Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, December 2, 2010
Aisifuye mvua imemnyea-4
‘Baba pasporti na viza havionekani..’ nikasema huku machozi yananitoka
‘Wewe acha mzaha, huo, bila hivyo huwezi kusafiri…’ akasema baba na alipoangalia saa muda umebakia mchache sana…
*******Sasa tuendelee na kisa cha dakitari wetu, na je kama alifanikiwa kuuvuka mtihani huo au la******
Nilikata tama kabisa ya safari, nikakaa chini, bila kujali kuwa suti yangu ya safari itachafuka, nikapiga magoti kumuomba mungu anisaidie kwani kama nitakwama, basi ten….wakati tunahangaika, mama alikuwa chumbani kwake kimiya, na hata baba alipomuuliza kuwa aliviona hivyo vitu hakujibu kwa majibu mazuri
‘Umuulize yeye mwenyewe kaweka wapi, unaniuliza mimi…’ aakibu kwa hasira.
Baba aliniangalia kwa Huruma, na alishindwa afanye nini, akachukua simu akawa anatafuta namba , sijui alitaka kumpigia nani, na mara mdogo, wangu mtoto wa huyu mama wa mwisho akaja mbio, mbio…
‘Baba kitabu cha safari cha kaka hiki hapa, mama alikiweka kwenye begi lako…’ ilikuwa sauti ya mtoto huyu mdogo wa mama yangu, sikuamini macho yangu, nikaangalaia saa na baba naye akafanya hivyo, hivyo, na pale akatafuta namba nyingine kwenye simu yake, akaja rafiki yake na pikipiki,anaishi nyumba ya jirani, tukapanda wawili kwenye pikipiki moja. Mwenye pikipiki alijua kazi yake, kwani tulikuwa kama tunapaa.
Njiani hatukuongea kitu, mimi nilikuwa nawaza safari, hata lile wazo lakufikiria zaidi kuwa nani alikuwa kaichukua viamabatishi vyangu vya safari sikuwa nayo tena. Nilikuwa namuomba mungu tufike uwanjani kabla hatujachelewa.
‘Tutawahi tu, msiwe na wasiwasi,…’ akasema dereva wetu wa bodaboda! Na kweli tulifika uwanjani bado dakika chache tu. Nikaangana na baba yangu akanitakia masomo mema, na kuniambia nisijali yote yaliyotokea, nione tu kama sehemu ya mafanikio katika maisha. Nilimshukuru, na kumshukuru dereva wetu, na hapo ikawa mwanzo wa maisha mengine mapya!
Na kweli nilipofika Ulaya, nikawa na mtizamo mpya, wa maisha yangu mapya, kwani nilipokuwa huko masomoni, walimu walinipenda sana kwa ajili ya kipaji nilicho nacho kwenye masomo, na wakasema watanidhamini kuendelea zaidi, kwahiyo nilipita masomo ya sekondari nikaingia chuo kikuu huko huko nje, na sikupenda kabisa kurudi likizo. Ingawaje kwakweli nilipakumbuka sana, hasa zile kazi za nyumbani na wadogo zangu!
Nilisoma huko nje na hapohapo nafanya kibarua hapa na pale, lengo langu ni kudunduliza nipate pesa za kutosha, nikirudi nyumbani ninunue nyumba yangu na kuwa na maisha yangu bila ya kuwa karibu na wazazi wangu hasa mama. Na hili nililifanya kwa malengo, kila nipatacho nusu kwa malengo ya baadaye nusu kwa ajili ya kujikimu kimaisha.
Wakati tupo chuoni, tulisikia kisa cha majengo yaliyohamwa huko nje, majengo haya yalikuwa karibu na chuo nilichokuwa nikisoma, na wanafunzi wengi wanaogopa kabisa kuyafikia, kutokana na visa vyake, wanasema kuna mizimu au wenyewe huita `ghosts’. Na waliamua kabisa kuweka walinzi wasisogelee eneo hilo, baada ya watu kuingia humo na kupata majeraha au kuchanganyikiwa kusiko na sababu yoyote.
Sisi katika moja ya vipindi vyetu tukaomba kwenda kupatembelea, na kibali kikatayarishwa, ila tulipewa muda mfupi ili kusije kukatokea madhara. Siku hiyo tulijiandaa kwelikweli na dhana za kujilinda na kila mmoja akijipa moyo kuwa haogopi na hizo fikira. Na wengine walibeba vitabu vya dini, ilimradi kila mmoja alikuwa na silaha anayoiamini. Imani ni kitu cha ajabu sana, na hasa zikihusisha mambo ya uchawi na mashetani!
Tulifika jioni, kwani maajabu hayo huwezi kuyapata mchana, zaidi ni jioni au usiku. Tukaingia eneo lililotayarishwa ambalo walihisi kuna usalama. Hapo tuliambiwa tusiingie maeneo yenye magorofa, kwani kuna watu walipanda wakajikuta wanaruka, na kuvunjika mikono, wengine miguu. Tukaambiwa pia, tunapokwenda kujisaidia twende wawiliwawili, kwani kunaweza kukatokea kitu kwa mmoa, mwingine awe tayari kutoa msaada. Hapo tukaanza kuingiwa na wasiwasi, kuwa kumbe mambo hayo ni kweli
Kwa ubishi wetu hatukujali, kila mmoja alijipa moyo kuwa hizo ni hadithi tu. Kutoka huko chuoni, tulikuja na mbasi hadi hatua chache , na mabasi yakaondoka, ili yaje yatufuate baadaye. Katika kutembea hadi kwenyehaya majengo, tulipata mshangao wa kwanza, kuwa sehemu ilikuwa ikionekana karibu, lakini tulitembea hadi kuchoka.Tulipofika kwasababu ya kutembea huko kwa miguu, wengi walikuwa wamechoka, na wengine walihitaji maji, angalau ya kunawa, kwani maji ya kunywa tulibeba wenyewe.
‘Jamani njooni huku, muone’ mara sauti ya mwenzetu mmoa akiwa chooni ikaita, tulipofika hatukuona kitu, yeye anadai aliona mkono wenye damu ukitokea kwenye tundu la choo, na akijaribu kuondoka hupotea, lakini akitaka kujisaidia mkono huo hutokea tena. Mwanzoni lifikiria ni ule uwoga wa akili, akawa hajali, lakini ulipotokea mara tatu, akaogopa.
Basi mmojawapo akataka kujisaidia, ili ahakikishe. Ile anainama tu,Maji yakaruka kama bomba kubwa lililopasuka, na maji machafu, yanayonuka , na yenye mchanagnyiko wa damu, yakaturukia, na yalikwa yakiwasha, kila mmoa aliyeingiwa nayo aliishia kujikuna! Wkati tunahangaika kujifutafuta na kujikuna huku na kule, marai, mlango ukafunguka kwa kasi, na upepo kama kimbunga ukawa unaingia ndani kwa kasi kubwa sana, kiasi kwamba ilibidi tujishikilie ukutani ili tusigongane. Wazo likatujia kuufunga ule mlango, lakini kwa vipi na upepo unakuja kutokea mlangoni!
Tulishikana na kujivuta kuelekea mlangoni, lakini ilikuwa kazi bure, kwani upepo ule ulikuwa ukija na vumbi, kwahiyo macho yalikuwa yakipata shida. Tukawa tunaita walinzi waje kwa nje watusaidie kufunga mlango!
Ilichukua dakika tatu tu, sote tulikuwa hoi, na ghafla ukanyamaza, na mara zikatokea sauti kama za ndege, au panya! Miongoni Wengine kuona vile wakatoka mbio kuelekea chumba tulichoambiwa ni salama, wabishi tukabakia. Tukiwa tumeshika fimbo kupambana na hao ndege au panya, haikuchukua muda kweli wakatokea panya wengi wa ajabu, inaonekana walikuwa na njaa ya muda mrefu, wakawa wanatuandama, ikawa kukimbizana humo ndani , mwishowe tukaona hapo hapan usalama tukakimbia nje!
Mimi na wenzangu watatu tukasema haiwezekani, ngoja tukakague nyumba sehemu nyingine. Tuliingia, chumba kimoja kilikuwa na giza, taa ukiwasha ukutani haziwaki, tukawa tunatumia tochi, ajabu kila tukisogea tunasikiwa watu wanatugonga kichwani kwa vidole. Ikawa tunafikiria ni sisi wenywe tunachezeana mchezo huo. Lakini tuligundua kuwa sio sisi, kuna vitu hatuvioni vinatugonga, na tulipofika ndani ya chumba, mara kukazuka sauti ya vyura, ni sauti ya kutisha, ambayo inaumiza masikiao, …tulijaribu kuziba masikio kwa vidole, lakini sauti ilikuwa haivumiliki, tukaona tutoke tu.
Tukarudi chuoni, mimi na wale wenzangu watatu tuliotoka Afrika tukaamua turudi usiku tuone kuna nini cha ajabu humo. Ni vitu gani vinaishi humo, kama ni mizimu ikoje. Unajua unapokuwa mtafiti, hukubali kushindwa. Tuliingia kwenye lile jingo bila kibali, na tulipofika ndani kulikuwa kimya. Mara tukasikia vitu kama sahani, zinagongana, na watu kama wanakula, na mara nyingine kama sauti za watu wanaongea lugha isiyoeleweka. Tulikuwa na kurunzi kubwa yenye mwanga, tukaiwasha, ukutani kulikwa na maruerue, kama vitu vinapitapita, kama vivuli na wakati mwingine tuliona vitu kama mfuvu ya watu yana meno yametokeza nje, na midomoni kunatoka miulendaulenda.
‘Jamani hapa sasa tumeenda mbali, tukidhurika hapa tutasemaje, tukumbuke sisi ni wageni nchi hii…’ mmoja akasema kwa woga.
‘Tumeshafika hapa turudi , hapana, lazima tuone hiyo mizimu ikoje..’ mmoja akasema kwa ujasiri.
Mara ile kurunzi ikazima ghafla, kiajabu, kurunzi ile kuzima, wakati imejaa chaji, na hata sekunde haikupita, tulisikia vitu vikiingia mle ndani, unasikia sauti ya nyayo za watu, lakini watu huwaoni.
`Yalllah…yalaah,..’ ilikuwa sauti ya kila mmoja akilalamika maumivu, kwani tulikuwa tukipata tukichapwa kwa fimbo, zisizo onekana, kila ukigeuka huku fimbo, na fimbo hizo zilikuwa mgongoni tu. Tukakimbia huku na huko, lakini tulikuwa tukifuatawa kila tulipojaribu kwenda, oooh, tukaona hakukaliki, tulitoka mbio mle ndani na kusahau kuwa tuliingia bila vibali, tukaeleeka mlangoni mwa getini walipo walinzi na fimbo zilikuwa bado zinatuandama! Wale walinzi walipotuona tunatokea mle kwenye jengo wakashangaa, tumepitia wapi bila ya wao kutuona, na walinzi walipotuona tunatoka mbio, na wao, sijui kwasababu ya uwoga, au kutokuamini kuwa sisi ni watu kama wao wakaanza kukimbia…....
*********Kama wanausalama wanakimbia, kuogopa mizimu je wewe, tuendelee kuwepo********
Ni mimi: emu-three
6 comments :
Asante mungu kwa kufanikisha passport yake kupatikana, Mmmmh! bora leo kidogo haihuzunishi maaana du! Sasa nyie watoto mwaenda kichwa kichwa huko kweli si ni kujitakia makubwa?? any way all the best katika utafiti wenu.Yaani nimempenda sana huyo mdogo wake aliyeleta hiyo passport yake.
mh mizimu!
Jamani mbona leo umekatisha sana? Yaani nilikuwa ndio kwanza nakusanya nguvu za kusomea mara ziiiiiiii.
Kwa kweli riziki ya mtu, binadamu hawezi kuzuia. Kama wa YES ni wa YES tu hata iweje.
Dogo katoa siri ya paspoti, sijui baba yake atasemaje?
ROHO MBAYA SI MTAJI JAMANIII!!!!!!!
Sasa Dr. huyo utafiti jamani, unatisha kweli!!!!!!!!! Haya tuone kinachoendelea.
BIG UP M3
BN
Inatisha,inasisimua na pia ni raha sana kusoma visa kama hivi ingwa vinakumbusha mengi yaliyopita. MMMmhhhhh ilikuwa inanoga ....ok nasubiri kwa hamu muendelezo
nakubaliana na Jane kuhusu passport, la sivyo huyo mama wa kambo ningemfanya nini sijui lol! Anyway uuuuuuuuuuuuuh....ghosts!!! Sasa ikifika vitu kama hivi M3 mwenzio sisomi nikiwa peke yangu, sasa sijui nani mwoga zaidi lol
bora alipata passport yake..inasisimua lakini
Post a Comment