Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 21, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-40




Adamu alibakia kwa muda ameshikilia simu mkononi, utafikiri bado anasubiri kuongea na huyo mtu aliyekwisha kuongea naye karibuni, lakini walikuwa wameshamaliza kuongea, ….kilichomfanya aduwae kwa muda ni hzio taarifa alizozipokea kwa huyo aliyempigia simu, …ilikuwa kama mtu kamtonesha kidonda kilichokuwa kimepona…Hakuamini kabisa kuwa Rose kawa na mwanaume mwingine, …haiwezekani,
…ina maana juhudi zote zile za kumuondoa yule mtu aliyekuwa akimzuzua ilikuwa kazi bure,…sasa kapata mtu mwingine, …lakini ni nani,huyo mwanaume . Akakumbuka jisni alivyokuwa akiwasilina na huyo mtu wake;

‘Kwanini mshindwe kumuona huyo mwanaume, ina hatoki nje, ….hata kama hatoki nje ina maana hamuwezi kuingia humo ndani ya hoteli mkamjua ….haiwezekani? ’akauliza Adam kwa hasira.

‘Tunaweza kuingia, lakini hatuna ruhusa ya kukagua kila chumba, ….’akasema jamaa yake huyo.

‘Hamuweze kumshawishi huyo mkuu wa ulinzi kwa namna yoyote ile hata kama ni kwa kutumia nguvu…mumeshindwa hilo?’ akauliza tena Adam kwa hasira

‘Bosi natumai unamfahamu vyema mkuu wa ulinzi wa hiyo hoteli,…sio mtu wa mchezo, ndio tunaweza tukamvamia au kitu kama hicho, lakini baada ya hapo labda awe maiti….. unakumbuka alivyokuwa kazini, polisi kabla hajaachia ngazi, huyo jamaa ni komandoo, unakumbuka jinsi gani tulivyo hangaika naye, juhudi kubwa zilishafanyika ili hatimaye awe kwenye kundi letu, zikashindikana,….’ Akasema huyo mtu wake.

‘Hazikushindikana, ila wakubwa waliona haina haja naye tena, baada ya kuachia ngazi,….au ni yupi huyo unayemuongelea isije ikawa namuongelea mtu baki, ni nani huyo au simkumbuki vyema, lakini hata hivyo , kama mliweza kupenya na kuingia ndani wakati wa kampeni yetu, na kama mliweza kufanya hilo tukio la kummaliza yule mnafiki mtashindwaje kumdhibiti huyo jamaa, au kazi imeanza kuwashinda….kama mumeshindwa nimwambie mkuu…maana hata mimi nachoka sasa kufuatilia kila kitu, hiyo ilikuwa sio kazi yangu, ila kwasababau ya Rose, umesema huyo jamaa ni nani..?’akasema Adam

‘Unamfahamu sana bosi, ni huyo huyo askari aliyestaafu polisi, wakati akiwa nahitajika sana na Serikali, yule aliyekuwa anatuogopesha sana, hashikiki…basi ndiye mkuu wa ulinzi wa hiyo hoteli..’akasema huyo mtu.

‘Una maana Ojong, mnoko yule…ooh, kumbe bado tunaye, kazi ndogo hiyo, nitaongea na mkuu atajua jinsi gani ya kumuweka sawa, sio tatizo hilo, nitawapa ishara ya kuingia humo ndai muda ukiwa muafaka, kama ni huyo msifanya papara, kweli mtaumbuka, ikishindikana nitakuja mwenyewe, najua nikikutana na Rose nitakuwa nimemgundu huyo mtu ni nani. …’akasema Adam na kwa muda huo aliskia mlio wa gari likisimama nje, akajua kuna wageni wamekuja kwake, akawa kaishikilia simu huku akiwaza, na huku askisubiri kukutana na hawo wageni asiokuwa na miadi nao..

Mara mlango ukagongwa na Adam akaishikilia ile simu kwa nguvu mkononi kama vile anamalizi hasira zake, hakutaka kukutana na mtu kwa wakati kama huo, lakini hakuwa na jinsi…mara mlango ukagongwa tena, ….akaiweka ile simu juu ya meza na kuusogela ule mlango, huku akiwaza ni wageni gani hawo, maana hata gari lilikuwa limesimama sehemu ambayo hakuweza kuliona vyema, hakugusa mlango akasogea pembeni na kusema `ingia..’ kwa sauti ambayo aliihis sio yake .

Mlango ulipofunguliwa moyo wa Adam uliyeyuka toka kwenye hasira na kurudi kwenye hali ya kunyenyekea, kumbe wageni hawo ni watu wa heshima kwake, ndio wanaomuweka mjini, walikuwa ni watu watatu, wawili ni viongozi wa udhamini wa hospitali, na mmoja hamjui vyema, …

‘Mbona mumeniingilia bila taarifa…kuna tatizo waheshimwa…?’ akauliza Adam huku akiinama kwa unyenyekevu, hutaamini ni yule mtu aliyekuwa na hasira ya kumvunja mtu shingo.

‘Hakuna tatizo Docta ila ni moja ya utendaji wetu, …na samhani kwa kukujia bila taarifa, lakini kama unavyokumbuka kikao cha mwisho tulitoa hitimisho la uchunguzi wetu na tukafikia muafaka kuwa Rose asipojitokeza katika muda tuliaainisha, basi inabidi hatua za haraka kuchukuliwa...,' akasema yule kiongozi wa wafadhili huku akikaa kwenye kiti , na wenzake wakafanya hivyo hivyo.

‘Ndio lakini nimekwisha waambia kuwa Rose ana matatizo huko mjini, …’akaongea Adamu kwa shauku, akiwa hajui wakuu hawa wamekuja ni jipi jipya, na alipoona wapo kimiya akaendelea kusema
`Nawahakikishia kuwa sio kusudio lake, na nina wahakikishia kuwa keshapata hizo fesa alizokuwa anadaiwa…’ Akaongea akionyesha uso wa furaha kuwa anaongea jambo ambalo litawasuuza mioyo ya hawa waheshimiwa, na alipoona hawajasema kitu tena akaendelea kuongea kwa kusema ;

`Je nini tulikuwa tunataka… ni pesa au sio, na sio lazima tumuone yeye mwenyewe,…lakini hata hivyo kama tunamuhitaji yeye mwenye kujieleza, tusubiri afike ili ajitetee, tusimuhukumu mtu akiwa hayupo tutakuwa tunakiuka haki za binadamu, na pili na ndilo la muhimu ni kuwa tunahitaji pesa, na huyu mtu anazo, kwanini tusumsubiri akalipa kwanza, kama ni mengine yakafuata baadaye, kwasababau tukichukua hatua nyingine, tutampa mwanya wa kukacha kulipa kabisa…’akasema Adam.

‘Tatizo lako Adamu, wewe sasa umegeuka kuwa mwanasiasa, na ujue kazi yetu haihitaji siasa, tunahitaji utekelezaji wa haraka, na kwa muda muafaka, …tupo vitani , tukisema mbele songa, hatuhitaji mjadala, na ukumbuke kazi iliyopo mbele yetu inahitaji muda mfupi sana, ujue nchi yetu inakwenda kwenye mabadiliko, na hujui nini kitatokea huko baadaye…ni bora tukafanya juhudi za makusudi kulinda vitega uchumi vyetu….na kwa hilo basi hatuna muda wa siasa, ngoja nikuambie kile kilichotuleta hapa….’akasema yule mwenyekiti.

‘Sawa nawasikiliza waheshimiwa….’akasema Adam akiwa anawakagua kila mmoja kwa wakati wake.
‘Ndio hivyo Adam,…’akasema yule mdhamini mwingine , halafu akamgeukia kiongozi wa udhamini, kama vile anamuonyesha ishara ya kuendelea kuongea. Na Kiongozi wa wadhamini, akamgeukia yule jamaa mwingine ambaye alikuwa mgeni kabisa kwa Adam, na kumshika begani, huku akisema ‘ Huyu hapa ndiye atachukua nafasi ya Rose, atakuwa msaidizi wako,…’akamgeukia Adam na kumkazia macho, huku akiendelea kuongea kama mtu anayetoa amri.

‘Huyu ana uzoefu wa kazi hii, Rose haoni ndani, na pili tunamjua vyema hana shida nasi, mtashirikiana naye na utaona juhudi zake,…anaitwa Docta Hama,’ akamgeukia Adam na kumkazia macho huku akisema ‘Docta Hama, huyo mbele yako anaitwa Docta Adam, ndiye mkuu wa hii hospitali toka ilipoanzishwa, yeye tunamuita muwanzilishi, …kwahiyo tunakuomba ushirikiane naye kwa hali na mali na mengine utaambiwa baadaye, na yeye atakuonyesha majukumu yako na yeye , na sisi tutawasikiliza nini mumepanga, ….hatuna muda wa kupoteza tena, huyo Rose akija kama ni lazima kuwepo humo hospitlini atakuwa kama docta wa kawadia tu….sawa…?’akasema yule kiongozi wa wazamini na kusimama kutoka kuondoka.

Adamu alitaka kulalamika kuwa taratibu zimekiukwa kwani, alitakiwa kushiriki katika mchakato wa kutafuta msaidizi wake, lakini leo imekuwa kinyume chake. Hii ilionyesha dalili kuwa walishamchoka na huenda hawamuamini tena, …alikuwa keshalitafakari hilo siku nyingi na matendo ya wadhamini hawa yalionyesha dhahiri kuwa hawapo naye sana kama ilivyokuwa awali, na sasa wanamtumia tu kwa manufaa yao kwa vile ni mzoefu na anajua siri na membo mengi ya hiyo hospitlini na miradi mingine.

‘Karibu Docta, nshukuru kukufahamu na tunakukaribisha kwa moyo mmoja, licha ya kutahiniwa na kuingizwa bila mimi kufahamu, lakini wewe isikutie shaka, nitashirikiana na wewe kwa moyo mmoja kwani lengo lengo letu kubwa ni kuhakikisha hii hospitli inakuwa na kuleta maendeleo, …yote hayo najua unayafahamu, …sijui ndio mumeshanikabidhi au ..leo mnanitambulisha tu…’akauliza Docta Adam, akishikana na huyo mgeni mkono.

‘Tumekuja kukutambulisha tu, najua utalalamika kuwa tumekiuka taratibu , lakini kipo kippengele cha kuturuhusu kufanya hivyo pale tunapoona kuwa inabidi…..na ilivyo kama tungelikuachia usingechukua hatua hii mapema, ndio maana tukaamua kuchukua jukumu hili, ila tunakuhakikishai kuwa tupo pamoja nawe, juhudi zako tunaziunga mkono…usiwe na wasiwasi Docta Adam…’akasema yule kiongozi wa wadhamini huku anamshika Docta Adam Mkono na wengine wakafanya hivyo na kutoka nje…

Adamu alibakia akiwa anawaza mengi, alihisi hatima ya ndoto yake haipo tena, na kila hatua anajikuta akikabiliana na mitihani mingi, sasa kama ni hivyo Rose keshamkosa, kwani hatakuwa karibu naye tena, na muda wa kumfuatilia utakuwa haupo, na keshaletewa msaidizi ambaye kila akimwangalia anahisi ndiye atakayechukua nafasi yake, akajaribu kukumbuka alimuona wapi, lakini akili yake haikuweza kumtambua vyema, ila anahisi alishamuona mahali.

Alikumbuka jinsi alivyoingi kwenye mambo hayo, akiwa katolewa kwenye dimbwi la umasikini, na kwa aili ya umasikini huo akawa anafuta kila anachoambiwa, hakuwa na jinsi kwani hawo waliomsaidia hadi kufika hapo ndio hawo hawo waliokuwa wakimpa amri kuwa afnye hiki au kile…na akwa anamfanya ilimradi maisha yake yawe mazuri ingawaje mengii aliyokuwa akiyafanya hakupendezwa nayo.

‘Sasa muda umefika wa kuamua moja, niishi hivii kama mtumwa au niitoe kabisa na hawa watu, naona maisha yangu na malengo yangu hayatakamilika kama nitakuwa na hawa jamaa, kwanza wananifanya niishi kwa mashaka, na pili hawanithamini tena…’akajikuta akiongea huku akitembea mbela na kurudi nyuma, ….

‘Ndio kwakweli wamenisaidia sana, lakini nini hatima yake, niwe mtumwa wao, hapana, lazima nifanye jambo, lazima nijitoe, lakini nikijitoa ina maana ndio basi tena, na huenda wakaniua, hawa watu hawana huruma katu, nawajua, sasa nifanyeje…akawaza, na kabla hajakaa kwenye kiti mlango ukagongwa, akajua labda na hawo jamaa wamerudi kwahiyo akainuka kwa ustaarabu kwenda kuwafungulia.

Alipofungua mlango akageukia ndani , hakuangalia nje kumwangalia aliyegonga, akijua ndio hawo, na hakuwa na hamu ya kuongea nao zaidi alichotka ni kuwasikiliza halafu waondoke zao ili pate muda wa kutafakari mambo yake…alirusi kukaa huku akiwa hajaangalia ni nani anayeingia, na alipokaa na kutulia na kuinua kichwa kuangalia mlangoni, ……

Alibakia mdomo wazi, …alibakia akiwa kaduwaa, akapikicha macho …na kujua sasa mambo yameanza…moyo ukaenda mbio, na shinikizo la damu likapanda….ndiyo yeye….akasema kimoyomoyo…
NB Nilitakiwa kuendelea kwenye sehemu hii, lakini muda ..na wenye mamlaka wanaingia, tukijaliwa na nawatakia Ijumaa njema, tuzidi kuombeana heri.


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Precious said...

mambo yanazidi kuwa mambo, M3 pole kwa majukumu na challenge unazokutana nazo kazini kwako...me bado ina imani kubwa ipo siku utajiajiri kwa kazi ya mkono wako mwenyewe ya uandishi maana Allah amekupa kipaji kikubwa sana. Mungu yu pamoja nawe na tuko pamoja nawe kimaombi pia...Inshallah Jumaa Kareem na w/end njema kwako M3 na wapenzi wote wa blog hii

emuthree said...

Ahsante sana Precious kwa kuwa nami, nami kama kuna kitu ninachokiomba ni kujiajiri ili kuondokana na huu utumwa, maana kuna kazi unafanya huku umetulia kichwa lakini sio kwa hawa jamaa, unafanya unasimangwa...taabu kweli kweli, ila wahenga walisema `unalalamika hakitoshi, hakifai...kwasababu unacho, je wale wasio nacho kabisa watasemaje..' kwahiyo namshukuru mungu, ingawaje mpaka sasa hawajaniambia lolote, mpaka mwenzangu atakapokuja kukaimu nafasi yangu!

Yasinta Ngonyani said...

ungu yu nawe na pia nimependa ulivyosema "kwasababu unacho, je wale wasio nacho kabisa watasemaje.." TUPO PAMOJA