Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 22, 2010

Ama kweli mazoea yana tabu

Ilikuwa asubuhi wengi wetu tulikuwa tunawahi makazini, na maeneo yetu kupata usafiri wa daladala asubuhi ni kazi kubwa sana. Tukabahatisha usafiri kwa shida na ndani ya gari tulikuwa tumebababa sana, ikabakia ugomvi wa kukanyagana. Wewe umekanyagwa unavumilia kwa shida, sasa ole wako uinue mguu kidogo, …`Yallah, wewe msh****z nini mbona unanikanyaga…’ basi ni balaa moja kwa moja. Lakini tumezoea!


Mara hali ya hewa ikabadilika, na hata kama ulikuwa umepitiwa na usingizi kwa wale waliobahatisha viti utatikisa pua, na wale wenye aleji basi ndio chafya mtindo mmoja, na wekundu wa pua kwa weupe utauona kwa wakati huo. Ndio hapa ni maeneo yajulikanayo kama `Mazizini’ wengine wanapaita sehemu ya hukumu za ngombe, au machinjioni.

Harufu kali sana, ilisikika na wengi tukajiuliza kama sisi wapiti njia imetuathiri hivyo, je hawa ambao wanaishi kulizunguka hili eneo la machinjio ya ngombe inakuwaje. Na kwanini kuwa na harufu kali kupita kiasi. Wengine walisema kuna watu wanachuka ile damu ya ngombe na kuianika, kwa ajili ya chakula cha mifugo, sasa inafikia ile hatua ya kuoza, ndipo harufu inapoenea maeneo yote hayo!

Wakati tunapikicha pua zetu , huku tukisema tumezoea, tukapita eneo jingine, hilo ni dampo la takataka, ni dampo lisilo rasmi, watu wanalundika matakataka yao hapo ili gari la halimashauri lije libebe, sasa sijui yale matakataka yamekaa pale kwa muda gani, manake taka zimejaa na kurudi barabarani. Watu wakapikicha pua zao mpaka tukapita eneo hilo! Oh, tumezoea

Wakati tunahangaiaka kupata hewa na kuendelea kupigiana kelele za unanikanyaga, nikasikia sauti ya wimbo wa Marehemu `Michael Jackson’ na hapo hoja ikazuka enzi ile alipoitemebelea Tanzania, kuwa aliposhuka uwanja wa ndege alisema `kuna harufu mbaya’ kwa wanaukumbuka watanisahihisha, kuwa ilikuwaje. Watu wakasema ni kweli kwa mgani akishuka uwana wa ndege kwa harufu za majalalani, harufu za mazizini, harufu za maji taka zinaweza kuwaathiri!

Kwanini nimeileta hii hoja, ni kwa ajili ya kuwatetea watoto ambao wanaishi maeneo kama ya mazizini, hatuoni tuwaathiri afya zao, tujue kuwa wao bado ile himile ya kuvumilia harufu kali au makelele ya majenereta inawaathiri afya zao. Kwani kuna athari nyingine za makelele ya majenerator hasa umeme unapokatika, jaribu kukatisha mitaa ya Kariakoo, kama una matatizo ya msikio ambayo hayataki kelele utatamani ukimbie. Sasa jiulize watoto wanaoishi hapo, au waliozaliwa hapo karibuni, hatuoni kuwa tunawatengenezea uziwi…siui labda mimi sio mtaalamu sana wa watoto lakini nahisi kuna athari Fulani zitawakumba! Sisi wakubwa tutasema tumezoea, na mazoea yana taabu yake!

Sasa ni nani alaumiwe, na tufanyeje? Nafikiri yote hayo ni majukumu ya halimshauri ya jiji, kuwa na mpango ambao nahisi upo tatizo ni ufutiliaji, kuwa maeneo ya mazizini au machinjioni kuwa na watu maalumu wa kuzibiti usafi. Na kwenye majalala, barabarani, kwanini tusianzishe ajira kwa wasio na kazi wakawa wanaifanya hii kazi kwa siku wanapata kiasi Fulani cha hela,…kwasababu kuna michango inapitishwa ya usafi sasa hizi hela zinakwenda wapi! Na kwa swala la `majenereta'…mmmh, sijui tuwalaumu Tanesco au halimashauri, au nani sijui….! Oh, tumezoea shida zetu tusiongee sana!

Hili ndio wazo langu la leo, samahani kwao tunaokanyagana kwenye madaladala, kwani sio makusudio yetu, ndio hali halisi ya nchi yetu hii, ambayo karibuni tutaipa nafasi ya miaka mingine mitano, huku tunafunga mikanda matumboni…tutafanyeje, tumezoea shida zetu…mmmh, wanasema usilalamike nenda kapige kura yako, kura yako ndiyo italeta mabadiliko…huo ndio ujumbe nilioupata asubuhi!

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Uchafu bongo ni kawaida na sijui hali hii inaweza kuzibitika kwa sasa, kwasababu tumeshajenga ile hali ya `mali ya umma' .Hii ni kasumba, kwamba kila kitu ni serikali, na cha serikali sio hasara kwako!
Unasikia sana, kama watu wangejali mambo kama yao, uchafu ungewekwa mahali pake, na kila kaya ingejenga mazingira ya kuhifadhi uchafu wake. Ama kwa hili la mzizini, hata mimi niliwahi kupita pale harufu iliyokuwa ikitoka, niliishiwa na hamu ya kula. Sijui tatizo ni nin, na kwanini watu wa maeneo hayo hawachukui hatua!
Mambo mengine ni serikali za mitaa kuwajibika, wawajibisheni serikali yenu ya mitaa. Na sasa uchaguzi ndio huo, muwarejeshe tena kama mumeipenda hiyo hali!