Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 9, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-24




Rose akiwa kwenye kiyoo akijitizama huku anamtizama mgonjwa wake kwa kupitia kile kiyoo, alimwangalia hivyo kwa kujiiba, bila yule mgonjwa wake kujua kuwa anatizamwa yeye, …alimtizama huku akiwaza jukumu kubwa aliloamua kulibeba, jukumu ambalo sio tu litampotezea wakati wake, lakini pia linamhatarashia hata ajira yake, na huenda hata kile kidogo anachokipata huenda kikaishia katika makato ya matibabu ya huyu mgonjwa. Akajiuliza kwanini anafanya hivyo wakati mtu huyo sio ndugu yake na wala hamjui wapi anakotoka,…ina maana kweli ni moyo huruma unaomponza, …labda sio huruma tu, kuna kitu kingine kimemsukuma kufanya hivyo, ambacho yeye mwenyewe hajaweza kukigundua….au ni kweli kampenda kama anavyodai Docta Adam….hapana, sihitaji mwanaume tena wa kupenda nimeamua kusihi peke yangu…

‘Kweli wewe una huruma sana docta, umeamua kunichukua na kuniweka nyumbani kwako, na pia upo tayari kubeba gharama zote za matibabu yangu, ….lakini mimi nakuhakikishai kuwa , tatizo hili likiisha nitakurudushiai gharama zako zote…hata kama ni kwa kufanya kibarua,….’ Akasema yule mgonjwa na kukaa kimiya kidogo kama anawaza kitu halafu akaendelea kuongea kwa kusema `Lakini nina imani kuwa huenda nilikuwa na kazi fulani, …..huenda nilikuwa mtu fulani mwenye kazi….nashindwa kugundua hilo, ila ndoto ya jana imenifanya niwaze sana, ..’ akasema Yule mgonjwa ambaye walishampa jina la Sweetie.

‘Ndoto …!, Ndoto gani hiyo Sweetie, maana kila siku unapiga makelele ya ndoto, lakini nikikuuliza unasema hakuna kitu,…hebu nisimulie hiyo ndoto uliyoikumbuka ilikuwaje , maana unanitia hamasa kusikiliza, au hizo ndoto nyingine ulikuwa unazikumbuka,lakini ulikuwa hutaki kuniambi, ….tafadhali naomba unisimulie , ni ndoto mbaya ya kutisha au ni ndoto ya namna gani…? Akauliza Rose.

‘Kweli siku nyingine kama nilikuwa napiga kelele, sikuwa najua kuwa naota, huena nilikuwa naota lakini sikuweza kukumbuka, na ndoto hii ya jana, ni ya ajabu kidogo, ni ya kutisha lakini, sio ….sio ndoto inayomfanya mtu apige ukulele wa kugopa, …., ila nilivyoota inaonyesha kuwa mimi nilikuwa mtu fulani , nafanya kazi mahali fulani, na nina ….nahisi hivyo kuwa nina mke, na sijui kama nina watoto, kwani hawo watoto sikuwahi kuwaona kwenye hiyo ndoto…ila inavyoonyesha ni kuwa huyo mke wangu anaweza kuwa kanisaliti…ndani ya ndoto hiyo nilimuona akinikimbia, na hata nilivyojaribu kumuita asiniache nikiwa nimenasa kwenye dimbwi kubwa la matope, yeye hakunisikiliza kabisa na hata hakutaka hata kugeuka nyuma kuniangalia, akawa anakimbia tu kuifuta hiyo sauti ilikyokuwa ikimuita…!’ akasema Sweetie.

‘Anakukimbia au anakimbia hatari fulani..?’ akauliza Rose.

‘Kabla ya kunasa kwenye hilo dimbwi la matope, ilionyesha kuwa tulikuwa pamoja na huyo mke wangu tunatembea sehemu fulani, karibu na maji, mara nyuma yetu kukatokea mlio wa kutisha, mlio kama wa Simba, au mnyama wa kutisha, na kwa muda ule hatukujua kuwa ni mlio wa kitu gani, ila mioyo yetu ilijua kuwa ni mnyama wa kutisha ambaye angeliweza kuhatarisha maisha yetu, basi tukaanza kukimbia, na mwanzoni tulikuwa tukikimbia pamoja, kuhakikisha kuwa hakuna atakayeachwa nyuma na kuliwa na huyu mnyama….’ Akasema Sweetie, huku akiwa kama anawaza kitu kwa makini.
‘Halafu ikawaje…? Akauliza Rose.

‘Basi mara tukasikia kwa mbele yetu mtu akisema kimbieni sana, kuna hatari nyuma yenu…na huyo mtu akawa anamuita mke wangu zaidi, na ….nakumbuka alikuwa akimuita kwa jina hilo la Sweetie, akimsisitiza kuwa akimbie zaidi….cha ajabu tukafika sehemu hiyo yenye matope, na mke wangu akawa anaweza kuyakanyaga na kupita kwa urahisi, lakini mimi kila nikiyakanyaga nakuta nazama kwenda ndani, na siwezi kutoa miguu…’ Akasema Sweetie

‘Je huyu mtu aliyekuwa akimuita mke wako unamfahamu, au ilikuwa kama sauti tu, nay eye alikuwa haonekani...?’ akauliza Rose

‘Inavyoonyesha huyo mtu namfahamu, ila sijui ni nani, hata jina simkumbuki, lakini inaonyesha kuwa anaweza akawa ndugu au rafiki yangu, na inaonyesha kuwa alikuwa anatujua sote ….na hata hivyo hakuonekana kisura…’ Akasema Sweetie.

‘Haya ikawaje….? Akauliza Rose, akiwa na msisimuko wa hiyo ndoto na alikuwa akiulizia hivyo zaidi huenda katika kuelezea hivyo ikasaidia kumzindua huyu mgonjwa kimawazo, huenda ikavuta hisia za huyu mtu na huenda ikamfanya azindukane na huo ugonjwa wa kusahau uliompata. Ugonjwa huu wa kusahau ulionekana kumshika huyu mgonjwa na ilitarajiwa kuwa huenda baada ya vipimo na matibabu hali ingeanza kuwa shwari, lakini haikuw ahivyo, muda umepita hakuna madaliko.
Rose akakumbuka, siku ile alivyokuwa na shauku kuwa sasa mgonjwa huu atagundulika nini tatizo na atapata matibabu ambayo yangemsaidia na hatimaye kitendawili cha huyu ni nani kingetatuliwa, …. Siku ile baada ya vipimo vingi na uchunguzi wa vyombo vya kitaalmu walivyokuwa navyo, waligundua kuwa tatizo hilo limetokana na baridi kali ambayo ilimletea huyu mgonjwa naimonia, na kwenye kichwa , kuligundulika kuwa kuna sehemu iligongwa na kuleta jereha, lakini jeraha hilo lilishapona,…wanahisi kuwa kugongwa huko huenda kulisababisha hitilafu fulani kwenye ubongo na kuwa moja ya sababu ya matatizo kama hayo.

‘Huyu mtu anahitaji uangalizi wa karibu, na vipimo hivi pekee haviwezi kuonyesha zaidi, kama ingeliwezekana mtu huyu angelipelekwa India kwenye utaalamu na vyombo vya ubongo, lakini nina imani kama atatulia vyema, akawa haapati msukosuko mwingine, anaweza akarudia hali yake, lakini haa akirudia hali yake bado atakuwa katika katika hatari kuwa kama atapata msukosuko mwingine hali kama hiyo iakwa ikimrejearejea mara kwa mara, ni bora kama kama ingeliwezekana akapelekwa sehemu yenye vipimo na huduma za ziada na kufanyiwa upasuaji…’ alisema mtaalamu ambaye ndiye alicyekuwa kachukua vipimo vyaka na kutoa tathimini hiyo.

Baada ya tathimini hiyo, Maua na Docta Adam walikutana kwa mazungumzo nyeti, na moja ya mazungumzo yao ilikuwa ni maamuzi yanayohitajika kuhusiana na huyo mgonjwa, je atahudumiwaje, je gharama zake ambazo zimekuwa kubwa zitapatikanaje na je baada ya hapo huyo mgonjwa atakwenda wapi kwani hana ndugu, haijulikani wapi anatoka,…!

‘Bosi kuhusu gharama mimi nilishajitolea kuchangia, lakini sio kubeba gharama zote, kwani najua kuna ruzuku unapata toka serikalini, kwahiyo, sehemu hiyo ya kuchangia nimejitolea sehemu ya mshahara wangu na nikijua sio peke yangu mchangiaji….’ Akasema Rose.

‘No, no…Rose, usiruke majukumu yako, uliisoma vyema ile nyaraka ya mkataba aliokusainisha mhasibu, au wewe ulikimbilia kusaini tu bila ya kusoma kwa vile ulikuwa na kimuhemuhe cha huyo mgonjwa, Sweetie wako, au sio, sasa nakuomba uende ukausome vyema, ili ujue nini unawajiba nacho. Kwa ujumla huo mzigo ni wako, kwa gharama na mengineyo kama utahitaji…. Na gharama hizo zimegawanyika sehemu mbili, ….ndio kuna sehemu hiyo ambayo italipwa kutokana na ruzuku inayopewa kituo…na ankubali kuwa kituo chetu kinapata hiyo ruzuku, lakini kunahitajika mtu wa kuifuatilia, na hilo kutokana na ule mkatana itabidi wewe mwenyewe ukafuatilie, na sehemu ya pili inatokana na gharama za kuchangia watu wengine, pia kutokana na huyu mgonjwa na kutokana na mkataba ule hilo pia ni juu yako, kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya matibabu…tafadhali tunaomba gharama hizi ziwe zimerejeshwa..’ akasema Docta Adam, akiwa kakunja uso, kuonyesha kuwa anachoongea sio cha utani.

‘Sawa Bosi kama umeamua hivyo, mimi nitafanya nini, nipo tayari kwa lolote lile, ilimradi huyo mgonjwa asidhalilike…kama hamna zaidi naomba niondoke naye maana kama ulivyosema ni mtu wangu, na …atakuja kukaa na mimi hadi tutakapogundua ndugu zake, kwa ujumla kwa hivi sasa najaribu kufuatilia hilo , ili nijue wapi anatoka, na ndugu zake ni nani, na nahisi sio mtu wa hapa nchini…’ akasema Rose

‘Unaona ilivyo ngumu hiyo, sio mtu wa hapa nchini, je anatoka wapi, kama sio wa hapa nchini, je gharama hizo za ruzuku, kama ulivyoita zitapatikana kweli…? Na unasema umchukue ukakae naye atakaa wapi pale kwako kuna nafasi ya mtu kama huyo hapo kwako?, maana una chumba na varanda, yeye atalala wapi na wewe utalala wapi…unanishangaza sana Rose, huyo ni mgeni humjui , ….mbona unapenda kuweka maisha yako hatarini hivyo, ili uonyeshe nini, kuwa ni mwema sana, au kuna kitu gani kinaendelea kati yako na huyo mgonjwa, maana sikuelewe, elewi….’ Akasema Docta Adam akiwa na wasiwasi uliojaa wivu.

‘Bosi, hayo mengine hayakuhusu, hayo ni maisha yangu, sidhani kuwa mkataba wangu wa ajira unahusisha maisha yangu ya ndani, ….usijali bosi najua unanijali, lakini sio kihivyo…tafadhali naomba niondoke…’ akasema Rose.

‘Rose kumbuka kile ambacho kila siku najaribu kukuambia, kuwa mimi sijali tu ajira yako, najali pia maisha yako, najali maisha yako ya baadaye, nimekuomba sana, kuhusiona na swala la uchumba, naona huniamini, mimi sasa hivi tumeshatengana kabisa n mke wangu, nipo peke yangu na wewe ndiye niliyekuwa nimekutegemea, lakini naona huniamini, na inaonyesha kuwa huni….sijui niseme nini…’ akatoka pale kwenye kiti chake na kumsogelea Rose.

‘Bosi huko unakotaka kwenda ni mbali, …kwa ujumla kwa maswala hayo sikutaki, …wewe ni bosii wangu tu, hakuna zaidi na hayo maswala hayalazimishwi, mtu mnapendana mkiwa na hisia hizo, mimi hisia kwangu kwako haipo zaidi ya ubosi, zaidi ya mtu wa karibu yangu tunayejaliana, ….naomba iendelee kuwa hivyo basi….

‘Ok, time will tell, lakini nakuhakikishia kuwa Rose, mimi nakupenda na nipo tayari kukusaidia kwa lolote lile ili uwe mke wangu, na hata hili swala la huyu mgonjwa, kama utanikubali kuwa nawe, basi nitatafuta jinsi ya kumsaidia…lakini kwa makubaliano yaliyo dhahiri, vinginevyo utabeba mzigo wako mwenyewe..’ akasema Docta Adam.

‘Nimekueelwa bosi, ….’ Akasema na kuondoka huku akimuacha bosi wake mdomo wazi, hakuamini kuwa Rose, yule anayemjua ndiye huyu kabadilika kabisa kwasababu ya huyo mgonjwa asiyejulikana, ina maana kweli anafanya vile kwasababu ya huruma, au kuna kitu kingine, hapana haiwezekani kuwa Rose kashikwa na mapenzi na huyu mtu, haiwezekani, kama ni hivyo, lazima afanye jambo la kukatisha kabisa hayo mahusiano, je afanye nini, ili kuhakikisha kuwa Rose hana mahusiano ya karibu na huyo mgonjwa…ni lazima itafutwe njia, kwa vyovyote iwavyo….akaahidi Docta Adam kimoyomoyo.

Rose akamwangalia yule mgonjwa wake ambaye amekuwa ndani ya nyumba yake na sasa zaidi ya miez sita, na kila akifika hospitalini anakumbana na barua ya madai, ….na jana tu kapata barua ya onyo kali kuwa kama asipolipia deni lake sheria itachukua mkondo wake….na kesho anahitajika kwenye kikao maalumu cha maamuzi , kikao kitakachowashirikisha wadau wa hiyo hospitali, na mara nyingi hawo wadau wakiwepo, kunakuwa na kuwabibishwa kwa watu, hata kufukuzwa kazi….je watamfanya nini Rose? ….


NB, Nimeona angalau niandike sehemu hii ndogo kwa shida, lakini kwa ujumla nipo kwenye wakati mgumu, ...ok, nitajitahidi hivyo hivyo.
Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Nahisi huyo "SWEETIE" ni Mhuja jamani mbona mkasa huu ni uhondo mtupu! Natamani uwe unapost kila siku!

Precious said...

Kwa kweli ni moyo wako wa kujitolea kama anavyojitolea Dk. Rose kwa mgonjwa asiyemjua tunajua uko katika wakati mgumu sana lakini tuna imani ipo siku hali itabadilika. Nawatakia w/end njema wadau wote wa blog hii na pia M3 na nakuombea Mungu azidi kukuzidishia pale unapotoa.

emuthree said...

Nawashukuruni wapendwa kwa kunipa moyo kwa kipindi hiki kigumu. Natamani ingekua ni ajira ili niondokane na vikwazo hivi

Yasinta Ngonyani said...

Pole kwa kuwa na wakati mgumu, hata hivyo twashukuru kuwa umetuletea sehemu hii. Hakika "mapenzi yana nguvu kuliko" mauti

Anonymous said...

M3 unajua mungu wetu ni mwaminifu siku zote hatuachi pekee yetu?? hicho kipindi kigumu ni cha mpito tu ndugu yangu soon kitaisha. Nami nakubaliana na mchangiaji wa mwanzo kuwa huyo sweetie ni Mhuja. all the best my dear