Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, January 11, 2011
Aisifuye mvua imemnyea-hitimisho
HITIMISHO:
Docta wangu aliniambia kuwa kutokana na ushauri wa watu wengi na usalama wa watoto na familia yake, hatimaye rafiki ynagu aliamua kuiuza ile nyumba, na hutoamini, siku aliyoweka tangazo la kuiuza ile nyumba walipatikana wanunuzi watatu na mmoja akakubali kuinunua kwa pesa taslimu ambayo ni zaidi ya alivyokadria, aliona ajabu isiyo ya kawaida.
‘Nyumba hii nataka niinunue sio kwa ajili yangu, ila kwa watoto wawili mayatima, walinihadithia kisa chao cha kudhulumiwa eneo lao na aliyewadhulumu alikuwa Mzungu, na hata walipofika mahakamani, kesi ikahukumu kuwa haki ni ya huyo mzungu, kwani aliyeisimamia nyumba na eneo hilo ilikuwa baba yao mdogo…wakati panauzwa kulikuwa na nyumba ya kawaida tu, baadaye huyo mzungu akajenga nyumba kubwa, na kulizungushia uzio eneo lote, sasa nilipoona maelezo ya hili eneo, nikahisi inawezekana likwa lenyewe, naomba sana uniuzie, ili tumalize haya matatizo….’ Akasema yule mnunuzi
Docta akashangaa kusikia hivyo, kwani maelezo na sifa za eneo zinafanana na eneo analoishi, akajaribu kumdadisi mnunuzi, lakini huyo jamaa hakuwa tayari kuongea lolote, zaidi ya kutaka kununua eneo, alisema mengine ni mambo ya kifamilia hayamhusu mtu mwingine, …Docta akasema moyoni, ni bora niiuze tu, lakini lazima nijue nini undani wa hili tatizo.
Kwahiyo siku moja akaamua kwenda kumtembelea yule mzee aliyeonana naye mara ya kwanza wakati ananunua hilo eneo, alifika muda wa mchana, na alipofika nyumbani kwa huyo mzee alikuta baadhi ya watu wamsimama nje ya hiyo nyumba, na baaadhi wamshikilia vitambaa kuziba pua zao. Ilikuwa dhahiri ya harufu mbaya iliyokuwa ikitokea eneo hilo. Docta akahisi kuna kitu kibaya kimekufa, na aghalabu harufu kama hiyo ni ya mnyama mkubwa.
‘Huo ni mzoga wa ng’ombe au mnyama gani, kwanini umeachwa mpaka utoe harufu kiasi hicho…’ Docta akauliza, huku nay eye akichukua kitambaa kuziba pua na madomo kwani harufu ilikuwa haielezeki.
Watu waliokuwepo hapo wakaangalia chini na wengine wakawa wanaondoka, akajikuta kabakia na watu wawili ambao walikuwa wakiulizana kwa kunong’ona nini cha kufanya, ni kila mmoja akawa anatafakari na kutafuta mwanya wa kuondoka pale, kwani kwa ujumla hali ilikuwa sana.
‘Mtu huyu hafi tu, anaoza akiwa mzima, anatutesa hata sisi …’ akasema mmojwapo kwa sauti, huku akisogea mbali na nyumba.
Docta akawaza, ina maana hiyo harufu ni ya mtu, haiwezekani…akaingiwa na hamasa ya kuuliza na kujua kama ni mtu imekuwaje…!
‘Jamani naombeni kumuona Mzee Kijuvingombe, yupo au kasafiri maanake mzee huyu kwa kusafiri..’ Docta akasema akiwa amezidiwa na ile harufu, na aligundua kuwa harufu ilikuwa aikitokea ndani mwa ile nyumba.
‘Mzee yupo ndani lakini kwa ushauri wetu huwezi kumuona,… na…’ kabla hajamaliza mwenzake akamfinya.
‘Bwana kama unahitaji kumuona ingia ndani, nakukumbuka kuwa wewe ni dakitari huenda ukapata ufumbuzi wa hili tatizo, ingawaje tunahisi huo ugonjwa sio wa kihospitalini na hautibiki tena..’akasema mzee mmoja ambaye alijulikana kama mtaalamu wake, lakini kwa hali ilivyo, utalaamu wake uligonga mwamba.
Docta akarudi kwenye gari na kuchukua aina Fulani ya mafuta ya kupoteza harufu, akapulizia mle ndani huku anaingia hadi chumba ambacho alicholazwa huyo mgonjwa, kulikuwa hakuna kitu, ila bakuli la uji ambalo huenda limewekwa tangu asubuhi, kwani mainzi yalikuwa yakiruka huku na kule, na kijiko kilikuwa bado mkononi mwa huyo mgonjwa kikiwa na uji usionyewa, na mgonjwa yule, hakuwa na uwezo wa kukisogeza mdomoni tena. Yule mgonjwa alikuwa kalala kama kuegemea kwenye mto ulibadilika rangi kwasababu ya damu au rangi za uchafu!
Yule mgonjwa alifunua macho yaliyochoka, na sauti kubwa, ambayo huwezi kuzania kuwa inatokea kwa mgonjwa ikatokea mdomoni mwake;
‘Docta aheri umefika, na natumai sasa naweza kufa kwa amani, nilikuwa nakusubiri kwa hamu nilijua ipo siku utafika…’ akakohoa, na kikohozi kilikuwa kikavu, akionyesha kuwa anahitaji maji. Docta akaangalia huku na kule akaona ndoo yenye maji akachukua kikombe na kumchotea, akamsaidia kumnyesha kwa kumwekea mdomoni…
‘H ii ndio kazi yetu madocta, huwezi kumkimbia mgonjwa hata kama yupo katika hali gani..’ akasema huku anajaribu kumnywesha kwa shida.
‘Ahsante sana Docta, najuta kuwa watu wema kama nyie mnakutana na watu wabaya kama sisi, sistahili hata chembe kupata huruma yako, kwani siku kadhaa nyuma nilikuwa natamani kunywa damu yako…’ akakohoa kwa shida na maji kidogo yakamezeka.
Docta alisema amewahi kuwahudumia wagonjwa wenye hali mbaya, lakini huyu alikuwa kazidi hali yake ilikuwa mbaya, kwani licha ya kupulizia yale manukato ya kuondoa harufu mbaya, lakini harufu ilikuwa ikikereketa kama ugoro. Mwili wa huyu mtu ulikuwa umeoza, unanuka, na sehemu nyingine zilikuwa zinatoa wadudu. Huyu mtu alikuwa akiteseka, lakini cha ajabu sauti yake ilikuwa inasikika vyema, na mara kwa mara alikuwa akikatiza mazungumzo kwa maumivu.
‘Kuna watoto wawili, hawa ni watoto wa marehemu kaka yangu, niliwadhulumu haki yao, baba yao alikuwa kaka yangu tumbo moja, yeye kwasababu alikuwa kipenzi cha baba alimiliki eneo kubwa likiwemo hilo eneo ambalo wazazi wetu waliishi na ndipo tulipokulia. Wazazi wetu walilirithi eneo hilo toka kwa wazee wao, na eneo hilo kimila haliuzwi, ni kwa mujibu wa mila zetu na taratibu zetu. Mimi nikawa na wivu na kaka yangu huyo, nikatafuta mbinu na kummaliza kaka yangu kwa uchawi, na baadaye mke wake nikataka kummaliza pia kwa uchawi, lakini alikuwa mcha mungu wa hali ya juu, alishituka akakimbia na hawo watoto wawili.
Lakini inavyoonekana ule uchawi niliomlogezea ukawa umemwingia huyo mwanamama kidogo , kwani wakiwa wanatangatanga kuombaomba mitaani, huyo mama alishikwa na shinikizo la damu akafariki na kuwaacha watoto hawo bila mtu wa kuwahudumia…’ akakohoa na kitu kama damu zikawa zinatoka mdomonim, docta akachukua sehemu ya kitambaa kilichokuwa pale kitandani akampangusa
‘Watoto hawo walikuwa bado wadogo sana, nahisi baadaye alitokea msamaria mwema akawapeleka kituo cha kulelea watoto. Nasiki bado wapo huko, mimi sijawahi kuwaona tangu waondoke hapa. Sasa hali ilivyo, sitakufa mpaka watoto hawo wapate haki yao. Nasikia umesalimu amri umeamua kuliuza hilo eneo, na aliyenunua ni mjomba wa hawo watoto akishirikiana na mimi, ilibidi niuze maeneoo yangu yote, ili kupata hizo pesa, na sasa nashukuru sana kuwa hatimaye eneo hilo litarudi kwa wenyewe., Lakini tatizo limezuka kuwa, watoto hawaonekani, mjomba mtu alinijia hivi karibuni na kuniambia hawapo kwenye kituo walipokuwa wakilelewa. Na amejaribu vituo vyote anavyovijua hawapo, watoto hawaonekani , sasa nifanyeje. Wewe najua itakuwa rahisi kuwatafuta, naomba sana ili nife kwa amani docta…’ akakohoa sana, halafu akatulia kimya, baadaye akazindukana
‘Chondechode Docta watafute hawo watoto, ili nife kwa amani, nitateseka kwa hali hii mpaka lini…unaona fedheha ninayoipta, sio tu nateseka mwenyewe hata majirani, ndugu wanateseka na harufu mbaya inayotoka kwangu..’ akakohoa kwa muda halafu ikawa kimya. Docta alifikiri kuwa kafa, lakini alipoangalia mapigo ya moyo aliyaona yakiwa bado yanafanya kazi. Akatoka mle ndani haraka na kuingia kwenye gari lake.
Alipofika nyumbani kwa wazee wake ambapo ndipo wanapoishi kwa muda wakati wakiwa wanasubiri kuhamia kwenye nyumba yao nyingine mpya, alimkuta mkewe akiwa na wasiwasi sana. Alimuhadithia mkewe kisa alichokisikia na mkewe akamwambia kituo hicho alichokitaja ndicho alichowahi kuishi kwa mara ya kwanza kabla hajahamia kwenye kituo kingine. Basi docta akamuomba waondoke pamoja hadi kwenye kituo hicho, walipofika wakamkuta mkuu wa kituo hicho na walipoulizia kuhusu hawo watoto, wakaambiwa watoto hawo wamechukuliwa na Mzungu mmoja na huend sasa hivi wapo Marekani.
‘Hiii sasa kali maana kama wapo Merakani wapi …akajaribu kumulizia yule mkuu wa kituo lakini yeye hakujua wapi, kwani hawakuacha maagizo yoyote zaidi ya jina la mfadhili huyo tu. Yeye aliwashauri waende kuulizia balozi za marekani wanaweza kujua anuani ya mtu huyo kwani alikuja na kibali rasmi.
Docta siku hiyohiyo akafuatilia mpaka huko balozi za Marekani, na kweli wakaambia kuwa mfadhili huyu ana vituo vya kuhudumia watoto mayatima kwenye nchi hizi za Afrika Mashariki na kwa ukarimu wake anajulikana sana, na mara kwa mara huja kuwachukua baadhi ya watoto kwenda kuwasomesha huko Marekani. Akapewa anuani za huyu Jamaa.
Docta hakupoteza mudaakatuma e-mail, haikujibiwa akaamua kupiga simu, Na jamaa akaipokea na kusema kuwa watoto hawo anao hakatai, lakini kwa maelezo yao wenyewe wamesema hawana ndugu yoyote na kwahiyo hawezi kuthibitisha hiyo habari kuwa wana baba mdogo na anawahitaji, inawezekana ni mbinu za kuwarubuni hawo watoto wasipate elimu yao ya baadaye, na akakata simu.
Baadaye Docta akaona ajitambulishe kama Docta ili ayazungumze kinamana nyingine, na kweli hiyo ilisaidia kwani huyo anayefadhili hawo watoto ni Docta pia na zaidi ya hayo alikuwa miongoni mwa madocta waliomaliza chuo alichosoma Docta wangu , Ingawaje Docta wangu hakumkukuta, alikuwa mbele yake mwaka mmoja! Wakafahamiana na hatimaye wakakubalioana kuwa watoto hawo watafanyiwa utaratibu wa kurudi nyumbani haraka, lakini kwa msharti kuwa wakimaliza hiyo shida warudishwe huko Marekani.
Baada ya tano wale watoto waliingia Tanzania, na Docta alihakikisha kuwa anakwenda kuwapokea mwenyewe uwanja wa ndege. Alikutana nao hapo uwanjani na kuwachukua moja kwa moja kwa huyo mzee, walifika na kukuta hali ni ile ile na kulikuwa na kundi la watu, wakiwa wanapambana na askari wa mgambo, inaonekana kulikuwa na tatizo kubwa kiasi kwamba, askari waliitwa kusaidia, walipouliza wakaambiwa kuwa watu wamehamaki na wanataka kuchukua hatua mikononi mwao, kwani wanasema harufu mbaya inawakera na makelele ya huyo mgonjwa yalikuwa yamezidi, kwani kila mara akizundukana hupiga makelele yanayo wasumbua majirani.
‘Nawaombeni mvute subira, kwani huenda jambo hili limefikia ukomo, hawa watoto walikuwa watoto wa marehemu kaka yake, sasa wamekuja na tunahisi huyo mgonjwa akiwaona itafikia hitimisho la mateso yake…’ Akasema mzee mmoja kuwatuliza watu, na akawaendea wale watoto ambao walikuwa bado hawajaelewa vizuri nini kinatakiwa kufanyika.
Walipoelezwa kuhusiana na nini wakifanye, wale watoto waligoma kabisa, wao wakasema waliambiwa kuwa wanakua kukabidhiwa eneo laoo na nyumba yao, sio kumuona huyo mzee, wanasema mzee huyo alitoa agizo kuwa wasionane naye, wakija atawaua kama alivyowauwa wazazii wao, kwahiyo waoo hawakubali kabisa kuonana na huyo mzee.
Walibembelezwa sana na wananchi mbalimbali na baadaye wakakubali, lakini kila walipojaribu kuihgia mle ndani,wakawa wanatapika sana kutokana na ile harufu mbaya, na kila juhudii zilizofanyika ikawa haiwezekanai, na mwishowe wengine wakashauri huyo mtu atolewe nje, lakini hata alipotolewa , watoto wale walishindwa kabisa kumkaribia, kwani walikuwa wakitapika kama maji, na ikaonekana wataathirika,
‘Yule mtaalamu wa huyu mgonjwa akasema kinachotakiwa ni kauli yao tu kuwa wamemsamehe, basi ikisikiwa na huyo mgonjwa inaweza ikasaidia, basi kwa mbali wale watoto wakasema kwa sauti kuwa wamemsamehe, na wanamuombea apone, kwani damu ni nzito kuliko maji.
Kauli hii ilipofika masikioni kwa yule mgonjwa, alianza kama kutetemeka ,alitetemeka hadi kile kitanda kakageula na kimdosha yule mgonjwa chini. Hafau akatoa kilio kikali sana cha maumivu akilalamika kuwa watu wanamchoma visu wengine wanamuunguza kwa moto…alendelea kulalamika hivyo kwa muda halafu baadaye akaanza kukoroma na hatimaye akakaa kimya, na walipomwangalia wakakuta kesha kata roho…lakini kabla hawajafanya lolote mara uvumi wa upepo ukasikika ukija kama kimbunga, michanga mavumbi matakataka yakawa yanapeperushwa kila mahala na kuwafanya watu wakimbie, na kuliacha lile eneo peke yake
Haukupita muda, mara ndege wakubwa kama kunguru wakaja kwa wingi na kuuvamia ule mwili walianza kuudonoa huku wanagombea minofu ya nyama waliyokuwa wakiitoa kwenye mwili wa yule marehemu, na hali ile ilichukua nusu saa tu, kilichobakia kilikuwa ni mifupa mitupu, watu wakawa wameshikwa na butwaa. ..
Baadaye watu wakafika kwenye mabaki ya ule mwili wakayaweka vizuri na kwenda kuyazika. Na huko makaburini wakakutana na matukio ya ajabu, mara nyuki, mara nyoka, na hata kaburi lile, wakati wanalifukia, kulitokea nyoka wengi, ikabidi watu wafukie kiharakaharaka na kukimbia.
Baadaye kikao kikafanyika, wazee na mjomba wa wale watoto akawakabidhi watoto wale eneo lao, na nyumba yao , pamoja na hati zote za kumiliki. Aliwaasa wale watoto kuwa kwa vyovyote iwavyo wasije wakauza hilo eneo, kwani ni maagizo toka vizazi na vizazi. Wale watoto walifurahi sana, na baadaye wakawa wanalia wakiwakumbuka wazazi wao hasa mama yao aliyekufa akiwa anawatafutia chakula cha kuomba mitaani. Na wakati yanaendelea hayo humo ndani ya nyumba yenye vioja, mara nye mvua ikanyesha kubwa sana, na watu wakasema ni ishara yaa Baraka.
‘Docta wangu, tunashukuru sana kwa juhudi zako, na tunaomba uwe aribu sana na hawa watoto, kama wanakwenda huko Marekani, uhakikishe wanakuwa kwenye mikono ya usalama, nah ii nyumba unaijua zaidi tunakuomba uwatafutie mtu wa kuaminika wa kuikodi hadi watakaporudi. Akasema mjomba mtu, yeye alisema anashughuli nyingi za kusafiri kwahiyoo hatakuwa na muda wa kufuatilia hayo maswala. Docta wangu akachukua hilo jukumu, na sasa watoto wapo Mareakni wanasoma.
Maneno ya kumalizia: Dhuluma haidumu, ikudumu inaangamiza. Na tusiwadhulumu mayatima, kwani Mungu anaweza kuleta miujiza ya kuilinda haki yao. Majumba mengi yametelekezwa kwasababu labda haki haikutendeka, kuna dhuluma zimepita ndani yake, …
MWISHO
Ni mimi: emu-three
16 comments :
mmh..nimemaliza kusoma ikawa kama nimetua mzigo ..huu mkasa umenigusa sana...nimekosa la kusema zaidi.
asante m3 kwa kweli hadithi hii uinafundisha na anaonya. nimesoma hadithi zako nyingi kln hii kiboko mungu akubariki
what a story to tell.Nimeipenda kwani inamafunzo.
Nilitamani kama isiishe vile....kazi nzuri EMU-3
Ni kweli, dhuluma haidumu
aaaah yaani I can't believe this is the end!!! kwa kweli M3 lazima nikupongeze kwa jinsi ulivyoendesha kisa hiki na kilikuwa kizuri saaaaana sana na pia ujumbe wake ni wa kuelemisha. You are so talented! Haya mimi nipo for the next one kama kawa! Much love :-)
Wanasema kumalizika kwa jambo moja ni kupata nafasi ya jambo jingine, nami naiandaa kuweka kisa chetu, vipo baadhi lakini ni heri kuanza kile kilichotangulia. Nashukuruni sana kuwa pamoja nami, na kunipa moyo, kunisaidia kukamilisha na kusema lolote, kwani ukisema lolote angalau najua kuwa nipo na watu pembeni!
Mama wawili, nakukaribisha sana, naona kama mara yako ya kwanza kusema lolote, karibu sana, na majirani zangu wa kila siku nashukuruni sana, TUPO PAMOJA DAIMA, AU VIPI?
Heri ya mwaka mpya M3 na wapenzi watoe wa visa vyake, Nashukuru nimekuta bado story ipo na nimeanzia nilipoishia na kupata mtiririko mzuri. Mmmmmh! Doctor wewe mwanaume wa kweli best hukati tamaa wala hukatishwi tamaa!!!!!!!. Story ilikuwa babu kubwa kwa kweli. ngoja tunaze nani kama mama.
Kisa hiki ni fundisho kubwa sana, kimeelezea kuwa chuki ni mbaya na si haki kumdhulumu mtu amdhumuye mti atalipwa hapa hapa duniani. Hakika M3 nakuaminia kwa kuiweka hiki kisa murwaaa kabisa ingwa kilikuwa kinatisha lakini pia kilikuwa kinasisimua. Endelee hivyo hivyo...kazi nzuri.
wow at last!! hongera m3 yani imekuwa njema kwisha kwa hitimisho jema kumbe chokochoko zote ni dhuluma na kijicho tena cha ndugu wa damu.. kwa wenye mali na watt ni vzr kugawa mali katika uwiano ili kucje tokea tafaruku kama hii iliyosumbua hata wasiohusika. Dr na maua hongereni saana napenda love story yenu mbarikiwe.
M3 nimepata mengi kutoka kwenye mkasa huu mungu akuzidishie afya na nguvu za kutuwekea mengine
M3 ,mimi nilitaka na huyo mama wa dr wa kambo limpate la kumpata kwa jinsi alivyomtesa Dr wakati mdogo lakini ndio kwanza linafaidi matunda ya Dr.
Lakini story hii ina mafunzo mengi na ina farijisha,kwangu mimi naona kama na mimi matatizo ninayoyapata yaliyosababishwa na watu ambao nawajua iko siku MUNGU atanionyeshea na atanirudishia HAPPINESS yangu.Nipatie contact za Dr nami anipiganie haki zangu...lol,
Ubarikiwe sana M3,nami naona wewe nikuite Dr M3.
Kashy pole sana kama na wewe ni mmoja waliowahi kupata matizo yanayofanana na kisa hiki, lakini usikate tamaa. Ipo siku utapata furaha na faraja!
Na pili akutendaye ubaya usimlipe kwa ubaya na wala usimuombee ubaya kwani `kila jambo hutokea ili iwe sababu' . Wapo walioteseka, na mateso yale ndiyo yaliyowafanya wafanye bidii na kufikia hatua waliofikia, kama isingekuwa mateso wangebweteka...kwahiyo mshukuru mungu na muombea mbaya wako mungu amfunulie aachane na huo ubaya...
Nakushukuruni kuwa mumekuwa wapenzi wa blog hii, karibu sana.
Jamaniiiii M3. Nimeipenda sana hii story, imenifindisha mengi sana.
Nasikitika sana kwani nilikuwa bize na funga mwaka kama ujuavyo na wale jamaa, wakaguzi wa mahesabu. Ndio leo angalau napata muda.
Niliku-miss mno. Nilishindwa hata kusoma hii story.
Thx m3. UPO JUU ZAID. MUNGU AKUBARIKI ZAIDI
BN
Jamani nilikua mkoa kama 2wks nimeona kama mwaka maana nilikuwa busy kiasi kwamba sikuweza hata kuchungulia huku lakini kila siku nilikuwa nawaza hii story jamani nimerudi leo mchana nimekimbilia kwenye hadithi yaani nimejiona kama nimetua bonge la mzigo baada ya kusoma hitimisho. M3 ur so talented Mungu kakupa kipaji kikubwa sana endelea kutupa mafundisho.Stay blessed always M3!
Zulu
Karibu tena Zulu, mambo yanaendelea na kama umemaliza hicho kisa, sogea mbele uendelee na kisa kingine cha NANI KAMA MAMA
Post a Comment