Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, August 18, 2010
Ndoto ya kuolewa na mzungu
Ndoto yangu kubwa ni kuolewa na mzungu, hata nikiwa shuleni, nilikuwa napenda kuigiza kizungukizungu mpaka rafiki zangu wakawa wananichukia, ilifikia hatua hata wavulana wakawa wananidharau, lakini mimi sikujali kwasababu niliwatamani sana wazungu kuliko waafrika, sijui kwanini. Na leo hii nimesimama mbele ya watu wa kidini wakinifungisha ndoa na mwanamume wa kizungu, raha iliyoje, ndoto yangu imetimia!
Kabla ya kuolewa na huyu mume wa kizungu niliwahi kuishi na mume mwafrika na hatukuweza kuendena kabisa naye, sikupenda utumwa ule, yaani kutwa kucha wewe na mashughuli ya nyumbani, ikifika usiku upo hoi, bado mwenzako anadai haki yake ya ndoa, ndipo siku moja nikakutana na huyu mzungu, nikampenda hapo hapo, sikuchelewa kumweleza mwenzangu kuwa nimepata nimpendaye kwahiyo atafaute mwingine, nilimpa siku kadhaa nikamwaga manyanga.
Nakumbuka siku namwacha aliniomba sana tusiachane akanipigia hadi magoti, lakini sikumsikiliza, hata siku moja kabla ya ndoa yangu alikuja kunibembeleza na kuahidi kuwa atakuja kuniwekea pingamizi, lakini nilimwambia kinagaubaga kuwa simpendi na akiweka pingamizi hatafanikiwa kwasababu tulikuwa tukiishi tu hatukuwahi kufunga ndoa. Na nashukuru kuwa hakuwahi kufika kuweka hilo pingamizi na leo baada ya kumaliza fungate tunaondoka kwenda uzunguni.
Huyu ni dada mmoja ambaye nilikutana naye akiwa anajiandaa kwenda uzunguni baada ya kuolewa na mzungu ambaye alidai ilikuwa ndoto yake toka akiwa shule. Hizo ndoto nafikiri wengi wanazo, wakijua kuwa kuolewa na mzungu ni kwenda kula maisha ya raha, je kuna ukweli ndani yake, kwa wale waliowahi kuolewa na wazungu? Sijui labda kama wapo wenye uzoefu wanaweza kutuambia.
Lakini hapa swali langu kubwa je kuna tofauti gani kubwa kati ya mapenzi na upendo wa mzungu na mapenzi na upendo wa mwafrika? Ndio ubinadamu upo kuwa watu wote tupo sawa, lakini ukiingia kiundani utakuwa mila na taratibu za kimaisha zinatofautiana sana, kati ya wazungu na waafrika, na hii inaweza ikaathiri ule muonekano wa maisha ya ndoa,na mapenzi, ya kuwa huenda kwa vile wazungu wana maisha mazuri basi hata maisha ya ndoa yanaweza kuwa ya raha zaidi. Ya raha zaidi kwasababu utapata kila ukitakacho, na utaishi vile upendavyo, ni kweli au ni ndoto za Abunawasi!
Wapo walioolewa uzunguni na hatimaye kukiri kuwa pamoja na raha zote za kimaisha , hali nzuri na kupata utakacho lakini bado walikuwa wakikosa yale maisha ya kiafrika yaliyojaa upendo wa udugu, upendo wa kuombana chumvi, upendo wa kutembeleana na kupoteza muda mwingi mkiongea hili na lile.
‘Huku bwana huna muda wa kuongea na mtu, wala kutembeleana, yaani hata mume wangu akirudi kazini yupo la laptop yake, …’ mmoja wa binti aliyeolewa na mzungu alilalamika.
Ndio huenda hali za maisha yetu ya kiafrika ni ngumu,na mwanamke mara nyingi anafanya kazi kupita kiasi, hlii kwa mume anayeona inabidi amuhurumie mke wake, lakini halileti kuwa mwafrika hajui mapenzi kama mzungu, au wewe uansemaje? . Nini mapenzi, na yale maisha kwa ujumla wake na yakuwa ukiwa na raha ya kipato na maisha mazuri na mapenzi yanakuwa mazuri zaidi na mkiwa masikini na kipato kidogo mapenzi nayo ni haba? Hili linahitaji uzoefu na tafakari ya kina. Swali ni nini maana ya mapenzi!
Hebu tuliweke hewani na wajumbe wachangie licha ya kuwa limeshaongelewa sana, je kuna tofauti gani kati ya mapenzi ya mwafrika na mapenzi ya mzungu? Na kwa kusheheneza unaweza ukauliza pia Je kuna tofauti gani kati ya mapenzi ya tajiri na masikini? Ndio wengine watasema binadamu wote ni sawa, lakini tuangalie hali halisi ya uzoefu na uliyowahi kukumbana nayo kama wapo, kwa kuangalia tafsiri pevu ya neno mapenzi kwa jumla wake na undani wake! Tuwe wawazi kwa hili.
Ukiipenda hii unaweza kusoma na hizi:
http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/01/wazungu-bora-kuliko-waafrika.html
http://matondo.blogspot.com/2009/08/utafiti-watu-weusi-ndiyo-wanaongoza-kwa.html
Ni mimi: emu-three
9 comments :
Tunapozungumza mapenzi hatuangalii huyu ni mzungu au ni mwafrika, kwasababu mapenzi hujengwa na hisia za ndani , kwahiyo uwe mwafrika au mzungu utapenda au kupendwa na yoyote Yule. Utashi wa mtu ndio utakaoweza kuchagua hayo mapenzi yawe vipi.
Kiuzoefu kuwa kwasabab u umeolewa na mnzungu utapata mapenzi mazuri kuliko ya mwafrika, huo ni mtizamo wa mtu binafsi, kwani hatuji yeye anataka nini ili mapenzi kwakwe yawe anavyotaka yeye. Hii ni kusema basi mapenzi ya mtu hujengwa na mtu mwenyewe, nipendavyo mimi sio lazima upende wewe. Wewe hoja yako ni kuolewa na mzungu mimi hoja yangu ni kuoa mwafrika, kwa mtizamo wangu!
Hali za kiuchumi zinaweza kuathiri mapenzi ya mtu kutokana na mtizamo wake binafsi, kwani mapenzi kwakwe kama ni hali za kiuchumi basi yataathirika, lakini kama mapenzi kwake ni mgusano wa moyo, akili na mwili hayatathirika kwasababu ya hali za kipato!
Mimi nakubali kuwa wazungu wanajua mapenzi kuliko waafrika, kwasababu wao mara nyingi jambo hilo hawalifanyi kwa kubahatisha kama yalivyo mambo mengine. Wanapoamua kufanya jambo wanakuwa wameshajiandaa, kwahiyo matatizo yakitokea ni ya kawaida.
Kinyume chake sisi mapenzi ni kama jambo lakulazimishwa inabidi ulifanye hata kama hujajiandaa, nazungumzia kwa aina zote , mapaenzi ya kimaisha na mapenzi ya ndani!
Ipo tofauti kati ya mwanaume wa kizungu na wa kiafrika..wanawake mnajidanganya sana kuolewa na mzungu wengi wanakufanya kama ni fashion bila kuangalia consequences miaka 10 ijayo. Hawa watu hamjui kama wana ubaguzi kupita maelezo..wanawake wa kiafrika oleweni na wanaume wa kiafrika wana mapungufu yao lakini msidhani hata hao wazungu hawana mapungufu pengine wana mapungufu. Hizi ndoto zenu mzitafakari sana kabla ya kujiingiza kwenye hilo.. Hao wazungu wengi wao ndoa zimewashinda kwao wanakuja kuokota makombo period.
Unajua nilipofika hapa Marekani kwa mara ya kwanza, ilinichukua muda kuelewa ni kwa nini binti wa Kizungu ambaye nilikuwa "nahangaika" naye alikuwa hajawahi kunitamkia neno "I love you" Ni baadaye sana ndipo niligundua kwamba neno hili kwao halitoki hovyo hovyo na akilitamka ni kweli analimaanisha. Siyo kama sisi unakutana na binti kwenye daladala au mtaa wa Kongo basi kitu cha kwanza kinachokutoka mdomoni ni I love you. Hata wanafunzi wangu wanaokuja Bongo kusoma huwa wanashangaa sana wanapokutana na mabrazameni kwenye daladala na kutamkiwa moja kwa moja kwamba I love you. Huwa wanashangaa sana.
Kipindi fulani kulikuwa na binti anaitwa Aika na aliwasha moto kwelikweli kuhusu suala linalohusiana na hili. Tazama maoni yake katika post hii:
http://matondo.blogspot.com/2009/08/utafiti-watu-weusi-ndiyo-wanaongoza-kwa.html
Mapenzi kichaa! Kama unachagua basi kunauwezekano hujapenda vizuri. Ukipenda umependa na ni wengine ambao watakuwa wanashangaa kwanini una zeruzeru, Mchina au tu mgagagigikoko.:-(
Jamani mi usema kweli naona kama mapenzi ya wazungu ni ya kweli, sio cc waafrika tunaambiana I LOVE U kumbe tunang'ong'ana visogo, Mzungu akikuambia I LAV U huwa anaamanisha bwana.
Napenda sana na mie niolewe an mzungu kwa kweli, kama ntapa address ya huyo dada kwa kweli ntashukuru sana, tuwasiliane kupitia mashauc@hotmail.com
mzungu akwambie ilove you iv ivi aah wapi..inachukua muda sana
Excellent article! We will be linking to this great post on our site.
Keep up the good writing.
Feel free to surf to my page; magento responsive template
Na mimi nina ndoto ya kuolewa na mzungu nyie napataje hivi
Mnisaidie wapendwa
Post a Comment