Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, October 20, 2010

Limbwata!

‘Kuna vitu vingine ukivisikia hutaamini mpaka vikupate, nasema hivi kwasababu …----‘ akainua kichwa na kuangalia huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayesikia anachotaka kuongea.` Ndugu yangu mama nanihii, siulisikia kuwa nimeachika, basi kisa hiki ndicho kilichonifanya ndoa yangu ichungulie kaburi..’ Hii ilikuwa sauti ya mama mmoja aliyekuja kumtembelea mama nanihii, nami nikawa na hamu yakukisikia, nikiwa kwa ndani ni nini kilichomsibu, nikafungua masikio.


‘Mimi na mume wangu tulioana miaka kumi iliyopita, mwanzoni tulikuwa na raha na upendo wa hali ya juu, lakini kama binadamu siku zilivyokwenda tukawa kama kaka na dada. Mimi nikawa sijalishi sana yale maisha ya `mpenzi nakupenda sijui nini tena, siunajua tena, yale ya kizungu..’ akaendelea kuelezea.

Baadaye nikaona mume wangu anabadilika, mara muda ule wakurudi nyumbani ukaanza kubadilika, na wakati mwingine akirudi mapema anarudi na kukaa kidogo halafu, anaaga, anaondoka, Siku moja nikaamua kumuuliza vipi kulikoni.

‘Kwani vipi, kumepungua nini, naona hivi ni sawa tu kwangu, hela ya matumizi nakupa, unashida gani,, maana wakati mwingine inabidi nikapoteze mawazo, na naona nikikaa humu ndani nakupotezea muda wako wa kazi….’ Akanijibu huku anaondoka.

Kwa wakati Fulani nikaona haina haja labda mimi ndiye nimesahau wajibu wangu, nikaanza kujikwatua na mambo mengine ya kumvuta mume wangu, lakini wapi, mume akawa akija hakai , mara anatoa sababu hii na ile. Sikujali lakini pale alipooanza kunipa mgongo, na nikimgusa anasema amechoka nikaanza kuingiwa na wasiwasi…’

Basi nikaona nimuulizie rafiki yake mmoja ambaye mara nyingi wanaongozana naye, yeye akasema hakuna kitu, wao wanakwenda kupoteza mawazo hapa na pale hakuna baya..’ jibu alilonipa nikahisi kuna kitu. Nikaanza uchunguzi wangu binafsi nikagundua kuwa kuna nyumba ndogo inaniingilia. Nikalipeleka hili kwa wanandugu wa mume wangu, walimuita kikao cha familia lakini walichosema au kuamua sikuambiwa, na hali ikawa ileile. Siunajua tena kesi ya ngedere unapompelekea tumbili unategemea nini…’ akacheka kicheko cha mzaha!

‘Siku moja nikamtembelea shoga yangu ambaye tulisoma naye shule ya msingi tunajuana tangu utoto, uajanani, nilikuwa siku za nyuma nikimtembelea mara kwa mara, na kwakweli ukifika kwake utaona raha, maana yeye na mume wake wameshibana kweli, na huwezi kumuona mume wake akitokatoka ovyo. Ikabidi niulize siri ya upendo wao huo.

‘Hivi rafiki yangu siunakumbuka maelezo tuliyopewa kwenye kitchen party, na pia siunakumbuka tulichezwa wote, umeasahau maagizo ya kungwi wetu. Mimi nayafuatilia moja baada ya jingine. Unakumbuka siku moja ulinitembelea ukakuta tukiwa na ugomvi na mume wangu, ulipoingilia tukakaosana na unakumbuka nilivyokuambia, yale maneno najua yalikuuma sana …nilikuambia huenda wewe ndiye unayetembea na mume wangu, kipindi kile kilikuwa kigumu sana kwangu. Mume wangu alibadilika sana, akawa hakamatiki nyumbani, Nilimfumania akiwa na msichana wa jirani yangu…’

‘Siku hiyo karibu niue,..’ alinisimulia huyo shoga yangu kwa hamasa kubwa akaendelea kusema kuwa alimvyaa Yule msichana na kumshushia kipigo ambacho hatakisahau maishani mwake. Lakini alisema baadaye alijiuliza sana, kuwa je hilo limesaidia nini. Kipindi anajiuliza hivyo alikuwa yupo kwao nyumbani kwani baada ya fumanizi hilo aliondoka kwa mume wake na kwenda kuishi kwao. Walisuluhisha kinyumbani , lakini akawa hataki kabisa kurudi kwa mume wake.

Shangazi yake ni mmoja wa makungwi na anajua mengi hususani mambo ya ndoa, alimdadisi sana na mwisho wa siku alimwambia eti yeyendiye mkosaji. Hutaamini hayo. Alimwambia kuwa kosa tunalolifanya wanandoa nikujisahau kuupalilia mche wa ndoa. Mche wa ndoa sehemu kubwa hutunzwa na mke ndio maana kuna vitu kama kitchen party, mara kuwekwa ndani nk. Hii ni kutuwezesha wanawake kujua wajibu wetu katika ndoa’ alimwambia shngazi yake hayo maneno.

Shangazi yake akasema kwa jinsi alivyosikia matatizo ya huyo mume wake, hatua kubwa inahitajika nayo ni kumtafutia dawa maalumu.

‘Dawa maalumu dawa gani hiyio, akamuuliza shngazi yake. Shangazi yakealicheka sana, na aliingia ndani na mara akamletea dawa Fulani kaifungia ndani ya karatasi, akasema hii ni dawa ambayo hupewa mume aliyeshindikana kaabisa, na ni hatua ya mwisho. Dawa hii hatari yake ni kuwa ikiisha nguvu zake mume anaweza akakuchukia kama hakujui. Kwahiyo wakati mumeo anaitumia, unahitajika uwe unahakikisha unatimiza masharti yote ya mume na mke. Hakikisha kila siku unakuwaa mrembo kwake, la sivyo ikiisha nguvu umeachika…

‘Dawa hii huitwa limbwata....'

‘Limbwata ! ….hapana, shangazi siwezi…Limbwata, hapana…'

***********
Tuendelee ,tusiendelee...ni nani aliwahi kutumia au kusikia au kuona limbwata na madhara yake? Basi toa maoni yako, na ushauriu wako, na tuwepo katika sehemu ya pili, ya kisa chetu hiki cha limbwata!

Ni mimi: emu-three

8 comments :

Anonymous said...

Mhhh, mimi naona haya yote yanafungamana na imani za kishirikina, ingawaje ni dawa kabisa kama, na ina nguvu kama madawa ya kulevya, ila inapumbaza akili na kumpeleka mhanga kwenye pumbao la akili ...
Sio vizuri kuitumia kwani ni hatari kwa akili za watu, inaweza ikamfanya mtu akawa zezeta kabisa! Na kwanini uitumie, na mbaya zaidi badala ya kuitumia wewe unampa mtu mwingine, kwa siri...huo ni ukiukaji wa haki za binadamu na...i dont know, kama nikigundua kuwa mke wangu kaniwekea...mmmh sijui...sijui, sijui....!

Yasinta Ngonyani said...

Libwata, pesa/mali/utajiri! kama mtu unampenda mtu kwa vitu hivi basi hilo si penzi. Ndio maana akaambiwa nguvu ikiisha basi ataachika na ni sawa na kuolewa na mwenye pesa kwa ajili ya pesa. HILO SI PENZI ni afadhali hata wangeachana tu. Libwata naweza nikasema hii ni imani kwa kweli. Haya ngoja tusubiri mwendelezo.....

Simon Kitururu said...

Hii kitu mie naisikia tu na labda mpaka nishuhudie ndio nitaamini kuwa inafanyakazi kwa kuwa najua Mwanamke anaweza kumpagawisha mwanaume bila dawa.

Mie nishawahikumsamehe msichana kipenzi wangu niliyemfumania baada ya siku moja tu baada ya fumanizi na nauhakika hakutumia dawa wala nini katika jinsi alivyoninasa na nilikuwa nimejifia tu mwenyewe.

Na chaajabu nilipomfumania ni mimi niliingiwa hofu naachwa na mtoto huyo mzuri na wala sio yeye aliyekuwa anatishika.:-(

Tunasubiri stori iendelee Mkuu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu limbwataz, lina wenyewe na sio mimi

Anonymous said...

Mimi naona limbwata ni jamii kama madawa ya kulevya, ila inaathiri hisia za kimwili.
Mimi nilishuhudia jamaaa akipagawa, na akawa habanduki nyumbani, anaosha vyombo, mkewe anasoma magazeti, yaani mpaka ndugu zake walipokuja na kumchukua, na kilichotokea ni kuachika kwa yule mwanamke, kwani alikuwa akitamba kuwa keshamtengeneza mumewe, hakuna wa kumchukua!
Haya yapo na ukitaka kuyajua uishi nyumba za kupanga za watu wengi wa hali ya chini!
Ni dhambi kubwa sana!

emuthree said...

Basi mimi naona nimalizie sehemu ya pili, kwani nilitaraji kupata watu wengi wanaoweza kutoa ushuhuda wa hili.
Nashukuru kwa waliochangia na nataraji mtachangia zaidi kwenye sehemu yetu ya pili ya limbwata!

EDNA said...

Mmmmh mimi kwa kweli limbwata nalisika sijabahatika kulishuhudia kwa macho.Nasikia wengi wakisema lipo.

Anonymous said...

Watu wengine mwajishauwa amjui libwata mwalijua vizuri na nyie ndo WA kwanza kulitumia!