Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, December 8, 2011
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-60 Hitimisho-4
‘Shangazi sasa mbona tumepoteza muda wetu bure kuja hadi huku nchi za watu, haya huyo mgonjwa mwenyewe yupo wapi, maana hata hilo jina lenyewe ukiwatajia hawa manesi wanaishia kutucheka tu, Sweetie, unajua hilo jina linanikumbusha mbali sana, sijui masikini Mhuja yupo wapi, au ndio ilikuwa ndoto y ajinamizi,..shangazi ilikuwaje siku ile, mbona kila nikikuuliza mswali kuhusu siku ile unanipiga chenga, au ilikuwa ni ndoto …?’akauliza Maua.
‘Tatizo lako una tamaa ya mambo mengi, mimi nahisi ilikuwa ni ndoto, kama sio ndoto, huyo mtu yupo wapi, siku ile tumekwenda sote hadi nyumbani kwao Mhuja, uliambiwa nini…..?’ akauliza shangazi mtu.
‘Waliniambi nisiwaletee uchuro, kwani wao wameshasahau , na nimeamua kuolewa basi, hawanijui tena….lakini yule aliniambia kiutani maana nataniana naye sana…’akasema Maua.
‘Ndio hata kama mnataniana naye sana, iweje wewe umuone wao wasimuone, ina maana aliamua kuja kwako tu, bila kuwajali ndugu zake, hebu jiulize mara mbili,tatu…’akasema shangazi huku akimkwepa kuwamgalia Maua usoni, maana hata yeye mwenyewe aliachwa njia panda, kwamba, huyo mtu alikujaje pale kwenye harusi bila kupitia kwake, na baada ya hapo alikwenda wapi, ..
‘Kama ni jinamizi basi hilo ni la mwaka, huwa namuota , lakini ile nina uahkika sio ndoto, labda alikwua ni yule Tajiri alijibadili na kuja kwa umbo lake ili niteseke, ..hata hivyo, sio mbaya kumuona tena sura yake, natamani aje tena…’akasema Maua.
‘Acha balaa lako, wewe siulisema ulikuwa karibu kuzimia, …unafikiri mchezo wewe, ukutane na mtu ambaye alishakufa, uso kwa uso, utaweza kuhimili vishindo vyake wewe, acha kuinidanganya wewe…hebu tukasubiri pale kwenye kiti.
‘Sasa tunasubiri nini tena, mimi naona turudi nyumbani kwetu, hapa naona hakuna cha mgonjwa wala nani, kwanza mimi nashindwa kujua nitaongea nini na huyo askari.
‘Wewe subiri, Inspekta akija tutajua utaonea nini na pia tutajua huyo mgonjwa kaenda wapi, siunajua hizi hospitali za serikali zilivyo, wanapokea wagonjwa wengi, na inategemea huyo mgonjwa alipokelewa na nani…’akasema Shangazi huki na yeye akiwa na mawazo mazito, kwani kama huyo mgonjwa haonekani kwenye wodi aliyoelekezwa basi kna mawili, kapona karuhusiwa au vinginevyo yupo chumba maalumu..hakutaka kukitaja hicho chumba maalumu ni chumba gani, akaishia kuomba mungu sisije ikawa hivyo.
********
Walipofika uwanja wa ndege. Inspekta yeye alichukuliwa na gari lao la kazini , na shangazi na Maua wakaelekezwa hospitali ilipo, kwani shangazi hakupenda kupelekwa kwenye maeneo ya jeshini ambapo maaskari wana nyumba zao, alipenda kutafuta chumba chake mwenyewe, na likuwa na sehemu yake maalumu anapofikia..
‘Mimi sio mgeni wa hii nchi, nimefanya biashara sana huku, na nina wenyeji wengi, ngoja sisi twende huko hopitalini, utatukuta huko…’akasema shangazi na wakaingia kwenye taksii hadi kwenye hiyo hospitali waliyoelekezwa, walipofika wakaingia hadi sehemu ya mapokezi….
‘Mnasema mgonjwa wenu anaitwa nani.?’ Akaulizwa tena.
‘Nasikia ameandikisha kwa jina la Sweetie..’akasema shangazi.
‘Hilo jina ..mbona geni kwangu, …mwanamke kama sikosei maana …’akasema yule mtu wa mapokezi huku akitafuta katika orodha ya majina.
‘Hakuna jina kama hilo, …’akasema huyo mtu huku akisumbuliwa na watu wengine, na kila alipopata muda alijaribu kutafuta hilo jina bila mafanikio, baadaye akauliza `huyu mgonjwa wenu anasumbuliwa na matatizo gani, na yupoje?’ akaulizwa shangazi na huyo mtu wa mapokezi, na hapo shangazi alishindwa aelezee vipi, licha ya kuwa hisia zake zilikwua zikimtuma kwa mtu fulani. Alikumbuka siku ile ya harusi alivyopata ile taarifa ya juu juu, lakini hakuwa na uhakika nayo sana, ila hisia zake zilimtuma kuwa huenda ndiyo yeye, na angelipenda kujua hatima yake, na kama sio yeye, bado ana mambo mengi ya kufanya , hasa swali analouliziwa na binti yake Maua.
‘Tumesikia kuwa anasumbuliwa na matizo ya kichwa…’akasema shangazi bila ya uhakika.
‘Basi nendeni word namba tisa, kule mnaweza mkasaidiwa zaidi…’akasema huyu mtu wa mapokezi na kuwafanya shangazi na Maua waondoke pale bila mafanikio na wakiwa wamekata tamaa, mara Inspekta akafika;
‘Samahanini sana, kwanza kwa kuwakalisha kwa muda mrefu, lakini hata hivyo, taarifa zilizotujia kule kumbe hazikuwa makini, maana huyo mgonjwa hali yake ilikua mbaya sana, na alipofikishwa hapa, wakawa hawana la kufanya, juhudi zai zikagonga mwamba, …’akasema Inspekta akionyesha uso wa huzuni.
‘Kwani huyo mgonjwa aliandikisha jina gani..?’akauliza Maua.
‘Rose,….’ Inspekta ikamwangalia Maua kwa makini, kuna utata mwingine ambao nataka tuongee kwanza mimi na wewe, maana naona, kuna maelezo nimeyapata, nahisi kuna jambo limekosewa, na wewe ndiwe wa kunipa huo uhakika, …twendeni ofisini kwangu kwasababu hapa hakuna la kufanya tena…’akasema Insepkta.
‘Hakuna kufanya , vipi tena, mbona hujatumalizia kuhusu huyo mgonjwa, amefariki au imekuwaje..?’akauliza shangazi kwa sauti ya huzuni.
‘Alivyochukuliwa hapa, ni kama nusu mfu, hatujui huko alikopelekwa hali yake inaendeleje, watu wetu wanajaribu kuwasiliana na huko, ili kujua hali yake,kwani hata hivyo, hawakuwa na shauku naye sana, hadi , mimi nilipowaomba kufanya hivyo, .. lakini mawasiliano hayapatikani…’akasema Inspekta.
‘Kapelekwa wapi..?’akauliza shangazi
‘Kapelekwa India,..matatizo aliyokuwa nayo ya kichwa, yanahitaji upasuaji wa haraka, na hata hivyo alishacheleweshwa sana..sijui itakuwaje,…’akasema inspekta.
‘Sasa kwanini hawakumuwahisha mapema..?akauliza Maua.
‘Siunajua tena, hali ya kifedha, wakipatikana wagonjwa kama hawo ni mpaka kutokee wafadhili, na hata hivyo kwa kesi yake, haikuwa wazi sana,…na alipokamatwa, kwa vile maaskari hawakujua kuwa ana tatizo la kichwa, wao wakamperekesha, na nahisi ndipo walipotibua tatizo hilo, ..’akasema Inspekta akionyesha kuficha jambo .
‘Kwahiyo kosa ni la hao maaskari na tuseme ni kosa la serikali, kwanini walipogundua hilo wasifanye taratibu za haraka za kumsafirisha huyo mtu, mpaka afikie hali hiyo mbaya..?’akauliza Maua kwa hasira.
‘Huyo mtu kwanza haongei, hajijui,…yaani ilishindikana wapi pa kuanzia, lakini kama isingelikuwa fungu lililoachwa na Adam, na kukaja taarifa kuwa hizo hela zitumike kumsafirishia huyo mgonjwa , yangezungumzwa mengine, kwasababu historia ya huyu mtu haijulikani, na kuna watu wengi wanahitajika kusafirishwa kwenda huko kabla yake,, na kutokana na hali yake ilivyo ya kukatisha tamaa na historia iliyojengwa kuwa huenda ni mmojawapo wa wapiganaji wa msituni, ambaye alikuwa akitumia mbinu kujifanya hana fahamu huku anachukua habari na kwuasiliana na wenzake…basi kesi yake ikawa ya kupigwa danadana, huku wakisubiria kuwa ajifie ijulikane moja…’akasema Inspekta.
‘Jamani watu war oho mbaya, yaani mnasema kabisa ajifie ijulikane moja, ..’akasema Maua.
‘hayo ndio maisha,..nanihii..Rose, nitakuita hivyo hivyo..’akamwangalia Maua kwa makini , halafu akasema `lakini kila mtu na siku yake, keshapelekwa India, na kuna mambo mengi yametokea huku, na vijana wangu hawakuishia hapo , wamegundua mengi zaidi na ndio maana nataka kuongea na wewe,…Rose,..’akasema Inspekta huku akisita kulitaka hilo jina Rose, hata Maua akahisi kuwa huenda keshagundua kuwa yeye sio Rose, na ndilo alilolihitaji sana, hakupenda kuitwa majina ya watu wengine.
Shangazi alipogundua hilo akasema haraharaka, ‘Huwezi kuongea na yeye peke yake, inabidi kama nikuongea uongee nikiwepo, huyu ni mja mzito na namjua mwenyewe hali yake, pili sizani kama unamfahamu kama ulivyodai…kuna mengi yanahitaji uwepo wangu, usije ukamwanga mtama kwenye kuku wengi,…tafadhali sana’akasema Shangazi, na Inspekta akamwangalia Shangazi kwa makini halafu akageuka huku akiwaza jambo.
‘ Sio mbaya nimekuelewa, ndio maana nataka kuongea naye, kwani huenda kuna makosa ya utambuzi …hilo sasa nimeligundua..ok, sawa ni vyema, maana wewe kama mzazi utakuwa unajua zaidi , lakini kumbukumbu zote nimeshazipata toka ofisini, ila ni kwa vipi ilitokea hivyo…kweli utanisaidia wewe kama mzazi,sio mbaya…twendeni ofisini kwangu..’akasema Insepkta.
‘Kabla hatuajenda huko ofisini kwako , kuna mtu nataka kuonana naye, na kupata sehemu ya kukaa, sipendi kukaa maeneo yenu, siyaamini sana ..’akasema Shangazi.
‘Kama huamini sehemu za walinzi wa taifa, utaamini wapi tena, sawa najua unataka kuonana na nani…lakini kwa taarifa yako hayupo …nimeshajua kuwa ni nani..au nimekosea?’akasema Insepkta kwa kuuliza lakini ilionekana hakutaka jibu la hapo hapo, akijua kuwa bado hajawa na uhakika na hilo analoliwazia.
‘Sawa vyovyote iwavyo , lazima nifike hapo nilipokuwa nikifikia, sizani kwamba nitazuiwa, kwasababu yule mlinzi pale najuana naye sana, na tukitoka hapo tutakuja huko ofisini kwako…’akasema shangazi
******
Walipofika kwenye nyumba moja kubwa iliyozungushiwa ukuta, walikwenda moja kwa moja kwenye kibanda cha mlinzi, na huyo mlinzi alionekana kachoka, na usingizi ulishampitia, na walipogusa mlango tu, yule mlinzi akainuka haraka, na kuwakabili kwa,maswali, kuwa wao ni nani na wanahitaji nini. Shangazi akajielezea, na yule mlinzi akawaambia kuwa mwenye nyumba hayupo, waliopo hapo ni wapangaji tu, hana zaidi la kwuasaidia.
‘Naomba namba yake anayotumia sasa hivi, maana ninahitaji kuwasiliana naye…’akasema shangazi huku akimsogelea yule mlinzi, ili amgundue kua ni nani yeye.
‘Siwezi kukupa namba yake , bila kukujua , ..kwani wewe ni nani, ….’akasema yule mlizi na kuwamgalia shangazi sasa kwa makini, na alipogundua macho yakamtoka kwa furaja na kusema kwa sauti `Ooh, nimekukumbuka, samahani sana, siku nyingi kidogo, habari za Tanzania, habari za nyumbani, maana mimi sijfika huko nyumbani muda sasa, siunajau tena kazi zetu hizi…’akasema yule mlinzi kwa furaha.
‘Wewe kama umeama kuukana utaifa wako na kuwa mtu wa huku sio mbaya,… sawa, lakini kwenu ni kwenu tu, ipo siku utarudi tu kwenu, hata ukiwa ndani ya sanduku…’akasema shangazi , na wakati huo Maua alikuwa kajichokea na alikuwa akitafuta sehemu ya kukaa, akasogea mbele kwenye kiti na kukaa huku akishika mgongo,alikuwa kachoka na safari na bado kuna mambo yanayoendelea ambayo hayajui kichwa wala mguu, na mapaka muda huo hakuwa anajua nini kinaendelea, anakokotwa tu kufuata shangazi yake anavyotaka.
Alipokaa pale kwenye kiti, mawazo yake yakawa yanamkumbuka Maneno, na alipokumbuka hivyo , roho ikatibuka karibu atapike,…alimkumbuka pale alipompa taarifa kuwa wanasafari ya kwenda nchi ya jirani, ilibidi amuachie jukumu hilo shangazi yake, maana hata yeye mwenyewe hakuelewa vyema msingi wa hiyo safari, na hata alipoulizwa maswali mengi akashindwa kujieleza.
‘Kuna ndugu zetu wapo huko Uganda na mmojawapo tumesikia hali yake ni mbaya sana, tunahitajika tondoke kesho, na bahati nzuri kuna lifti ya polisi, kwahiyo usijali mambo ya gharama kuhusu hiyo safari..’akasema shangazi mtu.
‘Lakini huyu mke wangu,kusafiri nisingelipendelea, hata wewe shangazi unajua hali yake ilivyo, ya utata utata…’akasema Maneno.
‘Hilo usijali , kama nikiwa naye karibu usitie hofu, wewe huoni, muda wote ananihitaji mimi, sasa nikiamua kuondoka mwenyewe, ukabakia naye hapa, kwanza atabakia na wasiwasi, pili utashindwa hata kufanya hiyo kazi yako,kwa jinsi atakavyokusumbua…na ni vyema nikamtambulishe kwa ndugu zake wengine ambao hawajui wanaoishi huko Uganda, usitie shaka…’akasema Shangazi mtu, na Maneno hakuwa na upingamizi , wakaruhusiwa.
‘Twende ndani Maua, tutakaa hapa hadi hapo tutakapo rejea nyumbani, ‘akasema shangazi na kumkatiza Maua kwenye dimbwi la mawazo yaliyokuwa yameanza kujijenga kichwani.
‘Tutakaa hapa , kwanini tusikae hotelini, kwani hapa ni kwa nani..?’akauliza Maua akiwa kama mtu aliyetoka usingizini.
‘Utajua hilo baadaye, kwanza twende ndani…’akasema shangazi mtu.
Na wakati huo huo yule mlinzi akawa kamsogelea Maua kutaka kumjua kuwa ni nani, na alipomwangalia akaishia kushika mdomo kwa mshangao akasema;
‘Duuh, unajua nilikuwa sijamwangalia vyema, huyu..ooh, Rose, hapana, ….mbona utata…Rose umerudi lini toka Ulaya, haiwezekani, …wewe mtoto, mbona unafanya vibaya, hata vizawadi, halafu unakuja hapa unajikausha, mpaka, mama wa watu anajitambulisha kama mgeni…wewe, wee, halfu umeacha ule uzungu wako…eeeh, umeoelwa nini…?’akasema yule mlinzi akimwangalia Maua kwa makini, lakini shangazi hakumpa muda wa kusema kitu, akamshika Maua mkono na kuingia naye ndani.
‘Shangazi huyo Rose ni nani…maana karibu nimtapike huyo mlinzi, hivi kwanini hawa watu hawaelewi kuwa nina `aleji’ na wanaume..’Maua akauliza kwa ukali.
‘Hiyo mimba ina kazi, …kwahiyo unazania kila mtu atajua kuwa mimba yako haipendi wanaume, …na kuhusu hilo lako na mengine tutayamaliza huku huku, usitie shaka, lakini kila kitu kwa muda wake, usilazimishe, nafanya hivyo kwasababu maalumu, wewe vuta subira.
nb Bado tupo kwenye hitimisho swali kubwa hapa kwanini wanamuita Rose, Maua?
Nani anaweza kukisia?
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Wacha leo niwe spoiler, Maua ni pacha wa kufanana au identical twin wa Rose, nilihisi hivyo siku nyingi tangia pale Mhuja alivyokuwa anamwita Sweetie.
hongera sana me sidhani kama kuna kitu umesahau unaenda ipasavyo hongera sana
fetty
rose na maua ni twins hao ambao hawajuani na siri yao aaijua shangazi pamoja na hiyo familia
Hongera sana M3 kwa kazi nzito unayofanya ya uandishi wako. Naamini kabisa kipaji chako ni kikubwa sana na Mungu akusaidie kukiendeleza.
Kabla hata hujaanza kuandika hitimisho lako, hivi ndio nilivyokuwa najua vitatokea. Na mengine nimeongeza ktk utabiri wangu.
1. Rose na Maua ni mapacha tena wale wa kufanana (identical twin).
2. Mapacha hao walitenganishwa tangia wakiwa wadogo sana mmoja alikwenda kuishi Uganda na mwingine ambaye ni Maua alibakia Tanzania na aliishi kwa shangazi yake. Na ndio maana Maua au Rose wote hawana kumbukumbu za utotoni kama wao ni mapacha au wanatoka nchi moja. Rose anajijua yeye ni mganda wakati Maua anajijua kuwa ni Mtanzania
3. Kutokana na ukweli kwamba Maua ameshaolewa na Maneno, na Maua ana mimba tayari basi Muhuja hatopenda kuvuruga urafiki wake wa kudumu na Maneno, na wala hatoweza kumlaumu Maneno sababu tosha kwamba kila mtu (familia ya Mhuja, Maua, Shangazi wa Maua, Maneno) walifikia maamuzi ya kukubaliana na ukweli kwamba Muhuja amefariki ktk ajali ya MV Bukoba. Na kwakuwa Maua alikaa zaidi ya miaka 2 hadi kufikia uamuzi wa kuolewa na Maneno hiyo Muhuja anaona ni dalili tosha ya kwamba kweli Maua alikuwa ana mpenda Muhuja na ndio maana hakuamini kama amefariki.
4. Baada ya Maua kutambua kuwa wapo mapacha na Dk. Rose, na tayari Dk. Rose na Muhuja wanauaja kama Sweetie, basi Maua na Shangazi yake watamuomba Muhuja amuoe Dk. Rose. Hivyo ktk hitimisho kutakuwa na harusi ya Muhuja na Dk. Rose
5. Dk. Rose baada ya kukutana na Sweetie (Muhuja) na kuondokana na ile kuwachukia wanaume.....Dk. Rose ndoto yake ni kuja kuolewa na Sweetie na hata huko Ulaya alipo masomoni kila wakati anamuwaza Sweetie wake na kutaka kujua hatma yake itakuwaje.
6. Dk. Rose anaporudi toka Ulaya anafungua hospitali yake na kuwa daktari bingwa.
7. Itagundulika kuwa Maua na Muhuja walikuwa hawawezi kupata mtoto (sio kutokana na matatizo ya kizazi) sababu ya damu zao kutoendana na sababu zilizo nje ya uwezo wao. Ndio maana hata Maua alipanya mapenzi na Maneno siku moja tu Maua akawa mja mzito. Hivyo kiukweli kwa furaha ya familia zao, Maua na Maneno watakuwa na watoto, wakati Muhuja na Dk. Rose watakuwa na watotot pia.
8. Kumbuka kuna kipindi Muhuja (Sweetie) alifanya mapenzi na Dk. Rose hotelini mjini walipokwenda mara ya kwanza mjini...basi siku ile Dk. Rose alipata ujauzito. Hivyo Rose akiwa Ulaya masomoni alijifungua mtoto wake huko huko, mtoto wa Muhuja.
Akufaaye kwa dhiki
Maneno na Muhuja wataendelea kuwa marafiki wa kudumu kwakuwa kipindi cha dhiki/shida walikuwa pamoja kila wakati
Dk. Rose na Muhuja (Sweetie) wataoana na kuwa furahani daima sababu Dk. Rose alimfaa kwa dhiki Sweetie na kumpenda kwa dhati
Shangazi ataomba msamaha wa kuficha siri nyingi za familia hasa kwa Maua na pia kupelekea utengano wa Maua na Dk. Rose wakati bado wadogo sana alipompeleka Dk. Rose Uganda. Hivyo Dk. Rose na Maua watamsamehe shangazi yao na furaha kwenye familia kurudi.
Dr. Rose ataamua kurudi kuishi nchini Tanzania ili kuweza kuishi na Muhuja na pia kwa usalama wake huko Uganda baada ya kasheshe alizopitia huko.
Dr. Adam na wenzake watapelekwa jela. Na Dr. Adam atadhoofika sana hasa baada ya kugundua Dr. Rose amefunga ndoa na Muhuja (Sweetie). Lakini Dr. Rose kwakuwa ni daktari bingwa atamsaidia Dr. Adam kwenye afya yake na kazi mara akitoka jela. Hivyo Dr. Adam kuja Tanzania naye, na kuachana na kundi la kijasusi la huko Uganda. Anakuwa mtu mwema na family friend.
MAKULILO
Utabiri wenu na mawazo yenu yapo pamoja nami Rose na Maua ni mapacha, swali ni kwa vipi, na jibu limeelezewa katika utabiri wa Makulilo, lakini mimi sina uhakika sana na hilo, maana mimi sijui nini nitaandika katika sehemu ifuatayo mpaka nikianaza kuandika ndipo mambo yanajileta yenyewe...Nashukuruni sana,
Mkuu Makulilo, kweli umeingia ubongoni mwangu na kunisoma, nasukuru kwa utabiri wako unaokwenda sambamba na niwazavyo,ngoja tuone kama itakuwa hivyo hadi mwisho, tuwe pamoja
Sina la kuongeza naona mkulilo kamaliza kila kitu. kitabu kitabu twangoja
Post a Comment