Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, May 20, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-32


 Mimi nikiwa kwenye sehemu ambayo nimekuwa kama nimegandishwa, niliweza kusiki akile kinachoongelewa kwenye sehemu nyingine ya chumba na kwa muda huo niliweza kumsikia binti akipambana na hao watu kwa maneno, akilalamika kuwa wamuachie…na mara huyo kiongozi wao akasema kwa sauti kali;

'Muda umekwisha, ...mleteni huyo bint huku, tusipoteze muda….na mara kukawa na vurumai baadae akaletwa …niliweza kusikia sauti lakini sikuweza kuwaona na iliyonisaidia ni kuwa mlango ulikuwa umefunguka kidogo, lakini kufunguka huko siwezi kuona huko walipo, na siwezi kusogea hapo nilipo…

 Na mara kukasikika sauti ya binti akilia, akiomba asifanyiwe huo ubaya, na wakati analalamika ndio kukasikika sauti nyingine, ilikuwa ni sauti ya kike, lakini yaonekana ni sauti ya mama hivi;

‘Subirini kwanza…’ilikuwa sauti ya kike lakini sio ile ya binti…

‘Wewe….unataka nini huku…’sauti ya huyo kiongozi ikauliza.

‘Achani, mnataka kufanya nini…?’ akauliza

‘Haya hayakuhusu wewe..rudi huko ulipokuwa…’akaambiwa.

Na mara huyo binti akawa analalamika, kuomba msaada zaidi

Tuendelee na kisa chetu….

****************

'Sitaki jamani, nimechoka…, niacheni, mnaniumiza...najua mnataka kuniua, kwanini lakini, ....sitaki...mama upo wapi,…mama jamani …baba …oh, nimewakosea nini hawa watu, kwanini hivi jamani, niacheni jamani..’ilikuwa sauti ya binti.

Huyo binti yawezekana ana miaka kama kumi nane hivi, kwa makisio yangu kwa kukisia sauti hiyo lakini sina uhakika maana sikuwa namuona sura yake, kiukweli alivyokuwa analia,…nilimuonea huruma sana, mpaka nikatamani niende huko nikajaribu kumtetea, lakini nikuembie ukweli, pale nilipo nilikuwa kama nimenatishwa.

‘Hivi ndio inatakiwa alie, ili shetani wetu, afurahi…inaniuma hata mimi lakini tutafanyaje….’ilikuwa sauti ya huyo mwanaume. Mara kukasikika kitu ama vurumai, baadae ikasikika sauti ya watu wanazozana, sikuweza kujua ni nani..lakini kulikuwa na sauti nyingine ya kike.


'Mshikilie...unafanya nini sasa..mlete hapa, …kwanini, …mnashindwa kumshika huyo binti,….hahaha, sitaki kumlegeza kwa madawa, shetani wetu anataka asikie kilio,…manunng’uniko, hayo ndio yanampa raha….halafu damu yake….hahaha…’ilikuwa suti ya huyo mtu.

 Ikatokea tena sauti ya kuzozana, …baadae sauti hiyo ikapaa hewani, na kusikika vyema, ikasema;

'Hawezi kuja hapo, nimechoka na haya machafu yako, wewe si ndugu yangu tena, na sitaki kuwasikiliza na kufuata haya mauchafu yenu, sitaki sitaki, nilishakuambia sitaki, kumbe ndio hii kazi unafanya,…hapana,wewe ni shetani….’ilikuwa sauti ya mwanamke, anaonekana ni mtu mnzima.

'Unataka kufanya nini dada,….unapoteza muda, kwanza ni nani kakuambia uje huku,…hii kazi ni ya wanaume, na …nakujua wewe hutaweza kuvumilia,…na muda unakwisha dada,…unaona sasa imebakia dakika tano tu, tusipofanikiwa hili, basi, mimi au wewe damu yetu itahitajika..upo tayari kufa eeh, hebu niambie..’akasema huyo mwanaume.

 'Mimi sijali kufa,..kama mambo yenyewe ndio haya, ..hapana ni bora kufa tu, na nimegundua ni wewe utakwua umemuua mwanangu…nimeshajua hilo,..na huyo binti yangu mwingine yupo wapi…unataka na yeye umuue au sio…kwanini unakuwa mnayama , shetani…’sauti ya kike

'Bint yako yupi..yule hatuna kazi naye, nilishakuambia, hatuna kazi naye, kazi yake uliiharibu wewe..sasa hivi tungelikuwa tumemaliza kazi…sasa unanipa wakati mgumu,.huyu binti wa watu hakustahiki kuwa hapa….unaona …sio kwamba mimi napenda…’akasema huyo mwanauma

'Usinifanye mjinga, niambie binti yangu yupo wapi…’akasema

‘Jamani binti yake yupo wapi,… niliwaambia huyo binti hana kazi tena kwetu,  arudi kwao, sasa…mlifanya nini..?’ akauliza na kukawa na ukimiya baadae akasema;

‘Dada nasikia ni watu wenu…muulize huyo anayeitwa docta,…huyo mtu mbaya sana, na ole wake, ngoja tumalizane na hili…huyo ni adui yetu, mkimuona msisite kuvuta trigger…maliza, ua..mumesikia, mtu atakayelata kichwa chake hapa nitampa dola elifu kumu, mumesikia…’akasema na kukawa na kama vurumai halafu sauti ikasema…

'Dada kuhusu binti yako mkubwa, nilikuambia wazi alijiua kwa sumu…hayo ni majanga uliyojitakia wewe mwenyewe, hukutaka kufuata niliyokuambia,…sikuwa na jinsi ya kuweza kumsaidia, ..hata hivyo, siku zake zilishafika au sio jamani…’akasema na kukawa na ukimia.

'Unafikiri mimi mjinga eeh…najua kabisa wewe uliamua kumuua kwa mbinu za sumu, kisa unataka mazindiko yako yafanikiwe,…na shukuru mungu huna watoto, ungekuwa nao ..ungelijua uchungu wa mtoto, usingelifanya hivyo…’akasema mwanamke.

‘Sikiliza dada mimi nakuheshimu sana, ndio maana nikakutaka uwe mwenza wa kazi hizi, ningelikuwa na roho mbaya nisingeku…lakini wewe huna shukurani, mali zote hizo nimekuambia ni zako..nyumba hii ni yako…mumeo, hana kitu tena…lile duka la..super market ni lako…..huyo ndugu yako ni…usitake niseme mengi…’akatulia.

‘Kwanini mnapoteza muda..huyu mchukueni mrudisheni huko chumbani, tukimaliza kazi atakuja, najua dawa yake ni nini..na kama unaleta ubishi dada…, mtoto wako hutamuona tena, nakuambia sasa ukweli..unanijua nilivyo…’akasema kwa ukali.

‘Nimeshakuambia uniue tu..hapa sitoki mpaka nihakikishe umemleta binti yangu, pili..uape kuwa hutaingilia familia yangu tena,…kwanini familia yangu,..nenda kazae wa kwako, ndio uwafanya ndondocha, shetani mkubwa wewe…’akasema huyo mwanamke.

‘Hahaha..dada uniniita jina ambalo tayari ninalo…shetani, mimi ndio dunia yangu, kwani kwenye dunia halisi naonekana mtu, lakini mimi sio mtu..hahaha, siku nilipopewa huo moba, uliouktaa,a nilisema nataka niwe kama mfalme…hahaha, sasa unaonaje, ..usiku napaa naenda nitakapo….mchana mimi ni bosi…watu wananinyenyekea, …wewe si utaki,…hahaha, …’ilikuwa sauti ya kejeli.

‘Nakumbia kila kitu kina mwisho wake,..mungu ni mkubwa, najua..wewe ulimuua binti yangu, wewe umemuua, ndugu yako mwenyewe….ulikuwa ukimtumia, kama mtumwa wako…lakini huna shukurani…unafikiri utaishi milele…ipo siku…utakufa na kifo chako..sijui,…’akasema.

‘Kufa nitakufa najua kabisa lakini ni nani hata kufa,..hata hivyo kabla ya kufa, najua nitakuwa nimefanya jambo, dunia hii itanikumbuka….ni nani angelijua hapa nchini …ninatawala…hahaha, hawajui, lakini siku watajua, ..watanikumbuka…mitandao yote hiyo, nina ….hahaha, watu kila siku wanatukuza, hawajui tu….sasa hili,likipita najua kabisa, nitaogopwa…’akatulia

‘Halipiti na hutafanikiwa, labda nife…’ilikuwa sauti ya kike

‘Usinilazimishe dada kufanya nisichotaka kukifanya..kama unataka wewe ugeuke tambiko…, itakuwa vyema,..amua tumuache huyo binti wewe uchukue nafasi yake… utafaa sana kuwa kafara la leo…’sauti ikasema

‘Kwanini wewe usichukue nafasi yake..wewe hufai kuishi kwenye hii dunia ya watu, wewe ni shetani, unafuga mashetani, unaishi na mashetani… na sasa unataka kuharibu dunia hii iwe ya mashetani…, kwa kuwekeza mashetani yako kwenye mitandao, ili watoto wetu wote wawe watumwa wako, si ndio hivyo…’akasema.

 'Dada, unajua unachokitaka…unanilazimisha nisiwe na jinsi nyingine…mimi nakupenda sana ndio maana nimekuwa nikitafuta mbadala wake…na kila nimekuap ahadi nyingi tu…unataka nini wewe…ukumbuke haya mambo yanakwenda kwa muda.., huo sio muda wa kulumbana...askari, hebu mshughulikieni huyu mama…’ akasema na mara kukasikika vurumai, mara milio ya risasi...

'Aaaah....'kilio cha maumivu

‘Umetaka mwenyewe,…’sauti ya kiume na mara kukawa na vurumai, mara…

 ‘Tumeingiliwa, askari maliza wote...hakikisha unawamaliza….maliza…’

Kulisikika milio ya risasi, baadae kukawa kimia..

********************

Docta aliyekuwa akiangalia haya yote kwenye komputa yake, akaona mkuu atashindwa kudhibiti hiyo hali kama hatamtahadharisha, ….kwani kwa nje kulikuwa na mtu mwingine ambaye anaonekana ni mmoja wa hilo kundi,kaja na watu wake, wanaonekana wamejidhatiti na silaha…na huyo mtu, alikuwa akitaka kuingia ndani.

‘Huyu ni nani…’docta akawa anajiuliuza.

Mara yule mtu akawa kama kashtuka, anataka kurudi, lakini akatokea mtu mwingine aliyekuwa pembeni, atakuwa ni askari wa mkuu, akamshika yule mtu,na walinzi wake wakataka kuingilia kati lakini yule mtu akawazuia walinzi wake wasifanye kitu,  akawa anaongea na huyu askari,…

Tendo hilo la huko nje, lilimfanya docta ashindwe kuangalia upande wa huko ndani na kuona ni kitu gani kinachoendelea kwa muda huo,  yule mtu akawekwa mikononi mwa askari waliokuwa nje..na walinzi wake wakawa wananyng’anywa silaha..haikuleta vurumai…

‘Huyu mtu ni nani…’docta akawa anaingiza picha kwenye kumbukumbu zake, na mara jina likatokea…

‘Haiwezekani…’akasema tu, na baadae akaachana na sehemu hiyo, akarudi ukumbini na muda huo ndio vurumai zimeanza, risasi,…polisi wakaingia, …kukawa na kutupiana risasi, na huyi kiongozi wao akaanza kukimbia, na sasa alikuwa akielekea pale alipojificha msaidizi wake, ikabidi afanye namna ili msaidizi wake ajifiche sehemu.

Na mara mtu huyu ambaye anaonekana kama ni kiongozi wa hilo kundi akatokea pale alipokuwa msaidizi wake awali , akawa sasa anatafuta nafasi ya kukimbilia,…na ghafla, msaidizi wake akatokea kwa nyuma na kumpiga huyo kiongozi kitu kwenye kichwa na huyo kiongozi akadondoka chini…

Na muda huo watu wa huyo kiongozi wakawa wanakuja kutaka kumsaidia mtu wao, na mara  ..polisi wakatokea…risasi zikarindima.

Haikupita muda, wote wakawa chini ya ulinzi, na yule kiongozi  bado alikuwa kalala chini..kapoteza fahamu…

‘Huyu ni kiongozi wao, sawa, lakini ni nani..maana hii sura haipo kabisa kwenye kumbukumbu zangu, huyu ni nani…’docta akawa anajiuliza bila kupata majibu ya haraka, lakini wazo likamjia akagundua kitu.

 Akaona ampigie simu msaidizi wake,..hakutaka kumpigia mkuu mbaye kwa muda huo alikuwa na shughuli nyingi sana.

‘Sikiliza fanya hivi…huyo kiongozi wao, anaweza akatupotea,… japokuwa yupo mikononi mwa polisi,yaonekana hiyo sura yake, sio yeye, atakuwa ni mtu mwingine kabisa,  atakuwa kafanya jambo…’akasema docta

‘Nifanyeje..?’ akauliza

‘Kwenye kichwa chake, hebu chunguza, atakuwa kavaa, sura ya bandia…’akasema docta na msaidizi wake akamuendea huyo kiongozi askari walitaka kumzuia, lakini mkuu akasema;

‘Wewe unataka kufanya nini..?’ akauliza huyo mkuu.

‘Huyu mtu kavaa sura ya bandia…’akasema msaidizi wake.

Na mkuu naye akavutika na hiyo taarifa, akamsogelea huyo mtu, na kumshika usoni, akavuta kitu,…ooh, ni kweli, ilikuwa kama anabadua ngozi kwenye uso wa huyo mtu,  na sura ya nje ikatoka..kweli alikuwa kava ngozi ya bandia, …na watu wote wakabakia midomo wazi…haiwezekani….hata watu wake hawakuamini….

‘Ni wewe….’akasema msaidizi wa mkuu.

‘Haiwezekani, siamini….’na mara huyo mtu akaporomoka na kudondoka chini,…akapoteza fahamu!

****************

Docta akajua kazi hapo imemalizika, iliyobakia ni kazi za polisi, watajua wenyewe..ila akahisi lolote linaweza kutokea, lakini hakuwa na la kufanya, yeye akarudisha mitambo yake sehemu ya pili, huko alipokuwa mpelelezi, kwanza aliivuita sehemu hiyo hadi awali, ili kujua kilichoendelea, tangia aachane na mpelelezi alipofika humo ndani.

Mpelelezi alikuwa kakamatwa, kawekwa kwenye kiti, kiti hicho ni cha maalumu cha kuulia watu, ni cha umeme…na watu wale walisubiria amri kutoka kwa bosi wao, lakini amri ilikuwa inachelewa, hawakujua kuwa mawasiliani yamekatika,..na hapo ndio docta akatoa amri, kuwa mtu huyo aoandelewe hapo apelekwe chumba kingine

Watu hao walijua kuwa ni amri ya bosi wao, maana hapo huwa wanawasiliana kwa mitambo…tu, ni uchawi wa kidigitali…

Mpelelezi alipoachwa kwenye hicho chumba, docta akamzindua kinamna na kuanza kumuelekeza cha kufanya, mpelelezi akatoka kwenye kile chumba na kutembea kuelekea kwenye chumba kile alichotaka mpelelezi aende..

Akamuelekeza afungue mlango wa kwenda chini…na  mpelelezi akafanya hivyo, na akawa sasa anasuka ngazi za kwenda chini, ilikuwa ni rahis tu, maana docta aliwaarifu walinzi waje juu, kuna kikao cha dharura, walinzi walijua ni bosi wao anaongea kumbe walinzi hao walitegwa kwenye chumba ambacho hawataweza kutoka hadi askari waje kuwakamata…

Mpelelezi akawa anatembea kuelekea jinsi pango hilo lilivyotengezwa, na alipofika kwenye chumba fulani, …kipo ndani kwa ndani, hapo docta akaingiwa na hamu, akamuelekeza mpelelezi akifungue hicho chumba…oh, ni chumba kizuri tu, kina kitanda na meza,…ni chumba maridadi, na pale kitandani kuna mtu kalala…ni mwanadada, lakini alivyolala ni kama..hajiwezi hata kuinuka.

‘Huyu ni nani tena..?’ docta akajiuliza , hakuwa na muda wa kutafuta picha hiyo kwenye mtandao, akamuelekeza mpelelezi aifanye hiyo kazi..

Mpelelezi akasubiria amri…mpelelezi kwa muda huo alikuwa hana nguvu zake za kawaida,…watu hao walikuwa wamezilegeza nguvu zake za kawaida.., na kumwekea nguvu zao, anakuwa kama zezeta fulani tu, au mtumwa wao…., lakini kwa vile ile mitambo sasa hivi inamilikuwa na docta, docta akawa ndiye anamuongoza mpelelezi.

Mpelelezi, akaamrishwa aende kumkagua huyo mdada, akafanya hivyo…na docta akatafuta kwenye mtandao, wapi huyo mdada kawekezewa, mpaka akapata hiyo sehemu,lakini bado picha ilikuwa ngeni kwake,,…akaamrisha huyo mdada azindukane…

‘Wewe ni nani..?’ mpelelezi akauliza

‘Mimi , hahaha, mimi ndiye Mpenzi wa facebook…’akasema huyo mdada, na docta hakuamini, akarudisha nyuma hilo swali, na alipojibiwa hivyo, akaikuza ile picha…na taswira ikajaa kwenye uso wa komputa…

‘Ooh…ina maana ndio huyu, haiwezekani,….’ docta akashindwa kabisa kuling’amua hilo, kwa jinsi gani lilitendeka, akalipa muda wa ziada, kwani kuna mengi ya kufanya, hakutaka kuuchsha ubongo wake kufikiria kililivyofanyika, akasema tu;

‘Oh…hatimaye…’akasema docta sasa akianza kutafuta kumbukumbu zote za huyo mdada ili ikiwezekana, baada ya kuondoa nguvu za giza kwenye huo mwili wa huo mdada, sasa awe tayari na kumbukumbu za huyo mdada,…na kama hajamalizwa kabisa basi yawezekana, huyo mdada akaweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida, yote hii itategemea huyo ….aliyemfanya hivyo,..…, na mara simu ya docta ikaita, akajua ni nani, msaidizi wake anampigia,anasubiria apewe amri afanye nini…

‘Huyu sasa atakuwa ni mzigo..’docta akasema, akaona jambo jema sasa ni kuanza kumuondoa huyo msaidizi wake kutoka kwenye minyororo ya hao watu kwa kuanza kuondoa sumu aliyowekezewa,….docta alijua kabisa hayo yote yapo kwenye huo mtandao wao wa ajabu…muda ukawa ni muhimu sana akaanza kazi kwa huyo msaidizi wake huku akiendelea na maelekezo kwa mpelelezi..

‘Kwanza ni kuondoa nguvu za giza za hawa watu..mungu ni saidie nimalize hii kazi kwa haraka, kabla ya hawa watu hawajaweza kurejesha mitambo yao…’akasema docta.

Ukumbuke hayo yote sasa yanafanyika kwenye mitandao ya hao watu, lakini sasa ipo mikononi mwa docta, na ni swala la muda, kama hao watu wataweza kurejesha mitandao yao,mambo yanaweza kubadilika,…muda ni muhimu sana hapo.

NB: Tutaona itakuwaje, sehemu ijayo..uone jinsi watu walivyoweza kuwekeza nguvu za giza kwenye mitandao..ni hatari, tuweni makini sana...


WAZO ZA LEO: Vyo vyote tufanyavyo, tuwe ana akili ya ziada, utundu, ujuzi, kipaji, elimu , madaraka, utajiri, tukumbuke kuwa kuna mungu, mola ndiye mpaji wa yoye hayo…, na ili uhakiki hilo, hebu kumbuka wangapi waliokuwa matajiri, wenye akili, warembo,  wenye nguvu, wenye kila sifa za kila aina, sasa hivi wapo wapi,…Mungu ni mkubwa , mrehemevu, mwenye kusamehe , tumuabudu yeye na kumtegemea yeye, na kumshukuru yeye kwa  kila mara mara.
Ni mimi: emu-three

No comments :