Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Friday, October 29, 2010
Kidole kimoja hakivunji chawa!
Gari liliposimama pale kituoni watu walipiga kelele za kumlalamikia dereva kuwa kwanini anasimamisha gari wakati watu wamejaa kupita kiasi, anataka kumchukua nani zaidi
‘Nyinyi kwasababu mumeshaingia ndani ya gari mnasahau kuwa kuna watu wamesimama kituoni zaidi ya masaa mawili, hebu msaidieni huyo mama aingie ndani’ akasema dereva.
Kwa nje alionekana mama akiwa katika kundi la watu, akiwa na Watoto wawili, mmoja kiwa kambeba kwa khanga na mwingine kamshikilia mkono, wote walionekana kuchoka sana. Yule aliyemshikilia mkononi alikuwa akilia , nafikiri sababu ya njaa au likuwa kachoka kusimama pale kituoni kusubiri mabasi.
Nilijiulizana moyoni, Yule mama na wale Watoto wataingiaje ndani ya basi kwani gari limejaa hadi mlango unashindikana kufungwa. Lakini kama kondakta alivyosea kuwa gari halijai, kinachojaa ni ndoo ya maji, Yule mama alijibanabana hadi akaingia ndani kwa shida, wakati huo mtoto wake wa mkononi alishapokelewa ndani kwa kupitia dirishani.
Yule mama mwenye mtoto alipongia ndani akawa kasimama karibu na kiti walichokaa mama wawili, na hata viti vingine vya karibu yake walikaa kaina mama, lakini wote walijifanya wamelala, kwasababu ya shida ile ya usafiri. Ni kweli watu walikuwa wamechoak sana, fikiria tangu saa kumi na moja kasoro hadi muda ule ambao ilikuwa saa moja kasorobo bado tupo kwenye msururu wa foleni, na mkifika kwenye mataa mtasubiria karibu ya saa zima , trafiki anaita upande mmoja tu.
Yule mtoto wa Yule mama aliyepokelewa dirishani akawa analia, anamtaka mama yake, ambaye alikuwa bado kasimama ndani ya mbanano wa abiria akiwa na mtoto mwingine ambaye alimbeba kwa kutumia kanga aliyojifunga shingoni kinamna, ili mtoto huyo mdogo akihitaji nyonyo yake aweze kunyonya kirahisi!
Nilimuonea huruma sana nilitamani nimuite aje akae kule nyuma nilipokaa, lakini ingekuwa kazi kwake kuwapita abiria waliojaa hadi nyuma ya gari. Lakini wazo likanijia akilini, kuwa wale akina mama aliosimama karibu nao watamuonea huruma kwasababu ni mama mwenzao . Lakini hiyo haikutokea. Kila mmoja alijikausha kama vile hajamuona.
‘Jamani nyie akina mama hapo mbele mpisheni mwenzenu akae, hamuoni ana mtoto , na mtoto huyo anataka kunyonyeshwa, na joto aliposimama hapo linamuumiza ndio maana analia…’ mzee mmoja tuliyekaa naye nyuma akasema kwa sauti.
‘Kwani wewe umekalia mkeka, kwanini usimpishe wewe’ mama mmoja kati ya wale wawili akajibu kwa nyodo.
‘Sisi tumelipa nauli ya kugeuza nalo, ili kukwepa adha hii ya kusimama, na afya zetu zina migogoro, nani asimama kwenye hii foleni, wewe siunajiona una huruma, mpishe aje akae huko ulipo’ akasema Yule mama mwingine.
Ni kweli kwasababu ya foleni na kukaa sana njiani watu wengi wanaamua kulipia nauli mara mbili, kwa kutembea vituo viilinyuma, huko unasubiri gari linalokuja likiwa halina watu wengi, unaingia kwa na kwenda nalo hadi mwisho linapogeuzia, ikiwa na maana unalipia nauli mara mbili, ilimradi upate kiti, kwani kusimama ni mateso.
Akatokea baba mmoja ambaye alikuwa katikati akamwiita Yule mama akaja kukaa na mtoto wake, na hapo pakazuka mabishano, kuwa akina mama mara nyingi hawaoneani huruma wenyewe kwa wenyewe. Watu walitegemea kwa vile wao wanajua sana uchungu wa kuzaa, wangemuonea huruma Yule mama menye Watoto, lakini haikuwa hivyo.
Akilini kwangu nikakumbuka mama mmoja aliyesema kuwa, kuliko kumpa kura mwanamke mwenzake anayegombea ubunge ni heri asipige kura kabisa, nikajiuliza kwanini, nikamuuliza kwani huyo mwanamke anayegombea hana sifa. Akasema hata kama anasifa akimpa kura ataishia kuwa na nyodo, na atawadharau wanawake wanzake, ndio maana anaona heri kumpigia mwanume kura hata kama hafai kuliko mwanamke mwenzake! Angalia wanawake wanaoteseka kijijini, mikopo, miradi ikija inaishia kwa wanawake wa wakubwa mjini… akaongezea kusema!
Jamani haya yapo? Na kama yapo nini tunataraji katika hiyo ajenda ya nusu kwa nusu katika uongozi, kama wenyewe kwa wenyewe hampendani, sasa hiyo haki mnayo-idai mtaipataje kama wenyewe hamshikamani. Je ule usemi wa kidole kimoja hakivunji chawa haueleweki na kuingia akilini! Nashangaa kwa kutafakari!.
Mimi sijui , hili ni wazo langu tu la leo, likikumbushia huu usemi wa usemao, kidole kimoja hakiwezi kuvunja, nini... chawa!
Haya twendeni tukaendelee na kile kisa chatu cha `kikulacho ki nguoni mwako sehemu ya tatu!
Ni mimi: emu-three
2 comments :
Hii M3, ni kweli kabisa, akina mama wengi hatupendani, sijui kwanini, hata mimi najiuliza bila kupata majibu.
Jamani umenikumbusha kadha ya usafiri wa dar, bora kwa sasa niko mkoani nimepumzika kidogo. Ilishawahi kutokea mama mjamzito alianguka kwenye gari baada ya kuzidiwa. Kwanza tulikuwa tumebanana kawaida ya magari ya Dar. Nikiwa niko kwenye siti akaingia mama na mtoto tena mchanga nikampisha akaa kituo kilichofuata aliingia mama mjamzito akasimama karibu yangu, tukawa tumesimama wote nikadhani mama aliyekaa kwenye kiti cha karibu atamwone huruma na kumpisha kwenye kiti lakini kama ulivyosema walifunga vioo vya macho, kutokana na foleni na kukosa hewa yule mama akadondoka kila mtu akashangaa mpaka baba aliyekaa kiti cha tatu kutoka tuliposimama ndo akampisha. Samahani kwa kisa ndani ya kisa, lakini haya yapo kila siku wala mtu haoni shida kabisa. Ndo maana tunaambiwa wanawake mwl wetu kipofu.
Post a Comment