Baadae wakawa wanafanya mambo yao,...kila mmoja na kazi yake, na walipomaliza huyo mkubwa wao akasema;...
‘Sasa hapo tusipoteza
muda, kwanza tukiendelea kukaa hapa ni hatari, hasa kwangu, mnaelewa nina maana gani, nyie ni mimi. muhimu kwasasa ni kutawanyika kila mtu kwenye mambo yake...
Na kutawanyika hapa ni hivi,...wewe pitia mlango wa kule, wewe ule wa mbele, wewe upande ule, na wewe huku..mumenielewa,..wakainamisha vichwa kukubali
'Hata…tutawanyike, tutarudi hapa kama muda wa saa kumi…naona kwa muda huo itafaa,
najua hapo kila kitu kitakuwa tayari,
kila mtu sasa na muelekeo wake…mimi narudi nje ya nchi…’akasema na wakaanza kutoka
taratibu, kila mmoja akawa anatokea mlango wake.
'Saa kumi...' muda wa kukutana
Tuendelee na kisa chetu
************
Docta, alimalizia kazi yake, ilikuwa kazi maalumu
akitumia ujuzi wake wa mambo ya mitandao, udakitari na elimu ya mambo ya
kienyeji, kwa kadri ya uwezo wake, alijua kuwa huo ndio mtihani wake wa mwisho,
kufaulu kwake, ndio anaweza kukamlisha, ‘project’ yake. ..na ndipo atajiona
kweli sasa kaiva kama dakitari wa kisasa!
Ilibidi awasiliane na rafiki yake wa nchi za nje, ili
aweze kupata maelekezo zaidi,…kama ujuavypo, itafute elimu hata uchina, kwake
elimu ilikuwa ni muhimu kuliko, na elimu nzuri ni ile inayowekezeka..usome na
uweze kuifanyia kazi, ndivyo alivyotaka yeye, sasa ana ujuzi huo, kwanini
asiufanyie kazi,…
Docta kwa kupitia mitandao, na kwa kupitia mawasiliano na marafiki zake, akaweza
kuongeza ujuzi wake wa mawasiliano kwa njia ya mitandao ya kisasa.., jinsi gani ya kuunganisha herufi zikazalisha kitu..jinsi
gani ya kuunganisha mawasiliano kwa kutumia herufi, au waya…na mambo ya
upelelezi kwa kutumia mitandao.
Docta alitaka utaalamu wake uende na wakati, na...sasa ilipozuka
hii elimu ya mitandao, akajua huku nako kunahitajia kujifunza, ili kuweza kuona dunia nyingine ipoje, au watu ambao wanataka kucheza na akili za watu kwa nia mbaya wanafanyaje kwa kutumia mitandao, ambayo sio wengi wanaifahamu, kwake yeye, alijua ni muhimu kujifunza ili kwenda na
wakati…,
'Ina maana hata udakitari...?' aliwahi kuulizwa na jamaa mmoja, na yeye akasema
'Ndio unahitajika zaidi, kutibu watu na mitandao yenyewe, na ujue ndani ya mitand hiyo kuna magonjwa, kuna virusi, kuna watu wanatumia mitandao kuwaumiza watu wengine, sisi kama madocta tunahitajika kufahamu hayo...'akasema.
Kwa namna hiyo, akaona kuna ulazima wa kusomea maswala ya mitandao, zaidi ya upeo wake...lakini akitumia taaluma yake ya kidakitari zaidi…haikuchukua muda kwake yeye kuifahamu taaluma hiyo,…kichwa chake ni
chepesi sana.
Sasa wakati anahangaika kuunganisha mawasiliani yake na viunganishi mbali mbali ambavyo vingi vipo kwenye miili ya watu, akafika sehemu akakwama, hapo akaona kuna umuhimu wa kuwasiliana na
rafiki yake huyo wa nchi za nje.
Alifanya haraka kwuasiliana naye kabla mpelelezi hajafika huko anapokwenda,…na akamuuliza alichotaka kukifanya, akiwa anamuamini,hakumuelezea
kiundani yeye alitaka namna ya kuwasiliana, kuonana, na kuzuia mtu kukuona
wakati wewe unamuona,..sio uchawi, ni elimu ya mitandao…hapo akapata maelekezo
mazuri tu….
'Hilo unalotaka
kulifanya , muda ni kitu muhimu sana,… ‘timing…’ …..’ akambiwa.
‘So ..do like this…kama umeshaweka point ya
mawasiliano, kama ni mtu ndiye ponti yako,…na huyo mtu anacho hicho kifaa kama point yako ya
mawasiliano..yeye akiingia tu eneo hilo, ujue kama wao wana chombo cha kuhisi,
watajua kuwa kuna ‘mwizi’au inasema 'intruder…kwahiyo wewe, unatakiwa, uwe mwepesi, kumlina huyo kwa kumuwekea kinga.
'Cha zaidi ni kuwa pale utakapounganisha mawasiliano yako na kwa huyo mtu akiwa ndani ya hilo jengo au eneo, ujue, na wao watakuona...'akasema huyo mtaalamu.
'Sasa nifanyeje
wasinione huko…ndio hapo nimekwama…’akasema.
'Ukishajiunganisha na huyo mtu, uliyemwekea hiyo waya,
‘whatever’…wewe sasa weka vizuizi hivi....'akamtajia herufi za kuunganisha ili
kujificha na kulizuia ili mtu mwingine asiwezi kukuona..
Baada ya hapo,
tuma ujumbe huu,…huu ni ujumbe wenye virusi, vya kuharibu mitambo yao…hairuhisiwi
kitaalamu, lakini kwa vile unahitajia kwa manufaa ya jamii, inabidi ufanye
hivyo…, na mitambo yao itakuwa haifanyi kazi tena…mpaka waje kuunganisha upya,…kila
kitu kwenye mitando yao…na itachukua muda…’akasema.
'Je ujumbe wa virusi hivyo, wataufunguaje wao..?’
akamuuliza.
'Kwasababu, ukiwazuia wao kukusoma huko ulipo,
watapata ujumbe kuwa kuna ugeni, ..’intruder..’..yaani kitu kimeingia kigeni,
na wao watajua kuna tatizo..na mara nyingi hutokea kama kuna mtu kaweka chombo
cha mawasiliano cha nje ya mitandao yao…na wanajua ni vipi kukizuia kama kina
madhara..
‘Kawaida
ikitokea hivyo, mitambo yenyewe hutuma ujumbe wa kujisafisha, kwahiyo, wao
wakipokea ujumbe uliotuma wewe, kwa haraka watajua ni huo ujumbe wa kujisafisha,…
wataufungua, …na wakiunfungua tu…haraka unaanza kufanya kazi,..wao kwa muda huo
watajua kuwa ni huo utaratibu wa kujisafisha… kumbe ndio mitambo yao inaliwa na
hao wadudu, na ikianza kuharibu huwezi kuizuia, ‘too late’...watagundua
mwishoni,
‘Ahsante sana..’akasema docta, hakupenda kufanya hivyo
, ila hiyo ni vita, na dawa ya hao watu ndio hiyo, wao wanatumia mitandao na
nguvu ya giza kuumiza jamii, lakini yeye anatumia kwa manufaa ya uma, hana
kosa.
***************
Docta alisubiria, hadi ishara kuwa mpelelezi
keshaingia eneo analotakiwa kwenda, ishara ya kuashiria kuwa unywele ule au
waya maalumu iliyotengenezwa kwa kazi hiyo, umeshahisi mitambo inayoendana
nayo, docta, kwa haraka akaanza kazi…nguvu za giza hazikuwa na nafasi hapo,
alishazizima kwa kumuomba mola wake, alijua ni nini akifanye kwa wakati gani…
Sasa anacheza
na mitambo halisi, inayohitajia elimu ya mitandao…’muda hapo ni kitu muhimu…’akakumbuka
hilo,…akawekeza zile herufi bila kukosea, na alipohakikisha zipo safi,
akazibofya kuwa zianze kazi mara moja…kazi ikaanza..
Ni wakati anamalizia kuhimiza mtando ufanye kazi, ndio hapo akapokea simu, kuwa mtu wake, yaani
msaidizi keshafika sehemu inayohitajika…huyo naye alikuwa akimfuatili hatua kwa
hatua, ni sehemu nyingine muhimu ambapo amewekeza ponti ya mawasiliano…akaona
ili ampe mataumaini, sasa anaweza kumpigia..baada ya kujiwekea kinga ya
kutokuoenakana…
Alipiga simu , huku akiendelea kuangalia maendeleo ya
kila anachokifanya,..haitakiwa kufanyika kosa, kosa dogo ataharibu kila kitu na
huyo alitewekezewa mitambo hiyo anaweza kuwa kwenye hatari y akugundulikana na
matokea yake atauliwa… hatimae akafanikiwa, na alipohakikisha kuwa kila kitu
kipo sawa, akampigia simu mkuu.
'Mambo sasa tayari
kama nilivyokuambia…sio uchawi, ni mitandao.., hawataweza kutuona tena…, ila
sisi kuanzia sasa tunaweza kuwaona na kuona kila wanachokifanya.
…
'Sawa kabisa, nimeona huku kwangu...'akasema mkuu, na
kumfanya docta ajiulize kumbe mkuu ana mambo yake , ... mkuu naye wamo..lakini akijiwa na neno jingine la kumuuliza, mkuu akasema;
'Unasemaje
kuhusu mke wa mzee…mliwasiliana naye au sio..umechukua hatua gani…?’ akauliza
'Huyo kwa sasa tuachane naye kwanza, maana
tukimalizana na hawa watu, hayo mambo mengine yatajileta yenyewe, huyo mama atakuwa huru, kama katekwa, ...na sijui kama ndio yeye, nilimuona mahali…nina imani ..atakuwa
salama…’akasema mkuu
‘Sawa nimekuelewa…ngoja tuendelee na kazi…’akasema
docta, sasa akijua kila anachokifany ahata mkuu wake anakiona,
'Natakiwa niwe makini na huyu mtu, sijamuamini bado...'akasema kiakili, na sasa akipanga jinsi gani y akuweza kujilinda kama lolote litatokea kutoka kwa huyo mtu.
'Hii kazi huwezi kumuamini hata mkeo...'akakumbuka maneno hayo kutoka kwa jamaa yake mmoja.
************
Docta alipoona kakamilisha kila kitu, sasa akaanza kazi nyingine, maana ukitaka kumshinda adui yako, mfahamu alivyo kabla hajakufahamu wewe, yeye alichofany ani kuazna kutengeneza mtandao wa kuisoma ramani ya jengo...hilo jengo lenyewe lilikuw anaramani kwenye mitandao yao, ambayo kwa ujumla alishaiiba ...na kuweka kwake, ni kama yeye ndio anafany akazi ndani ya jengo lao.
Alijua huko kwa hivi sasa wanafanya kazi ya kutafuta namna ya kurejesha mitandoa yao, lakini kwa jinsi akuavyo, itachukua muda karibu siku nzima, na hata wakifanikiwa bado yeye anao mtando wao wakuwasoma, na hawataweza kumzuia ...
Kwa kujiamini kabisa akaendelea na kazi yake sasa aliweza kutembelea hilo eneo ambalo ndilo makao ya
huyo mkuu wao, bila shaka….utafikiri yupo humo ndani,..ni mambo ya mitandao,
wala sio uchawi…akaangalia taswira ya eneo, na kila hatua aligunda mambo mengi
kwenye hilo jengo,.
'Kumbe hapa ndipo wanapofanyia mambo yao...sasa wamekwisha...'akasema docta.
Kwani jengo hilo linaloenekena la kawaida, lakini kwa
ndani, kuna mambo mengi ya siri , ambayo bila mitandao hiyo usingeliweza kuona,…na
kama alivyoambiwa kwenye njozi, mpelelezi ndiye atakuwa njia yake,…na kweli
mpelelezi kamfikisha kule alipokuwa akipatafuta kwa siku nyingi.
Jengo hilo
lilikuwa na nyumba za chini ya ardhi ambazo hazijulikani na kwa jinsi ilivyo,
kuna vitu kama mahandaki, yanayotoka hapo kwenye jengo na kuelekea sehemu
nyingine…alipogundua hilo, akatikisa kichwa, akawa anajiuliza kama mkuu
keshaliona hilo, hakuwa na muda wa kumuuliza.
Kwa haraka akafuatilia pango moja, laonekana ni refu
sana, kama bomba kubwa sana..akawa anajaribu kulifuata na ramani yake,..
akagundua kuna linakwenda hadi kutokea…oh, maeneo ya makaburini…ni rafu sana,
hawa watu ni wajabu sana, wanapita chini ya ardhi watu juu hawana habari.
'Duuh...kumbe....'akasema na mara simu yake ikalia…
Alipoangalia
saa akagundua muda umefika, saa kumi, na haikupita muda mkuu naye akaingia.
‘Umeona eeh…?’ akauliza docta.
‘Nimeona nini..ok, sawa nimeona, ..japokuwa sina
uhakika, na unachokiuliza, ila hapa nimekuja kwa ombo moja…’akasema mkuu,
‘Sawa ombi gani…?’ akauliza
'Sasa docta,
kazi iliyobakia ni yetu sisi watu wa usalama,…kila kitu kipo wazi, ..muhimu ni
kwenda kuwakamata hao watu, tukiwa na ushahidi kamili.., mimi nakuomba ubakie
hapa kwenye mitambo,tutawasiliana…au sio…?’..'akasema mkuu, na docta hakuwa na
kipingamizi, japokuwa alihis bado huyo mtu hajamuamini.
'Sawa, kwangu
haina shaka, mkinihitajia msaada wangu nipo tayari…Muhimu ni kumuwahi binti wa
Inspecta kabla hawajampiga hizo sindano za kumlegeza viungo vyake..wakifanikiwa
kufanya hivyo, itatuwia shida sana kumrejesha, katika hali ya kawaida, unaona
jinsi binti wa mzee anavyopata taabu, ...'akasema docta.
'Sawa, hilo
lipo makini..kila kitu kina watu wake..sizani kama vijana wetu watatuangusha
kwa sasa…’akasema mkuu.
‘Sawa mimi nawatakia mafanikio mema…’akasema docta, na
kupeana mikono na mkuu huyu.
Mkuu na kikosi chake kamili wakaelekea eneo la
mapambano, wakiwa na zana za kila namna mavazi ya kubadilisha kila hatua…
***************
Mimi nilianza kuwa na wasiwasi pale niliposhindwa
kupata nafasi ya kuingia ndani ya hilo jengo, ningeingiaje wakati jengo lote lilizingirwa na watu, ambao nilijua
ni watu wa hao watu…nilihisi hivyo!
Baadae sana,
niliona watu, wakiwa wamebeba majeneza, mawili…nilijua wanataka kuzika, sasa
kwanini hawaendi makaburini wanakuja kwenye hiyo nyumba..walipofika kwenye
geti, wakawa wanaongea na mlinzi, na mmojawapo akawa anazozana na mlinzi, na
mimi nikawa na hamu ya kusikia wanachoongea,nikasogea karibu.
'Sisi tulimuomba mzee kuleta hizi maiti hapa kabla ya
kuanza mazishi....'akasema mmojawapo.
'Haiwezekani, kwanza huyo mzee hana mamlaka na hii
nyumba tena…, mke wake ndiye anaisimamia kila kitu, je mliongea na mama mwenye
nyumba..?’ akauliza.
'Sisi tuliongea na mzee kwasababu tunajua yeye ndiye
baba mwenye nyumba, kama unabisha mpigie simu..’wakasema hao watu.
Basi kukawa na mzozano, na mara kukasikika mlio kama
wa bomu, ndani ya jengo..na jengo zima likatikisika, watu waliokuwa pembeni wakawa wanasogea karibu
kuona kuna kitu gani..na hapo kukawa na msukumano, watu wakitafuta upenyo wa
kuona kinachoendelea hapo..
‘Kuna nini kimetokea…’watu wakauliza
‘Bwanaeeh, hilo jengo lina viroja, sijui ni mashetani
yanapigana humo ndani…’mmoja wao akasema.
‘Kwani kuna mashetani humo ndan…?’ akauliza mtu
mwingine.
‘Unauliza jibu, jengo hilo limeguzwa chaka la wanga,
wanaoingia humo, wengi ni wachawi..angali hata mavazi yao..wanatoka huko
walipotoka, wakifika hapo wanabadilisha nguo zaao..’akasema mtu.
‘Wewe shauri lako ropoka tu, kama utauona usiku…’akasema
mtu mwingine na kukawa kimia.
Mara nikiwa naangalia huku na kule,nikaona watu kwa
nyuma ya jengo wakiruka ukuta kwa kasi sana,…walikuwa wepesi, .. sikujua ni
watu gani, baadae kukatulia.
Mimi nikahisi
sasa kama kuna kitu kinavuta, hisia ya kutaka niingie ndani, na nikafanya
hivyo, nikapita pale pale mlangoni, ….kilichotokea ni kuwa yule mlinzi aliinama
kama anaokota kitu, au kuna kitu kimeingia kwenye kiatu chake
kinamsumbua,..akawa anahangaika hadi kuvua kiatu…na mimi nikachukua nafasi hiyo
niliona kama bahati tu…, nikajikuta nimeshaingia eneo la jengo.
Nikawa nahisi
kuelekea nyuma ya nyumba,…nikatembea nikiwa samba mba na ukuta, ili watu wa
ndani wasije kuniona… na hapo nikafika mlango wa nyuma, ulikuwa wazi,…alitoka
mtu, na kutembea upande wa pili hakugeuka nyuma na mimi kwa haraka nikaingia
ndani.., nilihisi kuna watu wamejificha juu ya paa, cha ajabu, sikuona
wakinizuia..Nahisi ni kama wameniona..
Nikafika
sehemu, nikawa kama nimeambiwa nisubirie hapo…na mara nikasikia sauti ya hasira
ikisema;
'Haiwezekani...mitambo imekuwaje,..'sauti kali
ikasema, nikaikumbuka hiyo sauti, nilishaisikia mahali, kule kwenye jengo
nililotoroka, ni yule yule mtu aliyefika uwanja wa ndege….nikataka kwenda
kumuona lakini cha ajabu miguuu ikawa mizito, hataki kutembea, ni kama
nimeshikiliwa.
Nilikabakia
hapo hapo kwa muda, mara nikasikia sauti ile ikisema tena kwa hasira.
************
Hapo nilipo niliweza kusikia sauti hiyo kupitia kwenye mlango uliokuwa nusu wazi, kumbe ni chumba ambacho ukitoka humo unaingia hapo hao watu walipo...
'Muda umekwisha, ...mleteni huyo bint huku, tusipoteze
muda….
Na mara
kukasikika sauti ya binti akilia….
‘Msiniue msiniue….’
'Usiwe.na wasiwasi bint, tunataka kukuondolea hilo
tatizo lako, baada ya hapa, utasahau kila kitu…hii dunia ya mateso,
utaiacha,..na huko utaenda kuungana na baba yako...'sauti ikasema.
‘Baba yangu, ina maana mumeshamuua…?’ sauti ya kike,
nahisi ni huyo binti ikauliza
‘Hahahaha….usiulize kitu kama hicho, elewa kuwa na
yeye imebidi, kwasababu…anahitajika kupumzika,…unanielewa binti mrembo…’sauti
ikasema.
‘Wewe ni shetani, muuaji, kama nitapata nafasi ya
mwishi, nitahakikisha na wewe umekufa kifo kibaya…shetani mkubwa wewe…’sauti ya
kike ikasema.
‘Hahaha..usijali…haya yote utayasahau…sasa hivi, ngoja
tusubirie taarifa ya kutoka huko alipo baba yako…tunataka yeye atangulie kabla
yako..ndivyo inatakiwa..unasikia, na tulia ..mwekeni sawa…’akasema huyo
muongeaji.
‘Subirini kwanza…’ilikuwa sauti ya kike lakini sio ile
ya binti…
NB: Ni Nani huyo
WAZO LA
LEO: Watenda mabaya, hufikia mahali wakaona kuwa wao hii dunia ni
yao,..wana haki hata ya kuua, wanasahau kuwa kila nafsi itauonja umauti kwa
wakati wake…na wao muda wao utafika, na wao watarejea kwa hakimu wa
mahakimu,ewe mwanadamu tubia kabla muda haujafika, ubaya hauna heri hapa
duniani. Tumuombeni mola wetu atujalie tuishi vyema, atulinde na vitimbwi vya
shetani, na atujalie tuwe na mwisho mwema. Aaamin..
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment