Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, November 8, 2010
Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 9
Mzee tajiri aliwakaribisha wageni zake, mimi hamu yangu kubwa ilikuwa kumuona mke wangu , ambaye sikumuona mle ndani ya ukumbi, nilitaka nimuone nihakikishe haya yanayoendelea yana ukweli, kwani nilikuwa bado sijaamini vyema. Mke nimeishi naye miaka miwili, sikuwahi kusikia kuw ana tatizo kama hilo, leo hii ghafla nakutana na mtihani, mtihani ambao umeniweka njia panda. Njia ya kuamini na kama ni kuamini nifanyeje, na kama sitoamini hilo nitapata wapi ushahidi wa kutosha wa kuniaminisha zaidi ya hayo matendo.
Tulikaribishwa kweny e ukumbi wa wageni, kwani nyumba ya jamaaa huyu ni kubwa, kuna sehemu za wageni, kuna ukumbi wa mikutano kuna ofisi ndogo ya nyumbani na kuna eneo la familia. Kulikuwa na wafanyakazi wa aina mbalimbali na wote siku hiyo walikuwa tayari kwa wageni, lakini wengi wao hawakuruhusiwa kukaribia eneo la mikutano, kwahiyo wengi hawakujua nini kinachoendelea.
Tulipofika tuliwakuta watu wengi kidogo, na cha kushangaza zaidi tuliwaoana viongozi wa dini mbalimbali, na pia walikuwemo wataalamu wa tiba asilia. Utawajua tu kwa mavazi yao, kwani yupo mmoja alikuwa kava mishanga na manyoya mwilini na wengine walivaa nguo nyeusi. Nilishangaa kidogo na kujiuliza nini maana yake hii, ina maana mzee tajiri katafuta watu wa aiina mbalimbali ili kutafuta tiba ya mwane!
‘Karbuni waheshimiwa, kaeni kwenye viti eneo hili huku, sisi tuo darasani, kama unavyoona, kuna watu mbalimbali tumewaalika ili kupata darasa hili muhimu na wao kuchangia nini wanachokijua kuhusiana na tatizo hili…’ ilikuwa maelezo mafupi ya mzee Tajiri,
Tukakaa kwenye viti na kuanza kusikiliza.
Kwa mbele yetu kulikuwa na `screen ‘ ya kuonyeshea picha na wakati tunafika kulikuwa na video inachezeshwa, iliyokuwa ikionyesha wagonjwa mbalimbali wa tatizo linaloongolewa, ilionyesha jinsi gani walivyobainika na matendo yao, amabyo wengine walifikia kuumiza watu na hata kuua, na ikaonyeshwa kesi zao ambazo ziliibua utata wa kisheria. Na hatimaye hizo kesi zilifutwa na watuhumiwa kuonekena hawana hatia!
Tiba na maelekezo ya tiba yakaonyeshwa na hapo ndipo mtaalamu akainuka. Alipoinuka mimi na wenzangu tuliokuja nao tukabakia kimywa wazi. Kumbe jamaa yetu dakitari tuliyekuwa naye Dar, ndiye huyuhyuy aliyeitwa huku. Tulishindwa kujua jinsi gani walivyojuana, hadi baadaye alipoelezea historia yake na jinsi gani alivyofika Tanzania.
‘Ugonjwa huu sio ugonjwa wa mashetani ,ni ugonjwa unaotoakana na misongo ya mawazo’ Yule dakitari aliongea kwa Kiswahili fasaha, ‘…. na misongo hii husababisha mtu akashindwa kudhibiti fahamu zake, na kuweza kumilikiwa na matendo, ambayo wakati mtu kalala bado matendo hayo yanakuwa na nguvu za kumfanya afanye matendo bila mawasiliano na fahamu yake. Utaona kama mlivyyona kwenye picha yetu, mtu anaamuka na kufanya kitu halafu kesho yake anauliza nani kafanya jambo lile. Ina maana hana kumbukumbu kabisa kuwa yeye ndiye aliyelifanya. Ina maana wanakuwa kama watu waili tofauti.
‘ Nawaomba waganga wa miti shamba, wasilichanganye hili na mambo ya mshetani, haya sio mashetani, na nimeshangaa kidogo kusikia baadhi yenu, nyie wataalamu wa jadi mkisema kuwa ni aina Fulani ya mashetani yanayomteka mtu akili. Hapana, huu ni ugonjwa na ugonjwa kama huu una tiba zake, na tiba nuhimu ni mgonjwa mwenyewe kwanza kujijua na halafu tiba kama za dawa na watu kumsaidia kwa kutokumuongezea misongo ya mawazo.….’
Wakati maelezo haya yanaendelea mara watu wakageuza vichwa vyao upende wa mlangoni. Pale alisimama mwanamama, akiwa kavaa gauni refu na sehemu kubwa ya kichwa hata uso ilikuwa imefunikwa na kuvaa miwani mikubwa ya jua. Hata mimi nilishindwa kumtambua ni ni nani. Mara akaongea na mlinzi aliyekuwa mlangoni mwa mlango unaingia ukumbini.
Yule mlizi akamsikiliza , halafu akageuka na kwenda kuongea na Mze Tajiri, na mzee Tajiri akageuka kumwangalia mwanae, halafu taratibu akainua, na kwa mshngao, nikaona anakuja pale nilipoakaa na kuniambia mke wangu anataka kuonana na mimi kwa faragha. Nikawaza, ina maana mke wangu ndiye Yule mwanamama aliyevaa vile, mbona sijawahi kumuona akiwa kavaa vile. Nikasema moyoni, labda ni mtu wake wa karibu katumwa kuja kuniita.
Nikatoka pale ukumbini, na nilipotembe hatu ambili nikasikia sauti nyuma yangu ikiita, kwa jina ambalo mimi na mke wangu tumezoeana kuitana. Nikageuka na mbele yangu alisimama Yule mwanamama alieyevaa miwani ya jua. Akaivua ile miwani na kumbe ni mke wangu. Nikaduwaa hata nisijue la kufanya, ila yeye alinifuata pale niliposimma akaja na kunikumbatia. Nilikuwa mzito kidogo kumkumbatia kama ilivyo kawaida yetu mimi na yeye. Sijui kwasbabu ni ukweni au kuna sbabu nyingine ambayo mimi sikuielwa.
Yeye alinishika kwa nguvu, na alipoona mimi nipo baridi kidogo akaniachia kwa haraka, kama vile mtu aliyeshika barafu bila kuitambua, akaniangalia kwa mashaka. Nikajitahidi kutabasamu, na yeye akatabasamu halafu akanishika mkono na kuniambia ana mazungumzo maalumu ya faragha mimi na yeye. Nilimtizama mke wangu , na kweli nakiri kuwa kuna mabadiliko sana, sio Yule mke niliyemjua, mabadiliko haya sio ya maumbile wala sio mabadiliko yakuweza kuelezea, lakini ni mabadiliko ya hisia. Nilihisi kuwa mtu aliyesimama mbele yangu ni anaonekana mgeni machoni mwangu, siye Yule mke niliyemjua, sijui kwanini
Lakini pamoja na hayo yote huruma, na upendo vilinigubika na kusema vyovyote iwavyo huyu ni mke wangu na nitajitahidi kuwa naye !
Aliniongoza hadi chumbani kwake na pale akanishika na kunifanya tuangaliane uso kwa uso, na macho yake yakaniangalia moja kwa moja usoni. Mke wangu kwa kawaida ana aibu sana, na hawezi kumwanglia mtu machoni kwa muda mrefu, lakini nilishangaa uasiri ule kaupata wapi, kwani muda ule aliniangalia mpaka mimi nikaona aibu. Nikajiuliza moyoni, hii hali ndiyo imembadili kiasi hiki, mbona anakuwa na mabdiliko ambayo sijawahi kuyaona. Nilianza kuingiwa na wasiwasi, nikajisema moyoni isije ikawa bado yupo katika hali ya kuchanganyikiwa!
‘Mume wangu, nina mazungumzo muhimu sana na wewe, na mazungumzo haya yana muda mfupi sana, kwani nahisi muda umefika. …’ akaniangalia tena usoni. Na hapa nikaingiwa na wasiwasi mkubwa, na kauli yake hiyo ilinifanya niwaze mengi. Mazungumzo yana muda mfupi na muda umefike?? Niliinua uso wangu na kumkazia macho, na pale nikahisi machozi yakinilengalenga…sijui kwanini!
***********
Oh, naona kwa leo tuishie hapa , ili tuweze kutafakari haya. Najua wengi mna dukuduku la kujua hatima yake, na swali kubwa je ni nini mwanamama huyu anataka kumwambia mumewe? je mazungumzo hayo yana muda mfupi kwa vipi, na muda umefika kuwaje? hata mimi najiuliza bila kupata jibu, tuwepo kwenye hitimisho laa kisa hiki. Na kisa kingine cha Asiye na bahati habahatishi kipo mbioni! Karibuni sana!
Ni mimi: emu-three
5 comments :
Jamani M3 mbona short sana????????? Hope utaweka mwendelezo kabla ya kufika jioni, maana nikisema nisubiri hadi kesho naona kama vile itakuwa mbali sana, si unajua si wote wenye mitandao hadi hm?????? wengine mpaka tuwe makazini. But all in all nakukubali kwa kazi zako, sijui anataka kumwambia nini????? ngoja tusubiri.
kweli kabisa mi nilijua leo itakua mpaka mwisho..jitahidi basi leo..mmh sasa nafungua kila baada ya nusu saa lol..
Oh Elisa, nashukuru sana kwa kuwa nami, na nafurahi sana ukinitembelea kila mara, kwangu mimi ni faraja.
Unajua Elisa, ajira nayo ni muhimu, najitahidi sana kuandaa hitimisho hilo, lakini tupo kwenye ofisi za watu kwahiyo nafanya kwa uficho, usijali itakuwepo hewani karibuni!
Yaani!!!!!! Mi sina la kusema nipo pamoja na aliyetoa comment No.1 (12:06PM) Wewe ni MKALI, unatisha mno, upo juu.
Mi naogopo asije akajiua, kwa vile kaambiwa anatatizo hilo, na yeye hajalikubali hilo tatizo. Na akawa anajiuliza kuwa yeye ndie aliyetaka kumuua shemeji yake? Na kwa vile huwa anatenda hayo hajijui. Kwakweli inaumiza sana.
'Hayo ni mawazo yangu tu.'
***********
Lakini mbona ujatuambia kule kwy lile jengo alilokuwa anapanda? Ambalo mdogo wake alitoa wazo la kuchukua ngazi za Tanesco ili wapande ili kuona kama zile dhahabu zilifichwa kule?
**********
M3 usitubanie Bwana. Pls, naona unarukaruka sehemu fulanifulani. Au kuna mtu anasema stori ndefu nini? We tupe hii stori nzima hata kama pg 100, Poa tu. Hii ni stori nzuri na inafundisha sana.
Thx
BN
Mhh, nashukuru BN, kwa kunikumbusha sehemu hiyo, ipo katika hitimisho, na wakati mwingine unapoandika visa hivi kwa sehemu kama blog, huwa tunajaribu kutokuandika kila kitu, ina maana mengine tunaacha kwa wasomai wenyewe kujazilia!
Nitajitahidi kuleta raha, msikonde washikaji zangu(wadau)!
Karibuni sana
Post a Comment