`Vipi rafiki mbona umekuwa adimu siku hizi, na ukionekana mara moja moja unaonekana upo juu kwa juu…’ nikamuuliza jamaa yetu ambaye muda mwingi tulikuwa naye kijiweni lakini ghafla akaadimika.
‘Wewe huna taarifa jamaa kapata cheo ofisini kwao, na watu hawaamini alivyobadilika. Yale ambaye alikuwa mstari wa mbele kuyakataa yaliyokuwa yakiwakabili maofisini, na sehemu za kazi, ndio huyo nay eye anayafanya tena zaidi. Unakumbuka jamaa huyu kuwa, kuna siku alituambia kuwa kachaguliwa kuwa msemaji wa chama cha wafanyakazi ofisini kwao, na akawa anadai maslahi bora kwa wafanyakazi. Sasa kapewa rungu la umeneja ofisini kwao, …’ rafiki yetu huyo kusikia mwenzetu anaelezea kumuhusu yeye akataka kuondoka, mimi nikamzua na kumpa hongera ya kupata cheo kwanza.
‘Hiyo hongera yako naipokea ,lakini isije ikawa ya kinafiki kama ya hawa jamaa zetu, wao wanafikiri cheo kama hicho ni cheo cha mchezo, …inabidi ulinde dhamana ya watu. Nimepewa umeneja ndio nimeukubali, nisingeweza kuukataa, eti kwasababu nilikuwa mdai maslahi, lakini kuna mipaka yake. Natakiwa nibane matumizi ili, ile bajaeti niliyopewa isivuke lengo, sasa nitafanyaje, …hebu niambieani…sasa naukubali ule usemi usemao kuwa `ugumu wa mpira hutauona ukiwa mshangiliaji, ingia uwanjani ucheze …’ akaniangalia kusikia nitasemaje.
Nilivyosikia ni kuwa jamaa yetu huyu alipoupata umeneja, alifikia mpaka anaondoa chai ya ofisini eti inatumika ovyo, wafanyakazi badala ya kula mchana , wanashindia chai, kwahiyo inabidi chai inunuliwe zaidi na zaidi kinyume na bajeti yake. Watu wakamhoji, hiyo hela ya kula chakula kila siku ipo wapi. Akawajibu kuwa hilo sio jukumu lake, ni jukumu la kila mtu mfukono mwake, kwanii kila mtu ana mshahara wake..Watu wakabaki mdomo wazi, wewe ndiye uliyekuwa ukilalamika kila siku kuwa mshahara hautoshi, ukawa mstari wa mbele kudai mshahara upandishe, kuwepo na chai ofisini nk, leo hii umepata umeneja, umesahau ulipotoka, ama kweli `mwenye shibe hamkumbuki tena mwenye njaa.
‘Jamani kila jambo kwa wakati wake, mimi sipo katika ngazi ya kulalamika, nipo katika ngazi ya kutimiza majukumu ya kampuni, siwezi nikayafanya yale yote niliyokuwa nikiyadai, kwasababu nikifanya hivyo nitakiuka misingi ya kazi yangu ya `UMENEJA’ …akajitetea jamaa yetu na kuondoka pale kijiweni, kwani kama meneja hatakiwi kukaa kijiweni tena, kama sisi watu wa hali ya chini, yeye anatakiwa kukaa kwenye `viti virefu…, kwenye vilabu , wapi kule sijui’
Haya ndiyo maisha yetu ya kila siku wanasema kila ndege na mti wake, ..maisha kama haya huanzia majumbani, mitaani na maofisini. Na mabadiliko ya kimaisha hutokana na `kipato’ na kipatoo mara nyingine hutegemeana na wadhifa. Wadhifa ukiongezeka , kipato kinatuna na maisha yanabadilika, na hata tabia hubadika, kwahiyo tusione ajabu kuwa yule rafiki aliyekuwa karibu nawe baada ya kuwadhifika akawa sio rafiki tena. Angalia wale waliokuwa karibu nasi wakati wanadai `kura’ wameshapata `kula’ …leo wapo wapi…lol
Lakini vyovyote iwavyo, tusisahau kule tulipotoka, angalau tujaribu `kula na vipofu’ huku unalinda wadhifa wako, huku unasadia wenzako angalau kidogo, kwani ulikuwepo kipindi wanashindia chai ya ofisini, sio kuwa wanapenda, ila bajeti hapigiki. Utapigaje bajeti ambao inaishia na hasi, na hasi haiishi hata utambike.Itaishaje wakati `kile kinachoitwa mshahara’ kila siku kinashuka thamani yake. Leo angalia mabango ya thamani ya dola utathibitisha hayo, ile shilingi ya hamsini ya juzi, inanunua nini sasa. Inanunua kile ulichokuwa ukinunua kwa shilingi kumi…mmmh, utaniambia kuwa inakuwezesha kulongalonga…biashara hiyo. Hii ina maana gani, ina maana kuwa hela yako haithamaniki kutokana na kushuka kwa thamani!
Sasa niambieni mshahara ni ule ule, lakini bei za mafuta zimependa, bei za umeme ndio usiombe, kila wakiamuka wanawaza kupandisha huku wanaumwa ugonjwa wa mgawo usio na tiba, ugonjwa huu unatafuna faida yote na kuishia hasarani. Wewe jiulize siku nzima hakuna umeme, na kuwaka kwa umeme ndio biashara, ndio mauzo huongezeka, wewe unakata umeme na huku unadai kuwa unajiendesha kwa hasara, mbona `HATUELEWI’ Tulidhania kuwa kwasababu una hasara ungejitahidi kuuza zaidi na zaidi, na kuuza zaidi na zaidi ni kuwpo kwa bidhaa ambayo ni kuwaka kwa umeme….sasa masikio yanaingia ukungu kwa mingurumo ya majenerator, au kuna mtu ana ubia na haya wazalishaji wa majenerator na mishumaa nini…
Sijui, labda imekuwa kama rafiki yetu..yeye kaona kubana matumizi ndio kuiweka bajeti ya kampuni kwema, na kuwabana wafanyakazi hata kile cha kuwafanya `waishi’ ambacho ni chai, ndio kaona ni njia pekee ya kukabiliana na gharama kama ilivyokuwa kwa mgawo wa umeme…Msione nalalamika, nilianazisha kibishara kwa mkopo, na umeme ulikwa ndio moja ya mali ghafi yangu sasa umeme hakuna, ina maana bishara hakuna, …jamani kufa hatufi cha moto tutakiona,..
Ni wazo tu leo Ijumaa, labda nimekosea, wataalamu tunaomba mtusaidie kutupa mawazo.
6 comments :
Mmmmmmh! EM-3 Ulichosema ni kweli kabisa coz tunayaona huku mtaani na makizini kwetu pia. Sio siri ukisikia siku ya kufa nyani miti yote huteleza ndo huko. Mtu unaamua kuanzisha kamradi tena ka mkopo ili walau mtu usisubilie mwisho wa mwezi pale dirishani, sasa baada ya kuanzisha hiyo ofisi nyingine ndo matatizo yanazidi badala ya kupungua, kama hivyo umeme hakuna sehemu uliyofungua yenyewe umepanga unatakiwa kulipia kibanda, na kila mwisho wa mwezi sijui bank sijui ofisi wanataka kupata punguzo la mkopo wako na mengine mengi kama hayo, sasa jamani tumepunguza matatizo au tunaongeza?????? Tafakari na chukua hatua.
Wazo la ijumaa ya leo limenyooka kabisa kwani si uongo aliyeshiba hamjui kabisa mwenye njaa. Au ngoja nikuulize ina maana chakula cha mchana kilikuwa kinapatikana hapo kazini au nimeelewa vibaya? maaana mimi kila siku niendapo kazini nachukua chakula changu toka nyumbani pia hata chai. Kwa hiyo huyu anataka kuanzisha .....mmmhhh! naachia hapa
Kweli Jane, wanasema kufa, kufaana, yaani wanapoona wewe unachukua mkopo wanazani unaziweka mfukoni, na wao wanataka wapatie hapohapo...hawafikirii kuwa mwisho wa siku unatakakiwa marjesho, mbona kwenye marejesho hawakuungi mkono...
Dada Yasinta...hakuna chakula chakula kazini, ni wewe na mfuko wako, mara nyingi ikifika katikati ya mwezi kwa wafanyakazi wengi, hela imekatika..wanachofanya ni kununua mhogo au kama uitwavyo huku `chps dume, unashushia na chai...siku imepita!
Sasa bosi kaona chai inanyweka sio kawaida, bajeti ya sukari inakuwa kubwa, afanyeje?
Blogger wa pili wa siku moja naona mnalalamika sana kuhusu huo umeme mpaka naogopa kuja (nitakuja anyway lol) ila kwa kweli poleni, nchi yetu ni Mungu tu anajua yanatokea na siri zote (isipokuwa WikiLeaks loool) na ni yeye anayesaidia kusonga mbele na hali ya maisha - ila kwa kweli, poleni.
Mmmh!
Snitch
Post a Comment