Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, September 3, 2009

UONGOZI NI DHAMANA NYETI

Jamani hivi uongozi ni nini ? Hili swali nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara na leo tarehe 3-09-2009 nikaona niliweke hewani. Najua kila mmoja atakuwa na jibu lake zuri kutegemeana na anavyooona yeye, na wengi watajibu kutegemeana na utashi wake binafsi na hasa ni nini kiongozi angefanya ili afanikiwe katika malengo yake.
Uongozi ni dhamana kubwa sana, nafikiri katika dhamana kubwa hii ni mojawapo kwa nionavyo mimi. Kwa wale waliojaliwa kuwa na imani wanaogopa sana kuibeba dhamana hii, lakini kwa upande mwingine ni lazima kwa wale waliojaliwa kuwa na kipaji cha uongozi waibebe dhamana hii nyeti. Waibebe dhamana hii kwa wito na sio kwa tamaa.
Katika maisha ya kila siku tumeambiwa kuwa kila mtu ni mchunga(kiongozi) na utaulizwa kwa kile ulichokichunga. Kama ni mzazi mke au mume utaulizwa kuhusu familia yako, na hata kama upo peke yako, bado kuna mambo ambayo unahitajika kuyachunga nayo utaulizwa jinsi ulivyoyachunga. Sembuse wewe uliyepewa dhamana ya kuongoza jamii ya watu wengi maswali yake yatakuwaje. Jaribu kufikiria eneo dogo kama kijiji,hapo kuna matatizo,mangapi,kuna mambo mangapi wewe kama kiongozi ulitakiwa kuyafuatilia, au kuyafanyia kazi,na bado hayajafanyiwa kazi. Kumbuka kuna watoto yatima wangapi, masikini wangapi, wagonjwa, wangapi ambao kwa uongozi wako ulitakiwa uhakikishe wanapata haki yao,lakini kwasababu moja au nyingine wamekwazika. Je wewe kama kiongozi unaweza kuikwepa lawama kama hizi hasa za vilio vya watu kama hawa.
Nawasikitikia sana wale watu wanaodiriki hadi kuhonga ili waibebe dhamana hii, ama wanafanya hivi kwa kutokujali ili watosheke na sifa ya kuwa kiongozi na pia kubwa zaidi ni kupata kipato kwa kupitia mgongo wa dhamana hii nyeti. Ole wenu sijui mtasemaje mbele ya muumba, wakati jamii hizi zitakapoleta kilio chao wewe ukiwa kama mshitakiwa. Na sijui utajiteteaje wakati wewe uliahidi na baya zaidi uliununua huo uongozi kuwa utaubeba huo mzigo wa dhamana. Sawa wengine hawana imani za kidini na wanaiona dunia kama sehemu ya matanuzi,lakini kumbuka ipo siku.
Nawashauri wale ambao kwa nia njema wameamua kuubeba huu mzigo wa dhamana ya uongozi wajaribu kufikiria mbali, kwa kuangalia mifano inayomzunguka yeye mwenyewe, mfano mtoto wake anapoumwa jinsi gani anavyojisikia, ajaribu kukaa na njaa aone jinsi gani njaa inavyouma, ajaribu kutembea kwa miguu masafwa marefu aone jinsi gani adha hiyo ilivyo. Na kwa mitihani kama hii midogo aisogeze akilini mwake kuwa hiyo ni sehemu ndogo tu ya matatizo wanayoyapata raia wake. Je atajielezaje mbele ya muumba wakati tumeambiwa kiongozi ataulizwa hata ile mifugo iliyopenya na kuharibu mazao ya mwenzake!
Dhamana ya uongozi ni nyeti na kwa uoni wangu mdogo ilitakiwa wananchi wenyewe wakuteua kuwa wewe unatufaa uwe kiongozi wetu, sio wewe ujitokeze na kusema mimi ninawafaa. Wenzetu walikuwa wanabembelezwa kushika uongozi wanakataa, lakini sisi tunautafuta kwa udi na uvumba. Kweli tunautaka uongozi huo kwa nia njema?
Mimi nina imani kama viongozi wangeibeba hii dhamana ki-imani, kusingekuwa na matatizo duniani. Ki-imani nikiwa na maana kuwa kiongozi huyu angetakiwa awe kwanza anaangalia watu wake kuwa wameshiba kabla hajaanza kula yeye. Je ni nani anayeweza hivyo. Kumbuka kuwa `kila mchunga ataulizwa kwa kile alichokichunga, siku hiyo ikifika'

From miram3.com

No comments :