Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, November 9, 2010
Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 10
Sasa endelea na muendelezo wa kisa hiki:-
**** ***
‘Una maana gani kusema hivyo mke wangu, mbona unanitisha’ nikamuuliza huku nimshikashika mkono. Akatabasamu, na kusema, `usitishike kabisa, na nakuomba uwe na amani moyoni mwako, kwani uamuzi nilioupanga ni kwa manufaa yetu sote. Akasema na safari hii akaangalia pembeni. Na aliponitizama nikamuona kajaa machozi machoni.
Niliwaza mengi, lakini hakuna lilokuja akilini mwangu, nilifikiria labda mwenzangu kachok na maisha na aataka kuchukua uamuzi ambao sikupenda kuufikiria akilini, lakini nikaona hilo haliwezekani. Nilikumbuka visa vingi vya watu kuzungumza maneno kama haya na mwisho wake mnakuja kuyakumbuka kuwa aliyazungumza kama maneno yakuagana.
Niliwaza kuwa kutokana na matukio yaliyomtokea huenda kaona hatutamwamini tena, na kwa vile vile vitu alivyokuwa akichukua, viligundulika kwenye sanduku kubwa alilolinunua na kuliweka kwenye lile jumba la geraji. Hutaamini siku moja mchana alalilala mapema, kama saa moja usiku, na akaamuka na kwenda dukani ambapo alilinunua hilo sanduku na kufuli lake na kwenda kuliweka huko. Tendo hili la kununua sanduku aliligundua mdogo wake, lakini yeye hakujua mwenzake anahali gani, yeye aliona yupo kawaida, kumbe wakati anafanya vitendo hivyo alikuwa usingizini.
Mdogo mtu alisema siku hiyo alimshngaa dada yake kuamuka na kutoka na ngua ya kulallia hadi dukani na baadaye alimuoana akirudi na sanduku ka ajabu, sanduku la chuma, alipofika nyumbani hakukaa sana akatoa na hilo sanduku , lakini hakujua wapi alipolipeleka, baadaye alimuona dada yake akirudi na kuelekea kitandani na kulala. Yeye aliwaza , na baaadaye dada yake alipoamuka alimuulizia kuhusiana na tendo hilo, lakini dada yake alimkatalia kuwa hajafaya kitu kama hicho na hata kukasirkiana.
Mdogo mtu anasema yeye alichukulia kuwa huenda dada yake alifanya hivyo na hakutaka mtu ajue, na kwahiyo akanyamaza kimya, ila sasa akamejua kuwa alifanya hivyo akiwa usingizini. Na hakukumbuka tena kumuulizia dada yake, na hata dada yake hakuwahi kumgusia kuhusiana na sanduku hilo.
Polisi waliamua kwenda kulichukua hilo sanduku na walipofika hapo walishindwa kabisa kupanda eneo hilo , mapak ilipoleta ngazi ndefu, Kila mmoja alishngaa ni kwa jinsi gani huyu mwanamama alivyopanda pale n kuliweka lile sanduku.
‘Hii ni miuijiza, kumbe binadamu anaweza kufanya jambo akiwa na akili Fulani, na akiwa kawaida asiweze kabisa kulifanya’ akasema askari mmoja
‘Hizo ni nguvu za kishetani, alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa katekwa na shetani, hmjui haya’ akasem aksri mwingine, na hapo akafanya wenzake wambishie na hata wengine kuingiwa na woga, wakauliza kama ni nguvu za shetani, sasa lenywe likijua kuwa sanduku lake limechukuliwa silinaweza kuwajia na kuwadhuru.
‘Hiyo ni imani yako, ukiwa unayaamini, yatakujia, lakini kama huyaamini na unamuamini mungu hayakuwezi kukudhuru abadani’ akasema asksri mmoja wa kike.
Sandukuni kulikutwa mali nyingi, sio tu za mume wake, bali n amali nyingi ambazo hazikujulikana wapi zilipotoka. Zilipelekwa kituo cha polisi kama vielelzo vya kesi ambayo ilikuwa haijapata ushahidi.
Nilitamani sana kumuulizia mke wangu kuwa anakumbuka kuyafanya hayo, na kama anakumbuka angalau kidogo alikuwa na nia gani na mali hizo. Lakini niliona sio wakati muafaka, huenda tukiwa tuepumzika nyumbani nitamuulizia. Nikaona nimsikilize maneno anayotaka kuniambia. Nikamshika tena mikono yake na kutabasamu na kumsikiliza kwa makini.
‘Mume wangu nakupenda sana, hilo liweke akilini, na uamuzi huu ninaouchukua ni kwasababu nakupenda na anaipenda familia yetu kama tungejaliwa kuipata. Nasikitika katika miaka yetu miwili sikubahatika kupata Watoto na wewe. Watoto niliowakuta niliwalea kama Watoto nilowazaa mwenyewe, na natumai watanikumbuka kama mama yao mzazi.
‘Katika maisha ya familia Watoto ni fahari, na Watoto huchukuliwa kama matunda ya ndoa, hili hatukujaliwa mimi na wewe, na kwa hili nasikitika kusema kuwa ndugu ako walinisakama nalo. Sio kosa lao, najua ni kosa langu. Na huenda hata ingekuwa mimi nipo upande wao ningelalamika kumuona wifi anakula tu lakini haleti mazao ya ndoa. Huenda katika hili limechangia sana kunipa mawazo. Ingawaje sina uhakikika kiasi kikubwa kwani nilimtegemea sana mungu na kumshukuru kwa hilo.
‘Nasema nimemshukuru mungu kwa hilo, kwani kama ningebahatika kuzaa ningeishi kwa mashaka, na ningesononeka sana moyoni mwangu, kwani tatizo hili nililo nalo hurithiana, ingawaje katka kuulizia, katika familia yetu hatukubahatisha kusikia kuwa kuna mmoja alibahatika kuwa na tatizo kama hili. Mimi nimemshukuru mungu kuwa sikupata Watoto ambao wangetaabika kama mimi.
‘Kwa minajili iyo nimefikiria sana, nikaona lazima nichukue uamuzi, na uamuzi huu umepingwa sana na wazazi wangu, lakini mimi kama mimi nimeona Ndiyo njia pekee ya kuwapenda wote. Kwangu mimi ni faraja kubwa sana, na najua hilo nitakalo lifanya litakuwa na fadhila sio kwangu tu mimi lakini kwa wote niwapendao…’ akanishika mkono na kuniangalia machoni.
‘Mume wangu najua unanipenda, lakini nataka unijibu hili swali langu, usione kuwa nakutania lakini nakuuliza nikiwa na nia safi…’ akatabasamu nami nikatabasamu, nikijua kuwa ananiuliza swali la upendo. Nilimwangalia usoni na kukumbuka siku ya kwanza nilipokutana naye. Ilikuwa barabarani, mimi nipo ndani ya daldala, wao wanapita na gari lao, wakati wanatupita tukiwa kwenye foleni macho yetu yakakutana, na kujikuta tunatizamana kwa muda, nikajikuta nikitabasamu na yeye akatabasamu pia na kuangalia pembeni. Kwasababu ni kwenye foleni, mara tukiwapita na mara wanatupita na ikawa tuataizamana hivyo hivyo kwa kificho.
Siku moja nikiwa katika mishemishe zangu, nikakuta gari limeharibika, na watoto wa jiji wamelizunguka, nikasema ngoja nichungulie kuna nini, na kwa vile ni fundi, nikaona labda naweza kusaidia. Nikalisogelea lile gari, na kuliangalia sehemu ya mbele ambayo ilishafunguliwa na mwanadada akijaribu kutafuta tatizo lipo wapi.
‘Samahani dada gari lina tatizo gani..’ nikamuuliza
‘Aaah, hata najua naona hawa vijana hapa wananizingua kila mmoja ananiambia lake, hata naogopa nisije nikaibiwa’ akasema huku anaendelea kushikashika waya
‘Hebu sogea kidogo..’ nikamwambia na kuinama kuangalia nini kinaleta shida, nikamwambia aningie ndani awashe. Kwa fundi kama mimi alipoanza kuwasha tu nikajua tatizo lipo wapi. Nikaliendea lile tatizo na kumwambia aliwashe na mara likakubali. Kumbuka muda wote huo tulikuwa hatujaangaliana.
‘Ahsante sana kaka, sijui ni gharama ki=asi gani’ akasema huku anafungua pochi lake. Nilikuwa nahitaji hela, lakini nikaosna hakuna kazi kubwa niliofanya kwanini nichukue hela, nikamwambia asijali. Nikataka kuondoka, na mara nikashikwa mkono.
‘Nakaumbuka kukuona mahali Fulani, sijui lakini sura yako nimeshawahi kuiona.’ Akasema huku ananingalia kwa aibu. Na mara nilipomtizama nikakumbuka ile foleni ya magari. Nikamkumbusha kuwa huenda ni siku ile ya foleni ya magari. Na kwakweli tangu siku ile nilikuwa nikiiwaza sura ile, na kuomba kama inawezekana itokee kama vile.
Kwakweli nilikuwa natafuta mke wa kuishi naye na awe tayari kuwalea watoto wangu waliotelekezwa na mama yao. Hutaamini kuwa mke niliyemuoa awali, alikuja kunikimbia eti kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi akaniachia watoto , mmoja akiwa bado mdogo. Baada ya kupunguzwa kazi, tulianza maisha ya kubangaiza leo unacho kesho huna, mwenzangu hali hiyo hakuipenda, ikawa kila siku ugomvi ndani. Ilifikia hatua naamua kutokuonekana nyumbani ili tu niepuke shari, hadi nitakapo pata chochote. Nikikosa, natamani nitafute sehemu ya kujificha, kwani nitakutana na kero, kashifa na kununiana.
Mwisho wa siku nareea kutoka mahangaikoni, nikiwa nimechoka, siapata chochote nina njaa, nikasema labda nitakuta mwenzangu anagalau kasonga ugali na dagaa, au hta mkavu niondoe njaa. Nafika ndani nakutana na kilio cha watoto, wanalia njaa. Nilipotizama mezani nikakuta barua, amabyo nilipoisoma ilisema kuwa yeye kaamua kuondoka kwasababu kachoka kuteseka na mume asiye na mbele wala nyuma. Nililia sana, nikifikiria kuwa mimi sijaomba hiyo hali, na yote ni mapenzi ya mungu. Niliwashika wale watoto, tukawa wote tunalia.
Baadaye nikaamua kujifunza ufundi magari, na kweli ujuzi huu nikauwezea, na baadaye nikawa fundi mzuri, na maisha yakaanza kurejea katika hali nzuri. Nilitamani ni mtafute mwenzangu turejeane, lakini nilisikia yupo nchi za jirani na keshafunga ndoa. Nikasema ole wake ningeliua siku waliyofunga ndoa ningesafiri hadi huko nakuisimamisha hiyo ndoa. Lakini baadaye nilimuombea kwa mungu amsamehe na waishii vyema na mume wake moya kwani huenda kuna heri ndani yake.
Katika hali kama ile Ilinibidi nitafute mfanyakazi wa ndani awe ananisaidia huku nikihangaika na maisha. Ilikuwa kazi nzito lakini sikukata tamaa kama mzazi! Mwanzoni ilikuwa nikiwaomba majiani wanisaidie kukaa na watoto huku nahangaika huku na kule kuwatafutia chochote, ilifikia hata majirani kunichoka, kuwa nakwepa majukumu ya kulea, hasa pale inapotokea siku nzima zijarudi nyumbani. Lakini baada ya kupata utaalamu huo wa ufundi magari, na kumpata mfanyakazi mambo yakwa mazuri.
Kila siku nilikuwa nikiomba sana kwa mungu anijalie mke mwema, atakayenipenda mimi na watoto wangu. Na niliogopa sana kupata mke atakayeninyanyasia watoto wangu, na hili ndilo, lililonifanya nichelewe kumpata mke wa kuishi naye, licha ya hali ngumu ya uchumi.
Na siku nilipokutana na huyu binti, niliomba sana awe hivyo ninavyotaka, mke mwema, atakayependa watoto wangu, kwani watoto wale walikuwa ndio kila kitu kwangu. Niliwapenda sana, na walikuwa wakinikumbusha sana mama yao, amabye nilimpenda sana. Lakini ndio hivyo kizuri hakikosi kasoro. Tulianza kuzoeana na huyu binti kwanza kwa simu baadaye akawa tunatembeleana na gari lake likiharibika analileta kwenye gereji yangu, ilimradi tukawa tumezoeana na kushibana vyema. Na sikusita kumsimulia kisa cha maisha yangu na mke wangu wa awali, alisikitika sana. Akasema yeye haamini kuwa kuna mwanamke anaweza kutelekeza watoto wake eti kwasababu ya hali ngumu za kimaisha. Nilimwambia basi hiyo imenikuta mimi.
Katika kuzoeana huko akawa anakuja nyumbani kwangu anakutana na wale watoto , anawasaidia hili na lile na kweli nikaona huyu ndiye mke niliyekuwa nikumuomba nimpate, na yeye aliniambia huwa anapenda sana watoto, na kusema kuwa hata kama hatapata watoto yeye atajitolea kuwalea watoto wa wenzake. Nilimuuliza kwaninii anasema hivyo wakati hana matatizo. Alisema yote yapo na hutokea kwa yoyote, unaweza ukawa na afya njema nab ado mwenyezimungu akakupa mtihani wa kiazazi, na kwahiyo unatakiwa kujiandaa kwa yote.
Hapo ndipo urafiki wetu ulipoanzia , na mwezi mmoja baadaye tulishikana mikono kama tulivyoshikana leo nikamuuliza swali ambalo lilizaa ndoa yetu.
Nilimuuliza hivi’Je Maua unanipenda kwa moyo wako wote, na upo tayari kuwa mke wangu war aha na shida hadi kifo kitakapotutenganisha au mungu mwenyewe apende…’ Maua alinitizama akacheka sana, na kwa aibu tofauti na anavyoniangalia leo, akasema, ‘ndio nakupenda mpenzi wangu, na nipo tayari kuwa mke wako wa shida na raha, labda mungu…’ alipofika hapa akacheka, akasema mimi nasikia watu wakisema labda kifo kiwatenganishe, lakini hii ya labda mungu apende, inanichekesha sana. Tulicheka kwa raha na kesho yake niliwaona wazazi wake, na baadaye tukafunga ndoa.
Ndoa yangu mimi na yeye iliwekewa vizingiti vingi, na vizingiti vikubwa vilitokana na tofauti za kimaisha, ya kuwa wao wamejaliwa na familia yao ni ya kitajiri. Kwahiyo wazazi wao walitaka mtoto wao aolewe na familia kama yao. Na sio tu kuwa walitaka aolewe na familia hiyo, bali hata posa ilishaletwa toka kwa mtoto mmoja wa tajiri, lakini Maua alimkataa. Tendo hili liliwauma sana wazazi wake na kukatokea kutokuelewana kati yake na wazazi wake. Lakini hatimaye wazazi wake walisalimu amri na mimi nikakubalika kwa shingo upande.
Siku ya ndoa yetu, mtoto wa huyo tajiri aliyetaka kumuoa, alifanya vituko vya ajabu, kwani alimvizia Maua akiwa katokea dukani na kumteka nyara, Maua alijitahidi kugombana nao, lakini jamaa huyo akamweka dawa ya usingizi aliyoinyunyuzia kwenye kitambaa. Wakati haya yanatokea kumbe kuna mtu aliwaona, na akatuma taarifa polisi, ikawa ndio nafuu yake, kwani wakiwa njiani kuelekea Arusha akanaswa na askari polisi na Bahati nzuri hakufanikuwa kumfanyia lolote baya, akarudishwa na kesi ikamalizwa kifamilia.
Sasa leo hii , mke wangu, Maua anataka kuniuliza swali kwa mtindo ule ule niliowahi kumuulizia yeye takiribani miaka miwili nyuma, je ni swali gani na lina maana gani kwake na kwangu. Ooops, naona muda umekwisha hitimisho litaendelea toleo lijalo, nawaombe msicheze mbali!
Ni mimi: emu-three
6 comments :
heeh mi nilijua utamaliza leo ..nway ila inabidi tukubali yote ili na wewe ufanye kazi nyingine...siku njema
M3 Nimependa mtindo wako wa utungaji, hauchoshi na unampa mtu hamasa ya kutaka kujua ninii kitatokea baada ya hiki.
Nazidi kukushauri kuwa utunge vitabu, ingawaje sasa wasomaji ni wachache, lakini ni hazina isiyoharibika!
Waigizaji na watengeza filamu wangekuona wangepata mtunzi mzuri, lakini nchi yetu hii, mmmh,
Hongera na twasubiri anachotaka kusema huyo mwanamama, mimi nishakisia lakinii nasubiri nisikie ya uhakika
Jamani mwenzenu imenitoa machozi ati the way alivyo propose ndo anavyotaka kuambiwa ili waachane, Du! M3 mimi sitachoka kukwambia wewe ni mkali tena si kidogo. Mbona inasikitisha kiasi hiki??? Ngoja tusubili kesho itakuwaje!!!
Mi naungana na Anonym. No.2(2:04PM)
kwa kweli sina cha kusema ngoja tu nami nisubiri. Stori zako hazichoshi kusoma na zinatia hamu ya kuzisoma. Sina cha kuongeza.
GOD BLESS U
BN
Duh!!! Itabidi wikiendi nirejee zote. Nikikosa siku mbili nakuta nishaachwa.
Wacha nirejee kwenye stori mwaaanzo NIUNGANISHE mpaka sasa.
Shukrani M3
AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAHHHhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh bwana kaka wewe unanitekenya kwa mikito ya fasihi. ni tamu
Post a Comment