Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, December 1, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-3

 
Hutaamini baba akirudi nyumbani, mama anakuwa mtu mwema ajabu, ananifanyia wema wa ajabu, atahakikisha naoga, navaa nguo nzuri, nakula na wao mezani, yaani inakufany ahata usahau machungu ya mchana kutwa, na baba akiniuliza nina tatizo lolote kwa utoto wangu nasema hakuna, na kujilaza miguuni kwa mama huyu. Sijui kwanini nilkuwa mjinga kiasi kile.


Mambo hayo yalizidi mpaka majirani wakaamua kumwambia baba yangu, lakini aliponiuliza nilikatakaa katakata, na kusema mama ni mtu mzuri sana, hanitesi.

****** endelea na sehemu hii ya maisha ya utotoni, na utaona chimbuko la hisia zinavyojijenga kichwani***

Baadaye Mama huyu akajifungua mtoto wake wa kwanza, nilifurahii sana kupata mdogo wangu, lakini furaha yangu ikageuka kuongezewa mzigo, nikawa yaya wa mtoto huyo, nafanya kazi za ndani nafua nguo zake za mtoto. Yeye ikawa kiguu na njia, mara nyingi kama baba hayupo mama huyu alikuwa hakaii nyumbani, sijui huwa anaenda wapi, na cha ajabu akawa hamjali hata mtoto wake!

Mimi ndiye naachiwa kulea mtoto wake wakati mwingine kutokea asubuhii hadi jioni, ninapewa chupa ya kumnyweshea maziwa, na maziwa yakiisha namkorogea mengine wenyewe, Nilifanya yote hayo na baba alikuwa hajui kabisa, kwasababu yeye alikuwa hakai nyumbani, muda mwingi anakuwa safarini, kwa wiki anaweza akaonekana nyumbani mara mbili. Akirudi furaha ndani hutaamini, na anajua kabisa kuna amani, mambo mengine anayoyasikia kwa majirani yeye anayaona ni ya umbeya wa majirani!


`Ukiwasikiliza majirani utakosana na mke wako, mimi sina muda huo…au kuna lolote hapa mke wangu’ utakuta akimuuliza mkewe, na mkewe anamwambia huo ni wivu wa watu kwasababu wanaiona nyumba yao ina amani na upendo


Ilipofikia muda wa mimi kuandikishwa shule, nikawa naamuka asubuhi kufanya kazi zote kabla sijaenda shule, na kuhakiisha nguo za mtoto zimefuliwa,. Na vyombo vimeoshwa. Mama akiamuka anakagua, na ole wangu kipatikane kitu kichafu siku hiyo nitaenda shule nikiwa na uvimbe wa viboko, au masikio yakiwa na vidonda, kwani alikuwa akivuta masikio na kuniningiza juu kwa juu kama kipaka. Na kwa vile nilkuwa na mwili mdogo basi alikuwa akiniinua juu kwa kunivuta masikio , bila hata ya Huruma.


Hayo ni maisha yangu ya utoto ambayo sio rahisi kuyahadithia yote, na pamoja na shida zote hizo bado nikawa nasoma kwa bidii na darasani nikawa nafanya maajabu, nilkuwa nikifaulu kwa maksi za juu, hadi walimu wakapendekeza nivushwe darasa. Na taarifa hizi nilimwambia mama, akanibeza, na kusema toka lini mtoto kama mimi, mtoto wa marehemu kama alivyoniita niwe na akili kama hizo.


'Hawa walimu wa siku hizi bwana, etii ana akili za ajabu, labda za kupiga deki ...' akacheka na kunitupia dekio.


Walimu wakanivusha darasa, na bado nilikuwa naonyesha maajabu! Muda wa kusoma ulikuwa mdogo sana kwangu hasa niwapo nyumbani, lakini kile kidogo nilichofundishwa hukaa kichwani na mara nyingi napenda kujiuliza zaidi na zaidi kwani iwe vile isiwe vile, na kudadisi walimu, na kila nipatapo kitabu nitakisoma kwa bidii. Nikiwa shuleni kulikuwa na chumba cha maabara, nilikuwa nikipata muda namfuata mwalim wa somo la sayansi akiwa humo , nakumuuliza mengi kuhusina na binadamu! Mwalimu huyo alinitabiria kuwa nitakuwa dakitari bingwa!


Maisha yakaendelea hivyo hivyo , baadaye mama akapata ujauzito tena na kujifungua mtoto wa pili na watatu, alipatikana nikiwa najiunga ni kidato cha kwanza, lakini bahati ilivyo mbaya , watoto wa mama huyu wakawa watukutu, hawapendi shule, wakienda shule, wanaishia njiani kucheza. Hutaamini mama akiambiwa tabia ya watoto wake alikuwa akikataa na kuja juu, alidai kama ni mtoto mwenye tabia mbaya nitakuwa mimi, sio watoto wake.


Mimi kwa kuwapenda wadogo zangu tukiwa nyumbani nawafundisha vyema, na wadogo zangu hawa walikuwa wakinipenda sana , na kila mama aliponisakama walikuwa wakinisaidia kunigombolezea kwa mama yao, na hata mwishowe wakamwambia baba jinsi gani mama yao asivyonipenda. Baba hakuamini kabisa...!

‘Nyie vipi, mumezaliwa juzi juzi tu hapa mumeanza kuiga umbea wa majirani, mama yenu huyu kaishi na ndugu yenu miaka yote asimtese aje kumtesa sasa hivi, achene unafiki..’ akasema baba kumtetea mke wake. Masikini baba yangu hakuwahi kunikuta nikiteswa, na kwa ujanja wa mama, baba alimwaminii sana! Mimi sikujali kabisa, nikajionea yote sawa!


Nilifurahi kuwa sekondari niliyofaulu ni ya kulala bweni, kwahiyo mateso yale ya uyaya, na kazi za nyumbani nilizikosa, hadi kipindi cha likizo. Nikirudi likizo natamani niende kuishi kwingine, lakini sikuwa na jinsi, kwetu ni kwetu, nikawa naendelea namateso yale , ingawaje siku baada ya siku yalikuwa yakipungua, kwani mama alikuwa akiniona kuwa nimekuwa, na naweza kumwambia baba unyama wake, lakini sikuwa kabisa na wazo hilo, na sikuwahi hata siku moja kumsemea mama huyo kwa baba, watu, na watoto wake mwenyewe ndio waliomwambia baba kuhusu ubaya wa mama.

Kitu ambacho nilikuwa nashangaaa kuhusu mama huyu, siku za ibada, mama huyu alikuwa akituhimiza kabisa kwenda kufanya ibada, hapo alikuwa hachagui mimi au watoto wake, na hata tukila anatuamrisha kuomba, na yeye mwenyewe alikuwa mstari wa mbele kuhudhuria nyumba za ibada, hata alichaguliwa kuwa mmoja wa mama wa ulezi katika nyumba za ibada, ...niliwaza, kwanini anakuwa na sura mbili, kwanini anajidai kumcha mungu upande mmoja na upande wa pili anakuwa na roho za ukatili, au ni mimi tu ananichukia, na kwanini ananichukia! Kwaninii ananipenda baba akiwepo akiondoka anabadilika!


'Mungu amsamehe hajui alitendalao' nikawa najisemea mwenyewe

Huko sekondari niliendelea kuonyesha miujiza yangu, na darasani nilikuwa nikifaulu vizuri sana. Na bahti nzuri shule ile ilikuwa na mahusiani na shule moja huko Uingereza, na mara kwa mara wanafunzi na walimu toka shule hiyo ya Uingereza huja kukaa nasi kwa muda, na baadaye huteuliwa baadhi ya watoto kwenda huko Uingereza, na sifa ya kuteuliwa ni juhudi yako darasani.


Kwasababu ya akili yangu darasani, walipokuja wageni hao toka shule ya Uingereza, moja kwa moja nikachaguliwa mimi na wenzangu wachache kwenda huko, na mimi nikateuliwa kusoma shule maalumu nchini Uingereza, kwa ushirikiano na wa shule hizi mbili. Ilikuwa furaha sana kwangu, baba na wadogo zangu walifurahi na hata kunifanyia sherehe fupi.Lakini mama akawa na fundo rohoni. Alinisifia kwa vile baab alikuwepo, nilimuona akibinua mdogo wa dharau!

Basi siku ikafika ya kuondoka, vitu vyote vilikuwa tayari, lakinii passpot, ikawa haionekani.

‘Akili, …’ baba akaniita,

Naamu baba, nakua…’ nikasema kwa sauti ya kukata tama.

'Huoni kuwa utachelewa uwanja wa ndege, siunajua tena foleni za magari zilivyo, alikuwa baba akinihimiza ili niwahi hakujua kuwa natafuata paspoti na viza yangu vilikuwa havionekani. Nakumbuka kabisa, niliviweka kwenye begi langu usiku wa jana, lakini sasa havionekani. Nilitafuta kila mahali lakini havikuwepo, na tulivyoambiwa bila hiyo huwezi kusafiri, na tuliambiwa kuja kuwaonyesha wazazi halafu tuirudishe kwa walimu wa msafara, lakini mimi kwa ajili ya ile sherehe ya familia sikuwahi kuvirudisha, na sasa havionekani.

`Baba pasporti na viza havionekani..’ nikasema huku machozi yananitoka

‘Wewe acha mzaha, huo, bila hivyo huwezi kusafiri…’ akasema baba na alipoangalia saa muda umebakia mchache sana…

*********Mhhh, haya bahati hiyo inayeyuka hivihivi, je paspotii na viza zipo wapi, alikuwaje baadaye, tuendelee kuwepo*************

8 comments :

Anonymous said...

Yaani we acha tu M3. Nilikosa raha sana network ilipokuwa inasumbua sikupati.

Leo ndio nasoma stori zote yaani ni babuuu kuubwa. Umebarikiwa ahsante sana kwa ujumbe mzuri.

JAMANI, HIVYO SIJUI NISEMEJE? UNAVYOMFANYIA MTOTO WA MWENZIO ROHO MBAYA KAMA HII UNAFIKIRIA NINI?

HEBU FIKIRI KAMA NDIO WEWE UMEKUFA NA HUKU DUNIANI WATOTO WAKO WANAFANYA HIVYO UNG'EJISIKIAJE?

JAMANI TUBADILIKE, ROHO MBAYA SIO MTAJI. NA RIZIKI YA MTU HUWEZI KUZIBA HATA KWANINI.

KAMA MUNGU KASEMA 'YES' WEWE NI 'YES' TU HATA IWEJE.

POLE SANA DR. YAANI NA HAYO 'MAPEPO' YANAOTAWALA NYUMBA YENU YASHINDWE KTK JINA LA YESU.

UTASHINDA TU DR. MUNGU YUPO NAWE.
*********

M3 WEWE UPO JUU KWANI HIVI VISA NI VYA KWELI NA WATU HUWA WANAFANYIWA NA UPEO WAO WA UTOTO NDIO WANATESEKA SANA.

UBARIKIWE SANA.

BN

elisa said...

jamani..mimi hapo iliishia sina hamu kabisa..Mungu atusaidie tu.

Simon Kitururu said...

Mkuu wewe shusha vitu watu tupo kijiweni !

Jane said...

Mmmmmh! mwenzenu naishia kulia kila ninaposoma story hii. Kazi njema M3, Pole kwa mtoto na hope passport yake itapatikana.

Faith S Hilary said...

Jamani passport yake!!! aaaaaaaaah...

emuthree said...

Jamani msilie, mkilia na mimi mtaniliza nishindwe kuendika. Nashukuru kuwa hisia zimewaingia, na kweli jamaa ni miongoni mwa wale waliopitia maisha ya taabu, na kisa hiki ni maalumu kwa watu kama hao.
Kwa kweli ukidadisi asilimia kubwa kuna watu wamepitia maisha ya mama wa kambo, shangazi nk, na baadhi hawakupata shida, lakini kwa wale waliopata shida, kutokana na shida hizo zimekuwa kama changamoto ya kuwainua kimaisha.
Ndio maana tunasema , kila jambo hutokea ili iwe sababu ya kutokea kitu fulani
Tuendelee kuwepo, ngoja niingie jikoni, kutayarisha makulaji ya leo, ya kisa chetu kinachoendelea.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika watu wana roho mbaya!!!

Anonymous said...

yaani M3, nimejikuta nalia wakati nakisoma hiki kisa, kwasababu kimenikumbusha mateso niliyokuwa nayapata kutoka kwa shangazi yangu wakati nikiwa mdogo, yaani hayana tofauti yoyote na huyu mama wa kambo na nilikuwa nashindwa kumwambia mjomba wangu. sijui kwanini wanawake huwa wakatili kiasi hiki na kutesa viumbe visivyo na hatia hata kidogo.