Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 21, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-52




‘Kaka nimekujia tena, …nina jambo moja la kujadili na wewe, najua kwa ubishi wako, hili jambo hutaliona la muhimu sana kwako, lakini kwetu kama wanafamilia ni la muhimu sana…’akaongea dada mtu, aliyefika akionyesha kuwa kaja lakini ana haraka ya kuondoka. Na wakati anaongea aakawa anachnuza mle ndani , kama vile ndio mara ya kwanza kuingia, …aligeuka kumwangalia kaka yake ambaye alibakia kaduwaa, …kwani hakutarajia ujuio huo na alishapangilia safari zake,lakini kwa kumuheshimu dada yake ikabidi asitishe hiyo safari yake, akijua labda ni mazunguzmo mafupi tu.

‘Jambo gani tena hilo daa, usiniambie umekuja kwa ajili ya rusha roho zenu na ya kuwa pesa hazitoshi, najua mambo yenu yanakwenda bila nidhamu ya bajeti, haya niambie dada kuna nini zaidi..maana umenijia bila kujua kuwa utafika, nilisharatibu mipangilio yangu…lakini kwa vile wewe ni mtu muhimu sana kwangu itabidi nikatishe hii safari, haya kuna nini cha muhimu…?’akauliza Maneno akiwa kaangalia nje kwa kupitia dirishani.

‘Kaka kwa kujifanya mzungu, ..hilo la rusha roho ni mojawapo ya mambo ambayo nataka tuyajadili leo, najua huhitajiki sana kulijadili hili nililokuja nalo leo, sisi kama wanandugu tulikuwa na jukumu la kujadili na kuamua na mwisho wa siku tunakupa taarifa tu,…huo ndio utaratibu …..,lakini hili linahitaji uwepo wako. Kwanza ni kuhusu tarehe ya siku ya harusi, hiyo tarehe hatuiafiki, kwa sababau za msingi, sio tu tumeamua hivyo, tunazo sababau za msingi…’akasema dada huku akikaa vyema.

‘Tarehe hamuaifiki kwa vipi tena…’akauliza Maneno kwa mshangao.

‘Kama sikosei tarehe hiyo iliyokuwa imepangwa awali, ilipangwa na waolewaji, au sio…?’ dada mtu akauliza na kabla Maneno hajajibu kitu dada huyo akaendelea kuongea kuonyesha kuwa hakuhitai jibu la Maneno kwani alishajua jibu lake ni nini. `Katika maandalizi yetu tumejikuta shughuli zinagongana, na ujue kuwa shughuli ni watu, na kuna watu muhimu sana wanahitajik akuwepo, ….na ni lazima wawemo, kuna vikorombwezo kama rusha roho na mambo mengine lazima yawepo, kuna mambo mengi sana yanahitaji muda kidogo, kama wiki mbili mbele ya tareje tuliyopanga, hata kama ikiwezekana mwezi mmoja, lakini tunajali kuwa wewe ni mfanyakazi, kwahiyo angalau wiki mbili mbele….’ Dada mtu akawa anaongea kama cherehani, maana familia hii ilijalwia kwa kuongea.
‘Hapo siwaelewi, nasubiri hizo sabaabu za msingi maana sijasikia sababu hizo ni zipi, …..Nakusikiliza dada yangu mpendwa, maana umeshaharibu kila kitu kichwani mwangu,, …we ongea tu,…’akasema Maneno na kuja kukaa kwenye sofa, lakini macho yake yalikuwa yakikwepa kumwangalia dada yake kwani alijua kuwa hoja aliyokuja nayo hatakubaliana nayo kabisa.

‘Unajua mwanzoni tulipanga juu kwa juu, tukawatuma watu wetu huku na kule, na kwa ujumla shughuli hii mumeifanya ya haraka sana, kama vile mlitaka harusi iwe yenu pekee, kitu ambacho familia imekipinga sana. Sasa tulipotuima watu kwa kiherehere chao wakatupa uhakika kuwa tarehe hiyo haina tatizo, …nasikia kaka.’Dada akatulia kidogo kutaka kaka mtu amuelewe, halafu akakohoa kama vile kumshitu Akaka yake ambaye alishashikwa na butwaa.

‘Tatizo sehemu nyingine tukawa tumechelewa kulipia pesa, na hawa wafanya biashara wetu wanajali sana pesa, wakapata mtu mwingine aliyewaahidi pesa nyingi zaidi na kulipwa hapo hapo, unaona jambo hilo, ina maana kutafuta sehemu nyingine na mtu mwingine, na kikundi kingine, itachukua muda tena, na wengi wameahidi baaada ya wiki moja au mbili, kwahiyo ikabidi tuweke nafasi hiyo ya wiki moja mbele, …na hata ikibidi wiki mbili mbele kwa ajili ya watu wetu wanaokuja toka kijijini., …hili ni mojawapo muhimu sana kuwa kuna watu wetu muhimu tarehe hiyo hawataweza kuwahi, na ni muhimu sana katika mambo ya kifamilia na kimila hayo wewe utajifanya sio muhimu kwako, lakini sisi kama wanafmilia ni muhimu sana....’akaongea dada mtu safari hii kwa taratibu.

‘Dada mambo ya kimila, hayo nilishawambia sihusiki, kama ni ngoma, sawa, chezeni, lakini hayo mnayosema matambiko, sijui mambo gani ya kimila, ….hapana, dunia hiii haiendi hivyo, kwanza hata imani zetu za kidini hazituruhusu hayo, na nataka ndoa yenye maadili ya kidini, sio kimila, vinginevyo ningesema tukaoe kimila…hilo halina hoja kwangu na naona sio muhimu sana….’akasema Maneno, na dada mtu alijua kuwa hapo wanaweza kubishana mpaka kesho. Anamjua ndugu yake huyu toka utotoni, kwani wamkuwa karibu karibu sana, huwa wakianza kubishana jambo watakesha mpaka aingilie mtu, hakuna mtu anayekubali kushindwa.

‘Ndugu yangu, hili sio la ubishi wa utotoni, sasa tumekuwa watu wazima naongea kama dada yako, nikiwa nimeiva kifamilia, sio wewe umeiva kisasa, kisasa kina mpaka wake, kama tutaamua kila kitu cha kimila tukiache kwasababu ya kujitia, au kutaka tuonekane wazungu au watu wa kisasa, tutaendelea kuwa watumwa wa watu wengine, …hebu jiulize nini maana ya uhuru, mojawapo ni kuwa na uhuru wa mambo yetu ya tangu enzi za mababu zetu, ina maana wao walikuwa hawana akili walipoanzisha hayo mambo …achana na uzungu, achana na usasa, achana na kutawaliwa kiakili, angali sana ambo yenu ya asili tusiwe watumwa….’akasema dada mtu kwa hasira.

‘Hayo sio mambo ya uzungu, hayo sio mambo ya usasa, ni mambo ya kiimani, ndoa hujengwa na mambo ya kiimani, mila hapo hazina nafasi, ila kwa kunogeza, sawa, kachezeni ngoma zenu , hilo siwakatazi, na kwa kusaidi hilo, hapa kuna vikundi vingi vinajua mila zote za Kitanzania, na sio Kitanzania tu , hata kiduania nzima, tutaawalika kama mnataka mila zetu zionekane, sio lazima kuwaita watu toka huko kijijini…lakini sitaki hayo mambo mengine sijui mnaita matambiko …ya nini hayo, eti mpaka watu waje toka kijijini kuyafanya hayo…, mnataka nieleweke vipi na watu wa familia ya kikeni, nimeshaambia kuwa ndoa yetu ni ya kidini, sasa mnataka kuleta nini hapa…hapana hilo liwekeni pembeni…’akasema Maneno .

‘Hilo sio lengo langu kubwa sana, lengo langu kubwa sana ni tarehe ya ndoa, tumepanga kuwa isogezwe mbele, wiki moja au mbili mbele, ili tupate muda wa kujipanga vyema, kwa ajili ya wanafamilia muhumi kuhudhuria, na wageni wengine na hivyo vikorombwezo vinginevyo, naongea kama muwakilishi wa familia, hili sio swala la dada yako peke yake, ni swala la wanafamilia, hutakiwi kulipinga na nimekuja kukupa taarifa tu kwa vile wewe na mimi tupo karibu sana, ilitakiwa kupewa taarifa tu yamekwisha lakini mimi nakujua kuliko watu wengine wote, ndio maana nikaja kukuelzea hili, unanaielewa kaka…’akasema dada kwa ujasiri.

‘Mwanzoni umekuja vyema, ukasema tujadiliane, sasa unataka uharibu, hapo tutakosana, na mtakuta nafunga ndoa peke yangu na washikaji zangu haafu tutasubiri hayo mambo yenu , lakini wakati huo nimeshafunga ndoa yangu.Dada hili halitawezekana tarehe ni ile ile piga ua,….’akasema Maneno huku akiwa kakunja ngumi na kuitikisa.

‘Tarehe itasogezwa mbel epiga ua, penda usispende,…mimi ndio dada yako na unanijua vyema, na sio kwamba nafanya kuonyesha kuwa mimi ni nani, ila nafanya kwa nia njema ya kifamilia, ukiwemo wewe, utakuja kunisifia baadaye kwa hilo, na ni lazima ujue kuwa ndoa itafungwa kwa mujibu wa familia, sio kwa kujitakia wewe upendavyo na hao watu wako, kama ungelitaka ungelifunga kimya kimiya, lakini kwa vile unajua kuwa ndoa inaigusa familia ndio maana ukatuarifu, sasa fuatana na wanafamilia, umenielewa hilo kaka…?’akasema dada mtu kwa jaziba huku akiwa kashika kiuona licha ya kuwa kakaa kwenye sofa.

‘Hapana hilo halitawezekana dada , maana nimeshaongea na waolewaji, na waliniuliza mara mbili, mara tatu ya jana nilipoongea na shangazi mtu, ambaye ndiye muhisika mkuu nimemkubalia kuwa taerhe ni hiyo hiyo. Unasikia dada, nilimuhakikishia kuwa tarehe ya kuoa ni siku hiyo hiyo iliyopangwa toka awali, ..hebu kaa katika upande wangu utalielewa hilo…hayo maswala mengine sioni kama yana umuhimu sana, kama mnataka mtayafanya hata baada ya ndoa…hiyo ndiyo kauli yangu mimi muoaji…basi’akasema Maneno.

‘Hivi wewe unaongea kama nani , kaka, kwanza kwanini ukaingilia mambo yasiyokuhusu sisi tulishakuambia kuwa maswali ya harusi hayakuhusu kwa sasa, wewe ni mgeni rasmi, waandaaji ni sisi, ilitakiwa ukae na sisi kwanza kabla ya kutoa tarehe hiyo, kazi ya kuongea nini kifanyike kati yetu na wao, inasimamiwa na mshenga wetu, je mlikaa na mshenga mkaliongelea hilo, au uliamua kuongea na wao peke yako…mbona unatuzarau kiasi hicho, sasa utajua mwenyewe jinsi ya kuwaambia, kwasababu nakuona kuwa wewe ndio mshenga, wewe ndio muoaji , wewe ndio familia, na utafanywa muolewaji pia badala ya kuwa muoaji…usibiruzwe kaka…,’akasema dada mtu.

‘Dada naona sasa umenichoka, unataka kuleta ubishi wa utotoni, …unajua dada sio kwamba najiamulia mwenyewe tu bila kuwa na sababu za kimsingi, naomba unielewe hivyo, sio kwamba naizarau familia yangu, hapana, ….mimi na familia ya mtarajaiwa wangu tumekuwa tukiishi nayo kwakaribu sana, tangu marehemu akiwemo, na aliniaminimapaka akniachia familia yake, na hili la kuoa ni moja ya kuonyesha upendo wangu kwako,kwa familia ya mke matarajiwa na upendo wangu wa dhati kwa maarhemu….’Hapo Maneno akatulia akimkumbuka marehemu, na dada amtu akamuelewa , aye akautulia kidogo.

‘Sasa dada mimi nilionekana kama mmoja wa wanafamilia hiyo husika, na tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara..sio swala la kuburuzwa, mimi ni kama ndugu yao, na ilipofikia hili swala, tulishakaa nao na kuongea kwa mapana na kuangalia kipi kifanyike na kwa muda upi, kwa manufaa ya pande zote mbili, kwahiyo swala la lini sherehe ifanyike sikuona haja ya kukutana na familia yangu kwa muda huo, na nilipowaambia hamkupinga hoyo tarehe, mliikubali, …na kwa vile ilikuwa shughuli ya haraka kwasababu za afya ya mtarajiwa, muda huo ulitosha kabisa kwa sisi kujiandaa, na haikuwa na haja ya kufuata milolongo yote hiyo, sijui mshenga aende wakajaidli arudi, tukae tuongee …sijui muende mkaangalie tarehe hiyo ni…hapana dada hayo yamepitwa na wakati…naomba mnielewe, mengine sin haja ya kuyaongea…yana msingi …’akasema Maneno kwa kutulia.

‘Nimekuelewa sana kaka yangu, na kukuelewa huku sio kwamba nakubaliana na hayo maneno yako kama jina lako, hapana nimekuelewa kwasababu wenzetu wamkuwahi mapema,wameshakuweka hapa…’akanyosha kiganja cha mkono na kukigonga na kidole cha mkono mwingine. `Na hili tusipoliangalia mapema, tutakupoteza kaka yetu, tutakuwa hatuna usemi mbele ya wifi mtarajiwa, kaka utapotea , utakuwa mke badala ya mume, angalia sana hilo, sisi tunyajua haya yote hasa yanapoingiliwa na sisi wanawake, siumesema shangazi yenu alikuja hapa, mkaongea…nilijua tu, huo sio uamuzi wako,..’dada mtu akainuka haraka kutaka kuondoka.

‘Dada sasa unaondoak vipi, tumefikia wapi, nataka ukiondoka hapa ukanitetee, kumbuka dada tumekuwa pamoja, na tulikuwa tukisaidiana toka utotoni, hili unatakiwa unisaidie kwasababu lina umuhimu sana kwangu…dada mkikutana pigania tarehe hiyo hiyo kama kweli unanijali ndugu yako, na mkitaka kuibadili kinguvu, kwakweli mtakuwa mumeniweka mahala pagumu, na sijui kama nitaeleweka vipi,…naomba tafadhali uwaambie wanafamilia kuwa tarehe ni hiyo hiyo, vinginevyo tutagawana mapande, kitu ambacho sikitaki…’Maneno akawa anongea huku anamkumbuka shangazi mtu alipokuja hapo na kuongea naye, alikuja kama mbogo utafikiri kuna kosa limefanyika, alionyesha uso wa hasira.

‘Maneno nimekuja hapa kwa nia moja kuwa ndoa nataka ifungwe haraka iwezekanavyo, kwa ajili ya afya ya mwanangu, hili nalisisitiza tena, kwasababau wewe mwenyewe umelikoroga…na chanzo ni mimi kuwaruhusu mwende huko Arusha, umemweka mwenzako katika wasiwasi mkubwa, hajiamini,…’Akasema Shangazi mtu.

‘Kwanini hajiamini, kwani kuna ambolimetokea, anahis kuwa ana…’Maneno akasita kumalizia hayo maneno ayke akijua kuwa anaongea na mkwe wake.

‘Najau utawaza hilo, kwasababu wewe hukuon akuwa umefanya makosa, na najuta kwanini sikukuweka ndani kwanza ukawa ana adabu, kuwa familia yetu sio ya kuchezewa, …lakini nimekuja kuyazungumz ahaya nikiwa na maana kubwa sana, juzi alikuja mshenga wa yule jamaa ambaye toka siku nyingi anataka kumuoa Maua, akaweka mikwala kuwa yeye ndiye mwenye haki ya kumuoa Maua, sijui haki ghani hiyo…watu wengine bwana,anadai kuwa ana haki kwasababu ndiye aliwahi kuleta posa, …sasa kama hutumtaki …’akasema Shangazi huku akicheka, lakini kumbe moyoni kwa Maneno wivu ulishamjaa.

‘Eti anadai kuwa atafanya kila njia kuhakikisha ndoa hii haifanikiwi, kama atakataliwa yeye….kwangu mimi sikutishika, ila nyie vijana mkishauriwa mfanye nini cha muhimu hamfuatilii , matokeo yake mtaingia kwenye ndoa ka uanza kugombana na huyo jamaa kwani anajivunia pesa, ….sitalkipenda hilo …ndoa itakuwa inalega lega, lazima muanze kushirikiana kuanzia sasa, kuaminiana,…na dawa kubwa kwa sasa ni kuhakikisha mnaifunga ndoa hiyo haraja iwezekanavyo, msiwape hawo wabaya nafasi…hilo ni la kwanza ambalo nalilisisiza kwenu…tumekubaliana kuwa tarehe itakuw ile ile au sio…?’akauliza Shangazi.

‘Kwangu mimi hakuna mashaka, tarahe hiyo inajulikana labda itokee zarura, na mimi sio mungu, tunachoomba ni iwe hivyo, kwanini shangazi una mashaka na hilo, Maua ana lolote jipya..na umemuuliza kwanini ilikwenda kule hospitalini?’akauliza Maneno akiwa na mashaka.

‘Nimemuuliza, yeye alikuwa na mashaka ya afya yake, na nilimsuta sana kuwa ile hospitali ina jina baya, wengi wakeidna kule wanaonekana kuwa wamekwenda kutoa uja uzito, sasa yeye asijipeleka kule walimmwengu ni wabaya watazua mambo yao, na hata huyo docta ni muongo, anaweza akakubangika ugonjwa ambao huna ilimradi apate pesa…na ndilo nimekuja pia kukuonye akuwa yule jamaa sio wa kuamini sana, amewahi kumambikia msichana wa watu mimba kumbe hana, ilikuwa alimanusura angeingizwa kwenye kile chumba na mengine yangefuata, msiwe na hamasa za kumuona yule mtu atakuharibieni kila kitu…unanielewa mwanangu..? akasema shangazi.

‘Aaah, shsngazi kama unanihakikishia kuwa Maua hana tatizo alikwenda kule kwasababu ni ya kutibiwa tu, sina shaka, lakini nimekuwa nikiwaza sana, kwamba kwanini alitokea mlango wa nyuma, na…’akasema Manneno na shangazi aliposikia hivyo akashituka, kumbe Maneno alimuona akitokea mlango wa uani, …

‘Kumbe ulimuona, …Maua ananiogopa sana, na nilishampiga marufuku kutibiwa pale, kwahiyo aliposiki nakuja akaona anikimbie, …hakuna cha msingi cha kufanya hivyo zaidi ya kuniogopa. Sasa kunzia leo si wewe au yeye kukanyaga ile hospitali, nakushauri na kukuamuru kama mama, …vinginevyo mtakuja kuniambia, hakuna hata haja ya kukutana na huyo mtu kama ulikuwa na mpango huo, …yule namjua sana, ile nataka mliweke wazi, ni mmojawapo wa watu nisiowaamini…sawa, vinginevyo nitaisimamisha hii ndoa, akaolewe na mtu anayeniskiliza…’akasema Shangazi kwa msisitizo.

‘Shanagzi mbona umekwenda mbali kiasi hicho, na unaona hunitakii mema, unataka kuninya’nganya tonge mdomoni, Maua nampenda sana shangazi siwezi kumkosa, nakuhakikishia hilo, ilimradi umenihakikishia kuwa hakuna jambo lolote sina haja ya kuhangaika kwa hilo, ninakuamini wewe shangazi, lengo langu ni kumsaidia Maua kama kuna lolote, unajau yeye amekuwa akijifanyia mambo yake kwa lengo kuwa haihitajii msaada wa mtu yoyote, na matokea yake anaumia, ndio maana nilitaka kujua kama lipo hilo nimsaidie , sina nia nyingine mbaya nakuahidi kuwa sitakanyaga ile nyumba iitwayo hospitali maalumu, nimesikia sifa zake, na nitajitahidi kuhakikisha kuwa Maua hakanyagi hapo….’akasema Maneno kwa unyenyekevu na kumfanya Shangazi atulie roho yake akijua sasa ammbo yanakwenda vyema.

‘Na tumekubalaiana kuhusu tarehe, kwasababu kuna wageni wangu wanatoka nje, wamekata tiketi ya kwenda na kurudi, hawawezi kuja hapa waambiwe kuwa tarehe imebadilika, ….ni muhimu sana ujue hilo wewe ni msomi, mambo yanakwenda ki muda, usiyapeleke kienyeji maana najua wakikutana wanandugu wengi kila mmoja an lake, sisi tunajali sana muda, …tafadhali zingatia hilo ni kipindi cha kujua nini unachokifanya sio kuburuzwa huku na kule, sasa ni mueleeko mmoja wa wewe na mkeo hakuna cha wengine kukuingilia…nakuasa kwa hilo, kwaheri..’akasema shangazi na kuondoka.

Maneno alipokumbuka hayo Maneno ya shangazi na kauli za dada yake akajikuta njia panda, je afanaye nini cha kuhakikisha hii shughuli haitetereki, akachukua simu na kumpigia mshenga wake, ambaye alikuja baada ya muda mfupi na kuongea naye , alimweleza kuhusu mgongano wa siku ya harusi na anataka yeye asimamie uapnde wake, kuwa harusi tarehe ni ile ile, na anachotaka yeye afanye ni kwenda kwa waolewaji akachukue hizo sababu muhimu azifikishe kwa familia yao.

‘Afadhali nimeongea na wewe hili, maana hapa nilikuwa njiani kwenda huko huko kwa waolewaji, na bahati nikapokea simu yako, nimetumwa na familia yenu kwenda kuwaambia kuwa tarehe ya ndoa imebadilika, na hili nilijua mumeshakubaliana nalo, nashanga kusikia kuwa wewe upo kinyume na familia yenu, …naona ajabu, sasa niende kwa msimamo gani, wa tarehe ile ya awali au tarehe hii mpya?’ akauliza mshenga.

‘Nisikilize mimi muoaji, …tarehe haijabadilika,, wewe tafuta mbinu za kuja kuwaambia ndugu zangu ukitoka huko, kwani najua ukifika huko msimamo wao ni tarehe ya awali, na mimi nipo pamoja nao….’akasema Maneno.

‘Upo pamoja na famili yako au na famili ya waolewaji?’ akauliza Mshenga.

‘Si kwamba naipinga famili ayangu kwa tarehe hiyo, lakini henu animabie kama nilivyokuelezea awali, kama ingelikua wewe ungelifanyaje, maana waolewaji walishaniuliza swali hilo mata zaidi ya tatu nikawapa uhakika kuwa tarehe ni hiyo hiyo…’akasema Maneno.

‘Sasa mimi ni mshenga, hakujaharibika neno ngoja niende kuwaona, mabo yatajiweka sawa, ikishindikana inabidi familia zote mbili zikutane, zijadiliane, halafu tutaafikiana, sioni kuwa kuna tatizo, na kwa vile nmesikia kuwa wewe mhusika mkuu upo katika msimamao wa atrehe ile, ile sasa ninajua nini cha kufanya, hilo niachie mimi, ngoja nikaonane na waolewaji, hili muhimu sana kwangu….’akasema na kuondoka.

Kesho yake ilibidi kuwe na kikao cha familia mbili, kwani kila mmoja alikuwa kasimamia msimamo wake na kikao hicho kilikuwa kigumu sana, na hakuna aliyetaka kubadili msiamamo wake. Mwishowe shangazi akasimama na kusema;

‘Unajua tusiwe kama watoto kwa hili hatutaki kushindana kwa kitu kidgo kama hichi, ili twende sawa, kuna wageni wangu wametoka Ulaya, kama Maneno ana ubavu wa kuipia fidia ya tiketi ili kubadili siku zao za kukaa hapa sawa, pili gharama za makulaji , kwasababau wamefikia hotelini, tatu, gharama za usumbufu kwasababu siku hizi tunakwenda kitaalamu msizanie kuwa haya maswala ni ya kwangu mimi na Maua kuna wanafamilia wanaishi nje na wameamua kuja kushuhudia hi ndoa, ndio maana tukasisitiza sana hiyo tarehe, na tuliuliza mara nyingi sana…’akasema Shangazi.

‘Ulimuuliza nani, wewe ulimuuliza Maneno, Maneno hana mamlaka na familia, anayo lakini kwa ,makubaliaono, na hili linaonekana kuwa ulimshawishi Maneno kwa matakwa yenu, sisi ndio waoaji tunahitaji tarehe ile ambayo binti yenu akija kwetu kusiwe na shaka, kutokana na mipangilio yetu, kuna wazee wetu kwa haraka hivyo hawataweza kuhudhuria…tunakuomba utuelewe na sisi , …kwamba hata sisi tuna gharama kama hizo, …’akasema muongeaji wa waowaji.

‘Mimi naona tutashindana kwa swala dogo sana, hili tutalitatua kama muoaji atataoa kauli yake ya mwisho, naomba tumuite aseme mwenyewe anataka tarehe gani, kama atakubalaina na hilo la familia yao, basi tutaangalia jinsi gani ya kuchangia hizo gharama, kama atakuabaliana na tarehe ya awali inabidi wanafamilia mliangalie upya jinsi ya kuliweka sawa, tarehe isiwe kikwazoo cha jambo muhimu kama hili..’akaseme Mshenga.
‘Huyu muoaji hawezi kutuamulia , keshwekwa sawa, mkimuita hatatoa jibu lolote la muhimu..’akasema dada mtu.

‘Hpana yeye ni mtu muhimu sana, hasa ukiangalai kigharama , ukiangalia na muda wake wa kazi, na yeye ndiye anajua maisha yake ya baadaye, sisi ni wapiga debe tu, tunaomba hili mliangalie kwa makini…’akasema mshenga na wazee wengine wakakubaliana na hilo, na hapao akaitwa Maneno.
Maneno alipofika hapo kwenye kikao akakumbuka jana kuwa alipigiwa simu na baba yake mkubwa, baba yake huyu ni mtu maarufu katika familia yao, na alipenda aje kuhudhuria hiyo harusi , akaomba isigozwe mbele kidogo ili afike na kundi lake la wanafamilia wengine...

Maneno akabakia kuduwaa, na kujiuliza haya yote ni ya nini,na wakati anawaza haya huyu mzee alisisitiza kuwa kwa vile Maneno ni mwanaume peke katika familia ya ndugu yake, hakupenda kabisa kuikosa hiyo shughuli muhimu, …Maneno alishindwa kabisa kumshawishi kuhusu tarahe iliyopangwa awali, kwani alipomwambia kuwa tarehe ilishapangwa, baba huyu alimuuliza `ina maana hutaki mimi baba yako niliyekulea nihudhurie hiyo harusi…na tarehe hiyo sitaweza kufika kwasababu ya mipangilio ya hapa nyumbani, tafadhali naomba uisogeze mbele angalau wiki mbili mbele...!’ Basi Maneno akabakia kimiya,na hakujua afanye nini, sasa kaitwa kautoa kauli yake,…sasa afanyaje

NB JE INGELIKUWA WEWE Ungelichukua uamuazi gani,?

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Mimi said...

ingekuwa mimi ndo maneno ningekubali wiki 2 mbele. kwa sabb maua mimba yke haijaanza kuomekana. mana ingeonekna maneno angejua na asingekubali kuoa. da shangazi nae ana wasiwasi jamani. hadithi tam kweli. natamani kitabu hata kesho.mana hutaki kukosa kipengele hata kimoja. kila la kheri m3. tupo pamoja sana.

Anonymous said...

no way out hapo maneno akubali tu kulipa hizo galama maana yupo kwa wakati mgumu sana....

Anonymous said...

hawa nao wanachelesha mambo, mi naona tarehe ya harusi ni makubalianao ya watu wawili kwani wao ndio wanaangalia hali za kifedha na kiafya na kiimani, halafu ndio wanawashirikisha ndugu jamaa na rafiki. sasa kama ndugu walishakubaliana na tarehe ya mwanzo kwanini wabadilike ghafla, mi kama ningekuwa muoaji ningeshikilia msimamo ule ule, uwepo wa ndugu wote haumaanishi ndio mafanikio ya sherehe, unaweza kusubiri ndugu wote ulimwenguni wafike waone unavyooa na wasifike kamwe kila mtu ana dharura!

AMMY K said...

KAMA ME NINGEKUBALI NIBADILI TAREHE, SIWEZI KUFANYA HARUSI BILA NDUGU ZANGU , HASA BABA.HADITHI INAZIDI KUWA TAMU M3. I WISH INGEKUWA KITABU.

emuthree said...

Maneno akikubali kubadili tarehe, atakosana na shangazi ya MAUA, na ukumbuke alishaulizwa mara nyingii na kukubaliana na tarehe hiyo, sasa itakuwaje ilihali shangazi ana msimamo wake, huwa ni wale watu wakiamua wameshaamua, huyo anafanana tabia na dada yake Maneno.
Ukumbuke kuna baba mkubwa, huyu ndiye aliyemlea Maneno, na kifamilia ni mtu muhimu sana anatakiwa kuwemo kwenye hiyo harusi, akikosekana, mmmh, `kwa vile sijamzaa mimi, hakumbuki fadhila....'
Maoni kama haya nayataka sana, nashukuru kwa waliotoa maoni yao, na hili limetokea na linaendelea kutokea hasa inapokuwepo shughuli inayojumuisha familia zenye mtizamo tofauti.
Hapa tunakutana na wale wanawake wanaojiita wa `shoka'...mhusika anasema kama ungelikuwepo siku hiyo ungeangalia senema na akina Tyson na nani vile waliopigana nje ya ulingo.
Tupo pamoja, je wengine mnasemaje?

samira said...

mimi naona maneno apeleke mbele shughuli family ni muhimu sana ila sasa shangazi ndo ivo haelewi,m3 yote tisa mauwa mwenyewe mlengwa anasemaje maana ndo muhimu kuliko wote mtu mwenyewe hayupo happy na maneno
cant wait m3 upo ok lakini i ask you more than three time hujanijibu nakutakia kheri sana dear

emuthree said...

Tupo pamoja wapendwa. Samira nakushukuru sana kwa kuniwazia kuhusu maswala ya kikazi. Bado nipo palepale na yule aliyetakiwa kuja kuchukua nafasi yangu keshafika. Na taarifa nilizopewa ni kuwa tutashirikiana naye hadi hapo nitakapoambiwa vinginevyo. Kwahiyo nipo kwa kudra za maanani!

Jane said...

AM happy 4 u m3, maana pressure ilishaanza kupanda na kushuka.Huwezi amini nasoma usiku wa manane tena kuanzia sehemu ya 39 mpaka nimefikia 52 ambayo ndo ya mwisho uliyopost, sikuwa kwenye access ya internet karibu mwezi mzima. Jamani mi nakumbuka tarehe tulipanga mimi na mr then wengine tuliwapa taarifa tu juu ya tarehe tuliyopanga. Haarafu sijui kwa nini Maua na shangazi wanamficha Maneno kuhusu ujauzito aliyonao Maua??? Anahaki ya kujua hali ya mke wake mtarajiwa after all ni yeye mhusika sasa kwa nini afichwe????? naona wanafanya makosa makubwa. All the best m3 three can't wait to read your book. usiku mwema.

Anonymous said...

Hio