Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, November 24, 2010
Asiye na bahati habahatishi-7
.......‘Mimi..hapana, kama nimeweza kuokoka na hili janga, sitaki kabisa kurudi mikononi mwa hawa watu hivi mnawajua hawa watu vyema…hapana, nyie fuateni njia hii hadi kwenye lile jiwe kubwa, chini yake mtaona kitu kama kimsitu, mle ndani kuna kibanda, hamtapotea…’ akasema huku anawasiwasi akiangalia huku na kule wasije wakatokea hawo watu tena.
‘Sawa mkuu ngoja tufuatilie, akasema kamanda mmoja na wakati wanajiandaa kuondoka mara ghafla……
********** endelea tulipoishia**********
`Aaaah, ' kilio cha Mzee, mjomba wake Tausi kikasikika, na kudondoka chini. Ikawa anahangaika kutaka kuuchomoa mshale uliokwisha zama kwenye bega lake.
Haikujulikana mshale ule ulitokea sehemu gani zaidi ya kutoka juu angani, kwani kwa muelekea wa ule mshale ni kutoka juu , na mrushaji labda angelikuwa juu ya mti, lakini kwa pale hapakuwa na mti mrefu kiasi hicho, na watu walitaharuki na wote wakawa wanaangali a huku na kule, ili kugundua wapi huyo adui alipojificha. Lakini kwa binti Yule hakujali alimkimbilia baba yake ambaye alilala chini akilalamika maumivu. Akataka kuuvuta ule mshale kutoka kwa baab yake lakini jamaa ambaye ni mtaalamu wa matibabu ya kienyeji akamzua.
‘Wewe acha kwanza, utamuua baba yako ukifanya hivyo…’ akasema Yule mtaalamu. Yule mtaalamu akamsogolea na akatoa moba wake toka begani na kuanza kutoa vifaa vyake!
Binti Yule alivyosikia hivyo akauachia ule mshale na kumshilia baba yake kichwani, huku akihangaika kwa wasiwasi. Aliwalaani sana hawa watu wa msituni, akaapa kimoyomoyo kuwa huyo aliyefanya hivyo akikutana anye lazima atammaliza kwa panga. Akasimama pembeni ili kumwangalia mtaalamu anavyofanya vitu vyake. Hawa watu wa maporini wana dawa zao za asili na wanajua utaalamu wa kutoa mshale na hata kugundua kuwa ni wa sumu au ni wa kawaida tu.
Yule mkuu wa kikosi cha askari aliamrisha kikosi chake kizunguke na kumtafuta mrusha mshale na wkati huohuo madakirati wa kawaida walishaanza kumfanyia huduma ya kwanza Yule mzee wakishirikiana na Yule mtaalamu wa miti shamba, na ikizingatiwa kuwa mishale hiyo mara nyingi huwa na sumu, na sehemu ilipoingia ni sehemu hatari, kwani ni kwenye bega la kushoto
‘Baba usife tafadhali , nakuomba baba, mimi nitabaki na nani, baba tafadhali nakuomba usife…mama upo wapi unisaidie mimi jamani, baba anakufa huku…’ binti akawa anaruka huku na kule hakukubali kumuona baba yake akifa hivi hivi, na wakati huo mzee hali ilishakuwa mbaya, damu ingawaje hazitoki sana, lakini jicho lilishaanza kugeuka katika weupe….
Huku kwingine vijana wa serikali walicharuka na mori wa hasira ulishawapanda, wakasambaa maporini kwa hasira, Ilichukua dakika chache risasai zikaanza kurindima huku na kule, kwani walishagusa pabaya, na kila dakika paliletwa majeruhi , na wengi wao walikuwa vijana wa kienyeji wakiwa na mavazi yao ya kiasili. Ikawa operesheni maalumu na askari wa serikali walifanya kazi yao kwa haraka kuliko ilivyotegemewa kwani kwa muda mfupi walishawakamata vijana wengi na kuwaweka chini ya ulinzi.
Taarifa zikaenda kwa mkuu wa kabila hilo, naye kwa haraka akafika na wazee wenzake, akaomba mapigano yasitishwe, lakini vijana wa serikali wakasema mapaka hawo majangiri wajisalimishe wote na silaha zao. Ikabidi mkuu huyo afanye kazi ya ziada, na kwa juhudi zake baadhi wakajisalimisha. Ila wale wenye vichwa ngumu ambao walikuwa viongozi wa vijana wakasema hawakubali hadi hatua ya mwisho.
Wakati haya yakiendelea kikosi kile cha mwanzo kichotumwa kufuatilia pale walipoelekezwa mwanzoni na Yule binti kuwa huenda ndipo binamu yake alipofichwa, kilikuwa kimeshaingia ndani ya lile banda, lakini walikuta hakuna kitu, lakini baadaye waligundua handaki lililopo ndani kwa ndani kwenye lile jengo, na walipoliingilia kwa tahadahri kubwa wakakutna na vijana saba waliojiandaa kwa mapambano. Ilikuwa kazi ngumu, kwasababu vijana wale wanajua siri za pango, kwahiyo walikuwa wakijificha huku na huku huku wakivizia na kutupa mishale, ambayo ilisababisha majeruhi wengi.
Askari wa usalama walipoona hivyo wakaona watumie njia nyingine, wakapiga bomu la machozi kuhakikisha wote waliopo humo ndani wanasalimu amri, na hapo wakafanikiwa na vijana wale wakawekwa chini ya ulizi wengi wao watatu wakiwa katika hali mbaya ya majeraha.
Na wakati wanaendelea na mapambano, kumbe kwa mbele kulikuwa na mlango wa pango unaotokea kwa nje kwa upande wa pili, na kule ndipo yupo jamaa mmoja alikuwa akikimbilia kutorokea huko, lakini akaonekana na askari aliyekuwa analinda kwa juu, na akamtupia risasai iliyomuumiza mkononi. Akaadondoka chini akigalagala kwa maumivu, akawa anatoa sauti ya kuamrisha ambayo iligundulika kuwa anamwamrisha mtu mwingine kuwa asijionyeshe aendelee kujificha.
Ghafla akatokea binti mmoa aliyekuwa kajificha vichakani, alishindwa kuvumilia akaja kumwangalia Yule jamaa aliyeumizwa, akahamaki alipoona jamaa hajiwezi na analalamika kwa maumivu, akachukua mshale wa Yule jamaa mabo ulikuwa umedondokahatua chache na pale alipolala, na kwa hasira akageukaa nao kutaka kumchoma nao yule askari, na hapo askari akatumia ujuzi wake wa kiaskari na kumnyeng’anya kabla hajaleta madhara yoyote.
Yule askari akawa kawadhibiti wote wawili na bahati nzuri askari wengine walishafika na kutoa msaada uliohitajika. Wote walikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha muda cha polisi ambapo ndipo mzee alipokuwa akiendelea kupata mataibabu. Kwa utaalamu wa Yule mwenyeji, akawa kautoa ule mshale na kwa maelezo yake, ule mshale haukuwa na sumu, na haukuleta mdhara makubwa, ulikuwa umegonga kwenye mfupa wa begani na kuchimba kidogo. Alipewa dawa za kawaida na dawa za kienyeji ambazo nyingine zilikuwa za majani, na kweli haikuchukua muda, jereha lilikanywea na damu ikafunga kutoka!
Kwa vile alikuwa kapoteza damu nyingi, mwili ulikuwa mdhaifu na alikuwa akiona kizunguzungu, vijana wake wakamshauri arudishwe mjini, lakini akagoma Mzee mzima akasema hajakata tama mpaka aone mwisho wake, akasema yeye hajambo na hiyo kwake ni ajali vitani. Akainuka pale kitandani lakini kizunguzungu kikamrudisha chini, ikabidi alale kidogo.
Na wakati huo Yule jamaa aliyejeruhiwa alishafikishwa mbele ya wakuu wa usalama akiwa na Yule msichana waliyekutwa naye na vijana wengi wa kienyeji walishasema yeye ndiye mtaaamu wa kutupa mishale kwenda juu huku anamlenda mtu aliyepo chini, kwahiyo huenda ndiyo yeye aliyeutupa huo mshale akiwa na nia ya kulipiza kisasai cha ndugu yake aliyeuliwa na huyo mzee katika mapigano yaliyotokea karibuni. Kwao kisasi ni lazima!
Binti wa Yule mzee aliposikia hivyo akachukua panga na kumwendea Yule jamaa, akitaka kummaliza nalo, kwa hasira za kutaka kumuua baba yake na kabla hajamfikia, mke wa Yule jamaa naye akachukua panga wakakutana katikati, ikawa kizaa-zaa. Wasichana walivalia mavazi ya kienyeji walikuwa wanataka kuonyeshana makucha yao. Askari wa usalama wakainuka kuwakamata, lakini kile aliyesogea Yule manadada ambaye mume wake aliumizwa akawa mbogo…
Kwa kipindi hicho Yule mzee alishapata nafuu akainua kichwa kuangalia nini kinaendelea, kwani licha ya ushauri kuwa apelekwe mjini kwa matibabu na mapumziko yeye hakukubali. na mara akawaona hawa akina dada wakitaka kukaribiana na mapango mikononi, alimuona ni binti yake na msichana mwingine, kwasababu ya kizunguzungu alikuwa akiwaona kwa shida na bahati nzuri akaweza kuiona sura ya yue binti mwingine…Loooh, kila akijaribu kuinua mboni za macho zinakuwa nzito, mmmh, ina maana ndio nakufa nini akawaza, huku akijaribu kwa nguvu zote kujiinua, na giza likatanda usoni …!
i mimi: emu-three
8 comments :
Naona mtandao haukubali kuweka picha, kwahiyo ili nisizidi kuchelewesha nimeona niendelee bila picha!
Hakuna shida mkuu, vyovyote vile wewe tupe tu bwana. Maana story ni zaidi ya picha. Mmmh! asijekufa mzee wa watu bure bora wampeleke kabla khali haijawa mbaya.
kweli Jane umesema sawa kabisa.
Mkuu hiyo picha kiboko, mwe mwe!!!!
Kweli mkuu nafikiri inawakilisha hali halisi ya hiki kisa!
DUH! anakufa nini Mzee wa watu? Twasubiri enndelezo....
Kwenye picha:
Hayo mavazi vichakani si mchezo ukikutana na upupu.:-)
hehehe Simon na upupu..lol!...huyo mzee asifeeee!!!!...oh sorry, I am not the writer lol!
jamani naogopa!!!
Post a Comment