Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 30, 2010

siri ya mtungi aijua kata

                                     
  ‘Mbona nyumba yenyewe haionyeshi dalili ya msiba’ tuliuizana huku tukiikaribia hiyo nyumba ambayo kwa taarifa tulizozipata mmiliki wake ambaye ni baba wa nyumba amefariki, cha ajabu tulipofika kwenye nyumba yenyewe tulipakuta kimya . Tukasema labda msiba unafanyika kwa ndugu yake mwingine, lakini tumjuavyo haingewezekana kwani yeye ndiye aliyekuwa mkubwa katika familia yao, na pia nyumba yake ni kubwa na yenye nafasi, ndugu zake wanaishi nyumba za kupanga.


‘Jamani kama mumekuja kwenye msiba, msiba haupo hapo upo nyumba ya jirani mtaa wa pili’ Jamaa mmoja akatuelezea na kutuelekeza nyumba ambayo msiba upo na wote tukaelekea huko tukiwaza kwanini imekuwa hivyo.

Nikakumbuka siku moja nilikuja kumuona huyu jamaa niliposikia kuwa anaumwa na hali niliyomkuta nayo ilikuwa ya kusikitisha. Alikuwa kakonda na cha ajabu alikuwa akilalamika kuwa tangu asubuhi hajapata chakula. Nilipomuuliza mke wake yupo wapi akasema ametoka tangu asubuhi na hajui alipoelekea huenda yupo kwa yao. Nikamuuliza kwanini asingefanya mpango wa chakula kwanza ikizingatiwa kuwa yeye ni mgonjwa . Akasema kwa huzuni ,

‘Acha tu ndugu yangu, siri ya mtungi anaijua kata, na jamii inayonizunguka inanilaumu sana kwa kusema kuwa mimi ndiye niliyesababisha yote haya. Lakini sio kweli mimi nilikuwa nikitimiza wajibu wangu kama mume ampendaye mke wake. Nilijitahidi kila kitu hata kumsaidia kufanyakazi za nyumbani na hili wengi walinisakama nalo wakisema nimepewa limbwata. Ndugu zangu walikuwa wakija hapa wanakuwa hawapatani na mke wangu, nikawa namtetea sana mke wangu, nikijua kuwa natetea mpendwa wangu, ikafikia ndugu zangu wote wakasusia kabisa kuja hapa, wanaokuja ni ndugu za mke wangu.

‘Yote haya niliyafanya kwa nia njema kabisa nikijua mwenzangu tupo naye. Kibarua changu kikaisha nikawa sina kazi, mambo hapo yakaanza kubadilika, mke akawa si mke tena, tukawa hatuelewani, kila nikisema sisikilizwii. Na mwenzangu akabahatika kupata kazi kwenye shirika moja nikashukuru sana nikijua kuwa ule umasikini wetu na mtihani wa kukosa kazi sasa umekwisha.

Hutaamini nilikuwa na gari imebidi niliuze ili tuweze kuishi na kumridhisha mke wangu, kwani alikuwa akinilaumu mimi kuwa siwajibiki. Nikauza kila kitu cha thamani na kubakia na hii nyumba unayoiona, lakini hela zote mke wangu alikuwa haridhiki na kila hela ikipatikana ananunua vitu visisvyo na umuhimu na pesa nyingine anazichukua na sijui alikuwa akizipeleka wapi.

‘Nikaanza kuumwa, na huu ugonjwa ulipoanza sikujua mapema, nikawa nakohoa natumia dawa za kawaida, na siku nilipozidiwa nikaend kupimwa na kuonekana nina TB, na hapo nikakata tama ya maisha, kwani ugonjwa huu ulinipata kipindi ambacho sina kazi, lakini nilijua kwasababu mke wangu ana kazi atanisaidia, lakini hutaamini kuwa alikuwa hanijali kabisa, hasa aliposikia kuwa nina ugonjjwa huu wa TB, akaamua na kunitenga kitanda, na hata chumba. Sikumlaumu sana, kwani aliogopa nitamuambukiza.

‘Kumbuka kuwa ndugu zangu walishanisusa, kwahiyo sikuwa na msaada wowote, na nilichotegemea ni huyu mke wangu kunisaidia, lakini haikutokea hivyo. Akawa haachi hela ya matumizi , na akipika chakula anakula na Watoto mimi hanijali. Watoto wangu inabidi waniibie chakula na kuniletea huku chumbani, wakigundulika wanapata kipigo kisicho cha kawaida. Nilijiuliza kwanini ananifanyia hivyo, yeye anadai kuwa mimi ni mvivu sijui kuhangaika na kazi kufukuzwa ni uzembe wangu. Kwahiyo ananifanyia hivyo ili akili ipevuke, na kuhangaika kutafuta kazi. Kazi nimetafuta sijapata, sasa naumwa nani atachukua mgonjwa.

‘Hutaamini nilitaka niuzehata hii nyumba ili nipate angalau pesa za matibabu lakini nyumba nilikuwa nimeandikisha mimi na mke wangu na katika hati za urithi niliandika kuwa nikiondoka mimi basi mke wangu ana haki zote za urithi, na utashangaa kuwa hati zote hizo alizificha sijui ziko wapi, nikimuuliza anadai hata yeye hajui zipo wapi.

‘ Ndugu zangu wameamua kunichukua, na huyu mke kaapa kuwa nikitoka hapa ndani nisirudi tena, yeye anadai hajashindwa kuniuguza. Aliposema hivyo ndugu zangu wakaogopa kuja kunichukua , lakini juzi nikapoteza fahamu kwasababu ya njaa, nilipozindukana ikabidi niwatumie ujumbe waje wanichukue, kwasababu huyu mke hana nia njema na mimi.’. hayo ndio maneno ya marehemu wakati nilipomtembelea.

Je nini kiliendelea kwenye tukio hili, ngoja niache hapa, kwani kuna mengi yaliyotokea pale msibani ambayo yana mafundisho, nitakimalizia pindi, ngoja kabla muda haujaisha niwape tukio jingine,

Ni mimi:
emu-three

13 comments :

Anonymous said...

Mnajua hivi nyie visikieni tu, kuna familia ndani zinafukuta, lakini nyie nje mnaona kama kawaida, kuna midume ikitoka nje hutazani ndani ipo kondoo,lakini kijiweni maneno mengi, akifika kwa mkewe, sawa mke wangu, nitakupa...
Hatukatai kupenda kupo lakini jua wajibu wako kama mume, nawe mke juwa wajibu wako kama mke, msitesane, kwanini mfanyiane hivyo! Ndio maana mimi naogopa kuoa

Anonymous said...

Mwanamke akiamua kubadilika anakua mnyama, anaweza kukua huku anacheka, lakini akiwa na huruma ana huruma kweli, ni wewe utakavyocheza naye, ikitegemea wewe ni wa kwanza kwake, lakini kama ulimkuta akiwa na tabia yake utakoma ubishi, vinginevyo uwe ngangari kama mimi, ukishindwa mlete hapa, mimi ndio kidume chao

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli hapo alimfanyia roho mbaya. Au ndo kama mila zetu kuwa mwanaume ndiye anayetafuta pesa? Sijui ingekuwa kinyume ingekuaje?

Simon Kitururu said...

Stori inasikitisha sana!Na inaweza kutisha mtu koua kweli kama tu anonymous wa kwanza hapo juu.

Anonymous said...

Excellent goods from you, man. I have understand your stuff previous to and you're just too great. I really like what you've acquired here, really
like what you're saying and the way in which you say it. You make it enjoyable and you still take care of to keep it wise. I can't
wait to read far more from you. This is actually a terrific site.


Also visit my website - What is an IP telephony

Anonymous said...

I believe this is among the most significant info for me.

And i'm satisfied reading your article. However want to observation on some normal things, The site style is ideal, the articles is in point of fact great : D. Excellent task, cheers

Also visit my webpage green coffee bean extract for weight loss

Anonymous said...

Do you mind if I repost a few of your posts providing I
give credit and sources back to blogger.com? My blog is in the exact same niche as your site and my readers would easily benefit from much
of the information you give here. Please let me know if this would be
fine. Regards

my web site; 82994

Anonymous said...

When I originally commented I appear to have clicked the -Notify me when new comments are added-
checkbox and from now on each time a comment is added I receive 4 emails with the exact same comment.
Perhaps there is a means you are able to remove me from that service?
Appreciate it!

Also visit my web blog :: carretillas elevadoras

Anonymous said...

Really no matter if someone doesn't be aware of after that its up to other users that they will help, so here it occurs.

Feel free to visit my blog post: Originalbugpatch.Com

Anonymous said...

A fellow blogger here, found your site via Subrion, and I have a piece of advice: write
more. Honestly, you seem like you're tailoring the entire post around the video clip. You definitely know what you're writing about, so why blow your intellect only posting videos to
your blog when you could be giving us something insightful to read?


Visit my page ... celina

Anonymous said...

Hi there to every single one, it's genuinely a nice for me to pay a quick visit this site, it includes priceless Information.

My web blog: free video sex chats (www.jajagames.com)

Anonymous said...

Ѕuρeгb blog yοu have hеre but I
was сuriouѕ about if you knew of аny discussion bоaгds
that cover the same topicѕ discuѕѕed іn thiѕ
article? I'd гeally like to bе а рaгt of
online community where I can get suggestions frοm other experіenсеd people that shaгe the samе intereѕt.
If you have any suggestions, plеase lеt mе knоω.
Kudos!

my wеbρage :: each

Anonymous said...

I think it hаd beеn thе awе-inspiring Marсel Proust who expreѕsed
thаt thе real journey оf discoνery iѕn't сonsisted of
lookіng for nеω lanԁscapes, but more іn having
neω eyes. Many thanks fοr pгοviding me ωith а new sight.


Havе а look at my web site :: Great chat nude women