Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, November 2, 2010

Kikulacho ki nguoni mwako(Somnambulism story) 5



 Moyo ulinilipuka nikabaki nimeduwaa, nikatingisha kichwa kwa kutoamini, nikasema haiwezekani, lazima kuna kitu kinaendelea humu ndani. Nilikuwa na uhakika kuwa kweli ninayemuona mbele yangu ni mtu ninayemfahamu, ni mtu niliyeishi naye muda mrefu, na kwahiyo siwezi kufanya makosa ya kumtambua. Huyu alikuwa si mwingine bali ni mke wangu.


‘Mbona sielewi, huyu sio mke wangu jamani, nikajongea karibu, huku nahakikisha kuwa hanioni, alikuwa mke wangu bila shaka..’ nikajisemea moyoni. Sasa kwanini kashiklilia kisu, labda alikuwa akipambana na huyo jambazi na bahati nzuri kamshinda. Nikajipa moyo kwa mawazo hayo.

Nikaona ili kupata uhakika nimfuatilie kwa nyuma nyuma. Alisukuma mlango taratibu na kuingia ndani, na mwendo wake ulikuwa wa kunyata. Sasa kwanini ananyata hivyo, mbona sijawahi kumuona akitembea hivyo tangu nimuoe. Je ndio kuhakikisha kuwa hatoi sauti au huo ni mwendo gani wa kunyata kiasi kile. Mwendo ule ni sawa na ule unaonyweshwa kwenye runinga, mwendo wa kunyata, mwendo wa taratibu taratibu(slow motion), ndivyo alivyokuwa akitembea, kwahiyo ilikuwa inachukua muda mrefu sana.

Alitembea hivyohivyo hadi kitandani kwetu, nikashangaa anakiinua kisu juu, huku akiwa kakishikilia kwa mikono yote miwili na kwa nguvu sana, akakishusha pale nilipokuwa nimelala, ambapo ,kwa sasa ipo mito miwili iliyofunikwa na kutengeneza sura ya ntu aliyelala. Niliona kama kiini macho vile, kwanza nani aliyeweka ile mito vile na kuifunika kama mtu aliyelala. Mimi sikuwahi kufanya hivyo!

Mke wangu alirudia kukishusha kile kisu mara mbili, na kila mara alikuwa akisema maneno nisiyoyaelewa vyema na pigo la mwisho kisu kile kilipenya kwenye mto mmojawapo na hakutaka kuhakikisha kuwa kimefanya kazi yake vyema, bali alirudi kinyumenyume hadi akatoka nje ya chumba, nikamfuatilia hadi alipofika jikoni, kule akaangalia huku na kule na kuvua mifuko ya mkononi .

Oh, mifuko ya mikononi, mara nyingi tunaitumia pale tunapofanya usafi au kupulizia dawa ya kuua wadudu, kwanini aliamua kuivaa mikononi? Ina maana kuivaa ile mifuko mikononi ni kufuta ushahidii wa alama za vidole au alikuwa na maana gani?. Basi kama alifanya hivyo alikuwa na dhamira ya dhati ya kunimaliza mimi. Nikawaza na kujawa na uchungu mkubwa sana. Jamani mke wangu, anataka kuniua kwa kosa lipi jamani, mbona tunapendana sana…nikajikuta machozi yanalengalenga!

Wakati nawaza haya mke wangu akarudi polepole kwa mwendo wa taratibu, mwendo huu ulinipa wasiwasi, mbona hata wakati wa kurudi afanaye hivyo, kama kehsaniua alikuwa anamuogopa nani tena! Nikaaona hapa kuna kitu zaidi ya ninavyohisia, haiwezekani, labda ndio hayo mashetani wanayosema yanamwingia mtu na kumwamrisha afanye kinyume cha matakwa yake.

Nikasema hapana, siwezi kuhalalisha uhalaifu na imani hizo, ngoja nione mwisho wake. Mara mke wangu akarudi kuja chumbani kwa mwendo uleule, hadi alipofika kitandani na kujilaza sehemu yake alipokuwa amelala mwanzoni. Na mara akaanza kutoa sauti ya kuhema kuonyesha kuwa yupo katika usingizi mzito. Haya sasa maajabu, hili sasa ni balaa, …nikakuna kichwa kama mtu mwenye ukurutu!

Jasho lilinitoka, niliwaza mengi, na jinsi nilivyowaza nilishindwa kujizuia, nilitaka nimwamshe mke wangu na kumtoa wanguwangu hadi polisi . Nilimuona muuaji mkubwa asiyeweza kusamehewa, nikajua kuwa yeye ndiye aliyetaka kumuua mdogo wangu na sasa alitaka kuniua na mimi. Nilijiuliza kwa lengo gani, ina maana ugomvi mdogo kama ule unaweza kumaliza maisha ya wengine, je kuna haja gani ya kuishi na mtu kama huyu.

Sikutamani kurudi kulala kitandani tena, kwanza kwa kuogopa huenda usingizi utanijia na akiamuka na kuniona sijafa anaweza kunimalizia nikiwa usingizini. Pili utalalaje na mtu anayekuchukia, haiwezekani. Nikaona niende chumba cha mapumziko na kuyatafakari haya kwa undani.

Nikaelekea kwenye chumba cha mapumziko na kujilaza huko, huku nikiwa na wasiwasi. Nilijilaza kwenye kochi huku nikiwa ndani ya mawazo mengi. Na mara nikakumbuka uwa kulikuwa na sauti nyingine iliyokuwa ikitokea maeneo ya hapa, je ilikuwa ni ya nani, nikainuka haraka kwa woga na kwa wasiwasi mkubwa, nilitizama huku na huko, lakini hakukuwa na mtu yoyote. Sikuamini…

Labda ilikuwa hisia za uwoga, ndizo zilinifanya nisikie sauti za watu, lakini nakumbuka kabisa nilisikia sauti za watu wakinongonezana.

Baada ya kuhakikisha kuwa kweli hakuna mtu mwingine zaidi yangu, nikaajilaza kwenye kochi, huku nikijiuliza nitaenda wapi zaidi ya hapo. Hpa ndio kwangu, ina maana niikimbie nyumba yangu mwenyewe, hapana, nitalala humuhumu na kama nikufa nife humuhumu. Nikaweka ile mito vizuri, na kabla sijaweka bega vizuri, nikasikia sauti ikitokea kwenye kabati mojawapo la vitabu. Nilikurupuka kama mwizi na kujiandaa kukimbia.

Kwakweli sasa nilianza kuamini kuwa humu ndani nimeingiliwa, na kama sio watu basi ni mshetani. Nililaani kutokuchukua silaha yoyote. Nikajipa moyo nakusema kama ni mijambazi nitapambana nayo kwa mikono mitupu, kwani na mimi sipo mbali na karate na mieleka, ngoja yaje, nitakufa na mmojawapo. Kama ni mashetani nitayapa neno la mungu yatateketea, nikajipa moyo na kutizama pale sauti ilipotokea.

Zikapita dkika tatu bila kusikia kitu tena, nikasema lazima kuna kitu kimejificha kwenye kabati la vitabu, sidhani kuwa akili yangu imejenga mawingu ya sauti kiasi kile. Nikasema moyoni ngoja nisubiri kidogo halafu nitaenda kuhakikisha kama kweli hakuna mtu au kitu kimejificha pale. Wakati nawaza hili, huku nikisubiri, mara nikaona taswra ya mtu ikitoke nyuma ya lile kabati. Nikagwaya, huku nikisema sasa nimahakikisha kuwa kuna mizimu mle ndani, sasa kuna mijambazi mle ndani , sasa nijiandae vyema! Nikajiandaa kwa mapambano, kwa yoyote atakaye kuja, lakini kwanza lazima nitumie mbinu, nikijificha kwenye kona ya kochi, ili aweze kutokeza na mimi nimshitukizie kwa nyuma.

Mara nikamuona mtu huyo anatokea akiwa na panga, nikasema haya, kama mimi ni mtaalamu wa karate, sasa nitaipatapata, kwani ukirusha teke linakutana na panga. Nikagwaya tena…sasa nifanyeje, , lakini kabla sijakata tamaa, sauti ya kuita jina langu ikasikia, Looh, maajabu mengine, ina maana…..

Oh, ngoja niishie hapa, lakini unaonaje nikikuacha na swali la chemsha bongo: Je hii sauti iliyomuita ni ya nani, na je huyo aliyemuona ni nani, ni jambazi au ni nani? Tuwepo kwenye tolea lijalo!

Ni mimi: emu-three

7 comments :

elisa said...

mmmh inasisimua sana ..ila jamn mi natamani ungeweka mpka mwisho tuone nini kitaendelea unatukatisha katisha sana ..

emuthree said...

Na mimi ningetamani kufanya hivyo Elisa, lakini wakati mwingine nabanwa na mazingira, huwa naandika nikiwa ofisini au kwenye internet cafe, kote huko kuna muda wa watu wa kazi kuna muda uliolipia kama ni internet cafe.
Kwahiyo najitahidi kuandika harakaharaka na ku-edit, ili iwe sawa, na unakuta muda umekwisha!
Nashukuru kama kisa hiki kinakusisimua, na utajifunza mengi kwenye kisa hiki, kwani kuna mafunzo, na utaalamu utakuja kwenye muendelezo wake!
Karibu sana!

Anonymous said...

Mimi nahisi aliyeita ni mkewe!
Hongera kwa jinsi ulivyoipika, nakupa big up!

Anonymous said...

Kwa kweli M3, nashindwa hata ni comment nini. Kwani wewe ni kiboko. Hii stori inamwamsho fulani, na inasisismua mno pia inatisha sana. Kama ni muwoga unaweza kupiga kelele au ukatoka baluti. Hata hivyo huyo jamaa ni shujaa pia. Mi ningekufa kabla ya kuuwawa.

Sasa jamani ni nani tena huyo anayeita jina lake? Nahisi kama ni yule yule mke wake. au ni mdogo wa mkewe nae anaugonjwa huo huo nini? Manake magonjwa mengine ni ya kurithi.

Haya tungoje huo mtamu. Tafadhali usitucheleweshe kutupa huo uhondo.

MUNGU ABARIKI KIPAJI CHAKO. Naona tufanye mpango wa kuchangia Internet Cafe.

BN

emu-three said...

Mhhh, naona BN unaanzisha ule ,mjadala wa kapu chakavu! Nashukuru sana kwa kuniunga mkono, kusoma na kuandika kitu inatosha sana kuonyesha kuwa unajali kazi hii!
NA WEWE MUNGU AKUBARIKI PIA

Anonymous said...

Yaani nami nakushukuru sana, nilikuwa mvivu sana kusoma stori zako kwani nilikuwa naziona ndefu sana kama wadau wengine wasemavyo. Lakini kwa sasa nimekuwa hodari sana na nafuatilia kila siku na napenda sana kuzisoma hizi stori zako kwani zinamafunzo na unapanua uwezo wa kutafakali. Ndio maana nimeamua kujiita BN ili nawe ujue tupo pamoja ktk hii glob.

NASHUKURU KWA BARAKA ZAKO PIA

BN

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu