Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, November 8, 2010

Imani bila matendo!....!!???

 ‘Mwanangu yaani hapa Minazi mirefu hadi HAPO Mombasa unachukua shilingi mia mbili na hamsini, muogope mungu, unihurumie kwani nategemea kupanda gari jingine hadi Msasani…’ Hii ilikuwa kauli ya Huruma ya mama mmoja wa makamo, lakini kondakta alijifanya kama hasikii, na dereva wake ambaye alikuwa akizidisha sauti ya redio ili nyimbo za dini zisikike akasema.


‘Wewe mama kwani nauli ni shilingi ngapi, angalia nje ya gari imeandikwa nauli shilingi mia mbili na hamsini, hata upandie wapi…’ akasema kwa sauti ya kujiamini. Ina maana hapo kwasababu wote waliopanda wanakwenda Kariakoo, lakini wamepandia Minazi mirefu, inabidi walipe nauli mara mbili, kwasababu gari linageuzia Mombasa. Ni sehemu fupi sana, ambayo unaweza kumuita mtu aliyepo upande wa pili akakusikia, lakini kwasababu sio kituo cha kugeuzia, ukipanda hapo unalipa nauli kamili sawa na Yule aliyetoka Kariakoo!

Mimi nikajiuliza ,ndio ni kweli nauli imeandikwa mia mbili na hamsini, lakini toka wapi hadi wapi? Labda EWURA, Au sijui nani wanaoshughuli hili swala la usafirii wangeweka maelezo ya ziada kuwa kati ya kituo na kituo, (vituo vidogovidogo) itategemeana na `wingi wa abiria kibiashara, kwahiyo makubaliano yatakuwa kati ya mwenye basi na abiria’ kwasababu kwakweli asubuhi na jioni nauli zinakuwa juu, lakini mchana, ambapo hakuna abiria, unaweza ukapanda basi hata kwa shilingi mia moja, sehemu ambayo asubuhii umeipanda kwa shilingi mia mbili na hamsini!

Mimi yote hayo sikuyajali sana, kwani kwa vile adhabu ya usafiri asubuhi nimeizoea, nikaona ni mambo ya kawaida. Lakini kilichonivutia zaidi ni zile nyimbo za kwaya, ambazo dereva alikuwa akiziongezea sauti kila mara ili ujumbe ufike kwa abairia wake! Nikashangaa, kwani katika nyimbo zile, maneno mengi yalikuwa yakihimiza `upendo, kuhurumiana, kutokudhulumu, ndoa na mambo mengine yanayowahusu wenye imani hiyo’

Nikajiuliza huyu dereva anataka ujumbe huo ufike kwa abiria, mbona yeye haujamfikia! Mbona yeye Huruma hiyo haipo, anamdhulumu hata Yule mama mzee, ambaye shilingi mia mbili na hamsini aliyoitoa ya ziada kaiomba kwa jirani ili angalau afike msibani! Upendo upo wapi, mahali pa kufikiri kuwa hapa kwakweli hata shilingi mia nikiichukua kwa abiria si halali, lakini konda na dereva wake hayo hawayaoni, wanachoona ni yale maandishi ambayo yanasaidia upande wao,! Cha ajabu kila muda nilimsikia Yule konda akiyafuatilia yale maneno ya wimbo kwa ulimi wake huku akitingisha kichwa, kuonyesha kuwa anayajua!

Mimi nimewaza ile kauli isemayo kuwa `fuata maneno yangu usifuate vitendoo vyangu’ nikajikuna kichwa. Kumbe ndio maana watu wengi hawavutiki katika imani za dini, kwani wanapomuangalia kiongozi wa dini matendo yake ni tofauti na imani anayohubiri anashikwa na mshangao, je huenda kufuata vile nilivyohubiriwa au kupewa mawaidha ni makosa, kwasababu mkuu wa dini hafuati hivyo! Huenda, huenda… zinakuwa nyingi na mwisho wa siku mtu mwenye imani haba anasema `afadhali nibakie bila imani kwanimatendo yangu yanadhiri ukweli’

Tukirudi majumbani, utakuta watu wanagombana, watu hawapendani, watu wanasengenyana, lakini wamefungulia redio za kwaya au mawaidha au kasida, au hata wao wenyewe wanaimba maneno ya mungu yanayokataza hayo wanayoyafanya, swali ni kuwa tunamdanganya nani? Je hizi imani za dini ni kinga tu ya madhambi yetu? Imani na matendo hawashibani kabisa! Inakuwa kama hasi na chanya!

Mwisho wa safari yangu nikaguna na kusema `kumbe ndio maana hata tukiomba dua zetu kwa mwenyezimungu hazikubaliwi, kwasababu tunachofanya ni kumcheza shere, Yule asiyechezewa shere, Yule ambaye anaijua nafsi yetu kuliko tunavyojijua wenyewe, jamani huku ni kujidanganya wenyewe…! Imani bila vitendo, haiingii akilini…

*****
Naona ni wakati muafaka wa kujumuika kwenye mfululuzo wa kisa chetu kinachoendelea cha `kikulacho ki nguoni mwako!

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

We bwana achana na watu hawo, tupe kisa chetu, wikiendi nzima nilikuwa nikiwaza itakuwaje sehemu inayofuata. Hawo tunawajua wenyewe, na kila mtu atabeba zigo lake mwenyewe

elisa said...

hapana jamani..so sad..kuna vitu vingine ukisikiliza/ukiona vinatia huruma sana ..looh..unafikiri kama wewe ndio umekua umekosa hiyo 250 ..basi tu Mungu anajua kila kitu na ana makusudi na kila mtu..