Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 24, 2011

Dawa ya moto ni moto-25



 Ule mkanda wa CD, ukawa unaanza kuonyesha manthari ya jengo, kwa nje, mara kukaonekana magari mawili yakiingia kwenye geti, yakasimama na jamaa mmoja akatoka kwenye gari lake, na sura yake ikavutwa kuwa kubwa kuonyesha sura yake…ooh, ndio Bosi mwenyewe huyu, alikuwa `handsome’ au mlimbwende, akasogea kwenye gari jingine ambalo lina rangi nyekundu. ‘Kweli hili ndio gari la mke wangu, ushahidi tosha , kila mtu akiuona huu mkanda atalifahamu kuwa ni gari la mke wangu, yes, na namba zake ndio hizo..’ akasema Maneno.
Kilichofuata hapo alionekana  Bosi akifungua mlango wa gari jekundu na akatokea mwanadada akiwa na kivazi chake cha usiku,…. hapo Maneno akasonya kwa hasira na kusema `eti huyu ni mke wa mtu anajidhalilisha namna hiyo…’ akaendelea kungalia huku akiwa kalaza kichwa chake kwenye kochi.
Mkanda ukaendelea kuonyesha, wawili hawo wakiongea na hata kufikia kukumbatiana,…sauti ilikuwa ikisikika kwa mbali na sio rahisi kujua wanaongea nini…unachoona ni midomo kuchezacheza. Wakati bosi anataka kumbusu Maua, sura zao zilikuzwa ili kuliona hilo tendo vyema…hapo Maua akawa akageuza uso pembeni na Bosi akambusu shavuni, huku wanaongea, na walikaa pale nje kwa muda halafu wakaelekea kwenye mlango wa nyumba ambayo nayo ilikuzwa ili kuiona vyema. Walipofika pale mlangoni wakakumbatiana tena na tukio halikuwa tofauti na lile la kwanza, na hapa Maneno akawa anajiuliza kichwani kwanini Maua kama kweli ni mpenzi wa huyo jamaa na wapo sehemu ya siri, kwanini anajivunga kubusiana na mwenzake.
`Huyu anajifanya tu, eti anaona aibu…mnafiki mkubwa huyu…’ akasema Maneno akiisogelea ile `laptop’ yake, na hapo ule mkanda ukawa unaonyesha mazingira ya ndani ya nyumba. Ulionyesha chumba cha maongezi, halafu ukaelekea mlangoni, na kumuona Bosi akiingia mlangoni huku kashika funguo za gari, alionekana kuwa na wasiwasi, na Maua alikuwa kasimama karibu na mlango akiwa kashika kitaulo kidogo, akifuta mikono yake na hicho litaulo, na akawa anamwangalia Bosi na akauliza kwa sauti ya wasiwasi.
‘Una uhakika hujaona mtu, mimi nimesikia kabisa mtu anagonga dirishani…isije ikawa ndio hawo jamaa wenyewe…’ akasema Maua, akiwa kasimama, alikuwa katokea kunawa mikono, kwani alionekana kujifuta maji usoni na kwenye mikono!
‘Hakuna mtu, una uhakika ulisikia sauti kama hiyo, mimi nimeangalia sehemu zote sikuona kitu, nilichofanya nikuyasogeza magarii kwenye banda la magari, maana kuyaacha pale pale  kiusalama sio vyema, uzingatia mlinzi hayupo. Na wewe ulisahau ufungua wa gari kwenye gari…unaonyesha jinsi gani usivyojali,…’ akasema Bosi na kumfanya Maua ashike mdomo kwa aibu na kusema
‘Mungu wangu, mbona hili balaa…sina kawaida hiyo, kusahau ufunguo kwenye gari…duuh, naona sasa hili tatizo limeniharibu kichwa changu, nauomba huo ufunguo, maana nisije nikapitiwa tena…’ akasema na kuuchukua ule ufungua mkononi mwa Bosi.
‘Lakini Maua kwaninii tusiamue moja tu tukawa wapenzi, mimi mke ndio huyo kanitelekeza, na hatusemeshani kabisa, yeye chumba chake na mimi changu, nafikiri anasubiri siku anafukuze kabisa, na naona ina haja ya kuliharakisha hili jambo ili ajue kuwa kweli sivyo anavyodhania…’ akasema Bosi.
‘Maswala ya mkeo ni mkeo, tulishakubaliana hilo, mimi na mume wangu,wewe na mkeo…hayo hayaingilii hili zoezi, kazi kwako…’ akasema Maua akiingia kwenye chumba kilichokuwa mbele yao, na Bosi akamfuatilia kwa nyuma, hawakufunga ule mlango wa chumba, kwahiyo ukiwa kwenye chumba cha maongezi unawaoan vyema wakiwa kwa ndani na Bosi akawa anasema kwa sauti iliyofifia.`Sikiliza Maua,tunatakiwa kujiandaa kwa lolote, kama mke wangu atanitimua tunahitaji kuishi pamoja…mimi naona iwe hivyo, kwa sababu hui familia yangu ilivyo, wakinitimua wataninyang’anya kila kitu, sasa unafikiri nitakwenda wapi…?’ akasema Bosi.
‘Wewe siuna nyumba yako, unawaondoa wapangaji unaishi mwenyewe…hilo kwangu sio muhimu, tujadili jambo la maana, kwanini jana ulivurunda…?’ akasema Maua
Bosi alimwendea Maua pale aliposimama karibu na kitanda na kumkumbatia, lakini Maua akamsukuma na kusikika akisema kwa sauti;
‘Wewe sasa unazidisha…niachie bwana…’ ilikuwa sautii ya Maua.
‘Lazima iwe hivyo…kwanza…ilitakiwa tufanye kweli ili hawo jamaa kama wapo mahala au wameegesha vifaa vyao wawe wanaona kama kweli kuwa ….najua kweli, hii ni kazi nzito, lakini baadaye itatusaidia..’ Ikasikika sauti ya huyo jamaa akisema huku anajinyosha na kuelekea kutoka pale chumbani hadi kurudi chumba cha maongezi, alielekea kwenye kabati la vyombo, akachukua gilasi  mbili na kueleka kwenye jokofu na kutoa kinywaji, akamimina kwenye gilasi mbili,  akarudi na hivyo vinywaji hadi kule chumbani lakini alipompa Maua gilasi moja Maua akakataa, na kusema;
‘Hapana sitaki kufanya makosa mengine, tukiwa mimi na wewe nataka niwe na akili zangu timamu…’ akasema Maua.
 Baadaye ule mkanda ukawa unaonyesha chumbani ambapo Maua alikuwa kakaa kitandani na pembeni ya kile kitanda alisimama jamaa akiwa kavaa suti malumu, alikuwa anaongea jambo, na Maua anamjibu, lakini kujibishana kule kulikuwa kama kwa kuzozana, inavyoonekana walikuwa hawakubaliani jambo fulani, sauti ilikuwa haisikiki, sijui kwanini mtaalamu hapo alishindwa kuweka sauti isikike. Huenda kifaa chake kilikuwa hakina uwezo wa kunasa sauti za mbali.
 Maneno akwa anawaza ‘Siku hizi bwana, utaalamu ni mkubwa sana, sijui huyu jamaa alifanyaje mpaka akaweze kuchukua matendo yote hayo, halafu alivyoweza kuingia humo ndani…mmh kweli jamaa huyu sio mchezo…’.
 Mara Bosi akageuka na kuelekea sehemu ya ndani ambayo ilikuwa sio rahisi kumuona vyema, na huku Maua anaongea, akionekana kaka kitandani. Wakati huo  Bosi alionekana akiwa na nguo zake kama kawaida tu, halikadhalika Maua akiwa kakaa kitandani huku kabananisha miguu yake, na mikono yote miwili akawa imeshika magotini na kuinamisha kichwa kukaribia mapajani. Mara Bosi akamsogelea na akaonekana akivua tai…na mara akavua koti,…na kulishika mkononi, akaliweka pembeni mwa kitanda… hapo mkanda ukaganda kidogo, na wakati huo Maneno hasira zilikuwa zinaanza kumpanda, `kwanini mkanda usimame hapo, nataka niuone  ushahidi , maana jamaa alishaanza kusarura nguo moja moja….’ akasema Maneo kwa sauti.
  ‘Oooh, sasa nimeamini kuwa mbaya wangu ni yule yule…anajifanya mpole, anajifanya ananijali…kumbe nyoka mkubwa huyu…’ akasema Maneno kwa sauti.
`Mwanzoni nilipoambiwa kuwa mkewe anatembea na bosi, sikujua kabisa wanzungumzia bosia gani, kwani mabosi wapo wengi kwenye ile ofisi, …kwani bosii ni jina au ni cheo…’ akawa anajiliza mwenywe kwa sauti. Lakini jamaa hili wakati wote linaitwa bosi, labda bosi ndilo jina lake, basi hata mimi nitaliita Bosi…’ akasema kwa kimiyakimya. Ni kweli alikuwa hajui kuwa bosi anaitwa jina hilo la Bosi, tangu awali, alikuwa na hamasa sana  ya kuumjua huyo anayeitwa bosi ni nani ambaye amediriki kuuleta ubosi wake hadi nyumbani kwake na kufanya dhambi kubwa ya kutembea na mke wake, ….hata pale walipokuwa usiku wakifanya huo uchunguzi hakufanikiwa kumuona sura yake vyema, sasa kamuona vyema kwenye ile CD.
Ule mkanda uliendelea kuonyesha, lakini kwa kusuasua…na hali hii ilimfanya Maneno ashikwe na hasira, akakumbuka jinsi huyo Bosi alivyokutana naye Hospitalini, jinsi alivyotaka kuuliwa na yule mwanamke bonge, na akakumbuka kuwa alimtuma akachukue vifaa vya mkewe na DVD, ambayo alimwambia asiifungue au kuicheza, eti itaharibika…
‘Ole wake ningeupata huo mkanda, huenda kuna mambo mengi ya siri ndani ya huo mkanda…’ akasema huku akiuangalia ule mkanda ambao bado ulikuwa hauonyeshi kile alichokuwa akikitaka, walikuwa wanongea tu…hata pale huyo jamaa alipovua koti akabakiwa na shati, na baadaye kuvua shati akabakiwa na fulana, lakini hawakuonyesha kukaribiana, na kwahiyo hakuweza kuupata ushahidi anaoutaka kwa haraka. Baadaye ikaonyesha jamaa akitoka mle chumbani na kuingia chumba kingine, na kwa muda huo ikaonyesha Maua naye akiinuka pale kitandani akiwa na khanga,akasogea kwenye kabati na kuchukua Taulo…hapo mkanda ukaganda tena.
‘Labda wanakwenda kuoga pamoja…’ akasema Maneno, na kuendelea kusubiri
  Wakati Maneno anaendela kuangalia ule mkanda, Maua alikuwa chumbani kwake akiwa kajilaza kitandani, alikuwa mwingi wa mawazo, kwahiyo akili yake haikuwepo hapo.Alikuwa anajaibu kuwaza tukio la jana. Kwani, ilikuwa karibu wamnase huyo waneyehisi ni mbaya wao, huenda alikuja kuchukua picha nyingine ili waendelee na madai yao. Hata hivyo Maua hakuridhika na tukio zima na kumtupia mwenzake lawama.
 Ilikuwa usiku wakati wanaongea na Bosi ndipo waliposikia kama mtu akigonga dirishani, walihisi kuwa mtu huyo atakuwa kwa nje, kwasababu walikuwa na uhakika kuwa walipoingia ndani walikuwa wamefunga milango yote. Waliposikia sauti ya mtu akigonga dirisha, wakatulia, na walipoona kimya wakaanza kubishana kuwa nani atoke nje kuangalia,… baadaye Bosii akaamua kutoka mwenyewe na kumuacha Maua ndani. Bosi alipotoka nje,  hakumfahamisha mwenzake kuwa amemuona mtu, kinyume na makubaliano yao, hapo akakunja uso kwa hasira, akalaumu kwanini Bosi alipomfuatilia huyo mtu pake yake.
‘Anadai kuwa hakukuwa na muda wa kumuita, na pia alihisi kuwa huenda kulikuwa na mtu zaidi ya mmoja…kwahiyo huenda ni kundi kubwa sana linalowaandama…’ akawaza  Maua huku akijinyosha pale kitandani. Alipoona usingizi haumjii, akainuka na kutembea tembea pale chumbani, halafu mawazo mengine yakamjia…sasa aliwaza kuhusu mumewe…alijua kwakwelii anachofanya kitakuwa kinamumiza mumewe, lakini hakutaka kumfahamisha sasa hivi, kwani mambo hayajakaa vyema, wataishia kuzozana tu, ..wazo likamjia kichwani kuwa kuna umuhimu wa kukukaa na mumewe, kama inawezekana aondoke kidogo hapo nyumbani, aende kwao kijijini, ili akawaone wazee wake. Hii itampa nafasi ya kufuatilia haya matatizo bila kikwazo...
‘Sitaki nimuhusishe mume wangu, na haya matatizo, kwani ni hatari kwake, namjua saana mume wangu ni mtu kiherehere sana, anapenda kutumia nguvu hata pale pasipostahili, nikumhusisha  anaweza akaharibu kila kitu, tatizo hili linahitaji akili na utaalamu, sio mabavu..na hawa watu waliofanya hili jambo wanaonekana sio watu wa mchezo.’ akasema huku anaelekea mlangoni.
‘Ngoja nikamuone nimshauri hivyo, nitampa hela za matumizi na kuwapelekea wazazi wake nyumbani…na kumalizia ukarabati wa nyumba ya wazee wake…kweli hili ni jambo jema’ akasema huku anafungua mlango wa chumba chake na kutoka kuelekea chumba cha maongezi..
Alipofika chumba cha maongezi akasimama kidogo, macho yake yalikuwa yameona kitu kwenye laptop anayoangalia mume wake, akiaangalia kwa mbali nini mume wake anakiangalia, akasogea taratibu kwa kunyatia, mpaka akawa nyuma ya mume wake. Mume wake akili yote ilikuwa kwenye hicho anachokiangalia na alisikia akiongea mwenyewe kuhusiana na hicho anachokiangalia, Alipofika karibu alishikwa na butwaa…akawa haamini kabisa, kuwa mume wake ndiye huyo aliyeonekana nab OSI usiku…
 Bosi alikuwa kaka kwenye bar moja akipata kinywaji, na siku hiyo aliondoka ofisini mapema akawa anapita pita mjini, hakuwa na la muhimu sana, lakini aliona ni bora akapoteze muda nje ya ofisini. Alitaka kumpitia Maua, lakini akakumbuka kuwa Maua alisema leo hatakaa sana ofisini, atakuwa nyumbani kwake, kwani alikuwa na maongezi muhimu na mume wake, hakuambiwa ni maongezi gani.
 Aliwaza mengi, kwani hata yeye alikuwa na haja ya kukaa na mkewe, waongee, ili kama inawezekana maisha yao yarejee kama kawaida, lakini kila alipojaribu kuonana na mkewe, mkewe alikuwa hampi nafasi hiyo, akasema leo itakuwa vyema kuongea naye kama ndoa haipo ajue moja, …`lazima nielewe, nini msimamo wake, najua ndoa ikivunjika na mimi nitakuwa sina change, lakini naweza kujimudu mwenyewe, …hilo kwangu halina shaka, hata kama nitafukuzwa kazi, nitapata kazi sehemu nyingine, …’ akajipa moyo.
Alizunguka mitaani, mapaka akafika kwenye duka la zawadi, akavutiwa na uwa moja la waridi, akalinunua na kadi yake, akaandika jina la mkewe na kusema kuwa akifika atamwekea chumbani kwake au kama atakubali atampa mkononi na kumuomba waongee. Akaona kuwa hilo ni wazo jema, akatoka pale dukani na kuelekea nyumbani anapoishi, akiwa njiani akakumbuka tukio la jana, na kujialumu kumpoteza yule mtu kirahisi hivyo, akakumbuka kuwa aliokota kadi, ilikuwa sio kadi ni kitambulisho cha kupigia kura, usiku ule alikitazama, lakini hakuweza kuiona ile sura vyema, akaahidi kukitizama vyema mchana, lakini walipoanza kuzozana na Maua akasahau kabisa.
‘Hivi kwanini kila ninapotoa ushauri kwa Maua anakuwa hakubaliani na mimi, kila mara tunaishia kuzozana tu… hivi haoni hata yeye yupo matatani kama ilivyo mimi…ok, hili nalo ni jambo la kuweka sawa, kama anataka afanye kivyake , afanye…lazima niwe na msimamo wangu…’ akafika nyumbani kwake hakuliingiza gari moja kwa moja aliliegesha kwa jirani yake ambapo kuna fundi wa magari, alitakaliangaliwe na kufanyiwa `service’, akatoka pale kwa mguu hadi kwake, na alipoangalia mbele ya nyumba akaona gari la baba mkwe, …!
‘Oh, baba mkwe yupo humu leo, hapa hapanifai, lakini ngoja nifike ndani kwanza, bila wao kujua kuwa nipo, ninahitaji pesa kidogo…’ akasema, akikumbuka kuwa kuna pesa zake aliziweka ndani, kwahiyo akaona apitie nyuma ya nyumba ambapo sio rahis wao lumuona , na akizichukua anaondoka zake, hata hivyo imekuwa ndio tabia yake, akija hapo hupitia mlango wa nyuma, anafanya analotaka halafu huondoka zake!  Nyumba hiyo ni mali ya mkewe, yeye mwenyewe ana nyumba yake aliyojenga lakini wamepangisha, walikubaliana iwe hivyo.
Alipofika kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani, ili upite kwa nyuma, akasikia sauti ya baba mkwe ikisema kwa ukali, …sauti ile ikamvita asikilize nini hicho kinachofokewa, akasogea karibu na mlango kusikiliza;
‘Sikiliza mwanangu hata kama unamependa  sana mumeo, lakini yeye hakupendi, anakupenda kwasababu ya maslahi, hili nililiona tangu mwanzo, hata ndugu zako wanajua hili, sasa unaona…sasa nakushauri tena kabla hujazeeka achana naye,…’ akasema Baba mkwe.
‘Baba kusema hivyo ni rahisi sana, lakini inapofikia kwenye vitendo inakuwa ngumu, mimi kiukweli nampenda, lakini kila siku vitendo vyake vinanitoa doa, imefika mahali namuona sio kama yule mume niliyempenda tena…sijaamua ninii nifanye, ila natafuta ushahidi wa nguvu, nikiupata nitahakikisha naachana naye na nitahakikisha anajuta katika maisha yake yote…’ akasikia mke wake akisema.
‘Mwanangu hata huhitaji ushahidi tena…nakuhakikishia utapata mume mwingine atakaye kusahaulisha kabisa na huyu Bosi, sijui ni bosi wa nini…tunamjua sisi kuliko unavyomjua wewe…hutaishi nay eye kwa amani kabisa…ni mtu mwenye tama…, kwa taaarifa tulizo nazo anatembea na mke wa mtu…sasa nini unataka kutoka kwake, unataka tukupe ushahidi wa kuwa anatembea na huyo mke wa mtu…hapana haina haja,…lakini kama unataka hivyo utapata..vijana watafanya kazi hiyo , sio tutawatuma, tulishafanya kazi hiyo, na kila kitu kipo wazi, ni swala la kuamua tu…’ Bosi hakuamini hayo maneno, kwani wakiwa pamoja na huyu mzee anakuwa mwema kabisa na anampa ushauri kuwa ndoa ndivyo ilivyo, kuna kupanda na kushuka, wavumiliane…kumbe yote ni kudanganywa tu.
Mara akasikia mkewe akisema, `baba usitie shaka kabisa na mimi kuna ushahidi nimeupata, kama utakuwa kama ninavyohisi , mimi sitakuwa na huruma na huyu mtu…nina DVD, niliiona siku nyingi ofisini kwa huyo hawara wa mume wangu, siku hiyo nilikuwa na mawazo mengi sana, nilipofika sikumbuki ni niliibwaga sehemu gani , nimeitafuta sijaiona, lakini kuna CD, moja nimeipata jana ….kwa hawa vijana, wakawa wanataka vijisenti hii inaweza ikasiadia pia…lakini ninachohitaji sana ni ile DVD,  ,,,ile nahisi ina kila kitu ninachokitaka….ushahidi wa kutiosha kabisa…., …lakini baba huoni kuwa kuna watu  wapo nyuma ya hili jambo, kwani kwa uchunguzi wangu, hili ni kundi ndani ya kundi….baba,..’akasema binti.
‘Mwanangu , usione nipo kimya ukazani nimelala…kila linalofanyika tunalijua…lakini mara nyingi hatutaki kuingilia sana, hasa mambo ya kifamilia, labda…’Akanyamaza na kuuliza.
‘Una uhakika mumeo hatarudi, nahisi kama kuna mtu…’ akasema baba mtu.
‘Hawezi kurudi saa hizi, siku hizi analala nje, akirudi anakuja kubadili nguo..lakini baba, nahisi kuna zaidi ya hivyo tunavyofikiria, …kuna watu wawazunguka, inabidi kuwa makini sana, kwani mambo sivyo kama inavyoonekana, ndio maana sina papara, ….ulinisomesha mwanao katika fani ambayo dunia unaiona kiganjani, na mimi sitaki iwe kama fani tu, lakini kwa manufaa ya familia yetu, nami nitajitahidi sana kulinda maslahi ya familia kwa nguvu zote…huyu mume wangu ni kitu kidogo sana, achana naye…siku zake zinahesabika…’ akaseikia mkewe akiongea kwa majigambo kama ilivyo kawaida yake!
 Bosi akwaza sana, ina maana hwa watu wapo nyuma ya haya mambo yote, akasema kwa sauti ndogo ‘Inawezekana ni vijana wake aliwatuma jana usiku…oooh,…kama ndio walipanga iwe hivi ili wanifirisi hawapati kitu… lazima nikamwambie Maua kuwa kumbe baba mkwe wangu ndiye anayenitumia watu ili kuiharibu ndoa yangu, kwa vile hanitaki niishi na mwane …’ akawaza na kuondoka pale ,mlangoni
‘Ina maana baba mkwe  anatumia kila mbinu ili aniharibie maisha yangu…ngoja niondoke hapa, hapanifai kwa sasa…Akazunguka nyuma ya nyumba, kwa kupitia mlngo wa dharura wa nyuma, na alikuwa na ufunguo wake, akafungua ule mlango na kuingia ndani, na ili ufikie chumba chake inabidi upite chumba cha mkewe , na akakikuta kipo wazi. Alipofika kwenye mlango wa chumba cha mke wake akasikia sauti,..ilikuwa sauti ya TV, au …akaona ahakikusukuma mlango ukafunguka wote, na pale kitandani kulikuwa na `laptop ikiwa bado inafanya kazi…kwa mbali aliona kuwa ni mkanda ulikuwa unaonyesha…
Akaingia ndani taratibu na kuangali ni mkanda wa aina gani, kwani alisikia sauti kama yak wake, na shauku ikamjia kujua mkewe alikuwa anaangalia nini ambacho kinamhusu yeye…alipofika akatikisa kidogo ile laptop, kwani ilishaanza kuonekana giza, na akaanza kuona nini alichokuwa akianghalia mke wake….
‘Mungu wangu, ina maana mke wangu ndiye aliyekuwepo jana,…hata siyo yeye  hata hivyo yeye atakuwa alituwatuma watu…’ akasema wakati anaangalia kile kilichokuwa kikioonyeshwa kwenye ile Laptop, ulipoisha akautoa ule mkanda na kutafakari nini la kufanya..!
‘Hii ina maana hawa watu wamniwahi mapema, …natakiwa niwaonyeshe kuwa hata mimi sio mtoto mdogo…kwanza ngoja …’ Akaanza kutafutatafuta mle ndani, nia ilikuwa kutafuta mkanda mwingine auweke kwenye ile laptop badala yake…ili akiingia mkewe ajua kuwa ule mkanda bado upo. Akawa anawaza sana kuhusina na lile tukio la jana....akashikwa na butwaa na kukaa pale kitandani akiwa hana nguvu…wakati anautatafuta mkanda wa kuweka mara macho yake yakaangalia kwenye kikabati kidogo amabcho mkewe hukitumia kuweka nyaraka zake ambazo huziita nyaraka za siri, kilikuwa wazi hakijafungwa, akaingiwa na hamu ya kuangalia kuna nini, na pembe ya hicho kikabati akaona DVD…!
Hiyo DVD, ilikuwa na picha ya mvuto, picha za rangi, picha za, ….moyo ukaanza kumuenda mbio, kwani ingawaje haionekan vyema pale ilipojibanza lakini kwa mbali alishaona kitu…oh,` sio ile DVD, aliyoikuta ofisini kwa Maua kweli…’ akajaribu kuivuta lakini ilikuwa kama imenasa kwa ndani…akasogea karibu huku akiwaza; ‘Oh, ina mke wangu kama ndiyo yenyewe mke wangu atakuwa alipanga haya yote, kwanza alitaka kuniua siku ile, halafu kumbe chanzo ni yeye… haiwezekani…haiwezekani..’ akanyosha mkono kuivuta pale ilipojibanza, ilikuwa imebana kiasi kwamba kuitoa ilibidi kuvuta kwa nguvu kidogo, au kutoa nyaraka zote zilizopo mle ndani, na hii ingechukua muda, akachukua kustuli na kusimama ili afikie vyema …na kabla hajaichukua akasikia sauti kwa nyuma  ikimwambia,
‘Wewe unafikiri una fanya nini hapo….

Ni mimi: emu-three

2 comments :

samira said...

du mambo masikini bosi ndoa hana kazi hana huyu kweli inafunza na yote haya ni wazee wameingilia mambo yasowahusu mpaka wamekwenda toofar
cant wait m3 big up

chib said...

Ni kweli Samira