Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 19, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-17



Kilikuwa kikao katika hospitali moja ya serikali, docta mkuu alikuwa akikemea tabia ya manesi wake kutowajali wagonjwa hasa wale waliozidiwa na hawawezi hata kutembea, aliwaasa kuhusu wajibu wao, kuwa hospitali kama hospitali haihitaji mtu mwenye mgonjwa ndiye aje akae humo hospitalini ili amuhudumia mgonjwa wake, hilo ni jukumu lao, na sheria hairuhusu mtu ambaye sio mgonjwa kulala hospitalini… hiyo ni kazi yao manesi. Alipomaliza kuzungumza hayo akatoa onyo kali, kuwa kwa yoyote atakayerudia uzembe huo hatasita kumchukulia hatua kali. Wakaambiwa watawanyike kwenda kuwajibika…

‘Huyu bosi anaongea tu, anafikiri ni kazi rahisi hii, wagonjwa wengine, kila kitu unatakiwa ukifanye wewe, hawawezi kuinuka kitandani kwake, hawawezi hata kwenda kujisaidia, uwaogoshe, …inachosha jamani, angalia nini unapata mwisho wa mwezi,….’ akawa analalamika nesi mmoja akiwa anaongea na mwenzake.
Wakati wanaongea mazungumzo yao, hawakujua kuwa Rose alikuwa nyuma yao, akiogopa kuwakatiza, kwani alikuja kwa maswala ya kiofisi, na alihitaji kuonana na mtendaji mmojawapo, lakini hakumkukuta ofisini kwao, akaona apitie hapo wodini kwa hawo manesi kuwaulizia,…na alipofika kwenye ile wodi akakumbuka siku kadhaa nyuma alipofika hapo kumfuatilia yule jamaa ambaye anamtambua kama Sweetie, …kumbukumbu hizo hakuzitaka zimjie kichwani, kwani zinamtia uchungu. Alikumbuka siku ile alipofika hapo kumuulizia akijua kabisa atamkuta hapo na kukutana na hawo manesi wakiwa wanawajibika;

‘Nesi tafadhali nimekuja kumuulizia mgonjwa mmoja aliyelazwa hapa, mgonjwa huyo aliletwa toka kwenye kituo cha jeshi, na alikuwa kazidiwa sana…’ akaongea Rose
‘Kwahiyo unamtaka, au unamuulizia ili iweje, …samhani nipo busy, naomba uwe specific, umekuja kumuona au kuna lolote la zaidi…maana huu sio muda wa kuona wagonjwa hata kama wewe ni docta, lakini sio docta wa hospitali hii…’ akauliza yule nesi akiwa kavaa mifuko ya plastic mkononi na akionyesha kuchoka na kazi zliyokuwa akiifanya, au kukerwa, labda kutokana na kazi ngumu aliyokuwa akifanya.

‘Nimekuja kumuona, …maana..’ akasema Rose
‘Ameshakufa…’ akasema yule Nesi na kuendelea na shughuli zake.
‘Eti nini amekufa…hapana…ooh…haiwezakani…’ Rose akajikuta mwili ukinyong’onyea na karibu adondoke, lakini alijikaza kama docta, na kila alipojaribu kumsogela yule nesi ili apate maelezo ya kina, yule nesi akawa kama anamkwepa na hakumpa nafasi ya kumsogelea, baadaye yule nesi akakerekwa kwa kuona kama anasimamiwa akaanza kutoa maneno machafu.
‘Hivi wewe ningelikuja ofisini kwako na kukusimamia kama hivi ungelifurahi, unaona jinsi gani nilivyobanwa na kazi hapa wewe upo nyuma yangu kama mkia, au ndio umeshapata ajira hapa kuja kutusimamia, wewe siulikimbia kufanya kazi hapa ukaenda huko kwenye pesa nyingi, sasa kinakuleta nini hapa …nakuomba kama huna la kufanya nenda kakae kwenye viti vya wageni…’ akasema yule nesi huku kashika kiuona.

‘Tafadahli nesi , nilikuwa namuulizia huyo mgonjwa, ili nipate maelezo ya kina, ilikuwaje…’ akasema Rose kwa uchungu.

‘Wewe si docta, …mgonjwa anapokufa taarifa unazipata wapi, kwa nesi, au unazipta kwa docta, …nenda muchwari ukaulize, au kama unataka kumtambua nenda huko huko muchwari…nakuomba uishie, uniache niwajibike…’ akasema yule nesi na kumpita Rose kwa fujo kiasi kwamba lile beseni lililojaa uchafu karibu limwagikie Rose, na hapo Rose akaona haina maana ya kulazimisha mambo akatoka akiwa analengwa-lengwa na machozi, huku akiwa haamini kuwa yule mgonjwa kweli keshakufa.

Alijaribu kumtafuta mtu mwingine atakayemuulizia,au anayemfahamu pale hospitalini ampe taarifa kamili lakini wote aliokutana nao walisema hawajui lolote kuhusiana na huyo mgonjwa na hawana taarifa ya huyo mgonjwa, na mwishowe akakata tamaa akijua kuwa kama keshakufa, keshakufa na akimua kuulizia ngazi za juu litakuwa jambo jingine, na alitakiwa aje kiofisi zaidi, na hata hivyo alitakiwa kufuatilia mambo aliyotumwa, na muda ulikuwa umeenda sana, akajiona hana la kufanya kuhusiana na huyo mgonjwa…hata akija safari nyingine, atafanya nini labda aidai maiti kuwa ni ya kwake kwa ajili ya kuizika, na ataidai kwa mipango gani, kwa ushahidi gani kuwa ni ya kwake yeye sio ndugu yake. Akarudi ofisini na kumpa taarifa hiyo docta Adam.

‘Basi kama keshakufa, hatuna la kufanya, tulijitahidi kadri ya uwezo wetu, na mwisho wa siku akatutoroka, na sijui kama tuna la kufanya zaidi ya hapo, sisi hatuna udugu naye, sisi hatujajidhamnini kwake kama kuwa ni jamaa yetu, kwahiyo halimashauri ya jiji itamzika tu, kama hapatatokea mtu wa kumdai kuwa ni jamaa yake…’ akasema Docta Adam.

Rose hakusema kitu ikawa kila mara kumbukumbu za huyo mtu zikawa zikimrejea akilini mara kwa mara , kiasi kwamba hata kazi haikufanyika vyema, na alibaki kujiuliza kwanini imekuwa hivyo, kwani muda mrefu umepita, hayupo naye karibu, lakini kila akimuwaza anakuwa kama yupo karibu naye. Na kila muda ulipopita pale kazini akawa akili haitulii, hadi kichwa kikaanza kumuuma, baadaye aliamua kwenda kwa bosi wake kumuomba ruhusa ya kuwa hajisikii vyema , na kabla hajaondoka, docta Adam akamsimamisha kwanza, kuwa arudi ofisini kwanii alikuwa na mazunguzmo naye.

‘Unakumbuka siku moja niliwahi kukupa barua , ilikuwa ni ufuatiliaji wako wa masomo, na kwasababu ya pilikapilka za hapa na pale, tukawa tumeshindwa kulifuatilia zaidi swala hilo, sasa juzi nilipita huko wanaposhughulikia hili swala na kujaribu kuulizia limefikia wapi , wanadai nafasi ni chache, na zinatolewa kwa watu wachache wachache kwa kufuata kipaumbele hasa kwa wafanyakazzi wa serikalini, lakini nikalipigia chapuo la nguvu, nikijua namfuatilia mtu ninayempenda, hutaamini, jina lako limewekwa kwenye orodha ya watakaoenda kusoma nje…, kwahiyo ujiweke tayari kwa hilo, weka stakabadhi zako zote za kuasafiria tayari tayari, …’ akasema Docta Adam, akitabasamu kwa furaha, yeye akijua kuwa atapata busu la asente, lakini ikawa kinyume chake.

‘Docta mimi hapa sijisikii vyema kabisa, kichwa kinauma, akili haijatulia, na nimechoka, nahitaji kupumzika, hata hilo unaloongea, linaingia huku na kutokea huku , ngoja nikapumzike kidogo nyumbani, na kwa vile nilikesha, nahisi ndio sababu, nahitaji masaa mawili ya kulala, …sitaweza kuendelea leo kwa saa za ziada, naomba ruhusa niondoke…’ akasema Rose.

‘Sawa hilo halina taabu, kwasababu mwenyewe nipo nitawajibika sehemu yako ikibidi, lakini mbona hujaifurahia hii taarifa niliyokupa, kuwa umekuwa mmoja wa waliochaguliwa kwenda nje kusoma…’ Akasema docta Adam huku anainuka akiwa na kusudi la kumsogelea Rose, lakini aliposegea kidogo akasita na kutaka kurudi kukaa, akasimama akitafakari amsogelee au ….hapana sio vyema, akasimama vile vile. Alikuwa kajitahidi sana kumweka Rose karibu yake, amkubali kuwa mwenza wake katika maisha na alimuhitaji sana kipindi kama hiki kuliko wakati mwingine wote, hasa akiwa anapambana na mtalaka wake ambaye kagoma kabisa kupewa hiyo talaka, na ikiwa ni lazima itolewa itolewe kwaa masharti magumu ambayo Docta Adamu hakukubaliana nayo kabisa.

Kutokana na mzozo huo hilo swala likafikishwa mahakamani, ukawa mzozo wa mawakili wawili, …ambao mwisho wa siku waliwashauri wateja wao swala hilo lirejeshwe nyumbani, na kweli hakimu akakubali na likarudishwa nyumbani ili wakubaliane wenyewe,…hata walipofika nyumbani ikawa ni kuzozana tu, na mwisho wa siku wakaliacha kama lilivyo, lakini hata hivyo Docta Adam alishaamua talaka itoke kwa vyovyote vile , hataweza kukaa na mke ambaye hatosheki, msaliti…na akampa majina mengi mabaya. Ikawa wakiishi nyumba moja, lakini kila mmoja na chumba chake, hakuna kuwasiliana, kila mmoja na hamsini zake. Mke hataki katakata kuondoka kagoma kabisa, akidai kama ni kuondoka mali yote aliyo nayo docta Adamu igawanywe sawa kwa sawa…

‘Taarifa hiyo nimesikia mara nyingi, miaka inakwenda lakini hakuna cha safari wala kwenda kusoma, mimi nimefikia uamuzi kuwa nitatafuta njia yangu mwenyewe, kama nikusoma nitasoma tu, lakini siwezi kuweka mia kwa mia kuhusu hizo nafasi za kupendeleana na naona wewe sasa unaigeuza kama ndoana kwangu…kama ipo siku ikifika nitakwenda, lakini sio swala la kutumainia sana, …kwaheri kazi njema bosi…’ akainuka kwenye kiti na kuanza kuondoka na kumuacha bosi wake akiwa kasimama akisubiri busu la kwaheri.

Rose alipofika nyumbani alijaribu kupata usingizi , lakini haukupatikana na hata alipopata usingizi kidogo akawa anamuota Sweetie akimlalamikia kuwa kwanini kaamua kumuacha …na hapo akazindukana na hakuweza kabisa kulala, akiwaza haya maneno `kwanini kaamua kumuacha…’ akajuta sana kuwa mbona hakutilia maanani kumfuatilia, hadi imefikia kufa kwake.

‘Lakini mimi sikuwa na nia ya kumuacha , hilo limekwenda nje ya uwezo wangu, ningefanyaje, eti jirani yangu nishauri kwa hili maana linanitesa moyo wangu sana…’ Rose akawa anaongea na irani yake ambaye wanafanya kazi pamoja, na leo imetokea bahati wote wapo mapumziko, na baada ya kukosa usingizi, alitoka na kumuendea jirani yake huyo waongee kidogo.

‘Docta Rose, najua jinsi gani unavyojisikia kuhusu huyu mgonjwa, najua ulivyokuwa ukimjali, lakini kulikuwa hakuna jinsi, hilo hakuna wa kukulaumu, na usijitese bure moyo wako kuwaza, na nikuulize wewe kwa hili kama hiyo, na ndio imeshatokea, utafanyaje, unataka ukaitafute maiti yake uiombe msamaha, …hakuna jinsi kama ni kumuomba mungu muombe alilaze mahala pema peponi na kama unataka zaidi sioni , maana watu kama hawo wasio na ndugu wanazikwa na halimashauri ya jiji na huwezi kujua wanafanya hivyo lini, na huenda tayari wameshamzika…jaribu kusahau hilo na angalia mambo mengine yaliyopo mbele yako…’ akamshauri rafiki yake.

‘Na kweli mambo yaliyopo mbele yangu yapo mengi, na mojawapo nii kusoma, na nilitaraji sana kwenda kusoma nje, lakini naona bosi wetu ni mbabaishaji,...kila ukikutana naye anakupa matumaini tu, na nimehisi anatumia hilo kama chambo...nimemsshitukia....’ Akasita kumwambia kuwa bosi wake anamtaka.

‘Hivi nilisikia bosi ana mgogoro na mke wake wameishia vipi, maana yule mwanamke hana hata aibu, namjua vilivyo, na hata bosi aliposema anamuoa, nilimuonea huruma sana, niliwahi kumwambia akanidharau, akifikiria nataka kumharibia ili anichukue mimi,…sasa ameliona, …na kwanini wewe usimkubali tu kuwa naye, kwasababu uliyempenda kaingia mtini, sasa ni chaguo la pili , muache achukue nafasi hiyo, kwanza anazo , pili mnajuana vyema, usijali mvuto, usijali kuwa unampenda au la, mkioana mtajuana huko kwa huko, kiuweli sio wote wanao-oana, waliwahi kupendana , kama tunavyojenaga hisia, kama tusomavyo vitabu au kuangalia sinema, watu wanaoana, kwa kukubaliana mwisho wa siku mapenzi yanakua yenyewe…’ akasema rafiki yake Rose.

‘Sawa nimekupata, lakini sijawahi kuwazia hilo, na mgogoro wa bosi anaujua yeye mwenyewe na mke wake, mimi sipendi kabisa kuingilia mambo yasiyonihusu, hata kila anaponiomba ushauri huwa namwambia hivyohivyo, na nimemuonya asije akamuacha mkewewe kwa kisingizio kuwa ananitaka mimi, simuhitaji kamwe…hilo nilishamwambia lakini namuona hakati tamaa, hata hivyo huo ni mtazamo wako kuwa kupendwa kunakuja tu baada ya kuoana, mimi sio mtizamo wangu, licha ya kuwa nilyempenda alinisaliti, lakini bado naamini ni bora kuolewa kwa yule uliyempenda na `offcourse’ naye akupende...' akasema Rose

‘Wewe sikuwezi una msimamo wako ambao siuwezi, ila ninachoweza kukuambia kwa sasa ni kuwa usichezee bahati, mimi hapa kama akinitamkia tu kuwa ananitaka kunioa, nitampa jibu la moja kwa moja kuwa nipo tayari, na naweza kuachana na huyu mchumba wangu wa sasa, kwasababu namuona mbabaishaji tu….

‘Sawa, nimekupata,..’ na hayo mazunguzmo yaliishia hapo na kweli siku zikawa zimeenda na siku moja akawa katumwa na bosi wake kwenda kufuatilia madawa na alipofika pale kwenye hiyo hospitali ya serikali akamkuta yule nesi aliyemshobokea siku ile, akiwa anazungumza na mwenzake, kutoka na uzoefu wa siku ile hakutaka kuwakatisha mazunguzmo yao, akawa kasimama nyuma yao na kusubiri wakiwa tayari awaulize alichokuwa ametaka kuuliza, akawa kimiya anasubiri huku akiwa kazingirwa na mawazo yake likiwemo swala la kwenda kusoma nje.

Wale manesi walikuwa wakiongea na hawakuwa na mawazo ya kungalia nyuma na kwa muda ule walikuwa wakizungumza kuhusiana na mkutano na bosi wao, akamsikia mmoja akiongea hivi;

'Bosi wetu bwana kila siku mikutano, mikutano.....'akaongea mmojawapo

‘Hayo ya bosi na mikutano yake,tumeyazoea yanaingia sikio hili yanatokea sikio hili, wewe timiza wajibu wako pale unapoweza, ukichoka, unajua la kufanya, kama anataka siku moja aje tuwajibike pamoja, ashike mavi ya wagonjwa, awanawishe, awaogeshe …lakini mpendwa mbona bado nawaza, sijui kwanini nimewaza hili ingawaje muda umepita mrefu sana…kuhusu yule mgonjwa aliyeletwa siku nyingi hapa, na sasa ni kama mfu, mtu hainuki, mtu kalala tu, na zipo siku kidogo alijaribu kuinuka, lakini sijui anapatwa na nini…sasa anakuwa kalala tu, …..’ akasema yule nesi

‘Aaah, acahane naye mara ya kwanza nimipenda nikatamani apone haraka, maana yumo kweli, anamvuto, lakini siku zilivyokwenda nikaona ni mzigo tu…’akasema yule nesi mwingine.
‘Lakini kwanini kipindi kile ulimdanganya yule Docta aliyekuulizia kuhusu yule mgonjwa ukamdanganyaa kuwa keshafariki na wakati…’ akaulizia yule nesi mwingine.

‘Nilisema kwasababu maalumu, nilijua baada ya hapo angeliulizia yupo wapi, na wakati ule hakuwepo, alizundukana akatoroka, na sijui aliwezaje kutembea, maana muda mwingi alikuwa hawezi kutembea, tukamtafuta wee bila kumpata, tukajua keshawehuka na kuishia, mara siku kadhaa akarejeshwa akiwa hoi tena kama mwanzo, ndio tukamlaza, kimbembe kikanigeukia mimi tena, kumuogesha, …taabu kweli kweli nilitamani ajifilie mbali,…sasa majuzi kapotea tena, na sasa hivi ninaomba apotee kiujumla na niliongea na mlizi mmoja, kama atamuona anazagaa watafute njia za…..’ akaonyeshea kidole kupitia kooni kuwa wamuulie mbali…

‘Wewe unatakata kusema nini, ina maana umemchukia kiasi hicho…hapana kama nikufa aachwe afe mwenyewe, lakini kwanini anatoroka, ..?’ akauliza mwenzake.

‘Nahisi ni kutokana na huko alipokuwepo jeshini, nasikia huko vipigo ni kama kuua nyoka, na huyo jamaa walimweka kwenye kundi la watu wabaya, kwahiyo alikuwa akipata mkong’oto kwa kwenda mbele, kwahiyo kila akilala anaota hayo mapigo, ndio maana akizindukana anaogopa akizania kuwa yupo huko kwa hawo watesaji, na hata hivyo mtu mwenyewe yupo kama zezeta fulani….’ Akasema yule nesi akiwa anahangaika kupangapanaga vitu,…

‘Kwahiyo huna uhakika yupo wapi…?’ akauliza mwenzake
‘Kesahakufa bwana,unataka nikuambieje …huyo sahau, …yule mlinzi atakuwa keshawakamatisha vijana wa mitaani, na nijuavyo wale vijana ukiwapa kitu kidogo wanamaliza kazi, …huyo hayupo duniani tena, kasha…..’ mara yule nesi akahisi kitu na kugeuka nyuma kuangalia na mara akashikwa na mshituko na kulidondosha lile sinia la vyombo alilokuwa kalibeba, akabakia akigugumia akishindwa aseme nini, huku akiangaliana na Rose uso kwa uso….

NB: Nilishakata tamaa kuwa sitaweza kuandika chochote leo, lakini mungu bariki nimeandika chochote...wikiendi njema

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Iryn said...

Duuuuuuh hapo sasa face 2 face,yan i can't imagne hata itakuwaje jaman... Keep t up n'uve got T m3.. Upo juuu