Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, December 13, 2010
Aisifuye mvua imemnyea-9
**********Je kuna nini , hebu tujumuike tena kwenye kisa hiki anachotusimulia docta*********
*******
Nilitizama kwa tahadhari, na upande ule kulikuwa na jokofu na meza kubwa iliyojazwa vyombo vya kusafisha, sikuona kitu kingine, nikamwangalia tena yule msichana, akanyosha kidole kwa chini. Nikageuka haraka kutizama chini, niliona khanga ya mama imejitokeza, nikasogea pale na hapo nilimuona mama kalala chini kimya. Nikamwangalia yule msichana kujua nini kimetokea yeye akatikisa kichwa, na kuonyesha mikono kuwa hajui kitu.Alikuwa kiongea kama bubu, kitu ambacho kilitaka kunipandisha hasira, lakini nikaona haina haja, nikamsogelea mama pale chini, na kumchunguza mapigo ya moyo, nikaona presha yake imeshuka sana. Nikamfanyia huduma ya kwanza, na wakati naendeela naye baba akatokea.
‘Kumetokea nini..’ akauliza baba ambaye alikuja mara moja pale nilipokuwa nikimuhudumia mama, sikuwa na cha kumjibu wakati huo kwani nilikuwa kazini, na bahati nzuri yule binti akafungua mdomo na kumjibu baba.
‘Mimi nilikuwa naosha vyombo, upande ule, na mama alikuwa huku akivifuta maji na kuvipanga kwenye hili kabati, mara mama akaanza kutetemeka kwa nguvu na kupiga ukulele, na mara akadondoka chini, name nikapiga kelele kuomba msaada, na ndipo mwenye nyumba akaja…’ akasema yule msichana.
Baba akamkageukia mkewe, akanitizama kuwa kuna lolote baya, nikamwambia avute subira kwanza, kwani kwa hali ilivyo mpaka azindukane, lakini mapigo ya moyo yapo kwa mbali sana. Nikajaribu kumuuliza kuwa mama ana tatizo la shinikizo la moyo, akasema mkewe hana tatizo la shinikizo la damu, kama nikuanza lianze leo, nikawaita mafundi tukasaidiana kumpeleka sehemu nzuri, ambapo niliweza kumfanyia matibabau yanayofaa. Alizindika na kutoa jicho kama vile mtu aliyeona kitu cha kuogofya.
‘Vipi mama imekuwaje..’ nikmuuliza. Yeye kabla hajajibu akainuka na kuanza kukimbia, tukamshika kumtuliza, lakini akawa hashikiki, anatetemeka kwa nguvu na kujipigapiga, na mara sauti ile ile niliyoisikia kwa Maua ikamtokea mdomoni. Alianza kunguruma kama Simba, na kujipigapiga kifuani, akisema, leo nina hamu ya damu , leo ninataka niwaonyeshe kuwa mimi ni nani…nimewaambia hapa ni milki yangu mnakuja hapa kufanya nini…hili ni eneo lake la urithi kwanini hatutaki kuelewa..!
Baba alipoaana hivyo akamfuata mkewe, na kumshika kichwani akijaribu kumuombea, mama akauona ule mkono akausukumia mbali ule mkono wake na baba aliporudia mara ya pili kuuweka ule mkono kichwani mwa mama, mama akamgeukia na kumkaba baba kooni kwa mkono mmoja, alimshikilia kwa nguvu kooni na baba akawa anaomba msaada huku anajaribu kuuondoa ule mkono bila mafanikioa.
Fundi ambaye alikuwa karibu akataka kusaidia, akasukumwa kwa mkono na mama kwa mkono ule wa pili huku mkono mwingine ukiwa umemkaba baba, na fundi mwingine akachukua kipande cha mbao na kuupiga ule mkono, na ile mbao ikavunjika vipende viwili. Mama akanguruma kama Simba, akageuka kule alipo yule fundi, akacheka , na akamtupia baba pembeni na kumfuta yule fundi aliyempiga kwa mbao, yule fundi kuona vile akatimua mbio…na mama akacheka kicheko kikubwa cha sauti ya kiume, akitamba kuwa anayetaka usalama atokomee mbali, kwani yeye anahamu ya damu ya mtu.
Akamuelekea pale alipolala baba, wakati huo baba kshikilia shingoni, akiugulia , ikionyesha kuwa mkabo ule ulimuumiza , …mimi kwa muda ule nilikuwa nimeshikilia kamera ya video yangu nikichukua matukio hayo, nikaigesha pembeni, ili nije kutoa msaada, huku najiiuliza kwanini anamsakama mume wake tu…nikaona ni lazima nifanye kitu haraka, isije ikaleta balaa jingine, nikakumbuka ile dawa aliyotupa yule mtaalamu wa miti shamba na maruhani, nikaisogelea taratatibu.
Mama akaniona, akajua kuna kitu nataka kukichukua, akanigeukia kunifuta, huku anasema mimi naonyesha kiburi ndani ya miliki yake, atahakikiahs siingii tena mle ndani, akawa ananiia huku mimi nafungua mkoba wangu kwa haraka, na bahati nzuri ile dawa iliyopo kwenye kichupa kidogo ilikuwa juu, juu. Yalikuwa mafuta yakunukia,..nilipokifungua tu kile kichupa kwasababu ya harufu yake kuwa kali ikawa imesikika na kila mtu mle ndani na mara mama akasimama kama mtu aliyepigwa ganzi. Sikupoteza muda nikachukua kidogo kwenye kidole nikamrushia matone mama, kwani alikuwa keshanikaribia.
Akapiga ukulele na kudondoka chini, na akaanza kutetemeka, kwa nguvu, halafu akalala chini kimya. Nikamkimbilia baba kumwangalia kama kaumia , akasema hajaumia sana ilikuwa mshituko tu. Akaniambia niende kumwangali mama kama yupo salama, nikainuka na kumwendea mama, na wakati huo wale mafundi wengine walishafika kutoa msaada.Tukamwiina mama na kumweka vizuri na baadaye akainuka na kushangaa, kuwa kumetokea nini!
‘Kumetoe nini, mbona nipo hapa…sinilikuwa jikoni mimi..?’ akauliza
‘Tulia, kwanza tutakuhadithia baadaye,…’ baba akamwambia mke wake. Na tulipohakikisha kuwa hali yake imerudi kama zamani, baba akashauri kuwa tule chakula kwanza, kani chakula ndicho kitakachorejesha nguvu hata ikitokea jingine tuwe tuna nguvu ya kupambana nalo.
‘Mwanangu unaona, hapa hapana ema, maana haya sasa yanaonyesha kuwa kuna kitu humu ndani…’ akasema baba na mimi nikawa kimya.
Niliwaza jinsi gani ya kuwatuliza hawa wazazi, kwani mimi bado sikuwa na wasiwasi nikijua ni vitisho vya kupita. Kwani kwa vile kuna muda kidogo nyumba hii ilikaa peke yake bila mtu, labda kuna watu waliifanya makao yao, hasa hawo wanaoitwa wanga, ilikuwa dhana ambayo hgaiingii akilini, lakini nikasema huenda mama alikuwa na matatizo mengine, ambayo wao walikuwa hawajui, yapo malaria yanaweza yakamchanganya mtu, inabidi pia nikachukue vipimo vyake. Lakini kama ni madudu kama wanavyoongea watu mbona yanawaingia wanawake tu?
‘Wazazi wangu naona tumalize kula tuondoke, haya mambo ya nyumba hii niachieni mwenyewe, kama kuna tatizo nitalimaliza, hiyo isiwatie shaka. Mawazoni nilimkumbuka mtaalaamu aliyenipa ile dawa, na kwa vile niliiona imefanya maajabu nikaona nimpigie simu. Akaipokea na nilipojieleza akanikumbuka, na kusema eti alikuwa akiniona kwenye mitambo yake, na sasa kaiweka tayari kutulinda tusiwe na wasiwasi!
‘Itabidi tupange siku tuje pamoja hapo, kwani hapo ni nyumba ya jamaa, wamejazana hapo, hawo wadudu bila kuwaondoa mtapata shida…tukutane kesho kutwa ili unipeleke hapo, tuangalia la kufanya, hiyo kazi ndogo kwangu, akasema na kukata simu. Nilimkubalia lakini kichwani mwangu sikuamini kuwa kuna kitu humo ndani, mimi niliona kama ni vitu tu vya kutisha watu, kwani kama ni mashetani kwanini yachague wanawake, na cha ajabu ni shetani la kiume, linamwendea mwanamke, mbone lisimuingie mwanaume! Nikajisema mwenyewe kichwni `hayo ni mazingaumbwe tu..’
Tulirudi nyumbani na nilipohakikisha kuwa mama hana tatizo lolote, nikaona nitoke kidogo na nikampigia rafiki yangu wa Sinza kuwa nakuja kumtembelea , akaniambia atashukuru sana kwani hata yeye alihitaji mtu wa kuongea naye, nikaaga kwenda Sinza, lakini baba akasema ana maongezi na mimi kwanza. Tulikaa naye na mama akaja, inaonekana ni kitu walichokiongea wawili na walitaka kunipa taarifa.
‘Mwanangu, mimi nakushauri, najua umetumia gharama nyingi sana kwenye ile nyumba, nyumba ni nzuri na ipo mahala pazuri, hatukatai, lakini bado unaweza ukaiuza na ukanunua nyumba nyingine nzuri zaidi ya hiyo, sisi tunakushauri uiuze, kasababau yaliyotokea hapo umeyaona mwenyewe, …’ akasema baba.
‘Wazazi wangu mimi nimewaambia kuwa hilo swal la nyumba niachieni mwenyewe, kwanini tuogope vitu kama hivi, unajua haya maswala ya uchawi, mashetani, ni imani tu, na imani kama hizo ni kuzitupilia mbali, mimi nitatafuta njia ya kuliondoa kama ni imani hizo nitawatafuta watu wa imani hizo watapambana na huyo anayejioan kidume…kwangu mimi sioni kuwa kuna kitu cha kushindiakana. Hili ni changamoto kwangu…’ nikawaambia bila wasiwasi.
‘Lakini kama ni imani umejionea mwenyewe madhara yake, sio swala la kuhadithiwa tena, watu wanaongea na mara nyingi tunaoana ni hadithi tu, leo hii wewe mwenyewe limekukuta, nah ii ni mara ya pili, huoni kuwa haya mamabo yapo. Huoni kuwa mvua imekunyeshea mwenyewe, na aisifuye mvua imemnyea, haijakunyea hii…?’ Baba akaongea kwa simanzi kidogo. Niliwaza kwa muda lakini sikuwa na jipya kichwani .
‘Basi kama ni hivyo, tuwatumie hata watu wa dini wafike wapaombee, manake kama ni mashetani ,dawa yake ni maneno ya mungu yatakimbia tu..’ akasema mama.
‘Yote hayo tutayaangalia, lakini mimi nilitaka nimalizane na ukarabati kwanza, halafu nikiwa nipo tayari kuhamia nitafanya yote hayo..’ nikasema huku nikiangalia saa yangu. Nilishazamiria kuhangaika na hili swala, ili nipate kujua haya mambo kiundani, je kuna kitu kama hicho, na kama kipo nini dawa yake, maana mimi ni dakitari na dakitari unatakiwa ujua dawa ya ugonjwa, na sio kuukimbia na ikishindikana unashauri mgonjwa apelekwe kwa mtaalamu mwingine!
Nilionodoka nikiwa nisijawashawishi wazazi wangu kuhusina na swal la nyumba, lakini nilijua kama wazazi lazima watakuwa na wasiwasi kama huo kwa mtoto wao. Nashukuru kuwa mimi sikuwa na wasiwasi wowote kuhusiana na jambo hilo, niliona kama mazingaumbwe ya kutisha watu ili tu wasifanye mambo ya maendeleo.
Nilifika Sinza, jioni jioni na kabla sijakwenda kwa rafiki yangu nikaona nikatize mitaa ili kutizama maeneo huenda nikapata lolote la kuniliwaza akili yangu. Nikaingia mtaa mmoja nikaendesha gari hadi mwisho wake nikageuza gari kuelekea mtaa wa pili. Wakati naendesha nikiwa na nawaza hili na lile, mara mtoto mdogo akakatiza mbele,lilikuwa tendo la kushitukiza saha, na nikakanyaka breki haraka sana na gari likasimama papohapo, lakini yule mtoto alikuwa kama vile analifuata gari kwa mbele akajigonga mbele ya gari.
‘Kaua kagonga, kaua…’ kelele zikazagaa kwa vijana waliokuwa wamasimama, hapo barabarani, na wengine wakaanza kuja kwenye gari langu, nilifunga viyoo haraharaka nikijua mdhara ya watu kama hawa. Lakini wazazi wa yule mtoto waliliona lile tukio wakawatuliza watu kuwa ni kosa la mtoto wao, kwani lile gari lilikuwa likija taratibu na huyu mtoto alichomoka mikononi mwa mama yake akakimbilia barabarani. Na amjeigonga kidogo tu.
Nilifunga gari vizuri nikatoka na kumwangalia yule mtoto, hakuwa kaumia, bali ni mshituko tu. Nikawaambia wale wazazi wa mtoto kuwa , ili tuwe na uhakika tufike hospitali ya karibu ili wamchunguze. Wakambeba na kuingia naye ndani ya gari langu. Nilikuwa mbele kwahiyo wakati wanaingia sikutizama nani na nanii kaingia. Tukaondoka kuelekea hospitali iliyopo karibu.
Tulifiak hospitalini na wazazi wa mtoto wakamtoa mtoto ndani ya gari na kumwingiza kwa dakitari, na mimi nikiwa nawafuatilia nyuma. Niliongea na dakitari mmoja anayehusikak nikajitambulsiha jina langu , akawa kanifahamu na kushukuru kuwa nimefika hospitali kwake.
‘Nimesikia sana sifa zako docta, na nilikuwa na hamu sana ya kukutana na wewe,..’ akasema yule dakitari ambaye walisema ndiye mumiliki wa hicho zahanati.
Akmshughulikia yule mtoto na kusema hakuna tatizo lolote akatoa dawa za maumivu na akashauri kuwa kama kutatokea lolote wamrudishe, mimi nikalipia zile gharama, ingawaje yule dakitari alikataa kata kata nisilipe chochote, nikamwambia asijlai kwani yeye dawa kanunua , hajazipata bure, kwahiyo mimi nachangia gharama, sio vibaya.
Nikawarudisha nyumbani na tulipofika kwenye geti la hiyo nyumba, mama wa yule mtoto akamuita binti yake, sijui ni mdogo wake au ni mfanyakazi wake wa nyumbani, alitumia neno `nanihii..’
‘Nanihii tufungulie mlango..’ akaita
Na mara mlango wa geti ukafunguliwa na msichana mmoja akaja akiwa na shauku kumuona mtoto wao, kwani walishapata taarifa ya kugongwa na gari. Nafikiri atakuwa mama yake mdogo, au shangazi yake kwani wazazi wale waliniambia wana mtoto mmoja tu. Yule msichana anaweza akawa kamaliza shule au kama bado anasoma, atakuwa sekondari , alikuwa mrembo, na alinivutia sana, maumbile, sura yake na alivyovaa, alionekana mtoto wa heshima. Nilijisemea moyoni, kama hana tatio jingine na kama kasoma vyema, anaweza kunifaa kama mke, lakini siwezi kuhakiki haraka haraka hivyo.
Nakamtupia jicho la wizi kumwangalia wakati kambeba mtoto wao, na baadaye akanigeukia kunisalimu nikanyosha mkono kusalimiana naye, naye akaninyosha wakwake huku anatabasamu halafu akainama chini kwa aibu. Lile tabasamu lake liliniacha hoi, mwanya na vitobo vya mashavuni vilimpamba binti huyu na kuwa mrembo wa aina yake. Nikamsalimia huku namuulizia jina akasema anaitwa Rose, na anasoma kidato cha sita ….
‘Mhhh, msomi wewe, safi sana…’ nikaguna.
Mara akaitwa na ndugu zake akaambiwa anikaribishe ndani, na akanikaribisha lakini mimi nikawaambia kuwa sitakaa kwani nina miadi ya kukutana na mtu, kwahiyo ni bora niondoke, ili asije akawa na wasiwasi. Na wakati naongea hayo niligundua kuwa yule msichana alikuwa akinitupia jicho la wizi, sijui kwakuwa mimi ndiye niliyemgonga mtoto wao, na alikuwa akiniweka kiichwani kama mhalifu au alikuwa akinitizama kwa hisia kama nilizo kuwa nazo mimi. Nilipomwangalia akageuza shingo haraka kuangalia upende mwingine. Hali hii ya yeye kuniangalia niliigundua mara kwa mara, ikanifanya na mimi niwe na hamu ya kumwangalia mara nyingine, nay eye huwa akiona hivyo anaangalia pembeni.
Nikawa nawaaga, nakuwaambia wasiwe na wasiwasi na nikawapa namba yangu ya simu na kadi yangu ya kazini, kwa wazazi wa yule mtoto kuwa kama litatokea lolote wanifahamishe. Na wao wakashukuru sana kwani kuwa na namaba ya dakitari ni muhimu sana kwao..
Wakati huo wazazi wakawa wameondoka ndani, nikabakia na yule binti ambaye alinisindikiza kwenye gari, nikawa namuulizia masomo gani anayosoma, akasema anachukua masomo ya mchepuo wa sayansi ya `PCB’ akiwa na maana ya ‘Physics,Chemestry na Bilogy’, ambayo kwakweli yalikuwa katika mtizamo, wangu na kumwambia mimi ni dakitari kwahiyo hayo masomo nayapendelea sana, na kama akiwa anahitaji msaada wa taaluma ya dakitari inayoendana namambo hayo anaweza kuniuliza, lakini kwa sasa sina nafasi kwani nina mambo mengi sana.
Akaniomba namba yangu ya simu, nikampa. Na wakati anaiingiza kwenye simu yake mlango mkubwa wa ile nyumba ukafunguliwa, akatoke msichana mwingine, akiwa kabeba kinywaji kwenye gilasi, na akawa anatujia pale tuliposimama karibu na gari langu, nilikuwa nafungua mlango wa gari kuingia ndani ili niondoke, nikajikuta nimeuachia, na kubakia kumkodolea mcho yule msichana, na hata simu niliyokuwa nayo mkononi mwangu ikanidondoka, oh……..
Docto kazinguliwa na nini, ni urembo wa huyo binti mpya au kuna nini cha zaidi...tuendelee kuwemo!
Ni mimi: emu-three
4 comments :
Dawa ya moto maji doc kamuona maua wake aliekuwa akimtafuta!! Mapenzi bwana raha sana ukipata umpendae nae akarudisha pendo lako!! AAAAh Doc hata wewe una moyo bana haijalishi una hadhi gani kijamii.. m3 lete uhondo natamani ungetoa na sehemu ya kumi mchana lol
Kweli ndo Pamel ndo ujue kwenye mapenzi hakuna cheo, hata kama unanyota 20 begani ikifika kweli love nyota unaweka pembeni unafauta nini roho inapenda. Mapenzi hayachagui as longer mmpendana toka mvunguni mwa mioyo yenu wote. Sasa jamani mbona nami hiyo inanitisha hapa nilipo?????? Ngoja tumsubiri M3 atwambie mwisho wake itakuwaje maana yeye anajua hadi mwisho wake. All the best M3
M3 lete uhondo. Umemuona Maua nini?
Sasa kazi kwako Dr.
Pole sana kwa mikasa Dr.
M3 BIG UP.
BN
DUh! Umekatizia patamu kweli! :-(
Post a Comment