Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, October 13, 2011
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-37
Rose alijkiuta yupo Polisi bila hata kujua kafikaje, maana kiwewe kilichomkuta kilimfanya ashikwe na bumbuwazi,, mwili ulikuwa kama umekufa ganzi, na hata polisi walipokuwa wakimkamata na kumtia pingu, hakujijua kabisa..hata pale alipotolewa nje na kuingizwa kwenye gari, alikuwa kama sio yeye, kila mara alikuwa kiona damu, akiona sura ya mfu…damu, mfu…akashindwa hata kufumba macho yalikuwa bado yamemtoka kwa woga.
Alifikishwa polisi, na kila alipokuwa kihojiwa hakuwa anajibu sawasawa, na polisi wakisema ataongea vyema kesho, kwasababu ni usiku, lazima alale mahabusu, na hakuna cha dhamana kwasababu kesi hiyo ni ya mauaji, kama kuna dhamana yoyote hayo ni maswala ya kesho, na akashikwa mkono hadi sehemu wanapolala mahabusu, …alitanabahi pale mlango wa hicho chumba cha mahabusu kikifungwa, na hapo ndipo akili ikaanza kufanya kazi na kuanza kujiuliza, imekuwaje…mbona kafungiwa pale mahabusu, lakini alishachelewa, mlango ulishafungwa na maaskari walishaondoka pale mlangoni…
‘Hawa watu vipi, mbona wananikamata na kunifungia hapa wakati sina kosa,,,’akaanza kulalamika na kuita kwa nguvu, huku akiangalia huku na kule, alichoona ni giza totoroo, na hata macho yalipoanza kuzoea lile giza, bado alikuwa hajaona chochote, na kwa muda ule alijua yupo peke yake, lakini baadaye akaanza kusikia mkoromo na watu waliolala, hapa akajua kuwa hayupo peke yake mle ndani....
Akiwa ndani ya chumba hicho cha mahabusu, alijikuta akitaabika, kwani chumba kilikuwa kidogo , kisicho na dirisha, joto, kali harufu mbaya, hakuna kitanda wala godoro,…akaanza kujuta kimoyomoyo, huku akijalaumu mwenyew ,kuwa kwanini amejiingiza katika mambo ya kujitakia, akawaza sana, na muda wote huo alkuwa hajajua nini la kufanya, na hata akijua kwa muda kama ule angelifanya nini, baadaye akatafuta sehemu ya kujibanza, ili angalau aaribu kutafuta usingizi, akichukulia ujasiri wa kazi yake, kwanikuna wakati anakuwa aktika mazingira magumu, ya kuhudumia wagonjwa na hata asipate muda wa kulala…..lakini mle ndani hapana kumzidi, joto, harufu mbaya, hewa ndogo…mbu…., lakini baadaye…
Baadaye akakumbuka, oooh, Sweetie, ….itakuwaje kwa Sweetie, kwasababu, alimuacha akiwa kalala, je akiamuka akamkuta hayupo itakuwaje,…. kutokana na zile dawa, anaweza akalala hadi subuhi, kama hatagutushwa na kitu chochote, lakini wakati mwingine,zinaweza zikaisha nguvu akaamuka mapema zaidi, na hilo ndilo lililomtia wasiwasi Rose, je akiamuka mapema zaidi na ajikute yupo apke yake itakuwaje,…hapo akinuka haraka na kutafuta jinsi ya kuongea na wale maaskari, angalau wampatie simu aongee na kule hotelini, lakini maaskari hawakuwepo hapo karibu, na hata pale alipoita kwa sauti hakuna askari aliyefika, ..mwishowe akaamua kujipumzisha, akiomba Sweetie alale mpaka asubuhi bila kugutuka….na baadaye akapata usingizi wa mang’amung’amu.
‘Rose, unaitwa huku….’akasikia sauti ikimuita,…na ile sauti ilisikiaka kama ndoto, lakini baadaye akazindukana na kujua kuwa kweli alikuwa akiitwa na AKSRI, aliinuka haraka haraka pale alipojilaza, …hakuitamani ile hali, kwani alijihi kuwa ni mchafu na alihitai maji ya kuoga haraka iwezekanavyo,…hali kama ile, licha ya kazizake ambazo mara nyingi anaweza akajikuta katika mzingira magumu, lakini sio kama hali ili aliyokutana nayo pale mahabusu,…hata sehemu ya kujisaidi ani shida, …kuamuka asubuhi akiwa mchafu namna ile… hajawahi kuwa hivyo kabla.
Alisogea pale mlangoni alitamanai mlango ufunguliwe haraka atoke mle…na yule askari akamfungulia na kuongozana naye hadi sehemu ya mapokezi, na hapo akakutana na mtu asiyemfahamu.
‘Mimi ni wakili wa kujitegemea, nimetumwa na Docta Adam, kuja kukuchukulia dhamana, kwahiyo utatoka muda mfupi ujao, nakuomba usiwe na wasi wasi…kila kitu kimeshawekwa safi…na kama utaulizwa lolote, ukatae kuongea mapaka mimi mwenyewe niwepo,….’akasema yule mtu.
‘Mbona sikujui wewe ni nani, na huyo Docta Adam, kajuaje kuwa nimekamatwa..wakati sikuwahi kumpigia simu?’ akauliza Rose.
‘Hilo sio muhimu kwa sasa, kinachotakiwa ni wewe kutoka hapa kwa afya yako, kama kuna mengine tutayaongea baadaye, sasa hivi namsubiria mkuu wa kituo ili apitishe hiyo dhamana….’akasema yule mtu, na kuondoka, akimuacha Rose akiwaza mengi kichwani, e huyu Adamu amejuaje haraka kiasi hiki, wakati hakuwahi kumpigia simu? Isije kuwa kamuua kwasababu wameshindana katika malipo, au huyo jamaa kajulikana anataka kutoa siri?
Baadaye dhamana ikakamilika, kwa masharti kuwa sionoke hapo mjini mpaka upelelezi ukamilike, na hiyo ikiwa na maana hawataweza kuondoka tena asubuhi hiyo kama walivt=yopanga, na ina maana wakatafute hoteli nyingine.
‘Kwahiyo mna maana nitakatafute hoteli nyingine maana huyo mwenye hoteli alishanipa notisi niondoke,…?’akauliza Rose.
‘Utabakkia humo humo, hatuna muda wa kukutafuta kwenye hoteli nyingine, …’akasema yule mkuu wa kituo na yule mtu aliyetumwa na Adam, akasema atalifuatilia hilo asiwe na wasi wasi. Baadaye wakaondoka kurudi kwenye ile hoteli, walipofika kulikuwa kimiya kwani wapangaji wengine walishaondoka kwa kuogopa usalama wao, na hawakutaka kukutana na polisi.
Rose alipofika hotelini, hata kabla hajaingia ndani akakutana na yule bosi wa walinzi na akaanza kuongea naye kabla hajua nini kinachoendela, …‘Unaona jinsi gani ulivyonifukuzia wateja, nilikuwambia kuwa hawo watu wakifika mhala kuna ishara ya balaa, na nilikuambia usitoke kabisa humo ndani nilipowaambia make, kwanini ulitoka,kuna kitu gani kinachoendelea na huyo jamaa …? Akauliza yule mkuu wa ulinzi.
‘Mimi nilitoka kwenda kuchukua vitu vyangu nilivyosahau, nilipofika ndio nikakutana na hilo tatizo , sina miadi na huyo mtu, kwasababau simjui kabisa…’akasema Rose.
‘Huyu mtu ameuliwa na wenzake, inaonekana walisigishana katika mambo yao, …kwa taarifa za watu wanaowajua, wanasema mchana wa jana walionekana wakibishana na jamaa mmoja, …jamaa huyo ni mbaya zaidi, na anaogopewa kuliko, …huyo jamaa anatafutwa na polisi, ….lakini kama nilivyosema hawa watu wana mtandao mkubwa, hata kama watakamatwa haitachukua muda utawakuta mitaani, mnaambiwa kuwa hakuna ushahidi…’akasema yule bosi wa ulinzi wa hiyo hoteli.
‘Kwahiyo amepgwaje hiyo risasi…?’ akauliza Rose.
‘Amepigwa hiyo risasi kutoka jengo la pili, huyo mpigaji atakuwa alikuwa juu kabisa ya jengo la pili, ambapo ni rahisi kuangalia kwa ndani ukiwa maeneo hayo, na hii limetupa fundisho kuwa tuweke karatasi za kuzui mtu kuona akiwa nje…’akasema yule mlinzi. Rose aliposikia hivyo, kuwa watu wanweza kuwaangalia wakiwa kwenye jengo la pili, akishiwa hamu ya kuishi tena kwenye hiyo hoteli, na kumbukumbu za jana zikaanza kumjia hata kabla hajaachana na huyo mlinzi.
Alikumbuka jinsi gani alivyoingia mle chumbani,…ilikuwa kama ndoto mbaya ya jinamizi,kwani hakutarajia kabisa kukuta kitu kama kile, alikumbuk ajisni gani alivyomuona yule jamaa akiw akwenye kocho, mwanzoni alijua kuwa huyo jamaa kajipumzisha tu, akasogea kutoka nyuma ya lile kochi na kueleka mbele yake. Wakati anatembea, alihis ubaridi ukitokea dirishani, akawa na wasi wasi ina maana madirisha ya humo hayajafungwa, kwani mara nyingi wakiwa ndani wanahakikisha madirisha yamefungwa, na hasa walipondoka hapo, yule mlinzi alihakikisha amefunga madirisha yote.
Lakini hata hivyo, alishangaa kuona chupa chupa zimezagaa sakafuni, na hili aliligundua hata kabla hajawasha taa, kwani alipokuwa akisogelea kiwashio cha taa ya ndani, alikumbuka kukanyaga chupa, na wakati anasogea mbele ya kocho aliziona zile chupa zikiwa zimezagaa sakafuni, na kwa muda huo mawazo yake yalikuwa kutka kuangalia durishani, kuona kwanini kuna upepo unaingai toka nje, na usiku aka ule kunaubaridi mwingi sana, kwani hata yeye mwenyewe alikwua kavaa soksi za mkononi, kujisaidia na baridi.
Wakati mawazo ya kuangalia dirishani yakiwa yamemtawala kichwani, na hapo hapo mawazo ya kwanini kuna chupachupa humo ndani yakiwa yanamsumbua, na kumweka katika hali ya kubishana kwa akili, atangulie kauangalia kipi, chini sakafuni, kukagua ni chupa za nini,au achungulie dirishani au amsemeshe yula jamaa alliyeegemea pale kwenye kochi, na cha ajabu muda wote huo akusikia suti ya yule mtu. Alisema akilini ndio zao hawa watu wanakuwa wanajiamini kupita kiasi, ina maana hakutaka hata kuangali ni nani aliyeingia, alishahis kuwa alyeingia si chochote cha kumdhuru.
Akawa ameshasogea na pale alipo angeliweza kumuona yule mtu moja kwa moja usoni, lakini kwa muda ule kichwa chake kilikuwa kimeangali dirishani kwa uapnde mmoja, na kwa upande mwingine alikwua akimwangalia yule mtu, na hapo ndipo akashikwa na mshituko, mshituko ambao ulimfanya apige yowe, yowe ambalo hakulitarajia….na kwa vile hakutaka kujulikana kuwa kaingia humo kukutana na huyo mtu, akapandisha mkono wake kuzuia hilo yowe lisisike nje, lakini hakuwahi yowe likatanda hewani na kujaa chumbani na kutoka nje…
Pale kwenye kochi alimuona yule jamaa akiwa kaegeemea, kwenye lile sofa, akiwa kaangalia nje kwa kupitia dirishani, inavyoonyesha alikuwa kaona kitu fulani, na akawa kama anashngaa, kwani macho yale yalionekana kama yanashangaa, lakini kilichomfanya Rose atoe hilo yowe, sio hayo macho, sio kwasababau ya huyo mtu, kwani walishakutana naye, na anamfahamu vyema, na wala sio kwasababau anamuogopa, hapanauwowga kwa huyo mtu ulishamuondoka, na alikuw atayari kukutana naye, ili asikie nini kinachoendelea katu yake na Adam.
Alipofikia uamuzi wa kuja kukutana na huyo mtu licha ya kuwa alishaambiwa kuwa asitoke mle chumbani, aliwaza sana, na alishaona kuwa bosi wake Adamu huenda anajihusisha na makundi yasiyofaa, sio kweli kuwa watu hawo wanatumika kuwalinda wafanyakai wake wanapokuwa nje ya kazi, kwanini afanya hivyo, …akajiuliza, na kwanini yule mtu aseme alipewa kazi ya ziada ambayo alishaimaliza na alikuwa akidai pesa zake, ni kazi gani hiyo…na maswali mengi yalijijienga kichwani kila alipowaza zaidi, na aliona jembo jema ni kukutana na huyo mtu, na kama nikumlia kiasi fulani atamlipa ilimradi ajue ni kitu gani bosi wake anajihusisha nacho.
Alipohakikisha kuwa Sweetie kalala, akatoka na kufunga mlango kwa nje, hakuw ana wasiwasi kuwa atachelewa kurudi, kwani hakutarajia kuwa mazungumz na huyo mtu ayanweza kuwa marefu, alijua kuwa huyo mtu anachohitaji ni pesa, basi atatumia mwanya wa pesa kupata maelzo zaidi, ingawaje alijiuliz kuwa kama je atadanganywa atahakikishaje kuwa anachoambiwa ni kweli, akasema hilo atalijua mbele kwa mbele, ..
Rose akaingia kwenye kibaraza ambacho hutenganisha vyumba vya upende mmoja na mwingine na mle alikutana na watu mbali mbali wakitoka na kuingia kwenye nyumba vyao.
Alikumbuka kuna muda alitaka kurudi , lakini hamasa za kukutana na huyo mtu zilimzonga zaidi na kujikuta akiingia mle ndani bila ya uwoga, kuwa huenda huyo jamaa akamfnya lolote baya alijiamini, na lile koti refu alilovaa na kofia vilimpa ujasiri fulani, kuwa huyo jamaa anaweza kuhis kuwa kaficha silaha kwenye lile koti.
Tundu lilionekana wazi kwenye kichwa cha yule mtu , na damu zilikuwa zimezunguka lile tundu , na kifuani kulikuwa na damu, kuonyesha kuwa huyo muuaji halkutaka kufanya makosa, risasi ya kichwani na kifuani kwenye moyo, havingeliweza kumfanya huyo jamaa abakiwe na uhai, ….hayo ndiyo yaliyomfanya Rose apige yowe, …yowe ambalo liliwashitua hata wapangaji waliokuwa nje, kwani hakufunga mlango wakati anaingia akihakikisha kuwa kama kuna mtu hataweza kumdhuru, kama mlango upo wazi.
Yowe la pilililikatishwa na maaskari walioingia wakiwa na silaha zao na kusema kwa sauti kuwa `upo chini ya ulinzi…’waliingia mara moja na kumzunguka Rose na wengine wakiwa wamelizunguka lile sofa pale alipolala yule mtu, na kwa dakiak chache chumba kilikuwa kimejaa maaskari, na kila mmoja alikuw akatika kazi yake, na alichosikia baadaye ni amri aikitolwa kuwa afungwe pingu na afikishwe kituo cha polisi.
‘Huyu keshakufa, na risasi inaonekana imetokea nje kwa kupitia hapa kwenye dirisha,…’alikumbuka sauti ya mmojawapo wa wale maaskari akisema.
‘Inawezekana ni huyu huyu mwanamke, kafanya haya mauaji na kaja humu kuhakikisha kuwa kazi imekamilika au la…humuoni kavaa soksi za mkono za nini, ili kuzuia alama za vidole..’aliisikia mmoja wa maaskari akiwaambi awenzake, na wengine wakawa wanambishia, hata ikatokea kubishana wenywe kwa kwenyewe, hadi alipoingilia mkuu wao na kuwaambia wafnye uchunguzi wa kina badala ya kukimbili dhana zisizo na ushahidi, na haraka Rose alitolewa nje, ili maaskariwafanye kazi yao.
***********
Sweetie alishituka toka kwenye usingizi mzito, akainua kichwa kuangalia, ….akawa anawaza yupo wapi, …akatizama huku na kule,…akamuona huyo jamaa kasimama pembeni ya kitanda, akisema maeno ambayokwa muda huo hakuelewa anaongea nini…mara yule mtu akamtikisa tena, na hapo akili akifunguka, …na kuanza kuelewa nini kinachoendelea , ilikuwa kama vime masikio yamezibwa, halafua yakafunguka kwa ghafla, kwahiyo unahisi upepo au siku ikija kwa wingi sana…akainuka pale kitandani haraka, akatizam huku na kule…akawaza, hivi nipo wapi…mbona hakuna maji, kumbukumbu za maji zikawa zimetawala ubongo wake, maji…maji…
‘Nani kaniokoa, …ooh, mungu wangu, nimeokoka, niliua nimekufa….ooh, nipo wapi..akaanza kuweweseka, hadi kumfanya yule jamaa aliyesimama karibu yake kushangaa. Lakini hakuwa na muda wa kupoteza kwani alikuwa kazini, akamshika mkono Sweetie na kuanza kumvuta kutoka mle ndani ya chumba, …Sweetie akawa anamfuata kama goigoi haelewi nini kinaendela, muda wote alikuwa akiangalia huku na kule, hakuwa na uhakika …mawazo yake yote anaua yupo kwenye maji, na pale akaja kuokolewa.
‘Oooh, nakushukuru sana kwa kuniokoa, uliniokoaje…?’ akamuuliza yule jamaa baada ya kumfikisha kwenye chumba kingine. Yule jamaa akasema, usiwe na wasiwasi, nitakulinda hadi hatua ya mwisho, mimi nawajua sana hawa watu, ila utulie hmu ndani kimiya, usitoke kabisa…’akaambiwa an yule jamaa ambaye lionekana kuwa na haraka ya kutoka mle ndani…
‘Mimi ni mkuu wa ulinzi hapa hotelini, kuna dharura imetokea ndio maana nikakuhamisha kwa haraka toka kile chumba cha mwanzo , haieleweki kuwa hawa watu wanajua wapi mlipo, lakini kwa tahadhahari inabidi tufanye hivyo, nikuhamishe kwenye chumba hiki, huku hawafiki watu ovyo…’akasema huyo jamaa, na kumfanya Sweetie abakie akijiuliza kwanini yote hayo, ina maana baada ya kuokolewa, kuna watu wanatka kumdhuru.
‘Lakini kwani mimi nimewafanyia nini, kwasababu niliua nimeshakufa, nilijitahidi sana kuogelea hatu p[umzi ikaniishia, na mwishowe nikapoteza fahamu, ….nikaomba dua ya mwisho nikijua kuwa sasa siku yangu imefika,..toka hapo sijui nini kimetokea, kwani hapa ni wapi na nimefikaje huku..?’ akauliza Sweetie.
‘Aaah, hayo mengine, sasa hivi tunazungumzia usalama wako humu ndani, wapo watu wanawatafuta nyie, imegundulika hivyo,….sijui kwanini, kwa taarifa yako, mwenzako keshakamatwa na polisi, kwasabaabu kwanza kafnya vibaya kwa kukiuka msharti yangu na pili , sijui kwanini alikwenda kwenye kile chumba…aua mnaushirika na hawo jamaa nini, nisije nikafuga nyoka…lakini sawa, wkanza lazima nitimize wajibu wangu, nitahakikisha upo salama, sawa…?’ akasema yule jamaa
‘Sawa mimi nakushukuru sana, kwa wema wako huo, huyo mwenzangu ndio nani…maana najiona nipo peke ynagu….?’ Akauliza Sweetie.
`Sio muda wa maswali hayo, hili nafanya kwa ajili ya usalama wenu., mwenzako sasa hivi kachukuliwa na polisi, sitaki na wewe yakukuta mabaya hadi itakapojulikana zaidi…wewe panda hapo kitandani lala, tulia kimiya hadi kesho asubuhi, utajua nini kinachoendelea, usikaidikama mwenzako, mimi sitakuwa na dhamana tena kwenu,..lakini lazima hela zangu zilipwe, kwasababu bi uzembe wenu wenyewe..’akasema yule jamaa akitizama kile chumba huku na kule kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa.
‘Mwenzangu ni nani huyo, na kwanini kachukuliwa na polisi…anaitwa nani huyo mwenzangu…?’ akauliza Sweetie akiangalaia huku na kule bado akiwa haamini kua anaota au yupo wapi, au ni mbinguni….alikuwa haamini, akawa anajaribu kutafakari, lakini likuwa kama bado kichwa kinanguruma.Akapikicha masikio kama vile mtu aliyeingiwa na maji anavyofanya kutoa maji masikioni.
‘Utakaa hapa hadi kesho, naua mwenzako ataachiliwa , na akia mtaondoka, sitaku kuwaona tena hapa, mumeshaniletea mambo nisiyo yataka, najua mwenzako ataruhusiwa kesho, nina uhakika huo kwasababau ushahidi upo wazi na kuna vyombo humu ndani vinaonyesha matukio yote yaliyotendekea humu ndani, wakihitaji nitawapa, lakini kwa usalama wa hoteli hii hatuwezi kuliweka hili wazi..na siwezi kuwapa, mapaka iwe ni lazima..’akasema yule mtu.
‘Bado hujanijibu swali langu huyo mwenangu ni nani na anaitwa nani , na kwanini akamatwe na polisi, sikumbuki kuogelea na mtu mwingine, nakumbuka nilikuw peke yangu..?’ akauliza Sweetie huku akiwaza na kuangalia nje kwa kupitia dirishani, lakini alikuwa haoni kitu , kuna pazia kubwa limefunika dirisha.
‘Siwezi kukujibu zaidi ya hapo, huyo jamaa yako unamjau wewe zaidi, na hata hivyo mimi mwenyewe nashindwa kujua, hizi ndvu ziliota lini zikawa ndefu kiasi hicho, nakumbuka ulipotoka hapa wakati unaumwa, hukuwa na hata ndevu moja, ….lakini nikikuangalaia kwa makini, ni wewe yule yule mliyetoka na mwenzako, …mkeo kama sikosei,…lakini ndio hivyo kakamatwa na polisi kwa sabababu kakutwa kwenye chumba palipotokea mauaji…’akasema yule mkuu
‘Eti nini, mauaji,nani kafa, ….mke wangu, alifikaje toka ….hadi huku, hapa ni Bukoba au Mwanza….haiwezekani, atakuwa alikuja na nani., mbona mnanichanganya , mke wangu kakamatwa halafu unaniambia nilale…..hapana, lazima nitoke nikajue hatima yake…’akasema Sweetie akitaka kutoka nje.
‘Sikiliza, wewe sasa upo kwenye mamlaka yangu, nisingependa kutokee tatizo jingine, hilo lililotokea ni kubwa zaidi na sijajua hatima yake ….nakuomba tafadhali tulia, hadi kesho aubuhi, utajua kila kitu, nakuomba usitoke kabisa humu ndani, kila kitu kipo humu, na kwa usalama wako inabidi nikufungie na ufungua nitaondoka nao….’akasema yule mkuu na kuondoka.
Sweetie akabakia akiwaza…,, mke wangu kakamatwa, kwa kosa gani, anasema kakutwa na maiti ndani, maiti ya nani, ….mbona sielewi, nakumbuka nilimwambia rafiki yangu amlinde mke wangu hadi nitakaporudi, sasa iweje, au ndio rafiki yangu kafa….hapana haiwezekani, …lazima nijue nini kinechoendelea..’ akauendea ule mlango kujaribu kuufungua, lakini ulikuwa umefungwa na ufunguo
‘Mbona huyu jamaa ananifanya kama mfungwa, ….haiwezekani, sitavumilia hili kamwe,….’akaanza kugonga mlango kwa fuo, lakini haikusaidia kitu, kulikuwa kimiya…na mara akaanza kujisikia vibaya, alipohis hivyo akakisogelea kitanda, lakini hakukifikia, …akayumba huku na kule, mara giza likatanda usoni, na hata kabla hajakigusa kitanda akadondoka chini,….
NB. Sehemu muhimu sana hii lakini nimeiandika kwa haraka, …hivyo hivyo nitafanyaje, nimepata upenyo huu mdogo, wa asubuhi, nikaona niandike kipande hiki muhimu, kabla wenyewe hawajafika, sijajua wataniambi anini leo. Dua zenu ni muhimu sana, kwakipindi huki kigumu…nawapenda sana. Na pia naomba kama kuna watu wanaopita humu na wapo kwenye sehemu wanachapa vitabu tuwasiliane,kabla mambo hayajawa mabaya...siunajua tena ukitupwa mitaani inavyokuwa...mungu yupo
Ni mimi: emu-three
3 comments :
Maskini Rose i hope itajulikana hana hatia na sweetie nafurahi kumbu2 zimerudi.....tunazidi kukuombea M3 Allah ni mwema na hamtupi mja wake.
Mmmmnh jamani mambo yanazidi kuwa mambo...! Pole m3 kwa kila k2 hope evrthng ztakuwa poa.. Usione kmya bt 2ko pamojaa..!
Nashukuruni sana kwa kunipa moyo na kuwa nami katika kipindi hiki kigumu, kweli nimeamini kuwa wazawa hatuna thamani , wanathaminiwa wageni na hawo wageni wanatunyanyasa kama nchi yao!
Post a Comment