Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, November 30, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-2

 
 Akaona Yule mtu akiifungua ile kamba, ipo kama kitanzi, akakipanua kile kitanzi, ana…ana..akawa haoni vizuri, lakini kwa kumbukumbu ina maana Yule mtu…giza likwa litanatanda usoni, akajitahidi kulizuia


‘Nini unataka kufanya..' akajaribu kutoa sauti lakini haikutoka, akilini akawaza `Yule, mtu, sio mume wangu kweli,, sura haionekani vyema…’ akajitahidi kufunua macho kwa nguvu na akaona kitu cha ajabu kabisa. Akaomba mungu na kujitahidi kutoa sauti kwa nguvu…….

**************

Wakati macho yanagubikwa na giza akaona, kitu cha ajabu kabisa, kitu kama taswira ikipita mbele ya aliposimama mume wake, kitu hicho , kilikuwa kirefu ajabu, na kikaondoka na pale akabakia ,mtu anajivisha kitanzai, ...ni nani yule alijaribu kwa shida sana kuigundua sura ya Yule mtu, lakini kwa vyovyote Yule atakuwa ni mume wake…je kwanini anaamua kuiua, je afanyeje ili kumuokoa, naye ndiyo huyo anakufa, nani atawasaidia, ina maana watu watakuja mle wakute mume kajiua, mke kafa sakafuni

Akazidi kumuomba mungu amsaidie, na amsaidie mume wake, kwani akipona yeye ataweza kuja kumuokoa kwasababu yeye ni dakitari lakini macho yalikuwa mazito hayafunguki. Akaomba mungu na kujaribu kupanua mdomo na kwa sauti iliyopo ndani ya uwezo wake, akamuita mume wake, kumwambia aache kufanya anachotaka kufanya, na alipomaliza kutamka yale maneno akazama kwenye giza nene.

`Hii sauti sio ya mke wangu, mbona sijielewi’ Dokta akasema akiwa hajielewi

Ni kweli hii ilikuwa sauti ya mkewe wangu niliisikia kwa mbali ajabu, kama mtu anayeongea ndani ya maji na sauti kama hiyo unaisikia kwa mawimbi. Kwa muda huo nilisakamwa na sauti za majibizano kichwani mwangu, nyingine ni za mawazo ambayo yalikuwa yakinituma kujitundik kwa kamba, sauti hizi zilikuwa na ushawishi mkubwa sana, na kila mara zilisikika kwa jaziba. Inaonyesha anayetoa sauti hizi namuogopa sana, na nilikuwa sina hiari, lazima nifuate tu kama mbwa anavyomfuta chatu.

Lakini kuna sauti ya Huruma, sauti ya kunibembeleza, ikinipa moyo, na kunionya kuwa nisifanye hicho ninachotaka kukifanya, hii ni sauti niliyoihisi kuwa ni ya marehemu mama yangu!

‘Mwanangu umesahau wosia wangu, kuwa matatizo sio mwisho wa maisha ukijiua watoto wako, mke wako wataishi na nani…achana kuinyonga, acha kabisaaaaa’ Lakini sauti hii ilikuwa ikinyamazishwa na sauti kuu, sauti kubwa yenye nguvu na mvuto wa kuamrisha ndiyo iliyonishinda nguvu, sauti hiyo ilikuwa aikiniamrisha kwa nguvu kuwa nijiue kwani nikijiua itakuwa mwisho wa yote haya.

‘Unasubiri nini, kamba ipo tayari, panda juu ya kiti kile pale, weka kamba shingoni, basi kazi imekwisha hutateseka tena, kumbuka mateso yako toka utotoni, mapaka sasa, unapata faida gani, ni bora ufe umfuate mama yako….’ Hii ilikuwa sauti yamtu ninayemjua, ambaye akiongea sina hiari, lazima nifuate tu, nipende nisipende

Nikaiendea kamba ile, ambayo sijui niliichukua saa ngapi toka stoo, na ilishatengenezwa sehemu ya kuvalia shingoni, na ilikuwa imefungwa vizuri darini, sijui ni mimi nilifanya hivyo, sikumbuki kabisa kufanya hivyo, kwani pale ilipofungwa panahitaji ngazi…nikaweka kiti cha kukalia nikaifungua kile kitanzi nikajivisha shingoni.

Niliishika ile kamba vizuri huku nayumbayumba kwenye kile kiti, kwani miguu ilikuwa haina nguvu, ni kama mtu aliyelewa, nikaivaa vizuri shingoni shingoni, nikawa nasukuma kiti ili kidondoke, na hapo nitakuwa nishamaliza kazi.

`Fanya haraka, sukuma kiti, fanya haraka sukuma, fanya haraka sukuma kiti…’ ilikuwa suati ikijirudia rudia,

`Wewe mume wangu acha kujiua, unafanya nini hapo, acha kujiua…’

Niliposikia sauti ya mke wangu ikiniita, nikawa kama mtu aliyezibuliwa masikio, na nikahisi uhai, sauti ile ilinizindua na kujiona kama mtu anayeamuka toka usingizini. Ilikuwa kama ndoto, na ndoto yenyewe ya kutisha ajabu…., nikapangusa macho, na kujiona nayumbayumba, lakini ile kamba shingoni ikawa inanizuia nisidondoke, na kunikaba koo. Vipi tena, mbona nina kamba, shingoni, ina maana ile ndoto ni ya kweli. Nilijiuliza wakati fahamu zinanirejea na nilipofumbua macho vizuri, nikawa nashangaa, nani katundika ile kamba juu ya dari, alipandaje kule juu, na…’

‘Mke wangu kwani kumetokea ninI, mbona kuna kamba , kama vile mtu anataka kujiua, mbona…ina maana ni mimi, nilikuwa nataka kujiua, hapana haiwezekani, mimi siwezi kufanya ujinga huu…hapana, lazima kuna kitu, haiwezekani…nikajifungua ile kamba shingoni na kushuka juu ya kile kiti, nikakipiga kile kiti teke, na kuivuta ile kamba toka darini kwa nguvu hadi ikakatika.

Niliangalia huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliyeniona, na nilipotizama mlangoni nikakkuta mke angu amelala pale chini, nikamwendea na kumuinua, …damu, inatoka kichwani. Niliangalia mle ndani nikapata vifaa vya kumsafisha na kuhakikisha kuwa hayupo katika hali mbaya, baadaye akazindukana na kuniangalia kama mtu aliyeona mzuka. Akainuka kutaka kukimbia, nikashangaa vipi tena.

‘Wewe ulikuwa unataka kufanya nini, nimekuona wewe kwa macho yangu ukitaka kujiua, siulikuwa unataka kujiua wewe?’ akaniangalia kwa macho ya hasira na kushangaa.

‘Mimi nijiue, unauhakika na unachozungumza mke wangu’ nikamwangalia huku nacheka. Akaniangalia kwa macho ya kushangaa, huku anarudi kinyume nyume, kama anayetka kunikimbia. Mwenyewe kwenye akili nilikuwa nikiwaza ilikuwaje, nilijaribu kutafakari tukio zima, lakini sikumbuki kuwa na uamuzi kama huo. Niliangalia pale mezani na kukuta karatasi, eti nimeiandika mimi kuwa nataka kujiua ili kumaliza mateso yaliyoniandama toka utotoni…niliposoma hili neno utotoni, taswira ya maisha yangu ikanijia, kama picha kwenye runinga.

‘Wewe nyani amuka ukapige deki choo, unafikiri nanai atafanya kazi hii nani, amuka haraka., mimi sijaolewa kuja kuwa mfanyakazi wenu wa ndani, kinyago mkubwa weee.’ hii ilikuwa sauti ya mama yangu wa kambo, ambaye aliolewa baada ya mama yangu mzazi kufariki dunia. Mama yangu alifariki nikiwa na umri wa miaka mitatu, kwahiyo sikuwa na kumbukumbu naye sana, nilichokumbuka kwake ni ule upendo wake wakunibeba, kunilisha, na…jamani mama ndio sitakuona tena milele, huwa nikiwaza haya najikuta nikilia.

Ninachokumbuka sana ni maisha yangu na huyu mama wa kambo, ambaye alinifanya kama mfanyakazi wake wa nyumbani toka nikiwa na miaka mine, hutaamini, mimi nilikuwa nikifanya kazi zote za ndani, nikiwa bado mtoto, niliananza kulazimishwa kufagia ndani, na kwa vile nilikuwa mtoto, nilikuwa nikikosea, kufagia vizuri, hapo nilichapwa viboko mgongoni, hadi nikaweza kufagia vizuri. Nikalazimishwa kuosha vyombo, kwa viboko mpaka nikajua kuosha masufuria ya ugali.

Mama huyu aliolewa nikiwa na miaka mitatu, mwaka ule wa kwanza alikuwa akinipenda kweli, lakini nilipofikia miaka minne akiwa mja mzito, akawa ananichukia kama mnyama. Alikuwa akinipenda mbele ya baba, na kunidekeza kama mtoto wake, lakini baba akiondoka asubuhi kwenda kazini, basi anageuka kuwa mnyama, ananiamusha kwa kunimwagia maji kitandani, ili ionekane nimekojoa kitandani. Hapo nitaanza pilikapilika za kupiga deki ndani, kosha vyombo , na kazi zote amabazo kwa umri wangu ilikuwa haiwezekani, lakini niliweza.

Ilikuwa asubuhi baada ya kupiga deki, na kumaliza usafi wa ndani, nachukua vyombo vyote vilivyotumika usiku naviweka kwenye karo, kuwe na jua, mvua, ziruhusiwi kuondoak mpaka niwe nimemaliza kusafisha hivyo vyombo. Ole wangu kikutwe chombo kichafu. Akija mgeni naitwa ndani haraka, najaziwa chai kwenye kikombe ambayo haina sukari naambiwa nishikilie mkononi ili nionekane nakunywa chai, hadi mgeni aondoke, akiondoka napigwa mateke nirejee kwenye karo kuosha vyombo. Mchana hivyohivyo, chakula nakula makombo, akija mgeni naambiwa nikae mezani na kujifanya nakula na yeye, huku akinibembeleza kwa kinafiki.

Mwangu hapendi kula huyu, Napata shida sana kumlisha…basi atajifanya ananilisha kwa uwongo, hadi mgeni akiondoka, na hapo nitatemewa mate, kuwa niondoke haraka, mchafu mkubwa., na matusi makubwa, ambayo mengine yalielekezwa kwa marehemu mama yangu. Na wakati mwingine napigwa nakuambiwa nitauliwa nimfuate mama yangu kaburini.

Hutaamini baba akirudi nyumbani, mama anakuwa mtu mwema ajabu, ananifanyia wema wa ajabu, atahakikisha naoga, navaa nguo nzuri, nakula na wao mezani, yaani inakufanya hata usahau machungu ya mchana kutwa, na baba akiniuliza nina tatizo lolote, kwa utoto wangu nasema hakuna, na kujilaza miguuni kwa mama huyu. Nikikumbuka onyo lake kuwa, nikisema nafanya kazi zote hizo au nanyanyaswa nitakiona cha mtema kuni.

Nakumbuka siku moja, kipindi cha mwanzo nilijaribu kulalamika,baba alipoondoka tu, kisu kiliwekwa jikoni, nikachomwa nacho, shingoni, alama hii ipo mpaka leo, na akanitishia kunichoma nacho machono, na kuniapisha kuwa nitakuwa mtiifu, sitatoa siri ya mateso yale, na nikitoa mcho yangu ni halali yake.Sijui kwanini nilkuwa mjinga kiasi kile, kwani baada ya lile tukie la kuunguzwa na kile kisu nikawa nafanya kila kitu mama huyu alichoniambia, na udhaifu huu ulijijenga kichwani mwangu, kuwa anachosema mama huyu sina maamuzi ni kufanya tu!

Mambo hayo yalizidi mpaka majirani wakajua, na wengine wakaamua kumwambia baba yangu, lakini aliponiuliza nilikatakaa katakata, na kusema mama ni mtu mzuri sana, hanitesi.

Naona tuishie hapa, na tutaendelea na kisa hiki baadaye…tuendelee kuwepo!

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Pamela said...

hi m3 nimeguswa na mateso ya dr alipokuwa mdg mama wa kambo acha kabisa ingawa c wote wenye mioyo migumu cjui kwann alikuwa anamtesa malaika ambae hajui chochote.. pole kwa yaliyokukuta utotoni.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika kweli binadamu ni wanyama, nimesoma kisa hiki huku nikitoka na machozi na pia tumbo likiniuma. Kimenikumbusha mbali sana na pia kimenifanya nimkumbuke marehemu mama na......naacha maana najikuta machozi yanatoka tu....

Jane said...

Mmmmh! M3 unajua hatueleweki Ofisini??? Maana machozi yanatoka kama nimepata taarifa ambayo si nzuri!!! Why kila siku ni kama unaona maisha ya mtu aliyopitia??? Nashukru mungu kwa kila kitu kwa kunifanya mkubwa na kunikasahaulisha niliyopitia utotoni. Mmmmh! naomba niishie hapa hapa leo maana nikiendelea nitashindwa kufanya kazi