Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, June 16, 2011

Dawa ya moto ni moto-22



  
 Maua aliwaona watu waliovaa majoho meupe, wakiwa wameshika vitu kama visu na mikasi na sindano …Oh na sindano ndefu ajabu. Watu hawo walikuwa wakishughulika kila mmoja na kazi yake, mara wamsogelee, mara waondoke, lakini walikuwa hawamgusi. Mawazoni Maua alijua kuwa hawa watu wanakitu wanajiandaa kumfanyia. Aliwaogopa sana  hasa yule aliyeshikilia ile sindano, kwani ilionekana kubwa sana, akajiuliza ina maana lile sindani ni la kumdunga yeye mbona ni kubwa kupita kiasi. Akaanza kuogopa sana, alipomuona akimjia na kuanza kupiga kelele.
 Maisha yake yote Maua hapendi sindani, hapendi dawa, ….leo hii anataka kupigwa sindano, na sindano lenyewe ni kubwa…oh, kwaninii wanataka kumpiga sindani kubwa namna ile, kwani ile sehemu ya kupigiwa kwenye ncha yenyewe unene wake ni kama kidole kidogo cha mkononi…akasema sikubali , sikubali, akaanza kupiga kelele kwa nguvu sana….sitaki sitaki…na mara hali ya hewa ikabadilika….
‘Oooh, kumbe ilikuwa ndoto…’ akasema kwa sauti, ingawaje sauti hiyo haikusikika na mara akafumbua macho yake vyema na kujiona yupo kwenye chumba,ambacho kina kila aina na dalili zote za hospitalini. Akajiuliza ina maana ile ndoto ilikuwa ni ya kweli, ina maana yupo hospitalini. `Hivi mimi ninaumwa kweli, na ninaumwa nini…?’ akajaribu kujiinua na kugeuza kichwa upande mwingine mwa kitanda na akamuona  dakitari  mmoja kasimama akiangalia chombo fulani ukutani, kinaonyesha michoro inayobadilika kila mara. Na mara akasikia wale wengine waliokuwepo humo ndani wakiondoka. Akashukuru sana, kwani waliondoka na vifaa vyao, aliogopa wasije kumpiga sindano au kumpa vidonge.
‘Hivi mimi ninaumwa nini,…’ akajiluza, huku akiwaza, na mara  kumbukumbu zilkaanza kumrejea kwa haraka sana, zilianza kumrejea kwa kukumbuka zile ndoto za kutisha, ndoto zenyewe zilikuwa hazina mpangilio. Hakutaka kuzikumbuka vyema, akajaribu kutafakari mengine, lakini hata hivyo alishukuru kuwa zile zilikuwa ni ndoto ambazo sio za kweli. Akaendelea kuvuta kumbukumbu zake kuwa ilikuwaje akafika mahala kama hapo, nini kilimtokea mpaka aletwe pale hospitalini. Hakuweza kukumbuka vyema, akabakia kumwangalia yule dakitari aliyekuwa kasimama , na sasa alikuwa anageuka upende wake.
 Wakati yule dakitari akimgeukia akawa anajipa moyo kuwa mtu wa kumsaidia kwa tatizo alilo nalo la kutaka kutambua kwanini yupo hospitalini limefikia mahala pake, lazima amuulize huyu dakitari, lakini kwanza ngoja amsikia atasema nini. Akajitikisa kidogo ili yule docta aone kuwa kazindukana, hakujua kabisa kuwa docta alishagundua hilo, ila alikuwa akimpa muda wakuweza kupumzisha kichwa na kutafakari. Hata hivyo docta hakuwa na uhakika kuwa akili yake imerudia vyema.
Yule docta alimsogelea na kumwangalia, akainua mkono wake na kuweka vidole viwili kwenye mapigo ya moyo, halafu akasogeza kidole chake karibu na mboni za macho yake, na Maua alipoona hivyo akageuza kichwa pembeni.
 Docta akamuuliza Maua kuwa anajisikiaje, Maua alikaa kimiya kwa muda akiwaza kwaninii anaulizwa hilo swali kuwa anajisikiae ina maana yeye ni mgonjwa, je anaumwa nini, akaona ni vyema ajibu lile swali, ili kumpa moyo huyo docta, na baadaye atamuuliza yeye maswali kuwa alikuwa anaumwa nini mpaka akaletwa hapo hospitalini. Akajibu kwa sauti inayokwaruza kuwa hajambo.
Docta akatabasamu na kusema kimoyo moyo kuwa sasa kweli ile sumu au athari ya yale madawa waliyogundua kwenye damu ya Maua ndicho kilikuwa chanzo cha matatizo yake hayo. Akahema na huku akishukuru mungu kuwa sasa mgonjwa wake keshapona, iliyobakia ni kazi ndogo tu…alikumbuka insi walipohangaika mapaka kuja kugundua kuwa tatizo hasa ni nini…
Waligundua hayo walipochukua damu yake na kuipima kwa makini, na wakagundua kuwa kuna dalili ya madawa ya kulevya, na hilo walilichukulia juu juu na kudhani kuwa huyo mgonjwa alikuwa kaanza kutumia madawa ya kulevya, na yakamkutaa na hata kumletea matatizo. Lakini hali ya mgonjwa ilipozidi kutatika, kwa kuona kuwa mgonjwa anakuwa kama zezeta, na hawezi kabisa akuongea au kuinuka, wakaona kuna zaidi ya hayo. Ndipo huyu dakitari wake akaamua kumchunguza zaidi na alipochukua ile damu yake, na vipimo vingine akagundua kuwa hayo sio madawa ya kulevya, ni madawa mengine ambayo yamechanganywa na madawa ya kulevya .
Alipochukua ule mchanganyiko kwenye maabara na utafiti ulipofanyika iligunduka kuwa hayo ni madawa mengine ambayo pamoa na mchanagnyiko wa madawa ya kulevya, kuna aina nyingine ilichanganywa, na mchanganyiko huo ukiingia mwilini humfanya mtu akawa kama zezeta, na kufanya lolote atakaloambiwa, na humsisimua sana mtumiajii na mwanzoni huwa mchangamfu na husisimukwa sana ..na kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza anaweza akapata taabu sana, mpaka apate dawa za kupunguza hayo makali.
Kitu cha ajabu alichogundua huyu dakitari ni pale alipopima ile dawa aliyokuja naye yule docta wa viatu vyekundu na kugundua kuwa inafanana sana na ile dawa iliyogundulika katika vipimo alivyofanyiwa Maua. Akaingiwa na wasiwasi mkubwa kuwa hawa watu huenda wana uhusiano na Maua au, ndio waliompa hiyo dawa Maua bila kujua ili wafanikiwe katika mambo yao. Akaendelea kufanya utafitii zaidi ili kugundua kwanini dawa hizo zimatengenezwa. Alitafuta katika kumbukumbu n mitandao akagundua kuwa dawa kama hizo, zinatumiwa na watu wanaoigiza mapicha ya uchi, ili kuondoa woga,..na ili kuongeza misismuko mwilini, lakini hizo hazina nguvu kama hiyo waliyoipata au hiyo iliyogundulika katika vipimo vya Maua.
Docta aliingiwa na wasiwasi kuwa huenda waliyoitengeneza hawakuwza  kutumia vipimo maalumu, au walifanya hivyo makusudi kumdhoofisha mtumiaji, bila kujali madhara yake ya badaaye na matokea yake ni kuwaumiza watumiaji, au wahanga …ni hatari sana kwani inaweza kumpafanya mgonjwa akashikwa na kiharusi, na hata kuishiwa kabisa uwezo wa kuwaza,mwili unakuwa hauna nguvu tena, na hili humfanya mtu kiwiliwili,ila mwili unaonekana ni mzima….nini wanataka hadi kufikia kufanya madawa kama haya ya hatari?
Madakaitari walipogundua hili wakatafuta dawa ya kuondoa hiyo hatari mwilini na yale mabaki ya hiyo dawa kwenye damu , na hili lilisaidia kwani haikuwa nyingi sana mwilini , na baada ya kufanya hilo wakawa wakisubiri matokea yake. Haikuchukua muda, kwani  Maua baada ya kizindukana, alionekana kurudiwa na fahamu yake, na hapo wakagundua kuwa ile dawa imefanya kazi yake na sasa ilikuwa hatu ya pili ya kumweka sawa mgonjwa kimawazo, ili kuhakikisha kuwa kumbukumbu zake zimerejea vyema.
 Docta alipoona kuwa mgonjwa wake yupo tayari kuulizwa maswali na kuhakikisha kuwa kweli anaweza kuongea, akamsogelea  Maua na kuanza kumhoji vyema. Alipomuuliza mara mbili kuwa anajisikiaje na kujibiwa kwa kauli dhabiti kuwa  `hajambo’ akaona akili ya mgonjwa ipo vyema!
 Docta alipohakikisha hilo akamsogela mgonjwa wake na kumuinamia na akamuuliza tena kuwa anajisikiaje…Maua akajibu vile vile kuwa hajambo. Docta akatikisa kichwa na kumuuliza swali jingine, kuwa anajua yupo wapi,…Maua akageuza kichwa huku na kule akasema kama hakosei yupo hospitalini, Docta akamuuliza kwasababu gani, anajua anasumbuliwa na nini mapaka akafika hapo hospitalini. Maua akanyamaza kimiya halafu akasema, `hajui’ na docta akamwambia anakumbuka lolote lililotokea kabla hajapoteza fahamu,Maua akasema anakumbuka kuwa alikuwa ofisini kichwa kikawa kinamuuma sana, na akajikuta anasikia kizunguzungu, baada  ya hapo hakumbuki kitu.
‘Sikumbuki kitu kingine,…’ akasema Maua halafu akaongezea kwa kusema ` ila sijui kama ilikuwa ni ndoto au ni kitu gani, nilimuona docta akiwa na viatu vyekundu akiwa kashika sindano, ambayo alidai akinipiga itanifanya niishiwe uhimili wa viungo, na huyo dakitari alitaka kumuua dakitari mwenzake nikampiga na kitu, halafu sijui ilikuwaje…hapo sikumbuki tena…’ Yule dakitari akataka kumuuliza swali jingine lakini akaona mgonjwa wake anahitaji muda wa kupumzika kwanza akamwacha ili apate  muda wa kutafakari zaidi. Lakini kabla hajaondoka akakumbuka kitu na kumgeukia Maua akamwambia;
‘Nakushauri, usisumbue kichwa chako kufikiri sana, wewe chukua mambo taratibu,ili ubongo usichoke, na hata akija mtu , kama hujisikii kuongea, nyamaza tu, najua wanaweza wakaja watu kukuulizia hali, kwa hivi sasa tutawazua ila baadaye hatutakuwa na haja ya kuwazua na watu kama maaskari  wanaweza wakaja kukuhoji, mimi nitawaambia bado haupo tayari kuongea nao, …unahijai muda wa kutulia…sawa?’ akasema docta.
‘Sawa, lakini hawa maaskari wanakuja kunihoji kuhusu nini…kwani nimeua au nina kosa gani nimefanya..’ Maua akauliza na kujaribu kutafakari kuwa huenda kuna kosa kubwa kafanya, ila hakumbuki na wakati anawaza hivyo, kumbukumbu za nyuma zikaanza kumjia, akakumbuka mambo ya hotelini, akakumbuka, mambo ya DVD,…na alipokumbuka mambo ya DVD akainuka pale kitandani, alijiona mwili hauna nguvu kama kawaida yake, lakini aliweza kukaa, na hili lilimpa moyo docta kuwa sasa mgonjwa anachohitaji ni mzoezi ya viungo, …akamwangalia mgonjwa wake anataka kufanya nini, na kwanini alipokumbuka hivyo kashikwa na wasiwasi hivyo.
Maua alipoona hajakuwa vyema, lakini alihisi kama akijitahidi anaweza akainuka alimwambia docta anataka kutoka kwenda ofisini, kwani aliacha vitu vyake ovyo, na vingine vinahitaji usalama … Docta akamwambia kama anaweza kusimama basi itakuwa hatua nzuri ya kwenda huko ofisini, lakini ana uhakika kuwa bado haakuwa na nguvu hiyo. Maua akajaribu kuinuka pale kitandani lakini alijikuta mwili hauna nguvu ..bado!
‘Wewe usijali, mume wako ametumwa kuhakikisha kuwa kila kitu chako kipo katika hali ya usalama, na sidhani kuwa kuna tatizo kubwa, kwani chumba cha ofisi yako kilihakikishwa kuwa kimefungwa kabisa mpaka utakaporejea, kwani nimesikia ni chumba cha bwana fedha, kwahiyo mambo yote yapo salama mpaka utakaporejea, hata hivyo, hiyo ni ofisi, uwepo usiwepo mambo ya kiofisi yapo, na watendai wengine wapo…na wanajua kuwa una matatizo, sioni kwanini likutie hofu kiasi hicho…’akasema Docta.
‘Unasema mume wangu ndiye katumwa ofisini kwangu, ni nani kamtuma mume wangu…ni nani mwenye maamuzi ya namna hiyo, ya kumtuma mume wangu kwenye maswla yangu ya kikazi, yeye ni mume wangu kwa maswala ya nyumbani sio mambo ya kiofisini mbona wanachanganya mambo hawa. Mume wangu hajui mambo ya kiofisi…hapana… lazima niwahi mwenyewe ofisini….hapana docta niruhusu niende….’ Akasema Maua na  hapo kichwa kikaanza kumuuma, akashika kichwa, na docta akaliona hilo, akachukua dawa za maumivi ya kichwa akamwambia anywe, Maua akaiangalia ile dawa, na kitu kama kichefuchefu kikamjia, akashika mdomo, akitaka kutapika…lakini akajizuia, na docta akatabasamu, akataka kumwambia kitu lakini akaona sio mahala pake, akampa ile dawa anywe…ilikuwa kazi kwa Maua kunywa vile vidonge, na hapo docta akamuuliza kuwa inakuwaje anachukia dawa kiasi hicho.
‘Hakuna kitu ninachokichukia kama dawa, …sipendi kabisa dawa, ….sindano….i hate those items, I wish visingekuwepo…’ akasema Maua, na Docta akataka kumuuliza kitu , lakini akasita, alitafakari sana, na akamuuliza swali moja kuwa katika maisha yake alishawahi kutumia madawa ya kulevya, Maua akamwangalia docta na kushangaa, akasema `madawa ya kulevya, sijawahi hata kuyaona kuwa yapoje, na ukishasema madawa mimi naona kichefuchefu…hapana docta, naomba hilo liniepushie mbali, sijawahi na sitawahi kutumia kitu kama hicho katika maisha yangu…’ akasema Maua huku akitafakari kwanini docta amuulizie kitu kama hicho.
Docta akawa na mashaka kuwa huenda huyu mgonjwa atakuwa aliwekewa haya madawa kwenye kinywaji, au alipigwa sindano kama alivyotaka kumpiga yule jamaa aliyejidai kuwa ni dakitari…kwasababu hayo madawa yaliingiaje mwilini mwake kama yeye mwenyewe hatumii, kwani ndiyo yaliyomuathiri hadi kupata shida ya maumivu ya kichwa, na …
Docta akamwambia Maua kuwa hali yake hairuhusu kutoka mle hospitalini kwani bado yupo katika uchunguzi, na mambo mengine ya kiofisi, ayasahau kwa muda kwani cha muhimu kwanza ni afya yake, na kama kuna kitu anakihitaji haraka asema, mtu atumwe atamletea, na asiwe na shaka, kwani usalama upo kabisa. Na kabla hawajamaliza mlango ukagongwa, na docta akashangaa, kwani akiwa humo ndani na mgonjwa hairuhusiwi mtu kuja kuingilia kati, akamwambia Maua alale na ajifanye hajazindukana, kwani alijua huyo mtu aliyegonga atakuwa sio dakitari, kwasababu madakitari wanajua taratibu hizo, huyo mtu atakuwa mtu wan je  haraka akaenda mlangoni na kufungua.
‘Vipo wewe…ni nani kakuruhusu kuja chumba hiki,… unatakiwa uwepo kitandani mwako, mbona …’ docta  akasema alipomuona mmoja wa wagonjwa ambao bado walitakiwa kuwa mapumzikoni. Alimkumbuka huyu mgonjwa aliletwa akiwa mahututi kabisa, na upasuaji wake wa kichwa ulikuwa mgumu sana, …ingawaje walifanikiwa na kuondoa damu ambayo kama ingecheleweshwa ingeweza kuathiri ubongo. Lakini hata hivyo kiusalama Maua hakutakiwa kuonekana na mtu , huyu mtu amejuaje kuwa yupo huku, au anamtafuta nani
‘Docta nataka kumuona Maua nasikia wewe ndiwe mgonjwa wako, yeye ni msaidizi wangu ofisini, na kuna kazi nilimuachia ni muhimu sana, kujua kaiweka wapi ilinimuagize mtu akaichukue,ikikosekana tutakuwa tumeharibu kila kitu ofisini….’ Akasema yule mgonjwa. Docta akamuuliza ni nani kamwambia kuwa Maua yupo hapo, na alitaka kumuuliza zaidi kama angekuwa kafariki nani angefuatilia hayo anayotaka kuyafuatilia, lakini akaona hilo sio swali zuri kwa mgonjwa.
‘Maua hayupo hapa na hata hivyo Maua bado haruhusiwi kuonana na mtu yoyote, bado hajazindukana, nakuomba ukatulie kitandani mwako kwanza, akizindukana nitamwambia, tafadhali katulie kitandani mwako msiifanyekazi yetu iwe ngumu…’ akasema Docta lakini kabla hajamaliza hayo maneno Yule mgonjwa akawa kausukuma mlango wa kile chumba na haraka akaingia ndani huku docta akimfuatilia kwa nyuma.
‘Wewe vipi nimekuambia nini, ina maana hunielewi…’ akasema Docta. Na wakati huo huo Maua alishasikia sauti ya huyo mtu akaigundua ni sauti ya nani, hasira chuki na….zikawa zimempanda kiasi kwamba alishindwa kuvumilia na akajikuta akitaka kuinuka pale kitandani. Aliwaza sana, kwani muda mfupi uliopita alikuwa akiwaza jinsi gani ya kuonana na huyu mtu aliyesikia sauti yake kwani kamani yeye alimfanyia jambo lile la hatari, …atahakikisha anamfanyia kitu mbaya….atajua jinsi gani ya kumfanya hiyo kitu mbaya,`nitamuonyesha kuwa mimi ni nani….’ Akasema kimoyomoyo. Na aliposikia hiyo sauti  akafunua shuka taratibu kumwangalia ili aone kama ndiyo yeye au ni hisia zake tu,alifunua shuka ambalo alikuwa kajifunika gubigubi taratibu na kuacha uso wazi na mwili ulianza kumchemka kwa hasira, akatamani kupayuka kwa nguvu, kwanii alipofunua hilo shuka na kuangalia, macho yake  yakawa yanaangaliana na macho ya …….. 


Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

3 comments :

Anonymous said...

Mmmmmmm!!! hii ni kali, kwelikweli. Haya sasa, sijui itakuaje!!!!!!!???? Mungu wangu bora waseme tu mbele ya Dr. ili Docta hajue kinachoendelea.

Kazi kwelkweli, M3 tafadhali usicheleweshe utamu huo.

BN

samira said...

uwiii mauwa dvd haipo na bosi anaitaka pia ndowa na kazi zenu zipo mashakani
swali kwa nini wamefanyiwa unyama huu je mfanyaji anataka nini kati ya family hizi mbili
m3 cant wait kazi yako naiheshimu

Faith S Hilary said...

Eee bana eeee sasa wamekutana tuone itakuwaje maana wote wamekutana tuone wata "handle" vipi the "SITUATION"...nipo sibanduki