Jua hapa Dar ni kali kweli,...kulikuwa na dalili za mvua, lakini zimepotea...! nikawa napita karibu na mitimiti, ili kupata kivuli nikaona pembeni kidogo kwenye uwanja ulio wazi mbuzi wanne wamefungwa kamba, niliwaonea huruma sana, kwani pale walipofungwa hakuna majani, pakavu na jua linawaka mtindo mmoja, wanahema utafikiri mashine!
Niliwaza, kwanini huyu mwenye hao mbuzi hawaonei huruma hao wanyama, au kwasababu ni wanyama tu, nao wana haki yao,...vile sio haki kaabisa, nikawasogelea, huku nawaangalia kwa macho ya huruma, na wao wakaniangalia wakijua nakuja kuwaondoa kwenye hayo mateso..., mara akatokea kijana mmoja, na kuniuliza nahitai mbuzi, akaongeza kuwa wanauzwa, na nikichelewa kesho siwaoni tena, akaonyeshea kidole shingoni, kuwa wanakwenda kuchinjwa!
‘Hapana sihitai mbuzi, ila nimewaonea huruma, hapa jua kali hakuna majani, wanateseka..!’ Nikamwambia yeye akacheka
‘Unawaonea huruma, wakati muda wao wa kukatwa shingo umefika, hawa ni swala la muda tu, pesa ipo nje nje, mbuzi sasa adimu, hata kama nitawaweka hapa juani siku tatu bado wanalipa, naogopa kuwapeleka kwenye maeneo ya watu wanagomba….’ Akasema maneno mengi.
‘Sawa kulisha mifugo maeneo ya mjini sio haki au sio, na hawa wanyama unavyowaweka hapa sio haki, na huwatendeihaki kabisa, ..lakiniwewe mwisho wa siku unahitaji upate haki ambayo unaiona ni haki yako, au sio…mbuzi wako, …lakini kuwa na haki ya kumiliki hao mbuzi sio sababau ya kutowatendea hawo mbuzi haki…unanielewa lakini. Haki hujaitendea haki unatarajaki upate haki..? nikamuuliza
‘Sikuelewi mzee , kama huhitaji mbuzi, basi ishia maana watu wa halimashauri wakikuona hapa italeta shida…nimekuelewa, hiyo naijua sana, lakini…ngoja nishike mshiko wangu kesho nitajua hayo mengine baadaye…sawa, ishia basi mzee…’ akasema name nikaona isiwe noma nikaishia kama alivyosisitiza.
Mimi sikuishia hapo kuwaza, kwani wakati natokeza barabarani, nikakutana na wenzetu wa `tiaraei’ nikajua kabisa wanelekea huko mitaani kuwachakachua wafanyabiashara, kwani kodi sasa hazilipwi, nikajisema mwenyewe, kuwa ndio yale yale, ya kuwa `haki haitendewi haki, lakini mtu anataka apate haki, ambayo mwisho wa siku haitatendewa haki yake pia.
Hawa jamaa wanakusanya kodi, tunajiulza nini inafanya? Kweli inafanya mengi , mabarabara yanajengwa, mashule yanajengwa, mahospitali yanajengwa, hii ni kodi yako mlipaji, lakini kiukweli sivyo kigharama ilivyo…gharama inachakachuliwa, hili lipo, kuna `ten pacent’ ya mtu hapo, kuna `speed-up ya mtu hapo…kuna vifaa duni vimenunuliwa na kuitwa vifaa origion, kuna…mambo mengi ambayo sio `haki’ yametendeka,…na watendaji ni hao ambao mwisho wa siku wanalalamika, hali mbaya, viongozi hawawjibiki nk…wewe hujatenda haki yako na umepewa dhamaan ya kusimamia haki itendeke unaichakachua unatarai nini...? Itendee haki haki yake kwanza!
Wakati nipo kwenye daladala, nikiwaza mengi yanayaotokea nikakumbuka ajali zilizofululizana,…nawapa pole sana wafiwa, na waliotangulia mbele za haki mola awalze mahala pema peponi,…hiyo ndio njia yotu sote…lakini, wakati mwingine tujaribu kusema, sheria inapokiukwa, ni haki yetu kusema, ili haki itendewe haki….kwenye daladala hili, mambo yalikuwa yale yale, mwenye daladala alikuwa akikatisha sehemu ambazo ni hatari, abiria kimya, wanaomba tufike salama, kwani hata hivyo tutachelewa makazini, mwajiri hatatuelewa, …makosa kama haya ya kutenda isivyo haki, ndio mwisho wa siku inatokea ajali, tunaishia kusema dereva alikuwa akiendesha kwa kasi, kwanini hatumwambii muda ule, ule, tunasubiri kusema `kama ingelikuwa…wakati ishakuwa…’ nikapayuka na kusema dereva, unavyofanya sivyo, ingia barabarani,…utaleta ajali za kujitakia… abiria wengine wakaguna….
Nikaomba moyoni nifike salama maana nakumbuka `eniesiesi efu yangu’ imeiva, natakiwa kwenda kupata chochote, nikajaribu kupiga mahesabu kama inaweza kununua `bajaji’ , nikagundua hata baiskeli sasa hainunui, lakini kama kipindi kile ningeipata, kwa thamani ya miaka ile ingenunua bajaji , sasa hela nitakayopata haina thamani hiyo tena…haki yangu imeenda arijojo. Nakajiliza hivi hili wabunge hawalioni, hivi hili vyama vya wafanyakazi hawalioni, kuwa thamani ya hela ya leo sio sawa na ile ya kesho hasa hela yetu hii ya madafu! Basi iwepo sheri kuwa hela kama hizo zinazokaa miake nenda rudi ziwe zinathamanishwa na dola, ili siku ikifikia kuchukuliwa na mwenyewe awe anaipata kwa thamani yake ile-ile…ni haki ya mwenyewe…, lakini haki hiyo haitendewi haki, je kweli haki itakuwepo duniani.?
Niliangalia saa yangu, nikashukuru kuwa nimefika kwa mwajiri wangu kwa muda muafaka, kwahi huo ni wajibu wangu, nikichelewa ninaweza kukitia kitumbua mchanga, na haki yangu yote itapotea. Mwajiri anachotaka ni wewe uwepo kazini , utimize wajibu wako , hata kama anachokulipa ni kiduchu, bado anadai uwajibike, anaona huo ni wajibu wako…ndio yale yale ya wale mbuzi,w anawekwa juani, hakuna malisho,..lakini mwenye mbuzi ana ndoto za hela …mwajiri ana ndoto za kulitumia jasho lako vyema, …wanakodi wanasubiri kodi yako,…na wewe unaota kuwa ukimaliza muda wako wa kazi , huna ajira tena, basi utanunua bajaji ili likusaidie maishani kwa pensheni yako, lakini unafika dirishani unapewa ile hela hata baiskeli hainunui…haki haikutendewa haki, unatazamia nini mwisho wa siku, mimi sijui , nawaza na kuwazua kuwa kweli dunia itakuwa na amani…!
Hili ndilo wazo la Ijumaa ya leo.
Ni mimi: emu-three
7 comments :
Nadhani hadi unafika ofisini morali ya kazi ilishaisha kufuatia changamoto ulizokabiliana nazo njiani. Ndiyo maisha ya bongo lakini, safari bado ni ndefu na ni ya kukatisha tamaa wakati mwingine. Lakini kama mpiganaji huna budu kusonga mbele.
Kweli mkuu kama ulikuwepo, nilifika ofisini kwanza nimechoka kwa usafiri, daladala zinajaza utafikiri magunia, joto usiombe, ....akili haijatulia , mambo yakufikiri ambayo hayatekelezeki hayahesabiki....lakini ndio hivyo, inabidi utimize wajibu wako, ili angalau mwisho wa siku upate kitu kidogo, sehemu ndogo tu ya haki yangu!
TUPO PAMOJA MKUU, SILAHA BEGANI WEKA!
Ni kweli m3, "haki haitendewi haki", hili ni zaidi ya wazo. Ndio kiini hasa (kwa mtizamo wangu) wa sisi Watanzania na Taifa letu kupiga hatua za kinyonga kama si za konokono katika swala zima la Maendeleo. Ndio maana nchi yetu imekuwa mshirika mkubwa wa "struggle for existence na "survival of the fittest". Sheria hazitumiki kisheria, haki hazitendewi haki, utu umewekwa pembeni, ilimradi mtu keshapata alichotaka.
Yote Maisha ndugu yangu. Ni kuyakabili kadri yanavyokuja1 Weekend njema
oya sa umezidi mshkaji ile story ya "maisha yana kila aina ya mitihani" haijesha ushachomeka ingine huku "nani kama mama" inaendelea unatukata rythmn bwana!
Yani stori hii nimeirudia mara kibao yani na mpaka leo bado nakuna kichwa!
Mpaka nahisi labda itabidi fulu vita kwanza bogno ili ndio mambo yabadilike!:-(
Nawaza tu!
naona bado nipo mawazoni labda nirudie tena kuisoma hii stori. m3 ni wazo la kufikirisha kweli ngoja kwanza nijaribu kunywa majiau labda chai....Ahsante kwa wazo ingwa nimechelewa kidogo.
Post a Comment