja kwa moja kuwa ameshakata roho...mimi moyo wangu haujakubaliana na hilo, haiwezekani....’akasema shangazi huku akishika kichwa, na kusema; `Hali kama hii haijutakiwa kabisa iwakute wanetu, na hali zao hizi...’akasema shangazi.

‘Na kweli, lakini tutafanyeje...’akasema mama.

‘Hivi niambie unajua nini kuhusu uja uzito wa Rose, maana haijifichi, ni nani baba wa watoto wake, maana siku hizi ni kujizalia tu bila ndoa, umewahi kumuulizia?’ akauliza shangazi.

‘Nimuulizie wapi, kwani hajawahi kuniambia na hali hiyo nimeigundua huku kwa mara ya kwanza, nikuambie mimi na mwanangu tunaweza kukaa hata mwaka hatuonani, hasa nilipogundua yale yaliyokuwa yakitokea nyumbani, niliona njia bora ni kujenga umbali, kwasababu mimi nipo karibu na mume wangu, na kama ikuonana na motto, basii na mume wangu atakuwepo na matokeao yake ni ushirikina usio na maana...’akasema mama.

‘Kwanini mnayaamini sana hayo mambo, hawawezi kufanya kitu, labda mungu mweneywe apende, nina uhakika, ukiwa na moyo thabiti wa kutojali hayo mambo hakuna mtu atakaye kuweza....’akasema shangazi

‘Ni kweli kama hujawahi kukutana na mifano halisi,ukayaona mambo kiuwazi, huwezi amini, ...mpaka sasa najiuliza yule mzee aliyekuwa akikutana na mume wangu ni nani, kwani sikuwahi kumuona kitoka nje,au kukutana naye popote,ingawaje kuna wakati niliwaona wakiongea nje usiku, na wakihisi kuwa kuna mtu anawaangalia hutokea kitu, cha kunifanya nisiendelee kuwaangalia na nikiwaangaliana tena,huyo mzee keshaondoka....’akasema mama.

‘Kwahiyo unaamini kuwa ni mzimu,au ni shetani au ni mtu kweli....?’ akauliza shangazi.

‘Hapo siwezi kusema kuwa ni nani...’ akasema mama akionyesha uso wa kutafakari.

‘Tuachane na hayo,...ni mambo yako na mumeo na tamaa zako za pesa, kama ungeolewa na kaka yangu hayo yote hayangekuwepo, ....sasa nilikuuliza kuhusu Rose, je wewe unahisi mimba ya Rose ni ya nani,...’akauliza shangazi, nia ya mazungumzo hayo ni kupoteza muda, ili waondoe ile hofu iliyowatinga, na alipoona mwenzake anasita kujibu akaongeza kwa kusema, `U-si-iseme kaipatia huku shuleni...?’ akasema shangazi kwa uso wa kutahayari.

‘Mimi sijui, a simjui mwanangu tena, maana alibadilika ghafla hasa baada ya kuondoka hapo nyumbani , kuna kipindi aliniambia niachane na baba yake, nikamuuliza kwa kisa gani, akasema, hamuamini tena huyo baba, ana mambo asiyoyataka, sijui aliwahi kuyaona au vipi, na sikuwahi kumwambia lolote...nilijaribu kumdadisi bilamafanikio, lakini...niliona ni bota tujenge huo umbali kwa manufaa yake...’akasema mama akijaribu kukwepa swali aliloulizwa.

‘Sasa unahsi ujauzito huo ni wa nani, ina maana hakuna mtu ambaye unayemjua, ambaye alikuwa karibu na binti yako, maana sitegemei binti msomi kama yule, alijiachia tu , au ndio kaipata huko huko kwa wazungu, ...hapana shangazi yangu namuona alivyo...kajaa ujasiri na kujiamini, ni lazima ana mtu wake tena wa karibu anayejuana naye, ni lazima tumbane, na ina maana kweli wewe humjui huyo mtu, siamini, ..wewe ni mama gani usiyekuwa karibu na mwanao, hasa binti yako...’akasema na kugeukia mlangoni, pale walipomuona Docta akitoka, wakamsogelea na kumuuliza kujua kuna maendeelao gani.

‘Mhh, bado hatujawa na uhakika kamili, lakini kuna mafanikio kidogo yameonekana, tunajaribu kutizama sababu ya kupoteza fahamu kiasi kile hadi kufikia hatua iliyoonyesha kuwa kakata roho,na kuna jambp amablo tunalifanyiai uchunguzi, tutahitaji ushirikianao wenu baadaye, lakini kwa sasa mvute subira,...tutakuja na jibu muafaka baadaye kidogo...narudi huko kuona maendeleo...’akasema huyo docta na kuondoka.

‘Ana maana gani huyu , nahisi hajafa...’akasema shangazi.

‘Hawa ndivyo walivyo, kama mgonjwa haponi hawawezi kukuambia moja kwa moja, ila kama mgonjwa ni wa kupona wanakuambia moja kwa moja na hata kukupa matumaini, lakini inavyoonyesha hakuna cha matumaini wala nini sijui...sisi tuombe mungu tu, kwasababu niliyaona yale mashine kwa macho yangu mwenyewe, yakionyesha kuwa mgonjwa hana mapigo ya moyo...’akasema mama.

‘Useseme hivyo wifi....ooh, mungu wangu itakuwaje kwa hawa mabinti zetu, na wao wameamua kukaa humo humo ndani, sijuikwanini wamekubaliwa kubakia humo ndani, hivi hawa madakitari hawaoni ni hatari kwao...ooh, sijui tufanyeje, mimi hapa naona miguu yote imeisha nguvu,...’akasema shangazi.

‘Hawa mabinti zetu wapo kwa wataalamu hata likitokea , lakutokea watashughulikiwa haraka na hawo wataalamu wa hii hospitali, hilo lisikutie mashaka, ...mmh,...’akasema na kutulia,

Alimwangalia wifi yake kwa muda na baadaye akaongea peke yake kwa kunong’ona na kusema `Sijui kuhusu huyo mgonjwa, ina maana ndio keshatuaga hivyo, haraka kiasi hiki, hizo gharama tulizojitolea ndio zimepotea hivyo, mmh jamani, kweli maisha hayana thamani, mungu wangu na hawa watoto watawezaje kuvumilia hilo pigo, ooh, mungu wangu wajalie ujasiri wa kuvumilia, mmh, sijui tumuachie mungu...’

Licha ya kuwa mama alijifanya hajali, lakini moyoni kulikuwa hakukaliki, na baadaye liposhindwa kujizuia akasimama na kuangalia juu, na mara akakaa tena, na baadaye akasimama, na hilo miahangaiko ikamafanya shangazi amwangalie kwa mashaka na kabla shangazi hajasema kitu ...simu ya mama ikaita, mama alikuwa kama haisikii, ikaendeela kuita kwa muda , na shangazi akamuuliza kwanini hapokei hiyo simu.

‘Nishajua ni nani ananipigia,....’akasema huku akitamani kuizima ile simu, na vidole vilikuwa vikicheza cheza kwenye ile simu, huku akishindwa kuamua kwa haraka, kuwa aizime au aipokee, baadaye akasema; ’Huyu najua atazidi kunichanganya tu, ....’akaiinua ile simu na kutizama namba na alipogundua ndiyo huyo huyo aliyekuwa akimzania, akaipokea haraka haraka na kusema;

‘Sema mpenzi, kuna habari gani huko...?’ akauliza huku akijitahidi kuficha hisia zake zisitambuliwe kwenye simu.

‘Unasema nini, eti unasafari ya kurudi Uganda, kesho, kuna nini cha haraka hivyo, wakati tulishapanga hadi mwezi ujao..?’ akauliza mama kwa sauti ya kushangaa.

‘Biashara ipi hiyo, kuna biashara nyingine ambayo unaiendesha wewe na mimi siijui,niambie ukweli ,kuna nini kunakusukuma kwenda huko kwa haraka hivyo...?’ akauliza mama kwa hasira.

‘Mgonjwa hatujajua majaliwa yake bado, ...nani kakwambia kuwa haponi,...?’ akauliza kwa hamaki na kujiegemeza ukutani, huku anasikiliza nini mumewe anachoongea.

‘Yaani wewe unafuatilia kwa `remote control’ tu,....au sio,...?’akauliza mama, na akawa anaongea na wakati huo huo mumewe anaongea kitu kwenye simu, kwahiyo wakawa wanaongea kwa pamoja; na alipoona mumewe kanyamaza kumsikiliza akasema `Na atapona tu, mungu ni mkubwa, kama nyie mnasema hatapona nyie na mambi yenu,...kwani sijui nyie mumejiona ni Mungu au nani, lakini mtashangaa akipona...’akasema mama kwa kujipa moyo.

‘Sijasema hivyo kuwa unmuombea vibaya au kuhusika na lolote lile, usijahami kihivyo...’akasemakwa hamaki na kutulia kidogo na alipoona mumewe kanyamaza pia akaongezea kusema ‘Mimi ninachoshangaa ni wewe kusema kuwa haponi, wakati upo huko hujamuona huyo mgonjwa yupoje, hata kama unawasiliana na hawo madakitari, lakini sio cha kukatisha tamaaa kihivyo, sawa,...wewe ndenda safari yako, na nahitaji maelezo ya hiyo biashara, ukumbuke tuwashirika...sawa, nakutakia safari njema, mimi bado nahangaika na mgonjwa, safari njema...ahsante na matumaini yako mema ya kinafiki, kwaheri...’akasema mama na kukata simu kwa hasira.

‘Vipi mbona unamjibu mumeo kwa hasira hivyo...?’ akauliza shangazi huku kionyesha uso wa mshangao.

‘We acha tu, huyu tunajuana wenyewe, ukiona tunaongea hivi unaweza ukatufikiria vibaya, lakini muda mchache utashangaa utatukuta tunaongea lugha ya mahaba ya mke na mumewe, ndivyo tulivyo, ila ninachoshangaa ni hii safari ya harakaharaka ...ninashindwa kuelewa....’akasimama na kutemba huku kainama chini akiwaza.

‘Au yanahusiana na yale maeelzo uliyonieleza, kuwa ulimkuta akiongea na ndugu yake ambaye hujamgundua ni nani, huenda kuna jambo limetokea, lakini hayo hayatuhusu kwa sasa, usijiingize kwenye mawazo mengie makubwa , wakati hapa una mzigi usiobebeka wa mawazo...’akasema shangazi.

‘Nina mashaka makubwa, kuna uhusiano wa haya matukio, ...kumbuka binti yetu aliitwa, na hatujajua ni nani alimuita, kumbuka yale maelezo niliyokuambai kuwa nilimfuma mume wangu akiongea na simu na mtu, huyo anayemuita ndugu yake, kumbuka, huyo mtu aliaambiwa aafnye kila njia ili amuoe binti yetu...na kikwazo na huyu mgonjwa, huoni kuna kitu, je huyu mgonjwa kwanini afikie hatua ya kutaka kufa....ghafla ...’akakatisha ghfla, kwani walimuona docta akija kwa haraka, na mwendo wake uliwatia mashaka, ni kama mtu mwenye jambo nzito la kuwaambia,

Mama na shangazi wakawa wanasita kumsogelea,...ilikuwa kama vile wanataka kumkimbia docta kwa kuogopa taarifa mbaya, lakini kwa upande mwingine walikuwa wakihitaji kujua nini kimetokea huko ndani. Wakabakia pale pale wakiwa wamesimama kama wameshikwa na ganzi ya kiwliwili huku macho yao yakiwa yamewatoka kwa woga....yule docta akawasogelea kwa mwendo ule wa harakaharaka, na kuwakabili wale mama wawili na kabla hajasema kitu mara mlango wa ile wodi maalumu ukafunguliwa na Rose akatokea akiwakimbilia....na wote wakageuka kumwangalia.....

NB: Msishangae mkaona kama bado tunazunguka zunguka kwenye sehemu hii,, kuna mambo muhimu sana ambayo yalihitajika kuwekwa wazi ,... kwa wanaofuatilia kisa hiki kwa makini watayagundua hayo, na matokeo yake yataweza kutufikisha pale tulipopatarajia.

Neno muhimu la leo; Wakati wa matatizo, subira ni kitu muhimu sana, kwani mungu yupo na wenye kusubiri, hasa pale wanapokutwa na mitihani ya kimisha, tusikate tamaa...weka subira huku ukitenda haki,.
TUPO PAMOJA .




Ni mimi: emu-three