Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, July 11, 2017

DUWA LA KUKU....9Mume wangu nilimpenda sana,…utaniuliza kwanini natumia neno ‘nilimpenda,..kwanini sasa nashindwa ‘Ninampenda…’…sijasema simpendi, lakini kama binadamu kuna matendo ambayo yakitokea ukayashuhudia hata kama ulikuwa na moyo wa chuma, utabadilika tu…yanaumiza na kutesa sana, na baya zaidi ni pale unapomuuliza mwenzako, akakataa, na hata kukufanya wewe umechanganyikiwa.

‘Sijasema hivyo, ni wewe tu mke wangu…’mume akasema lakini mke hakutaka kubishana naye akaendelea kuongea.

‘Wazee wangu ,…sijui niseme nini, najua mungu anajua kilichopo moyoni mwanagu na machungu ninayoyapitia, maana mwanzoni nilipoona hayo kwa macho yangu,  niliumia sana, ikafika muda nikasema basi labda,..labda,..nisamehe tu, na nikajitahidi kufany ahivyo…, japokuwa moyoni nilikuwa naumia, lakini ilipojirudia tena na tena, nikasema sasa basi, kama mimi nina moyo wa chuma basi chuma hicho kimeshashika kutu….mimi siwezi tena kuvumilia…’akasema.

‘Mume wangu nampenda sana haya yeye, analifahamu hilo…’ akatulia pale mume wake aliposema

‘Hata mimi nakupenda sana ni wewe….’akasema na kutilia.

‘Kumpenda kwangu huko kulinifanya nikosane na wazazi wangu, hadi hii leo, ni wao kwa tatazo kama hili wangelifika hapa kunisaidia, lakini wapo wapi, huko walipo wakisikia haya, watasema, ‘’tulikuambia,..’ lakini ningefanyaje, na ili hali mtu nilishampenda. Namshukuru sana baba yangu huyu mkubwa, alinielewa, na mpaka sasa ananilewa..yeye ndiye aliyesimamia ndoa yangu, baada ya wazazi wangu kunisusia.

 Pamoja na yote, wazazi ni wazazi tu, wao walitupatia hii nyumba, na uone ajabu baba aliindikisha kwa sote wawili, ndio maana mwenzangu nikimtishia kumfukuza, ananijibu kwa jeuri kuwa nyumba hii ni yetu sote, lakini anasahau kuwa nyumba hii ilitolewa na wazazi wangu, na wao wanaweza kumuondoa yeye, kama…haya watakuja kuyafahamu, hilo halijui…sawa kisheria ipo hivyo, nyumba imeandikishwa kwa sote wawili,  lakini sheria nayo inaangalia sheria za ndoa, huwezi ukavunja sheria za ndoa, na sheria ikakubeba tu….’akasema.

‘Lakini nani kavunja sheriza ndoa mke wangu…?’ akauliza na mkuu wa dini akasema;

‘Usimuingilie muache aongee….’akasema.

‘Samahani wazee, haya ngoja tumsikilize…’akasema.

 ‘Najua baada ya haya yote, anajua nitamfukuza humu ndani…, lakini hata hivyo, ni nani angeliweza kuyavumilia hayo yote… natamani nisiyaongee maana kuyaongea zaidi ndio nazidi kujiumiza, lakini kwanini niendelee kunyamza wakati mwenzangu ananiona mimi ni ninaota tu, eti naota, sio kweli…hivi kweli mimi nimzushie uwongo mtu niliyempenda ikafikia hadi nitengane na familia yangu, kwanini nifanye hivyo…’akasema na kutulia kidogo.

Mwenzangu amesahau tulipotoka, amesahau, nilivyojitolea kwa ajili yake, nilifikia hadi kuiba pesa kwa wazazi wangu au kudanganya, ili tu nimpatie ada aendelee kusoma, na hata alipofika chuo kikuu, tukiwa pamoja naye, alikuwa hana mbele wala  nyuma, mimi nilikuwa namfadhili, aseme ukweli wake kama sikutafanya hayo kwa ajili ya upendo wetu, leo hii kafanikiwa, maana hana tatizo, tena, ana kazi nzuri, kipato kizuri, na nasikia kaanza kujenga nyumba yake, haniambii, nasikia kwa watu tu, mimi siwezi kumuingili huko.

‘Hilo nalo jipya….’akasema mume wake, na alipokumbuka kuwa kaambiwa asiingilie akatulia kwa haraka.

‘Hayo sio muhimu sana kwa leo, maana anaweza kusema hayo yliyokuwa ya kale, zilipendwa, sasa umezeeka, nataka damu mpya, kwasababu mume hazeeki, sawa, ..ni kweli mimi nimezeeka, hayo ya mapenzi ya ujana mimi sina tena, sina …nasema kweli sina..na sitaki tena kuendekeza mambo hayo.., ndio maana nilimpa uhuru wa kufanya pendavyo, lakini sio ndani ya nyumba yangu…’akatulia

Hayo nilimuambia mapema tu, akasema mimi mzushi, …nikamwambia ipo siku nitakuthibitishia hilo, na kweli nikaja kuyaona , sasa ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kaamua kunikomoa …hivi kweli mimi ni binadamu gani wa kuvumilia haya, na bado namuuliza hataki kusema ukweli, nitamsaidiaje mtu kama huyu…’akawa kama anauliza

‘Haya basi kama kaona mimi simtoshelezi, kama kaona anahitajia damu changa, basi aniambie tu…mimi  nitamsaidia hata kumtafutia mke mwenza anayefaa, sio kutembea na wafanyakazi wa ndani,…’akatulia pale mume wake alipotaka kuingilia . Mume akatulia hakusema neno.

‘Mimi naweza kukubali aoe tu…lakini iwe kwa utaratibu mnzuri na makubaliano…, yeye akasema hayo najitungia tu mimi mwenyewe kwa vile simtaki, kwa vile nataka yeye aondoke kwenye hii nyumba, kwanini kila kitu anarefaa kwenye hii nyumba, hii nyumba ni nini jamani...’akasema akionyesha nyumba.

 ‘Siyasemi haya kwa kujionyesha kuwa sisi tupoje, labda nafanya makosa kutoa siri hizo, lakini sasa nifanyeje, ni lazima niwaambie nyie wazazi wangu ili mfahamu hiki kinachoendelea humu ndani,  ili muone je hii ndoa kweli ipo au ni geresha tu…’akawaangalia wazee wake.

‘Huyu mume wangu nilimpenda sana, nay eye alionyesha kuwa ananipenda kwa vile, sasa naanza kufahamu ni kwa vile alihitajia kitu, na sasa kakipata, …sasa sina thamani tena kwake, naomba mnisaidia sana, kwa hili, labda mimi nimkosaji, kama nimekosea, basi mje mniambie, lakini hapa ilipofikia, siwezi kuvumilia tena…’akatulia
‘Mke wangu jamani..usiseme hivyo….’mume mtu akasema kwa sauti ya huruma.

‘Sisemi hivi kwa vile utasema mimi najivunia wazazi wenye uwezo, hapana, mimi sasa hivi sitegemei wazazi wangu, nilishajitoa kwao, na nilishajipanga kuishi maisha yangu bila kuwategemea wao, na ndio maana pale tulipopewa hii nyumba nilikataa,….unakumbuka mimi nilikuambie tutafute chetu, tuanzie nyumba ya kupanga, wewe ukanishauri nikubali tu, mpaka hapo tutakapojenga nyumba yetu, sasa…kipowapi,….’akageuka kumuangalia mume wake.

‘Ongea tu, ongea kila kitu, ila mimi nataka ushahidi, maana umeamua kunivua nguo mbele ya watu, haya endelea….’akasema mume wake kwa sauti ya huzuni.

‘Ni mimi nakuvua nguo au ni wewe umejivua nguo mwenyewe kwa tamaa zako za mwili, umejishushia hadi wewe mwenyewe japokuwa hutaki kuukubali ukweli….’ akauliza
‘Samahani wazee wangu, ngoja nimuulize swali…?’ akasema na wazee wakakaa kimia tu, nay eye akasema.

‘Mke wangu wewe unasema niimejitakia kwa vipi fafanua hapo ili na mimi nielewe,…wewe unazunguka, unaelezea mengi ya zamani, nia yako ni nini,kuwa mimi nilikuwa mtoto wa mitaani, ukanisaidia, na kufikia hapa, au sio, sawa ni kweli, nakubali hilo, na nakushuruku sana, lakini hili la kuniambia mimi nakusaliti, siwezi kulivumilia, niambie wapi , na nani nilifanya naye hivyo…, hilo tu…tusizunguke saana…’akasema.

‘Huko nitafika, maana hata mimi nashangaa baada ya kuongea na wewe na kukuelezea kuwa ninao ushahidi bado huamini, bado unaniona nakusingizia, hapo natilia mashaka,…wewe una tatizo, haupo sawa, sio yule mume niliyemfahamu kabla… ningekuwa mshirikina ningelisema wewe kuna kitu wamekuwekea, lakini mimi sio mshikirina na siamini mambo hayo, huo ni ulimbukeni wako tu…’akasema.

‘Sawa..sasa si useme,…unaogopa nini…unajua mke wangu kwanini hujiulizi, kwanini mimi nijiamini kiasi hicho, ..utakuja kuumbuka mwenyewe, …nakuatahdharisha mapema..’akasema.

‘Nitasema, leo nitasema kila kitu, na ..ushahidi ukitaka nitauonyesha, kama upo tayari wazazi hawa wauone uchafu wako mimi nitauonyesha, kwasababu mimi nilishauona, unatia kinyaaa…sasa sijui baada ya hilo utakwenda wapi, utaficha wapi hayo macho yako yenye aibu, nakuonea huruma jinsi gani utateseka…’akasema.

‘Hahaha, mimi au wewe…wewe ndio utaumbuka, kwa kuwapotezea hawa wazee muda wao,..maana sijafanya kitu jamani, wewe unakisia tu,…kama kweli huo mkanda wa video ulichukua hali halisi iliyokuwepo,…kuwa mimi nilikwenda mle ndani kuhakiki…maan nina haki, kelele zilisikika na mimi nakaenda kuhakiki, ..hao ni watoto wangu, …haya onyesha, labda uwe umetengenezwa huko mitaani…’ akasema kwa kujiamini.

‘Mume wangu nakuomba tena utubu madhambi yako, tuone ni nini cha kufanya, nakuuliza tena mbeel ya hawa wazee je hukufanya hayo madhambi…?’ akaulizwa.

‘Sijafanya ndio maana mpaka sasa naendelea kupinga, mimi sijafanya hayo madhambi unayoyasema wewe, huo uwongo na uzushi…kama ni kweli toa huo ushahidi wako..’akasema.

‘Kwanza, kabla sijaendelea na hilo, niwaulize nyie wazee, na kiongozi wetu wa imani, je nikifanya hivyo nitakuwa nimekosea…?’ akauliza mama mwenye nyumba.

‘Ukifanya vipi..?’ akauliza kiongozi wa dini.

‘Nikitoa huo ushahidi unaonyesha ukweli wa haya yote, maana unaonyesha matendo yasiyofaa, kwa mume kama huyu , mzee kama huyu,..…maana sio mnzuri kuangalia, na ..sikupenda iwe hivyo, kama angelikubaliana na mimi, basi ningeona jinsi gani nyingine ya kufanya, ili ajifunze, na dunia ingemfunza tu…’akasema.

‘Kwanini unazunguka kwanini mpaka uwaulize hao wazee kuwa utoe au la…wa kuulizwa ni mimi, kama ni aibu si zangu mimi au sio..,..nimeshakuambia mimi nipo tayari, kuuona na kuwasikia hao mashahidi wako, waite mmoja mmoja waseme ukweli hapa mbele ya wazee, kama kweli watasema ukweli, lakini kama ni wao ni waongo, haya tutawasikia…’akasema.

‘Mhh…haya, kwanza nimuulize huyu binti ambaye yupo hapa, asema ukweli wake, yaliyotokea humu ndani, je ni kweli hajawahi kufanyiwa mambo yasiyo faa, maana nisiende mbali, wewe binti, unamuogopa mungu wako,niambie ukweli kinachoendelea humu ndani..na ukumbuke, kama utaficha na ikatokea tatizo, ujue mimi sitakuwa nawe tena,….’akasema akimuangalia huyo binti.

‘Je ulishawahi kufanyiwa matendo yasiyofaa..?’ nikaulizwa , nilitarajia hivyo, lakini hapo akawa kaniwahi , bila kujiandaa, hapo nikajikuta natokwa na jasho jingi mwilini nikakaa kimia kwanza na yaliyokuja kichwani ni yale maneno ya kijana ya kunitahdharisha nisije kuvunja ndoa ya watu.

‘Binti hebu ongea ukweli, usiogope..’akasema mzee

‘Mhh..hapana mimi sipo tayari kuongea lolote, nahitajia muda hivyo..’nikasema.

‘Kwanini..unahitajia muda gani, wa kusema ukweli, sema ukweli kilichokutokea, unaogopa kusema ukweli, au unamuogopa baba mwenye nyumba..?’ nikaulizwa.

‘Kwasababu yote nayaona kama ndoto, sina uhakika…na naogopa kuja kusema uwongo, kumbe ni ndoto tu, mimi sijui, ..’nikasema.

‘Kwani hiyo ndoto ilitokeaje..?’ nikaulizwa

‘Kiukweli tangu nifike hapa nyumbani nimekuwa nikitokewa na vitu vya kutisha…’nikasema

‘Ukitokewa kwa vipi..?’ akaulizwa.

‘Huwa naota ndoto za kukabwa, na….’hapo nikasita kuendelea kuongea kwa kuogopa kuelezea mambo kama hayo mbele ya watu wazima.

‘Mnasikia, anafanya nini..anaota, ndoto zinatokea wapi…jamani tusaidianeni hili ndoto hutokea kichwani akilini, sio matendo…..’akasema baba mwenye nyumba.

‘Tulia,….’akasema kiongozi wa dini

‘Ongea ukweli, sisi tunataka kusaidia hili jambo…tumekupa nafasi hiyo, usiogope kutuvunjia wazee heshima kwa maneno yasiyofaa kuongelewa,…nia hapa ni kuwasaidia hawa wana ndoa wawili na nyie pia…, hatutakubali ndoa hii ivunjike, tunajua jinsi gani ya kuliweka hili jambo sawa sawa, nimegundua kitu hapa, lakini siwezi kukisema mpaka nipate maelezo zaidi yenye uhakika….’akasema mkuu wa dini.

‘Mimi kwakweli nashindwa kuongea maana naota tu, kuna vitu vinanikaba, mwili unaisha nguvu kabisa siwezi hata kugeuka, siwezi kufanya lolote ….ni majinamizi sijui….nahisi kama kuna mtu ananishika kwa nguvu, ananikaba, nakosa pumzi, hata kupiga kelele siwezi, nalegea mwili mnzima, nahangaika wee, na ..inafikia sehemu nahisi kama nazalilishwa,..nafanyiwa vitendo vibaya…’nikasema

‘Unazalilishwa kwa vipi, usiogope kufafanua …?’ akaulizwa

‘Nafanyiwa vitendo vibaya,…’akasema

‘Na nani…?’ akaulizwa

‘Simjui , maana simuoni, nahisi tu, sioni kitu, nahisi kwenye njozi tu….’akasema

‘Je kwa hali kama hiyo ya kuzalilishwa, ukiamuka unajiona kweli umefanyiwa vitendo kama hivyo..?’ akaulizwa

‘Aaah…,mimi siwezi kujua, maana ni vitu nimekuja kuvionea huku,…na sijui una maana gani kwenye hilo swali,…, na wala sijui nijibuje..…naona kama ndoto tu ndicho ninachoweza kukisema, lakini nateseka, sijui kwakweli…’akasema.

‘Imetokea hivyo mara ngapi..?’ nikaulizwa

‘Kwa kuzalilishwa, mmh, mara nyingi tu, sijaweza kupata amani labda nikiwa kwenye siku zangu, mara nyingine naweza kukabwa tu, nikasumbuliwa wee, aah, hata sielewi ni kitu gani na kinataka nini .…’akasema

‘Na ndio maana yule binti wa kwanza, ilimtokea hivyo mpaka akapata mimba, huyu mume wangu mwenyewe akamsaidia kuitoa, anabisha na hilo…’akasema mama mwenye nyumba.

‘Nani..mimi, wewe….hebu sema ukweli hapo…wewe mwenyewe unajua ni kwanini tulifanya hivyo, na wewe ndiye ulinishauri tufanye hivyo…., kama ningelikuwa na nia mbaya kwanini nikakushirikisha..?’ akauliza baba mwenye nyumba kama anashtuka!

‘Ulinishirikisha kwa vile alishaamua kuja kuniambia ukweli, ukaona ili ujikoshe, uje kuniambia kuwa mumesingiziwa wewe na mtoto wangu, nikaona sasa hayo yatakuwa makubwa, na sifa ya familia yetu itaharibika, ndio maana nilikukubalia ombi lako…’akasema mke wake

‘Mke wangu, mke wangu, ombi langu au ombi letu,..usikwepe hapo kabisa, umeamua kulisema hilo , basi liseme vyema, wewe ndiye ulipendekeza hilo la kutoa mimba, kweli si kweli, tutakubaliana tufanye hivyo, kweli si ikweli, sasa unajifanya kuogopa kusema ukweli eeh, sema ukweli wako, unaogopa nini sasa, muone jinsi mke wangu alivyo…’akasema.

‘Ninajua ni wewe uliyempa mimba binti wa watu, kwasababu nilikupenda, nikaona tuhakikishe hilo jambo halisambai, na wewe ukaniahidi kuwa utajitunza, ukasema kama ni kweli hutarudia tena…’akasema mke wake.

‘Wewe mwanamke sema ukweli wote, mimi nilikuambia kama ni kweli,…nilitamka hivyo,…mimi nilikuambia sio mimi, na kama ni kijana wetu basi amuoe, wewe ukasema kijana wetu hawezi kumuoa mtu kama huyo,  kweli si kweli…na kijana wetu kuna kipindi alikuwa hana raha, tulipomuhoji alionekana kuwa na mashaka, tukahisi ndio yeye kafanya hivyo, ndio maana tukakubaliana na hilo..inatakiwa hapa useme ukweli wote, muogope sana mungu kwa kuzua uwongo....’akasema mumewe.

‘Wewe ndio umuogope mungu wako, hutaki kuukubali ukweli ukasaidiwa…wewe una tatizo, mume wangu wewe una tatizo, kwanini usikubali ukasaidiwa,…mimi nahsi kuna kitu kimekutokea, sio bure…’akasema

‘Hahaha, huna jipya wewe…mimi ndio mwenye tatizo au ni wewe…wewe una tatizo, unaingiwa na akili ya kuzua mambo, unahitajia kusaidiwa, ….na kauli yako hiyo naona inaanza kukugeuza mtizamo wako, wa kuamini mambo kishirikina,…umempata wapi mganga wa kukudanganya, ?’ akauliza

‘Mimi naona tunapoteza muda hapa…’akasema mkewe.
‘Wewe ndio unapoteza muda,  na nakuambia sasa,  mimi leo hatumalizi hiki kikao mpaka uutoe huo ushahidi wako unaosema unao,…nimechoka kuzalilishwa na kauli zako zisizo na ukweli, …’akasema.

‘Ushahidi si ndio huo kwanza kwa huyu binti anapatwa na kitu gani, …na ni nani anamfanyia hivyo,na sisi tupo humu ndani wa ngapi…?’ akauliza.

‘Kwahiyo na hili pia, unataka kumsingizia hata mwanao au sio,..?’ akauliza.

‘Sijamsingizia mtoto wangu, na kama na yeye anafanya hivyo, ni wewe umemfundisha, maana alishaniambia…yanaoyoendelea humu, ila anakutetea, sasa umemsikia huyu binti alivyosema, kuna mtu anamkaba usiku, na kitendo hicho kinafanyika lakini anashindwa kujigeuza,…au kuona kuwa ni nani, sasa ni nani angeliingia humu ndani na kufanya hivyo, wakati tumefunga mlango, ni nani kama sio wewe…?’ akaulizwa.

‘Na mwanangu sio..?’ akauliza

‘Sijamsema mtoto wangu maana hata ushahidi huu nilio nao, unakuonyesha wewe peke yako, ukiwa na huyo binti…..’akatoa kanda ya video kwenye mfuko.

‘Unakuonyesha wewe….ukiwa na yule binti aliyeondoka mkifanya uchafu wenu,…si unataka tuuonyeshe huo uchafu wako mbele ya wazazi,..na utaabika kweli ukionekana…’akasema na hapo mumewe akabakia kimia akikodoa macho kuaangalia huo mkanda.

‘Wewe mwanamke umefikia hapo..umeupatia wapi huo mkanda?’ akauliza

‘Kufanya nini, si unataka ushahid wa video, wewe ulifikiria natania, sasa mkanda ni huu hapa, nionyeshe wauone wazazi wako…?’ akaulizwa

‘Kwanini nilikuambia unionyeshe huo ushahidi awali, ukakataa, ..sasa unautoa mbele za watu…’akasema mme mtu sasa akionyesha mashaka.

‘Swali je ni kweli ulifanya..?’ akaulizwa

‘Sijafanya..sio kweli na huo mkanda kama ni kweli utakuwa umeutengeneza huko na hao watu wako,…mimi nayafahamu hayo sana..siku hizi vitu kama hivyo vinafanyika…ila mimi bado nasema sio kweli, …kama ulichukua matendo halisi, basi hakuna cha maana kitakachoonyeshwa, mimi sijafanya madhambi hayo..’akasema, lakini sasa sauti ilikuwa sio ya kujiamini kama awali.

‘Nakuuliza tena mume wangu ..nakupenda sana, kwani  hayo yatakayotokea baadae hutaaamini, baada ya hili, basi tena, …maana ni aibu kuonyesha mbele ya wazazi hawa, kitu kama hicho…na mimi sitakuwa radhi kuendelea kuishi na wewe…’akasema.

‘Kwanini unanitisha maswala ya kuachana…, kwanini hutaki kuutoa huo ushahidi, huyu binti hapa ulisema ni shahidi yako kakataa, kasema ni ndoto tu, sasa hebu niambie ninaingiaje kwenye huo ubongo wake,…akilini mwake… na kuyafanya hayo anayosema anayaota, au unanishuku mimi ni mchawi, niambie…’akasema

‘Huyu binti, hawezi kusema maana hana uhakika, yeye anahisi kaota, lakini sio kweli, hayo yaliyomtokea ni kweli,..nilimdadidi akasema aliona hiyo athari mwilini mwake..hawezi kuyasema hayo hapa.. ninachojiuliza iweje,…ifanyike na yeye ashindwe kuzindukana, ina maana kuna kitu anafanyiwa, mpaka anashindwa kuzindukana, sasa ni nani anamfanyia hivyo…’akasema

‘Kwahiyo mimi ndio namfanyia hivyo…?’ akauliza baba mwenye nyumba kwa sauti ya kutahayari.

‘Hapo mimi sijui ni wewe au ni nani, ndio maana nikakuuliza na kama hutaki kukubali ukweli, basi tutafute njia za wewe kukubali, na kama hawa mabinti wengekubali kushirikiana, basi tungelishalimazlia hili,…’akasema na mumewe akatikisa kichwa, na kugeuka kumuangalia huyo binti, akauliza akimuangalia huyo binti;

‘Wewe binti uliwahi kuniona nikiingia chumbani kwako usiku kama anavyodai huyo mama yako, sema ukweli wako wala usiogope, maana kikao hiki ni cha kusaidiana, na ukisema ukweli, siwezi kukufany alolote, mbele ya wazee hawa, sema uliwahi kuniona nikiingia chumbani kwako usiku na kukufanya hivyo, inavyodaiwa, kuingia sikatai, niliwahi, lakini je niliwahi kukugusa, …?’ akauliza

‘Hapana….mimi sijawahi kumuona....hata kukuona ukiingia kama unavyodai kuwa unaingia usiku, kiukweli tangia nifike hapa sijawahi kukuona ukiingia chumbani kwangu usiku, nasema hilo kiukweli wangu,…, maana huwa nimelala,..huwa ninakuwa na usingizi mnzito, isingelikuwa ni hayo majinamizi.. kwahiyo mimi …siwezi kulithibitisha hilo…’nikasema na wazee wakamgeukia mama mwenye nyumba ili aendelee

Na baba mwenye nyumba akasema;

‘Umesikia…..jamani mumesikia wenyewe, ….shahidi wa kwanza kakukana, haya tafuta ushahidi mwingine, au unataka kuonyesh hiyo kanda kwanza, mimi ningelishauri, …tunampigie huyo binti mwingine au sio..mimi nataka tulimalize hili kwa amani,  ili tuone ni nani mwenye matatizo, ni mimi au ni wewe….’akasema mume mtu huku akianza kupiga simu kumuita huyo binti mwingine.

NB: Ushahidi utaendelea sehemu ijayo..je binti atakubali kuja, au utaonyeshwa ushahidi wa video,

WAZO LA LEO: Kila mtu ana udhaifu wake, na udhaifi mwingine unakuja kuwa ni ugonjwa mtu asipokubali kusaidiwa, kuna watu wanaingia kwenye ulevi wa pombe au sigara, au kwenye matatizo fulani,  kumbe ni kutokana na misongo ya mawazo!

Wengi wao, wangelikubali kusaidiwa huenda matatizo hayo yasingelifikia huko. Kama wewe ni mke wa mtu, au mume wa mtu, jaribuni kukaa na mwenzako, muongee matatizo yenu, kuliko kuyaweka kichwani, au kuanza kutafuta njia zisizo halali , eti kuondoa mawazo…ikishikindikana watafuetni wazee wenye busara, mpate mawazo ye hekima na busara!
Ni mimi: emu-three

No comments :