Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, December 14, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-10

Akaniomba namba yangu ya simu, nikampa. Na wakati anaiingiza kwenye simu yake mlango mkubwa wa ile nyumba ukafunguliwa, akatoke msichana mwingine, akiwa kabeba kinywaji kwenye gilasi, na akawa anatujia pale tuliposimama karibu na gari langu, nilikuwa nafungua mlango wa gari kuingia ndani ili niondoke, nikajikuta nimeuachia, na kubakia kumkodolea mcho yule msichana, na hata simu niliyokuwa nayo mkononi mwangu ikanidondoka, oh……..



                  
            *********Je alikuwa nani na ilikuwaje tusome sehemu inayofuatia************
                                 
                                                 ***************************

`Wewe umechelewesha kinywaji mpaka mgeni anaondoka‘ akasema Rose, kumwambia yule msichana, huku akaniokotea simu yangu, na wakati huohuo akiwa anaonyesha mshangao kwa jinsi nilivyomwangalia yule msichana, na hata kudondosha simu, na usoni nikionyesha uso wa mshangao.

Sikuamini macho yangu, msichana mrembo, sura ya kuvutia, mwili uliojengeka vyema, kutembea kwake ilikuwa kama Tausi au yule binti Mnyenyekevu aliyemuelezea Shabani Robert. Alikuwa na aibu ya haiba, na macho makubwa yenye nyusi ndefu nyeusi na mdomo ambao hauhitaji wanja. Alitembea taratibu sijui ndio mwendo wake au aliogopa kuimwaga ile juisi iliyoakuwa kaibeba kwenye gilasi iliyopo juu ya kisinia kidogo.

Macho yangu yalishindwa kubanduka na hayakuchoka kumtizama, na hili lilimfanya Rose aniangalie, kwa jicho la wivu. Akamgeukia yule msichana anayekuja, ambaye hakuonyesha dalili ya kushituka, na alikuwa anatembea huku nusu kaangilia chini anapokanyaga na nusu anaangalia mbele. Na akamwangalia Rose na kutabasamu. Msichana huyu akitabasamu anazisha ule uzuri wake , na kati ya wale wasichana wenye mpinyo mashavuni na mwanya kwa mbali.

‘Nilikuwa naiandaa, kwani ilikuwa imeganda, …’ akakatisha sauti aliponiangalia na karibu aidondoshe kile kisinia na alipogundu hilo akajifanya hajashituka akashikilia vizuri lile sinia na kusimama, ni mbali kidogo na nilipokuwa nimesimama na Rose.

Macho yangu yalishindwa kubanduka na hayakuchoka kumtizama, na hili lilimfanya Rose aniangalie, halafu amwangalie huyo msichana, na akatabasamu …Rose naye akitabasamu ananiacha hoi, lakini kiumbe kilichotokea sasa hivi kilikuwa na kila sifa ambayo ilinifanya nimuone Rose tofauti. Huyu alipewa sifa zote, huyu aliniweka roho juu, huyu alinifanya nianze kuwapenda wasichana kitu ambacho sikuwa nacho kabla.

Maisha yangu hasa ya shuleni yalikuwa tofauti na wenzangu, wakati wenzangu kama uuavyo shule za sekondari hasa za wavulana peke yao, huwa kuna tabia yakuhangaika kutafauta marafiki wa kike, mimi sikuwa na tabia hiyo, na ilifikia wakati wenzangu waliniona nina kasoro, lakini mimi sikujali, kwani muda huo mawazo yangu yote yalikuwa kwenye masomo tu. Na hamu ya kuwa na mpenzi ilifufuka pale tu baba aliponiambia kuwa kanitafutia mchuma! Hapo nilianza kuingiwa na wazo la kuwa na rafiki wa kike!

‘Jamani ndio wewe, Docta, ndio wewe, mimi nilidhania ni Dokta yule wa nyumba ya jirani, karibu Docta, kunywa kinywaji hiki angalau kidogo, nisikirudishe ndani tafadhali…’ akanishikisha mkono na nikawa sina jinsi nikakipokea na kunywa kwa haraka, bila hata kujua kuwa nimkunywa kama mtu anayekunywa maji, na alikuwa na kiu ya siku nzima, huku namtizama huyu msichana tena na tena.

‘Samahanini sana, naomba uniombee samahani kwa baba na mama, niliondoka bila kuaga, sio kusudi langu, ilitokea ghafla tu nikakutana na mama mwenye nyumba hii, ambaye niliwahi kufanya kazi kwake, na alikuwa anasafari ya haraka na alihitaji mtu wa kuja kukaa na mtoto na muda ule nilikuwa nimekata tamaa, kuwa huenda hamtanihitaji tena, hasa baada ya lile tukio, basi nikaondoka bila kuaga, …’ akawa anaongea kwa Huruma na sauti yake ndogo huku kainama chini.

‘Usijali Maua, pale ni nyumbani kwako, muda wowote ukijisikia njoo, hata hivyo bado nafasi yako ya kusoma ipo, na wiki ijayo masomo yanaanza, kwahiyo ni juu yako, kama utakuja kule nyumbani ni sawa, kama utakaa hapa huku unasoma haina shida..ni wewe tu..’ nikamwambia huku namtizama usoni, na kumrudishia gilasi yake ikiwa nyeupe.

‘Ahsante kwa ku---nikuongeze kinywaji…’ akaiangalia gilasi huku anatabasamu

‘Hapana nshukuru sana, na kinywaji hicho kiboko, kinanikumbusha vinywaji vyako ulivyokuwa ukinitengenezea..’ nikasema akacheka

‘Na wewe Docta, bwana hujaacha utani wako, mimi nina utaalamu gani wa kutengeneza vinywaji vizuri, mtaalamu ni dada Rose…’ akasema na kumshika Rose mkono, ambaye alionyesha kutahayari, na kutokuridhika nay ale yaliyokuwa yakiendelea, lakini baadaye akajifanya hakuna kitu akacheka na kusema hata yeye sio mtaalamu wa kutengeneza juisi anatengeneza kama wengine tu.

‘Ndiye Docto uliyekuwa ukisema..?’ Rose akamuuliza Mua na Maua akajibu kwa kutingisha kichwa huku akiona aibu na akanitizama usoni moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu niwepo pale. Mimi nikabasamu …. Na ile picha ya kunitizama moja kwa moja usoni ikawa imenijaa akilini!,

Nikawaaga na kumwambia Rose, asome kwa bidii kwani masomo hayo yanahitaji kusoma sana, yeye akacheka na kusema, anasoma sana, na atakuwa akinipigia simu kuniomba msaada pale akihitaji, nikamwambia mimi nipo tayari kumsaidia mtu yoyote anayehitaji msaada toka kwangu hasa wa masomo hayo.

Nikaingia ndani ya gari na kumwangalia Maua tena, yeye akatabasamu na kusema atakuja nyumbani kwani mama mwenye nyumba kesharudi na kaja masichana mmoja atakayefanya kazi hapo, ila leo hayupo. Nikamwambia wakati wowote, asiwe na wasiwasi kabisa, kwani pale ni nyumbani kwao, na yakuwa bado tunamuhitaji sana, akashukuru na kusema amefurahi kusikia hivyo.

Nikaondoa gari, nikageuza uso haraka kumtizama Rose, nikamuona kakunja uso , kuonyesha hasira, au kutokupendezewa mimi kuongea na Maua maneno yale, lakini mimi sikujali, nilipoliweka gari sawa nilitizama nyuma nikawaona wote wamesimama wananiangalia ninavyoondoka, nikawapungia mkono na wote wakainua mikono yao kwa pamoja na kunipungia …

Nilifika kwa rafiki yangu ambaye alionekana kukata tama, nikamhadithia yaliyonikuta, akasema kuwa kaipata hiyo taarifa,kwa mjirani, kwani Dar ikitokea ajali itavumishwa utafikiri kuna redio upepo, watu wamevumisha kuwa kuna dakitari kagonga mtoto, alikuwa anazunguka na gari mtaa mmoja baada ya mwingine, … lakini hakujua kuwa ni mimi, nikamwambia yameisha lakini nimeshukuru kutokea kwa tukio hilo kwani limeniletea neema.

‘Wewe badala ya kuomba tukio kama hilo lipitilie mbali wewe unashukuru, ajabu kabisa…’ akasema rafiki yangu.

Nikamkumbusha kuhusu yule msichana niliyemwambia alitoweka nyumbani kwetu, na kutokana na tukio hilo , limenisababishia kumuona huyo binti, kwani nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ndipo anapoishi huyo binti!

‘Ulisema anaitwa nani vile..’ akaniuliza rafiki yangu

‘Anaitwa Maua, na anaishi na rafiki yake anayeitwa Rose, wote wamepata majina yanayoelezea uzuri wao,…mmh, nilishikwa na bumbuwazi…lakini naona mambo sasa yataenda vyema’ nikamwambia rafiki yangu, ambaye likuwa ameduwaa, nilipomtajia jina Maua.

‘Vipi mbona umeduwaa, unamjua Maua…?’ nikamuuliza

‘Maua,aaah, kama ndiye huyo anayeishi nyumba hiyo namfahamu…mtoto yule we acha tu,…’ akakatisha maneno na kunifanya niingiwe na wasiwasi, isije ikawa Maua ana mahusiano na rafiki yangu huyu, ….hapana, haiwezekani.

Kesho yake nilikutana na yule dakitari mtaalamu wa miti shamba tukaongozana naye hadi kwenye nyumba, alikuwa kaja na vijana wake na vifaa vyao, tulipofika kwenye nyumba ile akasema nisingize gari ndani ya nyumba kwanza, akashuka kwanza yeye akazunguka ukuta wa nyumba, halafu akarudi, akawaambia vijana wake washuke, akawaongoza yeye kuingia ndani, na walionekana wanaongoza njia moja, kama vile kuna uchochoro mdogo na hakuna aliyeruhusiwa kupita pembeni. Mimi nikabakia ndani ya gari.

Mara ghafla nikawaona wanakuja mbio, hadi mlangoni, wakaangalia huku na huko, kama vile walikuwa wanafukuzwa na kitu Fulani. Wakatulia, wakapkana kitu kama mafuta, halafu wakaanza kuingia teana kama mwanzo na huku wanapiga manyanga, wakawa kama vile wanapambana na kitu ambacho hatukioni , wanarusha kitu kama unga, huku wanamikuki yao wakichoma huku na kule…mara vijana wawili wakadondoka chini..wengine watatu na huyo jamaa wakawa wanasonga mbele. Video yangu ilikuwa ikinasa tukio lote hilo na ilikuwa kama picha ya aina yake.

Haikuchukua tena muda jamaa wakarudi mbio, na sasa walitoka kabisa nje ya jengo wakawa mbali, na wanaangaliana, na wale vijana wengine wawili wakainuka, walipoinuka tu wakaangali huku na huko, wakatoka mbio. Kwangu mimi niliona kama wanaigiza mchezo Fulani, sikujua kuwa wanapambana na viumbe wasioonekana.

Ilichukua masaa matatu, nimekaa ndani ya gari siruhusiwi kutoka, na wao wanaingia wanatoka mbio, wanakimbia huku na huko, na wakati mwingine wanadondoka chini wanakuwa kama wamepoteza fahamu, na baadaye wanazindukana. Nikaona nimesubiri vya kutosha, kama wanaona vipi mimi niondoke niwaachie maigizo yao, kwani mimi nilikuwa sioni cha muhimu wanachofanya.

Mara nikasikia kilio kama cha yowe (ukunga), kikitokea nyumba za wenyeji, nikaingiwa na hamu kujua ni nini, lakini sikurusiwa kutoka, na baadaye jamaa yangu akaja na kuniambia kazi kubwa imeisha.

‘Inaonekana jamaa yako sio mtu wa kawaida, na nafikiri huko alipo, yupo hoi kitandani, na tunachotakiwa nikummaliza vinginevyo atakuchezea sana…na inaonekana hayupo mbali nanyi. Lakini huyu jini waliyemuweka hapa kawekwa kulinda mali ya urithi, ina maana hili eneo ni mali ya urithi ambayo ilichukuliwa kwa wenyewe bila ya ridhaa yao, kwahiyo wakaweka haya majini kupalinda…’ Mara alinyamaza ghafla, akatikisha kichwa harakaharaka na kunikodolea macho, huku anatetemeka, na mara akatamka maneno nisiyoyaelewa, halafu akatikisa kichwa haraharaka huku mdomoni anatamka maneno kama `mbruuuuuuuu…’ akatulia huku katoa jicho la uwoga, akaanza kuyumbayumba kama mtu aliyelewa, na akawa anataka kuniambia kitu lakini mdomo haufunguki, lakini baadaye akatamla maneno haya kwa shida

‘Hawa wa-wa-wa merudi te te-te-te-na, ingi-ingi-a ndani ya gari hara-hara-hara-ka…vijana kujeni wamerudi tenaaaaaaa…..’ akadondoka chini!

 **Nani tena hawa wamerudi..mmmh, hata mimi naogopa ngoja niishie hapa kwa leo, tuendelee kuwepo**

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Jane said...

Mmmmmh! sasa hapo tena ngoma nzito, bora lakini umekutana na maua. Maana mimi mwenyewe nilisikitika alivyoondoka ghafla, sasa hapo tena hadi whitch doctor anaogopa si balaa hilo??? Mmmh! sio siri inatisha balaa. kazi njema M4.

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmm!!!!!!!!! Sasa hii kali, hebu tusubiri tuone.

BN

Pamela said...

Nasikitika umekatisha uhondo kwa sehemu ya Maua jamani mana Dr kweli kapenda m happy 4u!
yani hiyo nyumba c ya kukaaa kabisa yani dr ni mbishi balaa cc ni wabongo na mizimu ipo inafanya kazi kuna ishara wakati mwingine zinakufanya ufanye maamuzi ndivyo cvyo...
M3 kazi nzuri inatia hamasa ya kufungua blog kila mara.

Faith S Hilary said...

heheheheh.....wamerudi tena...haya mi nipo