Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, September 9, 2010
tutaonana mungu akipenda
Tarehe kama ya leo namkumbuka mjomba wa ajabu aliyekuja kunitembelea, tarehe hii kila ikifika namshukuru mungu. Kisa kilichonipata kwenye tarehe hii nilikificha siku nyingi , lakini leo nimeona nikiweke hewani. Naomba ukiweke kwenye blog yako, tafadhali!
‘Kuna mgeni toka nyumbani, yeye ni mojmba wangu, alifika toka asubuhi’ akaniambia mke wangu
‘Vyema, ngoja nikamuone na nilikuwa na hamu sana na taarifa za toka huko nyumbani’ nikamwambia mke wangu kwa Furaha.
Mjomba mtu alikuwa sio mkubwa sana, huenda hata mimi nilimzidi kiumri umri, lakini kiheshima ni mkubwa kwangu, tukasalimiana na akaanza kunipa michapo ya kijijini kwao na kwa vile alikuwa mcheshi basi maongezi yalikuwa hayaishi na mara nyingi nilikuwa nikimsikiliza yeye tu.
Mjomba huyu tulikaa naye wiki mbili, na mara nyingi nikiondoka kwenda kazini na yeye ananiambia kuwa ana mambo yake anayafuatilia uhamiaji, kwahiyo hata kuwa anashinda nyumbani. Mimi nilimwambia hakuna taabu ila kama anahitaji msaada wangu wa kumpeleka huko uhamiaji asisite kuniambia. Akasema yeye hahitaji msaada , uhamiaji anaijua sana na kuna marafiki zake wengi sana, kwahiyo swala hilo ni dogo sana.
Basi siku moja wakati natafuta baadhi ya vifaa vyangu nikakuta `passpot ; nilipoikagua nikakuta ni passport ya mke wangu, na imetengenezwa hivi karibuni, nikashangaa, nikasema, labda mjomba kaamua kumtengenezea mke wangu kwa vile anajuana na watu wa uhamiaji. Nikasema ngoja nitamuuliza mke wangu vizuri. Lakini cha ajabu sikukumbuka kabisa kumuuliza tena, kwani nikirudi nyumbani nimechoka, na maongezi ya mjomba yakawa yananikwamisha hata kuongea vizuri na mke wangu, na usiku kwa vile nimechoka, tunaishia kulala tu.
Basi kazini kwangu kukatokea kupunguzwa wafanyakazi, nami nikawemo kwenye hiyo orodha, nikawa sina kazi. Hutaamini mjomba akaniambia kuna watu anajuana nao atanifanyia mpango kwenye kampuni , na kweli siku moja aliporudi akaniambia kuwa nimepata kazi, nilimuona mjomba mtu wa maana sana. Kazi yenyewe ikawa ya kwenda mikoani mara kwa mara.
Siku moja nikaambiwa niende Mwanza, na huko nitakaa wiki moja. Niliwaaga mjomba na mke wangu. Wao wakanisindikiza na kunipa matumaini kuwa nisiwe na waswasi.
‘Tutaonana mungu akipenda..’ haya ni Maneno ya mke wangu, kumbe yalikuwa na maana fulani iliyojificha.
Baada ya wiki moja nikarejea nyumbani, ilikuwa taerehe kama hii ya leo. Nilipofika nyumbani nikakuta komeo la nguvu mlangoni, nyumba ipo kama haijaishi mtu karibu wiki nzima. Nikazunguka nyumba ya jirani, huko nikapewa ufungua na kuambiwa kuwa ujumbe nitaukuta ndani. Sikuwa na wasiwasi sana, nikaingia ndani nakuweka mizigo yangu na Zawadi za mke wangu na za mjomba. Nikaziweka juu ya meza, ambayo ilijaa vumbi.
Nikaingia chumbani na kukuta barua iliyopambwa na maua. Kwa Furaha nikaibusu halafu nikasema nitaisoma baadaye, nikaenda kuoga halafu nikiwa na taulo nikajilaza kitandani, na kwa vile nilichoka sana kwa uchomvu wa safari ,usingizi ukanichukua.Niliamuka saa kumi na mbili, nikanawa uso halafu nikaichukua ile barua.
‘Mpenzi mume wangu, najua itakuuma sana , lakini imekuwa haina budi, kwani nafikiri muda ambao utakuwa unaisoma barua hii, nitakuwa nimeshafunga ndoa na mpenzi `mjomba wako’ ndani ya nchi ya wazungu. Ni mpango wa muda mrefu sana, na ndoto ya kuishi Ulaya na mtu nimpendaye imetimia.
Kwa kifupi, huyu sio mjomba wangu, ni mpenzi wangu toka shuleni. Niliamua kuja kuishi na wewe,kwasababu ya kupata pesa za kumsomesha mpenzi wangu huyu, na unakumbuka mara kwa mara nilikuwa nikikuomba pesa kuwa nawapelekea wadogo zangu kwa ajili ya ada, pesa hizo zilikuwa zikimsomesha huyu mpenzi , wangu. Yeye alikuwa akisoma hapo mlimani, chuo kikuu. Ipo siku tutakurejeshea pesa zako, usijali!
Naona nisikupotezee ,muda, najua utasikitika sana, lakini, ipo siku utampata atakayekupa pendo zaidi ya mimi, yote ni mapenzi tu.
NB. Kilichotokea baadaye, namshukuru sana Mungu, na kwa ushauri, ukipatwa na tatizo, usikate tamaa, omba mungu akuonyeshe njia. Nakiri kweli kuwa `kila jambo hutokea ili iwe sababu' huo usemo nimeupenda sana. Nikipata muda nitakuletea ilivyotokea baadaye.
Mpweke
9 comments :
Tatizo humalizii hivi visa, na unatuacha hewani, ila kwakweli huyo mwanamke sio mke, alikuwa anakuchuna, au ndio hao wanaowaita wanaume ATM.
Kwa ushahidi watu kama hawo hawadumu katika mapenzi, kwani ATM, ikiisha hela na mapenzi yameisha, na pia laana itakuwa ikimuandama! Usijali,
Tunaomba utumalizie kisa cha mwanzo, `Je wangefanya wanawake...
Stoi za hivi zinaweza kufanya mtu kuwa na machale na kila mtu!:-(
Ni kweli mdau wa kwanza, ninajitahidi sana kuzifupisha,na kama ningezileta kama zilivyo tungetengeneza kitabu.
Kuhusiana na stori ya `je wangefanya wanawake ingekuwaje' nilikuwa bado nawasiliana na huyu dada, ili animalizie na karibuni tutamalizia sehemu iliyobakia. Unajua huyu dada matatizo hayo yalimgusa sana, kiasi kwamba kila hatua akiongea hushia kulia...sasa inabidi nisimperekeshe.
Nashukuru kwa ushauri wako.
Mkuu bwana Simon, dunia hii imejaa `machale' na yote yamekeketwa hivi karibuni, na ukiyagusa, mtekenyo wake ni mchungu kama pilipili, ndio maana mguso huo unatakiwa kwa ncha za vidole, kwa machale manake.
Hakika visa vingine unaweza kucheka au sijui niseme kulia? Hivi kwani huyu mume hakwenda ukweni na kukutana na ndugu za mkewe mpaka amdanganye kiasi hicho? Jamani sisi wanawake.... ngoja nisubiri mwendelezo
Dada Yasinta swali hilo nilimuuliza mlengwa, alisema sehemu ya pili nitapata jibu, na hutaaminii utakayoyasikia kuwa kweli `hali na mali ni mhali kwenye halali'
stooooory nyingine!!
Kisa hiki ni (na visa vingine katika blogu hii) cha kweli au ni cha kubuni?
Nauliza kwa sababu niliwahi kusoma enzi zile riwaya pendwa zikitawala Bongo kuhusu kisa cha aina hii hii. Sikumbuki kama ni katika vitabu vya H.H. Katalambula, Nicko Ye Mbajo, Hammie Rajabu, Kajubi Mukajanga....
Kisa hiki kimemtokea hivi karibuni, kwa mtu ninayemfahamu, na kweli kinafanana na kisa katika moja ya vitabu vya tamithilia au hadithi, hata mimi nimewahi kukisoma.
Lakini kama ujuavyo, mtu hatunga hadithi au kisa kutokana na jamii, na utungo huo utakuwa ulitokea au utatokea kwasababu unachohadithia ni kuhusu watu, na nia ni kuelimishana au sio mwalimu Matongo na wengineo?.
Mimi nina visa vingi nimeviandika katika kitabu changu cha kumbukumbu, ambayo vimenikuta, au nimekutana navyo na baadhi tu nimeviweka katika blog hii, hasa pale tukio hilo linapotokea tena vingi ni vya ukweli, nilikutana navyo mwenyewe na vingine nimehadithiwa na watu na vichache nimetumiwa na vingine ni vya marejeo ili kufikisha ujumbe mahsusu!
Swali hili nimeulizwa sana na wadau kwa njia tofauti, na nashukuru kama ujumbe unafika.
Tuwe pamoja, ili tuweze kukiboresha kijiwe hiki na nashukuru sana wajumbe wenzangu mnaniunga mkono saana, mungu awabariki!
haya mambo yanatokea mimi nilimkuta mtoto wa dadangu kalala na mkewangu kitandani huwezi kuamini haya yanatokea
Post a Comment