Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 19, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-39




‘Sikilza Ojong, nimefuatlia sana taarifa zako, na nimegundua kuwa ulikuwa askari mwema na mchapakazi wa hali ya juu, lakini ghafla ukaacha kazi, na uliacha kazi kipindi ambacho serikali ilikuwa inakuhitaji sana…na sababu ulizotoa hazikuniingia akilini. Baadaye niliona mambo yaliyokuja kuchomekwa chomekwa, haya ni dhahiri kuwa yalipachikwa ulipoocha kazi kuwa ulikuwa sio mwaminifu, na mambo mengi yasiyokuwa na ukweli au ushahidi, ni ilikuwa kulichafua jarida lako kwa taarifa zisizona ushahidi, mimi nilipoletwa hapa nilizifanyia kazi nikagundua kuwa zimepandikizwa kwa makusudi, ili usipate mwanya wa kurejeshwa kazini….’akasema Inspekta Hoko huku akiwa kashikilia kadaftari kadogo alikokuwa akiandika kumbukumbu zake.

Inspekta Hoko, alikuja hapo hotelini kwa nia ya kuonana na Rose, ambaye kwa taarifa za polisi alitakiwa kukamatwa kama mshukiwa namba moja wa mauaji yaliyotokea hapo hotelini. Kwa upande wake alilipinga hilo na akaamua kufanya uchunguzi wa kina yeye mwenyewe…. Na aili fanikiwe hilo aliona ni vyema akakutna na Rose wakaongea uso kwa uso bila kuwepo mtu mwingine pembeni, hakutaka aongee naye akiwemo wakili wake, …hili limekuwa moja ya kikwkatika kazi yake ya kupambana na uhalifu unaotokea hapa nchini,…aliwaza kwanini anakutana na vizingiti kama hivyo, lakini ndio sehemu ya kazi, alijipa moyo kuwa kwa vyovyote hiyo hali itakwisha.

Leo alipanga kuja kuonana na Rose, akijua atamkuta yeye mwenyewe, lakini alipofika akaambiwa Rose kasema ataongea na maaskari tu pale wakili wake atakapokuwepo, ….akajisemea moyoni, kama Rose angelijua nini anachotaka kukifanya angelikubali akutane naye, kwani anachofanya ni kwa ajili yake,…lakini…. Alijua hizo ni mbinu nyingine zimewekwa na hawa mafisadi. Alipogonga ukuta huo akaona atumie mbinu za kiaskari, alichofanya ni kumwachia kazi hiyo msaidizi wake, yeye akarudi ofisni kwake, akabadili nguo na kuvaa kiraia na alipofika jioni akaingia pale hotelini kimiya kimiya.

Kwa uzoefu wake ilimchukua muda mchache kugundua alichokitaka, na kabla hajafanikisha hilo akaona kwanza akutane na mkuu wa uasalam wa hiyo hoteli, ambaye licha ya kuwa wanajuana, lakini imekuwa vigumu kukutana naye kutokana na majukumu yao. Leo akaona ndio muda muafaka, na huenda akafanikiwa makusudio yake.

Wakati anasubiri muda wa kueleekea juu ambapo alishagundua ni wapi ofisi za mkuu huyo, akawa anawaza, kuhusiana na kadhia nzima hii ya kundi haramu ambalo alishagundua kuwa lina mkono wa watu wakubwa wa serikalini. Watu hawo ndio pia kwa namna nyingine wana uhusiano na makundi yanayoongoza mapigano ya msituni. Kundi hilo limeweza kupenya kila nyanja, na kwasababau hiyo huwezi kumwamini mtu yoyote, ….Hata hayo auaji yalipotokea, alijua kabisa kuwa kuna mkono wa hilo kundi, na huyo binti anayezaniwa kuwa ni mshukiwa namba moja, katumiwa kama chambo tu.
Lakini ataonanan vipi na huyo binti, ikawa kikwazao kikubwa , hakutaka kutumia rungu la dola, alitaka kufanya uchunguzi huo kinamna yake, kwani akitumia rungu la dola lazima atakwama tu, ..akaweka dhamira kuwa alzima aonane na Rose kwa namna anayoijua yeye mwenyewe, hata bila kumshirikisha yoyote, lakini kwanza lazima akutane na mkuu wa hiyo hoteli, kwani alishagundua kuwa anajua mengi kuhusiana na hilo kundi, na huenda ndicho kilichomfanya astaafu kazi kabla ya muda wake.
***
Mkuu wa usalama wa ile hoteli alikuwa kashuku kitu, aligundua jambo, lakini hakuwa na uhakika nalo, kuna mtu amemgundua kuwa ni mgeni humo hotelini alimuona akiingia, lakini hakumuona akipitia njia ya kawaida ya kujitambulisha pale maulizo, …..lakini alimpotea katika kamera yake kiajabu ajabu, kitu ambacho hakijawahi kutokea, inaonekana huyo mtu sio wa kawaida, anawezaje kupita pale mapokezi bila hata walinzi kumuona….huyu anaweza kuwa ni jambazi lililokubuhu,..haiwezekani, katika kazi yake hiyo hajawahi kushindwa kiasi kile, …ni nani huyu mtu na kapotelea wapi, akajaribu kurudisha rudisha nyumba komputa yake kutafiti kuwa atamgundua, lakini kila alipokaribia kumuona, alijikuta akikumbana na tukio jingine muhimu la kuangalia….
‘Sasa kazi hii inakuwa nzito, ina maana ninatakiwa kupata msaidizi, kitu ambacho sikihitaji kwa sasa….’akajisema huku akiangalia huku na kule.

Alirudisha tena hadi kwa huyo mtu aliyemuona, akamvuta kwa karibu, lakini picha ya sura yake haikuonekana kabisa, akajaribu kuchunguza mienendo ya mwendo na umbile,…..hakuweza kumuhusisha na mtu yoyote. Huyu mtu alionekana ni mtaalamu sana, na inaoenakana anajua kuwa kuna vyombo vya kunasa matukio ndio maana alichukua tahadhari zote hizo, akaweka chombo chake sawa sawa, na kuanza kufuatilia alipotoka hapo alieleekewa wapi na wakati anafanya hivyo simu ikaita.
‘Kuna mgeni anataka kukuona huku chini….’akaambiwa.

‘Mgeni gani, mwambie kuwa sina muda kwa wakati huu…’akasema na kukata simu, alieleekza chombo chake hadi hapo mapokezi kumtafiti huyo mgeni…ooh, huyu ni kati ya watu asiotaka kuonana nao,…akachukua simu na kumpigia mmoja wa walinzi kuwa ahakikishe huyo jamaa anatoka humo hotelini, na amwambie kama ni kuonana naye wataonana kesho …na kabla hajamaliza kuongea mlango wa ofisini kwake ukagongwa.

‘Ni nani huyu kaja bila taarifa na ofisini kwake hapo anakuja mtu akiwa kafuatana na mlinzi wake anayemuamini…..akakumbuka yule mtu,aliyempotea kimiujiza kwenye kamre yake…harakaharaka akafungua kabati lake na kuchukua bastola.

Akaielekeza kamera yake hadi hapo mlangoni kumwangali huyo jamaa, …lakini hakuonekana mtu…, alikuwa na uhakika kuna mtu kagonga, inakuwaje asionekane mtu.Akawapigia walinzi wake kuwaulizia kuwa kuna mtu yoyote wamemruhusu kuja kwake, wakasema hakuna na wasingeliweza kufanya hivyo hata siku moja….kwani wanajua taratibu za kikazi. Aakona kuna kitu, akaegesha akmera yake iwe inachukua matukio yenyewe, na kufungua mlango, aliangaza huku na kule hakuona mtu. Akajua kuna ujanja unafanyika, akahakikisha kuwa kafunga mlango wake na ufunguo na kuelekea mapokezi.

Kabla hajafikia ngazi za kushuka chini akahisi kuna mtu anamfuatili kwa nyuma, akawa anatembea huku anasubiri muda muafaka wa kugeuka, na alipoifikia ngazi ya kwanza akageuka haraka na bastola ikiwa tayari mkononi.

‘Bado hujasahau mafunzo yako ya uaskari..?’ akakutana uso uso na yule mtu aliyemuona kwenye kamera yake na kwa ujuzi wake akamgundua kuwa ni nani licha ya kuwa kajibadili sura.

‘Siwezi kusahau hilo, kazi hiyo ilikuwa kwenye damu licha ya kunipotezea malengo….niambie kwanini uankiuka sheria,sizani kuwa aunafanya hilo ukiwa hujui sheria….’akasema mkuu wa hiyo hoteli.

‘Najua sana, lakini kwa kazi yetu hii bila kufanya hivyo huwezi kufikia malengo, nakuomba twende mahali tuongee, najua una majukumu makubwa sana, lakini hili ninalotaka kuongea na wewe ni kubwa zaidi ya hayo majukumu yako…’akasema yule mtu….

‘Kwakweli sina muda kabisa, …kama nikuongea tutaongea kesho…’akasema mkuu wa Uslama.
‘Ojong, hili ni pamoja na usalama wako, usalama wa ajira yako….’alikuwa kiondoka lakini aliposikia mambo ya ajira yake yake, akasimama na kugeuka kumwangalia yule mtu…
***********
Kilikuwa kikao cha dharura, kwenye chumba maalumu, baadaye mkuu wa ulinzi wa ile hoteli alikuwa kakaa na kuangaliana na Inspekta wa polisi, ambaye kwa alishavua sura bandia na kuwa kama kawaida, kwani mwanzoni usingelijua kuwa ni yeye, ila ni kwa kipaji cha huyu mkuu wa upelelezi ndicho kilichomgundua, hata kabla hajavua hiyo sura ya bandia…yeye alitulia kimiya na kumsikiliza kwa makini, akijua kuwa kuna jambo kubwa sana, la sivyo inspekta huyu asingelifanya jambo la hatari kama lile, kutokana na wadhifa wake.

Hata hivyo hakujali kuwa anongea na mtu mkubwa kama huyo, kwani alishakutana na watu kama hawo wengi, na moyo wake ulishajenga ujasiri, na katika maisha yake alishajiwekea kuwa hakuna jambo linaweza kutokea bila sababu na hata iweje, kama mungu kapanga iwe hivyo itakuwa hivyo, cha muhimu ni kujiamini …., akamsikiliza kwa makini huyo Inspketa, …anamjua sana mtu huyu kuwa ni mmoja wa watu mashuhuri sana katika kitengo cha upelelezi, na aliletwa toka nchi ya jirani kusaidia kazi hiyo na kutoa mafunzo.

Alimwangalia kwa makini jinsi anavyoshusha siasa za kutaka kumbadili mawazo, lakini alijifanya kama anasikiliza, lakini akili yake haikuwepo humo kabisa. Hakutaka kabisa kuongea lolote litakalomuingiza kwenye kesi za kipolisi, tangu aachane na kazi hiyo amekuwa akiwa mbali nayo kabisa, licha ya serikali kumtumia wayu ,mbalimbali kumshawishi arudi kazini,lakini msimamo wake ulikuwa ule ule, kuwa hataki tena kazi hiyo ya hatari kwa maisha yake na familia yake…. aliapa kabisa kuwa hatarudi tena kwenye kazi hiyo, kutokna na matatizo aliyopata ambayo yaliingizwa hadi kwenye hadi mwishowe aliambiwa achague moja,familia yake au kazi ….

Mwisho wa siku akawa hana jinsi akaamua kuacha kazi, na alipoacha kazi alijikuta katika wakati mgumu, kwani kiasi alichopata kama mafao kisingeliweza kumfikisha katika malengo aliyokuwa ametarajia, kusomesha watoto na hata kuwekeza. Ikabidi afikirie njia nyingine ya kuweza kumsaidia katika maisha, je afanye kazi gani ya kumuingizia kipato, na wakati anawaza hilo ndipo akakutana na rafiki yake mmoja, ambaye walijuana wakati yupo kazini, rafiki yake huyu alibambikiwa kesi ambayo kama asingelikua yeye kumsaidia angeliishia pabaya, lakini kwa juhudi zake akamasaidia na kumuwezesha kushinda hiyo kesi.

‘Nchi yetu imeharibika, kila siku mauaji,…sasa wameingia hadi kwenye anga zangu, licha ya uhdu kubwa niliyoifanya…’akalalamika Ojong.

‘Mambo hayo hayataisha mpaka nchi irudie kwenye utulivu, …mpaka sasa kuna vikundi mbalimbali visivyotii sheria, achilia mbali hawo wapiganaji wa msituni ambao wamapenyeza watu wao kila idara ili kuleta mambo yao haramu, hata ikibidi kuleta fujo au mgongano, ..sasa wao wanachotaka ni kuwa kila kitega uchumi kuwe na watu wao, ili waweze kujitajirisha, ili waweze kununua silaha…..ili waweze kuwa juu ya sheria…’akasema Inspekta.

‘Usemalo ni sawa, lakini ipo siku hali itatengamaa tu….sasa Inspekta niambie ulichonijia maana nipo kazini, na muda kwangu ni muhimu sana kama ilivyo kuwa kwako….ongea naskusikiliza….’akasema mkuu wa ulinzi.

‘Ojongo, kiutaratibu hata kama umeacha kazi serikalini , lakini sifa na wajibu bado unakuwa pale pale, wakati wowote ukihitajika huna budi kutii amri, vinginevyo ….’akatulia akijaribu kutafuta njia za kumuingia huyu jamaa.

‘Nimekuwa katika wakati mgumu katika utendaji wa kazi hii tangu nifike hapa, na baya zaidi nimekosa watu wa kunisaidia, …na hata yule unayemuona kuwa alistahili kukusaidia mwisho wa siku unamkuta ni mmoja wa watu unawaowatili mashaka…..Ikanibidi nijaribu kurafuta wastaafu,…mara nikakutana na jalada lako, nikashangaa, inakwuaje uslistaafu kabla ya muda wako,…. katika kufuatilia utendaji wako, nikagundua ndiwe mtu pekee ninayeweza kumhusiha katika kutimiza lengo langu la kukisambaratisha hiki kikundi haramu, lakini kisheria…kwani sheria sasa imeshaanza kusimama, ingawaje ni kwa shida, lakini tukiwa na ushahidi wa kutosha,…tutaweza kukishinda hiki kikundi, nakuomba unisaidie kwa hili…’akasema Inspekta.

‘Inspekta unanishangaza sana, mimi nimeshaacha kazi hii siku nyingi, na sitaki kabisa kuingia tena huko, au kujihusisha na mambo hayo tena, nikikuhadithia maisha niliyopitia, taabu niliyoipata nikiwa ndani ya uaskari hutaweza kuamini, niliweka maisha yangu rehani, nikaitetea nchi yangu kwa moyo mmoja, ….lakini nini nilikipata, …niliishia kudhalilika, familia yangu kutaabishwa kwa jambo wasilolijua, ….sitaki hata kukumbuka hilo…sitarudi tena huko hata kama ni kwa mtutu wa bunduki…hilo nakuambia,…’akasema Ojong, huku akinuka kutaka kumuacha Inspketa.

‘Sikilia Ojong, sijakuambia urudi kazini, najua hilo, hata mimi familia yangu imewekwa hatarini, ndio maana nikaamua kuirudisha nyumbani, lakini kuna wito, kuna dhamana niliyokabidhiwa na wananchi, dhamana ya kuwalinda wao na mali zao, mimi hilo siwezi kuwahini wananchi, katu siwezi kuwa msaliti,…ninachokuomba wewe ni kuwa msaidizi wangu nje ya pazia. Na huna jinsi, kwani hata ukikaa kimiya wao wameshakuanza, …hili lililotokea hapa ndio mwanzo wao, hilo nakuhakikishia kuwa tukio hilo sio bahati mbaya, huu ni mwanzo tu, …sasa kama mpiganaji hodari unatakiwa kuwawahi kabla hawajakumlaza….’akasema Inspekta na kumuacha Ojong mdomo wazi, kwani katika fikira zake alikuwa hajaligundua hilo.

Akakumbuka mkataba wake na mwenye hoteli, na kwa minajili hiyo moja ya sharti limevunjika, alikumbuka dhahiri walivyokubaliana, kuwa ikitokea mauaji au kesi mbaya ya kuhatarisha usalama, basi utakuwa ndio mwisho wa kuwa mbia,… sasa kumetokea mauaji, ina maana kazi ndio basi, hisa zake ndio basi…haiwezekani,….lazima kifanyike kitu kabla mwenye mali hajarudi, …mwenye mali yupo Ulaya, na sidhani kuwa anaua hilo, kama angelijua angelishatuma ujumbe…anamjua sana mwenye mali, huwa mkikubaliana jambo hageuki nyuma, hajui kuwa ni ndugu au rafiki, kama umevunja mkataba hakusamehi.

‘Ina maana kama anajua hilo ndio …hapana haiwezekani, ngoja nikumbuke ule mkataba vyema, akatafuta kwenye kabati na kuusoma ule mkataba, na kipengeel hicho kilikuwa wazi…wakati anausoma huoo mkataba ndio kumbukumbu za nyuma zikaanza kumrejea, insi gani alikutana na huyo mwekezaji, insi gani alivyomtoa kwenye jua nakumweka kivulini, na sasa inavyoonekana anatakiwa kurudi juani, haiwezekani, na kama haiwezekani afanyeje….oh, hapo ndipo akakumbuka jinsi gani alivyojiunga na mwenye hiyo hoteli kama mbia kivuli….kumbukumbu zikukutana na huyo jamaa tajiri zikamjia akilini..

***********
‘Mkuu , nilikuwa nakuhitaji sana, nilikuhitaji wakati ukiwa kazini, kama mtetezi wa haki, na sasa umeondoka huko kwenye uaskari…’ alikumbuka mazunguzmo yake na mwenye hoteli , siku walipokutana na kufungua ukurasa mpya wa maisha yake. Siku hiyo walikuwa akipata chakula cha mchana huku akili yake ikiwa haipo sawa, kwani alikuwa hana kazi, na likuwa kabuni miradi mingi, lakini yote ilikuwa haifanikiwi.

‘Kuondoka kwako ni pigo sana kwetu…lakini hata hivyo mimi bado sikuachii, bado nakuhitaji, kwani wewe ndiwe mtu pekee ninayemwaminii hasa katika maswala ya usalama, ….nakuomba sana, hata ikibidi nikupe sehemu ya hisa ili kuwa na wewe katika uwekezaji huu niliokwisha uanzisha wa hoteli,…’ akasema huyo jamaa huku akimuonyeshea kwa kidole, hoteli kubwa iliyokuwa katika hatua za mwisho za ujenzi kipindi hicho.

‘Ninachotaka ni kuwa wewe na mimi tuunge ubia, …mali ninayo, lakini mali bila usalama haisaidii kitu, hili nimeliona katika kuhangaika kwangu,…nchi yetu haina usalama kabisa, vita vya chini kwa chini, …makundi ya kiharamia kila mahali,…sasa nikaona ili nifanikiwe, lazima niwe na mtu anayejua usalama,…wazo langu ni mimi na wewe kuingia ubia ..’ akasema yule tajiri na kumuacha hoi yule askari aliyestahafu kabla ya siku zake, ataingiaje ubia na tajiri kama huyu, wakati hela hana….akasikiliza nini anachotaka kuambiwa.

‘Ubia unaweza ukawa wa pesa, lakini pia upo ubia wa ujuzi…ubia wa usalama, mimi nakutaka ujiungena mimi, tuwe pamoja, kwa wewe kutoa ujzui wako wa uslama, mimi nitatoa pesa na mengineyo….ila sitaki ujulikane kihivyo, kwani tutakuwa hatufanikiwi lengo nililokusudia, wewe utakuwa hujulikani kuwa una hisa kwenye hii hoteli, utaonekana kama mlinzi tu, …ninachotaka ni usalama wa hiki kitega uchumi, najua unawajua wahalifu karibu wote, sasa sipendi waingie humu ndani, …’akasema rafiki yake huyo, waliyejuana naye kipindi cha nyuma. Na maneno hayo yalikuwa kama ndoto kwa Ojong, akawa anashukuru kimoyomoyo na kusema kweli mungu hamtupi mja wake
‘Kwahiyo wewe lengo lako ni lipi, unataka kuniajiri au unataka ninunue hisa kwenye uwekezaji wa hoteli unayotaka uainzisha,….?’akauliza Ojong.

‘Mimi nataka uwe na hisa kwenye hoteli hiyo ninayotaka kuianziasha,… lakini wakati huo huo unafanya kazi kama mkuu wa ulinzi, najua sifa zako na kipaji chako, ukiwa humo kama mkuu wa usalama , hakuna mhalifu yoyote atakayeweza kuingia na kuleta mambo yasiyofaa kwenye mradi huo, …..wewe unaonaje?’ akasema rafiki yake huyo.

‘Kwangu sina shaka, ila sijui kiasi gani cha hisa, maana mafao niliyopata si chochoye kitu, kama unavyojua nimebambikiwa kesi nyingi za uwongo, ili tu nitoke bila chochote, na mimi kwa hasira niliamua kuchia kila kitu, ilimradi tu familia yangu iwe huru, bahati nzuri nikapata mwanasheria mmoja ndiye kanipigania , angalau nimepata kiasi kidogo na hicho kiasi kidogo kimemegwa kwenye kupambana na hizo kesi…kwahiyo sizani kama kitafaa lolote kama mwanahisa…’akasema Ojong.

‘Wewe mwenyewe ni hisa tosha, nitaliweka hilo kisheria usiwe na shaka, ninachotaka ni wewe tu kukubali, mengine niachie mimi, ila…naomba sana, usije ukanigeuka, …sitaki kabisa kesi yoyote itokee humo hotelini, kwahiyo kazi yako ni kuhakikisha kuwa unachunga kabisa, mtu yoyote mbya asiingie humo, nimenunua mitambo ya kisasa itakayosadia kuchunguz nyendo zozote za wateja, kwahiyo muda mwingi utakuwa ukitumia chombo hicho, ….mengine tutaongea baadaye, ila halahala, sitaki kesi …hasa za jinai na mauaji, kwenye hoteli yetu…ikitokea bwana tutaachana!

‘Usijali, mimi nawajua wahalifu wote wa nchi hii, na mtu yoyote akiingia humo hotelini nitakuwa nimeshamsoma kwa undani,…kipaji changu kikubwa ni kuwa nikimuona mtu kwa mara moja,nishamweka kichwani kuanzia sura miondoko, siwezi kumsahau tena….kwahiyo hilo halitanipa shida kabisa na ili kufanikiwa hili nitatafuta kumbukumbu zote za wahalifu toka huko kazini, huko nina watu wangu, watanipa habari zote muhimu, ….hilo lisikutie shaka…na sizani kama kutatokea kitu kama hicho, ….nimekubali na tupo pamoja…’wakakubalina na mkataba wa kisheria ukasainishwa, kwa masharti kuwa ikitokea kesi za jinai , mauaji, basi ndipo utakuwa mwisho wa Ojong kuwa mwanahisa na hisa zake zinaweza kuchukuliwa kama itagundulika kuwa amefanya uzembe.

NB Sehemu hii ni ngumu kidogo huenda ikawachanganya, kama tukijaliwa kutunga kitabu itakuwa katika muonekano unaostahili, hapa nimeandika harakaharaka tu lakini najua mtaelewa, ni moja ya sehemu muhimu sana katika tukio hili, tutakuja kuona baadaye.



Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Wakati mwingine nakuonea huruma sana, kwani unajitahidi sana kutujali sisi wapenzi wa visa vyako, na kwa ujumla unatupa burudisho adimu. Lakini watu hata asente hatuna, tunaprinti tunakwenda ku-enjoy, wewe tunakupa nini,...hakuna na nafikiri hata ajira yako imeguswa na hili,labda bosi wako anazania kuwa hufanyi kazi kwa ajili ya kuandika hivi visi, kumbe masikini inavyoonekana unaandika muda sio wa kazi au sio mkuu.
Pole sana, usione watu kimiya, wanasoma wengi, ila wengi ndio hawo hawataki kuandika chochote..
Hongera sana M3